Tanesco tawi la kibiti ubabaifu mwingi, umeme unakatika hovyo na baadhi ya mitaa SIKU mbili hauwaki, na hakuna TAARIFA yoyote juu ya kukatika kwake. Maelezo ya jumla eti " gari za emergency hazipo na zilizopo mbovu mathalani pancha, nyaya" n.k majibu mepesi kwa hoja sensitive. Mjifunze kujali wateja
 
TANESCO kuanziq asubuhi hadi jioni hii Kimara mwisho kote Mavurunza,DAWASCO,Matangini,TRA,Kanisani,yaani eneo lote la mji wa Kimara mwisho darajani halina umeme.Ndipo center ya mji wa Kimara lakini mna confidence ya kukata umeme zaidi ya masaa 8 nyie watu aisee!hamjali kabisa mmesimamisha shughuli zetu zote huku.
 
Tanesco mnaunguza vitu huku majumbani umeme hauna nguvu unawaka na kuzima kila baada ya dakika Moja Toka saa 12 jioni maeneo ya banana ukonga na staki Shari wilaya ya ilala
 
Habari ndugu mteja asante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu na pole kwa changamoto hiyo, tumepokea taarifa ya hitilafu kwenye miundombinu ya umeme wataalamu wetu wanafanya jitihada za kurudisha huduma, tunaomba radhi kwa adha zilizo jitokeza.^OK
 
Tumekua na tatizo ndugu la kupata kwa umeme maeneo ya kahama hasa bulungwa yaani mpaka imekua kero inaishi siku 2 hakuna umeme
 
Hbari ndugu mteja asante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu na pole kwa changamoto hiyo, tafadhali tupatie taarifa zifuatazo kwa msaada zaidi,
Jina
Eneo
Namba ya simu
Tatizo
Mita namba
Kitu maarufu
TANESCO Huduma Kwa Wateja
SIMU: 0748 550000
WhatApp: 0758346869^OK
 
Hapa Arusha jana wamekata anzia saa mbili asubuhi hadi saa tano usiku, na asubuhi hii wamekata tena. Niko hapa natukana kimoyo-moyo.
 
Habari. Bei ya kuunganisha umeme pembezoni mwa miji ambako ni sawa na kijijini ni shilingi ngapi? Maana ndugu yangu ameomba umeme hapo Igingilanyi Iringa mpakani na Nduli ambako watu wamehamia baada ya kuhamishwa na upanuzi wa uwanja wa ndege lakini amepewa bill ya malipo ya manispaa. Naomba ufafanuzi maana yeye alijua ni 27,000/= lakini kaletewa bill ya 360,960/= kiasi kwamba amekwama kulipa
 
Huku Kibada kuanzia saa tatu kamili usiku huu mpaka saa tatu na dakika tisa mmekata umeme na kurudisha mara 17, shida nini au mnataka kutuunguzia vitu vyetu?
 
Habari. Bei ya kuunganisha umeme pembezoni mwa miji ambako ni sawa na kijijini ni shilingi ngapi? Maana ndugu yangu ameomba umeme hapo Igingilanyi Iringa mpakani na Nduli ambako watu wamehamia baada ya kuhamishwa na upanuzi wa uwanja wa ndege lakini amepewa bill ya malipo ya manispaa. Naomba ufafanuzi maana yeye alijua ni 27,000/= lakini kaletewa bill ya 360,960/= kiasi kwamba amekwama kulipa
Habari ndugu mteja, ahsante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu na pole kwa changamoto hiyo, gharama hiyo ya shilingi 27,000 ni kwa wateja wetu wa vijijini wanao hudumiwa na mradi wa REA, kama eneo lako halipo chini ya mradi huo utalipia gharama za kawaida za kuunganishwa na huduma ya umeme, tunaomba kusisitia kuwa malipo yote ya TANESCO hufanyika kupitia control namba. ^HS
 
37249129745 we tanesco samahani embu angalia hiyo mita ina deni au maana kila nikitia umeme wanasema haitoshi hela niko miono hapa chalinze
 
Nimekwenda Ofisi za TANESCO Sengerema Mwanza kuuliza taratibu za kuunganishiwa umeme kwa umbali wa nguzo 1,nimeambiwa utaratibu umebadilika, siwezi kulipia hadi hapo utaratibu mpya utakapoanza. Kwa sasa TANESCO Sengerema wanashughulika na wateja waliolipia zamani na ndio nguzo zao zipo. Naomba kupata majibu au ushauri nifanye nini ili nilipie na nifungiwe umeme mapema?
 
Back
Top Bottom