Sofia Simba na Sakata la Mafisadi na Wapiganaji!

Sofia Simba na Sakata la Mafisadi na Wapiganaji!

Pasco,
Kwa jinsi ulivyoandika ni kama vile tuna options mbili tu, EL na JK. Nadhani tunweza kupata watu makini kuliko hawa. EL, ni mchapata kazi, hilo halina ubishi lakini ufisadi 'upo kwenye damu'. Hili la pili linafanya hata uchapaji kazi wake usiwe na manufaa kwa taifa. Bado sijashawishika, ni kwa vipi Tz bado inamwitaji EL.
Asante sana SMU, kwa kweli nafurahi kwa dhati kuwakuta baadhi ya wanabodi ambao ni objective na wenye total impartiality, ambao they dont take sides. Kwanza nakuunga mkono, EL ni mchafu na hasafishiki, kibaya zaidi, ni wanaotaka kumsafisha uchafu wa tope kwa maji tka ya cesspit, watantia na harufu mbaya kabisa, aishie kunuka. Pili we dont need him, lakini pia naomba lets not all be carried out na wanaojiita wapignaji, kwa sababu wengine sio kwa maslahi ya taifa, ni visasi na agenda za 2015.

Mimi sikufurahishwa na alichofanyiwa Salim, 2005 lakini ndio hivyo, jamaa wamefanikiwa na watendaji wameukwaa ulaji. Hawa wapiganaji wakifanikiwa its even worse.

Good leaders are groomed, lets groom good sucession system ili tusitoe mwanya kwa maoportunist kama kina Dr.Mwaki. Hebu angalia potentals za watu kama kina Zitto, Nape, Seleli etc. Tusichaguane kwa sura au kwa kambi bali kwa merrits
 
Mkuu katika hii thread umtoa maneno mazito sana. Naona picha jinsi gani tulivyo mbali ki siasa na kuleta maendeleo tanzania. Yani nachokiona tunahitaji kuanza upyaa kabisaaa.Sasa hivi kumekua hamna mipango endelev, nikama tunaziba mianya tuu.Kila siku EPA sijui nini...sijui nini, mpaka inakera mkuu.

Hamna kitu cha kufanya tuanze upyaa kabisa..tuwe tuna concentrate na service delievry na kuleta maendeleo nchini?

Nashindwa hata kuelewa tuanze wapi, inakatisha tamaa.
 
..jeuri ya kusema yote hayo anaitoa wapi?

..isije ikawa Sophia Simba, pamoja na rushwa ya kufa mtu aliyotumia kupata uwenyekiti wa UWT, ni kati ya wana-CCM "wasafi."

..kwa maana nyingine inawezekana humo ndani ya CCM kuna mijitu michafu kwelikweli kiasi kwamba they can tolarate kunyooshewa kidole na Sophia Simba.
 
Pasco said:
Mwanakijiji, be fair to Sophia Simba, mbona husemi kasema nini jana?. Kwa kusaidia huyu mama katapika mbovu, kaiponda ripoti ya kina Mwakiembe haikuwa ya nia njema. Kamponda mama Kilango kuwa alikuwa akiuza madawa ya kulevya. Kaponda Mzee Malechela kwa kampeni yake kuutafuta urais ilifadhiliwa na Jeethu Patel fedha za ufisadi wa Epa. Kamponda Spika Sitta ndiye aliyeileta Richmond alipokuwa TIC, Kaisoma barua nzima ya Kashilila kwenda Takukuru kuhusu Posho mbili na kuonyesha unafiki wa Spika Sitta, kathibitisha wamefanya uchunguzi na kuthibitisha hakukuwa na rushwa kwenye richmond, ndipo kashauri ufanyike uchunguzi huru kuweka mambo sawa. Hili ndilo kosa lake?.

..mhh!!
 
[Mtu wa namna hii lazima atakuwa na dosari kubwa sana, hasa kama kabila lenyewe ni Mndengereko...

...kabila gani liko serious?
 
