SMS iliyoniamsha.. kuna kusalimika?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Kuna sms mbili ambazo nimezipata tangu juzi. Moja inamhusu kijana Julius Mtatiro aliyekuwa mmoja wa viongozi wa TAHLISO. Hiyo sitaizungumzia sana kwa sasa lakini ni dokezo kwa watawala wajue tunajua wanachopanga.

Lakini ya pili ndio imenishtua sana kwani nimeipata usiku wa manane hapa kijijini. Mara nyingi ninapopata hizi za usiku wa manane basi najua ni jambo zito na nyeti. Nilikoipata na nilivyozunguka kuona kama watu wengine wameipata nimeshangaa jinsi ilivyosambaa kwa kasi.

Imekuja kama ile sms iliyotangaza kifo cha Zitto akiwa Mombasa wakati yeye mwenyewe akiwa hai na wiki moja baadaye tukasikia kifo cha Wangwe. Huwa sishei messages hizi hadharani lakini hii nimeombwa na watu ambao majina yao si mageni kabisa masikioni mwenu. Hivyo naitoa kama ilivyo nikiacha muamue kama kuna mtu mwingine kaipokea, kuna ukweli, ni uzushi wa kupuuzia, ni njama za kuchafuana au ni jambo ambalo la kupuuzia.

Nilichogundua kitu kimoja ni kuwa simu zinazotoka sms hizi ukipiga unapata error messages. Mojawapo ya simu hizo ni hii: 0757 079316. Na wanaofanya hivyo wamegundua kuwa Jeshi letu na UwT hawana uwezo wa kutrace simu za wireless na hivyo kuacha simu hizo kutumika kama vifaa vya matishio kwa watu wengine.

Message yenyewe inasema hivi:

Mtandao wa mafisadi unaoongozwa na marafiki watatu,
Rostam, Lowassa na Karamagi na mzee wao Kingunge kwa
ufupi KALOKIRO, umepoteza matumaini, umekata tamaa na
sasa umeamua kuleta balaa; Kuua kwa kutumia sumu ili
kupunguza kelele za EPA, RICHMOND na Jengo la UVCCM.
Kikao chao cha jana kimekua kuanza kampeni hiyo kwa
kuwapa sumu inayoua polepole wanasiasa mwiba wawili:
S. Sitta na H.Mwakyembe.

Sumu hiyo (allegedly) imeingizwa nchini
majuzi na Rostam kutoka Dubai. Muuaji anavaa glove ya
sumu na kumsalimia mlengwa kwa kumgusa. Hicho ni kifo
tosha! Sitta na Mwakyembe wamepelekewa ujumbe huu.
Wajihadhari maana vyombo husika vya dola vimenunuliwa!
Pole pole nchi inapelekwa vitani na mafisadi! KALOKIRO
insider
 
MODs haraka sana peleka hii habari kwenye tetesi, tumechoka na hizi habari tunataka tujadili masuala yakutatua shida za wananchi na siyo blah-blah.
 
Huh?........Miafrika Ndivyo Tulivyo!!

.

Nyani,

Nakubaliana nawe.

Pole Mzee Mwanakijiji, tunakoenda Watanzania ni kubaya sana. Tutaishia kuwa kama Wanigeria. Wameanza viongozi wetu kwa ufisadi, rushwa na mambo mengine. Ila sasa hata sisi wananchi tunaenda kwenye ujinga kwa kasi mno.

Inatakiwa mtu ashikwe na kuminywa p**** labda ndio wataacha ujinga huo. Bahati mbaya UWT nao wako busy kwenye ufisadi na kuwalinda mafisadi, wanashindwa hata kuwafuatilia wajinga kama huyu aliyekutumia hiyo sms.

Si ajabu yeye anajiona mjanja kweli, kumbe anaweza kugundulika kwa muda mfupi sana.
 
Tunaipokea na kuhifadhi kwenye draft hadi wakati mwafaka. Yakijiri tutaenda kwenye draft na kuipakua. Asante Mkjj
 
Mhmm it sounds like uzushi but the way ulivyoi-present Mzee inamfanya mtu ajifikirie zaidi ya mara mbili. I think Rostam can do but Ngombare? and why killing Mwakyembe? kazi yake juu ya Richmond si ilishakwisha?

Sasa hili ni onyo kwa kila mtu including JF members usikubali mtu akusalimie akiwa amevaa gloves, tena asikuguse popote. Mungu iponye Tanzania.
 
.... wazembe tu uwt, yaani kumtrace mtu anayetuma msg kama hizo wameshindwa nini?!

.... hata kama anatuma kutokea nje ya nchi kwa kutumia mtandao, bado anaweza kuwa traced. ni kutokuwa tu wajanja na watafiti wa mambo. na wanavyozidi kulaza damu ndiyo vitisho kama hivyo vitaongezeka na itafika wakati vitisho vya kweli vinafanyika na maovu kushindwa kuzuilika hali tahadhari zilishatolewa.

.... this is some sort of cyber bullying and need to be stopped. punguzeni misafara isiyo na maana nje ya nchi inayo cost taifa mamilioni ya kodi za wananchi mu-invest kwenye tools za ku-track wapuuzi wa message kama hizo.
 
Mtasema uzushi ikitokea je mtasemaje breaking news???Hapa nikuchukua tahadhari kila jambo linenalo lipo kama halipo basi laja......huu ujumbe si wa kupuuzia kabisa.
 
