Uchaguzi 2020 SPECIAL THREAD: Taarifa za Kampeni na Sera za Mgombea Urais kupitia CHAUMMA, Hashim Rungwe Sipunda

Napendaga sana kumsikiliza huyu Mzee, anahoja zake akitoa huku anachanganya na maneno flani hivi ya shombo + comedy flani,...Yaani full burdaaaniiii
 
Ndugu Spunda kweli namwelewa.. binafsi tokea mwaka umeanza najikuta nimekula spea za kuku tu ambazo nikiziunganisha hata kuku hatimii hivyo kukosa ladha ya kuku halisi. Kwa hiyo naunga hoja mkono!
 
Mkuu usilete utani, Mgombea wetu Mh Rungwe amezungumzia kwa undani sana umuhimu wa Lishe na faida zake kwa Taifa...Juzi wizara imetoa takwimu na kuelezea tatizo la udumavu kwa Watanzania na namna linavyoitesa jamii..

Sisi kama Chauma kupitia Mgombea wetu Mh Hashim Rungwe tunakwenda kutokomeza tatizo la lishe duni ili Taifa lijengwe na watu wenye lishe..
 
Wakuu,

Mzee wetu Hashimu Rungwe tumuunge mkono wale wote ambao tunajua utamu wa ubwabwa na nyama au ubwabwa na maharage. Sijui ataongeza na walau chai ya rangi?...
Nami naunga mkono hoja, twende na Hashimu Rungwe Spunda!
 
Nakuelewa sana Mzee wangu.

Na kama ulivyosema jana inawezekana kula wali kuku sio issue. Kama tunakula kuku kutoka mpaka Brazil kwa elfu 5000/-hatushindwi kuwazalisha wenyewe.

Inawezekana pia kilo ya mchele ikauzwa sh 400/- Kama mbuga nzuri za kulima mpunga toka Magu mpaka Kwimba, Misungwi mpaka salawe mahembe,mwakitolyo, kagongwa.mpyagula loya mpaka nyahua. Ugalla majimoto mpunze mpaka Ubaruku. ukiwawezesha vijana maeneo haya kilo ya mchele ni sh 400/-

Nikushauri Umchague Jummane Kishimba awe waziri wako mkuu.

Tunatoboa.
 
Back
Top Bottom