TANESCO Njooni huku kwenye uzi wa kawaida mtoe majibu, au anzisheni uzi wenu ili uunganishwe na huu ili mtoe majibu ya kuridhisha
Mkuu hata wakija hapa unadhani ndio watakubali kuwa kuna mgao, wakija watapiga porojo tuuh kuwa ni matengenezo kama walivyosema jana kwenye TV sijui gas ilikuwa inavuja lakini wamerekebisha ila sababu hawajui kuwa njia ya muongo ni fupi pamoja na kufix hiyo leakage ya gas ila umeme unaendelea kukatika kama kawa, so kama wakija kujibu hapa usitegemee jipya toka kwao mkuu, Nawaonea huruma sana watanzania haswa wale wenye biashara zinazotegemea nishati ya umeme.
 
Khabarini wadau muda huu naandika uzi huu kama nusu iliyopita mpaka sasa umeme umekatika.Nachojiuliza ni kuwa mgao wa umeme umerudi nchini ama nini ? na kama umerudi si wautangazie umma wa watanzania waelewe kinachoendelea.

Hii wanafanya kama siri kwa manufaa ya nani kwa sababu sisi wananchi ndio tumewaweka madarakani ila kwa nyendo za hapa karibuni hili suala la umeme imekuwa kero kwa wananchi mbalimbali. Hivi hivyo viwanda mnavyohimiza vijengwe vitaendeshwa kwa kutumia nini kama hali ya umeme ndio hii .

Wanasiasa kuweni wa kweli kwenye mambo ya maana mnakaa kimya ila kwenye upuuzi ndo mnatoaga matamko yenu ya kipuuzi puuzi.

Kama kazi imewashinda mrudisheni Prof. Muhongo maana kwa kipindi chake tatizo la kukatika ovyo kwa umeme halikuwepo na tulianza kusahau suala la kukatika ovyo kwa umeme.
Nawasilisha
 
Huku Mwanza UMEME hakuna tangu asubuhi na hatujapata maelezo yoyote pia MAJI imekuwa ni kawaida kukatika kila siku wakati Ziwa tunaliona hapo na hakuna maelezo yoyote kwa nini hakuna maji, yaani hizi taasisi mbili ni pasua kichwa sijui hivyo viburi wanavitoa wapi..!!
 
Yaan aibu....mnashinda kata 42 inatusaidiaje sisi tunaohitaji umeme kuendeshea shughuli zetu za kipato?sijaelewa bado.kila siku tunaomba radhi sijui kuna shida wapi....ina maana hawana uwezo wa kuiendesha Tanesco basi wapewe wawekezaji kwa ubia na serikali au la wahuruhusiwe wawekezaji kuna kuwekeza kwenye umeme nakwambia tutahama wote na tanesco itakufa kabisa
 
Watanzania bhana, unauliza chooni kunanuka nini wakati unatoka huko huko?

Matendo hukidhi maridhiwa kuliko maneno shekh....

Mgao sio mpaka tuambiwe, umesahau wamejitoa kwenye serikali yenye uwazi?

Unataka watangaze mgao ili nao waonekane wameshindwa?

Hii ni serikali ambayo iko KIKI-ORIENTED.

NB: Arusha Sakina umekatika saa tatu asubuhi.
 
saa 4 kamili tabata ushakatika. ngoja tuone utarudi saa ngapi? mkurupukaji ni mkurupukaji sana...laiti kama angejua asingetafuta kiki kwa profesa muhongo. yule profesa kweli siyo profesa wa maganda ya korosho.
Yaani hadi kero... mtu unasema upumzike home mara paap umekatika...
 
Watu wasijulikana wanajua sababu zisizojulikana za matatizo ya kukatika kwa umeme kwa muda usiojulikana.
 
Nchi ya condom inatabu sana. Imagine uko kwenye treni halafu umeme unakatikia kibaha porini huko
nimecheka km mazuri
Hata Babati ( Manyara ) wamekata toka saa 4 asubuhi na haueleweki mara urudi mara ukatike ni taflani.
Viwanda bila umeme naona inawezekana.
 
Tanesco hamna kitu nchi imewashinda.... Si bora mseme ukweli kama kujiendesha hamuwezi? Kila siku mchana kuanzia sa mbili hasubuhi hadi sa tano mnakata umeme tatzo ni nn?
 
Hivi kuna watu bado mnatumia umeme wa Tanesco? Kiukweli mimi nimezoea nina wiki ya Tatu nimekataa umeme wao na nijipanga nipate umeme wangu wa uhakika
 
Inawezekana usemacho ni kweli kwanini wasitoe taarifa?
Na hili tatizo mbona hii ni wiki ya pili umeme una katikakatika hovyo??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…