SMS iliyoniamsha.. kuna kusalimika?

SMS iliyoniamsha.. kuna kusalimika?

from Senior Activist <senior_activist@yahoo.co.uk>
reply-to senior_activist@yahoo.co.uk
to Mwanakijiji@jamiiforums.com
date Wed, Sep 3, 2008 at 5:56 AM
subject Narrow minded personnel
signed-by yahoo.co.uk

hide details Sep 3 (6 days ago)

Reply

Nimekuwa nifuatilia upuuzi unaouandika kwenye gazeti la Chama chenu kwa muda mrefu ukiwa chini ya kificho cha jina lako halisi. Justification ya watu makini walio wengi kwako ni kwamba wewe ni mpuuzi na mpumbavu mkubwa!!! Kijitu chenye fikra finyu ambazo hata harufu ya elimu hakijawahi kuinusa, na kama kimewahi basi kinafanana kabisa na wale wasomi mah...thi. Sasa upuuzi wako hatuwezi kuuvumilia tena, kilichobaki kwako ni kujichunga kimwili ili madhara yaliyokusudiwa kwako yasikufike mapema.

Keep on touch.

Toba,Washindwe na walegee.

Usitetereke na hawa wapuuzi kamanda,kizuri pia ni kuchukua taadhari
 
sijawahi, kwani siishi katika nchi ya kufikirika. Anayetaka kunijua ananijua kama vile anayetaka kukujua wewe anaweza kukujua. Au unadhani wewe hujulikani?

mimi mbona al watan sana tuuu? kwetu pale nje ya BIG MAYAI kariakoo mtaa wa sikukuu...opposite na kalbu ya Siagoni hivyo sina la kuogopa na kama nikikosekana pale Kariakoo napatikana ilala magorofani pale kwenye gorofa la akina MANI au ukinulizia kwa akina JUMBE au hata akina KALEONI au JC utanipata tuuu as i have nothing to hide na wala si mimi ninaye walaza macho wazi watawala kwa kuwatishia kupost picha ambazo wamekaa kwenye "compromising pozisheni" kama ulivyodai

tatizo liko kwako wewe uliyedai kuwa maisha yako unayaweka chini ya watu wachahche humu JF na hakuna anayeweka kukujua ID yako....halafu unasema eti hawana uwezo wa kukupata
we bwana weee hawajakutaka tuuu shekhe wakiktaka wala hawatahitaji kutrace simu yako wanazo namna za kukupata on a flip side

hivi hiyo GOLD CARD hapo chini ya kwako au ya nani?

2007-08-21T22_39_21-07_00.jpg
 
mimi mbona al watan sana tuuu? kwetu pale nje ya BIG MAYAI kariakoo mtaa wa sikukuu...opposite na kalbu ya Siagoni hivyo sina la kuogopa na kama nikikosekana pale Kariakoo napatikana ilala magorofani pale kwenye gorofa la akina MANI au ukinulizia kwa akina JUMBE au hata akina KALEONI au JC utanipata tuuu as i have nothing to hide

Hili uwe unawaambia wasiokujua na wanaoamini stori zako za hivyo.

na wala si mimi ninaye walaza macho wazi watawala kwa kuwatishia kupost picha ambazo wamekaa kwenye "compromising pozisheni" kama ulivyodai

Wala haikuwa watawala iliku mtu mmoja tu.

tatizo liko kwako wewe uliyedai kuwa maisha yako unayaweka chini ya watu wachahche humu JF na hakuna anayeweka kukujua ID yako....halafu unasema eti hawana uwezo wa kukupata
we bwana weee hawajakutaka tuuu shekhe wakiktaka wala hawatahitaji kutrace simu yako wanazo namna za kukupata on a flip side

