Umeme ushakuwa wa mgao tena na mbona hamsemi Kimara temboni Saranga yote Ijumaa tarehe 3-7 na leo umeme mnakata saa 4 asubuhi mpaka saa tatu usiku km ni mgao mseme mnaharibu biashara zetu
 
Tanesco leo mmekubwa na nini? Umeme unazima na kuwaka after every five minutes. Hivi kwa mfano vifaa vyetu vya umeme vikiungua kwa sababu ya hayo mambo yenu huwa mna lipa fidia?
 
TANESCO kimara hivi wakazi wa huku tuliwakosea nini?kwanini umeme unasumbua hivi?
Hatukai wiki lazima muanze katakata.Huu mwaka wa 10 sasa tunalalamika humu na mambo yale yale yanajirudia.Nyie mna faida gani kwa nchi ikiwa mmepewa dhamana ya kumletea mwananchi huduma ya umeme na bado mwananchi hapati huduma endelevu,kazi zinaharibika,mnatufilisi uchumi kila siku.
Ukija hapq unaandika majibu yako ya kutia moyo na samahani nyingi ila kesho mwendo ni ule ule kutiana hasara!mss!
Leo hii ni mara ya saba umeme unakatakata Kimara.Tangu saa sita mpaka usiku huu kazi hazifanyiki na maeneo mengine ndio hamjarudisha tangu asubuhi.Hapa Kimara mwisho mnakata mnarudisha mnakata tena...and on..and on...

Siku hazina biashara mtaacha umeme siku nzima,siku wateja wamejaa kibao mnaanza upuuzi wenu huu.Yaani mko kama wachawi nyie,msss!
 
Habari. Nini cha kufanya inapotokea submeter au kile kifaa cha kuingizia umeme kinapopotea? Hatua gani zifuatwe kupata kingine na gharama gani unaweza kuingia?
 
Habari. Nini cha kufanya inapotokea submeter au kile kifaa cha kuingizia umeme kinapopotea? Hatua gani zifuatwe kupata kingine na gharama gani unaweza kuingia?
Ndugu mteja ahsante kwa wasiliana nasi kupitia ukurasa huu, na pole kwa changamoto hio,utaratibu ni kwamba lazima upate loss report kutoka polisi kisha nenda ofisi za tanesco karibu yako utapewa utaratibu mwingine wa kulipia.^EB
 
TANESCO MIMI NI.MKAZI WA KILOMBERO-SIKU ZA NYUMA TANESCO WALIPITISHA WAYA WA UMEME KATIKATI YA UWANJA WANGU LEO NIMEJENGA BOMA NIMEMALIZA NAWAAMBIA WAONDOE WAYA WA UMEME WA UPITISHE KWA PEMBENI ILI NIWEZE EZEEKA MWAKA WATATU SASA NAOMBA MNISIDIE HUKU TUNATESEKA SANAA.
sasa mbona sioni kinachoendelea licha ya kuomba niwatumie details za lalamiko langu inbox
 
mitaa ya ipogolo hukuu mariasili nguzo hamleti kila muda tunashinda kwa mwenyekit jaman tunaomba tuletewe nguzo ipogolo mtaa mariasili machinjio ya nguruwee haiwezekan manspaa harafu kuna sehem umeme hmna
 
mitaa ya ipogolo hukuu mariasili nguzo hamleti kila muda tunashinda kwa mwenyekit jaman tunaomba tuletewe nguzo ipogolo mtaa mariasili machinjio ya nguruwee haiwezekan manspaa harafu kuna sehem umeme hmna
Ndugu Mteja!
Tunafurahia kukuhudumia, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora
Jina
Namba ya simu
Mkoa
Wilaya
Eneo
Namba ya meter
Tatizo
makao makuu 0748550000^NM
 
Ndugu Mteja!
Tunafurahia kukuhudumia, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora
Jina
Namba ya simu
Mkoa
Wilaya
Eneo
Namba ya meter
Tatizo
makao makuu 0748550000^NM
naitwa steve george nipo iringa mjin kata ya ruaha mtaan wa machinjio ya nguruwe /mariasili tatizo nikwamba tanesco hawajaleta nguzo mtaan apa nawalituahid kutuletea toka mwaka jana mwezi wa sita adi sasa hakuna kitu✅
 
Naomba kujua inachukua muda gani kuunganishiwa umeme, nimelipia new connection tangu mwezi wa 11 lakin mpka sasa hakuna majibu yoyote..
0710129170
Kaliua, Tabora
 
naitwa steve george nipo iringa mjin kata ya ruaha mtaan wa machinjio ya nguruwe /mariasili tatizo nikwamba tanesco hawajaleta nguzo mtaan apa nawalituahid kutuletea toka mwaka jana mwezi wa sita adi sasa hakuna kitu✅
Toka lini

Ndugu Mteja!

Tunafurahia kukuhudumia, tafadhali tunaomba namba yako ya ombi la kuunganishiwa umeme ( Application number) kwa ufatiliaji na hatua zaidi.

TANESCO Huduma kwa Wateja

Simu 0748550000. FURAHIA HUDUMA
 
IVI KUINGIZA UMEME NI SHINGAPI IKIWA SEHEMU INAHITAJI NGUZO MOJA??
Ndugu Mteja!

Zifuatazo ni gharama halisi za kuunganishiwa umeme kuanzia tarehe 5/01/2022
• Gharama za kuunganisha umeme mjini ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia moja kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 320,960/=,
• Mteja wa njia moja ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 515,618/=,
• Umbali wa njia moja ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 696,670/=
• Aidha, gharama za kuunganisha umeme mjini ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia tatu kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 912,014/=,
• Mteja wa njia tatu ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 1,249,385/=,
• Umbali wa njia tatu ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 1,639,156/=.
Zingatia
Gharama ya kuunganisha umeme vijijini kwa wateja wa njia moja ni shilingi 27,000/= kama ilivyoelekezwa na EWURA. ^SK
 
Back
Top Bottom