Mkutano wa Kitaifa wa wadau wa Demokrasia: AveMaria asema viti maalumu havina tija, kumuweka mwanamke kwenye kundi maalumu ni udhalilishaji

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
1692712622630.jpeg

Demokrasia ya vyama vingi nchini Tanzania ilianzishwa mwezi Julai 1992. Tangu wakati huo, serikali imejitahidi kukuza utawala wa kidemokrasia kupitia marekebisho ya kisheria na mikataba ya kukuza demokrasia. Hata hivyo, kuna changamoto za kidemokrasia.

Kuna makubaliano kati ya wadau wa kisiasa juu ya umuhimu wa kufanyia marekebisho Katiba ya 1977, Tume ya Uchaguzi, Sheria ya Vyama vya Siasa, Sheria ya Uchaguzi, na masuala ya vyombo vya habari na ushiriki wa kijinsia. Hatua zimechukuliwa kuanzisha Katiba mpya, lakini mchakato ulisitishwa mwaka 2014. Mikutano ya kisiasa ilipigwa marufuku kati ya 2016 na 2023.

Hata hivyo, mwaka 2022, Rais Samia Suluhu alianzisha Kikosi Kazi kwa ajili ya marekebisho ya kidemokrasia. Kufuatia ripoti ya kikosi hicho, marufuku ya mikutano ya kisiasa iliondolewa na kuanzia Januari 3, 2023. Marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi na Sheria ya Vyama vya Siasa yaliongezwa kwenye ajenda, na mkutano uliitishwa kuandaa marekebisho.

Hali ya sasa inahitaji mazungumzo ya kitaifa kuimarisha makubaliano ya kitaifa. Ingawa wadau wanaweza kutofautiana katika mitazamo, wanaweza kukubaliana kuhusu maslahi ya kitaifa. TCD inaendesha mkutano wa wadau kujadili demokrasia na uchaguzi, kufuatia juhudi za Rais Samia. Mkutano utafanyika Agosti 2023.

Mkutano wa awali wa TCD ulijadili marekebisho ya uchaguzi, matokeo yake yalipendekeza marekebisho ya Sheria za Uchaguzi na Vyama vya Siasa, na kuimarisha ushirikiano wa vyama vya siasa. Mkakati wa kudumisha amani ya kisiasa ulijadiliwa pia.

Mkutano wa wadau wa kitaifa utalenga kukuza demokrasia katika nchi. Malengo yake ni kujenga jukwaa la mazungumzo, kujadili mafanikio na changamoto za demokrasia, kufuatilia utekelezaji wa maazimio ya mkutano wa awali, na kutoa mapendekezo kwa mustakabali. Washiriki watakuwa viongozi wa vyama vya siasa, wanazuoni, mashirika yasiyo ya kiserikali, na wadau wengine.

1692712651908.jpeg

===
Katika kipindi cha mchana mada ni Ushirikishwaji wa makundi mbalimbali katika masuala ya kiuongozi na kisiasa.

Moderator ni Adv. Anna Kulaya - WiLDAF
Wazungumzaji ni
  1. CCM Women Wing(UWT) - Hawa Ghasia
  2. CHADEMA (BAWACHA)
  3. CUF Women Wing(JUKECUF) - Anna Lyoba
  4. ACT Wazalendo Women Wing (NGOME YA WANAWAKE)- Doroth Semu
  5. NCCR-Mageuzi Women Wing (JUMUIYA YA WANAWAKE)
  6. CHAUMMA Women Wing (JUMUIYA YA WANAWAKE) - Zaituni Hashim Rungwe
  7. ULINGO - Avemaria Semakafu
  8. TGNP/ WFT-T
Alivyozungumza kutoka BAWACHA
Amesema CHADEMA imeanisha namna ambayo kunakuwa na uwiano wa uwakilishi wa makundi maalumu ikiwemo wanawake na watu wenye mahitaji maalum. Amesema CHADEMA ipo kwenye mchakato wa kuhakikisha watu wenye ulemavu wanaingia katika Katiba, kuanzia ngazi ya chini hadi kamati kuu.

Aidha amekubali kuwa ushiriki wa wanawake katika ngazi ya vyama hauko vizuri.

Aliyoongea Anna Lyoba kutoka CUF
Amesema katika utaratibu wao wa chama wamehakikisha wanawake wameshika nafasi za juu ikiwemo masuala ya fedha na haki za binadamu katika chama. Aidha katika baraza kuu la chama kuna uwiano sawa wa wajumbe wanawake na wanaume, pia wajumbe hao ni wajumbe kwa kugombea. Aidha katika kugombea uongozi wa kitaifa CUF inaacha nafasi tatu ili kumpa fursa mwanamke kushiriki katika uchaguzi wa kitaifa.

Aidha katiba ya CUF amesema inaruhusu hata katika nafasi kumi za wajumbe zinaweza kuchukuliwa na wanawake tu.

Alichosema Zaituni Hashimu Rungwe kutoka CHAUMMA
Amesema wanawake wengi wanawoga, hivyo inaathiri utashi wao wa kisiasa, hivyo ni muhimu kutoa elimu kwa wanawake ili waweze kujitokeza kugombe nafasi mbalimbali za uongozi ngazi za kitaifa na ngazi za chama.

Katika mapendekezo ya nini kifanyike, Zaituni amesema elimu kwa umma inahitajika kwa wanawake ili waweze kushiriki uchaguzi. Pia polisi waache uonevu ili kuhakikisha wanawake wanajisikia salama kushiriki uchaguzi.

