Da Vinci XV
JF-Expert Member
- Dec 7, 2019
- 3,837
- 6,372
Leo wakati nadamka asubuhi, mishale ya saa 12 nikasikia kelele uko mtaa wa pili, sijui mchawi kanasa
Kijana nikajitusua kwenda kushuhudia maana sikuwahi kushuhudia mchawi kunasa naskia fununu tu mbalimbali
Wakati nikielekea nilikuwa na dada mmoja, ambaye tuko naye nyumba moja yule dada matusi yalikuwa yanamtoka kana kwamba yeye ndio kanasiwa na uyo mchawi ndani kwake hapo bado alikuwa hajafika eneo la tukio
Hapo njiani pia tukakutana na vijana kadhaa wakiwa na matairi ya gari kwa ajili ya kumtia kiberiti huyo mwanga alienasa,
Kufika eneo la tukio kweli namkuta mwanamama mmoja kapozi pale na vikorombwezo vyake kadhaa wa kadhaaa (nikaona kama igizo fulani hivi) inasemekana nyumba aliyonasa ina wataalamu zaidi.
Alikuwa naked huku wahuni wakijiandaa kufanya yakwao kabla watu hawajajaa.
Wengine waliokuja na visimu vyao wakaona fursa ya kuchukua video.
Kwa pembeni nikasikia bi dada mmoja aking'aka sana,namnukuu
"Choma huyo, wametunyoa sana nywele hawa ku***nina zao ,
Wametuharibia ndoa sana, wametupa ugumba mara mia na mwizi ila sio hawa wafirw***ji
Wametulimisha sana hawa
Tunapata vitambi kumbe wanatunyea vinyesi vyao Mdomoni choma kabisa huyo"
Lakini viongozi wa mtaa walikuwa tayari wameshamka na wataalamu kadhaa (waganga) ,viongozi wadini mchungaji na shehe nao walishatia mguu eneo la tukio
Mie taratibu nikajongea nyumbani nikiacha bado kuna mkwaruzano baina ya viongozi na wananchi wenye uchu na hasira kali.
Binafsi huwa siamini sana katika ushirikina , hii ni baada ya kusoma dini na sayansi vikanifunga kabisaa๐ ๐ ๐ ๐ , kwanza naona ni kinyume cha maendeleo
Nikajiuliza kama hawa watu wanafanya uchafu wote kuua watu kuroga, kufitinisha , na kama alivyosema yule dada eti maswala ya kunyeana mdomoni surely, naweza nikashika mchawi na mwizi na mwizi nikamuacha ila huyu mchawi ni kifo tu๐ ๐ ๐
Una kasumba yoyote kuhusu matukio ya wachawi???
NB: Picha zote hapo juu sio za Eneo la tukio