Manitoba,
Ndio maana nikakuuliza mfano. Jibu ni kwamba inategemea unamficha nani.
Kama ni suala ambalo wengine tulikuwa tunaongelea, yaani la kupambana na system (serikali) basi electronic gadgets karibu zote zinaweza kukuponza.
Inategemea na serikali wako prepared kwenda mbali kiasi gani.
Watu wengi wananaswa kwasababu ya kuamini kama ulivyoandika hapo juu kwamba
unaweza kufanya ujanja. Mfano yule jamaa aliyetaka kulipua mabomu UK, akakimbilia Ufaransa, akawasha handset yake baada ya kutoa simcard akiamini yuko salama, haikuchukua saa akawa mikononi mwa polisi.
Kama ni mafia wa kimataifa basi jitahidi usiguse electronic gadgets maana watakunasa tu.
Kama unapambana na hao polisi wetu basi unaweza ukasalimika kwenye baadhi ya mambo.
kwa taarifa yako hakuna Encryption iliyo salama, hata ibuniwe na nani.
Nakuelewa mzee, lakini mimi bado naamini kwamba kama unaelewa vizuri hiyo technologia unayotumia ndio unaweza kuchukua hatua muafaka.
Nadhani mamafia wa kimataifa ndio wanatumia electronic gadgets kuliko hata sisi wengine. They spend time and money kuelewe technolojia ipo wapi na inaenda wapi. Wenzangu na mie tunapenda vitu rahisi rahisi tu bila kushirikisha akili. Wakikudaka unasema technolojia imekuponza. Umejiponza mwenyewe.
Inaonekana unaogopa sana serikali mzee. Kuna maeneo ambayo hata kama wanataka kwenda mbali vipi, utakuwa na jinsi yako ndogo ya kuwapoteza. Cha msingi ni kwamba unatakiwa uielewe technolojia unayotumia na wanayotumia. Kama huielewi watakudaka tu na usilaumu techonologia, ni tatizo lako binafsi.
Kama huyo jamaa uliyetolea mfano angekuwa anajua vizuri GSM inavyofanya kazi, na wanaomtafuta watakuwa wanatumia technologia gani, asingethubutu kutumia simu hiyo hiyo. Hata wewe nadhani uyanatambua hili, hata kama hujui ni kwa nini. Simu yako ina unique id inayoitwa IMEI (
http://en.wikipedia.org/wiki/International_Mobile_Equipment_Identity )
na hiyo ndiyo wanayoitumia ku-track simu yenyewe (na sio sim-card). Wanokwambia utupe simcad halafu mchezo utakuwa umeisha wanasahu kwamba atakaye kuwa anatrack simu yenyewe wanakudaka hata kama umebadili sim-card.
Hiyo unayoiita system au serikali haitumii technologia zinazotoka mbinguni. Na waliopo huko ni watu wenye bongo kama wewe.
Iwe ni system au ni mtu mwingine, nadhani ni overstatement kusema kwamba kama unataka kuficha mambo yako basi usitumie techonolojia. Hiyo ni kweli kama wewe huielewi kiundani hiyo technolojia unayotaka kutumia. Unaenda kununua tu kwenye shelf kwa sababu umeona tangazo kwenye TV linaloelezea inafanya mambo gani. In fact, kama huielewe technolojia unayotaka kuitumia , i bora usiitumie maana itakuponza kweli.
Kwa mfano ushajiuliza inakuwaje watu wengine wana-hack computer za taasisi za maana tu duniani na they disapear without a trace? Ndio wapo wanokamatwa na haimaanishi kwamba walikuwa ni mbumbumbu. Lakini wapo wasio kamatwa na sababu ni kwamba wanaelewa wanachokifanya na wanachokitumia kufanya wanachokifanya.
Baba, elewa technologia unayotumia, usiilaumu pale unaponaswa.
Mimi napenda kufanya vitu kwa vitendo. Wewe sema unataka kufanya nini kuizunguka "system", as long as siyo kuvunja sheria (kwa sababu naamini sheria zinahitaji kuheshimiwa) pengine tunaweza kupata suluhisho. Na sio kufikiri tu kwamba "system" ndio mwanzo na mwisho wa techonolojia.