Date::11/5/2009CCM yafika pabaya waziri awalipua Malecela, Mwakyembe, Anne Kilango
broken-heart.jpg
Na Daniel Mjema,Dodoma

MALUMBANO makali yameendelea kuitikisa Kamati ya rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi baada ya makombora ya juzi kuelekezwa kwa Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango na mumewe, mzee John Malecela.

Kamati hiyo imekuwa ikipokea mashambulizi makali baina ya wabunge ambao wanaonekana kuwa vinara wa vita dhidi ya ufisadi na wale ambao wanaona kuwa vita hiyo inawalenga, kiasi cha kurushiana tuhuma nzito zilizo na mwelekeo wa kuchafuana.

Baada ya kulipuana Jumanne, juzi ilikuwa zamu ya Mama Kilango na mumewe Malecela wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba alipotoa tuhuma nzito akidai kuwa wawili hao pia wamekula fedha za ufisadi.

Habari kutoka vyanzo vyetu zilieleza kuwa Simba alidiriki kudai kuwa hata harusi ya makamu huyo wa zamani wa CCM na Kilango ilifadhiliwa na mtuhumiwa wa ufisadi, Jeetu Patel.

Patel kwa sasa ana kesi katika Mahakama ya Kisutu akituhumiwa kuiibia Benki Kuu (BoT) kwa kuchota takribani Sh11 bilioni kutoka katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA).

Akijieleza kwenye kamati hiyo, Simba alimtuhumu Malecela, ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu katika serikali ya awamu ya kwanza, kuwa wakati akiwania kuteuliwa kugombea urais kwa tiketi ya CCM mwaka 2005, Jeetu Patel alimpa Sh200 milioni kwa ajili ya kampeni zake.

Malecela, ambaye wakati huo alikuwa makamu mwenyekiti wa CCM, aliondolewa mapema kwenye mbio za urais, ikiwa ni mara ya pili baada ya kuenguliwa tena mapema mwaka 1995.

Waziri huyo mwenye dhamana ya utawala bora akiwa na taasisi nyeti kama Takukuru na Idara ya Usalama wa Taifa, alizidi kurusha makombora kwa wanandoa hao, akisema Mama Kilango ni mnafiki na sio msafi kiasi cha kuwanyooshea wengine vidole wakati harusi na kampeni zake za ubunge zilifadhiliwa na mtuhumiwa huyo wa ufisadi.

Habari zinasema kuwa Mama Simba alikuwa akizungumza kwa kujiamini na kwa ujasiri na kumtuhumu Mama Kilango kuwa kelele zake zote zinatokana na nongwa ya “kuukosa U-first lady (kuwa mke wa rais).”

Alieleza kuwa kelele zote za mbunge huyo wa Same Mashariki zinatokana na chuki na uchu wa madaraka na si kweli kwamba ni mpinga ufisadi, kwa mujibu wa mtoaji habari wetu.

Lakini Patel, alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo za Waziri Simba kwamba alifadhili harusi ya Malecela na kampeni zake za urais, alionekana kustuka na kusema: "Haa...we nani kakwambia... Bwana ehee, mimi sijui lolote kuhusu hayo.

"Kwa sasa mimi najiangalia mwenyewe, nina matatizo yangu mengi nahangaika nayo."

Hata alipofafanuliwa kwamba, maneno hayo yalisemwa na Waziri Simba, alijibu: "Kama wao wamesema wenyewe huko, mimi sijui."

Naye Kilango alisema alishuhudia wakati wakati makombora hayo yakirushwa na kueleza kwamba anajiandaa kujibu mapigo.

Mbunge huyo machachari alisema anajua kwamba mambo yote yaliyosemwa, yanamlenga yeye na si mumewe Malecela.

"Mimi ni mwanasiasa... andikeni yote yaliyozungumzwa bila ya kuacha baadhi na siwezi kuwashtaki," alisema Kilango.

