Spika Ndugai: Bunge lisilaumiwe kwa kupitisha sheria ambazo baada ya muda mfupi zinarudishwa bungeni kufanyiwa marekebisho

Nduguyao, jukumu la wabunge ni kuwasahihisha au kuwadhibiti hao mawaziri, hivyo mswada mbovu hautakiwi kupita hata kama mawaziri anauona unafaa, ikiwa macho ya wengine wameiona hafai au unamapungufu, Ndio maana kuna kuwa na mijadala. Na kupigiwa "kula" sasa kama hilo halifanyiki ina maanisha bunge linakimbia jukumu lake la kuidhibiti serikali "check and balances"
Ametudhihirishia kuwa hana say mbele ya mawaziri wakimkomalia. Kuna faida gani ya kupeleka miswada bungeni?
 
Anaongea nini huyu!! anathibitisha kuwa aliyosema prof. Assad kuwa kweli tena kweli tupu

Swala ni waziri kung'ang'ania au bunge kuchambua hoja na kufanya maamuzi sahihi kwamanufaa ya watu na taifa kiujumla?

Kumbe kweli ni rubber stamp tuu hao,kwao ni kupitisha kilicholetwa. AIBU, AIBU TENA AIBU KUUUUUBWA.

Kweli hatuna taasisi huru hapa ni fedheha tupu!

Kwanza alidai rais akisema yeye ninani mpaka abishe! Aki refer ishu ya bagamoyo. AIBU.

Pili akadai sheria zilipita yeye ama kalala ama kasafiri. Tunamlipa mamilioni akalale bungeni?? Akisafiri huwa anawaachia mazuzu ofisi?

Sasahivi anadai mawaziri wanang'ang'ania!!! Eti wao wanaona sio sahihi lakini wanasema basi sasa sheria ipite!!

Kazi ya bunge nikutunga sheria anatuambia wasilaumiwe wanapotunga sheria mbovu kwakuwa sio wao. Sio wao wanaotunga sheria wameporwa haki hiyo sasa ni mawaziri ndio hutunga sheria so tuwahoji wao mawaziri bunge hupitisha tuu wanavyoletewa.

VERY BIG BIG SHAME, WHAT A SHAMELESS LEADER

TUNAHITAJI KATIBA MPYA HARAKA, TUSICHELEWESHWE NA MAZUZU
 
Nduguyao, jukumu la wabunge ni kuwasahihisha au kuwadhibiti hao mawaziri, hivyo mswada mbovu hautakiwi kupita hata kama mawaziri anauona unafaa, ikiwa macho ya wengine wameiona hafai au unamapungufu, Ndio maana kuna kuwa na mijadala. Na kupigiwa "kula" sasa kama hilo halifanyiki ina maanisha bunge linakimbia jukumu lake la kuidhibiti serikali "check and balances"

Mbona walishasema wanafanya kazi kwa kushirikiana au umesahau?
 
Kuna mhimili mmoja umechimbiwa chini zaidi- Jiwe 2016
Nduguyao, jukumu la wabunge ni kuwasahihisha au kuwadhibiti hao mawaziri, hivyo mswada mbovu hautakiwi kupita hata kama mawaziri anauona unafaa, ikiwa macho ya wengine wameiona hafai au unamapungufu, Ndio maana kuna kuwa na mijadala. Na kupigiwa "kula" sasa kama hilo halifanyiki ina maanisha bunge linakimbia jukumu lake la kuidhibiti serikali "check and balances"
 
Ile dhana ya "Bunge linatunga sheria" ni muda muafaka kwa watu kuifuta mawazoni mwao ( kwa wale wanaofikiri hivyo)
 
Wakati mwingine kukaa kimya huwa ni vizuri zaidi, Kwa kifupi tu tanzania hatuna bunge bali tuna interest za watu
 
Wakati mwingine kukaa kimya huwa ni vizuri zaidi, Kwa kifupi tu tanzania hatuna bunge bali tuna interest za watu
Wananchi wanategemea maendeleo katika uongozi wa aina hii. Bila kuitoa CCM madarakani hata Msumbji watatupita kama China na Korea zilivyo tuacha.
 
SPIKA NDUGAI ATOA KAULI 'WABUNGE WASILAUMIWE KWA KUPITISHA SHERIA AMBAZO BAADA YA MUDA MFUPI HUREJESHWA BUNGENI KUFANYIWA MABADILIKO"

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema kuna changamoto ya baadhi ya mawaziri na mwanasheria mkuu wa Serikali (AG) hali inayosababisha baadhi ya sheria kurejeshwa tena bungeni kurekebishwa muda mfupi baada ya kupitishwa.

Ndugai alitoa kauli hiyo jana Jumamosi Oktoba 30, 2021 wakati akifunga mafunzo ya siku mbili ya mawaziri na naibu mawaziri yaliyoandaliwa na taasisi ya uongozi.

"Wakati mwingine unaona hii aah..., lakini waziri anang’ang’ana kwa kawaida wabunge watasema sawa ipite ukienda huko hata miaka miwili haishi unarudi na amendment (marekebisho),” amesema akisisitiza kuwa ndio maana kila mkutano wa Bunge kuna muswada wa marekebisho ya sheria.

Chanzo: Mwananchi

#edwinmoshiupdates

View attachment 1994084
Bunge linajua kabisa hii Sheria itawaumiza Wananchi ambao ndio waliowachagua kuwa Wabunge linapitisha hill ni Bunge Zuzu na ndio Maana Bunge hilo tunastahili Wabunge wake kuitwa MAZUZU
 
Back
Top Bottom