TANESCO kuzima Umeme siku 2 kwa saa 12 (Agosti 26 -28 2023), Mikoa 15 gizani

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
WhatsApp Image 2024-03-05 at 17.08.13_6e0cefbe.jpg
Shirika hilo la Umeme limesema njia ya umeme itakayozimwa ni kutoka Kidatu kwenda Kihansi kwa siku mbili kuanzia Agosti 26 hadi 28 2023

Umeme utakuwa wa mgawo kwa Saa 12 kuanzia Saa 1 Jioni hadi 12 Asubuhi huku Mikoa ya Njombe, Ruvuma na Mbeya ikitarajiwa kuathirika

Mikoa mingine ni Dodoma, Singida, Manyara, Arusha, Shinyanga, Kilimanjaro, Simiyu, Tabora, Mwanza, Geita na Iringa

Vipi Mdau, umejiandaaje kukabiliana na Mgawo huo?
 
Wale ambao tuliambiwa hawakufanya kabisa service kwa miaka mitano wanaenda kuwazidi ufanisi hawa waliofanya.😁.

Ni suala la muda tu kabla huu mgao kuwa rasmi wa bila kikomo,si juzi hapa nchi nzima ilikuwa gizani wakapiga porojo.

Toka jana kuna maeneo kibao tu mkoa wa Shinyanga hayakuwa na umeme 12hrs bila taarifa.

Hii wizara haiendi kwa porojo na propaganda,watasema tu ukweli au ukweli utasema wenyewe.
 
Jiulize mvua zote zilizonyesha mwaka huu .....wanakosa kisingizio sasahivi wanasingizia marekebisho....hakika aliyenacho ataongezewa na asiye nacho atapokonywa alichonacho ndio haya yanatukuta leo maana umeme ukishakua wa mgao yamaanisha sisi masikini tufe na umasikini wetu sababu bila umeme hakuna mzunguko wa fedha
 
Back
Top Bottom