Mzee Malecela hakutaka kuzungumzia lolote kuhusu tuhuma hizo wakati alipoulizwa juu ya uhusiano wake na Patel na kama aliwahi kupokea kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kampeni.

"Ahaa... kijana naomba uniache nipumzike," alisema Malecela.

Mbali na mzee Malecela na mkewe, Waziri Simba pia alimgeukia mwenyekiti mtendaji wa IPP, Reginald Mengi akimtuhumu kuwa anaendesha vyombo vya habari vinavyoichafua CCM na serikali yake kwa maslahi yake binafsi.

Pia alimshambulia mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe na mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, akiwatuhumu kuwa ni watu wenye njaa na kwamba, wanalipwa fedha kufanya kazi hiyo.

Waziri Simba alisema kuwa hata tuhuma dhidi ya mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge na mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, zimetokana na chuki binafsi.

Simba alisema kuwa uchunguzi wa kashfa ya rada ulishamalizika na Chenge akasafishwa na kuongeza kwamba hata uchunguzi wa Richmond umebaini kulikuwa hakuna rushwa, kwa mujibu wa mtoaji habari wetu.

Suala la Richmond liliibuka tena mbele ya kamati hiyo ya Mwinyi wakati mbunge wa Bukoba Vijijini, Nazir Karamagi alipolalamika kuwa ripoti ya kamati teule ya Bunge iliyoozwa Dk Mwakyembe haikumtendea haki.

habari hizo toka ndani ya kikao hicho zinaeleza kuwa Karamagi alisema ripoti ya Richmond ilionea baadhi ya watu na akapendekeza iundwe tume huru kupitia mchakato huo kuona kama wana makosa ili haki itendeke.

Mbunge huyo ambaye alijiuzulu uwaziri baada ya Lowassa kuachia wadhifa wake wa waziri mkuu kutokana na kashfa hiyo, alisema maamuzi yake kuhusu Richmond yalitokana na mapendekezo ya Bodi ya Tanesco.

Naye Dk Mwakyembe alijibu hoja iliyotolewa Jumanne na mbunge wa Ukonga, Dk Makongoro Mahanga aliyedai kuwa ripoti ya Richmond ni 'feki', akisema tatizo la Dk Mahanga ni uelewa mdogo.

Kuhusu hoja ya Karamagi, Dk Mwakyembe alisema malalamiko yake si sahihi kwa sababu yapo maeneo mengi ambayo Karamagi alishiriki na yako bayana hayahitaji mjadala.

Aliwatahadharisha Wabunge kuacha kudodosa sana ripoti ya Richmond kwani watazidi kumchafua Lowassa na kwamba wanaweza kufungwa kwa sababu upo ushahidi dhahiri.

Dk Mwakyembe aliwataka viongozi wa CCM wenye tuhuma kuiga mfano wa Mzee Mwinyi aliyejiuzulu baada ya mauaji yaliyofanywa na vyombo vya dola mkoani Shinyanga.

Akizungumza mbele ya kamati hiyo, kwa mujibu wa vyanzo vyetu, alimshambulia spika wa Bunge, Samuel Sitta akidai kuwa kama si mizengwe, suala la Richmond lingemalizwa kwa taratibu za kichama.

Habari hizo zinadai kuwa Chenge, aliyewahi kuwa mwanasheria mkuu wa serikali, alisema Lowassa alizungukwa na kwamba kulikuwa na njama za kummaliza ingawa hakusema njama hizo zilifanywa na nani.

Chenge aliitetea serikali ya awamu ya tatu kuhusu kuingia mikataba mibovu na kusisitiza hakukuwa na uzembe kwani mikataba yote ilipitiwa na kukubaliwa na Baraza la Mawaziri.

Hata hivyo, mbunge wa Muleba Kusini, Wilson Masilingi alisimama na kuomba kutoa taarifa na kumwomba Mzee Mwinyi na kamati yake wawabane wabunge wanaodai wanasema ukweli.