Hivi kweli unafikiri naishi katika illusion kuwa sifahamiki? Nazungumza na watu wote hawa, naweka sauti yangu, mji niliopo, nawapigia simu toka nyumbani, mkononi, na ofisini na sasa nimeweka na picha yangu kweli nitakuwa sifahamiki? Tatizo unafikiri mapambano haya ni ya personal. They are not. Wakinitaka wanajua pa kunipata namba yangu iko wazi, n.k so sijui kwanini unafikiri nina hofu ya kujulikana. Ningekuwa na hofu hiyo nisingefanya ninayofanya. Just think. Mwenye hofu ya kujulikana ni yule anayewaambia watu kuwa yuko mahali fulani kumbe hayupo huko.

hivi hiyo GOLD CARD hapo chini ya kwako au ya nani?

2007-08-21T22_39_21-07_00.jpg

sorry I can't see it tuma... ila inawezekana ni ya kwangu.
 
Checkers.jpg
 
Nimejihami vyema-Sitta (Raia Mwema)

Waandishi Wetu Septemba 10, 2008

SPIKA wa Bunge, Samwel Sitta na Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, wamepelekewa ujumbe wa kujihadhari na kudhuriwa kwa sumu kunakodaiwa kupangwa na baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi nchini.

Tayari Sitta amelithibitishia Raia Mwema kupata ujumbe huo, ambao amesema yeye amelazimika kuutuma kwa vyombo vya usalama nchini, ili viweze kuufanyia kazi kujua ukweli wake.

SPIKA wa Bunge, Samwel Sitta

Ujumbe huo unadai kuwa mtandao huo wa mafisadi umepoteza matumaini, umekata tamaa na sasa umeamua kuleta balaa kwa kuua kwa kutumia sumu ili kupunguza kelele zinazohusu ufisadi nchini kwa ujumla.

Kwa mujibu wa ujumbe huo, kikao cha watuhumiwa hao wa ufisadi kimeamua kuanza kampeni hiyo kwa kuwapa sumu inayoua pole pole, wanasiasa hao, na kwamba imeingizwa nchini kutoka Dubai.

"Muuaji anavaa glove ya sumu na kusalimia mlengwa kwa kumgusa. Hicho ni kifo tosha! Sitta na Mwakyembe wamepelekewa ujumbe huu. Wajihadhari, maana vyombo husika vya dola vimenunuliwa! Pole pole nchi inapelekwa vitani na mafisadi!," inasema sehemu ya ujumbe huo.

Alipoulizwa, Sitta alisema kwamba kimsingi amepuuza ujumbe huo ambao ametumiwa, lakini kutokana na kuwa kiongozi nchini, amelazimika kuutuma kwa vyombo vya usalama ili ufanyiwe kazi na kuweka ushahidi endapo jambo lolote litatendeka dhidi yake.

"Nimeipuuza taarifa ile kwa sababu imeonekana pia kwenye internet. Vitisho hatari kama hivi haviwezi kusambazwa kwenye internet. Lakini sikuupuuzia moja kwa moja, nimeutuma ujumbe huo kwenye vyombo vya dola, ili kama likitokea jambo kuwepo na ushahidi.

"Nimetuma kwa vyombo vya usalama kwa sababu jambo hili lina chembe ya uhalifu. Huwezi ukajua kitakachotokea. Kwa vyovyote likitokea jambo watu watapenda kujua undani wake. Naichukulia taarifa hii hivyo hivyo, ndivyo yalivyo mambo ya siasa," anasema Sitta.

Raia Mwema haikufanikiwa kuwasiliana na Dk. Mwakyembe ili kujua yeye ameupokea vipi ujumbe huo, tangu juzi Jumatatu na jana Jumanne, simu zake zote zilikuwa zimezimwa.

Robert Manumba

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba alipoulizwa alisema kuwa alikuwa nje ya Dar es Salaam, na kwamba wanaoweza kujua suala hilo ni maofisa wa chini yake, ofisi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) au ofisi ya Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Hata hivyo, IGP Said Mwema alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema kuwa pia alikuwa nje ya ofisi yake lakini akaahidi kuwa angewasiliana na Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kujua kama lipo na linafanyiwa kazi.

