Kuna sms mbili ambazo nimezipata tangu juzi. Moja inamhusu kijana Julius Mtatiro aliyekuwa mmoja wa viongozi wa TAHLISO. Hiyo sitaizungumzia sana kwa sasa lakini ni dokezo kwa watawala wajue tunajua wanachopanga.
Lakini ya pili ndio imenishtua sana kwani nimeipata usiku wa manane hapa kijijini. Mara nyingi ninapopata hizi za usiku wa manane basi najua ni jambo zito na nyeti. Nilikoipata na nilivyozunguka kuona kama watu wengine wameipata nimeshangaa jinsi ilivyosambaa kwa kasi.
Imekuja kama ile sms iliyotangaza kifo cha Zitto akiwa Mombasa wakati yeye mwenyewe akiwa hai na wiki moja baadaye tukasikia kifo cha Wangwe. Huwa sishei messages hizi hadharani lakini hii nimeombwa na watu ambao majina yao si mageni kabisa masikioni mwenu. Hivyo naitoa kama ilivyo nikiacha muamue kama kuna mtu mwingine kaipokea, kuna ukweli, ni uzushi wa kupuuzia, ni njama za kuchafuana au ni jambo ambalo la kupuuzia.
Nilichogundua kitu kimoja ni kuwa simu zinazotoka sms hizi ukipiga unapata error messages. Mojawapo ya simu hizo ni hii: 0757 079316. Na wanaofanya hivyo wamegundua kuwa Jeshi letu na UwT hawana uwezo wa kutrace simu za wireless na hivyo kuacha simu hizo kutumika kama vifaa vya matishio kwa watu wengine.
Message yenyewe inasema hivi: