Marekebisho Sheria ya Huduma za Habari: Serikali kuwa na uhuru wa kuchagua chombo cha habari itakachokitumia kwa ajili ya matangazo

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Bunge limepitisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali ikiwemo Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016

Akiwasilisha hotuba yake bungeni, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Eliezer Feleshi amesema kifungu cha 5 cha Sheria ya Huduma za Habari, Sura ya 229 kinapendekeza kufanya marekebisho kwa lengo la kumwondolea Mkurugenzi wa Idara ya Habari jukumu la uratibu wa matangazo yote ya Serikali.

Pia, amesema marekebisho hayo yataiwezesha Serikali kuwa na uhuru wa kuchagua chombo cha habari itakachokitumia kwa ajili ya matangazo kwa kuzingatia nguvu ya ushindani katika soko.

“Inapendekeza kukifanyia marekebisho kifungu cha 38 kwa madhumuni ya kuongeza haki na uhuru wa maoni. Muswada unapendekeza marekebisho ya vifungu vya 50, 51, 53, 54, 55, 63 na 64 kwa madhumuni ya kuweka adhabu tahafifu kwa makosa yatokanayo na ukiukwaji wa sharia hii,” amesema Feleshi.

AG amesema mapendekezo ya marekebisho ya vifungu hivyo yanakusudia kuondoa adhabu kwa wamiliki wa mitambo ya uchapishaji ambao katika hali ya kawaida hawana uwezo wa kudhibiti maudhui yanayochapishwa katika mitambo hiyo ya uchapishaji.

Waziri Nape Nnauye amesema kwamba kwenye sheria hiyo, wameondoa jinai ili kuijenga tasnia ya habari ikue. Ameongeza kwamba baadhi ya mambo walikubaliana kwamba yakafanyiwe kazi kwenye kanuni ambazo zitatungwa hivi karibuni ikiwemo suala la leseni na muda wa leseni.

Credit: Mwananchi
 
Upande wa Radio, Clouds FM ina nguvu kubwa.

Social Media, Millard is miles away.

Hivyo, serikali iingie ubia na hao wawili. TBC ikufe.
 
Naona wanatengeneza mazingira ya kuhonga vyombo vya habari kwa njia ya kunyima tenďa chombo kitakachokua hakiwi upande wao.

Wanajua mpango mbaya walio nao juu ya taifa hili wanafanya kila mbinu kujilinda.
 
Back
Top Bottom