Ndugu Mteja!

Tunashukuru kwa kuwasiliana na TANESCO Huduma kwa Wateja, Tunakujulisha kuwa sasa TANESCO imekurahisishia huduma ya wewe kuweze kufanya maombi ya kuunganishiwa umeme kwa kutumia mfumo bora wa Nikonekt popote ulipo na wakati wowote, Unaweza kufanya maombi kwa njia zifuatazo:

- Nikonekt.tanesco.co.tz

-Nikonekt App (Ipo Play store na Apple store)

- Kubofya *152*00#

-Kwenye ofisi za TANESCO



Kwa Maulizo au msaada wowote tafadhali wasiliana na kituo chetu cha huduma kwa wateja kwa

Simu;0748550000

WhatsApp: 0758346869^EB
Tanesco Kilimanjaro kuna shida gani? Umeme Toka jana unatusumbua , hamsemi tatizo, Leo Toka asb hakuna umeme na simu zenu zote hazipatikani ,mna shida gani? Je mtu akiwa na dharura Nini afanye?? Naomba majibu.

Sent from my M2004J19C using JamiiForums mobile app
 
TANESCO kimara mmeanza tena mambo ya kukatakata umeme nyakati za mchana Kimara mwisho.
Hivi ni lini watu tutatulia na kufanya shughuli zetu bila manyanyaso haya ya Tanesco?
Kila miaka mambo ni haya haya.
Maisha magumu now hizi habari za kukatiana umeme ni kumalizana kimaisha na kusababisha wananchi tuichukie serikali.
Kuna maana gani ya kulipa kodi ikiwa mara kwa mara nyinyi mnahujumu biashara zetu kwa uzembe wenu na kutokujali?mngekuwa mnajali miaka yote hii habari hizi za kukatakata umeme zingeisha kabisa.hamjirekebishi.
 
Kwa hili TANESCO pokeeni maua yangu.
Nilitoa taarifa ya tatizo la token za umeme kutoingia kwenye mita yangu mnamo tarehe 04/06 saa 7:26 jioni. Kufikia saa 11:55 usiku fundi wenu alifika nyumbani na kugundua kwamba mita yangu MBOVU. Aliahidi kulitolea taarifa swala langu ofisini ili nibadilishiwe mita. Jana 7/6 saa 4:06 jioni mafundi wamerudi kwangu na kufanikiwa kunifungua mita mpya. Kubwa zaidi taratibu zote hizi zimefanyika kupitia mawasiliano ya simu sababu sikuwepo nyumbani kipindi chote hicho, niliwaunganisha tu mafundi na kijana ambae yupo nyumbani kwa sasa.
Mteja wenu wa Kunduchi Mtongani nasema kwa hili TANESCO (Mbezi Africana) mmeonyesha mabadiliko makubwa, imani yangu kila mteja atapata hiki nilichokipata mimi.

Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app
 
Habari ndugu mteja, ahsante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu na pole kwa changamoto hiyo, gharama hiyo ya shilingi 27,000 ni kwa wateja wetu wa vijijini wanao hudumiwa na mradi wa REA, kama eneo lako halipo chini ya mradi huo utalipia gharama za kawaida za kuunganishwa na huduma ya umeme, tunaomba kusisitia kuwa malipo yote ya TANESCO hufanyika kupitia control namba. ^HS
Kuna mfumo wowote unaoonesha kuwa mahali Fulani ni huduma za REA? Maana watu wameunganishiwa Kwa REA mwaka huu tu lakini sisi wengine sasa hivi tunaambiwa ni malipo kama ya miji.
 
TANESCO, ningependa kufahamu kama Kijiji Cha Nkilizya wilaya ya Ukerewe kimeshaondolewa kwenye mradi wa REA, kama baadhi ya maeneo bado wanahudumia kwa mradi huo ningependa kuyafahamu. Nasubir majibu siwezi kufika ofsini kwenu nansio maana niko mbali
 
Guys,
Leo nimeshinda nyumbani siku nzima.

Mpaka sasa naandika uzi huu hakuna umeme Mji mwema kigamboni, ni tatizo gani kubwa hivyo la kutufanya tukose umeme hata kwa masaa ya usiku tu? TANESCO tafadhali tusaidieni hali ni mbaya sana majumbani, hatuwezi kupandisha maji kwenye matenki na maji yamekata. Ikiwa tutalala na hali hii basi huenda mambo yatakua mabaya zaidi.
MTUSAIDIE.
 
TANESCO utoaji wa huduma kwa wateja kwa tawi la TANESCO Ukonga ni mbovu.