Bado haifahamiki kwa yakini, ni kwanini hasa Spika Sitta, ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki, na Mwakyembe wanalengwa na ujumbe huo, kwani masuala yanayohusu ufisadi nchini yamekuwa yakijitokeza katika nyanja nyingi na kuwahusisha wakemeaji mbali mbali.
 
mimi mbona al watan sana tuuu? kwetu pale nje ya BIG MAYAI kariakoo mtaa wa sikukuu...opposite na kalbu ya Siagoni hivyo sina la kuogopa na kama nikikosekana pale Kariakoo napatikana ilala magorofani pale kwenye gorofa la akina MANI au ukinulizia kwa akina JUMBE au hata akina KALEONI au JC utanipata tuuu as i have nothing to hide na wala si mimi ninaye walaza macho wazi watawala kwa kuwatishia kupost picha ambazo wamekaa kwenye "compromising pozisheni" kama ulivyodai

tatizo liko kwako wewe uliyedai kuwa maisha yako unayaweka chini ya watu wachahche humu JF na hakuna anayeweka kukujua ID yako....halafu unasema eti hawana uwezo wa kukupata
we bwana weee hawajakutaka tuuu shekhe wakiktaka wala hawatahitaji kutrace simu yako wanazo namna za kukupata on a flip side

hivi hiyo GOLD CARD hapo chini ya kwako au ya nani?

2007-08-21T22_39_21-07_00.jpg

GT Hiyo office gani/ya nani? nimeipenda sana, iko complicated, pls tell me
 
Nimejihami vyema-Sitta

Waandishi Wetu Septemba 10, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

SPIKA wa Bunge, Samwel Sitta na Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, wamepelekewa ujumbe wa kujihadhari na kudhuriwa kwa sumu kunakodaiwa kupangwa na baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi nchini.

Tayari Sitta amelithibitishia Raia Mwema kupata ujumbe huo, ambao amesema yeye amelazimika kuutuma kwa vyombo vya usalama nchini, ili viweze kuufanyia kazi kujua ukweli wake.

Ujumbe huo unadai kuwa mtandao huo wa mafisadi umepoteza matumaini, umekata tamaa na sasa umeamua kuleta balaa kwa kuua kwa kutumia sumu ili kupunguza kelele zinazohusu ufisadi nchini kwa ujumla.

Kwa mujibu wa ujumbe huo, kikao cha watuhumiwa hao wa ufisadi kimeamua kuanza kampeni hiyo kwa kuwapa sumu inayoua pole pole, wanasiasa hao, na kwamba imeingizwa nchini kutoka Dubai.

"Muuaji anavaa glove ya sumu na kusalimia mlengwa kwa kumgusa. Hicho ni kifo tosha! Sitta na Mwakyembe wamepelekewa ujumbe huu. Wajihadhari, maana vyombo husika vya dola vimenunuliwa! Pole pole nchi inapelekwa vitani na mafisadi!," inasema sehemu ya ujumbe huo.

Alipoulizwa, Sitta alisema kwamba kimsingi amepuuza ujumbe huo ambao ametumiwa, lakini kutokana na kuwa kiongozi nchini, amelazimika kuutuma kwa vyombo vya usalama ili ufanyiwe kazi na kuweka ushahidi endapo jambo lolote litatendeka dhidi yake.

"Nimeipuuza taarifa ile kwa sababu imeonekana pia kwenye internet. Vitisho hatari kama hivi haviwezi kusambazwa kwenye internet. Lakini sikuupuuzia moja kwa moja, nimeutuma ujumbe huo kwenye vyombo vya dola, ili kama likitokea jambo kuwepo na ushahidi.

