TANESCO mnatuangusha sana...nimejenga nyumba ya kupangisha nimemaliza nasubiri umeme wapangaji waingie lakini TANESCO KIGAMBONI hawaeleweki nimelipia kila kitu...nikiiangalia nyumba naumia sana ...
Kwanini msiruhusu wawekezaji kwenye mita kama nyie zinawashinda? Mama kasema mnapokwama ombeni msaada
 
TANESCO mnatuangusha sana...nimejenga nyumba ya kupangisha nimemaliza nasubiri umeme wapangaji waingie lakini TANESCO KIGAMBONI hawaeleweki nimelipia kila kitu...nikiiangalia nyumba naumia sana ...
Je umelipia kiasi lini? Kwa jina gani na namba ya simu tafadhali
 
Tafadhali fika na umeme huo ofisi za eneo lako kuna form maalumu utajaza kwa hatua zaidi
Mkuu, wilaya ya mbogwe ktk mji wa masumbwe yapata wiki sasa tuna tatizo kubwa la Umeme, yaani Umeme ukirudi nusu saa unakatika tena masaa matano, kwa sisi wajiriamali tunaotegemea Umeme vipato vyetu vimeyumba kabisa, kiasi kwamba tumeanza kumkumbuka rais magufuli mapema sana make ktk utawala wake hatukuwahi kupata kero za namna hii.
 
Tunashukuru kwa taarifa tafadhali onyesha namba yako ya simu kwa ufatiliaji zaidi
 
Mbona mnauza nguzo kwa wateja wapya wakati waziri Kalemani anasema nguzo ni bure ?
 
Mbona mnauza nguzo kwa wateja wapya wakati waziri Kalemani anasema nguzo ni bure ?
Je umeuziwa wapi? Hakuna mteja anayepaswa kulipia nguzo bali mteja analipia gharama za kuunganishiwa umeme
 
Je umeuziwa wapi? Hakuna mteja anayepaswa kulipia nguzo bali mteja analipia gharama za kuunganishiwa umeme

Nipo Mwanza ,offisi zenu za Mkolani, saveya kaja Kapigia hesabu mpaka za Nguzo naambiwa nguzo Tatu zitanigharimu sio chini ya Milioni 1.5 , offisini naambiwa nikiwa tayari kulipia niseme nipewe quotation nilipie,
 
Ni siku ya tatu sasa tangu nguzo zimeanguka hapo mombo na kila linapoulizwa watu wanajibiwa kwamba eti head ofsi imekataa kutumia nguzo zilizopo kwa sababu zina kazi maalum, pamoja na hayo kila tatizo la nguzo likitokea hapa huchukua week nzima kudhughulikiwa.

Je, meneja wa Tanesco mkoa wa Tanga unajua haya wafanyayo wadogo zako yana akisi utendaji wako?
 
TANESCO Kimara kama kawaida yao.
Jinsi mlivyo mahiri katika kuvuruga mambo.

Mmesubiriiii leo sikukuu watu wako misikitini na kwenye sherehe mmezima umeme.

Usiku saa nane mlikata,asubuhi hii mmekata tena.

Watanzania mko vizuri sana kwenye mambo haya.
You are best at this!Congratulations.
 
Tafadhali onyesha Kimara eneo gani na namba yako ya simu
 
Tafadhali onyesha Kimara eneo gani na namba yako ya simu
Umerudi sasa hivi.
Ni Kimara mwisho yote umeme ulikatwa.
Ila wakazi wa kimara tunaomba embu fuatilia ujue kuna tatizo gani la muda mrefu Kimara.Umeme unakatikatika sana na haijaanza leo,ni tatizo la kihistoria.
Tusaidieni.
 
Kuunganishiwa umeme huchukua muda gani kutoka siku mtu aliyolipia?..
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM
 
Back
Top Bottom