Jinsi Simba ilivyodondosha points kizembe ambazo zingerahisisha safari ya Kombe la Dunia

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,129
7,898
Jana wakati nashushia pilau langu kwa mvinyo, nikaanza kukumbuka points ambazo Simba imezidondosha KIZEMBE SANA katika hii misimu minne iliyotumiwa na FIFA kujua timu za kwenda Kombe la Dunia. Nimegundua Simba ingekuwa makini, leo hii tunapoongea hapa ingekuwa na point si chini ya 70 na hivyo kuwa ndani ya michezo miwili tu kuweza kuipiku Esperance.

Katika mchakato wa kujua timu zinazofuzu kwenda Kombe la Dunia la Vilabu 2025, FIFA imetumia misimu ya 2020-2021, 2021-2022, 2022-2023 na huu wa sasa wa 2023-2024. Nitakuonyesha jinsi gani katika kila msimu, Simba ilidondosha points kizembe sana.

2020-2021
Simba vs Kaizer Chiefs. Hapa niliona nisikaze sana maana inawezekana uzoefu uliigharimu Simba ingawa unaweza kujiuliza jinsi timu ilivyojiachia ikafungwa 4-0 katika mechi ya kwanza na kufanya mechi ya marudiano kuwa ngumu zaidi. Kumbuka kuanza ugenini ni faida kubwa. Pia kumbuka jinsi gani Simba ilikosa magoli mengi katika mechi ya marudiano. Ili mambo yasiwe mengi nimeona isiwe tabu, tusiuhesabu huu msimu.

2021-2022:
Simba vs Jwaneng Galaxy. Hadi mapumziko mechi ya pili, Simba anaongoza jumla ya magoli 3-0 (majumuisho ya mechi mbili). Inakuwaje ndani ya dakika 45 unafungwa goli 3 katika mazingira kama hayo? Kwa kitendo cha kutofuzu makundi, huu msimu Simba haikuambulia point hata moja za FIFA.

Tuchukulie Simba ingevuka Ikaingia makundi na tuchukulie tu akashinda mechi 2 kati ya 6 za makundi na bila hata kufika robo fainali, msimu huo Simba ingeongeza point 9 zaidi.

2022-2023:
Simba vs Horoya. Hii mechi ya kwanza Simba ilipoteza nafasi nyingi za magoli na ilistahili kuondoka na point 3.
Simba vs Wydad. Mechi ya kwanza ya Robo fainali, Simba ilipoteza nafasi za magoli za wazi 3 au 4. Simba ingeenda Morocco na mtaji wa magoli 2 au 3 ingefuzu kwenda nusu fainali.

Tuchukulie Simba ingeishia nusu fainali na kupata walau ushindi katika mechi moja, msimu huo Simba ingeongeza point 9 zaidi.

2023-2024 (msimu wa sasa):
Simba vs ASEC Mimosas, Jwaneng Galaxy vs Simba
Bado kumbukumbu zetu ziko fresh kwa mechi hizi mbili. Iwapo Simba ingeshinda badala ya kupata zile sare, ingeongeza point 4 zaidi.

Hapa utaona kwa makadirio tu ya chini sana, Simba ilikuwa iongeze si chini ya point 19. Hivi sasa tunavyoongea ingekuwa na point 70, point 6 tu nyuma ya Esperance. Kwa point hizi, sidhani kama upande wa pili wangekuwa na ubavu wa kubeza uwezekano wa kufuzu.

Haki zote za bandiko hili zimehifadhiwa.
 
Simba tatizo kufungwa huwa hatuoni Dili.

Tungekuwa kama wenzetu wa mtaa wa pili bila ya shaka kufungwa kizembe usingekuwa ndiyo mtindo wetu.
Makosa ya Simba ni ya kujirudia na ni kama hatujifunzi. Ukiangalia hilo bandiko, shida kubwa imekuwa kupoteza nafasi nyingi za wazi na ona mwaka huu malalamiko yamekuwa hayo hayo na hili linasababishwa na kuwang'ang'ania kwa muda mrefu wachezaji ambao wanaigharimu timu. Baleke kwa performance yake ya msimu huu na magoli aliyokosa, angekuwa Yanga angesugua benchi hadi tumsahau ila Simba ndiyo kwanza hakosi first 11.
 
Makosa ya Simba ni ya kujirudia na ni kama hatujifunzi. Ukiangalia hilo bandiko, shida kubwa imekuwa kupoteza nafasi nyingi za wazi na ona mwaka huu malalamiko yamekuwa hayo hayo na hili linasababishwa na kuwang'ang'ania kwa muda mrefu wachezaji ambao wanaigharimu timu. Baleke kwa performance yake ya msimu huu na magoli aliyokosa, angekuwa Yanga angesugua benchi hadi tumsahau ila Simba ndiyo kwanza hakosi first 11.
Magoli aliyokisa Boko siku ya mechi ya kwanza na horoya, Simba wangeshamwacha na kutafuta mtu mwingine Ila bado wako naye na kumtegemea atafanya miujiza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom