SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,129
- 7,898
Baada ya ripoti ya FIFA kutoka kuhusiana na ushiriki wa Simba katika Kombe la Dunia la Vilabu 2025, kumezuka malumbano mbalimbali. Kuna upande umekuwa unasema Simba hawezi kwenda kushirki mashindano yale bila kuchukua Ubingwa wa Klabu Bingwa Africa msimu huu na kwa mtazamo wao ana nafasi sawa na Yanga.
Jana baada ya kushiba pilau langu la Krismasi, nikaangalia vizuri mkeka mzima wa FIFA nikaona Simba ana nafasi ya kwenda Kombe la Dunia bila kuwa bingwa wa CAF ndiyo maana hata wao katika chapisho lao wameonyesha Simba ni miongoni mwa timu zinazoweza kufuzu kwa points inazoendelea kujikusanyia. Hapa chini nitaenda kukuonyesha ni jinsi gani hilo linaweza kutokea.
Kwanza nianze kwa kusema, Simba mpaka sasa amejikusanyia point 48 na siyo 45 kama ilivyoainishwa na FIFA kwa sababu ile ripoti iliandaliwa kabla ya mechi ya mwisho ambayo Simba ilishinda 2-0 dhidi ya Wydad.
Tukienda kimahesabu tu, Simba inaweza kufuzu bila kuchukua kombe la CAF Klabu Bingwa kama mambo 3 yatatimia:
1. Bingwa msimu huu awe Al Ahly au Mamelodi
2. Esperance apoteze mechi mbili zilizobaki za makundi na atolewe katika mashindano ya klabu bingwa
3. Simba ashinde mechi mbili zilizobaki za Makundi halafu ashinde mechi zote mbili za robo fainali, halafu ashinde zote mbili za nusu fainali. Katika fainali Simba inahitaji angalau ipate sare moja
Mambo yote matatu yakitimia, Simba atafikisha point 76 sawa na Esperance. Sijajua FIFA watatumia kigezo gani iwapo hali hii itatokea ya timu mbili kulingana point katika rank.
Tuishi humo.
Haki zote za bandiko hili zimehifadhiwa.