mnamo tarehe 4,may, 2007, nilipata simu ya vitisho toka kwenye private number, na ilinionya kutoingilia mambo fulani au kumwaga hapa ni kuwa, kijijini kwetu kuna mkataba wa kifisadi unaomlinda mwekezaji mmoja feki, huyu anaendesha hoteli nzuri ambayo kijiji au chama chetu cha ushirika kiliachiwa na ma-settler waliokimbia , mwekezaji huyu amegeuka mbogo hajalipa kodi ya jengo kwa muda wa miaka 12, zaidi ya dola 123,ooo
kila swala hili likianza, viongozi wote wanaopokea hili tatizo wanakatiwa wanaingia mitini. mbaya zaidi waziri mmoja anamsaidia mwekezaji huyu apewe hati eneo hilo na mali za ushirika.
kwa kuwa tulikuwa kimbelembele ndo yakanikuta hayo ya kupigiwa simu ya na kuahidiwa kutwangwa risasi
nilienda kwenye mitandao yote, jibu walilonipa ni kuwa ,wanaweza kumpata mpigaji wa hiyo namba, shart ni lazima polisi wahusishwe na wao ndo wataweza kupewa hiyo information,
ni mwaka sasa na hakuna hatua yeyote, nilikanyaga polisi mpaka nikachoka, nikatoa elfu tano tano za vocha mpaka nikachoka
mwishoni, nikapeleka swala hili na details zote, yule niliyempelekea badala ya kufanya uchunguzi dhidi ya mwekezaji, yeye alienda kwake kuanzisha uswahiba! mpoooo