Masilingi alipinga maelezo ya Chenge kuhusu mikataba na kusisitiza kuwa maelezo yake yalijaa ushabiki na kusema Baraza la Mawaziri liliridhia mikataba kutokana na ushauri wake (Chenge).

Mbunge wa Kwela, Dk Chrisant Mzindakaya, ambaye aliwahi kupata umaarufu kwa kulipua kashfa, aliwataka wabunge wakubali matokeo kuhusu Ripoti ya Richmond ili taifa lisonge mbele badala ya malumbano yasiyokwisha.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, Mzindakaya aliwataka wabunge wafahamu kuwa ripoti hiyo ilishapitishwa na Bunge na haiwezi kurejeshwa ianze tena upya.

Naye Dk Mlingwa (Shinyanga Mjini), alisema mpasuko unaoinyemelea CCM unatokana na chama hicho kuacha misingi yake ya kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi na badala yake kinawakumbatia wafanyabiashara.
Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Emanuel Nchimbi alitumia nafasi yake kuomba maridhiano ya wabunge wa CCM, kujenga moyo wa kusameheana ili chama kisonge mbele.
Tuma maoni kwa Mhariri
Facebook
 
LOL inafurahisha mtu anavyojikaanga.. ila UWT si ipo nyuma yake?....usalama
 
Hivi SFO walimsafisha Chenge lini kwenye tuhuma za radar?

Chenge anasema mikataba iliridhiwa na baraza la mawaziri la awamu ya tatu, je, hao mawaziri ni wanasheria kitaaluma? Kwani hatujui kwamba vikao hivyo vya baraza la mawaziri walikuwa wanaburuzwa na ubabe wa Mkapa?

Ninasubiri majibu ya Mama Kilango, maana huu mjadala nimeupenda sana. Badala ya kujenga chama, sasa wanaanza kujimaliza wenyewe.

Waziri wa Utawala Bora anaamini kwamba "two wrongs = RIGHT". Sasa kama watu hao walikuwa na tuhuma hizo, kwanini serikali haikuwashughulikia? Anakuja kusema leo hii baada ya kuona watu wake wanabanwa? Kama wako ambao wana makosa, waunganisheni wote muwapeleke Kisutu ama Mahakama Kuu ili sheria ichukue mkondo wake badala ya kuanza kutishiana.

Kusema kwamba Mama Kilango na Mzee Malecela ni beneficiaries wa hela za EPA kwa kuwa Patel ali-fund harusi yao, kwani yeye Simba ana uhakika kwamba hela hizo zilikuwa ni sehemu ya hela za EPA? What if zilitoka kwenye sources nyingine?

Kupokea michango ya harusi ama hela za kufadhili kampeni tangu lini imekuwa ni kosa kisheria? Kuna sheria inayokataza kupokea hela za kampeni ama kuna kuna sheria inayotaka watu wa-disclose sources zao za hela za kampeni?

Hizi ni dalili za kuishiwa hoja na sasa naona wanakuja na vioja. Hebu wachukue KAGODA, Richmond, na EPA zilizosalia wazipeleke Kisutu ama Mahakama Kuu halafu wamchukue na Mama Kilango na Mzee Malecela kwamba walipokea hela za ufisadi kutoka kwa Patel, tuone ni nani atafungwa? Kwanza kuna wengine watakuwa hawana hata kesi ya kujibu maana sioni kosa kisheria, ingawa morally kunaweza kuwa na dosari hasa kama unajua kwamba anayekupatia fedha ni mwizi ama fisadi.

Waziri wa Utawala Bora anakuja na mipasho, hana concrete evidence zaidi ya kutaka kuumbuana tu na kudhalilishana. Hizi ni dalili mbaya sana naona serikali inatumia kila aina ya ushenzi ili kufunga watu midomo.

Ukiona wazee kama akina Mzindakaya wanasema wakubali yaishe, maana yake kuna mambo yanatakiwa kufukiwa maana mjadala unakoelekea ni kuzuri sana.