"Nimetuma kwa vyombo vya usalama kwa sababu jambo hili lina chembe ya uhalifu. Huwezi ukajua kitakachotokea. Kwa vyovyote likitokea jambo watu watapenda kujua undani wake. Naichukulia taarifa hii hivyo hivyo, ndivyo yalivyo mambo ya siasa," anasema Sitta.

Raia Mwema haikufanikiwa kuwasiliana na Dk. Mwakyembe ili kujua yeye ameupokea vipi ujumbe huo, tangu juzi Jumatatu na jana Jumanne, simu zake zote zilikuwa zimezimwa.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba alipoulizwa alisema kuwa alikuwa nje ya Dar es Salaam, na kwamba wanaoweza kujua suala hilo ni maofisa wa chini yake, ofisi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) au ofisi ya Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Hata hivyo, IGP Said Mwema alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema kuwa pia alikuwa nje ya ofisi yake lakini akaahidi kuwa angewasiliana na Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kujua kama lipo na linafanyiwa kazi.

Bado haifahamiki kwa yakini, ni kwanini hasa Spika Sitta, ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki, na Mwakyembe wanalengwa na ujumbe huo, kwani masuala yanayohusu ufisadi nchini yamekuwa yakijitokeza katika nyanja nyingi na kuwahusisha wakemeaji mbali mbali.
 
Mafisadi washaanikwa ata mkiwaua hao mpioneer bado sumu ishaenea mtaendelea kuumbuka tuu
 
I will tell you why ... mafisadi watashindwa.

It sseem like ..they are taking all the control at the moment.... Na nchi inadidimia toward the deep depth....

I tell you Tz kuna kina haiwezi kudidimia ikakigusa...! Not down there ..never ever!!!!

Haikuasisiwa hivyo..not at all ..

..the moment si coming nguvu kubwa ya kuisalimisha nchi itatokea na ita reboot ..all the good of our nation...keep on fighting all those woth good heart.

Mafsadi hawatashinda. The poison and all that.... wanachokifanya kiatakuwa ndio cha kuwa xpose wao..wait and you will see!
 
In the proverbial "makali na mpini"... kwa kadiri mambo yanavyokwenda inaonekana wao wameshika mpini...
 
Hofu yangu kubwa wala haiko kwa kina Mwakyembe na Sitta... moyo wangu ni mzito zaidi kwa ajili ya mtu mmoja tu. The cards are stacked heavily against the person. Tutahitaji kuliombea Taifa very soon.

???????????????????????????????
 
Game theory sijui kama maana yake kwa kiswahili ni nini,lakini katika thread hii umeonyesha kiwango cha hali ya juu cha majigambo na kiwango cha chini kabisa cha staha.

Unachotaka kutuambia ni kwamba unamjua sana Mkjj na unajua watawala wetu wanamjua sana na wewe pia unajua (unazo taarifa) kwamba kama wakimtaka Mkjj basi watamkamata. na kitendo chako cha kuonyesha kadi na kumuuliza Mkjj kwamba "kadi hii si yako" kwa tafsiri nyepesi ni kutuambia wengine na mwanakijiji kwamba,wewe na mafisadi tunaowachukia kuliko dhambi zetu lenu moja na mmeshafika anapoishi mwanakijij!!
 
not_this_shit_again-1.jpg
 
Siasa za vitisho

na Charles Mullinda (Tanzania Daima)

UPEPO wa kisiasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), unazidi kuchafuka baada ya kusambaa kwa tetesi kuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta, pamoja na wabunge kadhaa wa chama hicho wanaodaiwa kuwa wanamuunga mkono katika kupambana na ufisadi serikalini, kutishiwa kuuawa kwa sumu kali.

Habari zinazodai kuwepo kwa mpango madhubuti wa kumuua Spika Sitta na baadhi ya wabunge zilianza kusambazwa mapema wiki iliyopita katika mitandao ya intaneti na kupitia ujumbe mfupi wa simu za mikononi.

Jumatano wiki hii, habari hizo ziliripotiwa kwa mara ya kwanza na gazeti moja linalochapishwa mara moja kwa wiki, likiwa limemkariri Sitta akieleza kuwa taarifa hizo zimekwisha kumfikia na amekwishatoa taarifa polisi.

Ujumbe huo unaodai kuwa Sitta anawindwa kuuawa, unawataja vigogo wa chama hicho, wakiwemo baadhi ambao walijiuzulu nyadhifa zao mapema mwaka huu.

Akizungumza jana na Tanzania Daima Jumapili kupitia simu yake ya kiganjani, Spika Sitta alisema ujumbe wa kuwapo mpango wa kumuua umekwisha kumfikia na ametoa taarifa polisi ili iwapo atadhurika, polisi wawe na taarifa ya hali halisi ya matukio yaliyokuwa yakimuandama.

"Katika hali ya kawaida, naona kama ni upuuzi, lakini si vizuri kupuuza mambo kama haya. Sasa yanaonekana kwa vile yanaandikwa, lakini vinginevyo&#8230; inawezekana ni kunitisha ili niache harakati za kupambana na ufisadi uliotanda kila mahali nchini mwetu, lakini hata kama ni kunitisha, sheria zinasema ni lazima utoe taarifa, na ndicho nilichofanya.

"Taarifa nilizopeleka polisi ni mbili. Ya kwanza ni ile inayohusu vitisho vya kuuawa dhidi yangu na Dk. Mwakyembe, na ya pili ni ile inayowajumuisha pia katika mpango huo wa kuuawa kina Anne Kilango, Reginald Mengi, Mbunge wa Mbozi na wenzetu wengine kadhaa.

"Lakini hata kama tukiuawa, sidhani kama itasaidia kumaliza vita dhidi ya ufisadi. Binafsi ninaumia kwa sababu ninawindwa kila mahali, nyumbani hadi jimboni kwangu, nina sms za matusi zinazowatukana pia mke na watoto wangu ambazo ni za kusikitisha sana.

"Jimboni kwangu nako tayari kuna mabilioni ya fedha yamepelekwa, ili kuniangusha katika uchaguzi mkuu ujao, basi tu&#8230; wanatumia kila mbinu kutukatisha tamaa. Lakini naamini hawatafanikiwa," alisema Spika Sitta.

Sitta alisema ameamua kusimamia mapambano ya rushwa bungeni kwa sababu hakuna nchi maskini duniani iliyopata mafanikio ya uchumi bila kupiga vita rushwa, akibainisha kuwa Tanzania sasa ina bidhaa feki asilimia 40, jambo ambalo ni moja ya misingi ya nchi kutopata maendeleo.

Alisema yeye na baadhi ya wabunge wameshindwa kuendelea kuangalia jinsi uchumi wa taifa unavyovuja, lakini wapo baadhi wanaochukizwa na hali hiyo, ambao wanatumia kila mbinu kuhakikisha kuwa hawafanikiwi katika azima yao ya kuhakikisha uchumi wa Tanzania unasimama.

Akieleza kusikitishwa kwake na mikataba mingi ambayo taifa linaingia na wawekezaji, alisema mikataba mingi aliyoiona ilimsikitisha, licha ya kuandaliwa na wataalamu waliobobea, kwa sababu ina upungufu ambao unaligharimu taifa, na kwamba katika hali ya kawaida haipaswi kuachwa ikaendelea kutumika.

"Kuna mambo yanasikitisha kweli, katika baadhi ya mikataba ambayo taifa limeingia na baadhi ya wawekezaji, mingi ni mibovu, ukiisoma utashangaa, hata mtu wa kawaida akisoma mkataba wa aina hiyo lazima atajiuliza, huyu kiongozi aliyeingia mkataba huu na mwekezaji ni wa aina gani? Sasa wapo wenzetu ambao hawataki mikataba hii irekebishwe.

