Suala la Kitila na Mfanyakazi wake wa Ndani

Status
Not open for further replies.
Kitila, hujifanya mtu serious sana kwenye issue za watu, sasa yu wapi. Hiyo idara ya saikolojia ina mambo. Ni juzi juzi mmoja wa idara hiyo kafukuzwa kazi kutaka kumbaka mzungu mmoja mwanafunzi, itakumbukwa miaka ya nyuma kuwa Prof mmoja maarufu alidaiwa kutaka kumbaka mwanafunzi. Wanasaikolojia kulikoni?
 
Kitila kumbe jamaa wanakuonea tu hujatafuna wala nini duh WaTZ bana kwa kukuza ishu....sasa Kitila huyo binti yupo kwao Singida au yupo Dar? Nataka nimfanyie mpango Nyani Ngabu awe house girl wake hahahaha
 
Mazee unasema 'hajatafuna' ..ina maana wewe ndiye Mh.Daktari ? Kama sio wewe umejuaje kwamba 'hajatafuna'? Halafu mwisho unamalizia kwa kumfanyia dhihaka huyo binti aliyehusishwa na hiyo kadhia, hivi angekuwa dada yako wa tumbo moja ungesema maneno hayohayo uliyoyaandika?
 
Si wote tunakubali maelezo ya mtu bila kuswalisha pale ambapo mambo hayajumlishiki. Na si kila anaeswalisha basi ametoa madai. Aliyetoa madai ndio anadaiwa ushahidi. Hadithi ya Kitila ina loose ends.

Kitila kadai msichana alichoka Uingereza. Ukichoka kazi unaenda polisi?

Akadai alimwambia ni sawa kwenda polisi kama aliona ameonewa. Alidai ameonewa kwa kitu gani?

Kitila anatuambia Ubalozi walimwambia tatizo la mshichana ni kuishi Uingereza. Yeye Kitila mwenyewe anajiweka kama haelewi elewi kilichoendelea ndani mwake, eti balozi ndio ajue zaidi. Tusifanyane watoto.

Fundi, thread ya kumpongeza Kitila kwa udaktari sii hii, imo humu sehemu, pongezi zitafiti huko zaidi.

Ni vizuri na ni wajibu wetu sote kuuliza maswali pale ambapo hatujaridhika na lolote bila kujali nani anahusika. Kwenye hilo hamna mjadala na nina heshimu sana msimamo wako huo.

Kwangu mimi zote ni speculations. Kitila hakusema kuwa binti alichoka bali ni taarifa alizopewa na kuthibitishwa na binti alipomuuliza. Kuna namna nyingi za kuchoka. Inawezekana alikuwa home-sick. Inawezekana hali ya maisha nyumbani kwa Kitila hakuridhika nayo, tukikumbuka kuwa Kitila alikuwa mwanafunzi. Na kadhalika, na kadhalika. Na inawezekana kuwa huko kunakoitwa kuchoka ni fig leaf ya sababu halisi. Inawezekana binti alienda polisi ili apate msaada wa kuweza kuishi uingereza nje ya wigo la wakina Kitila. Yote haya yanawezekana.

Tuhuma walizotoa wakina Kyaruzi ni nzito na nazo zinahitaji substantiation. Kama kesi ilifikishwa ubalozini basi bila shaka kuna watu wanaoishi huko wanaweza kuthibitisha. Kama kesi bado ipo mahakamani, wanaweza kutuambia ni mahakama gani, case file n.k. Kudai kuwa mke wake Kitila ndiye alimdeport huyo binti sio kweli. Huyo mama hana mamlaka ya ku-issue deportation order. Vile vile hana uwezo wala mamlaka ya kumuondoa uingereza bila binti mwenyewe kuridhia kwa namna moja au nyingine. Ninavyojua hata ubalozi wetu uwezo huo hauna kwa mtu anaeishi uingereza kihalali.