Alichokisema Doroth Semu - ACT-Wazalendo
Amezungumzia uduni wa mifumo ambayo inakuwa changamoto kwa ushiriki wa wanawake na watu wa makundi maalumu katika majukwaa ya maamuzi. Lakini amesema hili suala ni la kijamii zaidi hivyo ni muhimu kwa kutoa elimu kwa ngazi ya jamii.

Pia amezungumzia mazingira finyu ya kisiasa kwa watu wa makundi maalumu na wanawake. Aidha mazingira ya siasa sio salama kwa kuwa mwanamke anataka kuona mazingira salama. Wanawake wanaingia woga kuona wanawake wenzao wanakamatwa na polisi kwa kujihusha na siasa.

Aidha masuala ya rasilimali fedha ni changamoto nyingine kwa wanawake kujihusisha na siasa kwa kuwa hata katika ngazi ya familia maamuzi ya rasilimali fedha yametawaliwa na mfumo dume. Hali inayompa vikwazo vya kushiriki katika siasa.

Pia amesema wanawake wana uchumi mdogo hali inayofanya awe na kizungumkuti cha kujua kipi akipe kipaumbele kati ya siasa au kuendeleza uchumi.

Aliyosema Valentina Robert kutoka NCCR-Mageuzi.
Amesema wanawake wana woga, yaani hawajiamini katika kushiriki michakato ya kisaisa. Aidha amesema hata jamii na wazazi hawawafungulii watoto wa kike wanaomaliza vyuo vikuu ili waweze kushiriki katika siasa.

Pia amesema hakuna kiongozi anayepewa uongozi kama hana sifa ya uongozi. Amesema hata kama ni mwanamke kama hagombei hawezi kupata kiongozi.

Aliyosema Hawa Ghasia wa CCM
Nilikuwa naangalia takwimu za Wagombea Ubunge kuanzia mwaka (2010 - 2015), mwaka 2010 wanawake 18% tu waligombea , 2015 ilikuwa 19%, 2020 walikuwa 23% sasa hapo unategemea utafike 40% kama nyie wenyewe mna idadi ndogo? Upande wa Madiwani Wanawake CCM waligombea 6.6%, CHADEMA 5.1%, ACT-Wazalendo 4%, NCCR-Mageuzi walikuwa 9.4% sasa kama tangu kwenye uchukuaji wa fomu asilimia iko chini tutafikaje huko kwenye ngazi za juu?

Amesema hakuna utashi wa kisiasa uko chini. Ametolea mfano kwa CCM wanajitahidi kuwapa fursa wanawake ambapo mwanamke akigombea hata akiwa wa pili au wa tatu basi huchukuliwa ndio agombee na wa kwanza kama ni wa kiume anaachwa.

Changamoto nyingine aliyoitaja ni Viti Maalumu ambapo wanawake wengi huanza kuangalia viti maalumu na kuacha kugombea ili kuonesha utashi wao wa kisiasa. Amesema yeye aliwahi kugombea ubunge na kupata ambapo wanawake wenzake hawakugombea waliacha tu apambane mwenyewe na alifanikiwa kupata ubunge. Amesema kugombea kwake alishinda kwa kura nyingi kwa ngazi ya chama.

Hivyo ametoa wito kwa wanawake wenyewe kujuamini na kuweka utaratibu ambao utafanya wanawake wasije kujiona wanyonge. Aidha amesema katika katiba waliyopendekeza ni kufikia 50% kwa 50%, aidha ametoa mfano wa sasa kuwa Spika wa Bunge ni mwanamke, na limeshawahi kuongozwa na mwanamke.

Alichokisema Ave Maria Semakafu
Tatizo kubwa tulilonalo ni kupambana na mfumo ambao umeendelea kuwepo hapa Tanzania. Wanawake wamekuwepo kwenye vyama lakini je kwenye vyama kuna demokrasia, Avemaria amesema vyama havina demokrasia.

Avemaria, amesema wanawake sio kundi maalum. Kwa kuwa wanawake ndio wengi nchini na wanakaa kusubiri fungu kutoka kwa makundi ya wachache. Amesema kwanza kuanza kwa msingi wa kuondoa wanawake katika tafsiri ya kundi maalumu ili kuwa na wanawake na wanaume kisha kuanza kuyatambua makundi maalumu kama vijana, wazee na wenye mahitaji maalumu. Kumuita mwanamke ni kundi maalumu ni udhalilishaji.

Amesema turekebishe mfumo ili kuhakikisha wanwake wanaishi kama watanzania kwa usawa. Amesema suala la ubunge wa viti maalum hauna tija. Ubunge wa viti maalumu ni kama kilema, kwa kuwa mwananchi hawezi kukutana na wananchi lazima uombe ruhusa kwa wabunge wanaume. Hii ndio inafanya wanawake wanashindwa kutoka kwa kuwa akienda jimbo ataambiwa anaiba jimbo.

MDAU AKOSOA MKUTANO KUTOKUWA NA USHIRIKI WA WATU WENYE ULEMAVU
Kwa kuwa mjadala huu ni kuhusu ushiriki wa makundi maalum, mdau kutoka SHIVYAWATA amekosoa mazingira ya mkutano huu kuwa si rafiki kwa watu wenye ulemavu, kwanza hata wazungumza mada wamegusia zaidi wanawake na hakuna mtu mwenye ulemavu aliyetajwa. Aidha hakukuwa na mtaalamu wa lugha ya alama ili aweze kusaida ujumbe kueleweka kwa watu wenye uziwi kama angekuwepo kwenye mkutano huu.

Akizungumzia ushiriki wa watu wenye ulemavu kwenye siasa, amezungumzia hata magari hayana nafasi nzuri za kuweka wheelchairs ikiwa mgombea ana ulemavu. Katika mapendekezo amesema walishawasilisha kwa raia kuhusu baadhi ya vitu kufanya.
 
Back
Top Bottom