TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Wakubwa hamtoi hata tangazo kututaarifu mtakata umeme asubuhi tuendelee na mambo mengine 😃
 
Wakubwa mmekata umeme bila taarifa yoyote. Wengine tunaonyesha mabanda ya TV bila umeme familia zitashinda njaa.
 
April 24, 2025 majira ya saa 05:28 nilinunua umeme kimakosa badala ya kununua umeme wa tsh 20,000/= nikanunua wa tsh 200,000/=

Tarehe hiyohiyo saa 05:49 nikafanya mawasiliano na Tanesco CC na kujulisha kadhia hiyo kwa qjili ya kurekebisha na kurejeshewa salio langu. Saa 05:55 Tanesco Mkanijibu kwa ushauri ambao sikuupenda kuwa eti niutumie umeme huo kwani ili kurejeshewa ni mlolongo mrefu na itachukua muda mrefu kwa sababu inabidi wahasibu toka Tanesco, Ewura,TRA,na REA inabidi wahakiki na kujiridhisha.

Nilisisitiza kuhitaji REJESHO langu na wapokee saa 0938 nikajulishwa kuwa ombi langu limepokelewa rasmi na kupewa kumbukumbu no 8646O18 Kwa utekelezaji.

kwakuwa nilipewa angalizo kuwa kutakuwa na uchelewaji wa mrejesho jambo ambalo kwa Karne hii ya WASOMI sikubaliani nalo hivyo nikataka nijiridhishe nili ona dalili za Mwanzo kitendo cha kufika nyumbani kwangu ili " waunyonye ule umeme kwa utaalamu wao kulikuwa na uchelewaji mpaka nilivyofuatilia kwenye ofisi zao ndipo wakaja.


Hivyo baada ya kuuchukua huo umeme, nimekaa toka muda huo mpaka 24/7/2025 takribani miezi 3 nikawaandikia sms Tanesco Customer C kukumbushia, jibu nililopata ni kuwa WATAALAMU wameshauri nifike ofisi za wahasibu kwa maelekezo.

Binafsi nilitambua tu, hili lilikuwa jibu la kawaida mno ambalo siyo la kujishughulisha kwa maana nilitegemea nitakapofika kwa wahasibu na kuulizia jibu litakuwa BADO, hivyo jana nilienda kwa wahasibu jibu nililopewa ni kuwa " sisi tayari tumeishawawasilishia mkoani " jibu ambalo nililitegemea .Jambo ambalo TANESCO CC wao ndo wangeweza kuwasiliana na idara zao na kunipa jibu lililonyooka lenye ukweli.

Nikawajulisha TANESCO CC jibu nililopewa na WAHASIBU wao wakanijulisha kuwa niendelee kusubiria wanalifuatilia nikawajibu kuwa ntawakumbusha tena mwezi NOVEMBER 2025.

Narudia tena, siamini, siamini kama Taifa letu, liko hivyo kwamba TEKNOLOJIA hiyo hatuna, uharaka huo hatuna, vijana wapo , wamesoma WAPEWE nafasi watatenda kwa haraka.
.
 
# 8646018 hiyo ni kumbukumbu number mliyonitumia kwa ajili ya taarifa ya tatizo langu toka mwezi APRIL .

Tafadhali nirudishieni fedha zangu.
 
Claim # 8646018 nipeni jibu nahitaji mrudishe fedha zangu miezi 4 inatosha kuelezea BUSSNESS AS USUAL .
 
Tanesco Tanesco Tanesco !! Tafadhali nirudishieni fedha yangu , HAIWEZEKANI dunia ya sasa mkae na fedha zangu kwa miezi 4.

Nasikiliza matangazo yenu mkiwahimiza wateja wenu wenye madeni walipe madeni yao nami NILIPENI fedha zangu.
 
Wafuatao ni vijana waharibifu wa miundombinu ya Tanesco, juzi mida ya saa4 usiku nilipita maeneo ya Toyota Tanzania Nyerere road nikaona vijana kama kumi na mbili hivi wakivuta waya mkubwa mzito kutoka kwenye bomba la chini na kukatakata na kuvusha ng"ambo ya reli ya kuelekea Bugurunin kwa sasa haifanyi kazi na kwenda kuchoma na kuuza, nilipomuuliza mama ntilie mmoja anayeuza chakula eneo hilo akaniambia hao vijana anawajua ni wa hapo Bodi hapo wanachimba Kopa nikataka kujua majina yao kwa siri akanitajia akimaanisha hapendi kile wanachofanya kwa kuwa ni karibu na eneo lake la biashara, akanitajia majina, Muha Kidari huyu ndiye mkubwa wa kazi, Zakayo huyu ndiye mtaalamu wa uteguaji wa umeme, White pamoja na Shamte aliwataja wale maarufu anaowajua lakini kulikuwepo na vijana zaidi ya kumi.
 
Naomba mobile no ya Mh Dotto Biteko naibu waziri Mkuu

Maana Tanesco mmeshindwa kutatua tatizo langu SIWAPENDI.
 
Ninazo taarifa za uhakika kabisa kuna vijana watatu Shamte, Muha kidari, pamoja na Sharo, wamepanga njama za kuchimba na kuharibu miundombinu ya TTCL maeneo ya banda la ngozi Nyerere road hapa pembeni mwa Toyota tz relini, sikuona jukwaa la TTCL ila nimeona niweke hapa ili muwasiliane maana nyote ni taasisi za serikali naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom