Wakuu, wengi mnanielewa tabia zangu hapa wengine kupitia key board, wengine hata uso kwa uso. Tatizo ni hizi accusations ambazo mwenzetu hapa kazitoa. Nisichoelewa ni nini hasa tuhuma hapa, maana yeye mwenyewe hakuwa wazi. Unapotoa tuhuma inabidi uwe wazi kwenye tuhuma zenyewe na uweke na ushahidi wako bayana. Sasa mtu anatoa tuhuma kimafumbofumbo, inakuwa kama una something personal, yenye mwelekeo wa personal vendeta hivi. Anyway, kwa faida ya wana JF, nitaeleza tukio lenyewe, then nyie muamue kama sisi tulimnyima huyo binti haki zake au la.
Nilipokuwa TZ kwa ajili ya tafiti September 2008, mke wangu alinipigia simu kutoka UK akiwa anatetemeka na kunieleza kuwa mfanyakazi wetu wa ndani (house girl) alikuwa ametoroka nyumbani na alikuwa hajui ameenda wapi. Nilishtuka maana mtoto wa watu kutoroka nchi za watu ni jambo la kutisha. Ilinibidi nirudi haraka UK kwa ajili ya kushughulikia hili jambo. Nikiwa uwanja wa ndege nasubiri kupanda ndege mke wangu akinipigia tena akiniambia kuwa binti amerudi akiwa na polisi. Polisi walimkabidhi nyumbani na kueleza kwamba wao baada ya kumsikiliza hawakuona kwamba kesi ile ni ya polisi, na kwamba walikuwa wameshatoa taarifa kwenye ubalozi wetu London waweze kulishughulikia. Polisi walieleza bayana kuwa hawakuona dalili zozote za binti kunyanyaswa; walichoelewa wao ni kwamba yule binti alikuwa amechoka kukaa UK na alikuwa anataka arudi nyumbani.
Niliporejea UK niliwasiliana na ubalozi, na kunieleza kuwa, kwa maneno ya afisa wa balozi niliyeongea naye "binti alikuwa amepishana na mke wako na angependa arudi nyumbani, na kwamba alienda polisi kuomba msaada wa kurudishwa TZ kwani alikuwa amechoka kukaa UK". Ubalozi ukanishauri nimrudishe binti nyumbani. Nami nilipomhoji binti akathibitisha kwamba anataka arudi nyumbani. Aliomba msamaha kwa kwenda polisi na kwamba alipelekwa na mtanzania mmoja aliyekuwa anaishi Southampton. Nilimweleza kuwa huna cha kuomba msamaha, maana polisi ni mahala pa haki na ulikuwa na haki kwenda huko kama uliona umeonewa. Tukampa kilichokuwa chake, nikamkatia ticket tukamkabidhisha kwa mtanzania mwenzetu aliyekuwa anakuja Dar akarudi na akabidhiwa kwa wazazi wake ambako anaishi hadi leo.
Kwa kadri mimi nijuavyo hakuna kesi yeyote iliyopo polisi wala ubalozi wetu nchini Uingereza ya kunihusu mimi.
PS: Tunapoletewa tuhuma za kuwahusu watu sisi nasi tuwe tunazimumunya kidogo. Katika hali ya kawaida ni kesi gani itakayokaa polisi wa UK kwa zaidi ya miezi sita isiende mahakamani? Na kama sisi tungekuwa na kesi kweli, tungeruhusiwa vipi kuondoka na kurejea nyumbani bila hatima ya hiyo kesi kujulikana? Na je mtoa hutuma ana habari yeyote pegine kama kesi hiyo basi imehamishwa Tanzania?