Je, ni nani atavuliwa uanachama wa CCM? Maana naona hapa ni mwendo wa kumwaga mboga na mwingine anamwaga ugali, mwisho wa siku wote wanakosa.

Ninatamani sana sasa hivi kungekuwa na chama ambacho kimejijenga mpaka vijijini, yaani kung'oa CCM ingekuwa ni kama kusukuma mlevi. Hebu kamati ya Mzee Mwinyi iendelee kufanya haya mahojiano ili tuone jinsi wanavyovuana nguo hadharani!

Huu ni wakati wa vyama vya upinzani kuongeza kasi kuelekea 2010. Ukiona CCM wanagombana wenyewe, chukua jembe ukalime (mwaga sera vijijini) na watakapopatana mwakani itakuwa ni wakati wa mavuno, ni kuchukua kapu na kwenda kuvuna kura!
 
Absolutely right!, kwani Jeetu hakuwa na hela isipokuwa za EPA tu?, kwani mtu akikuchangia harusi halafu baadaye anashikiliwa na tuhuma za uwizi ni KOSA?, mi ntajuaje kuwa ameiba?..mbona makamba alichangiwa harusi ya mwanae. Angemtaja pia Makamba.
 
Wenye utaalam wa sheria, naomba msaada: Hivi mipasho aliyotoa Sophia Simba ina merit ya kufunguliwa kesi mahakamani? Kwa sheria ipi na kwa kosa gani?
 
Huyu mama na aliyemtuma wote hawakupima mawazo yao kwanza kabla ya kuwasilisha.Yaani kama ni mtihani hata mbili asingepata, badala ya kuonesha kwa nini hao anaowatetea ni wasafi yeye anajibu maswali ambayo hajaulizwa halafu majibu yenyewe anayotoa bado yanakua hayajitoshelezi,
 
- This is very interesting, Sophia Simba waziri wa Usalama wa Taifa, anawajua mafisadi lakini ameshindwa kuwafikisha wanapotakiwa, badala yake anakwenda kulia kwenye kamati ya Mwinyi ndio tatizo la kukosa sheria na taifa hili, ingekuwa nchi zinazojali sheria hapa angeanza yeye Sophia kupelekwa Segerea, and then mawakili wake wangekata deal ili aseme yote anayoyajua kuhusu anaowashutumu na atoe ushahid, yeye angeachiwa na aliowataja wangeshikwa mara moja na kama hana kama in this case angebaki huko huko Segerea, kumbe Masilingi alikuwa tough, maana Kitine alipotoa tuhuma kama hizi bungeni alimpa masaa kuwataja majina viongozi wote anaosema wezi au angemrundika Segerea, ikabidi wakuu wa Kihehe kina Marehemu Siovelwa waingilie kati ndio Kitine akapona kwa kwenda kijificha nyumbani kwa kigogo mmoja wa CCM kwa miezi kama miwili.

- Kuhusu harusi na ufadhili wake, Auntie Sophia hakusema ukweli kwa sababu harusi iliandaliwa na kamati maalum kama inavyokuwa kwenye harusi zote bongo, Mwenyekiti wa kamati alikuwa Chiligati, akishirkiana na DC wa Dodoma Mjini, ikiwa ni pamoja na wanakamati kama Kimbau na Kitwana Kondo, na kina General Gau, sasa hawa hasa Chiligati wangetakiwa kuonyesha mahesabu waliyoyatumia ili kuweka ukweli unapotakiwa, kwa sababu ninazo copies zote za matumizi ya ile harusi na pesa zilizochangwa na majina wala sio tatizo.

- Maneno ya Auntie Sophia, siyaamini hata kidogo na ni uzushi mtupu kwa sababu ni mimi ndiye niliyetoa hela zangu za mfukoni kwanza kununua suti zote mbili za bwana harusi, na pia nilitoa hela zangu za mfukoni za kulipia honeymoon yao, ama sivyo hata honeymoon isingekuwepo, na kama kawaida yangu huwa ninatunza risiti ya kila kitu ninachofanya duniani, kwa hiyo ninasema kwamba Auntie Sophia, ana kazi kubwa sana kuthibitisha madai yake akiwa waziri wa Usalama wa taifa, kwa sababu ninazo risiti nyingi sana za hela zangu nilizotumia on the harusi, sasa kama kweli harusi ilifadhiliwa na fisadi, mimi na ndugu zangu hatukuwa na sababu ya kutoa hela nyingi sana tulizotumia kwenye ile harusi.

