Mkuu wa Mkoa Kigoma azitaka Halmashauri kudhibiti upotevu wa mapato

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,816
4,566
Mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amezielekeza timu za Menejimenti za Halmashauri mkoani humo kuhakikisha zinasimamia na kudhibi upotevu wa mapato yanayotokana na makusanyo ya ndani katika Halmashauri hizo

Andengenye ametoa maelekezo hayo alipokuwa akifunga kikao kazi kilichomkutanisha na timu za Menejimenti za Halmashauri nane (8) za mkoa wa Kigoma na kuwasisitiza watendaji hao kuongeza ufuatiliaji wa mashine za kukusanyia mapato kwa lengo la kudhibiti upotevu wa fedha za mapato ya ndaniAmesema ili kudhibiti mapato ya Halmashauri Wakurugenzi wanapaswa kuweka vigezo vya mafanikio kwa wakusanya mapato wa Halmashauri na ambao hawatofikia vigezo hivyo watakuwa wamejikosesha sifa za kuendelea na kazi hiyo

Aidha, Mkuu huyo wa mkoa amewakumbusha wataalamu hao kuwatembelea wakusanya mapato mara kwa mara ili kudhibiti ubadhilifu unaofanywa na baadhi yao ambao wamekosa uaminifuKatika hatua nyingine Andengenye amewaelekeza Watendaji wa Halmashauri za Uvinza pamoja na Kasulu kuhamia katika Ofisi mpya za Wakurugenzi watendaji zilizojengwa katika Halmashauri hizo ifikapo Machi 2024

"Serikali imetumia fedha nyingi kutekeleza miradi ya ujenzi wa majengo hayo, hivyo nyote mnatakiwa kuhamia na kuanza kuzitumia Ofisi hizo wakati ukamilishwaji wa sehemu zilizobaki ukiendelea" -Andengenye
 
Back
Top Bottom