TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Wazee hivi ikitokea tuna share meter watu zaidi ya mmoja halafu mmoja wetu akasafiri na kuacha amefungia kile ki mita cha kujazia umeme sisi wengine tunaingizaje umeme
Habari ndugu mteja,

Asante kwa swali. Ikiwa mnatumia mita moja kwa pamoja na kifaa cha kuingizia token (CIU) kimechukuliwa na mmoja wa watumiaji anayesafiri, mnaweza kuwasiliana na TANESCO Huduma kwa Wateja kwa msaada wa kupata ufumbuzi wa namna ya kuingiza token bila kifaa hicho.

Tafadhali tueleze Eneo ulilopo, namba ya mita na namba ya simu kwa msaada zaidi.

Asante.^PK
 
Nisababu gani inafanya umeme kukatika kila wakati,hata mara tatu kwa siku hapa Dumila morogoro?
Habari ndugu mteja,

asante kwa kuwasiliana na TANESCO huduma kwa wateja na pole kwa changamoto hiyo, tafadhali fahamu kuwa mara tunapolazimika kusitisha huduma ya umeme kwa ajili ya matengenezo yaliyopangwa au hitilafu za ghafla, huwa tunatoa taarifa mapema pamoja na maelezo ya sababu ya usitishwaji wa huduma.
Taarifa hizi hutolewa kupitia kurasa zetu rasmi za mawasilianao, ikiwemo ujumbe mfupi (SMS) pamoja na makundi ya WhatsApp yaliyogawanywa kulingana na maeneo.
lakini pia tufahamishe jina la Kata, Mtaa, karibu na kitu gani maarufu na namba ya simu kwa msaada zaidi.^HN
 
Serikali inahamasisha matumizi ya nishati safi lakini TANESCO mnaihujumu serikali kwa kukatakata umeme tena mida kama hii tuko jikoni tunapika. Radiant cookers na induction cookers zinahitaji umeme na mnapokatakata umeme mnatuharibia majiko yetu. TANESCO kuweni serious, karne ya 21 bado umeme mnakatakata!!!
 
Serikali inahamasisha matumizi ya nishati safi lakini TANESCO mnaihujumu serikali kwa kukatakata umeme tena mida kama hii tuko jikoni tunapika. Radiant cookers na induction cookers zinahitaji umeme na mnapokatakata umeme mnatuharibia majiko yetu. TANESCO kuweni serious, karne ya 21 bado umeme mnakatakata!!!
Habari ndugu mteja.

Asante kwa kuwasiliana nasi na pole kwa changamoto hiyo, tafadhali tufahamishe Mkoa, Wilaya, Kata, Mtaa na namba ya simu kupitie inbox yetu kwaajili ya msaada zaidi.^RS
 
Back
Top Bottom