"Tumeamua kulipigania taifa letu, hivyo kuandamwa hakutakwisha, kwa baadhi ya hawa wanaotuandama hawawezi kubadilika, hivyo ni lazima watuandame. Na sisi tutazidisha mapambano," alisema Sitta kwa sauti thabiti.

Akieleza zaidi kuhusu taarifa alizozipata zinazolenga kumwangusha kisiasa, alisema baadhi ya wanasiasa, bila kuwataja majina, lakini akisema wanatokea ndani ya chama chake, wamepeleka mabilioni ya fedha jimboni kwa ajili ya kuwahonga wapiga kura wake, ili wamkatae kuwa mbunge wao katika uchaguzi mkuu ujao.

Alisema taarifa za uhakika alizonazo zinaeleza kuwa yeye pamoja na wabunge 23 wa CCM ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kupambana na ufisadi serikalini, mipango imeandaliwa ili kuhakikisha hawarudi bungeni, jambo aliloeleza kuwa baada ya muda litabainika kwa kila Mtanzania.

Mmoja wa viongozi aliyejiuzulu miezi kadhaa iliyopita, ambaye anatajwa katika ujumbe unaosambazwa sasa kuwa mmoja wa vigogo waliosuka mpango wa kuwaangamiza wanasiasa wanaoonekana kumuandama, alipoulizwa na gazeti hili kupitia simu ya kiganjani kuhusu yeye kuhusishwa na njama hizo, alikataa kuzungumza lolote.

"Sina taarifa hizo, sitaki&#8230;sitaki ku-comment chochote kuhusu jambo hili, samahani sana, naomba uniache, kwaheri," alisema kisha akakata simu.

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Abdallah Msika, alipoulizwa kama Jeshi la Polisi limekwisha kuanza kufuatilia kuhusu ukweli wa taarifa hizo, hasa baada ya Spika Sitta kutoa taarifa za vitisho kwa jeshi hilo, alisema hana taarifa za kiongozi huyo kutishwa.

"Sina taarifa hizo, labda kama aliripoti Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, lakini mimi sina taarifa. Nashukuru kusikia taarifa hizo, ngoja sasa nianze kufuatilia," alisema Msika.

Jitihada za kuwapata vigogo wengine wanaodaiwa kuhusika katika mtandao huo wa kuwaangamiza baadhi ya wanasiasa na wale wanaodaiwa kulengwa kuangamizwa hazikufanikiwa hadi tunakwenda mitamboni.

Taarifa ya kuwepo mpango wa kumuangamiza Spika na baadhi ya wabunge zinaeleza kuwa walengwa watakuwa wakiuawa kwa sumu kali ambayo watakuwa wakipakwa na mtu aliyevaa glovu yenye sumu, ambaye atakuwa akimgusa mlengwa aliyemkusudia kumuua.

Inadaiwa kuwa sumu hiyo hatari imeingizwa nchini na mmoja wa viongozi wa kisiasa ndani ya chama tawala kutoka moja ya mataifa ya Kiarabu.
 
__________________

NIMEIPENDA HII LINE ZAIDI
 
game theory sijui kama maana yake kwa kiswahili ni nini,lakini katika thread hii umeonyesha kiwango cha hali ya juu cha majigambo na kiwango cha chini kabisa cha staha.

Unachotaka kutuambia ni kwamba unamjua sana mkjj na unajua watawala wetu wanamjua sana na wewe pia unajua (unazo taarifa) kwamba kama wakimtaka mkjj basi watamkamata. Na kitendo chako cha kuonyesha kadi na kumuuliza mkjj kwamba "kadi hii si yako" kwa tafsiri nyepesi ni kutuambia wengine na mwanakijiji kwamba,wewe na mafisadi tunaowachukia kuliko dhambi zetu lenu moja na mmeshafika anapoishi mwanakijij!!

kigarama;

so far sijaelewa gt katupa karata ipi lakini naona kama anareveal too much for no reasons
 
Siasa za vitisho

na Charles Mullinda (Tanzania Daima)

UPEPO wa kisiasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), unazidi kuchafuka baada ya kusambaa kwa tetesi kuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta, pamoja na wabunge kadhaa wa chama hicho wanaodaiwa kuwa wanamuunga mkono katika kupambana na ufisadi serikalini, kutishiwa kuuawa kwa sumu kali.