Dilunga, hauwezi kum'fault' Kitila kwa kumwambia binti kuwa ana haki ya kwenda polisi kama anaona ameonewa. Ni binti anaetakiwa kuona kuwa hajatendewa haki na si Kitila ili aende polisi. Kutaka Kitila atuambie binti alihisi alionewa vipi si kumtendea haki.

Kitila kutokujua kinachoendelea nyumbani kwake, unfortunately, si ajabu kwetu wanaume wakiafrika. Wengi nyumba tumemwachia mama na sisi kujiweka pembeni. Wangapi hawajui hata matatizo yanayowasibu wanao, itakuwa mfanyakazi wa ndani? Kama alivyosema Obama, we need to get more involved kwenye maisha ya wanaotuhusu. Wengi hatuko hivyo.

Kitila si aliyeleta hii habari. Yeye alijibu tuhuma zilizoelekezwa kwake. Basi ni wajibu kwa hao waliozileta kututhibitishia uovu na uongo wa Kitila na si otherwise.

Kama Kitila alifanya anachodaiwa kufanya, yaani kutembea na mfanyakazi wa ndani halafu kutomtendea haki ilipojulikana, anastahili laana zetu wote. Lakini vile vile tukumbuke kuwa tuhuma kama hizi zimetumiwa sana kuwabomoa wale tuliotofautiana nao. Ni wanaume wengi tu wamesulubiwa kwa sababu tu wameonekana wakimtendea haki mfanya kazi wao wa ndani wa kike hata bila kutembea nae. Pengine ni kuogopa hili ndiko kulikomfanya Kitila akae mbali na huyo binti.

Nakumbuka Capo Kuhani ( sijui kama ulimkuta humu jamvini) aliwahi kushutumiwa kutembea na hausigeli wake alipokosana na mmoja wa wanachama wa jamvi hili. Hata mimi nimewahi kushutumiwa hivyo.

Asante kwa kunisahihisha kuhusu sehemu ya pongezi. Bahati mbaya pamekuwa na utitiri wa mabandiko kiasi cha kutufanya wengine tuchanganyikiwe.

Amandla...........
 
Sasa hapo tatizo ni kwamba hawakumueleza hali halisi ambayo atarajie kuikuta.
Kama ulieleza hali halisi hiyo haitakuwa shida tena. Watu ambao wapo wawazi katika kueleza kwa kinagaubaga kamwe hawatakutana na hii hali.

Watu wanatofautiana. Shukuru Mungu umempata anaeelewa. Usidhani ni kwa sababu yako tuu bali ujue hulka ya huyo mfanya kazi wako nayo imechangia kwa kiasi kikubwa.

Amandla.......
 
Mazee unasema 'hajatafuna' ..ina maana wewe ndiye Mh.Daktari ? Kama sio wewe umejuaje kwamba 'hajatafuna'? Halafu mwisho unamalizia kwa kumfanyia dhihaka huyo binti aliyehusishwa na hiyo kadhia, hivi angekuwa dada yako wa tumbo moja ungesema maneno hayohayo uliyoyaandika?

Mkuu nenda page 3 nafikiri amequote Maxence maelezo ya Kitila rudi usome vizuri alivyo eleza ishu hapa ni kwamba Kitila hajatafuna kama wengi wanavyo fikiri maelezo mazuri yanajitoshelesha.
Angekuwa dada angu ningempa tu Nyani Ngabu awe shemeji yangu tu jumla kama hata taka afanye kazi kwake....kwani ukiwa na dada unategemea nini mkuu?
 
Mosi, hakuna sehemu yeyote kwenye hii thread ilipothibitishwa madai yako. Kwa hiyo wewe kaa chini utulie wakati mada inazidi kuchambuliwa. Huwezi kuutumia utetezi wa mtuhumiwa kama ushahidi uliothibitishwa bila kuzingatia vyanzo vingine, unless uniambie you are not aware of this simplest of the commonest of logic.

