Spika Ndugai: Bunge lisilaumiwe kwa kupitisha sheria ambazo baada ya muda mfupi zinarudishwa bungeni kufanyiwa marekebisho

Kinuju

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
2,390
5,310
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema kuna changamoto ya baadhi ya Mawaziri na Mwanasheria mkuu wa Serikali (AG) hali inayosababisha baadhi ya sheria kurejeshwa tena bungeni kurekebishwa muda mfupi baada ya kupitishwa.

Ndugai alitoa kauli hiyo jana Jumamosi Oktoba 30, 2021 wakati akifunga mafunzo ya siku mbili ya Mawaziri na Naibu Mawaziri yaliyoandaliwa na taasisi ya uongozi.

"Wakati mwingine unaona hii aah, lakini waziri anang’ang’ana kwa kawaida wabunge watasema sawa ipite ukienda huko hata miaka miwili haishi unarudi na amendment (marekebisho),” amesema akisisitiza kuwa ndio maana kila mkutano wa Bunge kuna muswada wa marekebisho ya sheria.

Chanzo: Mwananchi
 
Wasisingizie mawaziri, kuna Muswada wa mapato ya gesi na mafuta 2015. Bunge tena spika alitumia nguvu sana muswada ujadiliwe na upitishwe tena kwa hati ya dharura wakati ni jambo nyeti.

Nakumbuka wapinzani walipinga ila walifukuzwa na kuitwa "makuwadi wa mabeberu" sijui wanapinga kila kitu n.k

Fast forward 2017, JPM aliuita ule muswada ni wa kifisadi. Hapo hapo Ndugai akapokea ammendments za ule muswada na akadai "wabunge walipitiwa" n.k. Huu unafiki wa wana CCM ndio umefikisha taifa hapa lilipo.

Bunge la ndiooo ni udhaifu wa bunge, maana wao ndio wanaisimamia serikali sasa kama mawaziri wanawaforce then bunge ni dhaifu kama alivyosema CAG Assad!!
 
Ndugai aulizwe je kwa dharula ambayo serikali hupeleka miswada bungeni, yeye binafsi anapata muda wa kuisoma? Au na yeye huruhusu kwa mtindo wa mwanaharamu apite!
 
Nani alaumiwe?? Sasa

Daaah tz tusafar ndefu Sana
Mlipitisha nyie lkn hamtaki kulaumiwa??
 
Tulisema mkimalizana na upinzani mtaanza kumalizana wenyewe kwa wenyewe. Na bado
 
Asante Mh. Ndugai kuwa mkweli miongoni mwa sababu million madai Katiba Bora.
 
SPIKA NDUGAI ATOA KAULI 'WABUNGE WASILAUMIWE KWA KUPITISHA SHERIA AMBAZO BAADA YA MUDA MFUPI HUREJESHWA BUNGENI KUFANYIWA MABADILIKO"

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema kuna changamoto ya baadhi ya mawaziri na mwanasheria mkuu wa Serikali (AG) hali inayosababisha baadhi ya sheria kurejeshwa tena bungeni kurekebishwa muda mfupi baada ya kupitishwa.

Ndugai alitoa kauli hiyo jana Jumamosi Oktoba 30, 2021 wakati akifunga mafunzo ya siku mbili ya mawaziri na naibu mawaziri yaliyoandaliwa na taasisi ya uongozi.

"Wakati mwingine unaona hii aah..., lakini waziri anang’ang’ana kwa kawaida wabunge watasema sawa ipite ukienda huko hata miaka miwili haishi unarudi na amendment (marekebisho),” amesema akisisitiza kuwa ndio maana kila mkutano wa Bunge kuna muswada wa marekebisho ya sheria.

Chanzo: Mwananchi

1635729648458.png
 
Nduguyao, jukumu la wabunge ni kuwasahihisha au kuwadhibiti hao mawaziri, hivyo mswada mbovu hautakiwi kupita hata kama mawaziri anauona unafaa, ikiwa macho ya wengine wameiona hafai au unamapungufu, Ndio maana kuna kuwa na mijadala. Na kupigiwa "kula" sasa kama hilo halifanyiki ina maanisha bunge linakimbia jukumu lake la kuidhibiti serikali "check and balances"
 
Back
Top Bottom