Habari zinazodai kuwepo kwa mpango madhubuti wa kumuua Spika Sitta na baadhi ya wabunge zilianza kusambazwa mapema wiki iliyopita katika mitandao ya intaneti na kupitia ujumbe mfupi wa simu za mikononi.

Jumatano wiki hii, habari hizo ziliripotiwa kwa mara ya kwanza na gazeti moja linalochapishwa mara moja kwa wiki, likiwa limemkariri Sitta akieleza kuwa taarifa hizo zimekwisha kumfikia na amekwishatoa taarifa polisi.

Ujumbe huo unaodai kuwa Sitta anawindwa kuuawa, unawataja vigogo wa chama hicho, wakiwemo baadhi ambao walijiuzulu nyadhifa zao mapema mwaka huu.

Akizungumza jana na Tanzania Daima Jumapili kupitia simu yake ya kiganjani, Spika Sitta alisema ujumbe wa kuwapo mpango wa kumuua umekwisha kumfikia na ametoa taarifa polisi ili iwapo atadhurika, polisi wawe na taarifa ya hali halisi ya matukio yaliyokuwa yakimuandama.

“Katika hali ya kawaida, naona kama ni upuuzi, lakini si vizuri kupuuza mambo kama haya. Sasa yanaonekana kwa vile yanaandikwa, lakini vinginevyo… inawezekana ni kunitisha ili niache harakati za kupambana na ufisadi uliotanda kila mahali nchini mwetu, lakini hata kama ni kunitisha, sheria zinasema ni lazima utoe taarifa, na ndicho nilichofanya.

“Taarifa nilizopeleka polisi ni mbili. Ya kwanza ni ile inayohusu vitisho vya kuuawa dhidi yangu na Dk. Mwakyembe, na ya pili ni ile inayowajumuisha pia katika mpango huo wa kuuawa kina Anne Kilango, Reginald Mengi, Mbunge wa Mbozi na wenzetu wengine kadhaa.

“Lakini hata kama tukiuawa, sidhani kama itasaidia kumaliza vita dhidi ya ufisadi. Binafsi ninaumia kwa sababu ninawindwa kila mahali, nyumbani hadi jimboni kwangu, nina sms za matusi zinazowatukana pia mke na watoto wangu ambazo ni za kusikitisha sana.

“Jimboni kwangu nako tayari kuna mabilioni ya fedha yamepelekwa, ili kuniangusha katika uchaguzi mkuu ujao, basi tu… wanatumia kila mbinu kutukatisha tamaa. Lakini naamini hawatafanikiwa,” alisema Spika Sitta.

Sitta alisema ameamua kusimamia mapambano ya rushwa bungeni kwa sababu hakuna nchi maskini duniani iliyopata mafanikio ya uchumi bila kupiga vita rushwa, akibainisha kuwa Tanzania sasa ina bidhaa feki asilimia 40, jambo ambalo ni moja ya misingi ya nchi kutopata maendeleo.

Alisema yeye na baadhi ya wabunge wameshindwa kuendelea kuangalia jinsi uchumi wa taifa unavyovuja, lakini wapo baadhi wanaochukizwa na hali hiyo, ambao wanatumia kila mbinu kuhakikisha kuwa hawafanikiwi katika azima yao ya kuhakikisha uchumi wa Tanzania unasimama.