Pili, si busara kumuelezea huyo binti aliyehusishwa na hii ishu kwa minajili ya kuolewa kwa 'kumpa' NN au kuwa housegirl. Mazee kumbuka kama hujafa bado hujaumbika na hamna binadamu ambaye hapendi kula bata bali ni majaaliwa tu ndio yanatufanya tuwe tofauti ndo maana mwingine muuza mkaa, mwingine mchoma vitumbua ili mradi tu maisha yanaenda mbele. Sijui kama umenisoma.
 
Mkuu napingana na wewe katika hili. Inategemea wakati huyu binti unamleta huku Ulaya mmekubaliana mambo gani na kama mlikuwa na mkataba mahalum. Mia nina miaka mingi tu hapa UK pamoja na familia yangu na kwa kipindi hicho chote nimekuwa na binti wa kazi wa kutoka Tanzania na kabla ya kumleta huku tuliandikishana mkataba wa nini atarajie pamoja na staha zake zote na kadhalika. Na sijawahi kumsikia hata siku moja akilalamika kuhusu lolote la ziada.
Cha msingi ni kuwa na mkataba wa kisheria kabla ya yeye kuja huku Ulaya na yeye aridhie makubaliano kwa upande wake na vile vile mwajiri kutekeleza wajibu wako.
Mtu wa Kawaida,

Kama wewe umefanikiwa kumleta mfanyakazi wa ndani na kukaa naye miaka yote bila matatizo basi hongera sana.

Nafikiri hata wewe unajua kwamba kwa walio wengi hali haiko hivyo. Tatizo kubwa ni kwamba kwa kipato cha wengi wetu hatuwezi kuwalipa hao wafanyakazi mishahara ambayo inatosha na inaendana na sheria za nchi hii na hapo ndipo huwa mwanzo wa matatizo.

Nakubaliana na wewe kwamba kwa vyovyote kuna watu ambao wameweza kukaa na hao wafanyakazi inavyotakiwa lakini pia ni ukweli mtupu kwamba kuna familia nyingi zimeshindwa kukaa na hao wafanyakazi na imeishia kuwa matatizo.
 
Mimi niliongea na TAWA na wanasema case ya Dr. Kitila haikufika kwao.

Ina maana ni ubalozi wa TZ ndio walishughulikia na wao ndio wanaweza kusema waliambiwa nini na huyo msichana.

Bado ushauri wangu ni ule ule, kama mtu unakuja kusoma au kufanya kazi, jiepushe kabisa na hao wafanyakazi wa ndani. Labda kama ni ndugu ambaye unamsaidia ili atumie nafasi hiyo na akifika huku aendelee na mambo yake.

Ukileta mfanyakazi wa ndani na ukamtreat kama tunavyofanya kule nyumbani kwa kweli utaishia tu kwenye matatizo.

Mimi niwe TZ au Ulaya, kazi zangu nafanya mwenyewe, kwa kweli sihitaji house girl. Bibie akitaka house girl sharti ni moja tu, awe tayari kumtreat kama mtoto/mdogo wake mwenyewe, vinginevyo sihitaji mfanyakazi wa ndani nyumbani kwangu.
 
Kisheria Dr Kitila HANA kesi ya kujibu kwa sababu mlalamikaji wala jamhuri ya mamlaka ya UK hajaithibitisha mashtaka yeyote hadi sasa dhidi ya mtuhuhumiwa,na habari za kusikia maarufu kama hear say hazina nguvu kisheria na mimi kama kawaida yangu nazitupilia mbali!
 