- Ya kugombea urais, hivi Mzee si alikuwa na hela za Iran, zilizobaki toka mwaka 1995. Halafu Auntie Sophia hapa tena anakuwa sio mkweli wala anayejali sheria, kwa sababu kampeni za urais wagombea wote walipokea hela toka kwa watu na sekta mbali mbali na haikuwa uvunjaji wa sheria za jamhuri, na ukweli niujuao ni kwamba kampeni ya mzee ilifadhiliwa na Shabibu, na kampeni ilikuwa na hela ndogo sana ndio maana haikufanikiwa, unless Shabibu ni fisadi then kweli mzee alichukua hela chafu, na kama ilivyokuwa kampeni ya Rais wa sasa ambako Auntie Sophia alikuwa mshiriki sasa angelinganisha hela zilizotumiwa na kambi zote na walikozitoa hela zao ndio ingependeza, lakini si kweli kabisa kwamba Patel ndiye aliyefadhili ile kampeni, walioifadhili kampeni ni shabibu na Mstaafu wa Idara, sasa the question inapaswa kuwa alikuwa akizitoa wapi zile hela kama at the sametime alikuwa akishirikiana na kina Rsotam na Lowassa? Kwa sababu all this came to the light baada ya uchaguzi na mtoto wa mstaafu kupewa ubunge wa bure na mtandao Sophia angekuwa mkweli angeisaidia sana hii kamati na taifa kwa ujumla na hasa kutokana na nafasi yake ya uwaziri wa Usalama wa Taifa.

- Anyways, ninaamini kwamba Mheshimiwa Anne Kilango, atamsaidia sana kumjibu itakapofikia zamu yake, maana kama alivyosema haya ni mashambulizi yake sio ya mzee na atayajibu ndio uzuri wa demokrasia na hii kamati itapata mengi sana ya kulisaidia taifa, I wish ingepewa nguvu ya kuwashika wanaotuhumiwa na ushahidi unapokuwa wazi, na kuwahsika wasio na ushahidi.

Ahsanteni.

William.
 
Naweza kusema hii ni serikali ya ajabu sana kupata kutokea hapa nchini kwetu tangu tupate uhuru. Ina mawaziri ambao huwezi kujua aliyewateua alikuwa anafikiria nini! Huyu Sofia Simba simfahamu vizuri sana. Sina uhakika kuhusu elimu yake kwani nasikia aliwahi kufanya kazi kama karani wa kawaida sana kwenye idara ya habari (Maelezo) miaka ya nyuma. Wanaomfahamu vizuri wanasema alikuwa na tabia za kichangudoa. Lakini naambiwa pia amezaa watoto wanne na wanaume tofauti tofauti. Mtu wa namna hii lazima atakuwa na dosari kubwa sana, hasa kama kabila lenyewe ni Mndengereko... Hakuna seriousness nchi hii tunahitaji mabadiliko makubwa sanaa kuirejesha nchi kwenye mstari.

Yakhe mbona waja na mpya....ubovu wa mtu hauendani na kabila lake....acha kudharau makabila, zungumzia mada.
 
Ni kweli mkuu, tunakaribia kwenye kiitikio (chorus)!!! Bado nipo nasubiri subiri, kwani ni kosa kubwa sana kuukosa huu muziki🙄

Mkuu DC,

Amini usiamini kny thread hii na ile ya Zitto kuna mambo mengi sana mapya nimejifunza kwa kweli!

Siasa za Tanzania ni zaidi ya tunavyozijua!
 
Back
Top Bottom