Akieleza kusikitishwa kwake na mikataba mingi ambayo taifa linaingia na wawekezaji, alisema mikataba mingi aliyoiona ilimsikitisha, licha ya kuandaliwa na wataalamu waliobobea, kwa sababu ina upungufu ambao unaligharimu taifa, na kwamba katika hali ya kawaida haipaswi kuachwa ikaendelea kutumika.

“Kuna mambo yanasikitisha kweli, katika baadhi ya mikataba ambayo taifa limeingia na baadhi ya wawekezaji, mingi ni mibovu, ukiisoma utashangaa, hata mtu wa kawaida akisoma mkataba wa aina hiyo lazima atajiuliza, huyu kiongozi aliyeingia mkataba huu na mwekezaji ni wa aina gani? Sasa wapo wenzetu ambao hawataki mikataba hii irekebishwe.

“Tumeamua kulipigania taifa letu, hivyo kuandamwa hakutakwisha, kwa baadhi ya hawa wanaotuandama hawawezi kubadilika, hivyo ni lazima watuandame. Na sisi tutazidisha mapambano,” alisema Sitta kwa sauti thabiti.

Akieleza zaidi kuhusu taarifa alizozipata zinazolenga kumwangusha kisiasa, alisema baadhi ya wanasiasa, bila kuwataja majina, lakini akisema wanatokea ndani ya chama chake, wamepeleka mabilioni ya fedha jimboni kwa ajili ya kuwahonga wapiga kura wake, ili wamkatae kuwa mbunge wao katika uchaguzi mkuu ujao.

Alisema taarifa za uhakika alizonazo zinaeleza kuwa yeye pamoja na wabunge 23 wa CCM ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kupambana na ufisadi serikalini, mipango imeandaliwa ili kuhakikisha hawarudi bungeni, jambo aliloeleza kuwa baada ya muda litabainika kwa kila Mtanzania.

Mmoja wa viongozi aliyejiuzulu miezi kadhaa iliyopita, ambaye anatajwa katika ujumbe unaosambazwa sasa kuwa mmoja wa vigogo waliosuka mpango wa kuwaangamiza wanasiasa wanaoonekana kumuandama, alipoulizwa na gazeti hili kupitia simu ya kiganjani kuhusu yeye kuhusishwa na njama hizo, alikataa kuzungumza lolote.

“Sina taarifa hizo, sitaki…sitaki ku-comment chochote kuhusu jambo hili, samahani sana, naomba uniache, kwaheri,” alisema kisha akakata simu.

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Abdallah Msika, alipoulizwa kama Jeshi la Polisi limekwisha kuanza kufuatilia kuhusu ukweli wa taarifa hizo, hasa baada ya Spika Sitta kutoa taarifa za vitisho kwa jeshi hilo, alisema hana taarifa za kiongozi huyo kutishwa.

“Sina taarifa hizo, labda kama aliripoti Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, lakini mimi sina taarifa. Nashukuru kusikia taarifa hizo, ngoja sasa nianze kufuatilia,” alisema Msika.

Jitihada za kuwapata vigogo wengine wanaodaiwa kuhusika katika mtandao huo wa kuwaangamiza baadhi ya wanasiasa na wale wanaodaiwa kulengwa kuangamizwa hazikufanikiwa hadi tunakwenda mitamboni.

Taarifa ya kuwepo mpango wa kumuangamiza Spika na baadhi ya wabunge zinaeleza kuwa walengwa watakuwa wakiuawa kwa sumu kali ambayo watakuwa wakipakwa na mtu aliyevaa glovu yenye sumu, ambaye atakuwa akimgusa mlengwa aliyemkusudia kumuua.

Inadaiwa kuwa sumu hiyo hatari imeingizwa nchini na mmoja wa viongozi wa kisiasa ndani ya chama tawala kutoka moja ya mataifa ya Kiarabu.

Hii inatisha zaidi.
 
Back
Top Bottom