Awali ya yote napenda kukupongeza Dr. Kitila Mkumbo kwa kupata degree hiyo kihalali na kwa nguvu zako, huku mwenyezi Mungu akikupa uzima na uwezo wa kufanya hivyo. Sijafanikiwa kusoma alishopost Kyaruzi bali nimejaribu kupitia post zote na ile ya Kitila through Maxence. Hii ni tuhuma nzito na ya kchafua personality ya binadamu yoyote yule ambaye anapenda kuheshimu na kuheshimiwa. Ninavyofamu huko UK or most of the developed nations masuala ya uyaya/hg ni serious sana, katika haki zake za msingi. Katika maelezo ya Dr. Kitila haijaonyesha kama binti alikosa haki kama mshahara na mambo yote ambayo walikuwa wamekubaliana, bali naona ni kuhitilafiana kati ya Mrs Kitila na binti. Ninapenda tujiulize yafuatayo:

1. Je binti alikuwa anapata stahili zake kama mshahara? Nionavyo ni ndiyo. Kwani halijajitokeza katika maelezo bali alichoka maisha ya UK!!! Je kuchoka maisha ya mahali ni kwenda polisi au kuongea na mwajiri uondoke? Au kama ni ajira rasmi then unatafuta mwajiri mwingine. Nafikiri kuna tatizo lingine, nje ya allegations za sexual harassment!! Kwa binti au mfanyakazi yeyote kama ana heshima ni lazima aondoke au kuacha kazi kwa busara, binti huyo hakuwa na nidhamu.

2. Je unafahamu kuwa mabinti wengi wao ni waongo sana? Ni kawaida ya mabinti wengi wa kazi pale ambapo wanataka kondoka na hawana sababu ya msingi, huwa wanasingizia kwa majirani kuwa mara silipwi mshahara, mara mama/baba mwenye nyumba yuko vile na vile, ili mradi tu wapate sympathy kwa majirani au kwa yule mwajiri mpya mtarajiwa. Kama unatafuta binti ukikutana na ambaye anaelezea past employer kwa ubaya fahamu na kwako atafanya vile vile. Kwa mantiki hii, je binti hawezi kusingizia kuwa kafanyiwa ubaya hasa kama walipishana na mama mwenye nyumba??? Na ili kuwakomoa akaanza kusambaza uvumi kuwa nimekuwa de-ported kwa kuwa mama anahisi natembea na baba!!! Huwa wengi wanafanya hivyo, hawana aibu.

3. Je yawezekana kuwa mama alishtuka pia mwonekano wa binti na mazoea kwa mume kuwa ni hatari kwa ndoa na akaama ku-deport???? Hii pia yawezekana. Nataka tufahamu kuwa mabinti wengi wa kazi wa kileo huwa wana agenda mbili kuu, kumpata baba mwenye nyumba na/au kutengeneza mazingira ya wizi yeye binasfsi au na mtandao wake!!! Haya yamefanyika kwa nyumba nyingi na nyingine ni za marafiki zangu. Fahamuni kuwa kuna makabila ambayo huwa wanafundishwa kuwa ni lazima uhakikishe baba mwenye nyumba unamchukua, niwieni radhi na Singida hasa Wanyiramba ndiyo wanaongoza kwa hili. Tafadhali niwieni radhi ila ndiyo ukweli wenyewe maana tuna uzoefu nao kwa ndugu zetu na marafiki. Kwa DSM kuna nyumba ambazo nina uhakika na nimeshuhudia mabinti wa Kinyiramba wakimwondoa kabisa mke ndani, na mbaya zaidi wanatumia hata waganga wa kienyeji. Na kwa sasa ugonjwa huu umesambaa kwa mabinti wengi wa kazi. Noamba binti akija kwako, mwambie mkeo awe anafanya several secret checkups za suitcases au kabati la nguo, utajionea mwenyewe. Naomba uanze leo.

4. Je nafahamu kwa wanaume wengi idara ya house girls ni ya mke?? Hii ni kwa waafrika hasa watanzania wengi. Na ukiona mume anakuwa karibu na housegilr ni abnormal na inabidi mama anze kuchunguza kwa ukaribu!!! Unless mke ametoa kwa mume habari za house gilr si rahisi mume kuzifahamu na hasa kama binti anafanya kazi yake sawasawa. Binti anapokuwa mjeri au na tabia sugu ambayo ni hatari kwa familia ile ndipo baba anapewa taarifa. Kwa mantiki hii yawezekana Mrs. Mkumbo alikuwa anahitilafiana na binti kwa mambo madogomadogo na hakuchukua hatua kumtarifu Dr. Mkumbo na yakajengeka na binti akashindwa ku-take up sasa option ikawa ni kutaka kuondoka kwa nguvu na bila ustaarabu kama alivyofanya. Binti ni mjeuri nakuambia.