Mimi ni wakala pamoja na huduma ninazotoa ni kulipia malipo ya serikali ikiwamo kuuza token za umeme. Kwa malalamiko makubwa naomba kuwasilisha kwenu juu ya tawi la Ukonga, ambalo kwa Sasa lipo Magereza.

Tarehe 5 mwezi huu tulipata tatizo ofisini mtoa huduma alifanya malipo ya umeme wa 750,000/= badala ya kiwango sahihi cha 75,000/=. Tulipo tafuta namna ya kupata msaada makao makuu walituambia tuandike barua ya kuomba kurudishwa kwa fedha kwenye akaunti husika. Tumetakiwa kuandika barua shida majibu TANESCO ni vikwazo kibao kwamba mhasibu hajasaini. Hata walipo tushauri kuepuka ucheleweshaji tutafute mtumiaji mkubwa wa umeme tubadilishiwe token kwenda mita nyingine. Tumeomba zibadilishwe muda wa wiki ya pili hii na bado kila siku jibu hamna. Mpaka unawaza hivi ni kweli hii namna bora ya utoaji huduma?

Nimekuwa na mashaka kwa sababu nilipatwa na tatizo linalofanana na hilo mwaka 2021 umeme wa 350,000 hatujajibiwa mpaka leo kwa utaratibu huu huu waliotuelekeza. Au hamjali huduma tunazozitoa? Inakuwaje mashirika mengine yana ufanyaji nzuri na kuchukua hatua mapema? Hivi hamuoni inampa nguvu mtu ambae umeme umekosewa inampa nguvu ya kutumia token hizo na kuniacha na hasara Mimi ninayefanya kazi zenu?

Ninaomba namba ikibidi niwasiliane na hata mkurugenzi wa shirika, sisi ni wajasiri amali tumeamua kujiajiri kupoteza kwa kiwango hicho cha pesa ni hasara kubwa. Naongea kwa kwa huzuni kubwa juu ya utendaji wa TANESCO tawi la Ukonga- Magereza.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Habari ndugu mteja asante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu na pole kwa changamoto hiyo, tafadhali tunaomba namba yako ya simu kwa huduma zaidi.^OK
 
Tunaomba ufafanuzi kuhusu kodi ya jengo.maana naona imekua too much nimekatawa elfu Tsh 6000 x 2 wakati nanunua umeme mwaka huu alafu bado nikinunua umeme naendelea kukatwa Tsh. 1000
 
Habari ndugu mteja asante kwa kuwasiliana na TANESCO huduma kwa wateja na pole kwa changamoto, zifuatazo ni gharama halisi za kuunganishiwa umeme kuanzia tarehe 5/01/2022
•Gharama za kuunganisha umeme mjini ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia moja kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 320,960/=,
•Mteja wa njia moja ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 515,618/=,
•Umbali wa njia moja ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 696,670/=
•Aidha, gharama za kuunganisha umeme mjini ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia tatu kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 912,014/=,
•Mteja wa njia tatu ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 1,249,385/=,
•Umbali wa njia tatu ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 1,639,156/=.

Zingatia
Gharama ya kuunganisha umeme vijijini kwa wateja wa njia moja ni shilingi 27,000/= (REA)

Gharama hizi ni kama ilivyoelekezwa na EWURA.

NB: Gharama zote zimejumuisha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) 18%
Ili upate gharama halisi ni lazima wapimaji wafike katika eneo lako.

TANESCO Huduma kwa Wateja
SIMU : 0748550000.
^ OK
 
Maelezo yenu ni mazuri ila watendaji wenu ni tatizo,nataka kuunganisha umeme kijiji(nyumbani) walikuja wakafanya survey,hadi leo sikuwahi kutumiwa control number,baada ya mzee wangu kufuatilia kwa muda mrefu akaambiwa zinahitajika nguzo tatu na anapaswa kulipia sh 3m ili kuunganishiwa umeme,hii ni halali?
 
Maelezo yenu ni mazuri ila watendaji wenu ni tatizo,nataka kuunganisha umeme kijiji(nyumbani) walikuja wakafanya survey,hadi leo sikuwahi kutumiwa control number,baada ya mzee wangu kufuatilia kwa muda mrefu akaambiwa zinahitajika nguzo tatu na anapaswa kulipia sh 3m ili kuunganishiwa umeme,hii ni halali?
Hao matapel kwel SI wanasema nguzo 1 laki2
 
Hello! Naomba kufahamu, Hivi mteja anayehitaji kuunganishiwa umeme anapaswa kumlipa surveyor ili kumfikia mahali pake?
 
Back
Top Bottom