Mtasema uzushi ikitokea je mtasemaje breaking news???Hapa nikuchukua tahadhari kila jambo linenalo lipo kama halipo basi laja......huu ujumbe si wa kupuuzia kabisa.
......Ukiona moshi wafuka ujue moto utaripuka muda si mrefu.....Watch out people..
 
Imekuja kama ile sms iliyotangaza kifo cha Zitto akiwa Mombasa wakati yeye mwenyewe akiwa hai na wiki moja baadaye tukasikia kifo cha Wangwe. Huwa sishei messages hizi hadharani lakini hii nimeombwa na watu ambao majina yao si mageni kabisa masikioni mwenu. Hivyo naitoa kama ilivyo nikiacha muamue kama kuna mtu mwingine kaipokea, kuna ukweli, ni uzushi wa kupuuzia, ni njama za kuchafuana au ni jambo ambalo la kupuuzia.

Mwanakijiji u bigger than this pls spare us we have enough in our plate au na wewe umeingia kwenye mkumbo wa kututoa kwenye ajenda muhimu (EPA, Richmond, etc) jamani tupunguze mizaha ya kuokota okota udaku na kumwaga hapa.

Pole sana kamanda, na kama kamanda unakatishwa usingizini na sms kama hizi tuna kazi kubwa mbeleni...........
 
Last edited:
MODs haraka sana peleka hii habari kwenye tetesi, tumechoka na hizi habari tunataka tujadili masuala yakutatua shida za wananchi na siyo blah-blah.

Kama unaona hii ni blah blah subiri uone, zilikuja message kama hizi kuhusu wangwe na wengine wengi na hazikuwa blah blah subiri breaking news uone na utajua kuwa hii sio blah blah. Binadamu wanaotakiwa kupukutika wanaweza kunusurika kwa kuweka wazi njama kama hizi, hii sio blah blah.
 
Kwa nini huyo kalokiro insider ameamua kutoa ujumbe huu kupitia kwa watu wengine badala ya security organs?
Kwa nini ameutoa ujumbe huu sasa hivi na si kabla 'sumu' haijaingizwa?
Kuna watu wana utamaduni wa kusalimiana wakiwa wamevaa gloves tanzania?
 
......Ukiona moshi wafuka ujue moto utaripuka muda si mrefu.....Watch out people..

...ndo maaana mimi nasema huu ujumbe si wa kupuuzia watu tutashuhudia wanatutoka gafla mara bidu.........
 
Sasa Mafioso imeanza kazi Bongo!Tutakuwa akina Tomaso ambao hawakuamini mpaka walipoona Yesu Kafufuka!
Amen!
 
Mwanakijiji u bigger than this pls spare us we have enough in pur plate au na wewe umeingia kwenye mkumbo wa kututoa kwenye ajenda muhimu (EPA, Richmond, etc) jamani tupunguze mizaha ya kuokota okota udaku na kumwaga hapa.

Pole sana kamanda, na kama kamanda unakatishwa usingizini na sms kama hizi tuna kazi kubwa mbeleni...........

Masatu, nakubali kuwa hamna haja ya mkjj kuogopa sana kwa ujumbe uliotolewa. Hata hivyo jambo muhimu hapa ni kwamba kama text inatumwa kwa viongozi, kwanini UWT wanashindwa kui-trace back kwa mtumaji. Huoni kama swala hili iwapo linaachiwa kushika mizizi basi kila mmoja wetu mwenye chuki ataanza kuwa anatishia maisha ya viongozi wetu?.... msululu wa txt ukiongezeka ndipo serikali au UWT washughulikie?.... miye wala siangalii content za hiyo iliyotumwa kwa mwkjj bali hoja ni pale anaposema kuwa msg kama hizo haziko traceable.
 
I believe anything is possible underneath the sun despite our poor technology!If we have money disposable for people to steal then we should actually have the money to bring in investigative organs with more advanced technology to trace people endagering the lives of our leaders!
 
Masatu, nakubali kuwa hamna haja ya mkjj kuogopa sana kwa ujumbe uliotolewa. Hata hivyo jambo muhimu hapa ni kwamba kama text inatumwa kwa viongozi, kwanini UWT wanashindwa kui-trace back kwa mtumaji. Huoni kama swala hili iwapo linaachiwa kushika mizizi basi kila mmoja wetu mwenye chuki ataanza kuwa anatishia maisha ya viongozi wetu?.... msululu wa txt ukiongezeka ndipo serikali au UWT washughulikie?.... miye wala siangalii content za hiyo iliyotumwa kwa mwkjj bali hoja ni pale anaposema kuwa msg kama hizo haziko traceable.

SteveD,

Nadhani tuna work on assumption hapa. Wewe umejuaje kama UWT hawajaifanyia kazi hii sms (kama ipo) Lakini kubwa zaidi haya ni mambo ya ki usalama zaidi tusitegemee taarifa za undani namna wanavyo trace (if traceable) hizo msg.

By the way hiyo picha ya Brazemeni inafanya nini hapo kwenye avatar yako?
 
SteveD

Hii nimeizima kutoka kwako na ni ujumbe tosha kwa Mwanakijij

Fikra ni kitu kizuri, uzushi unatokana na fikra, fikra za uzushi ni kitu kibaya na ni uzushi, kutotenganisha uzushi na fikra ni kitu kibaya zaidi kwani mwisho wa fikra ni matendo pale fikra hazibakii kuwa fikra.
 
Back
Top Bottom