5. Je tujiulize, huyu binti alikuwa UK kwa muda gani?? Ana umri gani?? Kwa mabinti wa kileo, ngono huwa wanaanza wakiwa na umri mdogo sana!!! Sasa sijui huyu wa familia ya Kitila alikuwa virgin au alishazoea kulamba asali na sasa kaikosa??? Kama alishazoea kulamba asali akiwa Tz na kama aliacha bwana au mchumba Tz ni lazima baada ya muda atatamani hayo mambo na atatafuta mlango wa kutokea, uwe wa heri au shari. Hivi katika hali ya kawaida wewe, yule na mimi je, sexual pleasure si sehemu ya maisha yetu??? Imagine umekosa hiyo kitu kwa kipindi fulani jinsi ambavyo unaweza run mad!!! Tuwe wakweli hapa, japo stamina zinatofautiana hapa, wengine hata siku tatu zikipiata bila kupata ile tunda kichwa kinauma??? Je natania hapa!!!?? Tuwe fair pia kwa hawa mabinti, tunapenda kuwafuga mno bila hata kwapa off wakatoe uchovu. Mpe Sundays or Saturdays off at least kila mwezi kama ana ndugu akapumzike. Tatizo ni la wale wa kijijini tunao na hawana ndugu, hivyo wataishia kwa houseboy wa jirani. Hata hivyo uchaguzi ni wake, mruhusu awe anatoka kidogo kujifanyia shopping, itampungzia usongo. Sasa huko UK kama binti hakupata hata a soulmate sasa huoni ni tatizo, ni lazima akimbie. Tena fahamu kuwa makabila mengine wanaogopa sana umri wa kuolewa kupitiliza!!!!

7. Je tumeshapata uthibitisho kuwa Dr. Mkumbo alifanya tendo la ndoa na huyu binti au tuseme kuwa alikuwa ni hawara wa ndani kwa ndani?? Hakuna aliyeweza ku-prove hili. Kwanza kuweka habari kama hii ni kuharibu kabisa reputation, credibility and personality na binadamu. Issues kama hizi zinahitaji kuhakikiwa kabla ya kupost hapa. Wewe ndungu aliyeleta mada bila hard facts naomba utoke hadharani uiombe JF radhi na Dr. Kitila Mkumbo msamaha maalum. Kitila ninamfahamu na misimamo yake pia, si mtu wa short-cuts!! Huenda kuna personal hatred hapa!!!!! Kama gentlemen hatuendeshi mambo kihivi. Tutumie zaidi busara. Tusipende kuchafuana hasa pale ambapo tunajua mtu ni potential kama Dr. Kitila Mkumbo, pengine unaogopa atakuingilia mambo nyeti fulani au?? Samahani sana kwa wale ambao wameamini kuwa Dr. Mkumbo anaweza kufanya such low move na tushikamane wale wote ambao wanalaani uharibifi uliokusudiwa na mwanzisha tread ya kumchafua mpiganaji mwenzetu. Long live JF.
 
Kwani kufanya mapenzi nje ya ndoa ni kosa kisheria?

mkuu kama unafikia kujiuliza hivyo itabidi kwanza niwe sooo doubtful na age yako au kama upo ktk ndoa.

Shekhe. Hilo ni kosa kubwa sana kama ushahidi upo kwani umekiuka kiapo. nadhani unaelewa maana ya kiapo.
 
......
7. Je tumeshapata uthibitisho kuwa Dr. Mkumbo alifanya tendo la ndoa na huyu binti au tuseme kuwa alikuwa ni hawara wa ndani kwa ndani?? Hakuna aliyeweza ku-prove hili. Kwanza kuweka habari kama hii ni kuharibu kabisa reputation, credibility and personality na binadamu. Issues kama hizi zinahitaji kuhakikiwa kabla ya kupost hapa. Wewe ndungu aliyeleta mada bila hard facts naomba utoke hadharani uiombe JF radhi na Dr. Kitila Mkumbo msamaha maalum. Kitila ninamfahamu na misimamo yake pia, si mtu wa short-cuts!! Huenda kuna personal hatred hapa!!!!! Kama gentlemen hatuendeshi mambo kihivi. Tutumie zaidi busara. Tusipende kuchafuana hasa pale ambapo tunajua mtu ni potential kama Dr. Kitila Mkumbo, pengine unaogopa atakuingilia mambo nyeti fulani au?? Samahani sana kwa wale ambao wameamini kuwa Dr. Mkumbo anaweza kufanya such low move na tushikamane wale wote ambao wanalaani uharibifi uliokusudiwa na mwanzisha tread ya kumchafua mpiganaji mwenzetu. Long live JF.

point ya saba ni mustkee kabisa kwani siku hizi nyumba ndogo huishi ndani ya nyumba kubwa ili kubana matumizi....

labda... labda nasema labda
 
7. Je tumeshapata uthibitisho kuwa Dr. Mkumbo alifanya tendo la ndoa na huyu binti au tuseme kuwa alikuwa ni hawara wa ndani kwa ndani?? Hakuna aliyeweza ku-prove hili. Kwanza kuweka habari kama hii ni kuharibu kabisa reputation, credibility and personality na binadamu. Issues kama hizi zinahitaji kuhakikiwa kabla ya kupost hapa. Wewe ndungu aliyeleta mada bila hard facts naomba utoke hadharani uiombe JF radhi na Dr. Kitila Mkumbo msamaha maalum. Kitila ninamfahamu na misimamo yake pia, si mtu wa short-cuts!! Huenda kuna personal hatred hapa!!!!! Kama gentlemen hatuendeshi mambo kihivi. Tutumie zaidi busara. Tusipende kuchafuana hasa pale ambapo tunajua mtu ni potential kama Dr. Kitila Mkumbo, pengine unaogopa atakuingilia mambo nyeti fulani au?? Samahani sana kwa wale ambao wameamini kuwa Dr. Mkumbo anaweza kufanya such low move na tushikamane wale wote ambao wanalaani uharibifi uliokusudiwa na mwanzisha tread ya kumchafua mpiganaji mwenzetu. Long live JF.

Kitila kummega housegirl wake itakuwaje low move? Kumega ni jambo la kujivunia bana labda uniambie alimbaka. Mimi hongera zangu bado ziko palepale. If anything Kitila amedhihirisha yeye ni rijali. Go Kitila.
 
NN... kila baada ya few posts, unakumbushia kwamba jamaa kamega!!! huo uchokozi na mnyiramba mie simo maana moto wake hauna extinguisher aisee

Get the mask and gloves bro...
 
NN... kila baada ya few posts, unakumbushia kwamba jamaa kamega!!! huo uchokozi na mnyiramba mie simo maana moto wake hauna extinguisher aisee

Get the mask and gloves bro...

Sijaleta mimi hizo habari. Kichwa cha mada kinasema Kitila na mfanyakazi wake wa ndani. Sasa kama hamtaki watu tuzungumzie yeye kummega housegirl wake ifungeni hii mada. Msinilaumu mimi kwa kujadili mada zilizoanzishwa na wengine
 
Kuna mada ilianzishwa juu ya sakata la kitila mkumbo na mfanyakazi wake wa ndani hapa jf lakini imefutwa,
jee kitila mkumbo ni nani hadi asijadiliwe?

Jf tunadai ni watetezi wa wanyonge lakini tunashindwa kumsaidia dada wa toka singida aliyedhulumiwa na kunyanyaswa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom