Agizo la majini

Azer Zepha

Member
Apr 29, 2020
22
23
Agizo la majini 1-5RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu ya 1

Naitwa Mr Roynoo a.k.a mnyama dumaa wengine wanapenda kuniita kwa kwakufupisha hasa hasa mabinti wazuri wazuri wananiita "Roy" nilishaumwaga magonjwa baadhi ya kidunia mfano, homa na Nk. ila yote nilitumia dawa na nikapona. Ugonjwa ambao nilikuwa nimeshindwa kupona kabisa ni ugonjwa wa mapenzi, totoz zilikuwa zikipita mbele yangu aiseee nilikuwa nahisi mwili wangu unasisimka balaa. Nilijipachika jina la mzee wa swaga maana nilikuwa nikimtaka Dem aisee hawezi kuchomoka Kwa swaga zangu nilizonazo.
Aisee huyu Dem alinisumbua sana pamoja na swaga zangu ila nilifua dafu kwake, Hadi nikahisi siwezi kumpata kabisa ila kipindi naenda kukata tamaa ndio wakati Dem alikuwa ameshaanza kunielewa sasa. Aisee Ilikuwa hivi.....

Nakumbuka ilikuwa ni siku ya mwaka mpya tarehe 1/ 1/ 2018, mida ya jioni jioni inaelekea saa 1 usiku. Nikiwa nimenyuka pamba za kinyamwezi Kodi za mambele shingoni bring bring cheni za kimamtoni, chini Sasa ndio usiseme, Laba kalii utasema nimeinunua hela nyiiingi kumbe niliisakuluwa mnadani Kwa buku tano tu😅. Nikiwa naelekea kwenye party huku nikizipiga hatua za kudunda dunda kinyamwezi kama marehemu sharobaro jina lingine Sharo millionea, nikamuona binti mkaliii mbele akija njia hiyo hiyo ninayo pita. Aisee nilihisi kama kengere inagonga kwenye ubongo wangu, Binti alibalikiwa aisee mwendo wake kama hakanyagi chini, mwendo wa kunengua shepu lake daweeee umbo namba nane, chuchu sasaaaa kama ni mda basi ni saa sita kamilii kabisaaa bila hata kuongeza dakika Moja. twende mguu Sasa aiiiiih na kile chake kimini balaa hata bia yenyewe ikasome, Twende face sasa tumadimpoz twake tunaonekana hata asipo Cheka, tumacho twake daah kama kameza kungu, midomo sasa aiiiiiih lips 👄 denda. Nyie Kuna mabinti warembo duniani ila huyu niliona amewazidi wote mnao wajua nyie.

Yule mdada alizidi kuzipiga hatua kusogea karibu na nilipo akiwa na smart phone yake akichat chat, mi nilikuwa nimesimama tu nimeduwaa nikishangaa ule uzuri wake.
Yule mdada akiwa ameishika sim yake kwa mkono mmoja, Ghafla!!.. akakwapuliwa Ile sim na kibaka, Yule mdada alibaha akaanza kupiga kelele za mwizi watu wakaanza kumkimbiza. Yule kibaka akakimbilia Ile ile njia ambayo nilikuwepo, alipofika karibu yangu nikamtega akadondoka chini akataka kuinuka Ili aendelee kukimbia nikamtuliza kwakumuwekea mguu juu ya mgongo wake. Nikamnyanganya Ile sim nikaondoka, nikamuachia msala wa wale wananchi wenye hasira Kali waliokuwa wanamkimbiza, Nikampelekea yule mdada sim yake.

"Kaka Asante sana jamani sijui nikulipe nini maana hii sim inavitu vya muhimu sana ningepoteza Kila kitu Hadi maisha yangu ningepoteza kama ingeondoka"
Nilishtuka kidogo kusikia maneno ya yule mdada et Hadi maisha yake angepoteza kisa simu TU? Mmh niliguna kimoyo moyo ila nikapotezea nikazingatia jambo la pili alilo sema kwamba "Sijui nikupe nini"
Aiseee nilihisi furaha ya ajabu sana kuambiwa vile na binti mrembo kama yule pisi ya mambele, nikamjibu.
"Aah hamna hata usijali ni mambo ya kawaida tu hata usinilipe chochote kile ila naomba nikuombe kitu kama hautojali"
"Kitu gani hicho sema tu hata usijali mi takupa hicho kitu maana umenisaidia sana" alisema yule mdada, nami nikasema.
"Kwanza unaitwa nani?"
"Mi naitwa Yusrat"
"Waooo unafanana na jina lako kama mapacha nyote wazuri"
"Hapana Bhan kawaida tu na wewe je unaitwa nani?" Daah aiseeee nilihisi kama nimelewa bila kunywa bia Kila nilipo mtazama yule binti ndio nilizidi kuchanganyikiwa, nilibaha zaidi baada yakusikia ananiuliza mi ni nani nikamjibu.
"Mi naitwa Mr Roynoo a.k.a mnyama dumaa pull up gang unyamwezi ni mwingi unyama kibao siku hizi wananiita vampare" nikapiga swagga zangu pale, mtoto akacheka.
"Hahahaha unavituko wewee"
"Hapana bhan kawaida tu by the way nilikuwa naomba namba yako"
"Ooh jaman kaka Roy namba tu? Hata usijali andika 0786978618" nikaitoa sim yangu mfukoni nikaiyandika ile namba Kisha nikaisevu "Queen Yusrat" nilipo maliza kuisevu nikairudisha sim yangu mfukoni.
"Bye kaka Roy, nitafute leo Leo Please Usiache kunitafuta"
"Usijali Yusrat mzuri mzuri" tuliagana akaondoka akapita ile ile njia niliyotokea Mimi. sehemu ambapo yule kibaka alipo pigiwa na wananchi wenye hasira kali, Sasa watu walikuwa wameshatawanyika baada ya polisi kufika na kuziwia yule kibaka asiendelee kupigwa baada ya kuwaziwia waliondoka na yule kibaka, mi nikaendelea na safari yangu yakuelekea Kwa Wana kuwapitia ili twende kwenye party.

Siku hiyo ikapita kesho yake mida ya saa mbili usiku nikiwa na sim yangu nachat chat kwenye magroup ya Whatsapp hasa hasa kwenye group la Smart guys la mwanangu side mnyamwezi. Nikapata wazo nimtumie meseji yusrat ila roho ikasita, nikaiseach jina lake kwenye contact zangu za Whatsapp ikaja nikaangalia picha aliyoweka Dp, "Mmh!." Niliguna kidogo baada yakuona ameweka picha nyeusi tiiiiii halafu katikati ya ile picha kuna macho mawili kama ya paka hivi. Nikapotezea nikajua ni picha tu, sikumtext iyo siku nikapotezea. Wahuni tunaelewa plan hiyo huwaga inafanyaga kazi sana hasa hasa ukute huyo Binti amekuweka kichwani halafu usimtafute lazima atakuwaza Sana na ndio mwanzo wakujizolea point zako tatu, Wahuni mnisamehe nimetoboa Siri😅.

Zilipita kama siku mbili hivi sijamtafuta siku hii nikasema ngoja nimtafute, ilikuwa mida ya saa tatu usiku nikamtext.
"Mambo cute Binti uliyebalikiwa uzuri" baada ya dakika kama mbili hivi akajibu
"Poa nani mwenzangu"
"Niite mnyama duma hapa Mr Roynoo, swagga boy"
"Oooh jaman we mkaka mamboo"
"Poa tu mchuchuu Binti mzuri uliyeshushwa kutoka mbingu ya Saba"
"Mmh jaman we mkaka unavituko wewe, kwanza mbona Ile siku nilikwambia unitafute halafu hukunitafuta ona Sasa umeshaikosa zawadi yako" mmh nilishtuka kidogo kusikia alikuwa anataka kunipa zawadi, nikajilaum kutokumtafuta ile siku mi nikiwaza mitego yangu tu.

"Aaah sorry sim yangu ilipata shida kidogo kwahyo sikuwa hewani kabisa ndomana sikukutext bibie"
"Ooh sawa ila ndio hivyo ulishaikosa hiyo zawadi"
"Mmh kwani ilikuwa zawadi Gani hiyo?" zikapita kama dakika 10 bila kujibiwa ile meseji nikamtext Tena.
"Uko bize au?" nayo pia haikujibiwa. Sikumtext Tena nikajilaza kitandani huku nikimuwaza tu yusrat nikivuta taswira ya ule urembo wake daah alikuwa Binti mzuri sana alinichanganya ubongo wangu mnoo. Ghafla nikasikia mlio wa sms kwenye sim yangu nikajiinua haraka haraka halafu nikaichukua sim nikijua ni meseji ya yusrat..
"Aaaaah huyu nae." niling'aka baada yakuona sio meseji yake, alikuwa ni dem frani hivi aliyekuwa ananikubali sana ila Mimi sikuwahi kumuelewa kabisa, aliniambia Kila siku kama ananipenda ila mi sikumkubalia kabisa maana nilikuwa simpendi hata kidogo hata kumtamani pia sikumtamani Bora hata ningekuwa nimemtamani ningemkubalia hivyo hivyo Ili awe ananipa mambo mambo tu, ila hakuwa kichwani mwangu kabisa Kwa vyote yani. Nikaipotezea ile meseji yake sikuijibu, mwisho nikapitiwa na usingizi siku hiyo ikapita.

Asubuhi nilipo amka niliibonyeza sim yangu kitufe chakuwashia mwanga ili nione kama yusrat alinijibu zile meseji nilizo mtext jana ake, ila nishtuka!!.. baada yakukuta meseji za ajabu ajabu kidogo niitupe sim yangu chini...ITAENDELEA..

RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
Whatsp No: 0786978618

Sehemu ya 2

TULIPOISHIA..
Asubuhi nilipo amka niliibonyeza sim yangu kitufe chakuwashia mwanga ili nione kama yusrat alinijibu zile meseji nilizo mtext jana ake, ila nishtuka!!.. baada yakukuta meseji za ajabu ajabu kidogo niitupe sim chini...

SONGA NAYO SASA..
Zile meseji zilikuwa zinasomeka hivi...
"Siku zako za kuishi duniani zinahesabika" nyingine ilisema hivi
"Jiandae kwa kifo" Nilikuwa kama nimechanganyikiwa hivi zile meseji zilinivuruga kiasi frani na zilikuwa zimetumwa kwa namba ngeni nikajaribu kuipiga Ile namba ila ikaita tu haikupokelewa nikaipiga Tena, safari hii haikupatikana kabisa sikukata tamaa nilitaka nimjue yule mtu ni nani aliyenitumia meseji za vitisho vile nikapiga Tena Kwa mara nyingine ila haikupatikana, Hofu ilinitawala sana ila badae nikawaza "Itakuwa ni limtu linalo nijua vizuri linataka kunitisha tu" hofu ikapungua nikatulia kidogo.

Mara meseji ikaingia kwenye sim yangu..
"Habari za asubuh kaka roy" alikuwa ni yusrat
"Ooh jaman salama za wewe bibie umeamkaje"
"Nashukuru nimeamka nikiwa mzima wa afya kabisa kaka angu"
"Ooh sawa halafu mbona unapenda sana kuniita kaka? Kwani unataka kuninyima Nini?"
"Mmh!!.. kwani wewe ulitaka nikuite nani?"
"Uniite tu Roy au ukipenda zaidi niite jina nililopewa na wazazi wangu Yani My love ndo jina langu halisi kabisa hayo mengine ni swaga tu"
"Hahahaaaa usinichekeshe mie, maana naona kabisa unanifunga kamba kweupee"
"Kweli Tena ndo jina langu uwe unaniita ivyo"
"Hapana bhan mi nakuchukulia kama kaka angu, maana unafanana nae sana tena yuko hivyo hivyo kama wewe sema mmetofautiana kidogo tu"
"Mmh!!.. Acha basi naye ni mweusi kama Mimi sio asili yenu ya kiarabu?"
"Ndio yeye ni mweusi maana baba yetu pia ni mweusi sema mimi ndio nimefata asili ya mama"
"ooh sawa ila mi sipendi hilo jina la kaka, Bora hata uniite chawa wako kuliko kuniita kaka"
"Hahahaaa et chawa, haya Bhan mambo chawa wangu"
"Eeeh Bora kuwa chawa wa mdada mzuri kama wewe kuliko kuwa kaka ako"
"Kwanini Sasa?"
"Nikiwa kaka ako sitofaidi vitu vingi kutoka kwako, ila nikiwa chawa afadhali kidogo tafaidi baadhi ya mambo"

"Mmmh!!.."
"Nahisi kama vile nimepigwa kipapai😒, macho hayaoni🙈 na mdomo hausemi🤐ghafla nimekuwa zuzu wako 🥴 aiseee Kamoyo kangu kama vile kanataka kunisariti maana mapigo yananidunda kama vile yanataka kutoka nje😔😘, yote sababu yako.
Nakupenda Sana yusrat❤️🥰💋 nahisi akili yangu haitofanya kazi kama ukinikatalia hili ombi langu🙏 naomba uwe nyota🌞 ya huu mchezo wangu wa mapenzi, naomba 🙏 ukubali uwe derava wa moyo wangu🌹" niliandika meseji fran ya mahaba nikaituma nikiwa na Imani atajaa kwenye chupa yangu ya malavidavi.

baada ya dakika kama 3 hivi akanijibu.
"Hapana mi siko tayari kuwa na wewe"
Aiseee nilihisi kama nimechomwa mkuki mkali kwenye moyo wangu niliumia kupita kiasi cha kawaida, asikwambie mtu mapenzi yanauma sana kama ukimtongoza mtu unayempenda harafu akakukataa.
Aisee maumivu yake hayaelezeki, nilijitetea sana nikimuomba anipe nafasi hata kidogo anipime aone upendo wangu kwake ila bado aligoma kata kata hakutaka kuwa na Mimi kabisa.

Siku kadhaa zikapita, bado sikukata tamaa kila siku nilikuwa namtext meseji zakumjulia Hali na zingine zakuchekesha chekesha nikiwa naimani atanikubalia tu taratibu, nilikuwa naongea nae sana tu kwenye sim, pia voice note Whatsapp na hata video call tulipigiana Sana. Siku Moja tukiwa tunachat chat akaniambia.
"Kaka angu Roy napenda sana kampani yako jinsi unavyonijali zaidi hata ya kaka yangu wa kuzaliwa nae, wanasema unaweza kuwa na ndugu wa hiyari tu lakini mkasaidiana vizuri na mkaishi Kwa upendo mkubwa kuliko hata ndugu mwenyewe. mi naomba uwe ndugu yangu kabisa, nikuite kaka rasmi nawe uniite dada rasmi"

Aiseee nilihisi kama nimedumbukizwa kwenye shimo kubwa lililo jaa moto kote, niliumia sana nikamjibu tu.
"Poa" akatuma meseji ila sikuijibu, baada ya dakika kadhaa akatuma meseji nyingine Tena, ila zote nikazikaushia.
Nilikasirika sana yani ananiambia niwe ndugu yake wakati mi nampenda kimapenzi, jioni Tena akatuma zingine mfurulizo ila zote sikuzijibu, Tena nikamblock kote Whatsapp na kwenye mawasiliano ya kawaida. niliwaza kumtoa moyoni kabisa.

Baada ya siku kadhaa nikaona meseji imeingia Kwa namba ngeni, ilisema hivi.
"Hongera umefaulu mtihani" nikamuuliza
"We nani na mtihani Gani huo nimefaulu?" akanijibu
"Nimelidhia kuwa na wewe na familia yangu pia imekulidhia." nikahisi kabisa atakuwa ni yusrat, sikumjibu nikakausha. Ila nilishangaa kidogo kwamba wazazi wake wamelidhia awe na mimi wakati hawajawahi hata kuniona? Ila Wazo lingine likanijia nikawaza labda atakuwa aliwaonesha picha zangu nilizo mtumiaga Whatsapp.

Ile siku alijitahidi sana kunitumia meseji za mahaba kujitetea kwingi kuonesha kiasi Gani ananipenda kwamba kipindi kile alikuwa ananitania tu aone tachukuliaje ila yeye moyoni mwake alikuwa ashanipenda, Zote meseji zake zikuzijibu akapiga sim ila pia sikupokea kumuonesha kwamba nilichukia kiasi Gani Yani ananifanya kama mdoli ananichezea anavyotaka wakati anajua kabisa naumia.

Kesho yake pia alipiga sim sana pia alituma meseji nyingi akiomba nimsamehe ila sikutaka kabisa kumsamehe kirahisi rahisi siunajua tena lazima ukaze kaze kwanza ili na yeye aumie kama mimi nilivyoumia, siku hiyo ikapita ikaingia siku nyingine bado tu nimeamkaushia.

Siku Moja mida ya asubuhi, niliamka nikachukua mswaki nikachukua na dawa ya meno ila nilipofungua ile dawa nikakuta imeisha ikabidi nizunguke kwenye njia ya nyuma ya nyumba ili niende duka la jirani kuinunua, nikafika yule mzee wa lile duka akanihudumia Kisha akasema.
"Kijana unanyota sana Yani Kila siku ukinunuaga kitu hapa mida ya asubuh asubuhi nauza sana hiyo siku, ila usipokuja kununua kitu chochote hiyo siku biashara yangu inakuaga ngum sana inaonesha nyota yako inang'aa sana"
"Mmmh!!.." Ilibidi kwanza nigune baada ya kusikia maneno ya yule mzee.
"Hapana mzee wangu itakuwa inakuaga tu bahati labda kuna siku unauza sana na kuna siku hauzi basi tu ila sio kwamba mimi nikinunua kitu ndo unauza hapana"
"Kijana ingekuwa ni siku Moja ingekuwa ni sawa ila ni kila siku ukija kununua kitu hapa, Na naimani na leo pia tauza sana maana umeshakuja kuacha baraka hapa"
"Hahahahaha hapana mzee ni mungu tu sio Mimi" ilibidi nicheke maana sikuwahi kusikia maneno kama yale sehem yoyote ya kwamba naachaga baraka.
"Nakushukuru sana kijana wangu uwe unakuja kila siku kuniachia baraka hata kama hauna kitu cha kununua, unachukua hata kajojo tu kahamsini basi."
"Sawa mzee wangu takuwa nafanya hivyo"
"Tashukuru Sana"
"Usijali" nilimjibu Kisha nikaondoka mahala pale, ila kichwani nilikuwa nayawaza sana maneno ya yule Mzee, nikapotezea.

Siku ile ikaenda ikafika hadi mida ya usiku wakati nimelala nimesinzia usingizi mzito nikaota ndoto ya ajabu, nikaota nimefungwa kamba na paka wengi halafu weusi wote. Zikanipeleka Hadi kwenye uwanja hivi na kwenye uwanja huo kulikuwa na paka wengine weusi wote, Nikapelekwa Hadi katikati ya zile paka katikati ya mstari nikakalishwa pale chini. Kisha nikasikia zile paka zinasema.
"Huyu ndio mwangaza wetu inabidi tumtoe kafara tumchinje Ili mambo yetu yaende vizuri" Kisha zile paka zikaanza kucheka zilikuwa na maumbo ya paka ila sauti zao zilitoka za kibinadam wakawaida.

Ghafla!!.. Akatokea paka mkubwa kuwazidi wale wote na yeye alikuwa mweusi pia, na alionekana ndo mkuu wao maana alipofika tu paka zote zikainamisha vichwa chini zikionesha ishara ya kumpa salam. Yule paka mkubwa akasogea Hadi karibu yangu, akaniangaliaa Kisha akaomba apewe kisu frani hivi ambacho kilionekana ndicho wanakitumiaga kutolea kafara, alipopewa akanishika kichwa akaniinamisha chini Kisha kile kisu akakishusha kwenye shingo yangu.....ITAENDELEA..

Usikose sehem ya 3

RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu ya 3

TULIPOISHIA..
Yule paka mkubwa akasogea Hadi karibu yangu, akaniangaliaa Kisha akaomba apewe kisu frani hivi ambacho kilionekana ndicho wanakitumiaga kutolea kafara, alipopewa akanishika kichwa akaniinamisha chini Kisha kile kisu akakishusha kwenye shingo yangu.....

SONGA NAYO...
Kabla kile kisu hakijafika kwenye shingo, ghafla zikatokea paka nyeupeee nyingiii kuzidi Hata zile zilizo kuwepo pale, yule mkuu akasitisha lile zoezi lakunichinja. Ukaanza mpambano Sasa zikaanza kupigana zile paka nyeusi na zile nyeupe, ukatembea mkono ulikuwa ni mwendo wakukwaruzana makucha na kung'atana, wale weusi wanakaonekana wanaelekea kuzidiwa. Yule paka mweusi mkubwa akanifata ili animalize kabisa, mara nikasikia sauti kutoka kwenye zile paka nyeupe ikisema "kimbiaa kimbiaa roy" ile sauti kama nilikuwa naijua ila sikukumbuka niliisikia wapi, kabla hajanifikia yule paka mkubwa nikainuka kwenye duara lile nikakimbia, yule paka akanikimbiza Kwa nyuma mi nikaongeza speed.

Ghafla!! nikashtuka kutoka usingizini, nikainuka nikakaa kitandani ile nageuza shingo chini ya kitanda nikamuona paka mweusi akiniangalia nikajirusha pale pale kitandani huku nikipiga kelele, nikafikicha macho Kisha nikaangalia Tena pale chini sikuona kitu nikahisi labda ilikuwa mawenge yangu tu. mapigo ya moyo wangu yalidunda dunda Kwa Kasi sana, nikavuta pumzi Kwa ndani Kisha nikapumua Kwa urefuu, hofu kidogo ikapungua yakaanza kunijia yale matukio ya kwenye ndoto niliwaza sana ile ndoto inamaanisha Nini, ila sikupata jibu.

Nikanyosha mkono nikaichukua sim yangu kwenye meza iliyokuwa pale pembeni, nikabonyenza kitufe chakuwasha mwanga. Nikakuta missed call na meseji nyingi za yusrat alizonitumia kipindi nimepitiwa na usingizi. Nikafungua meseji Moja tu iliyokuwa imetumwa kwa namba ngeni iliyosomeka hivi.
"Please usilale maana ni hatari Sana kwako jitahidi utafute chakufanya chochote Hadi ifike saa kumi kamili ndo ulale" nilishtuka baada yakusoma Ile meseji, nikaipiga ile namba ila haikuwa inapatikana nikajisemea "taitafuta asubuh" maana nilipoangalia saa ilikuwa saa kumi na dakika 6, nikawaza "Kuna wengine wanalalaga wamezima sim". Nikawaza Tena "huyu ni nani na amejuaje kama Kuna hatari inakuja mbele yangu?" sikuwa na majibu ya maswali yangu wazo nililo pata nikufanya kama naitumia pesa ile namba ili nijue ni nani, nikafanya hivyo ila jina lilikuja ambalo sikulifaham kabisa lilisomeka hivi "Jackline Gerald" Nikairudisha sim yangu kwenye meza Kisha nikajilaza kwenye kitanda ila usingizi uligoma kabisa kuja ile ndoto bado ilizunguka sana kwenye kichwa changu, Baada ya mda mrefu kidogo ndo nikapitiwa na usingizi.

Ilikuwa ni siku ya jumatatu, Nilikuja kuamshwa na sim ya msela wangu mecky.
"Oya niaje mwambaa"
"Safi inakuaje mwanangu"
"Kizazi sana vp leo haufungui duka"
"Daah kwa leo sijihisi poa mkali nahisi kuumwa umwa hivi, labda kesho"
"Ok Dua mzazi"
"Haina kwele" alikuwa ni jamaa yangu pia ni jirani pale kazini kwangu kwenye duka langu la nguo "Roy pamba Kali" na yeye pia alikuwa na duka lake pembeni kidogo la vifaa vya sim, protector, chaji na Nk. Baada ya msela wangu kukata sim nikaangalia saa ilikuwa ni saa 3 na dakika 12, Nikakumbuka niipigie Ile namba iliyonitumia meseji usiku nikaingia kwenye meseji nikaibonyeza Kisha nikaipigia. Iliita tu bila kupokelewa nikapiga Tena ikaitaa mwisho ikapokelewa.
"Halloo"
"Eeh halloo"
"Vp we ni nani?" aliniuliza
"Mi naitwa Roy Jana usku ulinitumia meseji ya kwamba nisilale mapema sjui ni hatari, naomba unielezee vizuri Sasa"
"Hapana labda utakuwa umekosea namba kaka angu, mi kwanza Jana usku sijatuma meseji yoyote tofauti na kupigiwa tu" ilisema ile sauti ya kike.
"Mmh!!...dada acha basi, labda hukumuazima sim mtu yoyote yule?"
"Hapana sim nilikuwa nayo mda wote Hadi kipindi nataka kulala ndo nikaizima"
"Ooh sawa samahan dada angu"
"Poa" Kisha nikakata sim, nilihisi kama maajabu Yani meseji imetumwa kwenye namba yake halafu anasema yeye hakutuma meseji yoyote na wala hakuazima sim mtu. Duuh nilibaki na viulizo vingi, wazo likanijia nizijibu zile meseji za yusrat maana ukweli nilikuwa nimemmis Sema ndo hivyo lazima uvunge kidogo, ili asikuchukulie poa poa.

"Poa vp"
"Duuh Leo ndio umeamua unijibu?"
"Achana na hayo maswali vp uko poa?"
"Salama tu sjui wewe?"
"Mi siko poa sana nahisi kuumwa umwa unaweza kuja kuniona?"
"Mmh!! saa ngapi?"
"Mda wowote tu hata sasa hivi"
"Sawa ngoja nimalizie kazi hapa halafu nitakucheki unielekeze"
"Poa" Duuh sikuamini kama mtoto amejaa kiwepesi vile, nikainuka haraka haraka nikatandika kitanda vizuri Kisha nikapanga vitu vyote sawa halafu nikaenda kuoga nikapiga na mswaki huko huko, nilipotoka nikapiga pamba za kiaina mixer maperfume perfume nikanukia bomba, nikaenda kuchukua vitafunwa, sukari na majani ya chai, kisha nikarudi nikaviweka mezani kwakuwa gesi ilikuwa imejaa nikatulia ili akija aje achemshe chai chap chap, Wahuni Simnajua kale kafeeling Dem akikwambia anakuja geto? Basi Mimi ndo kalikuwa kamenivaa kabisa.
Baada ya mda kidogo ikaingia meseji
"Tayari nishamaliza nielekeze Sasa ni wapi"
Sikutaka kumuelekeza kwa kutumia meseji nikamvutia waya Kisha nikamuelekeza Hadi mtaa ambao nakaa, kwakuwa maelezo yangu yalikuwa yamekaa unyama basi alielewa haraka.

"Nishafika hapa uliponiambia" iliingia meseji ikisomeka hivyo, nikatoka ndani chap nikaenda kumchukua nikamleta Hadi geto.
"Hili ndio getto langu mama angu karibu Sana"
"Asante baba, getto lako zuri liko safi halafu linanukia"
"Hamna kawaida sana, siunajua mi na usafi ni dam dam" nikajivimbisha kichwa pale mixer miswaga swaga kama yote.
"Nimependa Kila kitu kilivyo pangwa humu ndani hata sipati tabu kupanga Tena maana nilijua takuta pako shagala bagala nije nisafishe nipange kila kitu vizuri ila hapa umenisaidia." Alisema yusrat, nikajisemea kimoyo moyo
"Duuh huyu mtoto alivyoumbika leo hatoki lazima achinjwe nimle, cheki hizo chuchu cheki hilo paja duuuh hatari aisee"
"Kwahyo unataka unile mi ni msosi?"
Nilishtuka!!.. Baada yakusikia najibiwa vile, maana mi nilikuwa naongea kimoyo moyo sasa yeye alisikiaje, nilishangaa huku nikirudi nyuma kidogo.

"Sasa mbona unashangaa siumesema mwenyewe tena kwa sauti et unataka unile, au umejisahau ukahisi unaongea kimoyo moyo?"
Mmh nilishangaa maana mi kumbukumbu zangu nakumbuka sikutikisa mdomo kabisa iweje aniambie et nimeongea kwa sauti, ila nikawaza "huenda kweli nilijisahau Sasa yeye alisikiaje kama sikutoa sauti?" nikapotezea baada ya kuwaza hivyo hofu yote ikatoka. Sikumwambia chochote alijiongeza yeye mwenyewe akawasha jiko la gesi Kisha akatenga chai, baada ya mda kidogo ikaivaa tukanywa huku tunacheka na kufurahi. Sasa sijui nini kilinipata kikombe Changu cha chai kikaniponyoka mkononi kwa bahati mbaya, kwa speed ya ajabu yusrat akakidaka hata chai haikumwagika Wala hata haikutikisika. Nilishangaa uwezo ule aliokuwa nao.
"Duuh ushawahi kuwa mwana sarakasi Nini?"
"Hii michezo yakudaka vitu niliicheza sana kipindi niko shule kwahyo hata sio kazi kubwa kwangu."
"Mmh!! hongera" Baada yakunywa chai mi macho yalikuwa yananitoka tu Kila nikitazama uzuri wa yusrat, Hadi udenda nilihisi unataka kunitoka nilikuwa na usongo nae sana. Akatoa sahani na vikombe tulivyo nywea chai akaviweka kwenye beseni ya vyombo vichafu Kisha akajirusha kitandani.
Nikajisemea kimoyo moyo
"Hapa Sasa ndipo nilipokuwa napataka" nami nikajirusha kitandani, Tukaanza kucheza michezo ya wapendanao kutekenyana kurushiana mto na Nk. Tukiwa tunaendelea na ile michezo ghafla!!..akabadilika akawa na sura ya hasira Kisha akanishika kichwa Kwa nguvu halafu akasema....ITAENDELEA..

Tukutane sehemu ya 4.

RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: Mr Roynoo
Whatsp No: 0786979618

Sehemu ya 4

TULIPOISHIA..
Tukaanza kucheza michezo ya wapendanao kutekenyana kurushiana mto na Nk. Tukiwa tunaendelea na ile michezo ghafla!!..akabadilika akawa na sura ya hasira Kisha akanishika kichwa Kwa nguvu halafu akasema....

SONGA NAYO SASA...
"Nenda hapo dirishani uone" Nikashuka kutoka kwenye kitanda Nikasogea hadi dirishani nikafunua pazia kisha nikachungulia kwa nje nikamuona mtu anaishilizia.
"Vp ni nini?"
"Huyo ni mtu mbaya kwako na alikuwa anachungulia ili ajue kama upo"
"Mmh!! we umejuaje kama ni mtu mbaya na umemuonaje?"
"Mi kipindi natazama dirishani nimemuona anachungulia na jinsi alivyokuwa anachungulia inaonesha kabisa anania mbaya"
"Mmh!!.. Wezekana ni mwizi tu sio kwamba ni mbaya kwangu."
"Mmh!! haya ila chunga sana na hao majirani zako, sio kila mtu anania nzuri na wewe"
"Unajua unanipa mawazo sana we ni mganga au ni mtabiri unayeona ya mbeleni au we ni nani? Maana sikuelewi maneno yako"
"Mi sio mganga wala sio mtabiri ila nakupa ushauri tu Hii dunia inamambo mengi sana mi nakupa na tahadhali pia, sio kila unayemuona anakuchekea ni mzuri kwako, wengine wanajificha kwa tabasam lao ila moyoni mwao Nia Yao nikuona unapotea kabisa kwenye huu ulimwengu"
"Ila ni kweli unayosema baadhi ya binadam ndivyo tulivyo" nilisema Kisha nikapanda kitandani, michezo ikaanza upya tukacheza mwisho hisia zikatuteka tukapeana mahaba mengi mengi Hadi mengine yakamwagika, baada ya mda tukawa hoi Kila mtu akawa ameushusha mzigo mzito aliokuwa ameubeba. Tukaenda kuoga wote pamoja, wakati tunarudi nilishtuka kidogo baada ya kumuona yule mdada anayenipendaga akiwa anatuangalia Kwa mbali kidogo, nikapotezea tukaingia zetu ndani.

Hiyo siku niliinjoi Sana penzi la yusrat maana alishinda na Mimi kutwa nzima ilikuwa ni mwendo wakupeana tu kila mda, chakula cha mchana akapika tukala akaosha vyombo vyote vichafu akapanga vitu vizuri vilivyokaa vibaya, ilipofika jioni ndo akaaga anaondoka. Nikamshindikiza wakati tunazipiga hatua za kuelekea zinapopaki bodaboda, tukawaona wazee wawili wakiwa wamekaa kwenye benchi wanapiga story tukapita pale pale njiani tukawasalimia Kisha tukaendelea kusonga mbele, mara yusrat akasema.

"Unawaona hao wazee?"
"Ndio nawaona situmewapita pale na tumewasalimia kabisa"
"Basi walikuwa wanakusema wewe na Hadi Sasa hivi ndo wanakuzungumzia"
"Kwani nimefanya nini hadi wanizungumzie au Kisa kukuleta wewe"
"Hapana hicho sio chanzo chakuzungumziwa, ni kwamba hawakupendi tu wala hawataki hata kukuona hapa duniani"
"Mmh unajua unanipa mashaka we umejuaje?" nilimuuliza na yusrat akajibu.
"Hivi kipindi tunapita pale hukusikia wanaongea au wewe ulikuwa unawaza Nini?"
"Mmh!!.. Kiukweli mi sikusikia kabisa"
"Mi nilisikia na inaonekana ni watu wabaya Sana kwako jichunge nao"
"Sawa nimekuelewa tajichunga nao" tulifika kwenye stend ya bodaboda akapanda Kisha tukaagana mi nikarudi zangu geto nikapita ile ile njia tuliyopitia mara Mzee mmoja akaniita kati ya wale wawili waliokuwa wamekaa pale kwenye benchi, nikaenda Hadi pale.

"Kijana kaa hapa tuongee kidogo" alisema mzee mmoja, nikakaa
"Niambieni wazee wangu"
"Hivi yule uliyekuwa nae ni nani Yako?"
"Ni mpenzi wangu"
"Mmh!!.. Unamjua vizuri?"
"Mmh!.. Mzee Sasa mpenzi wangu nisimjue"
"Ni nani kama unamjua?"
"Anaitwa yusrat"
"Sio hivyo yani unamjua kiundani?"
"Ndio najua Hadi familia yao pia naijua"
"Hahahaha acha uongo we kijana, unauhakika familia yake ushawahi kuiona?"
"Kiukweli hapana bado sijawahi kuwaona"
"Siunaona Sasa, we humjui vizuri yule mdada ni mtu mbaya sana kwako unatakiwa ujichunge tena ukae nae mbali"
Mmh nilishtuka!!..kusikia maneno yale nilishindwa nimuelewe nani kati yusrat au wale wazee.
"Kijana mbona unawaza sana, sikia siunajua mi ndio mganga hodari mtaa huu kwhyo mtu yoyote mbaya akipita mbele yangu lazima nimjue yule mdada hayajaja kwako kwa wema anataka akuuwe."
"Heeeeeh!!..." Nilishtuka!! sana kusikia maneno yale, nikainuka nikawaaga kisha nikaondoka.
"Kijana usipuuzie maneno yetu, tunakupenda ndomana tunakwambia hivyo" nilisikia sauti zao kwa mbali kidogo zikiniambia, mi kichwa kilikuwa kimeshachanganyikiwa nilishindwa nimuamini nani Kila mtu kwangu nilianza kumuona kama adui yangu.

Nilipofika Getto nilishangaa kumkuta yule mdada anayenipendaga akiwa amekaa kwenye ngazi za kupanda kwenye mlango wangu, aliponiona akainuka akanisogelea Kisha akasema.
"Roy kwhyo ndo umenikataa Mimi mchamungu ukamfata yule Pepo"
Kichwa changu hakikuwa sawa kabisa na huyu pia akaniongezea mengine, nilishangaa Sana kusikia maneno Yale Kwa hasira nikasema.
"Wewe naomba ukome kumuita mpenzi wangu Pepo, hata kama ni Pepo we haikuhusu amempata Pepo mwenzake, wewe mchamungu kamtafute mchamungu mwenzako." nilisema kwa hasira huku nikiwa nimemshika shingo, nikamuachia nikapiga hatua za kwenda kuufungua mlango.
"Itabidi nikuombee maana sio akili zako hizo inaonekana unapelekwa pelekwa tu na mapenzi yakijini" alisema yule mdada aliyekuwa anajulikana Kwa jina la Lucy, nikahairisha kuufungua mlango nikageuza shingo nimtazame vizuri.

"We hivi umekosa kazi zakufanya et eeh? Nenda ukajiombee mwenyewe upate bwana anayekupenda Mimi sikupendi elewa niache na Pepo wangu."
"Sawa najua hunipendi ila mi nakupenda na sitochoka kukwambia hili neno naimani we ni wangu tu Bado uko kwenye njia yenye miba ila ipo siku tu utafika kwenye njia yangu salama."
"Usijidanganye nilikuwa sikupendi hata kabla sijawa na huyu kwhyo hata kama nikiachana nae Bado sitokuwa na wewe maana sikupendi hivi hujui kama mapenzi ni hisia?"

"Najua sana tu na pia hisia zinatengenezwa naimani tazitengeneza za kwako ziwe kama za kwangu"
"Acha kujisumbua tena usiniumize kichwa changu ondoka hapo kabla sijakufumua fumua."
"We njoo tu unipige maana ndio fursa pekee yakushikwa na wewe kwanza ukinipiga ndo tajisikia Raha"
"Heeeeeh!!! We Binti we ni kichaa au? Mbona huelewi, nishakwambia sikupendi sikupendi sikupendiii elewa basi"
"hivi ulikuwa hujui? Ndio mi ni kichaa tena kichaa wa penzi lako"
nilibaki nimeduwaa kumfata kumpiga nilishindwa, ilibidi nifungue tu mlango niingie zangu ndani ili kuepusha matatzo mengine. Kisha nikaufunga ule mlango kwa ndani, nikajitupa kitandani. Niliwaza sana maneno niliyoambiwa pande zote mbili aliyoyasema yusrat na walio yasema wale wazee pamoja na Lucy, mmh nilibaki njia panda nikafananisha maneno yusrat alisema wale wazee hawataki kuniona duniani, na wale wazee walisema yusrat anataka kuniua na Lucy alisema nadeti na pepo. Wanasema maneno ya watu wengi ndio yananguvu, nikaanza kuyaelewa maneno ya wale wazee pamoja na lucy haiwezekani wote wamuone ni mbaya Hadi Lucy? Mmh!! Nikawaza Tena Ila Lucy wezekana ni wivu tu wa mapenzi ndomana anamwita vile? "Mmmh!!." niliumiza kichwa sana ila sikupata majibu sahihi ya maswali yangu.

Niliwaza sana baada ya mda kausingizi kakanipitia, nilikuja kushtuliwa na mlio wa sim mida ya saa 3 usiku. Alikuwa ni yusrat kanipigia, nikapokea sikutaka kumuonesha wasi wasi wowote nikaongea nae vizuri tu.
"Hello darling ulikuwa umelala?"
"Ndio nilipitiwa na usingizi"
"Umeshakula chakula Cha usku?"
"Mmh hapana nahisi nimeshiba Sina ham yakula kabisa vyakula vyako vimenishibisha."
"Mmh vyakula Tena sio chakula?"
"We siulinipa aina mbili tofauti za vyakula au umesahau?"
"Ooh sawa, nimekuelewa nilikuwa sijaelewa maana Yako."
"Wewe je umeshakula?"
"Mimi pia ni kama wewe tu sina ham kabisa ya kula, Nikwambie kitu Roy?"
"Niambie"
"Najua unamaswali mengi sana juu yangu, ila tafadhali usiniwazie vibaya mi nakupenda sana na nina nia njema na wewe, naomba kwa leo upumzike Kesho takwambia yote yanayo nihusu Mimi"
"Mmh kwanini usiniambie leo Leo"
"Hapana saizi ni mda mbaya wa kuzungumzia mambo hayo."
"Sawa, usiku wema Sasa"
"nawe pia" akakata sim, nikafunguwa sasa meseji nilizotumiwa kipindi nimelala Moja ilikuwa niyababa mwenye nyumba ilisomeka hivi.
"Mwezi umeisha Leo, kesho ndio siku yakulipa kodi, tafika hapo asubuhi kabla haujaenda kazini" niliisoma nikaipotezea sikuijibu nikaiweka sim pembeni ya mto.
nikahisi nimebanwa na haja ndogo, nikajiinua pale kitandani nikashuka chini nikasogea Hadi mlangoni nikaufungua mlango ili nitoke nje, wakati nainua mguu ili nikanyage pale chini kwenye ngazi nikashtuka!!.. Baada yakuona kitu...ITAENDELEA...

Usikose sehemu ya 5

RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu ya 5

TULIPOISHIA..
nikahisi nimebanwa na haja ndogo, nikajiinua pale kitandani nikashuka chini nikasogea Hadi mlangoni nikafungua mlango ili nitoke nje, wakati nainua mguu ili nikanyage pale chini kwenye ngazi nikashtuka!!.. Baada yakuona kitu...

SONGA NAYO...
kwakuwa kulikuwa na taa ya nje niliweza kuona vizuri, pale chini kwenye ngazi Kulikuwa na maandishi yameandikwa na mkaa, yalisomeka hivi.
"Roy takupenda siku zote za maisha yangu. By Lucy"
"Duuh" Nilistaajabu kidogo maana binti namwambia simpendi lakini haelewi, nikashuka chini nikaokota kakaratasi nikayafuta yale maandishi. Kisha nikazipiga hatua za kwenda uwani, mara akatoka nje mpangaji mwenzangu kwenye chumba Cha pembeni maana kutwa nzima alikuwa kazini kwahyo hatukuwa tumeonana ile siku, tukasalimiana Kisha nikaenda kujisaidia halafu nikarudi kulala.

Usiku mnene nikiwa nimelala fofofo, walikuja paka wawili weusii tiii ghafla wakabadilika wakawa watu, wakaichomoa nafsi yangu kutoka kwenye kiwili wili changu. Safari hii haikuwa ndoto ilikuwa ni live kabisa, niliuona mwili wangu ukiwa umelala pale kitandani Mimi nafsi nikavutwa Hadi pale waliposimama wale wazee wachawi walioniambia et yusrat anataka kuniua. Nikatoweka nao, nikapelekwa sehemu ambayo niliifaham kwenye mti mkubwa sana uliokuwepo mtaani hapo ila tulikuwa tunaupitaga tu bila kujua kama ndio sehemu wanapofanyia vikao vyao wachawi.

Pale kwenye ule mti tulikuta paka nyingi, zikiwa zimekaa na zote zilikuwa nyeusi. Nikafikishwa Hadi katikati ya zile paka nikawekwa pale chini, katika hali yakushangaza nikamuona yule paka mkubwa niliyemuona kwenye ndoto akisogea Hadi pale nilipo. Ghafla paka zote zikabadilika zikawa binadam wakawaida tu, nilishtuka!!.. Baada yakuona yule paka mkubwa kumbe ndo yule mzee mwenye lile duka kubwa pale mtaani aliyeniambia et mi Nina bahati sana et nikinunua kitu chochote pale dukani kwake lazima hiyo siku auze sana. Nilishangaa Sana maana pia niliziona sura baadhi za watu nao waonaga pale mtaani, wale wazee wawili walio nileta wakasikika wakisema.

"Mkuu kama ulivyotuambia tumeileta nafsi ya yule kijana"
"Mmh!!.. Naomba mnisaidie wenzangu leo ni siku ya kafara?" aliuliza yule mkuu
"Hapana mkuu, leo nikikao tu cha dharula" zilisikika sauti za wale wachawi wengine wakijibu. Kisha yule mkuu akawageukia wale wazee walionileta.
"Mmesikia? Sasa nyie mnamleta huyu wa nini wakati sio Leo?"
"Mkuu nakumbuka ulisema kikao kinachofata tuje na nafsi yake" alisema mzee mmoja kati ya wale walionileta.
"Ndio niliwaambia kikao kinacho fata yani jumatano siku ya kafara, Leo ni kikao Cha dharula tu sio kikao maalumu."
"Kwhyo tumrudishe au?"
"Hapana mkimrudisha itakuwa tatizo kwetu maana ameshatutambua kama sisi ndio wabaya wake, mi taenda nae nimuweke kwenye chumba changu cha misukule ikifika siku ya kafara ndio takuja nae" alisema mkuu wawale wachawi aliyejulikana kwa jina la mzee nyanda, wakamuitikia.
"Sawa mkuu" waliitikia wale wazee wawili Kisha wakaniacha pale kwenye duara nimekaa wenyewe wakaenda kukaa Kwa wachawi wenzao, nilikuwa nimejawa na uoga Sana na nilizidi kushangaa maana nilikuwa nawaona watu ambao sikuzania kabisa kama wanaweza kuwa wachawi.

"Mmmhh!!.." niliguna baada yakumuona boda boda anayenipelekaga kwenye miti kasi yangu akiwa amevaa kichawi, macho yangu yalizidi kuangaza nilishtuka sana!!.. Baada yakumuona mama mmoja hivi ambae nilikuwa namuheshimu sana maana alikuwa anataka kufanana na mama yangu kimaumbile na sura kwa mbali, nilistaajabu sana baada yakumuona pale. Nilikuja kuchoka zaidi nakujua kwamba nilikuwa nimezungukwa na watu wabaya kila sehemu, baada yakumuona jirani yangu yule jamaa aliyepanga kwenye chumba cha pembeni yangu kwenye ile nyumba nayoishi tuliyesalimiana usiku ule ule wa jana ake, akiwa miongoni mwa wale wachawi.

Nilichoka roho, mwili na akili nikaanza kuyakumbuka maneno ya yusrat aliyoniambia kwamba "chunga sana hao majirani zako, sio kila mtu anania nzuri na wewe"
Alisema pia.
"Mi sio mganga wala sio mtabiri ila nakupa ushauri tu Hii dunia inamambo mengi sana mi nakupa na tahadhali pia, sio kila unayemuona anakuchekea ni mzuri kwako, wengine wanajificha kwa tabasam lao ila moyoni mwao Nia Yao nikuona unapotea kabisa kwenye huu ulimwengu"

Nikawaza "Sasa yeye alijuaje kama Kuna baadhi ya majirani zangu ni wabaya au na yeye ni mchawi mwenzao ndomana aliwajua? Mmh Sasa mbona simuoni kwenye Hawa wachawi au yeye amepata udhuru Leo? Mmmh!!"
Kichwa changu kiliwaka moto nikaona hata yusrat ni wale wale tu, nikiwa kwenye dimbwi zito la mawazo mara nikasikia mchawi mmoja anamalizia kusema
"Kwahiyo mkuu ndo hivyo leo hatoudhulia kwenye hiki kikao, amesema tutachojadili tutamfikishia taarifa"

Moja kwa Moja nikahisi aliyepata dharula atakuwa ni yusrat, Mara nikasikia mkuu wao mzee nyanda anasema.
"Tumeitisha hichi kikao Cha dharula Kwa mambo makuu mawili, Kwanza tunamsaidiaje mwanachama mwenzetu mama kombo, anayeumwa Sana baada ya kupita juu ya nyumba ya shekh mahmudu, mtaa wa jirani. Pili ni huyu Binti aliyekuja kwenye maisha ya huyu kijana yani yusrat, tunafanyaje kumuangamiza kabla haijafika jumatano siku ya kafara, Maana atatibuwa mipango yetu kama tusipo muangamiza mapema, ndomana nimewaita hapa tuone tunamuangamizaje huyo Binti kwanza halafu tukishamaliza hilo swala ndo jumatano tushughurike na huyu kijana sasa."

Nikishtuka!!.. Baada yakusikia Yale maneno ya mzee nyanda, ndo nikaamini kweli yusrat anania nzuri na Mimi, wale wachawi ndo wanania mbaya na Mimi. Nikaona mchawi mmoja kati ya wale wachawi waliokaa chini akinyosha mkono na kuinuka.
"Mkuu ningependa kuchangia neno, Nianze na mama kombo, mama kombo kwanza anakiburi sana yani hataki kuambiwa kabisa anajikuta yeye ndio yeye anaenda kinyume na taratibu zetu mara nyingi tu, na tumeshasema kabisa tukiwa kwenye safari zetu tupite njia zote ila tusipite kwenye ile njia juu ya nyumba ya shekh mahmudu ila yeye alivyo najeuri hakusikia akajiona ananguvu sana akapita ona sasa kilicho mkuta, mi nashauri tuachane nae maana hatuwezi kumtibu."

"Hapana hata kama anakiburi lakini bado ni mwanachama mwenzetu lazima tumsaidie kwa namna yoyote Ile, mi natoa amri Sasa wewe mwenyewe na mzee pago pamoja na mzee fundikila mtaende Hadi kwa huyo shekh mahmudu mumuombee msamaha mama kombo ili amponyeshe, tumeelewana?"
"Ndio mkuu laki..."
"Hakuna Cha lakini mnatakiwa kufanya kama nilivyo waambie mmenielewa?"
Wakaitikia wote watatu walio teuliwa.
"Ndio mkuu"

"Nafikiri hilo jambo la kwanza tumelimaza tuingie sasa la pili nala mwisho, tunafanyaje kumuangamiza paka mweupe yusrat au tufanyeje hiyo siku ya kafara asituharibie mipango yetu yakutoa kafara kubwa sana itayo tufanya mali zetu ziongezeke hata maisha yetu pia yawe mazuri"alisema mkuu wawachawi Mzee nyanda, mara akaonekana mchawi mmoja akinyosha mkono.
"Haya wewe hapo wazo lako ni lipi?"
"Nashukuru kwakunipa nafasi hii, mi napendekeza tumfate Leo Leo pale anapoishi tumuangamize"
"Mwingine, eeh na wewe unasemaje?" alisema Mzee nyanda akimteua mwingine aliyenyosha mkono atoe wazo lake na yeye.

"Mkuu mi nashauri tusimuangamize maana ananguvu sana tutachukua mda sana kufanikisha jambo Hilo mi naona tutume nguvu zetu za kichawi tumpumbaze hiyo siku ya kafara apate usingizi mzito asiweze kuamka" alisema yule mchawi Kisha akakaa
"Nyote wawili mmetoa mawazo mazuri ila sio kazi rahisi kama nyie mnavyo chukulia maana ananguvu sana pia anasaidiwa na wazazi wake kwhyo sio rahisi kufanikisha kumlaza usingizi mzito, mi naona tulifanyie kazi lile wazo la kwanza Yani tumvamie sasa hivi tukamuangamize kabla hajajipanga." alisema mzee nyanda, wachawi wote wakasaport wazo lake wakachaguliwa wachawi 13 ambao wanauwezo mkubwa ndo wakapewa kibarua cha kukamilisha mission ile, Mzee nyanda akiwemo na wale wazee wawili walio nipeleka pale wakiwemo pia.
Mzee nyanda akanisogelea akanishika kichwani, ghafla!!.. Nikatoweka nikatokezea kwenye chumba Cha kutishaa.....ITAENDELEA..

USIKOSE SEHEMI YA 6
 
Bring bring? No ni bling bling.
Laba? No ni raba.

Mwanetu pitisha andiko lako chatgpt lirekebishwe hizi L na R
 
Agizo la majini 6-10

RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: Mr Roynoo
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu ya 6

TULIPOISHIA..
wakachaguliwa wachawi 13 ambao wanauwezo mkubwa ndo wakapewa kibarua cha kukamilisha mission ile, Mzee nyanda akiwemo na wale wazee wawili walio nipeleka pale wakiwemo pia.
Mzee nyanda akanisogelea akanishika kichwani, ghafla!!.. Nikatoweka nikatokezea kwenye chumba Cha kutishaa...

SONGA NAYO...
Nilishtuka!!.. Baada yakujikuta nimetokezea sehem tofauti na nilipokuwa, nilijikuta nimekaa kwenye chumba kikubwa na kilikuwa kichafu Sana kilitoa halafu ya uozo, kichwa changu hakikuwa kimetulia kabisa kutokana na ile hali yakutoweka ghafla kule halafu kujikuta sehem nyingine nilikuwa naona mawenge tu. Baada ya dakika kadhaa ndo macho yangu yakaanza kuona vizuri Sasa nikaanza kukiangaza angaza kile chumba vizuri nikawaona watu wenye asili ya misukule wakiwa makundi tofauti tofauti wengine wakiwa wamelala wengine walikaa karibu na ukuta wengine katikati ya chumba kile, udelelee uliwashuka Kila sekunde halafu walikuwa wamechakaa Sana nywele zao zilijikunja kunja huku zikiwa na uchafu mwingi sana kama vile imepita miaka mingi Toka maji yaingie kwenye nywele zao pamoja na miili yao.

kwenye hicho chumba walikuwepo wadada, wakakaa, wamama, na wababa pia. Nilizidi kushangaa sana maana Kuna wengine sura zao hazikuwa ngeni machoni mwangu, miaka miwili niliyokaa kwenye mtaa huo ilitosha kabisa kuwafaham baadhi ya watu. Macho yangu yalitua Kwa kijana mmoja aliyekuwa amelala ameegamia ukuta, alionekana zaidi ya Teja wa madawa ya kulevya alitia huruma Sana, taswira yake ikaanza kuja taratibu nikamkumbuka ni kijana aliyefariki mwaka mmoja uliopita na maziko yake niliudhulia. Wazazi wake, ndugu jamaa na marafiki walilia sana maana kifo chake kilikuwa nichakutatanisha sana. Alikuwa anatembea tu njiani ghafla akadondoka chini akafariki pale pale njiani, kifo chake kiliusishwa na uchawi japo watu wenye Imani zao walisema siku Yako ikifika haijalishi uko wapi utakufa tu. Nilimfata mama ake nikampa mkono wa pole kisha nikamwambia. "Pole sana mama ni mipango ya mungu, yeye ametangulia na sisi tutamfata huko huko alipokwenda."
Kumbe sikujua mungu hakumpenda zaidi Bali binadam ndo walimpenda zaidi, na niliposema tutamfata huko huko ndo hapo sasa nilipomfata alipo yeye, niliumia sana nilijikuta machozi yananitoka bila kutaka.

Nikamsogelea yule kijana aliyekuwa rafiki yangu japo haikuwa sana kiihivyo, nikasema.
"Pole sana raso, baada ya miezi 5 ya kifo chako cha uongo mama ako nae alifariki, naamini ukishatoka hapa kwenye miliki ya mtu mbaya utamfata huko kwenye wafu wa kweli" Nilimuhurumia sana, ila nilikuwa sijawatazama vizuri wengine ndomana nilisema vile. Baada yakuangaza angaza macho kuona nani mwingine nayemjua zaidi
"Heeeeh!!!.." nilishangaa baada yakumuona mama wa yule kijana niliyekuwa namzungumzia kumbe na yeye yupo hapo hapo kwenye wale misukule wamama wamama.
"Duuuuh!!.." nilichoka Kila kiungo.

(Hapa nahadithia matukio ambayo sikuyaona ila nilikuja kuhadithiwa kwa badae ndo nikayajua.)
Upande wa wale wachawi 13 walio chaguliwa kwenda kumuangamiza yusrat, walifika kwenye nyumba anayoishi wakataka Wazame ndani mazima. Waliposogelea nyumba tu wachawi 8 wakadondoka chini, wakabakia juu wale wenye uwezo mkubwa wa 5 wakiwa juu ya ungo zao za kichawi. Wakazama Hadi ndani ya nyumba, wakaanza kumsakanya yusrat ila hawakufanikiwa kumuona.
"Mkuu tunafanyaje maana humu ndani hayupo" alisema Mzee fundikila
"Amejua mpango wetu ndomana amekimbia" wakati wanajadiliana mule ndani mara sikasikika sauti za paka zilkilia nje ya nyumba Ile, wakatoka nje upesi upesi kwenda kuona kinachoendelea kule nje. Walishangaa sana baada yakuona wale wachawi wenzao walio dondoka chini waking'atwa na paka nyeupe, zile paka ziliwalarua kweli kweli wengine walikatika vichwa wengine viungo vyao vyote vilitolewa hakuna ambae alikuwa hai wote waliuwawa zilitapakaa dam tu pale nje.

Kwenye zile paka nyeupe ikasikika sauti yakike ikisema
"Unaingia kwenye nyumba za watu bila kibari unaingia tu kama kwako haya niambie unashida gani na mimi?"
Alikuwa ni yusrat akiwa kwenye umbile la paka.
"Shida yetu tumekuja kuutoa uhai wako" alisema mzee fundikila
"Ooh sawa njoeni muuchukue mkiweza mtaondoka nao" alisema yusrat.

Wale wachawi watano wakajigeuza wakawa paka weusi wakubwaa, wakaanza kupigana na wale paka wengi wenye rangi nyeupe. pambano lilikuwa kali sana walikwaluzana wakang'atana mwenye kutoka na sikio, jicho, pua, mkono, mguu, walitoka navyo. Wale wachawi watano walipigwa vibaya mnoo Kila pande ya miili yao ilikuwa na vidonda wengine hawakuwa na viungo baadhi, aliyekuwa Bado ng'ang'ari ni mkuu wao mzee nyanda yeye viungo vyake vyote bado vilikuwepo, alipata majeraha madogo tu. Vile vile kwa yusrat majeraha alikuwa nayo madogo tu, na wale watu wake walikuwa Bado wako imara. Wale wachawi watano wakajibadirisha wakarudi kwenye umbo la kibinadam, Mzee fundikila hakuwa na mkono pamoja na sikio, Mzee Pago alibaki na jicho Moja pamoja na mguu Moja. Wale wengine wawili ndo walikuwa wamepigwa vibaya mnoo hawakuwa na miguu yote miwili pamoja na mikono hata macho pia hawakuwa nayo walikuwa wanapumua kwa mbali sana.

"Tutakuja Kwa mara nyingine kuifata roho yako" alisema mzee nyanda akiwasaidia wenzake kuwainua na kukusafanya baadhi ya viungo vya wale wenzake walio katwa ili watimke.
"Siunaitaka roho yangu?, haya njoo Sasa uichukue hahahahaha!!.." alisema yusrat huku akicheka, akiwa tayari ameshabadilika na wenzake wakiwa kwenye umbo la kibinadam, wote walikuwa wanaasili yakiarabu halafu wote walikuwa wanawake.
Mzee nyanda hakutaka kujibizana nae maana alikuwa amezidiwa, alitoweka na wenzake akatokezea kwake.

Yusrat na wenzake walicheka sana baada yakuushinda mpambano ule, Kisha wakatulia majonzi Sasa yakashika hatam yusrat akaanza kulia.
"Mwanangu ulihisi vizuri kama kuna watu wabaya wamekuja kwenye nyumba yako, sawa tumekusaidia kulimaliza hili tatzo sasa tuendelee na safari yetu kumbuka tunaenda kwenye msiba wa baba ako, kwhyo Kila kitu kiache huku huku usiwaze mambo ya vita vita twende ukamzike baba Ako kwanza msiba ukishaisha utarudi sasa." alisema mama yusrat aliyekuwa amekuja kumjuza mwanae kama baba yake amefariki na kusudi aende nae kwenye mazishi, na walikuwa tayari wameshaanza safari ya kwenda ila walipofika njiani ndo yusrat akahisi kuna watu wabaya kwenye nyumba yake ndomana wakawa wamerudi, yusrat alikuwa Bado analia mama ake alimbembeleza Kisha wakatoweka mahala pale wakaendelea na safari Yao.

Mzee nyanda alifikia kwenye chumba chake cha kichawi, akawalaza wale wawili waliomia vibaya pale chini palipo tandikwa na kaniki, mzee Pago na mwenzake wakakalishwa pale chini. Wale wawili waliolazwa walisikika wakiugulia maumivu Kwa mbali sana hawakuwa na mikono wala miguu pamoja na macho, Mzee nyanda akaanza kufungua makopo ya matunguri yake akachukua dawa hivi anayoikubali akachanganya na mafuta ya Simba, Kisha akaanza kuwapaka mwilini kote. Baada ya kumaliza zoezi lile akachukua mguu wa Mzee pago akasogea Hadi karibu yake akaubandika pale ulipokatwa Kisha akapaka dawa akanuia maneno frani yakichawi ukaonekana kukaza kidogo akasogea kwenye matunguri yake akachukua dawa nyingine ya unga unga akainyunyuzia pale alipounganisha ule mguu, pakaanza kuonesha dalili yakujiunga taratibu. Akahamia kwa mzee fundikila aliyekatwa mkono wa kulia na sikio akafanya kama alivyo fanya kwa mzee pango. baada yakumaliza ile kazi akatoweka kwenye chumba kile.

Upande ambao nilipokuwa mimi, nikiwa nimetekwa na dimbwi la mawazo, nilishtuliwa na baadhi ya misukule walionekana wakilia na wengine wakisimama hata wale walio kuwa wamelala waliamka. Nilishindwa kuelewa wanasimama kwa sababu ipi, nilishtuka sana baada yakuona kitu kinatokezea karibu yangu...ITAENDELEA..

Usikose sehemu ya 7RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu ya 7

TULIPOISHIA..
Nilishindwa kuelewa wanasimama kwaajili ya nini na wameona nini Hadi wanalia, nilishtuka zaidi baada yakuona kitu kinatokezea karibu yangu...

SONGA NAYO..
Aliyekuwa mbele yangu ni mzee nyanda, ile nashangaa mara nikawaona wale misukule wakiinama chini na kupiga magoti, nikiwa natazama lile tukio nikasikia naulizwa swali.
"Mbona we bado umekaa hujafata wanachofanya wenzako" alisema mzee nyanda, Nilijikuta napandwa na hasira za ghafla nikainuka nikampiga ngumi. Ila ilipita tu kama Hewa sikuwa nimepiga kitu, nilishangaa maana hakuwa amekwepa au kutoweka alikuwa Bado pale pale amesimama.

"Kijana we hauna uwezo wakugusa hata nguo yangu, uwezo ulionao wewe ni waumvuto tu yani unanyota Kali sana ndomana tunaihitaji nyota Yako Ili mambo yetu yazidi kwenda vizuri, umebakiwa na siku Moja tu ya nafsi yako kuwepo hapa siku inayofata itakukuta uko kwa wakuu wetu majini wakishetani ukiwa unatumika kutupa maisha mazuri, nasi wachawi tuwe matajiri sio kila siku tunawanga halafu hatupati chochote." alisema mzee nyanda.

Nilishangaa kusikia yale maneno, nikamuuliza.
"Sawa mi mmenichukuwa kwaajili niwape utajiri, je? Hawa ambao hawana hatia kwanini umewafanya misukule wanakusaidia Nini?"
"Hahahaha kijana, mi ni mchawi sawa lakini napenda niwe na utajiri tofauti na wachawi wenzangu wanaopenda kuroga tu."
"Kama unapenda uwe tajiri kwanini sasa usingekuwa freemason unakuja kuwa mchawi" nilimuuliza swali, akanijibu.
"Kijana kitu ambacho hujui uchawi wangu mi ni wakulidhi siwezi kuacha hadi nifariki"
"Sawa umesema unapenda utajiri, Tokea umelidhishwa huo uchawi wako hadi sasa hivi mbona huna mafanikio yoyote?" nilimuuliza swali lingine.
"Sikia kijana kuuwa watu ni mafanikio tosha kujenga nyumba kama hii pia ni mafanikio tosha, kumiriki duka kama lile? Bado tu hauoni mafanikio yangu? Ngoja nikwambie kitu kimoja kilichofanya niuwe watu wengi hivi. Wakuu zangu majini wa kishetani waliniambia Kuna mtu ananyota kali sana ukimuuwa huyo utakuwa tajiri mkubwa sana, hawakuniambia ni jinsia gani wala ni mtu gani. Mi kwakuwa nilihitaji utajiri wa haraka haraka ndo nikawa nauwa watu hovyo hovyo kila niliyekuwa na muhisia niliimuuwa, nina misukule wengi sana wengine wako kwenye vyumba vingine. Baada yakuuwa sana wakaniambia nitulie wameshaipata taswira ya huyo mtu, ndo wakanitumia taswira yako wewe na wakaniambia nisikufanye kama hawa yani usiwe msukule bali niichukue nafsi Yako halafu niitoe kafara ndo itawafikia huko walipo ili waifanye iwe inatupa mahela. Naimani tumeelewana kijana mpaka hapa utakuwa umeshaelewa sababu yakuchukuliwa hii nafsi Yako." alisema mzee nyanda.

"Kama ni hivyo naomba uwaachie misukule wote wawe wazima halafu mi niubebe msalaba wao mnichukue Mimi tu" nilisema
"Hahahaha, kijana ni kitu ambacho hakiwezekani humu kuna watu nimewauwa mda mrefu sana nikisema niwarudishe watu siwatakimbizana huko mtaani hilo wazo futa kabisa japo inawezekana maana niliwachukuwa na miili Yao yani kule kwao walikuwa wanazika migomba ya ndizi tu tofauti na wewe ambae tumekuchukuwa nafsi tu na ikipita siku Moja tu basi hauwezi tena kurudi kwenye mwili wako maana utakuwa umekufa kiukweli ukweli."

Mzee nyanda alisema maneno yale Kisha akatoweka mahala pale, wale misukule ndo na wenyewe wakakaa sasa. Nami nikakaa nikiwa na mawazo sana nilikuwa najiona tayari nishakuwa mfu sikuona sehemu ambayo naweza kuponea. Masaa yalizidi kwenda hatimae ikaingia saa Moja na nusu ya asubuhi.

Upande wa kule nilipopanga alifika mwenye nyumba, kama alivyoniambia kwenye meseji jana ake kwamba anakuja kuchukua kodi yake. aligonga hodi kwenye mlango wa chumba nilicho panga, ila mlango haukufunguliwa.
"We kijana ni mimi baba mwenye nyumba amka unipe hela ya kodi niondoke nawahi" alisema huku akigonga mlango ila yote ilikuwa ni kazi bure tu hakuona dalili ya kufunguliwa.

"Kijana unajua kabisa huwaga sikusumbuagi asubuh mapema mapema kama hivi, yote ni kwasababu nina matatzo mke wangu amezidiwa jana usku nimempeleka hospital na zinahitajika pesa za kulipia nami sina hata mia, ndomana nimekuja kwako unisaidie kahela kakodi nikawape wamuhudumie kwanza nyingine tajua nafanyaje akishaanza matibabu." Mzee wawatu alielezea matatizo yake pale, ila Bado mlango haukuwa umefunguliwa.
"Kijana haunisikii au ndo unavunga umesinzia ili usiamke kunipa kodi yangu" alisema huku akizidi kugonga mlango, ila alishangaa Sana maana mlango ulionekana umefungwa Kwa ndani akaanza kupata hofu Kwa jinsi alivyogonga mlango na kuita juu ila bado haukufunguliwa akahisi nitakuwa nimepatwa na tatizo, akaanza utaratibu wakuvunja mlango maana nyumba niya kwake kwhyo hakuona shida kuubomoa ule mlango.

alijitahidi kuusukuma Kwa nguvu na kupiga mateke ila mlango ulikuwa mgum kufunguka akiwa anaendelea kupambana kuufungua mara akatoka nje mpagaji mwenzangu yule mchawi aliyekuwa anajulikana kwa jina la choki, akasalimia.
"Baba mwenye nyumba shikamoo"
"Marhaba kijana, njoo tusaidizane tuubomowe huu mlango maana nahisi huyu kijana atakuwa anatatzo maana nimegonga sana ila naona kimya"
"Nimekusikia kipindi unagonga, mi nahisi huyo atakuwa na mwanamke tu au hana Hela ndomana hataki kuitika wala kufungua"
"Mmh!!.. Sizani ndo ashindwe hata kuitika tu, hapana huyu kijana namfaham vizuri asingeweza kunikalia kimya akiwaga hana hela huwaga ananiambiaga na namuelewa, nahisi atakuwa na tatizo we njoo tusaidizane." alisema mwenye nyumba. Choki akaingia ndani akachukua upanga akaenda nao Hadi pale mlangoni alipokuwa mwenye nyumba.
"Sogea kidogo nikuoneshe jinsi yakuufungua huu mlango" alisema choki mchawi, Kisha akaupitisha ule panga kwenye kaupenyo kamlangoni pale akawa anapekecha pekecha pakajiachia akafanya hivyo hvyo pia kwa upande wa juu, mlango ukafunguka. Wakaingia ndani, wakaukuta mwili wangu pale kitandani, mwenye nyumba akaanza kuniita huku akiutikisa mwili wangu sikuwa na uwezo wakumuitikia wala kujichezesha viungo vyangu. Alipoona ananitikisa Bado sishtuki akapata hofu zaidi akainamisha kichwa chake kwenye kifua changu upande wa kwenye moyo, akakuta mapigo ya moyo wangu hayadundi akajua Moja kwa moja nimeshakufa.

"Kijana nilikwambia huyu atakuwa na tatzo ndomana hafungui, siunaona sasa ameshafariki hatuko nae tena duniani, chukua hiyo sim yake uwapigie marafiki na ndugu zake uwape taarifa." alisema mwenye nyumba
"Mmh! hii sim yake Inapassword ningeipeleka kuirestore ila saizi bado mapema sizani kama yule fundi sim atakuwa ameshafungua labda badae badae." alisema choki, mwenye nyumba akachukua shuka nayojifunikaga akaitandika chini kwenye kapeti. Kisha Akaubeba mwili wangu akisaidizana na choki wakauweka pale chini alipotandika ile shuka, halafu wakalitoa godoro nje pamoja na kitanda wakakichomoa chomoa wakakipeleka kwenye chumba cha mwisho ambacho hakikuwa na mpangaji yoyote kwa wakati ule, vitu vyote wakaviweka kule. Walitoa vitu vyote ndani ikabaki nafasi kubwa, wakatandika ile kapeti wakaweka na zulia juu na nguo wakanilaza hapo wakanifunika na nguo.

"Sasa hapa, Subiri ufike mda ambao huyo fundi anafunguaga ukairestore hiyo sim uwape taarifa watu wake wakaribu" alisema mwenye nyumba
"sawa, ila mmh!. Nimekumbuka kuna mwanangu anaweza hizi inshu ngoja nimpelekee akaistore"
"Sawa wahi maana mi mwenyewe na matatzo nataka niende kumuona mgonjwa anaendeleaje"
"Sawa sasa hivi tu narudi" alisema choki huku akitoka ndani. akaenda hadi kwa huyo mtu bahati nzuri akamkuta nje anapiga mswaki nakunawa uso, akamuelezea kila kitu akampa na sim akaingia nayo ndani, baada ya dakika kadhaa akatoka na simu akiwa tayari ameshairestore, akamkabidhi choki.

"Shukrani mwamba"
"Kwahyo mazishi saa ngp?" alisema yule jamaa
"Hadi ndugu zake waje ndo wataamuwa wenyewe wamzikie wapi" alisema choki
"Sawa ila inatakiwa mwili wake uzikwe mapema ili yasije yakatokea yakutokea nafsi yake ikarudi kwenye mwili wake, kafara yetu ikashindwa kukamilika" alisema yule rafiki yake.........ITAENDELEA...

Usikose sehemu ya 8

RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu ya 8

TULIPOISHIA..
"Hadi ndugu zake waje ndo wataamuwa wenyewe wamzikie wapi" alisema choki
"Sawa ila inatakiwa mwili wake uzikwe mapema ili yasije yakatokea yakutokea nafsi yake ikarudi kwenye mwili wake, kafara yetu ikashindwa kukamilika".......

SONGA NAYO...
"Hapana haiwezekani anatokaje pale Kwa mzee nyanda hata kama akiweza tumeshaharibu kila kitu hawezi kurudi kwenye mwili wake."
"Mmh! sawa wapigie sasa hao ndugu zake"
"Ooh kweli umenikumbusha ngoja, niangalie namba hapaa ihiiii!!. Hii apa imeseviwa (mumy) itakuwa na ndo mama ake" akaipiga ikaita mwisho ikapokelewa.

"Hello mwanangu habari za asubuh"
"Mi sio mwanao, mwanao amefariki Jana usiku wakati amelala. Mi ni jirani yake nimepiga hii namba kukujuza mje mchukue mwili wake"
"Unasemaaa?..."
"Ndio hivyo, Hello hello hellooo!!.. Ohoo itakuwa amezimia" alisema choki huku akikata sim.
"Mmh!!.. Wamama kuzimia ni kugusa tu na hivi amepata taarifa ya kifo Cha mwanae lazima azimie, tafuta namba zingine uzipigie." alisema yule jamaa rafiki yake na choki mchawi mwenzake.
"Kuna hii namba imeseviwa (My soulmate) ngoja niipigie"
"Hapana hiyo usiipigie itakuwa ndo ya yusrat sindio mpenzi wake?"
"Eeeh ila kweli itakuwa ndo yeye"
"Tafuta tu zingine uzipigie hiyo iache"
"Sawa" alisema kisha akaanza kupiga kwa namba mbali mbali kuwajuza juu ya kifo changu, alipomaliza zoezi lile alirudi magetoni akamkuta mwenye nyumba amekaa kwenye ngazi anamsubiria yeye.

"Mbona umechelewa sana shida Nini?"
"Aaah! Yule jamaa angu niliyekwambia sijamkuta kwhyo ikanibidi niende kule kabisa kwenye senta kubwa ndo wakanitolea"
"Ooh sawa, mi naenda kumuona mgonjwa wangu tarudi badae kidogo, hivi hauna hela yoyote unisaidie?"
"Ninayo tena ngoja nikuletee Kabisa maana siku zimebaki chache, tuishane huo mwezi unaokuja usinidai" alisema choki Kisha akaingia ndani akachukua elf 45 akaja akampa mwenye nyumba.
"Sawa ngoja nikawape kwanza hii japo sijui kama watakubali, badae kidogo tarudi"
"Sawa mzee" mwenye nyumba aliondoka akabaki choki peke yake, akaufungua mlango wangu akaingia kuutazama mwili wangu huku akicheka sanaaa!!..
"Hahahaa hahahahaha bye bye Roy uwasalimie huko uendako" alisema hivyo Kisha akatoka nje, akaufunga mlango kwa nje halafu akaenda kwenye chumba chake.

Upande wa nyumbani walionekana ndugu zangu wakimpepea mama angu baada yakupokea taarifa ya msiba wangu na kuzimia.
"Hebu leta hiyo sim tuone namba ya mwisho kumpigia" alisema mjomba wangu aliyekuwa amekuja kumtembelea mama hiyo siku. Kisha akapewa sim akaona Mimi ndio nilimpigia, akaipiga ikapokelewa na choki, akamuelezea kila kitu ndo na mjomba akajua sababu iliyo mzimisha mama angu. Wakaleta marimao wakawa wanamsugua nayo kwenye magoti na kwenye unyayo taratibu taratibu akaanza kujitikisha viungo, mwisho akazinduka kilio kikaanza.

"jamaniii!!..Mwanangu Mimi jamaniii aaaaaah!!!.. Babaaaaa inamaana sitokuona Tena roy wanguuuu" mama alilia sana huku akijigalagaza chini. Majirani walizidi kuongezeka wakawa wanambembeleza anyamanze ila haikusaidia kitu mama alilia sana hadi akazimia Tena, wakafanya kama mwanzo wakampepea na kusugulia marimao akazinduka tena akaanza Moja tena kulia.

Mjomba alienda kukodi gari wakapanda na watu kadhaa ikawapeleka Hadi nilipokuwa nimepanga, wakakuta watu wengi wengine wakiwa wanalia maana yule rafiki wa choki aliwajuza watu juu ya kifo cha changu ndo wakawa wanakuja kutazama wakakuta ni kweli kadri dakika zilivyozidi kwenda ndo watu walizidi kuongezeka choki alikuwa anawafungulia mlango wanaingia kunitazama, watu ambao walikuwa wananifaham jinsi nilivyokuwa mkalim walikuwa wanalia sana.

Mjomba baada ya kufika, na baba mwenye nyumba na yeye akawa amerudi, mjomba akajitambulisha pale yeye ni nani, mwenye nyumba na wakina choki wakamuelewa. Mjomba na wale watu aliokuja nao wakaingia ndani wakanifunua ile shuka maeneo ya usoni wakakuta ni kweli ni Mimi nimefariki, Mjomba akatoka nje akaita wanaume kadhaa kwa wale waliokuwa wamekaa pale nje, wakaja wakasaidizana kuubeba mwili wangu wakaupeleka Hadi kwenye gari wakauweka vizuri watu baadhi wakaingia ndani ya gari, baba mwenye nyumba, choki na wengine wachache safari ikaanza yakuupeleka mwili wangu nyumbani kwetu.

Baada ya dakika 40 gari ilifika maeneo ya nyumbani kwakuwa palikuwa ni tambalale gari iliweza kufika Hadi kwenye mbuga ya nyumbani. Vilio vilisikika Kwa wingi baada ya ile gari kufika pale, Ndugu zangu mama angu pamoja na majirani walio nifaham walikuwa wanalia Sana baada yakupewa zile taarifa nakujazana nyumbani. Wakina mjomba wakaushusha mwili wangu wakaupeleka Hadi ndani wakaniweka kwenye chumba kilichokuwa kimesafishwa mda si mrefu na kimeandaliwa kwaajili yakuuweka mwili wangu, wakauweka kwenye mkeka uliokuwa umetandikwa pale chini. Kisha wakatoka nje wakaanza taratibu za kwenda kuchimba kaburi, watu walizidi kuwa wengi vilisikika vilio tu. Mda ulikuwa umesogea sogea ilikuwa saa 5 na dakika 14, Mda wa mazishi yangu ulikuwa umepangawa saa 10 jioni.

Jina langu halisi naitwa maulid ila jina la roy lilikuja ghafla tu, nakumbuka lilianza kipindi nasoma shule ya msingi, mwalim wetu wakiswahili alikuwa anapenda sana kuniita roy sikuwa najua sababu gani ananiita hivyo siku Moja nikamfata nikamuuliza.
"mwalim kwanini unapenda kuniita Roy?" akanijibu
"Kwasababu unafanana sana na mwanangu Roy Yani kila kitu" nikamuuliza Tena
"Sasa huyo mwanao yuko wapi?"
"Hayupo tena duniani ameshafariki ndomana nikikuona nafarijika sana nakuwa kama vile nimemuona mwanangu na ndo sababu yakuwa nakuita Roy"
"Ooh sawa nimekuelewa mwalim" kadri siku zilivyozidi kwenda ndivyo jina la roy lilizidi kujulikana sana, jina langu halisi likasaulika kabisa. Hadi nyumbani ndugu zangu pamoja na marafiki wakawa wananiita roy tu.

Mi ni muislam ndomana mazishi yangu hawakutaka kuyachelewesha, maana kwenye dini yetu haitakiwi kuchelewesha kumzika mtu akishafariki. Mda ulizidi kutaradadi Hadi ikaingia saa nane mchana, walikuwa wameshagiza sanda na ilikuwa njiani inaletwa waliniogesha tena Kisha wakanifunika na nguo zingine. Baada ya mda kidogo sanda nayo ikawa imefika wakaanza kuishona.

Upande ambao nilikuwepo kwenye chumba kile cha misukule, Nilikuwa nimekaa tu nimeshajikatia tamaa mawazo yalinizonga sana nilikuwa nimeshakubali kuwa usukani wa utajiri wao, ghafla nikaona wale misukule wanakaa makundi matatu wakakaa mikao ya kula mara zikatokezea sahani tatu za vyakula wakaanza kuufakamia ule msosi niliwaonea huruma sana.

Ghafla!!. Akatokezea mzee nyanda.
"Kijana mbona huli na wenzako hahahah" nikamjibu
"Sihisi njaa"
"Hahaha nakutania tu we ni nafsi hauwezi kula, hahahaha" alicheka sana mzee nyanda. Jinsi alivyokuwa anacheka mi ndio hasira zilikuwa zinazidi kunipanda nilitaman niamke nimkabe nimuuwe ila ndo hivyo sikuwa na uwezo wakumfanya chochote.
"Kijana unaonekana unahasira sana unataka kunimeza Nini!!.. Hahahah hahaha" akasema tena.
"Sikia kijana mda si mrefu mwili wako unazikwa saizi ni saa 8 ikifika saa 10 mwili wako tunauwaga bye bye, hahahaha!.. hahahaha!!.." alicheka sana nilishindwa kujizuwia nikamrukia ili nimnige ila nikadondoka chini sikuwa nimegusa chochote niligusa hewa tu.
"Hahahaa kijana ukiambiwa uwe unasikia Yani huna uwezo wakunigusa we ni nafsi au umesahau?.. Ambae anaweza kukugusa ni mimi tu" ilinibidi nitulie maana sikuwa na jinsi japo nilikuwa na hasira Sana.

"Kijana nikuachie ukaingie kwenye mwili wako?" nikamjibu haraka haraka
"Ndio niachie nakuomba Sana"
"Hahahaha!!.. Yani Hadi hapa hesabu tayari we ni mfu japo mda haujafika ila hata kama nikikuachia uwende hauwezi kurudi kwenye mwili wako"
nilishtuka kusikia vile nikamuuliza
"Kwanini?" akanijibu
"Ni siri yangu mwenyewe siwezi kukwambia, hahahaa!!.. hahahaha!!.." alisema mzee nyanda huku akicheka. Sikuwa na namna ilinibidi niwe mpole, ilikuwa ni saa 8 na dakika 30, Ghafla!!!.. Ukatokea mwanga mkali kwenye kile chumba wote tukashangaa...ITAENDELEA..

Usikose sehemu ya 9.RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu ya 9

TULIPOISHIA...
"Ni siri yangu mwenyewe siwezi kukwambia, hahahaa!!.. hahahaha!!.." alisema mzee nyanda huku akicheka. Sikuwa na namna ilinibidi niwe mpole, ilikuwa ni saa 8 na dakika 40, Ghafla!!!.. Ukatokea mwanga mkali kwenye kile chumba wote tukashangaa....

SONGA NAYO..
Ule mwanga ulikuwa mkali sana kiasi kwamba wote mi mzee nyanda pamoja na misukule tukajiziba nyuso zetu ili kupunguza makali ya mwanga ule, Ulichoma sana pamoja na kujiziba na mikono bado tuliipata pata wanasema nafsi haiumii ila ile siku niliumia nilihisi kama ule ndo moto sasa wajehenam.
Baada ya dakika kadhaa ule mwanga ukaanza kupungua ukali taratibu mwisho ukaisha kabisa, Ukatokea Moshi Moshi ukatanda chumba kizima Wakaanza kukohoa wale misukule, Mi na mzee nyanda hatukuwa tumeshikwa na kikohozi.

Ghafla!!.. Ule moshi ukajitengeneza ukawa taswira ya mtu ikatokea umbo la kike, alikuwa ni yusrat, tulishtuka!!.. Mi na mzee nyanda.

"Hahahaha!.. Mzee Nyandaa Nimepata taarifa ya mpango wako wa kumuangamiza roy wangu, ndomana nimetoka safari nimekuja kwaajili ya hilo." alisema yusrat, mzee nyanda akajibu huku akicheka.
"Hahahaha!!.. Hahahaha!... Mbona aliyekuletea taarifa amechelewa sana, Hahaha!.. Kama unamlipa mshahara basi mfute kazi kabisa, Hahaaaaaahaha!.." Mzee nyanda alicheka kicheko cha zarau sana hadi akakauka kwa kucheka tu, Yusrat kwakutumia ishara ya mkono akachora kaduara hivi kwenye ukuta ikaonekana njia Kisha akaniambia.

"Roy wangu pita hapo uende" kabla hajamaliza sentensi yake mi nilikuwa tayari nishapita nikatokezea nyuma ya nyumba ya mzee nyanda, Nikaangaza angaza huku na kule kisha nikatoka mbio kuelekea kwenye geto langu, njiani nikakuta na mtu kwakuwa nilikuwa lesi sana nikampitia ila nilishangaa maana nilimpita kama hewa tu hata yeye wala hata hakushtuka aliendelea na safari yake nikamwambia.
"Samahani sana bro ni bahati mbaya tu nawahi sehemu ndomana niko na haraka sana hadi nimekugonga" ila hakunijibu chochote alizidi kwenda tu, Nilishangaa sana wazo lingine likanijia labda atakuwa amevunga tu nikaendelea kukimbia hadi nikafika kwenye getto langu nililokuwa nimepanga.

Nilishangaa maana nilikuta mlango wangu umefungwa na kufuli na nilipotazama pale chini kulikuwa na alama za viatu tofauti tofauti, Nikaachana na Hilo nikazunguka nyuma ya nyumba Karibu na njia nikaona Vijana wa nne kwenye eneo liliota majani vizuri kama bustani wamekaa wanapiga story, kwakuwa nilikuwa nawafaham nikasogea hadi pale kisha nikawasimilia.
"Niaje wanangu?" ila hakuna hata aliyeitikia wala kuonesha ishara ya kushtuka kama wamesalimiwa, Nikasema Tena.
"Oya Side? We Mecky wewe? Acheni kunivungia wanangu inamaana hamnisikii?"
Bado walikuwa bize na mambo yao sikutaka kabisa kuamini kama sionekani, nikawa nawapiga magwenzi ili washtuke ila nilikuwa napiga hewa tu sikuwa nagusa kitu.

Nikatulia nisikie wanazungumzia Nini.
"Oya tunatembea tukiwa wafu wanangu jana tu nilionana nae tukasalimiana vizuri tu hakuonesha hata dalili kama anaumwa daaah!!.. Apumzike mahala pema peponi roy" mwingine akasikika akisema.
"Alikuwa ni mtu mkalim sana japo sikuwa na urafiki nae kihivyoo ila alikuwa haringi akipita akakuta Wana mmekaa kama hivi lazima apite awasalimie, Daaah nakumbuka kuna siku nilikuwa nimewamba vibaya mnoo nilikuwa na matatizo nikakutana nae njiani nikamuelezea kisha nikamuomba anisevu buku tano tu ya nauli tamrudishia, uwezi amini wanangu alinigei Msimbazi halafu akasema nisimrudishie Aisee yule mwamba alikuwa mtu poa sana" Mwingine akasikika akisema.
"Oya wanangu saizi ni saa 9 kamili, Mda wa mazishi unakaribia Oya mecky utanipakia kwenye boda yako halafu na Rich utampakia side twende kwao msibani tukamzike mwanetu"
"Haina kwele twenzetu" walimaliza maongezi yao kisha wakanyanyuka wakaenda walipozipaki boda boda zao Kisha wakapanda wakaondoka.

Nilikuwa sijui mazishi ya mwili wangu yanafanyikia wapi kwhyo niliposikia maongezi yao pale ndo nikaelewa, Nami bila kuchelewa nikaanza kukimbia kuelekea nyumbani nilikuwa najihisi mwepesi sana nilikuwa nakimbia kuzidi hata boda boda yenyewe, nilikuwa najigongesha kwenye gari ila nilikuwa napita tu kama hewa sikuwa nahisi maumivu yoyote nililiona fuso kubwa likija nikasimama katikati ya barabara ili linigonge tuone kama taumia, ila lilipita tu pale pale niliposimama sikuhisi kuguswa na ile fuso.

Upande wa kule kwenye kile chumba cha misukule kulikuwa ni vita kali baada ya mimi kupita kwenye ile njia na kuondoka.
Mzee nyanda naye akataka kupita ile njia ili aje anikamate anirudishe kwenye chumba. Yusrat akaifunga ile njia ghafla Mzee nyanda akajigonga kwenye ukuta, akataka kutoweka kimiujiza ila akatulizwa, na nguvu za kutoweka zikaondoka. Ukaanza mpambano mzee nyanda akatengeneza njia nyingine ili apite atoke ndani ya chumba kile ila ile njia ikazibwa na yusrat, mzee nyanda akakusanya nguvu za kichawi akamrushia yusrat, Yusrat akazikwepa zikaenda kumpata msukule mmoja akapasuka kichwa nyama nyama zikatapakaa mule ndani, macho, nywele, meno na masikio vilionekana vikiwa vimedondoka chini huku dam zikitiririka kama bomba la mvua.

Yusrat alikuwa na hasira sana ukichanganya na majonzi ya msiba wa baba ake ndo alikuwa zaidi ya mbogo na hasira zikimpandaga ndo nguvu zake zinaongezeka zaidi, Alimtupia kombora moja mzee nyanda likaenda likampata, akayumba yumba kama vile amekunywa pombe kali akadondoka chini kama limzigo akazimia.

Baada ya mimi kuona nagongwa na gari lakini siumii nilianza kuamini kweli itakuwa sionekani na watu japo ilikuwa ngum kunikaa kichwani, Nilikimbia sana wale jamaa waliokuwa wanakuja kwenye msiba wangu na boda boda niliwaacha mbali sana, baada ya mda kidogo nikafika nyumbani kwetu, watu walikuwa wengi sana wengine walikuwa wanalia tu. Nilishtuka!.. baada yakumuona na Lucy yuko pale msibani analia hadi macho yake yalionekana kuvimba maana alionekana kama Amelia kwa mda mrefu, mawazo yangu yote yalikuwa ni kwenda kuingia kwenye mwili wangu.

Nikampita lucy nikaingia ndani nikawa naingia kwenye vyumba mbali mbali kuangalia mwili wangu umewekwa wapi, nikauona wakina mjomba ndo walikuwa wanajiandaa kuuvika sanda maana ilichelewa kuletwa kwhyo ndo walikuwa wanamalizia kuishona. Nikaenda Hadi pale ulipolazwa mwili nikafunua nguo waliokuwa wamenifunikia nikajaribu kuingia kwenye kwenye mwili wangu, Ila ilikataa nikajaribu Tena kujing'ang'aniza kuingia ila ikashindikana kabisa. Nilihisi kama kuchang'anyikiwa hivi nilibaha nikayatoa mashuka yote, mwili wangu ukabaki kama ulivyozaliwa nikaulalia kwa juu vile vile mwili ulivyokuwa umelala, ila bado haikuwezakana nilijikuta machozi yamenitoka bila kutaka nililia sana nikapiga na kelele huku nikiuwangalia mwili wangu, niliona kabisa naenda kuwa mfu rasmi. Mda ulikuwa umeenda sana ilikuwa ni saa 9 na dakika 48, Baada ya kumaliza kuitengeneza vizuri sanda waliushika mwili wangu kwaajili sasa yakuuvalisha sanda.

Upande wa yusrat baada yakumtupia kombora ambalo lilimzidia nguvu mzee nyanda hadi akazimia, Yusrat alitoweka mahala pale kwakupotea.

Upande wa kule nilipokuwa.
"Jamaniiii!!..mi sijafa mnataka kunivalisha sanda ya nini sasa naomba muuwache mwili wangu tafadhali sana, mjomba inamaana na wewe hunisikii hebu uachie huo mwili wangu." Niliongea huku machozi yakinitoka nilikuwa nawapiga piga migongoni ili wasiuvalishe sanda mwili wangu wakati bado nipo hai, nilipiga hadi magoti nikiwaomba wasitishe kile ambacho walichokuwa wanakifanya huku nikiongea kwa sauti kubwa ili wanisikie ila nilikuwa najisumbua tu waliendea na shughuri Yao, nilikuwa nalia huku nikitazama jinsi sanda ilivyokuwa inaingia kwenye mwili wangu.

Walimaliza kuuvisha sanda mwili wangu, mi nilizidi kupambana ili niingie kwenye mwili ila ilishindikana, Mara nikasikia sauti inaongea...ITAENDELEA...

Usikose sehemu ya 10RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu ya 10

TULIPOISHIA..
Walimaliza kuuvisha sanda mwili wangu, mi nilizidi kupambana ili niingie kwenye mwili ila ilishindikana, Mara nikasikia sauti inaongea...

SONGA NAYO..
"Mashekh wameshafika kaleteni ile Tusi pale nje tuuweke huu mwili ili tuupeleke msikitini ukaswaliwe." alikuwa ni mjomba ndo alisema vile, nilizidi kubaha huku nikimshika mshika mjomba atengue kauli yake.
Baada ya mda tusi likaletwa mule ndani mwili wangu ukiwa na sanda ukafunikwa na mkeka kisha ukawekwa kwenye lile tusi, wakina mjomba wakaibeba ile tusi wakaitoa nje mi nikaipandia kwa juu huku nikiwa staki mwili wangu upelekwe nje. Baada yakuutoa nje wakaja wanaume wengine wakaanza kupokezana kubeba, Watu walikuwa wengi sana na wengi walikuwa wanalia, msiba wangu uliwagusa watu wengi Sana.

Nikasimama huku Nikiangaza angaza kumtafuta mama yangu ila sikumuona nikahisi yeye atakuwa ndani. Nikamuona Lucy pale nje akilia na kujigalagaza chini baada ya mwili wangu kutolewa nje, Nilimuonea huruma sana nikajaribu kupaza sauti.
"Jamaniii mnalia nini mi sijafa hamnioni hapa?.. Hebu waambieni hao waushushe mwili wangu wanaupeleka wapi?.." nilijiona kama naelekea kuchanganyikiwa maana hakuna hata mtu ambae alishtuka Bado waliendelea kulia.

Nikatoka pale mbio kwenda sehem mwili wangu ulipo pelekwa, nikawakuta njiani watu wengi wakizidi kwenda.
"Jamanii nyie hebu urudisheni mwili wangu nyumbani mnaupeleka wapi huko wakati mi bado ni mzima?.." Bado waliendelea kusonga mbele hadi wakafika msikitini, baadhi ya watu ambao ni waislam wakaingia ndani ya msikiti na mwili wangu ukiwa ndani ya tusi wakauweka pale mbele Kisha wakatawadha walipo maliza, shekh akaongoza swala ya maiti yangu.
"Nyie mnaniswalia nini wakati mi bado mzimaa acheni masihara na mwili wangu hebu uleteni huku nje mi niingie zangu kwenye mwili wangu." nilisema Kwa sauti kubwa nikiwa pale nje ya msikiti, huku nikilia.

Baada ya kumaliza kuuswalia mwili wangu walitoka nao nje Kisha wakaanza kuelekea sehem yalipo makaburi, nilizidi kupiga kelele huku nikidandia juu ya tusi ili walishushe chini. Ila hawakulishusha walizidi kwenda Hadi wakafika kwenye makaburi. Wakaenda hadi pale walipochimba kaburi lakuuzika mwili wangu, Wakaniweka pembeni kidogo Kisha wakaanza utaratibu wakunizika wakadumbukia watu kadhaa nami Nikadumbukia ndani ya kaburi ili niurudishe juu mwili wangu ila haikuwezekana waliushusha ndani ya kaburi, nikatoka ndani ya kaburi huku nikilia. Ghafla... Nikaona mwanga unatokezea nilishtuka!!.. karibu yangu akatokea yusrat Kisha akasema.
"Roy mwili wako nishauchukuwa mda Sasa kipindi uko kule chumbani kabla hata hawajauvalisha sanda, huo ni mgomba wa ndizi sio mwili wako hebu chungulia ndani ya kaburi uone" nikachungulia ili nione.

kweli bhan niliona mgomba wa ndizi nikamuuliza.
"Sasa mbona tokea kule nilikuwa nauona ni mwili wangu?"
"Kwa jinsi nilivyo uchukua mwili wako isingekuwa rahisi kuona kama kilicho bakia pale ni mgomba wa ndizi, sasa hivi ndo nimeufichua ndomana ukauona." nikamuuliza
"Tunafanyaje Sasa?" akajibu
"Ngoja tuupoteze na huo mgomba wa ndizi" alisema yusrat Kisha akaanza kufanya mambo yake. Wale watu walio ingia ndani kaburi walikuwa wanauweka mgomba wa ndizi kwenye mwandani ambapo kwa macho yao waliniona ni mimi, ghafla!!... Wakiwa wameushika mwili ukapotea wakashtuka!.. huku wakipiga kelele hata waliokuwa wameshika nguo kwa juu Ili mwili usionekane na wenyewe walishtuka kusikia zile kelele wakafunua ile nguo wakashangaa hawaoni maiti. Wale waliokuwa ndani ya kaburi wakapanda haraka haraka juu wakaanza kukimbia mbio huku wakipiga kelele hata wale waliokuwa wameshika nguo wakakimbia huku wakisema.
"Maiti imepoteaaaa, maiti imepoteaaaa." watu baadhi ambao walikuwa wamesimama pembeni kidogo walipo sikia yale maneno na wenyewe wakaanza kukimbia, Palikuwa ni mkanyagano pale makaburini kila mtu alipita njia yake wote walikimbia.

Nikamuuliza yusrat.
"Mbona umefanya hivyo?" akanijibu.
"Ni afadhali kidogo kuliko kujua wamekuzika halafu ukutane nao live ndo ingekuwa tatzo kubwa zaidi, hebu twende Kwanza ukaingie kwenye mwili wako" Alisema yusrat kisha akanishika mkono tukatoweka mahala pale, tukatokezea ndani kwenye geto langu, nilikuta Kitanda kimepangwa vile vile kilivyokuwa usiku wa jana ake na mwili wangu ukiwa juu ya kitanda ulikuwa umefunikwa na mashuka kama jinsi nilivyokuwa nimelala usiku. Akasema yusrat.
"Panda kwenye kitanda uingie kwenye mwili wako" Nikafata maelekezo yake nikapanda Kisha nikalala vile vile mwili ulivyokuwa, yusrat akaushika mwili wangu huku akisema maneno kwa sauti ya chini. Baada ya mda nafsi ikaingia kwenye mwili, nikashtuka nikajiinua nikiwa na mwili wangu. Nikashuka Hadi chini nikiwa uchi wa mnyama nikasimama nikaangalia pale kitandani kama tauona mwili, lakini sikuuona nikapiga kelele ya furaha huku nikimkumbatia yusrat na kumbusu busu sikuwa na muogopa pamoja na kutoweka kwake kimiujiza niliona ni kawaida tu, nikiwa nimemkumbatia nikamwambia.

"Naomba nikuulize maswali mawili, swali la kwanza mbona mwanzo nilikuwa naingia kwenye mwili wangu halafu nashindwa kuingia shida ilikuwa ni nini?.. Na swali la pili, mbona ulikuwa umechelewa? Kuja kuniambia kama ushauchukua mwili wangu hadi mi nikahangaika mda wote ule?.."

"Nakujibu maswali Yako Kwa jibu Moja, Kilichofanya ni chelewe, nilikuwa nakipanga kitanda vizuri maana walikibomoa bomoa nikapanga na kila kitu kilivyokuwa mwanzo maana bila hivyo usingeweza kuingia kwenye mwili wako ilitakiwa nafsi yako ilipotokea ndo irudie hapo hapo mwili ukiamishwa hauwezi kuingia ndani ya mwili"
"Oooh sawa nashukuru sana kwa majibu yako mazuri" nilisema huku nikimpiga busu la mdomo, sikujali kabisa maajabu yake japo nilikuwa na maswali mengi yakumuuliza. Tukapeana denda baada ya kushikana shikana hisia zikatupanda tukajitupa kwenye kitanda tukacheza mchezo pendwa kwa wakubwa. Baada yakumaliza kupeana malavidavi na kulizishana, tukalala wote usingizi mzito.

Upande wa kule nyumbani msibani wanawake walikuwa wanalia wengine walikuwa wamekaa tu wanapiga story mbili tatu, watu walizidi kuongezeka kila mda ulivyozidi kwenda. Ghafla!.. Wakina mjomba walirudi wakiwa nduki huku wakihema wengine wakipiga kelele.
" Maaajabu!!..Maiti ya roy imepoteaa, maiti imepoteaa!!.."
"Heeeeeeh!!!.. Maiti imepotea?" Walisikika wamama wakishangaa. Ingekuwa ni mmoja anasema vile wangejua ni chizi ila wanaume wote waliorudi kutoka makaburini walisema hivyo hivyo Hadi na mjomba, watu walianza kukimbia baada yakuona wanaume wote waliorudi pale walikuwa wanakimbia nakusema vile wengine hawakukaa kabisa pale walipitiliza wengine waliunganisha kule kule kwenda makwao. Pale msibani wote wakaondoka baada yakupewa story kamili ilivyokuwa, wakabakia ndugu tu.

Nilikuja kushtuka kutoka usingizini mida ya saa moja usiku ndo nikakumbuka toka nimeingia kwenye mwili wangu sikuwa nimeoga nikachukua gauni la yusrat nikajifunga kiunoni kisha nikashuka chini nikamuacha yusrat amelala, nikaona maji kwenye kandoo kadogo pale pembeni nilishangaa maana nakumbuka kipindi tunatokezea mule ndani hakukuwa na chochote tofauti na kitanda godoro na zile shuka yani yakutandikia naya kujifunika. Nikapotezea nikayachukua yale maji kisha nikaenda hadi mlangoni nikaanza kuufungua ila uligoma kufunguka ndo nikakumbuka unefungwa kwa nje, nikarudi hadi kitandani nikamuamsha yusrat kwa kwakumgusa gusa akaamka akiwa na marue rue, nikamwambia.
"Mlango umefungwa Kwa nje tunafanyaje nami nataka kuoga" hakusema kitu aliinuka akaenda kwenye mlango akaigusa gusa ile komeo ya ndani mlango ukafunguka, "Duuuh!!.." Nilishangaa, hakusema kitu akarudi kulala akiwa uchi vile vile tulivyo lala.

Nilikuwa namtazama huku nameza mate binti alikuwa amenona sana kila kiungo chake kilivutia sana, nikatikisa kichwa Kisha nikatoka nje kwakuchungulia nisionekane nikaenda hadi bafuni kuoga. Nilipomaliza nikatoka ile nimefika katikati ya mbuga uso kwa uso nikakutana na....ITAENDELEA..

USIKOSE SEHEMU YA 11.
 
Hii story ndiyo iliishia hapa au mlihamia Whatsapp.
 
Agizo la majini 11-15
RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu ya 11

TULIPOISHIA..
Nilikuwa namtazama huku nameza mate binti alikuwa amenona sana kila kiungo chake kilivutia sana, nikatikisa kichwa Kisha nikatoka nje kwakuchungulia nisionekane nikaenda hadi bafuni kuoga. Nilipomaliza nikatoka ile nimefika katikati ya mbuga uso kwa uso nikakutana na...

SONGA NAYO..
Nikakuta na choki aliponiona alishtuka!.. Akageuka nyuma akakimbia huku akisema.
"Mzimuuu mzimuuu" ilinibidi nicheke😂maana sio kwa mbio zile nikarudi ndani nikafunga mlango Kisha nikapanda hadi kitandani ila nilipomuona yusrat alivyolala tena akiwa uchi uvumilivu ulinishinda tukaanza Moja tena kucheza ule mchezo wa mwanzo, tulipo maliza tukalala Tena.

Tulishtuliwa na sauti zikibisha hodi mfurulizo ilikuwa ni usiku Sasa.
"Fungua mlango we mzimuu" sauti zilisikika Kwa nje zikisema.
"Sweetie siunaweza kuleta nguo kimiujiza fanya hivyo tuvae tukawasikilize" nilisema haikupita hata dakika zilitokezea nguo ye akachukua za kike akavaa mi nikachukua za kiume nikavaa Kisha mi nikasogea Hadi mlangoni nikaufungua.
"Heeeh!.. Kweli ni mzimuuuuu jamani ni mzimuuu" alisema baba mwenye nyumba baada ya kuniona ni Mimi, huku akikimbia na watu aliokuwa amekuja nao wakina choki na vijana wengine. Wote walikimbia na mapanga yao pamoja na miti waliyokuwa wameishika.

"Heeeeh!!.." nilishangaa huku nikicheka.
"We unacheka? ila ndo tayari washakuchukulia we ni mzimu na ni ngum kuwaaminisha hao watu, wakati walishuhudia kabisa umekufa halafu maiti Yako imetoweka kaburini"
"Mmh!!.. Kwahyo tunafanyaje baby?"
" Kesho asubuh twende kwanza kwa ndugu zako hasa hasa mama ako ukamuelezee vizuri"
"Sawa" niliitikia kisha tukalala, asubuh ilipofika akanishika mkono tukatoweka kwenye chumba kile tukatokezea karibu na nyumbani kwetu kwa nyuma ya nyumba.

"Nenda Sasa mi nakusubiri hapa"
"Hapana situngeenda wote tu ili nimuelezee kwamba we ndo umenisaidia"
"Mmh!!.. Sawa twende" alikubali yusrat kisha tukaenda, nikajibanza kwenye ukuta nikachungulia kama pale nje kuna watu nikawaona baadhi ya watu. Tukajitokeza sasa hawakuwa wametuona tukasogea hadi karibu yao tukawasalimia.
"Habari za asubuh?" walishtuka!!..
"Heeeeh!!.. Mzimuuuuu!!!... Jamani mzimuuuu" walipiga kelele huku wengine wakikimbia wengine wengi wakiingia ndani na kufunga mlango, Nikasogea hadi mlangoni nikagonga.
"Jamani mi sio mzimu fungueni mlango niwaelezee"
"Hapana we ni mzimu ondoka rudi kuzimu siku zako zakuishi duniani zimeshaisha."
ilikuwa ni ngum kunielewa wengine walikuwa wanatuchungulia dirishani ili wahakikishe kweli ni Mimi.
"Rudi kuzimu na huyo mtu wako uliyetoka nae kuzimu." nilisikia sauti ya shangazi mke wa mjomba ikiongea vile. Sikujua mjomba yuko wapi mda huo labda yeye angenisikiliza akanielewa kwakuwa ni mwanaume mwenzangu. Tukiwa pale nje tumesimama mara wakapita watu njiani maana nyumbani kwetu ni karibu na njia, Tuliona wamesimama wakiangalia upande tulipokuwa tumesimama mi na yusrat Kisha wakakimbia huku wakisema "Maiti imefufukaa jamaniiiiiii maajabuuu!!!..."
"Duuuh!!.." Niliguna huku nikitikisa kichwa.

Mara nikamuona mama anachungulia dirishani.
"Mama ni mimi mwanao usinichungulie kwa mbali hivyo njoo uhakikishe." nilisema huku nikilia, dam ni nzito kuliko maji mama alishindwa kuvumilia akatoka kule chumbani ili aje sebureni kunifungulia mlango.
"We wifi unaenda wapi wakati unaona kabisa huo ni mzimu" alisema shangazi
"Hapana sio mzimu fungueni nikamuone mwanangu" alisema mama
"Mwanao siulishuhudia kabisa amefariki tena wakampeleka kumzika akapotea? Ushawahi kuona wapi mtu wa kawaida anapotea kimiujiza?" alizidi kukazia shangazi na wengine wakiwa wamesimama mlangoni ili mlango usifunguliwe.

kipindi nageuza shingo kwenye njia nikamuona mjomba yuko na wanaume wawili wakija nyumbani, akiwa anakaribia nyumbani nikamkimbilia huku nikisema.
"Mjomba naomba unisikilize mi sio mzimu simama nikuelezee"
"Heeeeeh!!!.." Mjomba alishtuka!.. Aliponiangalia vizuri akakuta ni mimi, akageuza alipotokea na wale watu aliokuja nao wakakimbia mbio za kufa mtu.
"Hehehee!.. Kumbe mjomba wako ni mkimbiaji mzuri tu siaende sasa akashiriki kwenye mashindano ya mbio za marathon, hahahaaaaa😅😅" alisema yusrat huku akicheka, nami nikajikuta nacheka😂😂. Maana mjomba alikimbia akawaacha mbali wale watu aliokuja nao, miguuni kama vile alikuwa amefunga mota.

Mama sijui alifanyaje akawaponyoka wale waliokuwa wamemshika akaufungua mlango haraka haraka akatoka nje akafika ananikumbatia huku akisema.
"Mwanangu jamani ni wewe kweli babaa!!.."
"Ndio mama ni Mimi kabisa, siunaona umeweza kunishika mzimu unashikika?" Hadi wale waliokuwa ndani walishangaa baada yakuona mama amenikumbatia bila kutokea chochote, wakaanza kuamini amini kidogo japo ilikuwa ni ngum maana walishuhudia maiti yangu kabisa nikiwa nimekufa.
"Twende tukakae pale mwanangu ukanielezee vizuri kilitokea Nini"
"Sawa mama" tukasogea hadi kwenye benchi zilizokuwa pale tukakaa, mama hakuonesha kuniogopa kabisa chako ni chako tu.

Nikaanza kumuelezea Sasa, baadhi ya watu walikuwa wanasikia maana tulikuwa tumekaa karibu na dirishani na wengine walitoka nje kabisa wakisogea taratibu ili wasikie nachoongea na mama.
Nikamuhadithia mama jinsi mzee nyanda alivyoniambia et nina bahati, Hadi ile siku nafsi yangu inachukuliwa ili aitoe sadaka na jinsi mwili wangu ulivyobaki ndani na baba mwenye nyumba alivyonikuta ndani akajua nimekufa hadi walipo uchukua mwili wangu na Hadi nilivyosaidiwa na yusrat kurudi kwenye mwili wangu na nilivyopotea kule kaburini vyote nilimuelezea.

"Ooh pole sana mwanangu" alisema mama huku akinikumbatia
"Asante mama yote kwa yote nikumshukuru mungu aliyemleta yusrat anisaidie Mimi bila hivyo ningekuwa mfu wa kweli"
"Ubarikiwe sana binti" alisema mama huku akimpa mkono yusrat.
"Asante mama usijali ni jukumu langu kumlinda mwanao maana ndio chaguo la moyo wangu na kwakuwa nimejaliwa na mungu nguvu kidogo tamlinda siku zote za maisha yangu." alisema yusrat,
"Heeeh!!.. Tulipogeuza vichwa tulishangaa watu walikuwa wamejaa pale nje, wote waliokuwa ndani walitoka wakaanza kusikiliza nilivyokuwa na hadithia wote hawakuniogopa sasa waliyaelewa vizuri maelezo yangu.

"Pole sana kaka kwa yaliyokukuta" alisema mdogo wangu wa kiume huku akija kunikumbatia, na shangazi pia akanipa pole watu wote pale walinipa pole, tulishinda pale tukipiga story mbili tatu huku tukicheka na kufurahi, wapita njia walishangaa sana kuona wale ndugu zangu na watu wengine wamekaa na mimi mtu ambae nishakufa wakaanza kukimbia huku wakitunga maneno Yao.
"Wale walikuwa wanatuigizia tu et kijana wao amekufa ili wapate hela za lambi lambi wameona maisha magumu wanatafuta pesa kwa njia nyingine." alisema mbaba moja akiwa na jamaa zake wawili ni baada ya kupita pale njiani nakuniona pale nikiwa na ndugu zangu tukipiga story na kucheka.
"hapana wale itakuwa ni familia ya kichawi tu, siunakumbuka Roy alivyotoweka kimiujiza kule kaburini? Itakuwa labda walitaka kumtoa kafara halafu wakahairisha utajionea mwenyewe kuna mtu anaweza akafa siku si nyingi ndo atakuwa mbadala wa Roy." walizidi kutunga maneno yao wale jamaa hadi wakafika kwenye kijiwe wakawaelezea na wale walio wakuta pale na wenyewe wakaja kutuchungulia ili wahakikishe kama ni kweli baada yakuona ni kweli sasa waliyaamini maneno ya wale jamaa wakajazana uongo mtaa mzima ukaelewa hivyo kwamba sisi ni familia ya kichawi haiwezakani mtu afariki harafu afufuke.

Sisi hatukuwa tumeelewa lolote tulizidi kupiga story kisha chai ikapikwa tukanywa wote kwa pamoja, kulikuwa na ndugu wengi wengine walitoka sehemu mbali mbali kuja kwenye msiba wengine hata sikuwa nawafaham, mama akaanza kunitambulisha baadhi ambao sikuwa nawajua, wakati tukiwa tunatambulishana mara tukasikia sauti ya mdogo wangu wa kike akisema.
"Muoneni mjomba kule anachungulia" tukageuza shingo wote kuelekea kule alipoelekezea mkono mdogo wangu.
"We baba issa unachungulia nini sasa siuje?"Alisema shangazi akimwambia mjomba, Mjomba akasikika akisema.
"Nyie ondokeni hapo mnakaaje hapo na mzimu mnataka awanyonye dam et eeh?.......ITAENDELEA..

Usikose sehemu ya 12.

RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu ya 12

TULIPOISHIA..
Muoneni mjomba kule anachungulia" tukageuza shingo wote kuelekea kule alipoelekezea mkono mdogo wangu.
"We baba issa unachungulia nini sasa siuje?"Alisema shangazi akimwambia mjomba, Mjomba akasikika akisema.
"Nyie ondokeni hapo mnakaaje na mzimu mnataka awanyonye dam et eeh?......"

SONGA NAYO..
"Ushawahi kuona wapi mzimu unashikika?.. Sihuyu hapa namshika kabisa, Hebu njoo tukuelezee" alisema shangazi huku mkono wake ukiwa kwenye bega langu.
"Mmh!!.. Ila inaweza ikawa kweli mbona wamekaa nae karibu na hajawafanya chochote, Twendeni." alisema mjomba akiwaambia wale wageni aliokuja nao.
"Hapana sisi ngoja tunarudi tulipotoka tutarudi hata badae we nenda" walisema wale jamaa kisha wakaigeuza miili yako wakaondoka zao.

Mjomba akaanza kuja kiuoga oga hadi akafika pale tulipokuwa akakaa pembeni kidogo, Shangazi akamfata akaanza kumuelezea ilivyokuwa hadi mjomba akamuelewa.
"Pole sana anko" alisema mjomba huku akinyanyuka kuja kunipa mkono.
""Asante mjomba ndo hivyo kama ulivyo ambiwa"
"Daah kuna baadhi ya binadam ni watu wabaya sana kisa utajiri ndo wanataka kukuuwa?.." alisema mjomba, nikamjibu
"Mjomba kama mtu anaweza kumtoa kafara mama ake mzazi kwaajili yakupata mali nyingi sembuse mimi Ambae sina hata undugu nao?.."
"Ila kweli ni jambo la kushukuru mungu mpaka Sasa uko hai." alisema mjomba kisha akanyanyuka akaingia ndani kwenda kunywa chai.

Mi nikabaki napiga story na bibi ambae sikuwa namkumbuka.
"We mtoto mkaidi sana tokea ukiwa mdogo Hadi umekuwa mbaba hujawahi kuja kabisa kuniona hadi umenisahau mi mdogo wa bibi yako au kisa mkubwa ameshafariki ndo hauji kutuona tuliobakia"
"Hapana bibi shule tu ndo ilikuwa imenibana, mbona wewe hukuja kuniona mme wako"
"muulize mama ako mi nakujaga sana tu, kipindi cha nyuma niliambiwa uko masomoni na kipindi cha hivi karibuni niliambiwa vya shule vilikushinda ukaamua kwenda kupanga utafute maisha vipi ameshayapata yalipodondokea hayo maisha?.."
"Hahahaha bibi bado sijayapata yamedondokea kwenye mchanga mwingi ndo bado nayatafuta njoo basi tusaidizane kuyatafuta?"
"Akaaaa!.. Ushampata bi mdogo mwambie akusaidie kuyatafuta mi siumenitelekeza"
"Aaah jamani siunajua Sheria yetu ya kiislam bado wengine wawili muwe wanne, mbona utakonda kama ndo hivyo kidogo tu unazila"
"Nikiona wivu umenizidia sana naomba taraka nisije nikajifia mie."
"Hahahaa.. Sijuagi kutoa taraka najua kuoa tu kwhyo utapambana na hali yako, hahaha" Tulipiga story na bibi pale na ndugu wengine wengine, hadi ikafika mida ya 12 jioni tukawaaga wote kisha tukaondoka.

Upande wa kule kwenye chumba cha misukule kwa mzee nyanda. Ilionekana misukule ikihangaika na njaa huku ikimuamsha mzee nyanda aliyekuwa amezimia baada ya kile kipigo kutoka kwa yusrat jana Ake. Mzee nyanda Familia yake haikuwa hai familia yake yote aliiyagamiza ye mwenyewe, sababu yakuiyagamiza familia yake ni kwakuwa kila aliyemwambia ajiunge nae awe mchawi alikataa ndo wakuu zake wa kichawi wakamuambia awatoe kafara, alianza na mke wake akamtoa, wakafata watoto wake wote wawili akawatoa. Kwhyo pale kwenye ile nyumba aliyekuwa hai ni yeye mwenyewe tu, wote walio kuwemo mule ndani ni misukule.

Mke wake msukule akasogea hadi pale alipolala mzee nyanda Kisha akaanza kumpulizia pumzi huku udelele ukiwa unamshuka tu mwingine unaingia mdomoni kwa mzee nyanda, baada ya sekunde kadhaa mzee nyanda akazinduka. Alishtuka baada yakuona mdomo wa mke wake ukiwa mdomoni mwake akamsukuma akaanguka chini, watoto zake misukule wakamuinua mama Yao. Mzee nyanda akainuka huku akijinyosha nyosha viungo maana alihisi mwili unauma sana, alipokaa sawa akatoweka kwenye chumba kile.

Mi na yusrat baada yakutoka pale nyumbani tulitoweka kisha tukatokezea kwenye geto langu yusrat akasema.
"Twende ukamuelezee na baba mwenye nyumba maana bado anahisi we ni mzimu." Bila kupoteza mda tukazipiga hatua za haraka haraka kuelekea kwa baba mwenye nyumba maana haikuwa mbali sana. Tukiwa tunazidi kuzipiga hatua njiani tukakutana na mecky yule jirani yangu kwenye duka langu la nguo.
Alishtuka!!.. Baada yakuniona Kwa mbele nikiwa na yusrat, macho yakamtoka akaanza kurudi nyuma taratibu.

"Oya mecky usiniogope mi ni mtu wa kawaida tu kama wewe wala sio mzimu naomba usimame nikuelezee" Maneno yangu yalifika kwenye sikio lake la kulia Kisha yakatokea kwenye sikio la kushoto hakuelewa chochote, alipoona nazidi kusogea akageuka nyuma Kisha akatoka nduki huku akipiga keleleee "Yalaaaaaah!!.. Nakufaaa mzimu jamani mzimuuuuuuuu!!..." watu waliosikia zile kelele wakaanza kuja kuangalia kuna nini, walikimbia na wao baada yakuniona, kila Kona ikawa ni mzimu mzimu. Nikamgeukia yusrat nikamwambia
"Ona wale watu wanavyonichungulia mtaa mzima unajua mi ni mzimu, Kwanini umetaka tutembee wakati unauwezo wakutoweka."
"Kwa sababu mzee nyanda ameshazinduka tungetoweka tungepitia njia yake kwhyo angetuona"
"Kwani unamuogopa? Fanya tu tupotee siwezi kufika kwa hali hii kila kona wananitazama Mimi"
"Huoni kama ndo wataamini kuwa we ni mzimu wakiona unatoweka kimiujiza maana wako wanatutazama ona kule lile kundi la watu limejibanza linatuangalia, We tutembee tu" alisema yusrat nikaona kweli ameongea point maana kila kona watu walikuwa wanatuangalia kitendo cha kupotea ndo wangejihakikishia kweli mi ni mzimu.

Tukazipiga hatua za haraka haraka kila tulipopita watu walikimbia hadi tukafika kwa baba mwenye nyumba. Tukamkuta nje alipotuona akakimbilia ndani punde si punde akatoka ameshika panga.
"Ishieni hapo hapo mi siogopagi mizimu mkizidi kusogea nawakata kata." alisema baba mwenye nyumba.
"Naomba unisikilize mi sio mzimu kama unavyofikiria naomba unipe dakika chache tu nikuelezee" nilisema
"Hamsikii!!.. Nimesema msisogee ishieni hapo hapo kisha mrudi mlipotokea, Kama mnahitaji dam kawanyonyeni maboya sio Mimi." alisema baba mwenye nyumba akiwa amefura kama mbogo hakutaka kuelewa nilichokuwa namuomba.
"Roy subiri nimfanyie kitu" alisema yusrat
"Kitu gani hicho?" niliuliza
"We tulia uone" alisema yusrat Kisha akafanya mambo yake pale, baba mwenye nyumba akaganda kama sanamu.
"Sasa umemgandisha taongea nae vipi?" niliuliza.
"We sogea Hadi karibu yake halafu umuelezee kila kitu anasikia vizuri tu sema hawezi kujibu wala kujitikisa" Aliponiambia hivyo nikasogea hadi karibu yake nikaanza kumuelezea baba mwenye nyumba yote yaliyo nisibu sikubakiza hata moja nikamtaja hadi na choki kama na yeye ni mchawi alikuwa ni mmoja ya wale watu wachawi. Nilipo maliza kumuelezea nikarudi nyuma hadi alipokuwa yusrat.
"Tayari nishamuelezea mganduruwe Sasa" Yusrat akamganduruwa.

"Pole sana kijana kwa yote yaliyo kukuta" alisema baba mwenye nyumba baada yakuganduruka huku akitupa panga chini kisha akasogea hadi karibu yangu ila alimuogopa kidogo yusrat kwa kitendo kile alichomfanyia binadam wa kawaida asingeweza.
"Nisamee sana sikujua maana nilishuhudia kabisa ukiwa umekufa kwhyo ilikuwa ni ngum sana kuamini kwamba we sio mzimu."
"Mzee wangu Hauna haja yakuomba msamaha maana hukuwa unaelewa chochote wanasema usilo lijua nisawa na usiku wa Giza kwhyo we ulikuwa kwenye Giza usingeona bila kuwa na mwanga."
"Mi nimekuelewa vizuri kijana, na choki anatakiwa ahame kwenye nyumba yangu kumbe ni mchawi na alikuwa anayajua yote haya."
"Hapana mzee muache usimfukuze"
"Lazima atoke kwenye nyumba yangu siwezi kumpangisha mchawi nikiwa najua kabisa."
"Basi hata kama ukimfukuza usimwambie sababu yakumfukuza maana anaweza kukufanyia kitu kibaya." nilisema mara yusrat akadakia
"Mzee Wala hata usihangaike kumfukuza ataondoka mwenyewe maana hatoweza kukaa karibu na roy maana anajua ashajua kama yeye ni mchawi na kingine ukimfukuza lazima atakuzuru tu hata kama usipo mwambia sababu yakumfukuza maana anaroho mbaya sana sema bado hujamjua vizuri."
"Sawa nimewaelewa tafanya kama mlivyosema."
"Na tena usimuoneshe dalili zozote kama umejua" alisema yusrat.
"Sawa" aliitikia baba mwenye nyumba kuashiria ameelewa, tukamuaga Kisha tukaondoka Mahala pale.

Giza lilikuwa tayari lishatanda, tukaanza kuzipiga hatua za kurudi magetoni njiani tukakuta na watu bahati nzuri hawakuwa wananifahamu kwhyo walitupita tu, Tukazidi kusonga mbele tukafika sehem yenye kichaka kidogo Ghaflaa!!..Ukatokea mwanga wa kiasi chake ule mwanga ukajitengeneza akatokezea mtu.......ITAENDELEA..

Usikose sehemu ya 13.

RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu ya 13

TULIPOISHIA..
Giza lilikuwa tayari lishatanda, tukaanza kuzipiga hatua za kurudi magetoni njiani tukakutana na watu bahati nzuri hawakuwa wananifahamu kwhyo walitupita tu, Tukazidi kusonga mbele tukafika sehem yenye kichaka kidogo Ghaflaa!!..Ukatokea mwanga wa kiasi chake ule mwanga ukajitengeneza akatokezea mtu.....

SONGA NAYO..
Alitokezea mzee nyanda huku akicheka sana, nikashtuka!!.. Nikarudi nyuma kidogo.
"Tulia simama hapa hapa" alisema yusrat huku akinishika mkono
"Hahahaha!.. Nimerudi kwa nguvu mpya lazima kafara yangu ifanikiwe, kijana nakupa siku chache tu za kuishi duniani." alisema mzee nyanda
"Hahaha!!.. Labda tukupe wewe hizo siku, huwezi kumfanya chochote mi nikiwepo"
"Haahaahaa.. Haijalishi uwepo au usiwepo lazima kafara ifanikiwe siku chache zijazo jiandae kumzika, hahahaha.." alicheka sana mzee nyanda kisha akatoweka mahala pale.

Niliogopa Sana, lakini yusrat akanitoa hofu huku akinishika mkono tukaendelea na safari.
"Usijali mi nipo pamoja na wewe takulinda kwa nguvu zangu zote kwakuwa nakupenda niko ladhi chochote kinikute ila wewe uwe salama."
"Mmh!.. Sawa nashukuru kwa upendo wako"
"Usijali nimetoka kwenye msiba wa baba sijakaa hata, nimekuja kwaajili yakukulinda wewe."
"Mmmh!!.." nilishangaa maana taarifa zile zilikuwa ngeni masikioni mwangu nikamuuliza.
"Kwhyo baba ako amekufa?."
"Ndio baba alifariki ule mda yanakutokea yale matatazo mi nilikuwa kwenye mazishi, tulipomaliza kumzika ndo nikaja haraka."
"Ooh pole Sana, halafu eheeeh!!.. Nimekumbuka ile siku uliniambia utanielezea we ni nani"
"Usijali subiri tufike nikuelezee" Ilibidi niwe mpole tukazidi kuzipiga hatua za taratibu hatukuwa na haraka maana ilikuwa ni usku watu kunijua kama ni mimi ilikuwa ni vigum kidogo, sehemu zingine tulikuwa tunakaa tunapiga story kidogo mixer michezo michezo ya wapendanao.

Upande wa pili, mzee nyanda alionekana akitua kwenye kile chumba alicho walaza wale wachawi wenzake walio tolewa viungo baadhi vya mwili. Alikuta wapo wawili tu, mzee pago na mzee fundikila walikuwa washaondoka baada ya viungo vyao kujiunga na kurudi kama zamani.
Mzee nyanda akasogea Hadi pale walipo lala wale wawili waliokuwa wamejeruhiwa vibaya, akawashika kwenye shingo zao, akakuta wameshafariki. akawatoa kimiujiza kwenye chumba kile Kila mmoja akampeleka kwenye nyumba yake, mmoja akampeleka kwenye kitanda chake akafika anamlaza huyu hakuwa na familia yoyote alikuwa anaishi mwenyewe tu. Yule wa pili na yeye akaenda kumuweka kwenye kitanda chake anacholalaga yeye na mke wake, huyu alikuwa anafamilia yake alikuwa anamke na watoto wawili. Mzee nyanda baada ya kumaliza kazi ya kuwaweka kwenye vitanda vyao alitoweka.

Ndani ya nyumba ya yule mchawi mwenye familia, anaonekana mke wake akiwa amekaa sebureni na watoto wake wakiongea kitu.
"Tokea juzi baba yenu haonekani sjui atakuwa ameenda wapi, maana nakumbuka tulikuwa tumelala nae kabsa asubuh naamka simuoni, sjui hata aliondoka mda Gani na anaondoka ananiacha na hali hii ya ujauzito sijui anafikiria nini, wanangu Sina hata mia ya akiba nilikokuwa nako kameisha leo mchana, mwanangu juma nenda dukani kwa mzee nyanda ukakope unga robo usonge ugali ule na mdogo wako zai, mboga zilibakia kidogo ziko kule jikoni.." alisema mama yule, akimwambia wanae wa kwanza anaeitwa juma mwenye miaka 15.
"Mama leo duka la mzee nyanda halijafunguliwa kabisa, nahisi atakuwa hayupo." alisema juma.
"Duuh sasa tunafanyaje mwanangu na kesho mnaamkia shule mnatakiwa mle."
"Hapana mama mbona naweza kuvumilia tu"
"SAWA wewe unaweza na mdogo wako zai je? naye anaweza? Hebu nenda kule mbele kabisa kwenye duka la mangi ukajaribu japo nahisi hawezi kukupa maana anaroho ngum sana yule nenda tu ukajaribu mwambie baba amesema umkopeshe unga robo hela atakuletea keshoo, sawa?"
"Sawa mama" alijibu juma kisha akaondoka akiwa anakimbia, baada ya dakika kadhaa alirudi akiwa anakimbia vile vile.
"Mama na kwa mangi duka limefungwa"
"Jamani sasa tunafanyaje wanangu, au mtazila zile mboga hivyo hivyo tu, mfanye hivyo wanangu halafu zai mkimaliza uje ulale na mimi ngoja mi nikapumzike maana najihisi vibaya." alisema mama yule akijiinua pale kwenye sofa ili aende chumbani mara mlango ukagongwa.

"Karibuuu, juma fungua huo mlango" alisema mama yule akikaa Tena, Akaingia ndani mmama mmoja hivi akiwa na sufuria iliyojaa unga akafika anampa mama juma.
"Ooh jirani asante sana."
"Usijali shoga angu nimekutana na juma hapo njiani nikamuuliza ametoka wapi akanijibu ametoka kukopa unga ila amekuta maduka yamefungwa. Shoga ukiwa unashida na kitu uwe unakuja kuniomba kama ninacho takusaidia, maisha haya nikusaidiana."
"Sawa nimekuelewa asante sana na ubarikiwe"
"Usijali bhan icho ni kitu kidogo tu, mi niende kesho Sasa"
"Sawa karibu Tena" aliondoka mama yule.
"Kwhyo unasonga ugali sasa hivi au unasubiri kidogo" aliuliza mama juma akimuuliza mwanae juma.
"Nasonga sasa hivi ili tulale mapema" alisema juma huku akiinuka na kwenda jikoni, kwakuwa juma alikuwa mkubwa na alishafunzwa kupika na mama ake haikuwa shida kwake alisonga ugali chap chap akapasha na mboga akaleta sebureni wakala pale na mama yao akigusa gusa kidogo. Baada ya kumaliza kula na kupanga vitu vizuri wakaenda kulala, juma akaenda kwenye chumba chake na zai akaongozana na mama ake hadi kwenye chumba cha mama ake na baba ake. Zai alikuwa anatembea haraka haraka ili akawashe taa mama ake akawa anaenda mdogo mdogo, zai akafungua mlango akaingia Kisha akasimama kwenye stuli akawasha taa ya chumbani.

Alipiga kelele baada ya kuona kitu.
"Maamaaaa!!.. Maaamaaaa!.. Njoo umuone babaaa!!..." Aliongea huku akikimbilia nje ya chumba, mama ake alikuwa bado hajafika kwakuwa alikuwa anatembea kwakujivuta vuta kutokana na kuwa na ujauzito wa miezi 8 inayoelekea 9. Alishtuka!!.. Kusikia kelele zile za mtoto wake huku akimtaja mme wake wakati anajua mme wake hajarudi hadi mda ule. Zai alimfikia mama ake huku akilia, Hadi juma mwenyewe alisikia kule chumbani alipokuwa, akatoka akaenda na yeye kuangalia kuna Nini. Mama juma alijivuta vuta hadi akafika chumbani akaufungua mlango akaingia ndani macho yake yakatua kitandani, alishtuka!!..hakuyaamini macho yake baada ya kuona mme wake hana mikono wala miguu hata macho hakuwa nayo.. Presha ilimpanda halafu ikamshuka akayumba yumba akapigiza kichwa kwenye ukuta halafu akadondoka chini akazimia.

Juma na yeye akachungulia chumbani kuona kuna Nini, hakuamini alichokiona akaanza kulia huku akimuamsha mama ake aliyedondokea kifudi fudi akililalia tumbo, dam nyingi zilikuwa zikimtoka. Zai alikuwa anamiaka 10 na alizaliwa na matatizo ya moyo baada ya kuona mama ake dam zinamtiririka vile matatizo yake yakampanda akadondoka chini na yeye akatulia kimya.
Juma alihisi kuchanganyikiwa alishindwa aende kwa nani, alipiga kelele huku akiwa analia kwa nguvu hadi majirani wakasikia.

"Mmh!!. huyu mama juma mbona anampiga mtoto hivi" alisema yule mama aliyewaletea unga
"Achana nao hayatuhusu, kwanza mtoto wenyewe mkubwa yule we kinakuuma nini" alijibu mme wake.
"Hapana sikia analia anasema mamaa, babaa, Ngoja niende nikamkataze asimpige mtoto hivyo."
"We mwanamke tuliza mbaliga zako hapa badala upike chakula unawaza mambo ya watu we yanakuhusu nini?.. Ole wako uvuke huo mlango usirudi humu ndani."

Juma alizidi kulia hadi sauti ya mwisho hadi majirani wengine wakawa wanatoka nje wanasogea kwenye ile nyumba ili wajue kwanini juma analia vile. Yule mama uvumilivu ulimshinda ilibidi tu atoke nje hakujali maneno aliyoyasema mme wake, akaenda hadi kwenye mlango akawa anasema.
"We mama juma mbona unampiga mtoto hivyoo" hakusikia akijibiwa bali alisikia sauti ya juma ikizidi kulia.....
sasa hivi juma akabadilisha style ya kulia akawa analia anasema maneno.
"Mama anguuuuuu!!... jamani dam zinamtokaa!!.., babaa angu eeeeh!!.. amekufa kikatiliii.... Mdogo wangu amka jamaniiii!!...".....ITAENDELEA....

Usikose sehemu ya 14RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu ya 14

TULIPOISHIA..
sasa hivi juma akabadilisha style ya kulia akawa analia anasema maneno.
"Mama anguuuuuu!!... jamani dam zinamtokaa!!.., babaa angu eeeeh!!.. amekufa kikatiliii.... Mdogo wangu amka jamaniiii!!..."

SONGA NAYO..
Ndo yule mama pamoja na majirani wengine waliokuwa wamesogea pale ndo kujua kumbe kuna matatizo, wote wakasogea mlangoni wakaanza kugonga ila juma hakuwa na nguvu za kwenda kuwafungilia. Ikabidi waubomowe ule mlango wakaingia ndani, Moja kwa moja wakapitiliza hadi sauti ya juma inapotokea.

"Heeeeeh!!.. Mungu wanguuu jamani eeeeh!!.... angalieni pale kitandani" alisema yule mama jirani akiwaonesha waliokuwa wanakuja nyuma yake.
"Yarabiiiiiiiii!.. Heee!!. heee!!. Watu makatiri kweli kweli nani kafanya haya mauwaji jamaniiii!!...." alisema mama mwingine huku akifumba macho yake baada yakuona mwili wa baba juma ukiwa kitandani umekatwa katwa.. Kila mwanamke aliyechungulia kwenye kile chumba alirudisha kichwa chake haraka sana maana mwili ulikuwa umejeruhiwa vibaya mnoo Wanaume ndo walioweza kukaza kumtazama.

Mi na yusrat tulifika karibu na Ile nyumba tukiwa tunapita njiani kuelekea kwenye geto langu, tukaona watu wengi pale huku wengine wakipiga kelele nikamwambia yusrat.
"Twende tukaangalia kuna Nini" akanijibu
"Kwhyo umeshasahau kama wewe unaonekana ni mzimu kwenye macho yao au unataka wakimbie wale wote."
"Duuuh!!.. nilikuwa nishasahau"
"Halafu pale kuna mtu amefariki na yule aliyekufa mi ndio niliyemuuwa."
"Heeeh!!... We ndio uliyemuuwa kiaje mbona sikuelewi"
"Walinivamia nyumbani akiwa na mzee nyanda pamoja na wachawi wengine ndo baadhi nikawauwa na yeye akiwemo wengine wakakimbia, Ila nahisi kuna huruma inajia juu ya familia yake, hata kama yeye alikuwa ni mbaya lakini familia yake haina hatia."
"Duuh!!.. Kumbe ndo ilivyokuwa, Sasa sikia pale kwenye ile nyumba ndo anaishi mke mdogo wa marehemu baba angu."
"Mmmh!. Inamaana mke wa huyo mwanaume aliyekufa alikuwa mke wa baba Ako?.."
"Ndio ila marehemu baba alimpaga taraka hata kabla hawajazaa maana huyo mwanamke alikuwa malaya sana wakashindwana na baba, Na mara ya kwanza nilipo muona nilishtuka sana nilimkumbuka japo kipindi kile anaondoka nilikuwa mdogo, ndo nikajua kumbe anaishigi huku na ameolewa Tena na anawatoto, nilikuwa napitaga kumsalimia siku moja Moja."
"ooh kumbe ndo iko hivyo, Kesho tutakuja kuwapa pole."
alisema yusrat, mara tukaona gari ya polisi inafika wakashuka wakaingia ndani wakafanya utaratibu wanao ujuwa wao mda si mrefu na gari nyingine ikaja ilikuwa ni haisi ikaenda hadi kwenye ile nyumba watu wakatoka wakiwa wamembeba mama juma na wengine wakatoka wameubeba mwili wa baba juma ukiwa umestiliwa pamoja na mtoto wao zai, wakawaweka ndani kwenye ile gari aina ya haisi. Nilishtuka kidogo maana yusrat aliniambia aliyefariki ni baba juma tu halafu nikaona anatolewa na mamdogo na mtoto wake zai nikawa na maswali mengi kichwani ila sikutakiwa kufika pale maana ningeonekana ni mzimu. Gari ikaondoka kuwapeleka hospital, na polisi wakaondoka, Yule mama jirani akatoka ndani amemshika juma mkono wakaufunga mlango wa ile nyumba watu wakatawanyika, nami na yusrat tukaendelea na safari ya kuelekea geto.

Baada ya mimi na yusrat kufika geto, yusrat akaanza sasa kunielezea yote yalitokea mtaani hapo ambayo nilikuwa siyajui maana yeye alikuwa anauwezo wakuyaona na akanielezea na yeye ni nani na ametokea kwenye familia gani.
"Mi Naitwa Yusrat Adel ni mtoto wa kwanza kwenye familia ya Adel kareem pamoja na lamia Amar ambao ndio wazazi wangu yani baba na mama, Kaka angu Yani Mdogo wangu anaitwa Fahad adel. Marehemu baba yangu alikuwa ni mzanzibar na mama yangu anatokea nchi za kiarabu Saudi Arabia.

Historia yao hadi kukutana ilikuwa hivi, Mama akiwa binti alikuja na wazazi wake Zanzibar kibiashara kuna mladi wazazi wake walikuwa wamekuja kuwekeza Siku moja mama akiwa na wazazi wake wakitembea tembea kuangalia maadhari walienda hadi maeneo ya beach mama akataka kuogelea wazazi wake wakamruhusu wenyewe wakaendelea kuzunguka zunguka, mama akaenda kubadilisha nguo alipomaliza akaenda kuogelea alikuwa anajua jua kuogelea japo sio sana alisogea hadi mbele kidogo maji yakamzidia akawa anazama, wazazi wake walikuwa wameshasogea mbali kidogo hawakuweza kumuona. Kuna kijana mmoja alikuwa kwa mbali kidogo aliweza kumuona mama akizama akaogelea haraka haraka mpaka akafika alipo zamia akamuokoa akamtoa kwenye maji akampeleka nchi kavu akamlaza Kisha akaanza kumtoa maji kwakumkandamiza tumboni na mikono Kisha na kumpa pumzi kwakutumia mdomo.

Baada ya mda mama alizinduka huku akitoa maji mdomoni, alishtuka baada yakumuona yule kijana akiwa amemuwekea mdomo kama vile anampiga denda, akamsukuma pembeni kisha akamuuliza.
"Who are you? ( we ni nani?)"
"I have helped you after sinking in water(Nimekusaidia baada ya kuzama ndani ya maji)"
"Oooh!!!.. Sorry and thank you ( Oooh !!! Samahani na asante)"
"Don't worry, and why are you going long distances when you don't know to swim (Usijali, na kwa nini unakwenda umbali mrefu wakati hujui kuogelea)"
"It was as bad luck i knew that i can continue (Ilikuwa ni bahati mbaya nilijua kwamba ninaweza kuendelea)
"Ok what is your name? And who have you come with? (Sawa, jina lako ni nani? Na wewe umekuja na nani?)"
"My name is lamia i came with my parents and are those who come (Jina langu ni Lamia nilikuja na wazazi wangu na ni wale wanaokuja)"
"My name is Adel, where do you live?. (Jina langu ni adel, unaishi Wapi?.)
(We are not in this place we have come to the business, we're in the hotel. (Hatuishi mahala huku tumekuja kwaajili ya biashara, Tuko hotelini)"

Basi mama alimtajia yule kijana ambae ndo baba yangu, jina la hotel waliofikia. Baba akarudi kuogelea, jioni yake baba akaenda kwenye ile hotel aliyomtajia akamkuta mama sehem ambayo alimwambia amkute wakapiga story pale wakafahamiana kwakiasi chake. Siku kama mbili sikapita wakawa washazoeana, baba alimtembeza mama sehemu mbali mbali kumuonesha mazingira ya Zanzibar. Wazazi wa mama Walishtuka kidogo baada ya mtoto wao kuwa na ruti nyingi ila mama akawaelezea wazazi wake kuwa kuna mtu amekutana nae anaujua mji vizuri na ndio anamtembezaga sehem mbali mbali. Wazazi wake hawakumbana sana walimruhusu japo baba ake aliwaza ni jambo la hatari sana kumuachia binti ake kutembea tembea hovyo wakati yuko ugenini, hakusema chochote alionesha kuelewa alichosema Binti yake. Akaajili vijana wawili wawe wanamfatilia binti yake kisiri siri bila yeye kujua.

Adel na Lamia ambao ndo baba na mama, sasa walikuwa wapenzi baada ya kuzoeana na kuziweka hisia zao wazi wakawa wanajiachia na ndio mimba yangu ikapatikana. Walitembea sehem mbali mbali wakishikana na mabusu kama yote, wale vijana walio pewa kazi na baba ake wamfatilie waliyaona matukio yale wakampelekea taarifa. Baba ake alikasirika sana akawatuma wale vijana wamuangamize baba angu.

Siku hii baba na mama walikuwa wameenda beach ile sehemu waliyokutania ila ilikuwa kwa pembeni kidogo hakukuwa na watu upande ule walikaa kwenye mawe ya pale kisha wakaanza kuyachezea maji huku wakimwagiana na kufurahi, walitokea kupendana sana.
Wakiwa hawana hili wala lile ghafla wakatokea wale vijana walio tumwa na baba ake na mama.
"Tulia kama ulivyo usiinuke wala kujigeuza" alisema mmoja wa wale vijana, wakiwa wamesimama kwa nyuma kidogo na bastora zao, Mama alishangaa akawauliza.
"What has he done? (Amefanya Nini?)
"Its problems being in relationships with you (Matatizo yake nikuwa katika mahusiano na wewe)"

Mama akahisi moja kwa moja wale watu wametumwa na baba ake akawauliza
"So the father has instructed them? (Kwa hiyo Baba amewaagiza?)" Wale jamaa hawakujibu chochote walizikoki bastola zao Kisha wakataka kumfyatulia risasi baba, Mama akamkinga baba.
"It is impossible( Haiwezekani)"
"Exit there (Toka hapo)" ila mama alikataa kata kata kutoka akitaka apigwe kwanza yeye ndo wampige sasa baba. Mara sim ya mmoja kati ya wale vijana ikaita akaitoa mfukoni Kisha akaiweka sikioni.
"Halloo mkuu"
"Nimepeni ripoti mmefikia wapi nilicho waagiza" ilisikika sauti ikiongea kiswahili chakujifunza.
"Mkuu tuko nao huku beach ndo tunataka kummaliza huyu kijana"
"Bado mnasubiri nini nyie muuweni haraka mtoke huko mje na mwanangu."
"Mkuu binti yako ndio anatuchelewesha amemkinga anasema tumuuwe kwanza yeye ndo tuweze kumuuwa huyu kijana"
"Nyie ni wapuuzi kweli kweli, mnashindwa kumshika na kumuweka pembeni Kisha mfanye kazi yenu?"
"Sawa mkuu nimekuelewa"
"Fanyeni haraka nataka kusikia ripoti kuwa mumemuangamiza."
"Sawa mkuu" sim ilikatwa Kisha yule Kijana akaenda kumkamata mama Kisha akamsogeza pembeni halafu akamwambia mwenzake.
"Mmalize haraka." yule jamaa akamshuti baba risasi mbili, baba akadondokea kwenye maji akazama kabisa. Mama akachoropoka kwenye mikono ya yule jamaa na yeye akajidumbukiza ndani ya maji......ITAENDELEA...

RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu ya 15

TULIPOISHIA..
"Mmalize haraka." yule jamaa akamshuti baba risasi mbili, baba akadondokea kwenye maji akazama kabisa. Mama akachoropoka kwenye mikono ya yule jamaa na yeye akajidumbukiza ndani ya maji......

SONGA NAYO..
Wale jamaa walishangaa.
"We unashangaa nini, we sindio umemwaachia kamfate haraka."
"Nenda wewe mi sijui kuogelea naupenda uhai wangu"
"Hivi we ni mjinga, boss akijua hili siatatuuwa"
"Siuingie wewe kama unaona ni rahisi, kwanza boss mwenyewe haujui huu mji vizuri nikijichimbia sehem atanipatia wapi, ebana eeeh potelea mbali mi hiyo hela ya kazi siitaki nasepa zangu kujichimbia kitaa ndani ndani." alisema yule jamaa huku akiondoka, yule mwenzake ilibidi ajitupe yeye ndani ya maji.
"Kufa mwenyewe huko na hivi haujui kuogelea mi nasepa zangu, bahati nzuri huyo boss wako hanijui, anakujua wewe mwenyewe, bye bye kama ukipona sawa kama ukifa sawa tutaonana kuzimu." alisema yule jamaa huku akizidi kuzipiga hatua za kuondoka.

Yule jamaa aliyeingia ndani ya maji kumuokoa mama alijitahidi sana kumtafuta lakini hakumuona, na nguvu zilikuwa zimeshaanza kumuishia maana hakuwa mjuzi kwenye kuogelea. bahati nzuri akaiyona boti kwa mbali kidogo ikipita akainua mkono juu kuonesha ishara, wale watu wakaja kumsaidia alikuwa ameshakunywa maji kama Lita kadhaa akazimia. Wakamnyanyua wakamuweka kwenye boti kisha wakaenda nae nchi kavu.

Mama baada yakuzama ndani ya maji alipoteza fahamu, Alikuja kushtuka akiwa ndani ya chumba kizuri kilicho pambwa na vito vya thamani chumba kiling'aa kwa dhahabu, alishangaa kujikuta mahala pale akainuka kutoka kitandani akaanza kuangalia maadhari ya kile chumba kilikuwa kimepambwa haswa, pamoja na kuwa alikulia kwenye maisha yakitajiri huko kwenye falme za kiarabu ila jinsi kile chumba kilivyopambwa hakuwahi kuona chumba kilicho pendeza kama kile chumba kilikuwa kimepambwa kisawa sawa zaidi ya wahindi.
Akazipiga hatua taratibu hadi maeneo ya mlangoni akataka kuufungua, mara mtu akafungua Kwa nje akaingia mdada mzurii mwili wake ulivyaa nguo zilizo ng'aa sana kama vile amevaa nguo za dhahabu, akaongea.

"Mambo" mama akamjibu.
"Who are you? ( We ni nani)"
Yule mdada akamshika kichwa mama Kisha akanuia maneno kadhaa halafu akasema.
"Ongea kiswahili bhan mi ndio napenda sipendi hayo marugha yenu japo nayajua." Yule mdada alipomshika kichwa mama alikuwa anaiweka rugha ya kiswahili kichwani kwa mama, kwahiyo Sasa mama alikuwa anaweza kuongea kiswahili vizuri sana.

"We ni nani, na mi nimefikaje fikaje hapa?" alisema mama.
"Ewaaah nilikuwa nataka uongee hivyo maana nakipenda kiswahili Sana mtu akiongea nahisi raha kweli kweli."
"Nijibu maswali yangu kwanza." alisema mama
"Tulia usiwe na pupa takuelezea mwanzo mwisho, Kaa kwanza hapo kwenye sofa." alisema yule mdada kisha mama akakaa, yule mdada akaanza kuongea na yeye akiwa amekaa kwenye ile ile sofa.
"Mi ni jini naitwa Sarha"
Mama alishtuka baada yakusikia vile akaanza kusogea pembeni kabisa kwenye ile sofa.
"Hapana usiniogope ningekuwa mtu mbaya nisingekuleta huku ningekuacha ufie ndani ya maji"
"Kwahyo umeniokoa mimi peke yangu?" aliuliza mama.
"Tulia kwanza nikwambie uko wapi Kisha ndo takuelezea Sasa."
"Sawa" alijibu mama akikaa kwakutulia
"Hapa uko kwenye mji wa MAJINI WA MAJINI. Sijui umenielewa au nimekuchanganya, Nisikilize vizuri namaanisha MAJINI WA BAHARINI, Huu mji wetu unaitwa JOZI. Mi Na ndugu yangu tulikuwa tunaenda duniani kutembea tembea kabla hatujafika tukawaona wewe na kijana mmoja mkiwa mmezama ndani ya maji, huku mkiwa mmepoteza fahamu yule mwenzako alikuwa anatokwa na dam nyingi sana maeneo ya pegani."

"Heeeh!!. Yuko wapi!!.. Yuko wapii!.. Adel wangu na anaendeleaje nataka kumuona!!.." alisema mama akiwa amebaha baada yakukumbuka jinsi alivyopigwa risasi baba.
"hebu tulia kwanza mbona unapupa sana, tulia nikuelezee." alisema sarha akimtuliza mama.
"Yule kijana yuko vizuri kabisa ameshatolewa risasi zote na ametibiwa yuko sawa kabisa, sema bado amezimia hajazinduka hadi sasa hivi."
"Naomba unipeleke nikamuone hata kidogo tu tafadhali sana." alisema mama
"Sawa twende ukamuona" alisema sarha, Kisha wakaufungua mlango walikuwa kwenye jumba kubwa sana ilikuwa inapendeza sana pale chini kulikuwa kama kuna kioo ukitembea unajiona chini, kwa jinsi marumaru ilivyokuwa.

Wakafika hadi kwenye chumba alicholazwa baba, Sarha akafungua mlango wakaingia ndani, Mama alikimbia kuwahi kufika pale alipolazwa baba akafika anamkumbatia vile vile akiwa amezimia na kumpiga mabusu. Akamfunua shati aliyokuwa amevaa akatazama sehemu alipopigwa risasi.
Alishangaa hakuona hata alama yoyote akahisi labda sio pale akamgeuza kidogo Kisha akaangalia upande wa pili, alizidi kushangaa baada yakuona hamna hata kovu akajiwazia.
"Au zilikuwa risasi bandia wala hakuumia?." Mara sarha kamjibu.
"Najua unachowaza, hazikuwa risasi bandia zilikuwa risasi za kweli na zilimuumiza sana ndomana hadi sasa bado amezimia"
Mama alishtuka huku akijiuliza "amesikiaje?" Sarha akasema Tena
"Unajiuliza nimesikiaje kwani umesahau kama mi ni jini?.. Sikia nikwambie Ilikuwa bado kidogo tu afariki tukaona hadi tumtoe risasi tunaweza kuchelewa halafu akapoteza maisha ndo Tukamrefresh mwili wake ndomana unaona hana kovu lolote hata kama alikuwa nayo mengine yote yametoka, mda si mrefu atazinduka baada ya mwili wake kukaa sawa" alisema sarha.
"Halafu twende muache kwanza" alisema sarha, huku akimshika mkono mama akimtoa nje, wakiwa wamefika mlangoni mara baba akasikika akikohoa ikabidi warudi.

"Lamia niko wapi hapa?" alisema baba baada yakuzinduka nakujikuta amelala pale.
"Vipi kwanza hali yako unajihisije?"
"Mbona sihisi chochote najihisi niko sawa tu? Nakumbuka nilipigwa risasi mbili kwenye hizi bega zote nikadondoka ndani ya maji baada ya hapo sikumbuki chochote niambie imekuaje hadi nikafika hapa."
"Adel ngoja nikwambie nilivyoambiwa" mama akamuelezea baba yote aliyoambiwa na Sarha, baba akaelewa.

***************
TURUDI...
"Haya sasa, Saa 4 hii tulale kesho tutaendelea tulipoishia."
"Aaaah jamani bado mapema endelea kidogo tu nijue ilikuwaje" nilisema
"Hapana Roy kesho tutaendelea." alisema yusrat, Ilibidi niwe mpole.
"Halafu nahisi njaa, fanya manduva nduva yako nipate msosi siwezi kulala hivi" nilisema
"Duuh hauogopi kula chakula ambacho hujui kimetoka wapi?" alisema yusrat
"Mi sijali imladi umekileta wewe maana nakuamini sana najua huwezi kuniletea kitu kibaya, nataka tupendane mapenzi ya kweli kama walivyokuwa mama ako na baba ako." nilisema, Yusrat akatabasam kisha akainua mkono mmoja juu ikatokea sahani imejaa minyama ya kuku pamoja na viazi mviringo, nikasema.
"Eheeeeeh!!...., Miujiza kama ileee ya yesu, yani unainua mkono juu kinatokea chakula duuh!.. nami nataka niwe kama wewe." nilisema huku nikiula ule msosi baada ya maji yakunawa kuja kimiujiza.
"Nyoooo... Ili usiwe unafanya kazi hapana pambana kwa nguvu zako"
"Sio hivyo sweetie nikwaajili ili nipambane tu na watu wabaya"
"Kwanini umesema sasa hivi ulipoona chakula kimetokea, we mawazo yako unawaza siku ambayo utapata uvivu wa kupika unyoshe mkono tu msosi uje ndo unawaza hivyo."
"Hapana siwazi hivyo, lakini inawezekana kuzipata hizo nguvu?"
"Ndio inawezekana kuzipata ila hadi niende kwenye mji wa JOZI kule kwenye majini wa baharini."
"Hivi inawezekana kwenda kule?"
"ndio inawezekana vizuri tu lakini kwa mimi tu sio wewe maana hufahamiki kule." Alisema yusrat
"Mmmh!!.. kwa jinsi ulivyo hadithia inaonesha kule nipazuri sana, kwhyo unataka kuniambia huo mji uko chini ya bahari?"
"Ndio"
"Mi hata sasa hivi niko tayari kwenda huko."
"haiwezekani hadi uwe umechaguliwa kwa kazi maalum yani upate AGIZO LA MAJINI Ndo wewe unaweza kwenda bila hivyo haiwezekani" alisema yusrat, ilibidi nimuelewe sikubisha nikalala.

Mida ya usiku wa manane nikiwa nimelala fofofo, Zikasikika paka zikilia "Nyauuuuu Nyauuuuuuu" yusrat alizisikia zile sauti akatulia kuona kitajiri nini, mara ikasikika miguu ya paka ikitembea juu ya bati huku ikilia vile vile, Yusrat akajisemea kimoyo moyo.
"Hahahaha, wamezani Roy amelala peke Ake Ngoja waje niwaadabishe."
Punde si punde Zikatua ndani ya chumba paka mbili........ITAENDELEA...

Usikose Sehemu ya 16
 
Agizo la majini 16-20RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

SEHEMU YA 16

TULIPOISHIA...
"Hahahaha, wamezani Roy amelala peke Ake Ngoja waje niwaadabishe."
Punde si punde Zikatua ndani ya chumba paka mbili.......

SONGA NAYO...
Zilipotua chini zikajibadilisha zikawa watu wa kawaida, Alikuwa ni mzee fundikila na mzee Pago.
"Hahahaha!!.. Naona viungo vyenu vimeunganika hamjakoma bado et eeeh"
Walishtuka wale wazee huku wakirudi nyuma hadi mwisho kwenye ukuta, maana hawakutegemea kama watamkuta yusrat kwenye chumba changu. Yusrat akainuka kutoka kitandani Kisha akawasogelea.
"Mzee nyanda ndo amewatuma eeeh!!..?"
"Nd..i.o" walijibu wakiwa wanauoga.
"Ok sasa sikieni leo mmeyatimba, nataka nimpe soma mkuu wenu ajue kama mimi sio mtu wa mchezo mchezo maana bado anakiburi hataki kukubali."
"Tunaomba utusamee hatutorudia tena tuache tuondoke" "mbwiiiii!!.. Mbwiiii!!.." walisema wale wazee misuzi ikiwa inawatoka mfurulizo.

"Hahahaha!... Kuwa samehe Hilo mmsahau kabisa nyie hamstahiri kuishi duniani maana mnawatesa binadam wasio na hatia mnawauwa mnawafanya misukule, sasa leo ndio mwisho wenu wakuiyona Dunia hii nzuriii yenye kupendeza, kwahyo nyie watu wabaya hamstahiri kuishi kwenye hii Dunia maana nyie ni wachafu wa roho." alisema yusrat, makucha yake ya kwenye vidole yakionekana yakizidi kuwa marefuu, akauwinua mkono wa kulia juu akamchoma machoni mzee Pago kwa vidole viwili kisha akavichomoa vikatoka na jicho zote mbili, mzee pago alipiga kelele akijishika machoni.
"Yalaaaaaaah!!.. Nakufaaaaa!.."
"Kufaaa una faida gani duniani zaidi ya hasara?.., Harafu sitaki kusikia kelele kaa kimyaaaa!.. Usije kumuamsha roy wangu." wakati huo mi nilikuwa kwenye usingizi mzito sana sikuweza kusikia chochote nahisi yusrat ndio alinipa ule usingizi ili nisisikie.

Mzee Fundikila pembeni alikuwa ameshajisaidia haja kubwaa ndani ya suruali yake mzigo ulionekana ukining'inia, mwili wake wote ulikuwa unatetemeka kama Jenereta huku jasho likimtiririka kama kuna maji ya mvua yanammwagikia, alikuwa anajaribu kutoweka kimiujiza ila hakuweza alishindwa kabisa ikabidi atulie tu asubiria aone atachofanywa.

"Kumbe mkuki kwa nguruwe ni mtam ila kwa binadam ni mchungu et eeeh?.. Unalia nini sasa wakati ulikuwa unawafanyia wenzako hivi hivi." alisema yusrat, akaunyosha mkono wake mwenye vidole vyenye makucha yaliyo chongoka akauchomeka tumboni mwa mzee pago akauviringisha mkono akauchomoa ukiwa umeshika utumbo, ule utumbo akamtupia mzee fundikila kwenye kichwa alikuwa amejiziba usoni ili asione ukatiri ule, alishtuka akapiga kelele baada yakutupiwa ule utumbo.
Yusrat baada kumuangamiza mzee pago akamsogelea mzee fundikila, akafika anainama chini akamshika shati akamuinua juu akambananisha ukutani huku sura yake ikiwa imebalidilika alitisha sana na ule muonekano aliokuwa nao, macho yake yalikuwa ya blue yenye mwanga wakuumiza, Yalitokeza meno mengine marefu kwenye kinywa chake. Mzee fundikila akiwa anatetemeka aliigeuza shingo yake pembeni ili ashikutanishe macho kwa macho na yusrat.

Yusrat akaacha kuishika ile shati akaanza kumchoma choma na makucha yake alianzia tumboni Kisha akapanda juu hadi usoni akamtoboa toboa juu kote akajaa matobo, dam zikaanza kutiririka kutoka kwenye yale matobo alipiga kelele huku akilia kama katoto kachanga. Yusrat hakutaka kumchelewesha akavichomeka vidole vyake kwenye kifua cha mzee fundikila upande wa kushoto akakandamiza kabisa mkono ukazama ndani kabisa hadi kwenye moyo akaushika kisha akauchomoa moyo wa mzee fundikila ukiwa unadunda dunda akautazama Kisha akautupa chini, Mzee fundikila alikuwa ameshakata kamba kitambo. Yusrat akaanza kucheka.
"Hahahaha!... Mzee nyanda kidogo kidogo utaelewa mi ni hatari kiasi Gani." alisema yusrat huku mwili wake ukirudi kwenye hali ya kawaida, Akaunyosha mkono kuelekeza kwenye ile miili, ikatoweka yote pakarudi kama mwanzo hakukuwa hata na tone la dam pale chini. Ile miili ilienda hadi kwenye chumba cha mzee nyanda ikajitandaza chini ya kitanda alicholalia mzee nyanda akiwa fofofo hana habari.

Yusrat baada yakumaliza ile kazi alipanda kitandani akauchapa usingizi.
Asubuh mi ndio nilikuwa wa kwanza kuamka nikamuamsha yusrat ili anihadithie kwanza ile story kabla ya mambo yote ya usafi na nakunywa chai, Aliamka akiwa na mang'amung'amu ya usingizi.
"Amka sweetie unimalizie ile hadithi"
"Mmh!!.. roy asubuh yote hii unataka hadithi?"
"Ndio darling jana ulinikatishia utam endeleza ulipoishia."
"Hapana badae sio sasa hivi, maana siko sawa najihisi vibaya vibaya ngoja nipumzike kidogo kwanza."
"Mmh pole, sawa endelea kulala acha mi niamke nifanye fanye usafi."
"Sawa roy wangu" alijibu Kisha nikashuka kutoka kitandani nikaenda kufanya usafi.

Upande wa pili kwenye chumba cha mzee nyanda, Alionekana mzee nyanda akifumbua macho akaamka akatanguliza miguu chini mwili ukiwa umekaa kwenye kitanda. Alistaajabu kidogo baada ya kuhisi kama kuna kitu amekikanyaga chini akajiinua haraka haraka akaelekeza kichwa chake chini ya kitanda kuona ni nini kile. Alishtuka baada yakuona miili ya wachawi wenzake ikiwa pale chini imetapakaa dam, alikumbuka jana ake aliwatuma waende wakaichukue roho yangu halafu wampelekee. Akiwa anajua mi siku hiyo nimelala mwenyewe kumbe sivyo, moja kwa moja akahisi kazi ile imefanywa na yusrat. Akashuka chini kama kawaida yake akaichukua ile miili kimiujiza akaipeleka hadi kwenye nyumba za wale wachawi akawalaza kwenye vitanda vyao kisha akatoweka akarudi zake kwake kufungua duka.

Upande mwingine ndani ya chumba ulionekana mwili ukizidi kuharibika, funza zilionekana zikitembea tembea kwenye vile vidonda. Ni yule mchawi aliyeuwawa style Moja na baba juma.

Upande wa hospitalini, madaktari waliwapa majibu majirani wa baba juma waliokuwa wamekuja kujua hali zao asubuh ile.
"daktari anasema mama juma amefariki pamoja na mtoto aliyekuwa tumboni wote wamekata roho, na yule binti yake zai pia na yeye amefariki. Hivi hamna ndugu yoyote unayemjua wa familia hii tuwape taarifa waje wachukue hizi maiti wakazike?" alisema mbaba mmoja ambae ni jirani yake.
"Hapana kwakweli simjui yoyote hivi mule ndani hamkukuta sim tukaangalie namba tuwapigie ndugu zake pamoja na marafiki zake wengine ambao hawana hii taarifa."
"Hapana baba juma hadi yanamkuta haya hakuwa na sim maana ilipotea kama wiki mbili hivi zilizopita."
"Na mke wake je?"
"Na yeye pia hakuwa na sim, Story nilizo zisikia nikuwa et ndugu zake wote wameshariki sasa sina uhakika kama ni kweli"
"Sasa kama unajua hivyo kwanini uniulize mimi wakati unaelewa kabisa hana ndugu."
"Mi nimeongelea baba juma sijajua sasa kwa upande wa mke wake ndomana nimekuuliza kama unajua ndugu wa hii familia nikimaanisha ni familia moja haijalishi kama ni ndugu wa mme au mke."
"Oooh hapo sasa nimekuelewa, kiukweli siwajui ila hii swali ulitakiwa ulijbu wewe maana wewe ndo rafiki mkubwa wa baba juma"
"Ni kweli mi ni rafiki yangu ila habari za ndugu zake hatukuwahi kuongelea kabisa wala sikuwahi kuwaona." alisema yule jamaa ambae alikuwa ni mchawi mwenzake na baba juma.
"Duuuh sasa urafiki gani huo mmh!!.. Sawa tuachane na hayo Vp polisi walifika?..."
"Ndio walifika tokea jana sijui Sasa kitajiri Nini"
"Sawa, tunafanyaje Sasa?.."
"Hapa ni kwenda kuulizia majirani kama kuna mtu anayewajua ndugu wa hii familia."
"Sawa" walikubaliana hivyo Kisha wakaondoka maeneo yale ya hospital.

Upande wa pili, Yule mama aliyemchukua juma jana ake usiku. Alionekana akitaka kuamka, alipapasa kwenye kitanda upande anaolalaga mme wake lakini hakumuona, akaamka akakaa kitandani akakumbuka jana ake usiku ilivyokuwa.
Baada miili yote kuwekwa kwenye gari alienda kwake akachukua kufuri kisha akarudi kwa mama juma akamtoa juma ndani kisha akaufunga mlango maana ndo maagizo aliyopewa na polisi, Akaenda nae juma hadi kwake, ila baada yakufika tu ndani mme wake akamuuliza.

"Kimetokea nini mbona nilikuwa nasikia makelele tu halafu watu wamejazana je kuna Nini?"
"We unaona watu wengi badala utoke uangalie we umejivundika ndani tu, sasa sikia baba juma amefariki Tena amekufa kifo cha kikatiri sana na hatujui ameuwawa mda gani na nani alimuuwa vile hatujui ila amekatwa katwa viungo vyote, halafu mkewe alidondoka akalilalia tumbo akazimia dam nyingi zinamtoka na kale katoto kao kazai na kenyewe kamezimia." .......ITAENDELEA...

RIWAYA: AGIZO LA MAJINI.
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu ya 17

TULIPOISHIA..
"We unaona watu wengi badala utoke uangalie we umejivundika ndani tu, sasa sikia baba juma amefariki Tena amekufa kifo cha kikatiri sana na hatujui ameuwawa mda gani na nani alimuuwa vile hatujui ila amekatwa katwa viungo vyote, halafu mkewe alidondoka akalilalia tumbo akazimia dam nyingi zinamtoka na kale katoto kao kazai na kenyewe kamezimia." .......

SONGA NAYO...
alimsimulia mme wake mama yule anayeitwa mama Lucy. Juma baada ya kusikia mama lucy anaelezea vile akajikuta anaanza kulia tena alilia kwa uchungu, ikabidi mama lucy ampeleke kwenye chumba cha lucy ambae kwa siku hiyo alikuwa ameenda kwa bibi yake.

Alipombembeleza bembeleza akimwambia.
"Jikaze we ni mkubwa sasa, waombee dua wazazi wako pamoja na mdogo wako sio kulia." alisema mama lucy
kilio kikapungua kidogo, akarudi sebureni kuongea na mme wake.
"Duuuh!!.. Maskini kumbe mda ule juma analia alikuwa anawalilia wazazi wake?.. Mi nikajua anapigwa Duuu!!..."
"Ndo iko hivyo majirani wote walikuwa wamekusanyika hapo nje wewe tu ndo ulikuwa ndani sijui ulikuwa husikii?.."
"Nilikuwa nazisikia ila nikajua ni mambo ya umbea tu wanashangaa mtoto kupigwa"
"Ila wewe mwanaume wewe unaroho ngum, inamaana hata gari lilipokuja kuwachukua ili liwapeleke hospital hukulisikia?"
"Nililisikia ila nikapuzia, Naomba unielezee hospital waliyopelekwa kesho asubuh niende nikawaone." alisema baba Lucy.

Mama lucy Baada ya kukumbuka hivyo ndo akaelewa mme wake alipoenda, alienda hospital. Na ndo yule aliyekuwa anaulizana maswali kule hospital na yule jamaa mchawi.

Baba Lucy na yule jamaa mchawi walifika pale mtaani wakaeneza taarifa za vifo vile, mtaani kote ile taarifa ilifika kwenye masikio ya watu. walienda hadi kwa mwenyekiti wakamwambia afanye tangazo, Mwenyekiti akampigia sim jamaa anayepitaga mtaani kutoa taarifa za Msiba. Akafika Kisha yule jamaa akaianza kazi yakutembea mtaani akiwa na kipaza sauti mkononi.
"Tangazo tangazoo, tangazo la kutafuta ndugu wa bwana Hassan Lunde pamoja na mkewe bi Samia Luhango, Waliofariki jana usiku. Ndugu yoyote au anayewajua ndugu zao walipo aende kwa mwenyekiti akatoe taarifa." alisema yule jamaa huku akikatiza kila chocho ya mtaa ule.

************
Siku hiyo nilifanya usafi ndani hadi kwenye mbuga, nilipomaliza nikatenga chai jikoni nikaenda kuchukua na vitafunwa. Baada ya Kila kitu nilienda kuoga na yusrat nae akamka akaenda kuoga Tulipo maliza mambo yote, tukaanza kunywa chai.
"Haya sasa niambie kiliendelea Nini?" nilikuwa na shauku ya kujua kilicho jili kwenye story ile inayowahusu wazazi wake na yeye mwenyewe, Yusrat akaendelea.

*********************
"Baada ya baba kuamka na kuelezewa alifikaje pale na risasi zilivyotolewa mwilini mwake, basi alielewa, akashuka chini kutoka kwenye kitanda kile mama akahisi anaweza kuanguka akamuwahi akamshikilia ila baba alimwambia Yuko sawa. Sarha akawaambia wamfate bila ajizi baba na mama wakamfata nyuma, baba aliushangaa sana ule mjengo ulivyokuwa mkubwa na jinsi ulivyopendeza. Baada ya hatua za mwendo kidogo walifika kwenye mlango wa kioo, sarha akaugusa ule mlango ukafunguka Kisha wakaingia ndani.

"Mamaa yangu, malkia Yurha"
"Abee mwanangu, princess sarha" alisema mama yule aliyejulikana kwa jina la Yurha akiwa amesimama karibu na ukuta wa kioo, alikuwa anatazama nje maana chumba kizima kiliweza kuonesha vyema madhari ya nje ila yule wa nje Asingeweza kumuona wala kuona maadhari ya mule ndani, alikuwa amewapa kisogo akimuangalia mtu nje.
"Sarha Sogea uone anachokifanya mdogo wako Surha, kule chini kwenye bustani." sarha akasogea kisha akaangalia chini.
"Mmh!!. Ni hatari kwa maisha yake na pia anajisumbua bure hajachaguliwa yeye hawezi kufanikisha chochote zaidi tu atapata matatizo." alisema sarha, mama ake nae akaongea
"Hivi alisemaga ni wawili?.."
"Ndio Mamaa alisema ni wawili na nahisi Ndo hawa niliowaleta" alisema Sarha, malkia yurha akageuka nyuma akawatazama mama na baba walikuwa na hofu maana waliyasikia maongezi Yale.
"Sawa nimewaona mwanangu na sizani kama wamefika huku kwa bahati mbaya lazima kuna sababu, wapeleke kwa baba ako tuone atakuwa na maamuzi gani." alisema malkia yurha, Sarha akatekeleza agizo la mama ake akatoka nje akiwa nao.

"We sarha unatupeleka wapi?" aliuliza mama
"Tulieni msiwe na wasi wasi nawapeleka sehem salama" alipiga hatua kadhaa wakafika sarha akaushika ule mlango ikasikika sauti ndogoo ikitoka kwenye mlango ikisema. "Subirii" baada ya mda kidogo ikasema "Tayari" mlango ukafunguka wakaingia ndani ya kile chumba.
"Mwanangu karibu kaeni hapo." wakakaa wote kwenye sofa kubwa mle kwenye kile chumba.
"Asante baba, wale watu nilikwambia ndo hawa"
"Mmmh!!.. Unauhakika ndo wenyewe?" alisema baba ake ambae ndo mfalme, alijulikana kwa jina la mfalme Tarhi
"Hapana sina uhakika asilimia mia ila nahisi tu, maana niliwakuta ndani ya maji nahisi hata kama tusinge wapokea wangekuja huku tu."
"Kama unakumbukumbu vizuri alisema ni wangapi?." aliuliza mfalme Tarhi
"Alisema ni wawili."
"Sawa waandae waende sasa"
"Sawa baba" alijibu sarha Kisha akawainua wazazi wangu moja kwa moja akawapeleka kwenye chumba maalum, walipoingia ndani wakawakuta watu wakiwa bize na shughuri zao. Sarha akawatanguliza mbele wazazi wangu yeye akawa nyuma yao akawasogelea akawashika vichwa, ile wanauuliza "Unataka utufanye Nini?.." wakakata moto wakaanguka chini kama mizigo.

Walipo zinduka wakajikuta amelazwa juu ya vitanda, mama alilazwa kwenye kitanda kingine na baba pia kitanda kingine ila kwenye hicho hicho chumba. Walishangaa kuona watu wamewasimamia huku wakiwa wanaongea rugha ambazo hawakuzielewa, Walivaa nguo kama zakikabila hivi. Baba akajiinua kichwa ili akae, alijihisi mwepesi sana alishangaa hali Ile akashuka hadi chini akaanza kutembea tembea alijihisi kama karatasi maana alikuwa mwepesi mnoo. Wale watu wala hata hawakumjali waliendelea na maongezi yao, Baba alishangaa sana yeye kuwa vile akaruka ruka kupima uwepesi wake ukoje. Alidunda kama mpira akaenda mpaka juu kabisa karibu na Paa ya ule mjengo mkubwa, akarudi chini akadunda Tena alikuwa ni zaidi ya mpira safiri hii alipodunda kichwa chake kilienda kujigonga kwenye paa juu mwisho wa nyumba, akarudi tena chini. Mama akiwa bado kitandani amelala vile vile alishangaa kumuona baba anadunda dunda vile na yeye akajiinua alijihisi mwepesi pia, akashuka chini akasogea hadi pale anapodundia baba.

"Wee Adel kimekukuta nini mbona unadunda dunda hivyo" aliuliza mama
"Miiiii siiiiijuuuuii!!..." alisema baba akiwa anaenda juu nakurudi chini akikanyaga chini anadunda Tena anarudi juu.
"Nirikuuuwaaa naaruuka ruuka!!. Tuuu ndo ikanitokea hii Hali!!.."
"Mmmh!!.. Hivi na mimi itakuwa niko hivyo?.. Ngoja nijaribu na mimi tuone" mama alisema vile kisha akaruka ruka na yeye, mara akadunda kama baba naye akapaa hadi juu akarudi tena chini, wakawa wanapishana mmoja akienda juu mwingine anashuka chini, baba alikuwa anahisi kizungu zungu alihisi kama anataka kutapika hivi.
"Nyie watu njoeni mtusaidie." alisema mama akiwa amebaha aliwaambia wale watu walikuwa wamesimama pale karibu na vitanda walivyokuwa wamelalia. Wale watu wakageuza shingo zao wakawaangalia ila hawakusema chochote waliendelea na mambo Yao.
"Nyie mbona mnaroho mbaya hivyooo!!.. Mnaambiwa mje mtusaidia mnatuangalia tu tunavyoteseka" alisema baba ila hawakumjibu chochote. Kwa mama pia hali ilikuwa mbaya alihisi kizungu zungu na kichefu chefu.

Mara akaingia sarha ndani ya chumba kile akawaangalia wanavyodunda dunda Kisha akatabasamu.
"We sarha sisi tunaumia hapa we unacheka sindio?.. Umetufanya nini kwani??.." alisema mama.
"Nimewaona mmedunda dunda kwa mda mrefu sasa bado tu hamjajicontrol?.." aliuliza Sarha.
"Sasa tutajuaje bila kuelekezwa." aliuliza baba.
"Kama nyie ndio wahusika basi mnatakiwa kuwa na uwezo wakujiongeza, fanyeni hivyo jiongezeni." alisema sarha kisha akazipiga hatua zakuondoka kwenye kile chumba.
"Weweee sarha weeeee unatuachaje hivi tutakufa."
"Kufa hamuwezi ila mnatakiwa mjiongeze" alisema sarha kisha akatoka nje.
"Duuuuuuuh!!.." baba alihema Kwa Kasi akionesha kushangaa, sarha kuwaacha vile. Mara akatua chini akasimama akatulia kizunguzungu kikamzidia akadondoka chini akalala Chali pale pale chini.
"Weee adel umefanyaje hadi ukaweza?.." mama aliuliza akiendelea kudunda dunda. Baba alikuwa anaona mawenge mawenge tu sauti ile aliisikia Kwa mbali sana akamjibu kwa taabu......ITAENDELEA..

RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu ya 18

TULIPOISHIA...
"Weee adel umefanyaje hadi ukaweza?.." mama aliuliza akiendelea kudunda dunda. Baba alikuwa anaona mawenge mawenge tu sauti ile aliisikia Kwa mbali sana akamjibu kwa taabu...........

SONGA NAYO.....
"Fanya kama unashusha pumzi" alisema baba kwa taabu.
"Sawaa" alijibu mama Kisha akafanya kama alivyoambia. Akadondoka chini akafikia mgongo akapigiza kisogo chini akazimia.

Baada ya mda kidogo baba hali yake ikarudi kuwa sawa, akainuka akasogea hadi alipo mama akawa anamtikisa huku akimuita ila hakuonesha hata dalili yakuzinduka.
Punde si punde akaingia sarha akiwa na mdogo wake Surha, kwa mwendo wa madoido kama walimbwende.

"Ooh hongereni mmeweza kujicontrol" alisema sarha
"Muamshe kwanza lamia ndo useme hayo maneno yako ya kejeli."
"Oooh hilo tuu hata usijali" alisema Kisha akasogea hadi alipolala mama akainama halafu akaupeleka mkono wake kwenye uso wa mama akafanya kama anauosha uso akapitisha viganja vyake mara moja tu, mama akakohoa akainuliwa akiwa na maruwe ruwe.
Baada ya sekunde kadhaa mwili ukakaa sawa akarudi kama mwanzo.

"Sasa sikieni tunawapeleka mkaianze kazi iliyowaleta huku."
"Kazi Tena? Nyie sindio mlituleta huku mnasemaje sasa hivyo wakati ilikuwa bahati mbaya tu kuzama ndani ya maji.." alisema baba.
"Hakuna bahati mbaya kila kitu kinamakusudi yake nyie mlipangwa mje huku kwa style hiyo kwahyo sio bahati mbaya hamtakiwi kuleta ubishi mnatakiwa mtekeleze AGIZO LETU LA MAJINI."
Baba na mama walishangaa kusikia et kuna kazi wanatakiwa waifanye.

Baba akauliza
"Kazi gani hiyo mnataka tuifanye?" Sarha akamjibu
"Swali zuri kwanza nikupe story kwa ufupi. Wiki moja iliyopita ufalme huu ulipata mgeni kutoka falme ya jirani, Mgeni yule alitumwa na mfalme wa kule alipotoka atuletee zawadi ili kudumisha urafiki wa falme zetu.
Baba aliipokea ile zawadi japo haikuwa kubwa kwetu kwasababu zilikuwa ni dhahabu ambapo kwetu zipo zimejaa kila sehemu.
Hatukutaka kuiona ni ndogo tuliithamini kama vile ni kubwa, Yule mgeni baada yakutupa ile zawadi aliondoka, Tukiwa tumekaa kibarazani tunapiga story kama familia. Mara akaingia mtabiri wetu wa mji wetu huu wa Jozi anayeitwa mtabiri Gurhi, alifika hadi ndani bila salam akatuambia
"Nifateni mkaone." baba alimuuliza
"Tukaone nini mtabiri?.."
"Achana na maswali nifateni" tulitii wote tukamfwata tukashuka chini kabisa, akatupeleka hadi kwenye bustani kisha akatuonesha kitu.
"Mnakiona hiki?."
"Ndio tunakiona kwani ni kinini?" aliuliza mama.

"Hiki amekiweka hapa yule mgeni aliyekuja, na hakuja kwa nia nzuri alikuja kwa nia mbaya hili ni bom limetengenezwa na mashetani wa mfalme wao, na nia yakuleta hili bom anataka mfalme tarhi ujiuzuru Ili aimiliki hii falme yeye yani aongoze kote kule na huku. Na remote ya hili bom la kishetani anayo huyo huyo mfalme, hiyo remote Ina vibonyezeo viwili sehemu ya kulipua nayakulizima kabisa yani linakuwa halina madhara tena, kama akibonyenza tu sehemu ya kulipua basi Mji wote huu wa jozi utateketea ni bom kubwa mnoo tofauti na muonekano wake ulivyo."

"Heeeh!!... Kwahyo tunafanyaje mtabiri mi siwezi kuachia madaraka." alisema mfalme tarhi.
"Kama hauwezi basi tusubiri kupasuliwa tu maana sina msaada wowote"
"Mtabiri kwani hauwezi kulitoa hili tukaenda kulitupa mbali kabisa." alisema malkia yurha, mtabiri akajibu.
"Ni kitu ambacho hakiwezekani, hata uite mashetani na mashetani hawawezi kulinyanyua Wala kulisogeza limeletwa kishetani ila wale mashetani waliyoitengeza hii na kuileta huku wananguvu kubwa mnoo kuzidi mashetani wa miji yote ya huku chini ya bahari. Kuna njia moja tu ambayo inaweza kulitatua hili tatizo, ni hivi kama mnavyojua kila tatzo linalotokeaga basi kuna star wa hilo jambo Yani watu waliochaguliwa na miungu wetu kulitatua hilo, Utabiri wangu unaonesha ambao wanaweza kulimaliza hili tatizo ni watu wa kutoka duniani na sio huku, hakuna anayeweza huku, hata mmoja akisubutu basi atakufa vibaya mnoo."

"Duuh!!.. Sasa mtabiri watu wenyewe waduniani tunawazidi nguvu watawezaje sasa kutatua hili tatzo wakati sisi wenyewe hatuwezi." aliuliza surha.
"Maono yangu na miungu ndio inasema hivyo hakuna mtu wa huku anayeweza tofauti na watu waduniani."
"Sasa hao watu watakuja lini sasa, wakichelewa tukauwawa?"
"Haijulikani watakuja lini ila miungu wa huku itawaleta tu na sio kila mtu anayeishi duniani anaiweza hii kazi hapana ni watu maalum waliochaguliwa"
"Ni wangapi wataokuja."
"Ni kwaanzia wawili hakuna idadi kamili ila naona wanaanzia wawili ndo wanataifanya hii kazi."
"Sawa mtabiri sasa wakija wenyewe ndo wanaweza kulibeba hili bom nakwenda kulitupa mbali sindio?.."
"Hapana sio hivyo hata wenyewe kulibeba hili jiwe hawawezi ila kazi yao kubwa itakuwa ni kwenda kule kwenye ile falme wakaiibe ile remote wailete huku ndo tuizime kabisa yani tuiharibu au wazimie hata kule kule tu inawezekana."
"Kwahyo tutasubiri mpaka lini sasa wakati we umesema anataka nijiuzuru haraka bila hivyo anatulipua, kwanini nisitume vijana waende wakaiibe we utuambie tu ameificha sehem Gani."

"Nyie naona hamnielewi sikieni kwa makini niwaambie, watu ambao wamechaguliwa siku zote huwaga wanabahati hawawezi kufa kama wamechaguliwa kuwa watatuzi wa tatizo hilo yani kama starling wa mchezo, hata sehem ambayo unafikiri atashindwa lakini anaweza akafauru, tofauti na watu ambao hawajachaguliwa, kama sasa hatuaminiani basi wapelekeni hao watu wenu muone kitacho wakuta, Remote iko kwenye chumba cha mfalme Goru upande wa kabati kwenye huo mji wa TroFi, Msiseme sikuwaambia wapelekeni hao watu wenu mi naondoka naenda kufata dawa mpakani kule. Halafu mmeangalia tu ile zawadi aliyoileta yule mgeni ila hamjaangalia vizuri pembeni kuna ujumbe bado hamjausoma nendeni mkaangalie vizuri kwenye lile sanduku" alisema hivyo mtabiri gurhi kisha akaondoka, baba alikimbia ndani kuangalia vizuri aone ni nini alichokuwa anasemea mtabiri wa mji wetu wa Jozi, na sisi tulikuwa nyuma tunamfata tukafika pale tulipokuwa tumekaa baba akasogea hadi kwenye lile sanduku akaliinamisha chini kakaonekana kakaratasi kadogo kakiwa kamejibana pembeni ya lile sanduku, akakatoa Kisha akakakunjuruwa kisha akaanza kusoma kwa sauti.

"Pokea zawadi yangu na pia ukaangalie zawadi nyingine nje kwenye bustani, zote hizo kwaajili yako naimani umeelewa namaanisha nini, kama usipojiuzuru basi mji wako wote na watu wako pamoja na wewe pia mtakuwa majivu tu, kwaheri rafiki. By Mfalme Goru" ile barua ilisomeka hivyo, wote tulisikia kila mtu alibaha tulishindwa tufanye nini maana hatukujua hao watu wanaotoka duniani wanakuja lini, na kuachia madaraka ilikuwa ni jambo kubwa sana kulifanya baba kila alipowaza kuachia madaraka roho ilikataa, alikumbuka kipindi kile wazazi wao ndo wafalme walikuwa maadui sana waligombania maswala ya mipaka, walikuwa maadui hadi pale walipo fariki ndo hali ikatulia, mfalme tarhi hakutaka zile bifu ziendelee siku zote aliitisha mazungumzo ya amani ila goru alikuwa anakubali kishingo upande tu alikuwa na mpango kabambe wakuendeleza alipoishia baba ake yani mzee wake mpango wake mkuu ulikuwa nikuumiliki mji huu wa jozi ili uwe wake na mtoto wake ndo mpango aliouendeleza.

Baba yangu mfalme alitoka kwenye mawazo Yale, alibaha sana hakutaka kusubiri hadi hao watu wakutoka duniani waje alituma vijana anaowaamini wanaosifika kwa wizi wizi mtaani akawaongezea na nguvu za kimiujiza wakaenda kule kuiiba ile remote ila wakiwa mpakani tu ili waingie kwenye huo mji wa trofi wakakamatwa nakuuwawa. Akatuma wengine tena na wao wakauwawa, Akaona bora tu ajiuzuru amuachie madaraka mfalme goru ili watu wake wasiteketee....ITAENDELEA....

RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu ya 19

TULIPOISHIA...
Akatuma wengine tena na wao wakauwawa, Akaona bora tu ajiuzuru amuachie madaraka mfalme goru ili watu wake wasiteketee....

SONGA NAYO...
Ni jambo ambalo lilipingwa sana na mama pamoja na watu wote tulilipinga kabisa, baada ya kumshauri aache kujiuzuru ndo akakubali japo alikuwa na wasi wasi sana, imepita wiki sasa toka yule mgeni aje hapa." alimaliza kuelezea Sarha.

"Ooh sawa tumekuelewa, kwhyo sisi ndio tumechaguliwa tukaichukue hiyo remote?.."
"Hatuna uhakika asilimia mia ila tunahisi ni nyie maana hakuna watu wengine waliokuja kutoka duniani tofauti na nyie."
"Sawa sasa kama mlikuwa mnajua kama sisi ndio mkombozi wenu mbona mlikuwa humtujali?.."
"Sio kwamba hatuwajali ila Tulitaka mjitambue mmekuja kufanya Nini."
"Tupeni maelekezo tunafanyaje" aliuliza baba.
"Kwanza kipindi tunaingia kwenye hichi chumba niliwazimisha ili tuwawekee nguvu na sasa hivi mnanguvu kubwa sana mwilini mwenu kuzidi hata za kwangu kikubwa kwanza mnatakiwa kuelezwa jinsi yakuzitumia hizo nguvu mkishaelewa mtaenda sasa kuifanya kazi na kama nilivyo wahadithia, hiyo falme iko jirani tu sisi tutawapeleka hadi mpakani kazi itabaki kwenu mtafikaje fikaje hadi muichukie hiyo remote ni nyie ndo mtajua."

"Duuuh!!.. Mbona kazi ngum sasa yani mnatuachia twende peke yetu mnataka tuuwawe?.."
"Hapana hamuwezi kuuwawa nyie ndio mmechaguliwa kwhyo lazima mkutane na bahati nyingi kuna wakati mtaponea chupu chupu ila kufa hamuwezi kufa"
"Unauhakika gani kama ndio sisi?"
"Sasa huku mmekuja kufanya nini kama sio nyie?.."
"Sisi tulikuwa na majanga yetu tu ndomana tukazama kwenye maji ila sio kwamba tulikuwa tunakuja huku hapana.."
"Mkubali mkatae ila ukweli ndo huo nyie mlikuwa mnakuja huku sema tuliwahi kuwapokea tu." alisema surha.

"Mmh!!.. Sawa tufundisheni jinsi yakuzitumia hizi nguvu twende tukajaribu bahati, halafu kwanza hivi tukiileta hiyo remote mtatupa Nini?"
"Hilo sio swali la kuuliza mnaona nyumba yetu tu ilivyojaa madhahabu?"
"Ndio tunaona"
"Basi tutawapa dhahabu nyingi muende kuuza duniani, mtakuwa matajiri wakubwa sana huko."
"Kumbe!!.. Sawa tuko tayari kuifanya kazi yenu." alijibu baba. Kisha wakaanza kuwaelekeza jinsi yakuzitumia zile nguvu hadi walipo elewa elewa.

"Sasa mshaelewa twendeni sasa mkaianze kazi, mipango yote jinsi yakuingia mpakani mpaka kwenye jumba la kifalme ni juu yenu mnatakiwa mtumie akili sana." alisema sarha.
"Sawa tumekuelewa" walijibu wote baba na mama. Wakiwa nje ya jumba la kifalme wakijiandaa kwenda mara vikaonekana viumbe kama dragon vikitua pale karibu Yao, hawakuwa dragon ila walifanana nao sana walikuwa wawili halafu walikuwa na mabawa makubwa.

"Pandeni huyo na sisi tumpande huyu." alisema sarha Kisha wakaanza kuwapanda walipokaa sawa vile viumbe vikaanza kuondoka vikapaa juu kabisa, viliwapeleka hadi karibu na mpaka vikashuka chini, Wakashuka wote.
"Njia ndo hii yakwenda hadi mpakani, tumeshukia huku mbali kidogo ili tusionekani" alisema sarha.
"Sawa tumekuelewa acha sisi twende." alisema mama.
"Sawa muwe na kazi njema sisi tunarudi" alisema Sarha akipanda juu ya kile kiumbe na mdogo wake pia akimpanda yule mwingine wakaanza kuondoka kurudi kwenye kasri ya kifalme.
"Poa" alijibu baba, kisha wakaanza kuzipiga hatua zakuelekea mpakani, Walitembea mpaka wakaona kambi Moja nje kukiwa na askari wengi wakiwa wameshika mikuki, wakasogea hadi pale karibu. Mara wakazungukwa na wale askari wengine walitokezea kimiujiza haikujulikana wametokea wapi, Wakawa wengi wakazidi kuwasogelea mkuu wao akauliza.

"Nyie ni wakina nani? Mmetokea wapi na mnaenda wapi?"
"Jamani hamuoni hata aibu yani sisi tuko watu wawili tu nyie mko zaidi ya hamsini kweli?.." alisema baba.
"Jibuni swali letu kwanza kabla hatujawageuza chakula sasa hivi."
"Ok sawa mi naitwa raju na huyu hapa ni mke wangu anaitwa ruhii, sisi ni watabiri wa mambo yajayo Tumetoka masafa ya mbali tunapita kila mji tunatoa utabiri wa maisha yao ya mbeleni kisha tunaondoka tunaenda mji mwingine hivyo hivyo." alisema baba.
Askari mmoja akamvuta mwenzake pembeni kisha wakaanza kuteta jambo.
"Hivi toka yule mtabiri afariki mfalme ameshapata mtabiri mwingine?"
"Hapana bado hajampata na anamtafuta sana na anasemaga mambo yake hayaendi sababu hana mtabiri."
"Basi tuwapelekee hawa, nahisi watamsaidia Sana we unaonaje?"
"Ni jambo jema ila subiri kwanza twende tukawaulize kitu."
"Kitu gani unataka kuwauliza?.."
"Usijali we njoo utasikia." mwenzake hakubisha wakarudi hadi pale waliposimama.

"Nyie mmesema ni watabiri sindio?."
"Ndio sisi watabiri tena uwezo wetu ni mkubwa sana."
"Sawa naomba unitabirie Mimi maisha yangu ya mbeleni."
"Sawa leta mkono wako" yule mlinzi wa mpakani akasogeza mkono kisha baba akamshika.
"Wewe inaonekana mfalme atakupandisha cheo utakuwa mtu mkubwa kwenye jumba la kifalme."
"Waoooh!!.. Asanteni sana nimefurahi kusikia hivyo." alisema yule jamaa akiamini kweli wale ni watabiri wazuri watu sasa wakaanza kuomba waangaliwe na wenyewe.
"Na mimi niangalie"
"Na mimi hukuuu"
"Nimenyosha mkono nioneni hukuu." Ikawa tafrani kila mtu akataka kuangaliwa.

"Jamani hatuwezi kuwamaliza wote hawa, naombeni waje viongozi wenu tu tuwaangalie." alisema baba kisha wakasogea viongozi watatu.
Wakaanza kuwaangalia
"Wewe ni kama yule mwenzako ndo mtakuwa mawaziri wa badae kwenye jumba la kifalme"
"Weweeeeee!!... Kweli mtabiri?.."
"Kweli niamini mimi." alisema baba, alifurahi sana yule msaidizi wa mwisho. Akaja mwingine.
"Wewe naona mwisho wako utakuwa mbaya utasingiziwa kitu halafu utauwawa"
"Hahahaa hahahaa kumbe atauwawa." watu walianza kuamcheka.
"Nasema wote nyamanzeni kimya mnajua mi ndio kiongozi wenu hapa halafu mnanicheka mnamaanisha Nini? Halafu hawa sio watabiri ni feki TU."
"Hapana sisi sio feki namaanisha nachosema yani wewe pamoja na huyo msaidizi wako mtasingiziwa kosa ambalo hamjalifanya halafu mtauwawa." wale viongozi hawakutaka kuelewa wale askari wenzake wakasikika wakisema.
"Hawa ni watabiri wakweli nyie kwasababu mmeambiwa ukweli ndomana hamtaki kukubali." wale askari wengine waliwaandama viongozi wao hadi ikabidi tu wawe Wapole.

"Hawa tuwapeleke kwa mfalme watamsaidia sana" walisikika askari baadhi wakisema hivyo, na wengine wakajibu.
"Ndiooooo" basi bila kupoteza mda walinzi wawili wakaenda kuchukua farasi kadhaa ndani ya kambi Yao Kisha wakawapa moja na askari wale wawili waliovutana pembeni kuteta jambo, wakapanda kwenye farasi zile zingine wakaongoza njia wakaanza kuwapeleka kwenye jumba la kifalme kulikuwa na umbali sana baada ya mda mrefu walifika. Wale askari walikuwa wanafahamika vizuri tu hawakuulizwa maswali yoyote Waliingia ndani ya jumba lile kubwa moja kwa moja wakawapeleka hadi kwa mfalme, mfalme akiwa amekaa kwenye kiti chake cha kifalme alishangaa kuona maaskari wake wa mpakani wamekuja na watu pale akawauliza.

"Vipi kuna tatzo huko mpakani kuna watu wamevamia Tena au?"
"Hapana mtukufu mfalme, hawa ni watabiri wenye uwezo mkubwa sana wanasema wanapitaga kila falme kutoa utabiri wa maendeleo yao ya mbeleni, halafu tulipokumbuka kuwa unamtafuta mtabiri tukaona sio mbaya tukikuletea Hawa."
"Mnauhakika hawa ni watabiri kweli?.."
"Mtukufu mfalme ndio niwatabiri kweli sisi wenyewe tulikuwa na wasi wasi nao ila baada yakutabiria mambo yetu ya mbeleni ndo tukawaamini wako vizuri sana wana uwezo mkubwa mnoo." alisema askari mmoja.

"Mmmh!!.. Hawa kweli ni watabiri?.. Sina Imani nao, mbona kama sio watu wa dunia yetu hii ya chini ya bahari?.." alisema mfalme goru akiinuka kwenye kiti chake cha kifalme, akaanza kuwasogelea baba na mama huku akiwa ameikunja sura yake mbaya na inayotisha, baba na mama wakaanza kurudi nyuma.....ITAENDELEA....RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu Ya 20

TULIPOISHIA..
"Mmmh!!.. Hawa kweli ni watabiri sina Imani nao, mbona kama sio watu wa dunia yetu hii ya chini ya bahari.." alisema mfalme goru akiinuka kwenye kiti chake cha kifalme, akaanza kuwasogelea baba na mama huku akiwa ameikunja sura yake mbaya na inayotisha, baba na mama wakaanza kurudi nyuma.....

SONGA NAYO....
"Sisi ni watu wakutoka mji wa Rosha ndomana unatuona tuko hivi." alisema baba
"Oooh!!..hapo sawa, nilitaka nishangae inakuaje mnakuwa na rangi mbili tofauti, huyu muarabu halafu wewe muafrika, hapo nimeelewa naomba mnitabirie kuhusu mji wa jozi mfalme wao kweli atajiuzuru?. Na mji ule utakuwa chini yangu?.." alisema mfalme goru, baba akamwambia.
"Leta mkono wako wakulia tuone." mfalme akampa mkono baba akaushika Kisha akaubonyeza bonyeza halafu akasema.

"Hapa naona mfalme wa jozi atajiuzuru halafu miji yote miwili itakuwa chini ya kiongozi wa mji huu, yani mji wa jozi na huu mji wa trofi utabaki kwenye miriki ya kiongozi wa hapa." alisema baba.
"Kweli mtabiri??.."
"Kweli mtakufu mfalme."
"Hahahaha.. Umenifurahisha sana, halafu naomba na huyu mwenzako anitabirie kuhusu ugonjwa huu unao nisumbua nitapona au nitakufa?.."
"Leta mkono mfalme" alisema mama, mfalme akatekeleza ombi lile akampa mkono mama.
"Mmmh!!.. Huu ugonjwa ni hatari sana lakini utapona hautokufa na watao kuponyesha ni sisi wenyewe.."

"Heeeeh!!.. Unajua siamini? Nyie ndio mtaniponesha?.."
"Ndio mtukufu mfalme."
"Wamesha jaribu kunitibu waganga na waganga lakini wote wameshindwa, mnanishangaza mnaposema nyie ndio mtanitibu."
"Kikubwa weka imani tuamini utapona."
"Hebu kaeni hapo mniambie vizuri" alisema mfalme huku na yeye akikaa kwenye kiti chake cha kifalme, Wale walinzi walio waleta baba na mama wakaaga wanaondoka wakarudi kule mpakani, Mama na baba wakakaa wakaanza kuongea.

"Huo ugonjwa kwetu ni mdogo sana ni kama kunywa maji tu, tutakupa dawa utatumia baada ya siku kadhaa utapona"
"Mnauhakika na mnachokisema?.."
"Ndio mtukufu mfalme tunauhakika asilimia mia."
"Haya nipeni hiyo dawa nitumie maana huu ugonjwa umenisumbua sana nashindwa kuelewa umetokea wapi maana huku hamna ugonjwa kama huu, na nawa ahidi kama nikipona tawapa zawadi nzuri sana."
"Kupona ni uhakika mfalme, agiza maji ya moto nikuwekee dawa unywe sasa hivi."
"Sawa" alisema mfalme kisha akapaza sauti kuita kijakazi mmoja aje, akaja mmoja akafika anapiga magoti karibu na mfalme.
"Nenda kachemshe maji, yakichemka kabisa weka kwenye glass unieletee."
"Sawa mtukufu mfalme" aliitikia yule kijakazi kisha akainuka akaelekea jikoni kuchemsha maji.

"Karibuni sana jisikieni mko huru, mnatumia kinywaji gani?.."
"Hapana mfalme tuko sawa hatuhitaji kinywaji chochote."
"Nimewaambia kuweni huru jiachieni, Semeni tu msiwe na wasi wasi kila kinywaji mnacho kijua kipo ni nyie tu mnataka kipi."
"Basi chochote tu utacho sema tutatumia."
"Sawa ngoja niite kijakazi mmoja akawachukulie kinywaji cha biriso maana ndo kinywaji nacho kipendaga Mimi." akaita kijakazi mwingine akamuagiza hicho kinywaji.
"Mtukufu mfalme hicho kinywaji ndo kinywaji Gani?.."
"Mmmh!!.. Acheni kunishangaza inamaana hamkijui?.."
"Ndio hatukijui wala hatujawahi kukisikia." alisema baba.

"Mmh!!.. Mnanipa mashaka, mbona hicho kinywaji kinategenezwa kwenye mji wenu wa rosha na ndio kinywaji kikubwa kwenu huko inakuaje nyie hamkijui?.."
"Sisi ni wazaliwa wa rosha ila hatujakulia huko tumekulia kwenye mji wa hasifu ndomana hatukijui hicho kinywaji"
"Oooh!!.. Hapo nimewaelewa." alisema mfalme baada ya mda kidogo kinywaji kikaletwa yule kijakazi akafika anawapa glass kisha akawamiminia, chupa akaiweka pale mezani halafu akaondoka. Wakiwa wanataka kunywa kinywaji kile, mara ghafla mfalme akaanza kutetemeka pale alipokuwa amekaa kila sekunde zilivyokuwa zinazidi kwenda ndo hali yake ilivyokuwa inazidi kuwa mbaya alikuwa anatetemeka zaidi ya jenereta, akadondoka chini akaanza kugalagala.

Baba na mama walishangaa hali ile, walinzi wawili wa mfalme waliokuwa wamesimama nyuma ya kiti chake wakasogea wakamshika wakamnyanyua juu ili wampeleke chumbani, mara yale maji ya moto yakaletwa yakiwa kwenye glass, Mama akaipokea ile glass kisha akatoa kamfuko kadogo kadawa akakafungua akaimimina dawa ile kwenye yale maji kisha akaitikisa tikisa ile glass ili dawa ijichanganye vizuri. Wale walinzi walikuwa wameshamnyanyua wakaanza kuzipiga hatua za kumpeleka chumbani kwake, Mama akawastopisha.
"Msimpeleke huko mleteni nimpe dawa yakumponyesha." wale walinzi wakamrudisha wakamkalisha kwenye kiti chake, mama akampa baba ile glass ili akamnyweshe mfalme. Baba akatekeleza agizo lile akaipokea Kisha akainuka akasogea hadi alipo kalishwa mfalme akiwa ameshikiliwa na wale walinzi.

"Muasamisheni nimnyweshe hii dawa." wale walinzi wakamuasamisha, baba akamnywesha ile dawa pole pole ikiwa vile vile ya moto hadi ikaisha yote.
"Muacheni sasa atakuwa sawa tu mda si mrefu." alisema baba akirudi kwenye kiti alichokuwa amekaa. Mama akasogeza mdomo kwenye sikio la baba akamnongoneza.
"Vipi unauhakika mpango huu utaenda sawa?."
"Ndio na naimani nao" alijibu baba, mama akatikisa kichwa kuashiria kukubali. Baada ya dakika kadhaa hali ya mfalme ikatengemaa akakaa vizuri baada yakupata pata nguvu.
"Nashukuruni sana, hii hali inanisumbuaga mara kwa mara na bila ile dawa yenu ningehangaika vile ndani ya lisaa lizima, kila baada ya siku mbili lazima initokee hali hii nawashukuru sana tena sana na shukrani zangu hazijaishia hapa na zawadi nyingi sana kwaajili yenu na kama nikipona kabisa ndo zitaongezeka mara dufu." alisema mfalme.

"Mfalme naimani utatuamini mdogo mdogo, sisi sio watabiri feki kama ulivyokuwa unatuhisi mwanzo."
"Naombeni mnisamee sana maana nilifikiri na nyie ndo kama wale wale waliokuwa wanakuja wanajitapa kwamba ni waganga kweli halafu wanashindwa kunitibu, Na nilipokuwa naelekea ni pabaya sana maana nakumbuka miaka ya nyuma ilikuwa inaweza kupita hata mwezi bila kunitokea hali hiyo ila kila miaka inavyozidi kusogea ndo hali inazidi, Kutoka kwenye mwezi zikaja wiki tatu zikasogea zikawa wiki mbili, wiki Moja hadi sasa hivi hazipiti siku mbili bila kunitokea hali hiyo.

"Pole sana mtukufu mfalme, amini kwaanzia leo umepona kabisa."
"Tazidi kuwashukuru sana kama ikiwa hivyo na taomba kabisa muwe watabiri wa mji wangu huu mtaishi maisha mazuri sana na tawapa kila mtacho kihitaji, Naomba niwaulize swali kwanza nyie ni wapenzi?.."
"Ndio mtukufu mfalme sisi ni wapenzi.."
"Ohooh! vizuri sana mmechanganya rangi, na ndo sifa ya mji wenu wa rosha unatoa rangi tofauti tofauti kuna wa blue, kuna wa njano kuna weusi, weupe, kila rangi kule ipo. Mmependezena." alisema mfalme goru.
"Asante mtukufu mfalme ila kuna jambo umeliongea la kuhusu kuwa watabiri wa mji huu, Hapana sisi hatukaagi sana kwenye mji mmoja tumeumbwa kusaidia watu tukitoka hapa tunaenda kwenye mji mwingine ndo tumezoea hivyo na ndo kazi yetu."

"Kila kitu kina mwanzo wake na mwisho wake huu ndo mwisho wa nyie kutembea tembea nataka mtulie hapa mi tawapa kitu chochote mnacho kihitaji imladi tu mbaki hapa."
"Unauhakika mfalme tukitaka kitu chochote kile utatupa?.."
"Ndio chochote kasoro roho yangu na ufalme tu, hayo mengine yote mnaweza kuomba na tawapa nimeona nyie ni watu wa muhim mtatusaidia sana kwenye matatizo mengi yatayo tokea."
"Naona kama hilo jambo litakuwa gumuu!!. Ila tumeongeza siku za kukaa hapa tutakaa wiki moja huku tukilifikiria ombi lako, kabla ya hiyo wiki kuisha tutakuwa tushakupa jibu kama tutaendelea kukaa hapa hapa au tutaondoka, na kama tukibaki basi unatakiwa utekeleze ombi ambalo tutakuomba.." alisema baba....ITAENDELEA...
 
Agizo la majini 21-25

RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu ya 21

TULIPOISHIA..
Naona kama hilo jambo litakuwa gumuu!!. Ila tumeongeza siku za kukaa hapa tutakaa wiki moja huku tukilifikiria ombi lako, kabla ya hiyo wiki kuisha tutakuwa tushakupa jibu kama tutaendelea kukaa hapa hapa au tutaondoka, na kama tukibaki basi unatakiwa utekeleze ombi ambalo tutakuomba.." alisema baba...

SONGA NAYO...
"Bila shaka" alijibu mfalme kisha akaita kijakazi mmoja akamuagiza awaletee chakula, baada ya mda kidogo chakula kikaletwa wakala walipo maliza wakapelekwa sehemu ya kupumzika kwakuwa walisema ni wapenzi mfalme aliagiza wapewe chumba kimoja wakae wote, agizo likatekelezwa.

"Vipi adel mpenzi wangu unajua sielewi hiyo miji ya huku we umeijuaje?."
"Mmh!!.. Mi mwenyewe sijui naona kila nachokitaja kinakuwa sahihi nahisi ni zile nguvu tulizo pewa kule ndo zinafanya kazi."
"Mmh!!. nambie tunafanyaje mfalme amesema chochote tutacho muomba atatupa unaonaje tumuombe ile remote au?.."
"Mmh!!.. Hapana hata mi aliposema vile nilipata wazo hilo hilo ila nikakumbuka kitu kwenye maongezi yake alisema tusiombe roho yake pamoja na ufalme, inamaanisha hiyo remote anaitumia ili aupate ufalme wa mji jozi. Kwahyo ni kitu ambacho hawezi kutupa zaidi na zaidi atatugeukia na maswali yatakuwa mengi atahisi sisi tumetumwa na lazima atatukamata nakutuuwa, sisi tuendelee na mpango wetu tu naona asilimia kubwa za kufanikiwa." alisema baba na mama akaliunga mkono lile wazo.

"vipi katoto kangu kanasemaje huko tumboni?"
"Mmh!!.. Jamani ndo kwanza mwezi mmoja, bado sana"
"Mmh!!.. Hivi ni mwezi mmoja kweli?.."
"Hata mwezi wenyewe bado haujafika nahisi itakuwa zimebaki siku chache tu ndo ufike mwezi"
"Mmh!!.. Sawa bhan twende tukaoge" waliinuka wakaenda kuoga, siku hiyo ikapita ikaingia siku nyingine.

"Mtukufu mfalme!!.. Kuna tatzo kule nje walinzi pamoja na maaskari wamekutwa wamedondoka chini wamelala hawajielewi" alikuwa ni kijakazi wa ndani ndo alikuwa anatoa maelezo hayo akimwambia mfalme.
"Unasemaaa??... Wamelala hawajielewi kwani unaona wamepigwa sehem?.."
"Hapana mtukufu mfalme hawajapigwa twende ukaona mwenyewe."
Mfalme akazipiga hatua kumfata yule kijakazi huku walinzi wake wawili wakiwa wanamfata nyuma.

"Wale pale wamelala"
"Heeeh kimewakuta nini Tena?.." alisema akasogea hadi pale wale walinzi walipolala akawa anawatikisa tikisa ila hawakuamka walionekana kama vile wamezimia.
"Na upande wa kule wamelala askari" alisema yule kijakazi huku akizipiga hatua zakuelekea kule aliponesha kwa mkono, na mfalme akamfata, mfalme alishtuka baada yakuona askari karibu mia wakiwa wamelala chini. akaamrisha mlinzi wake mmoja asogee awachunguze aone kimewakuta Nini, yule mlinzi akasogea akamuinua mmoja Kisha akampima mapigo yake ya moyo, yalikuwa sawa alihema kama kawaida ila alionekana hana nguvu kabisa, akarudi hadi aliposimama mfalme akasema.
"Mtukufu mfalme inaonekana wako sawa mapigo ya moyo yanadunda kama kawaida ila nguvu ndo hawana sijui inasababishwa na Nini"
"Nenda kule kwenye kile chumba walicholala wale watabiri ukawaite waje."
"Sawa mtukufu mfalme." alisema yule mlinzi kisha akazipiga hatua za kuingia ndani ya jengo lile la kifame.

Baba na mama walikuwa chumbani wanapanga mipango yao, walikuwa wanataka kazi waimalize hiyo hiyo siku. Mara mlango ukasikika unagongwa baba akasogea hadi mlangoni akaufungua.
"Mfalme anawaita kuna tatzo huko nje limetokea." alisema yule mlinzi wa mfalme.
"Sawa tunakuja sasa hivi" alijibu baba Kisha akamwambia na mama alichoambiwa wakatoka nje.

"Afadhali mmekuja naomba mtuangalizie hawa wamepatwa na Nini" alisema mfalme akiwaambia baba na mama baada yakufika pale. Baba akasogea hadi walipolala wale askari akainama chini akamshika mmoja mkono akamuangalia kisha akainuka akasema.
"Hawa watu wamevuta hewa yenye sumu mbaya sana na inaonekana ni sumu ya mashetani, mfalme watu wako wenyewe wanakusariti."
"Watu wangu?.. Watu Gani?" aliuliza mfalme.
"Sogea huku pembeni tuongee" wakasogea sehem wakaanza kuongea.
"Hii sumu sio ya kawaida na huku haipo sumu kama hii, kati ya mashetani wako wakukulinda wanakusariti"
"Mmmh!!.. Yupi huyo?."
"Yule shetani ambae yuko kwenye chumba chako unayemfanya mlinzi wa kile chumba ndo amewapulizia ile sumu hao maaskari anataka auwe vikosi vyako vyote ili ubakie hauna nguvu akuangamize na wewe pia sio mtu mzuri hata kidogo na umemuamini kwa mda mrefu na yule ndo aliyekupa huo ugonjwa ambao tumeuponyesha." alisema baba.

"Unasemaaa??.. Hapana haiwezi kuwa kweli ni mlinzi wangu ambae namuamini sana."
"Kama hautaki kuniamini sawa ila ndo ukweli huo na sasa hivi ametoka kidogo ameenda kwenye mji wao wa mashetani kuongeza nguvu ili arudi akuangamize kabisa."
"Heeeh!!.. Unauhakika na unachosema??.."
"Nauhakika asilimia mia, hivi ukiamkaga siunajihisigi mwili kuchoka choka sana na kujihisi vibaya vibaya?.."
"Ndio huwaga nahisi hivyo naa.." akakatishwa
"hakuna cha naa, yeye ndo anakufanyiaga hivyo we umemuweka awe mlinzi wa jumba hili zima ila asionekane kwa macho ya kawaida umuone wewe tu, hiyo nafasi ndo anaitumia kufanya mambo yake na huo ugonjwa uliokuwa nao ulikuwa unaongezeka kila siku we unahisi nani alikuwa anauongeza kasi?.."
"Sijui" alijibu mfalme.
"Yeye ndo alikuwa anauongeza kasi ili ufe mapema, akawaite mashetani wenzake waje waishi kwenye huu mji na wale mashetani wote unao watumia kwenye mambo yako sio watu wazuri kwako wanataka ufanikishe kumfanya mfalme wa jozi ajiuzuru halafu wakugeuke watawale wao sehemu zote hapa kwenye huu mji na mji wa jozi."

Mfalme alihisi kichwa kinawaka moto yale maneno aliyokuwa anaambiwa yalikuwa yanauchanganya ubongo wake maana yeye alikuwa anajua wale mashetani anaoshirikiana nao wako upande wake kumbe wanataka afanikishe jambo lao wamuangamize. alijikuna kichwa alihisi kina washa, baba akasema.
"Nikuibie siri nyingine?.."
"Eeh!!..Ndio nambie" alisema mfalme akiwa hayuko sawa.
"Hivi unajua mtoto wako alipoenda?.."
"Ndio najua aliniaga kuwa anaenda mpakani kuangalia ulinzi kama uko imara"
"Mmh!! hapana hakwenda mpakani na sisi tulipitia pale pale mpakani lakini hatukumuona."
"Kwani nyie mnamjua mwanangu?"
"Hapana ila viongozi wote pale tuliwatabiria na hatukuona mtoto wa mfalme pale."

"Mmmh!!.. sasa atakuwa ameenda wapi?."
"Ameenda kwenye mji wa mashetani na mda si mrefu atarudi akiwa na nguvu kubwa Sana, Mtoto wako na yeye anatumiwa na wale mashetani kama wewe tu, wameona wewe unauchelewesha mpango wao ndomana wanataka wakuuwe, ufalme arithi mtoto wako afanikishe swala Zima la kuuteka mji wa jozi maana ndo mji mwenye thamani kubwa sana kwanza unamadhahabu kibao na vitu vingi vingi, ndomana wanautaka wale mashetani."

"Mmh!!.. Sasa mimi najiuliza swali nashindwa kuelewa kama mashetani wanautaka ule mji siwaende wavamie wenyewe tu siwananguvu nyingi tu zakuangamiza mji wote." alisema mfalme, baba akamjibu.
"Kwani wenyewe hawana akili, pamoja na nguvu zao zote hawawezi kuvamia mji ule bila kupanga mipango kama hiyo wanayokuambiaga maana wanajua kitacho wakuta."

"Duuh!!.. Sasa unanifungua ufaham taratibu"
"Nataka nikwambie siri nyingine."
"Niambie siri gani hiyo?.." alisema mfalme akionekana kama vile amebaha.
"Hata baba ako mfalme wa zamani wa mji huu, mashetani wenyewe ndo walimuuwa baada yakushindwa kukamilisha kazi Yao."
"Heeeeh!!. Unasema kweli?.."
"Ndo ukweli wenyewe huo."
"Duuh!!.. Sasa nimekuamini naomba unanishauri nifanyaje?"
"Chakufanya ni hivi kuna bom mashetani walikupa ili ukatege kwenye mji wa jozi nje ya jengo la kifalme sindio?.."
"Ndio niliagiza kijana akaliweke na kweli alifanikisha"
"Vizuri, siwalikupa na remote?"
"Ndio walinipa"
"Basi chakufanya nenda kaichukue ile remote kisha ubonyeze sehemu ya kuizima, lile bom kule life kabisa lisiweze kufanya kazi."
"Sawa ngoja niende nikaibonyeze" alisema mfalme akizipiga hatua za kuingia ndani....ITAENDELEA...RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu ya 22

TULIPOISHIA..
"Basi chakufanya nenda kaichukue ile remote kisha ubonyeze sehemu ya kuizima, lile bom kule life kabisa lisiweze kufanya kazi."
"Sawa ngoja niende nikaibonyeze" alisema mfalme akizipiga hatua za kuingia ndani....

SONGA NAYO..
"Subiri kwanza niwatibie hawa halafu twende wote" alisema baba akimwambia mfalme, mfalme akarudi kwanza. Baba akatoa dawa kwenye mfuko wa nguo yake kisha akaifungua akaanza kuwanyunyuzia wale askari wote wakaamka.

"Sasa tunaweza kwenda" alisema baba akimshika mkono mama wakazipiga hatua zakumfata mfalme anapoelekea.
"Daaah!!.. Shukrani sana kweli nyie ni watabiri wa kweli sasa nawaamini asilimia mia." alisema mfalme.
"Usijali sisi tuko kwaajili yakusaidia watu wasio na hatia." alijibu baba huku wakizidi kuzipiga hatua hadi wakafika kwenye mlango wa chumba cha mfalme.
"Subirini hapa niingie nikaichukue." alisema mfalme goru akaingia ndani, baada ya sekunde kadhaa akarudi.

"Hii yapa ile remote"
"Sawa, ibonyeze sasa hapo sehemu ya kuizima kabisa." mfalme hakubisha alikuwa ameshashikwa akili na baba alimuamini ghafla bila yeye mwenyewe kujielewa, Akabonyeza ile sehemu.
"Sasa hapo tayari bom lile limeshaharibika haliwezi kufanya kazi Tena, na tena acha kabisa kutumika wanakufanya chambo."
"Sawa nimekuelewa mtabiri." alisema mfalme akiwa mpole, ukali wake wote uliisha sura aliyokuwa anaonesha hadi wale walinzi wake walikuwa wanamshangaa maana walizoea kumuona kwenye sura ya ukali kila wakati ila toka waje wale watabiri alikuwa mpole sana tena mnyenyekevu kila walichosema watabiri wale yeye aritii, walimuogopa na walimtii sana hawakuweza kumuuliza chochote waliganda kama sanam tu.

Baba akamshika mkono mama akaenda nae hadi chumbani.
"We! adel wewe!!.. Umefanya nini hadi ametoa remote kirahisi hivyo nakulizima lile bom?"
"Nimeenda kinyume kidogo na mpango wetu ila tumefanikisha ule mpango tungechelewa sana ila huu umewahi Sana, Baada yakuwapulizia sumu wale askari nikamsogeza pembeni mfalme nikamjaza uongo na kweli, kwamba ile sumu walio puliza ni mashetani wake wanamsariti wanataka wamuuwe wamemfanya chambo kwamba hata ule ugonjwa wenyewe wamempa ili afe taratibu, Nimeupanga uongo unao endana na ukweli hadi ameniamini."
"Duuh!!.. Adel we kiboko"
"Mmh!!.. Mi sio kiboko bhan bora hata ungeniita mnyama duma hiviii!!.."
"Hahahaaaa!!.." wakacheka pamoja huku wakipigana mabusu.

"Ratiba inayofata ni ipi?.." aliuliza mama
"Nikuondoka TU" baba alijibu
"Tunaagaje Sasa?.."
"Tunasema Kuna dawa tunaenda kuichukua tutarudi mda si mrefu, halafu tunaenda mazima."
"Halafu tunatumia usafiri gani hadi kufika kule mpakani maana ni mbali."
"Hivi umesahau kama tunanguvu nyingi tu tuweza kutoweka hata kimiujiza ila tutaanza kutembea kwanza na tukifika pale mpakani tutatembea Tena kawaida maana wale walinzi wananguvu pia wanaweza kutuona wakahisi tumefanya jambo baya halafu tunatoroka."
"Ooh!!.. sawa nimekuelewa halafu nilikuwa nimeshasahau kama ninanguvu za kutoweka."
"Hata za kupigana tunazo tena wale walinzi wote tunaweza kuwapiga nakuwauwa ila inatakiwa tutoke kwa amani tusifanye vurugu yoyote tutumie akili tu."
"Sawa mpenzi wangu nimekuelewa."
"Inuka sasa twende" alisema baba kisha wakafungua mlango wakaanza kuzipiga hatua zakutoka nje, wakafika nje wakamkuta mfalme akiongea na maaskari wake.

"Vipi tena mnaenda wapi mbona kama mmekaa kisafari safari"
"Hahaha!! Hapana mfalme nguo tulizo kuja nazo sindio hizi hizi unasemaje tumekaa kisafari"
"jinsi mlivyo tu mnaonekana kama vile kuna sehemu mnataka kwenda"
"Kweli mfalme kuna sehemu tunaenda ila tutarudi mda si mrefu, tunaenda kuchukua dawa moja hivi ni kiboko inatibu ugonjwa wowote unao ujua wewe naimani itawasaidia sana, wewe pamoja na wananchi wako kama mkipata tatizo"
"Ooh!!.. Sawa lakini mngeenda na walinzi wakuwalinda"
"Hapana sisi wenyewe ni moto wakuotea mbali hakuna ambae anaweza kutugusa."
"Sawa lakini sio vye..." mfalme alikatishwa kumalizia neno lake na upepo mkali uliopita pale, punde si punde wakatokea mashetani watano wa sita alikuwa ni mtoto wa mfalme Goru, kikasikika kicheko.

"Hahahaaaa!!.. Hahahaaaa!!... Umejua mipango yetu et eeeh!!.." ilisikika sauti ya mkuu wa wale mashetani waliofika pale ikisema.
"Mi nimejua mpango wenu upi?.." aliuliza mfalme akijifanya haelewi chochote.
"Hawa kenge siwamekwambia mpango wetu wakukuuwa"
"Heeeeh!!.." Baba na mama walishtuka, maana baba alijisemea tu hakujua kama ni kweli yeye alihisi anaongea uongo ili mfalme aingie mkenge aizime lile bom, kumbe ilikuwa ni kweli walikuwa wanampango wakumuuwa, walishangaa.

Mfalme akasikika akisema.
"Ndio nimejua mpango wenu na kwaanzia leo staki kushirikiana na nyie ondokeni hapa staki kuwaona"
"Hahahaha!!.. Umeshachelewa mwisho wako wakuishi umeshafika, maana umeenda kinyume na makubaliano yetu na bom umeshalitegua, sasa unategemea nini kama sio kifo tu tena mwanao ndio anakuangamiza" alisema mkuu yule akamwita mtoto wa mfalme mbele kisha akamuuliza.
"Siunataka uwe mfalme?.."
"Ndio nataka"
"Basi Chukua hichi kisu chenye sumu umuangamize baba ako" akakipokea Kisha akasogea hadi karibu na baba ake akakishika vizuri ili amchome nacho baba ake.
"Mwanangu usifanye hivyo hao sio watu wazuri watakugeuka na wewe pia" ila mwanae hakutaka kabisa kumsikiliza, akaurudisha nyuma mkono kwa nguvu akamkita baba ake mfalme goru, kisu kikadunda, wote walishtuka mfalme akiwa amejiziba usoni na mikono yake ili asishuhudie mtoto wake anavyomuangamiza, alishangaa kujihisi yuko sawa akaishusha mikono yake nakushika tumboni hakukuwa na tatzo lolote tumbo lilikuwa sawa.

Mtoto wake alikuwa ameduwaa, akajikakamua tena kwa nguvu akamchoma tena kwa mara ya pili kikadunda.
"Heeeeh!!.. kwani amekuwa jiwe??.." ilisikika sauti ya shetani mmoja ikiuliza.
"Hebu kamateni hao watabiri wenyewe ndo watakuwa wamefanya kitu" Mashetani watatu wakasogea wawakamate mama na baba, weeeee!!.. walichezea moto mwingine ile wanataka kuwashika tu walirushwa mbali wakadondoka kama magunia. Mkuu wao akashtuka
"Heeeh!!.. Nyie ndio mmewarusha watu wangu hivyoo?.."
"Ndio sisi njoo ujaribu na wewe kama unaweza." alisema baba, akasogea yule mkuu wao akarusha pigo moja baba akalikwepa upepo ukasikika ukilia tu akarudi nyuma kidogo akaikunja mikono yake halafu akaifunua ukatokea moto kwenye viganja vyake akaurusha kwenda Kwa mama, mama kwa kasi ya ajabu akaruka tikitaka ule moto ukapita chini. Yule shetani mwingine aliyebakia akataka kujitutumua na yeye akaenda kichwa kichwa akapigwa teke Moja takatifu na baba, ikamtoa nje ya geti kabisa akaenda kudondokea huko akafikia kichwa kikapasuka vipande vipande ubongo ukamwagika.

Mfalme na mwanae walikuwa wameduwaa tu wanashuhudia mpambano ule, yule mkuu wa mashetani akautunisha mwili wake, akawa limtu likubwa kama hulk. Watu waliokuwepo pale chini aliwaona kama sisimizi tu, akainyosha mikono yake mikubwa ili awakamate baba na mama, ila aligusa hewa akaunua mguu ili awakanyage, akakanyaga mkuki wenye sumu uliotegeshwa na baba. akadondoka chini huku akiugulia maumivu kwakulalamika, akauinua mguu wake akauchomoa ule mkuki akainuka tena akasimama kwakuchechemea.

Akiwa amesimama kirege rege akahisi miguu kama inazidi kuisha nguvu, kumbe baba na mama walikuwa wanamchoma choma miguuni wakutumia mikuki, hadi miguu yote ikajaa matobo tobo zikaanza kutiririka dam, akadondoka chini huku akipiga kelele, pale chini pote pakajaa dam zilikuwa zinatiririka kama vile mpira wakupitishia maji ya Bomba umekatika.

Yule mkuu wa mashetani akanyosha mikono juu kama anaomba kitu ukatokea moshi ukajaa kwenye mikono yake akaishusha akaishika miguu yake, yale matobo tobo yote yakajiziba. Baba na mama wakiwa wanashangaa shangaa wakapigwa pigo moja, wote wawili wakarushwa mbali....ITAENDELEA...

RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu ya 23

TULIPOISHIA...
Yule mkuu wa mashetani akanyosha mikono juu kama anaomba kitu ukatokea moshi ukajaa kwenye mikono yake akaishusha akaishika miguu yake, yale matobo tobo yote yakajiziba. Baba na mama wakiwa wanashangaa shangaa wakapigwa pigo moja, wote wawili wakarushwa mbali....

SONGA NAYO...
Wakadondoka kama mizigo ya viazi, mama akadondokea mgongo, baba akadondokea ubavu. Wote wakawa wanaugulia maumivu huku wakijishika sehem zinazo uma, wakajizoa zoa pale wakainuka wakashikana mikono wakainama chini kama vile wanasali mara kikatokea kimbunga chenye kasi ya ajabu kikaenda kuzunguka sehemu alipo yule mkuu wa mashetani, kikamchukua kikamuinua hadi juu ya fensi halafu kikamuachia akadondokea kwenye vyuma vilivyo chongoka pale juu vile vyuma vikamchoma vikatokezea nyuma kwenye mgongo, nafsi ikamsariti ikachomoka ikaondoka, ikawa ndo mwisho wa uhai wake.

"Nawashukrani sana watabiri wangu kwa msaada mlionipa" alisema mfalme, mwanae akamuangalia akamsonya kisha akazipiga hatua zakuingia ndani.
"Unanisonya baba ako?.. We hunijui vizuri et naomba isimamishe miguu yako hapo hapo hakuna kuingia ndani sina mtoto shetani kama wewe toka nenda ulipokuwa" alifoka mfalme, mwanae hakutaka kubisha alizipiga hatua za kurudi nyuma akaenda hadi getini akafungua mlango Kisha akaishiria zake.

"Usijali mfalme, sisi twende sasa tukachukue dawa" alisema baba
"Mkitoka wakaja wengine siwataniua?"
"Hapana hawawezi nimekuwekea kitu kwenye mwili wako wakikupiga inadunda wanaumia wao yani upo kama chuma."
"Mmh!!.. naomba msichelewe kurudi maana wale mashetani nawajua vizuri, wananguvu kubwa sana wale tu waliokuja ni cha mtoto wapo wakubwa wao hao ndio hatari."
"Hatuto chelewa" alisema baba huku wakizipiga hatua zakutoka nje, wakatoka Kisha wakaanza kuondoka.

"Kwanini Tusingebaki kumsaidia?.." aliuliza mama, baba akajibu.
"Kazi yetu maalum iliyo tuleta huku imeshaisha, hiyo sio kazi yetu kwahyo tukicheza tunakufa maana hiyo kazi hatujachaguliwa sisi hatujapewa agizo na majini watakuja binadam wengine waliochaguliwa, wakutoka duniani watakuja kuifanya hiyo kazi sisi hii haituhusu tukilazimisha tu kufa lazima."

Mama na baba wakizipiga hatua zakuondoka, ila walikuwa wanaona tukio kwenye mikono yao, kwenye jumba la kifalme kwa mfalme walitokezea mashetani wengine watano wakiwa na yule mtoto wa mfalme aliyejulikana kwa jina la Damor. Mfalme akaanza kurudi nyuma huku akitetemeka, walinzi wake wakasogea ili wapambane nao walipulizwa na upepo wa mdomo tu wakaenda kujipamiza kwenye ukuta wa fensi habari yao ikaishia hapo, mara wakatokezea maaskari wengine zaidi ya mia mbili na mikuki yao wakataka wapigane na vile viumbe, wale mashetani hawakuhangaika nao.
Shetani mmoja akawanyoshea tu kidole wakaanza kupigana wao kwa wao hadi wakaisha akabakia mmoja tu, yule shetani aliye wagombanisha akamkotro yule askari aliyebakia akachukua mkuki akajichoma mwenyewe habari yake ikaishia pale.

Wale mashetani wakamsogelea mfalme, mkuu wa kile kikosi akatoa amri mfalme auwawe. Shetani mmoja akasogea akanyosha mkono akamniga shingoni akaanza kumnyonga kwa nguvu, ila mfalme alikuwa hahisi chochote kama vile tu hajashikwa.

Wakati yule shetani akiendelea kumnyonga, mmoja wao wakati anapepesa pepesa macho akamuona shetani mwenzake akiwa juu ya fensi amechomwa na vyuma vilivyo chongoka, akamshtua mkuu wake.
"Mkuu ona kule juu" mkuu wake pamoja na yule aliyekuwa anamniga mfalme wote wakaangalia nini wanaoneshwa, walishangaa kuona mwenzao aliuwawa vibaya vile kiongozi wao akakasirika akasema akimuangalia mfalme.
"Waliofanya hivi wako wapi?" mfalme hakusema chochote, mara ikasikika sauti ya mtoto wake damor ikisema.
"Watakuwa wameondoka, kama nilivyowaambia wenyewe ndo wamewauwa wale wote niliokuja nao mwanzo."
"Oooh!!.. Hii ni kazi ndogo nyie bakieni hapa hapa mbaki mkimshikiria mfalme, ngoja mi niwawahi kabla hawajavuka mpakani." Mara damor akasema.
"Wale ni watu hatari sana ungeongozana na wengine wakakusaidie"
"Hapana!. Mi mwenyewe naiweza hii kazi kwangu ni watoto wanao nyonya" kwisha kusema vile akatoweka mahala pale.

Damor akawaambia wale mashetani wengine.
"Huyu baba angu kuna kitu amewekewa na wale watabiri kwahyo hamuwezi kumuuwa kirahisi rahisi hivyo, labda mtumie kwa njia ya hewa yani mpulizieni sumu ndo anaweza kufa."
"We mtoto unalaana wewe na wewe sio dam yangu na hupaswi kurithi kiti changu na kama ukikaidi yatakukuta makubwa sana." alisema mfalme ila mtoto wake alibaki tu kucheka huku akimbinulia mdomo baba ake.
Wale mashetani wakakubaliana na lile wazo alilotoa damor, shetani mmoja akavuta hewa Kisha akaipulizia kwenye uso wa mfalme Goru. Sumu ikaanza kumuingia taratibu akaanza kukohoa mfurulizo, nguvu zikamuishia akaanza kuyumba yumba mwisho akadondoka chini akatulia tulii, akafariki.

Mtoto wake damor akaanza kucheka huku akisema kwa sauti kubwa na iliyokali iliyopenya vyema kwenye masikio ya kila jini wa mji ule wa trofi.
"Hahahaha!!... Hahahaha!!.. Mimi Damor Goru ndio mfalme wa mji huu kwaanzia leo, Baba angu ameshafariki zama zake tumezifunga zinaanza zama zangu sasa mnatakiwa mfate sheria zangu mkiwa wakaidi mtakipata cha mtema kuni." Sauti ilisikika kama vile inatokea mbinguni kila jini wa mji ule aliyasikia maneno yale, majini wananchi waliogopa sana maana walimjua mtoto yule alivyo na roho mbaya kuzidi hata baba ake na walijua pia alivyokuwa na nguvu kubwa za kishetani.

Ile sauti ilipenya hadi kwenye masikio ya wazazi wangu watabiri, maana pia walikuwa wanamuona kwenye mikono yao.
"unasikia hiyo sauti?.. Unaona mfalme wameshamuuwa." alisema mama, baba akajibu.
"Ndio naona wameshamuuwa" kisha lile tukio lilokuwa linaonekana kwenye mikono Yao wakalitoa mikono yao ikarudi kama kawaida.

"Halafu mbona tunatembea tu, hatutoweki tutafika saa ngp unajua sikuelewi?.." alisema mama, baba akajibu.
"Haya jaribu kutoweka kama utaweza?.." alisema baba Kisha mama akajaribu lakini akashindwa.
"Umeona eeeh!!.."
"Kwanini sasa siwezi?.."
"Haya maeneo haiwezekani kutoweka, tumekaribia kufika sehem ambayo tunaweza kutoweka sio mbali ni pale tu ndomana nilikwambia tutatembea kwanza."
"Hivi haya mambo we umeyajulia wapi au ulikuwa unauwezo nayo tokea zamani ulikuwa unanizuga tu?.." mama alimuuliza baba na baba akajibu.

"Mi mwenyewe nashangaa nimekuwa nauwezo mkubwa mnoo na nikitoa utabiri hata kama najisemea semea tu nahisi kama yanatokea kweli nimekuwa tofauti kabisa na nilivyokuwa mwanzo, Ni zile nguvu tulizopewa kule kwenye falme ya jozi ndo zimenifanya niwe hivi."
"Mmmh!!.. ila kweli hata mimi niko tofauti pamoja nakuwa tulifundishwa kuzitumia lakini nahisi kama kuna vitu vinaongezeka ambavyo hata hatukufundishwa."
"Ni kweli halafu nahisi kuna kitu cha hatari kinaku..." kabla hajamalizia sentesi yake wakapigwa teke za mgongoni, wote wakadondoka chini. Wakajizoa zoa pale chini wakageuka wakaangalia ni nani aliyewapiga, ilikuwa sio sura ngeni kwao, walimuona kwenye kavideo kalikotokea kwenye mikono Yao.

Alikuwa ni yule kiongozi wa wale mashetani.
"Mmeniulia watu wangu kikatiri sana, lazima na nyinyi muwafate huko huko walipoenda" lilisema lile lishetani likiwa linabadilika taratibu taratibu mwisho likawa na sura yakutisha, uso wake ulikuwa na alama kama yakupasuka pasuka halafu lilikuwa na rangi ya moto, kichwani lilikuwa na mapembe, mkononi kwenye vidole lilikuwa na makucha marefu halafu mdomoni meno yake yalitokeza hadi nje, miguuni sasa alikuwa na vidole sita halafu viganja vilikuwa vimechongoka kama misumari, alitisha sana.

Likawasogelea wazazi wangu, mama akaanza kurudi nyuma uoga ukamuingia akakaa nyuma ya baba. Lile shetani kwa kasi ya ajabu likamvaa baba likamshika mkono wa wakushoto likamkata, mkono ukadondoka chini. Baba alihisi maumivu makali sana akajikaza akataka kupambana wakutumia mkono wakulia. akapigwa ngumi kwenye ule mkono hadi vidole vyake vikapinda akadondoka chini, mama yeye alikuwa anamlilia baba tu. Baba akajikakamua akainuka, mama akamshikilia kwa nyuma, lile shetani likatuma kombora takatifu lilojaa moto, likawapitia wote....ITAENDELEA...

RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu ya 24

TULIPOISHIA..
Baba akajikakamua akainuka, mama akamshikilia kwa nyuma, lile shetani likatuma kombora takatifu lilojaa moto, likawapitia wote....

SONGA NAYO...
Wakaenda kudondokea mbali kabisa na pale, walihisi maumivu makali sana maana walipigiza chini, hali zao hazikuwa nzuri kabisa. Yule shetani akasogea hadi pale walipo dondokea akaanza kuwacheka.
"Hahahaaaaa!!!.. Hahahaaaa!!... Nyie ni maboya tu hamna lolote." alisema huku akijipiga piga kifuani, Baba akajiinua kidogo akaangalia sehemu aliyodondokea, ilikuwa ni sehemu ile ambayo unaweza kutoweka akamshika mama mkono. Yule shetani akiwa bado anajigamba, kwenye mbavu za baba yakatokeza mabawa akamkumbatia mama kwa kasi ya ajabu wakapaa juu kama ndege huku yale mabawa yake yakizidi kupiga hewa. Yule shetani alishangaa kuona wameondoka ghafla kwakupaa, Na yeye akatoweka huku akisema.
"Nawafata huko huko lazima nilipize kisasi cha watu wangu mlio wauwa."

Baba na mama wakiwa juu wakikata mawingu, wakaona upepo mkali ukiwafata kwa nyuma ukiwa kasi ya ajabu wakajua ni yule shetani, baba akaongeza na yeye kasi yakupiga mbawa wakapita mpakani. Yule shetani na yeye akataka kupita akapigwa na kitu kama vile amegonga ukuta akadondoka chini.

Alipodondokea ilikuwa sio mbali sana na ilipo ile kambi, wale walinzi wa pale mpakani walishuhudia ile mikimbizano, mkuu wao akasema.
"Jamani kule kwenye kasri ya kifalme kuna tatizo simnaona shetani wa mji wetu anawakimbiza wale watabiri waliopita hapa tukawapeleka kwa mfalme, itakuwa kuna kitu kibaya wamefanya, twendeni tukaone ni nini kinaendelea." alisema kiongozi wa kile kikosi wakajibagua walinzi wanne wakashikana mikono Kisha wakatoweka kimiujiza.

Yule shetani alipodondokea akajiinua akawoteka kurudi kwenye kasri ya kifalme maana alishindwa kuwapata baba na mama.
Shetani na wale walinzi wakatokezea kwenye kasri ya kifame, Wale walinzi walishtuka baada yakuona mfalme amelala pale chini akionekana kama amekufa.
"Mnashangaa nini kipi cha ajabu?.." alisema damor.
"Hamna!!.. Hamna!!.." wakajibu kwakubabaika.
"Haya nini kimewaleta huku?.."
"Tumehisi kama kuna tatizo huku ndomana tumekuja kuangalia."
"Hayawahusu rudini muendelee kulinda mpakani!!.. Halafu kabla hamjaondoka nani aliwaruhusu kuwapitisha wale watabiri waje huku?.." aliuliza damor
"Ni Hawa!!.. Ni Hawa!!.." wakawa wanarushiana mpira.
"Mbona siwaelewi, ni wakina nani wariwaruhusu waingie kwenye mji wetu semeni kabla sijawamaliza wote" alitishia damor,

Wale wawili walio waleta watabiri wakaanza kuongea.
"Hawa ndio viongozi wetu kwahyo wenyewe ndio waliwaruhusu wale watabiri waje huku"
"Vizuri kwahyo nyie ndio mriwaruhusu wale watabiri waje huku waharibu mipango yetu sindio?.. Nyie ni wasariti et eeeh!!."
"Hapana!!.. Sio sisi mfalme ni hao" na wenyewe wakajitetea.
"Siwezi kuwaelewa maana nyie ndio viongozi mtasemaje ni hawa wakati nyie ndio mnatakiwa kutoa amri." alisema damor huku akiwasogea huku mkono wake wakulia ukiwa unatoa makucha kama visu. Akamshika yule mkuu akaanza kumdunga tumboni na yale makucha yake akamdunga hadi usoni dam zikawa zinaruka tu, yule mlinzi mkuu akadondoka chini akapoteza maisha. Akamsogelea na yule msaidizi wake akaanza kumchoma na yeye hadi akafariki pia.

"Safisheni hapa halafu mkimaliza muende mtaani mkatafute vijana wenye nguvu waje wawe maaskari wa kwenye kasri hii na nyie ndio mtakuwa viongozi wao." alisema damor akiwa kama mfalme sasa, akaingia ndani huku wale mashetani wakiwa wanamfata kwa nyuma.
"Shukrani sana mfalme" walisema wale walinzi waliopewa uongozi, wakasikika wakinongona.
"Pamoja nakuwa hatujui kilicho tokea ila wale watabiri niwa kweli, waliwatabiria hawa viongozi wetu watauwawa na kweli wameuwawa, wakatutabiria sisi tutakuwa viongozi na kweli tumekuwa viongozi, wale wanauwezo mkubwa mnoo mi nawapenda japo sijui kama ni watu wabaya au ni wazuri." alisema mmoja na mwenzake akamuunga mkono. Wakafungua geti wakatoka nje wakaingia mtaani sasa kutafuta vijana.

Upande wa baba na mama, walitua kwenye kasri ya kifalme kwenye mji wajozi wakiwa hoi, baba akatua chini mabawa yakajifunga akalala chali akazimia mama akiwa juu.
"We adel amkaa!!.. Adel wangu!!!.. Amka jamani!!.." alisema huku machozi yakimtoka akihisi labda amekufa. Mara maaskari wa kasri ile wakasogea pale na mmoja akaingia ndani kuwaita mfalme, mkewe na watoto wao.

Mama machozi yalikuwa yanamtoka kama maji huku akilia kwa nguvu, Punde si punde mfalme na wanae wakafika wakiwa na walinzi wa mfalme, sarha akasogea akainama pale chini alipodondokea baba akayashika mapigo ya moyo wake akakuta yanadunda.
"Usilie yuko sawa!!.. Nyie maaskari njoeni mumbebe mumpeleke ndan kwenye chumba cha matibabu." alisema sarha huku akimshika mkono mama akimuinua juu. Wale maaskari wakafanya kama walivyo ambiwa na princess sarha, wakamnyanyua wakampeleka ndani.

Mfalme hakusema chochote wakaingia ndani na familia yake.
"Vipi hali ya adel ni mzima?.." aliuliza mama akimuuliza sarha huku wakizipiga hatua zakuingia ndani ya mjengo, mama alikuwa amemshika kabisa adel ila wazo lakusikiliza mapigo ya moyo wake hakuwa nalo kabisa alibaha tu.
"Ndio ni mzima kabisa ila inaonekana ametumia nguvu nyingi sana ndomana amezimia."
"Vipi mkono wake unaweza kurudi?.."
"Kwa huku kwetu hauwezi kurudi ila mkienda huko duniani atakuwa na mkono wake kama mwanzo tu."
"Kiaje sasa?.."
"Yani Ni hivi kila kinacho tokea huku kinabaki huku huku, hata kama huku ukikatika viungo vyako vyote ukirudi kwenu duniani viungo vyako vitarudi kama kawaida na kama ukifa huku kule duniani utakuwa mzima, na maisha yako yataendelea kama kawaida, sema hauwezi kuja huku tena maana umeshakufa. Mfano mimi nikifa huku nakuwa nimekufa kabisa maana ndio nyumbani ila nikienda duniani nikafie huko huko, huku tatokezea nikiwa mzima ila sitoweza kwenda duniani tena maana kule takuwa nimeshakufa." Sarha alimuelezea vizuri mama.

"Oooh!!.. Sawa, Nimekuelewa."
"Unaswali lingine?.."
"Mmmh!!.. Labda nikilipata takuuliza"
"Swali unalo sema umelisahau, unataka kujua huku mmekaa mda Gani?.."
"Eheeeh!!.. kweli nataka kujua tumekaa huku siku ngap?.."
"Huku mmekaa siku tano tu ila kule duniani ni miezi tisa sasa baba ako ameshakutafuta mpaka amechoka anajua umeshakufa, alishaweka msiba wako akijua umekufa maana kuna kijana alikamatwa kati ya wale waliompiga risasi adel, akasema ulizama na wewe ndani ya maji ndo wakatuma kikosi wakazama ndan ya maji kukutafuta lakini walikukosa ndo wakajua tayari utakuwa umeshakufa na maiti yako itakuwa ilipelekwa na maji sehemu nyingine ya mbali."
"Heeeeh!!.. Inamaana tumekaa miezi tisa yote hiyo?.."
"Ni Kwa duniani lakini sio huku."
"Heeeh!!. Inakuaje inamaana mimba yangu duniani inamiezi Tisa?."

"Ndio inamiezi tisa ukifika tu duniani utajifungua na ni mtoto wakike, naomba umuite yusrat jina la marehemu bibi yangu nalipenda sana." alisema sarha akimuomba mama
"Hilo hata usijali ila bado nazidi kushangaa haya mambo yanavyoenda, kwahyo ni sababu gani inafanya tutofautiane hvyo?.."
"Kwa sababu dunia yenu kule inazunguka na majira yanabadilika kuna jua kuna mvua kuna giza kuna mwezi ila huku kwetu kuna maji tu hamna jua hamna giza wala mwezi ukitazama juu yetu unaona Nini?.."
"Mi mara ya kwanza natoka nje nilishangaa sana kuona maji yanaelea juu kwa juu halafu hayadondoki ila sikutaka kuuliza nikajua dunia yenu ndo ilivyo."
"Ndomana tuko hivyo halafu sisi kuna kitu tunakitumia kuhesabu siku, kuna mwanga unatokezega juu kule kwenye maji ndo tunajua imeingia siku nyingine."
"Duuuh!!... Kwahyo wewe unamiaka mingapi?.."
"Mi namiaka mia tatu themanini"
"Heeeeh!!.. Acha basi?.."
"Ndio ilivyo na huyo baba angu anamiaka mia saba sitini na mama pia anamiaka mia saba ishirini."
"Heeeh!!.. Unajua unanistaajabisha.."
"Huku ndio tulivyo na mdogo wangu surha anamiaka mia mbili tisini na nane, bado ni binti mdogo." alisema sarha wakiwa ndo wamefika sebureni kwenye gorofa ya kwanza wakakaa kwenye kiti wakaanza kupiga story.

"Miaka yote hiyo unasemaje ni mdogo?.."
"Kule kwenu duniani ni kama tu ametimiza miaka kumi na nane, ndo tunavyomuona kwa umri wake huku" alisema sarha...ITAENDELEA...RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu ya 25

TULIPOISHIA..
"Miaka yote hiyo unasemaje ni mdogo?.."
"Kule kwenu duniani ni kama tu ametimiza miaka kumi na nane, ndo tunavyomuona kwa umri wake huku" alisema sarha...

SONGA NAYO...
"Duuuh!!.. kwahyo umri wenu wakufa ni miaka mingap?.."
"Ukishafika miaka elfu moja naa, ndo unaweza kufa."
"Kwahyo chini ya hapo hamfi?.."
"Ndio njia inayoweza kutuuwa chini ya hapo, labda mtu akuuwe ndo unaweza kufa."
"Duuuh!!.. Usinichoke kwa maswali kwahyo huku hamna magonjwa"
"Magonjwa yapo ila hayawezi kumuuwa mtu mwenye chini ya miaka elfu Moja atajihisi vibaya kidogo tu halafu atakuwa sawa hatutumii hata dawa, mwenye miaka elfu Moja na, ndio yanaweza kumuuwa maana kinga ya mwili wake inakuwa ndogo sana."

"Na swali lingine la mwisho, mbona mfalme wa kule kwenye mji wa trofi alikuwa anaumwa?.."
"Yule anaumr kama wa baba tu ila yeye ule ugonjwa alitengenezewa na mashetani wake wala hauwezi kumuuwa, wenyewe walicho fanya wale mashetani ni kumpandikizia ule mgonjwa ili nguvu yake ya kinga ishuke kabisa na magonjwa yaweze kumuingia afe mapema." alisema sarha wakiwa wamekaa kwenye viti vilivyopambwa na almasi. Na mama akajibu.
"Ila sasa hivi yule mfalme ameshakufa."
"Heeeh!!.. imekuaje Sasa? nyie ndio mumemuuwa au?.."
"Hapana sisi tulipanga mpango wetu na ukaenda sawa akaibonyeza ile remote sehemu yakuizima, Badae mashetani ndio walikuja kumuuwa baada yakujua amejua mpango wao."

"Mmh!!!.. Bora baba ake kuliko lile litoto lake linaroho mbaya sana na sizani kama tutakuwa salama kabisa maana sisi hatuna nguvu kama zao maana wenyewe wanapewa nguvu na mashetani wao"
"Halafu mbona yule shetani alishindwa kupita pale mpakani?.."
"Kama sio muhusika wa huku huwezi kupita mpakani ukiwa na nguvu za kishetani."
"Mmmh!!.. Mbona yule aliyelileta bom aliweza kupita wakati alikuwa na nguvu za kishetani."
"Elewa kwanza yani kama sio muhusika wa huku huwezi kupita."
"Kwahyo yule mgeni aliyekuja na bom alikuwa ni muhusika wa huku?.."
"Ndio mji wetu unamjua vizuri tu maana amekulia huku huku ameenda kule akiwa mkubwa ndo anaishi huko sasa hivi."
"Heeeh!!.. Basi hilo ni tatzo kubwa mnoo wabaya wenu siwatakuwa wanawatumia watu ambao wamehama kwenye huu mji na kwenda kule kama walivyo fanya kwa yule kijana."
"Hiyo hali haipo tena tumeifunga kabisa hata kama amezaliwa huku hawezi kurudi akiwa na nguvu za kishetani tuliifunga kabisa baada ya lile tukio."
"Oooh!!.. Hapo sawa."

"Japo tunahofu maana wale mashetani wananguvu sana wanaweza kutumia mbinu yoyote tu wakafanikisha kupita."
"Duuuh!!.. hapa sasa nimeelewa elewa jinsi miji hii ilivyo, nipazuri sana huku kushinda hata duniani kila sehemu inapendeza mijengo yenu mizuri ina maadhari nzuri hamna jua wala Giza kila siku kuna mwanga wakupendeza, nimepapenda sana sema wale mashetani wa mji wa trofi wanawaonea wivu maana mmewazidi mbali kimaendeleo ndomana wanataka wauteke na huu mji."

"Ndio, maana huu ndio mji mkubwa zaidi na wenye mijengo mikubwa kuzidi hata miji ya duniani, ukitoka kwenye mji huu ukaingia kwenye mji mwingine wa huku nikama umetoka mjini umeenda kijijini hapa ndio mjini ndomana wanapambana miaka yote kutuangusha ila kinacho tusaidia mpaka sasa ni ulinzi mkubwa uliowekwa na mababu zetu kuhusu maadui kuingia na nguvu za kishetani kwenye mji huu haiwezekani lazima wakwame mpakani."

"Halafu naomba nikuulize swali lingine"
"Uliza tu hata usijali"
"Hivi huku hamlagi au?.."
"Tunakulaga mbona"
"Yani mi toka nifike huku sijawahi kuhisi njaa"
"Hahahaha!!.. Ndio ilivyo yani ukiwa huku hauwezi kuhisi njaa huku tunakula kama kufurahisha midomo tu sio kwaajili yakushiba, maana miili yetu sisi inaweza kuishi bila hata chakula, na mgeni wa kutoka duniani akija huku lazima na hali ya huku imvae kama nyie simnaona hata hamhisi njaa kama sisi tu."
"Duuuh!!!.. Huku kuna maajabu mengi."
"Ndio mengi sana ungekuwa na mda ningekutembeza mji wote huu ukajionee maajabu yalioko huku."
"Mi mbona nina mda mwingi tu twende nikapaone"
"Hapana hauna mda adel mda wowote atazinduka mnatakiwa muwahi kwenda duniani ukajifungue mtoto maana ujauzito wako kule duniani ushafikisha miezi tisa." mama aliposikia yale maneno ya sarha alilishika tumbo lake alishangaa maana tumbo lilikuwa kawaida tu kama hana mimba ila anaambiwa duniani inamiezi Tisa aliguna ila akaelewa maana alishaambiwa hali ya kule ilivyo tofauti na duniani.

"Mda wowote mkijisikia kurudi mtarudi, nguvu tulizo wapa hatuzitoi mtarudi nazo duniani ndo zitawawezesha kurudi Tena huku kutusalimia au kupambana na watu wabaya huko duniani, japo wengi waliokuja kutoka duniani kwaajili ya kazi maalum tuliwanyang'anya nguvu wakarudi duniani kama walivyokuwa ila nyie tumewaachia." alisema sarha akiongeza maneno mengine baada yakusema yale ya mwanzo.
"Twende tukamuone adel kama ameshazinduka." wakainuka wakazipiga hatua wakapanda ngazi za kuingia kwenye gorofa nyingine ya juu, wakafika kwenye chumba cha matibabu sarha akafungua mlango wakaingia ndani wakamkuta baba amelala kwenye kitanda.

"Ooh!!.. Adel wangu umeamka!!.. Vp unajihisije?.."
"najihisi Niko sawa tu"
"Vp ulipokatwa mkono hauhisi maumivu?.."
"Hapana sihisi maumivu yoyote"
"Tuone mkono wako wakulia vidole vikoje"
"Viko kama kawaida tu nimeamka nakuta vimenyoshwa haviumi Tena."
"Inuka sasa twende duniani maana mda wakujifungua umeshafika."
"Kujifungua nini?.."
"Hapana kujifungua mtoto."
"Mmh!!.. itakuwa umechanganyikiwa ujifungue mtoto gani wakati hata tumbo lako halioneshi chochote."
"We twende tukifika takuelewesha."

"Kabla hamjaenda ngoja niwaletee zawadi zenu" alisema sarha kisha akatoka nje ya chumba kile baada ya mda akarudi na mabegi mawili. Akafika anayaweka chini akalishika begi moja akalifungua, baba na mama walishangaa huku wakiasama midomo kwakuduwa kulikuwa na dhahabu nyingi sana zilijaa hadi juu, akalifunga lile begi, akafungua lingine.
"Heeeeh!!.." Baba na mama walishangaa tena baada yakuona lile begi limejaa maburugutu ya pesa hela za kimarekani naza kitanzania."

"Hizi pesa ndio mtaanzia maisha kabla hamjaziuza hizo dhahabu"
"Weeee! Sarha hizo dhahabu zote tukikamatwa tutasema tumezitolea wapi?.." aliuliza mama.
"Hawawezi kuwakamata nyie mnanguvu kubwa sana, na sio lazima muuze zote mtakuwa mnauza kidogo kidogo na pia nashauri msiende kuishi kwenye mji wa Zanzibar maana mnajulikana kule mshakufa maana picha zenu zilitembea sana kwamba mnatafutwa hadi leo watu wazanzibar wanajua nyie ni wafu, japo baba wa lamia na mke wake wamesharudi nchi za kiarabu hawapo Zanzibar Tena ila nashauri hivyo na kingine tena naomba msaidie watu masikini mayatima muwape misaada ikiwezekana muanzishe kituo cha kulea watoto yatima" alisema sarha. Baba na mama wakakubali ombi lake.

Wakiwa wanaongea mule kwenye kile chumba cha matibabu mara mlango ukafunguliwa wakaingia mfalme, mkewe na mtoto wake wa mwisho surha.
"Hongeren kwa kazi nzuri mliyoifanya." alisema mfalme akiwapa mkono baba na mama, na mkewe pia akasema hivyo na surha pia.
"Halafu mimi sijawapongeza et? au nimesahau?.." alisema Sarah.
"We umetupongeza saa ngp wakati tumepiga story tu hata pongezi hujatoa." alisema mama
"Ooh!!.. Jamani mnisamee nilijisahau nilihisi nimeshawaambia, hongereni sana tena sana"
"Shukrani sana sasa hapa ndio nimeisikia pongezi yako kwa mara ya kwanza."
"Mmh!!.. Jamani mtu akifanya vizuri si lazima apongezwe."
"Ila wewe ulikuwa hutupongezi pamoja nakuwa tulifanya vizuri kwenye yale mazoezi ya jinsi yakuzitumia nguvu mlizo tuwekea."
"Ooh!!.. Kumbe mliliweka rohoni naombeni mnisamee sana kweli pale nilikuwa sina imani na nyie ila kiukweli mmenisurprise sikutegemea."

"Halafu nina swali, nyie mmejuaje kama tumefanikisha wakati sijawaambia." aliuliza mama swali likimrenga mfalme na familia yake, Mfalme akajibu.
"Nguvu tulizo wawekea mwilini zilikuwa zinatuwezesha kujua kama mmefanikiwa au mmefeli." alisema mfalme....ITAENDELEA....
 
Ukimaliza ni tag
 
Agizo la majini 26-30RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu ya 26

TULIPOISHIA..
"Halafu nina swali, nyie mmejuaje kama tumefanikisha wakati sijawaambia." aliuliza mama swali likimrenga mfalme na familia yake, Mfalme akajibu.
"Nguvu tulizo wawekea mwilini zilikuwa zinatuwezesha kujua kama mmefanikiwa au mmefeli." alisema mfalme....

SONGA NAYO...
"Ooh!!.. Sawa" alisema mama, na sarha akaongea
"Sasa mnaweza kwenda."
"Tunaendaje Sasa?.."
"Ficheni kwanza hayo mabegi kwakutumia nguvu zenu" alisema mfalme, kwakuwa walikuwa wameshaelekezwa jinsi yakuzitumia nguvu haikuwa kazi waliyashika yale mabegi halafu yakatoweka.
"Haya nendeni sasa"
"Subiri kwanza hivi tukitaka kurudi huku tunafanyaje?.."
"Kwakuwa mnanguvu mnanuia tu maneno kwamba 'tunataka kwenda kwenye mji wa jozi uliyoko chini ya bahari' Mtatokezea huku." alisema sarha
"Sawa" aliitikia mama, sarha akasema tena.
"Semeni mnataka mtokezee Tanzania mkoa Gani?.." baba akajibu.
"Mkoa wa pwani tukatulie huko."
Sarha akawanyoshea mkono huku mdomo ukitikisika kuashiria anaongea kitu, mara mwanga mkali ukatokezea baba na mama wakatoweka.

Wakatokezea pwani nje ya hospital ya medwell hospital, mama akiwa na tumbo kubwa uchungu ukiwa umemshika manesi wakamuona wakaleta kiti cha wagonjwa akakalishwa Kisha akapelekwa ndani ya hospital kujifungua, Baada ya dakika kadhaa mbele akajifungua mtoto wakike ambae ndio Mimi, Siku zikaenda hatimae mama akakaa sawa siku moja wakiwa wamekaa kwenye nyumba waliyopanga kwa mda, mama akaanza kumuelezea sasa baba yale yote aliyoambiwa na sarha kipindi yeye amezimia. Baba akaelewa sasa kwanini mkono wake ulirudi ghafla wakati kipindi Yuko kwenye mji wa jozi alikuwa hana mkono, Na pia akaelewa kwanini mama ujauzito wake ulikuwa haraka vile.

Siku zikaenda miezi ikakatika tukiwa tunaishi maeneo ya kibaha ambapo tulijenga nyumba kubwa yenye gorofa mbili, maisha yetu yalikuwa mazuri sana maana baba na mama walifungua miladi mingi na kituo cha kulea watoto yatima kwa mda mfupi ambao tulikaa pale tulifahamika sana, watu walishangaa kuona watu tumekuja ghafla tu halafu tukaanzisha miladi mikubwa kama ile ilikuwa ni gumzo pwani nzima iliijua familia ya Mr adel.

Siku moja baba na mama pamoja na Mimi nikiwa mdogo tulifunga safari ya kwenda saudi Arabia kwa wazazi wake na mama, walipo muona mtoto wao walishtuka sana maana walijuaga ameshakufa, ila walieleweshwa wakaambiwa kila kitu wakaelewa, walifurahi sana kuniona mjukuu wao, hawakuwa na kipingamizi wakawapa baba na mama baraka zote wakawaruhusu waowane, tukarudi na wazazi wa mama tanziania ndoa ikaenda kufungiwa Zanzibar kwa wazazi wa baba, na wenyewe walielewa baada yakuelezewa, baada ya ndoa wazazi wa mama wakarudi saudi Arabia, mama na baba pamoja na Mimi tukarudi pwani kibaha ambapo ndipo nyumba yetu ilipo.

Miaka ikaenda hatimae wakapata mtoto mwingine ambae ndio mdogo wangu Fahad, miaka ikazidi kwenda hatimae nikafikisha miaka 8 nikiwa darasa la pili Mdogo wangu fahad akiwa na Miaka minne, siku hiyo tulikuwa tumefunga shule mwezi wa sita, gari ya baba ikaja kunichukua shuleni nikaenda nae hadi nyumbani tulipofika akaniambia.
"Leo mimi, wewe, mdogo wako pamoja na mama ako, tunaenda sehemu nzuriii kutembea." Sikujua ni wapi ila nilikubali tu maana nilipenda kutembea sehem mbali mbali, baba aliniambia nilale kwanza nikiamka ndo tutaenda, nikalala nilipoamka nikajikuta niko sehem tofauti na nyumbani pembeni yakitanda kile kizuri kilicho pambwa na vito vya thamani nilichokuwa nimelala Mimi pia alikuwa amelala mdogo wangu fahad.

Mda si mrefu nikaona mlango unafunguliwa wakaingia ndani wazazi wangu baba na mama pamoja na watu ambao sikuwajua ila mbaba mmoja alikuwa amevaa kitu kichwani kama cha kifalme nikasikia wakiongea.
"Sarha!.. huyo ndio yule mtoto uliyesema tumuite jina la bibi Yako yusrat"
"Waooo!!.. ndo huyu" alisema yule sarha huku akininyanyua kutoka kitandani huku akinibusu busu.
"Na yule aliyelala ni mdogo wake anaitwa Fahad" alisema baba.
"Hongereni sana" alisema mfalme huku akimpa mkono baba, wote waliokuwa mule ndani wakawapongeza wazazi wangu.
"Asanteni sana" alisema baba akipokea hongera yao wakati sarha akiwa anacheza na mimi mara fahad akamka.
"Na kenyewe kamesema msinitanie ngoja na mimi niamke" alisema surha wote wakacheka. Surha akasogea hadi kitandani akamnyanyua fahad akaanza kucheza nae.

"Nyie mshacheza nao sana tupe na sisi tuwashike hata kidogo" alisema mke wa mfalme malkia bi yurha.
"Mmh!!.. Mama haya na wewe mshike yusrat ila kumbuka ni mama yako huyo mshike vizuri."
"Hahahaha!!.." wote wakacheka, ilikuwa ni furaha wale watu wote walitushika huku wakicheza nasi. Hiyo siku walifanya kasherehe kadogo tulikunywa tulikula tuliinjoi sana, baada ya hapo tukatoka mimi mdogo wangu wazazi wangu pamoja na sarha akiwa na walinzi, akaanza kututembeza sehemu mbali mbali za mji ule wakati mwingine nilikuwa naogopa niliona vitu vya ajabu sana, wakatupeleka sehemu nyingine kule ndio nilipapenda kulipendeza sana kulikuwa na vitu vingi mnoo tulicheza kule mi na mdogo wangu hakika tulifurahi sana, Badae tukaanza kurudi kwenye ule mjengo wa kifalme tukiwa na walinzi pamoja na mwenyeji wetu sarha.

Ila nilishangaa kitu nikamuuliza swali baba.
"Baba mbona huku kuna mijengo mirefu lakini hamna hata gari?.."
"Sarha kazi yako hiyo mjibu mtoto" alisema baba akimtupia mzigo Sarha.
"Ooh!!.. Bibi yangu huku usafiri wetu ni ule kule" nikageuza shingo kuangalia alichonionesha, Ilikuwa ni mnyama ambaye sikuwa na mjua ila alikaa kiajabu ajabu sikuwahi kumuona popote ila alikuwa amembeba mtu juu huku yeye akitembea alikuwa anataka kufanana na farasi kidogo tu ila hakuwa farasi kabisa. Sarha akanionesha usafiri wao mwingine.
"Tazama kule juu" alisema sarha nami nikatazama, nikaona mtu anapaa juu akiwa na mabawa.
"Heeeeh!!.." nilishangaa nikamuuliza.
"Hichi ni nini mbona binadam anamabawa na anapaa? Inawezekanaje?.."
"Ndio usafiri wetu huku kila mtu anapaa" alisema Sarha, mi nikazidi kushangaa, baba akamvuta sarha pembeni Kisha akamwambia sarha.
"Huoni kama unamuwekea fikra mbaya mtoto anaweza kuwa anayaota kila siku, ndomana mi nimewafunga wasione kitu chochote, we umemfumbua yusrat anaona hadi watu wanavyopaa we unahisi ni jambo la kawaida Hili tukio linaweza kumsumbua sana kichwani."
"Hapana haliwezi kumsumbua maana na yeye mwenyewe anaweza kupaa, umemfungaje wakati yeye mwenyewe anauwezo hakuna ulichomfunga kila kitu alikuwa anakiona mengine ameamua tu kuyakalia kimya ila alikuwa anayaona vizuri tu.." alisema sarha baba akashangaa akamuuliza.
"Anaweza kupaa?.. Kiaje?.."
"Mmesahau mliondoka na nguvu mwilini mwenu?.. Basi zile nguvu zipo hadi kwa watoto wenu."
"hapana naomba uwatolee staki watoto wangu wawe hivyo." alisema baba akionekana kushangaa.
"Ambae tunaweza kumtolea ni fahad tu ila yusrat hapana maana anaonekana anakipawa kikubwa sana atasaidia watu siku za mbeleni kuna watu wengi huko duniani wanateseka na wachawi na mashetani, majini yanawasumbua sana, huyu ndio anaweza kuwa mkombozi wao hili ndio agizo letu la majini." alisema sarha, baba alimuelewa sarha akasema.
"Ohoooh!!!..Kama ni hivyo basi hata fahad msimtolee" sarha akakubali wazo la baba tukaendelea na safari.

Mi nilikuwa pembeni kabisa ila nilikuwa nauwezo wakusikia kila walichokuwa wanazungumza, nilishangaa kusikia et na mimi naweza kupaa nikajisemea.
"Nikifika kwetu tajaribu kupaa tuone kama naweza." Nikamfata sarha nikamuuliza swali lingine.
"Hivi hapa tuko wapi duniani au?.. Mbona pako tofauti sana na duniani? Ona juu kuna maji yakimwagika je? Situtalowana?.."
"Haina haja yakukuficha maana wewe unaroho ya kijasiri angekuwa mtoto mwingine angekuwa ameshalia sana baada kuona vitu vya ajabu kama hivyo ila wewe unashangaa kidogo tu huna hata wasi wasi unaonekana unauwezo mkubwa sana, Hapa tulipo tuko chini ya bahari"

"Heeeh!!.. Chini ya bahari?.."
"Ndio chini ya bahari ila ukifika duniani usimwambie mtu yoyote iwe siri Yako"
"Sawa nimekuelewa." nilisema huku nikiwa na mshangao kidogo ila baada ya sekunde kadhaa mshangao wote ukaisha nikaona kawaida tu. Tukazidi kuzipiga hatua hadi tukafika kwenye jengo la kifalme nyuma tukiwa tunalindwa na walinzi wengi, Nilishangaa kitu...ITAENDELEA..

RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu Ya 27

TULIPOISHIA..
Tukazidi kuzipiga hatua hadi tukafika kwenye jengo la kifalme nyuma tukiwa tunalindwa na walinzi wengi, Nilishangaa kitu...

SONGA NAYO...
Nilikuwa sijaiyona vizuri ile kasri ya kifame kwa nje, ilikuwa ni bonge la mjengo uliopambwa na vito vya thamani ulikuwa na gorofa nne ila ulivyojengwa sijawahi kuona tanzania mjengo kama ule. Nilikuwa nashangaa tu nikashtulia na baba ndo nikaweka umakini wakutazama kule napoenda.

Baada ya kufika ndani ya mjengo, baba na mama wakatupeleka mi na Fahad kwenye chumba ambacho tulikuwa tumelala ule mda, wenyewe wakafunga mlango kwa nje wakaondoka tukabaki mi na mdogo wangu kwenye kile chumba. Sikuwa nahisi njaa nikamuuliza na fahad akasema na yeye pia hahisi njaa na kwakuwa tulikuwa tushaoga, tukapanda juu ya kitandani tukalala baada ya mda usingizi ukatupitia, nikiwa nimelala fofofo Niliota ndoto yakutisha sana nikashtuka!!!....Huku nikipiga kelele!!!.

"We yusrat kuna Nini?.. Mbona unapiga kelele hivyo?.." walisema mama na baba wakifungua mlango nakuingia ndani ya kile chumba, sasa nilijikuta niko kwenye chumba cha nyumbani kwetu, nilihema kwa kasi huku nikiwa nimejishika shingoni.

"Nimeota napambana na majitu yakutisha yakanizidia nguvu yakataka kunikata shingo ndo nikashtuka.."
"Pole ni ndoto tu pumzika mwanangu" alisema mama.
"Hapana mama sina usingizi Tena" nilisema huku nikishuka chini ya kitanda kile.
"Kama huna usingizi twende sasa sebureni ukaangalie Tv" alisema baba huku akinishika mkono tukatoka ndani ya chumba kile tukazipiga hatua hadi sebureni tukakaa kwenye sofa, mfanyakazi wetu wa ndani alikuwa pia amekaa kwenye yale masofa akiangalia naye tv.

"Baba hivi tumefikaje huku situlikuwa chini ya bahari?.."
"Weeee!!.. Mtoto wewe unaongea manini hayo?.." alisema mama huku akinikonyeza nisiendelee kuongea. Baba na mama wakavutana pembeni kwenye korido wakaanza kuongea jambo.
"Mnaona yanayo mtokea binti yangu hadi anayaota yale mavitu ya ajabu mlishindwa kufanya chochote asiyaone yale majitu?.."
"Mke wangu mi nilifanya hivyo ila kumbe na yeye ananguvu kama za kwetu tena yeye ni zaidi kwa maana amechanganya nguvu zangu na za kwako, kwahyo nilivyofanya vile asione kumbe haikusaidia chochote alikuwa anayaona yote." alisema baba, mi nilikuwa nasikia kila kitu walichokuwa wanazungumza maana mi uwezo wangu ni mkubwa sana.

Yule mfanyakazi wetu wa ndani akanisemesha, nikatoa umakini kusikiliza kule nikamsikiliza yeye.
"Za siku nyingi yusrat" alinisalimia yule mdada wa kazi.
"Sijakuelewa za siku kiaje we situliachana jana tu hata siku yenyewe haijaisha."
"Mmmh!!.. Jana?.. Wakati mmekaa wiki mbili kabisa, unasemaje ni Jana."
"heeeeh!!!.. We utakuwa unaumwa marelia wewe!!.. Mwambie mama akupeleke hospital, we jana sindio tulifunga shule?.."
"Hahaha!!.. Acha nicheke Jana?... Wakati shule mmefunga wiki mbili zilizopita."
"Duuuuh!!!.." nilihisi naota nilitulia nikafikiria kwa makini ila nikawa naona ni jana.
"inakuaje ananiambia et wiki mbili zimepita kiaje?.." nilijiuliza bila majibu, bahati nzuri mama na baba wakarudi hata kabla hawajakaa nikawauliza.

"Et mama tulifunga shule lini?.."
"Mmmh!!.. Swali gum, Hebu muulize baba ako."
"Baba umesikia swali langu naomba nijibu."
"Kwanza kwanini unaniuliza hivyo?.."
"Dada safia anasema et tulifunga shule wiki mbili zilizopita wakati mi najua ni jana, na tena jana sindio tulienda kule chini ya bahari? et?..."
"Heeeh!!.. We mtoto mbona lopo lopo sana hebu funga huo mdomo wako" alisema mama akiniziba mdomo. akainuka kisha akazipiga hatua za kuondoka na baba akamfata nyuma, wakaondoka huku wakiongea.
"Unaona madhara yanayotokea?.. Hili ni tatizo na anaweza kuwaambia wanafunzi wenzake wa shuleni kwamba alikuwa chini ya bahari." alisema mama, na baba akauliza.
"Duuh!!.. Sasa tunafanyaje?.."
"Hapa inabidi tumwambie ukweli wote kwamba yeye ni nani? Akuwe anajua.."
"Ni jambo jema kumwambia ili awe anajielewa asaidie wenzake mwenye matatzo." alisema baba.

Mi nikiwa pale sebureni, fikra zote hazikuwa kwenye tv iliyokuwa inaonesha movie nzuri sana ya katuni, Mawazo yangu yalikuwa yanawaza inakuaje jana inakuwa wiki mbili.. Nilitoka kwenye dimbwi la mawazo baada yakusikia sauti ya safia ikiinita Kwa kwa mkazo.
"Wee! Yusrat wewe!!.. Inamaana hunisikiii?.. Mtoto mdogo unakuwa na mawazo hivyo?.. Unawaza Nini?.. Kwamba unafamilia, hahahaha!!... Unawaza watakula nini watoto wako?... Hahaha!.." hapa alikuwa anaongea huku anacheka nami ikanibidi tu nitabasam.

"Yusrat nimesikia unasema et mlikuwa chini ya bahari, kiaje?.. Et ni kweli mlikuwa chini ya bahari?.." wakati najiandaa kujibu mara sauti ya mama ikasikika ikitoka nyuma yangu.
"We safia maswali gani hayo unamuuliza mtoto?.. Yeye alikuwa amelala akaota alikuwa chini ya baharini, nawe kwa akili yako ukaamini maneno Yale?.. We unaweza kuishi baharini?.. Kwa akili ya kawaida tu unaweza?.. Maswali mengine sio yakuuliza uwe unajiongeza tu...." alisema mama akionekana kuwa na hasira.
"Zima hiyo tv uende ukalale usiku huu ushakuwa mkubwa, nawe yusrat inuka twende ukalale." alisema mama, dada safia akazima tv akaenda kwenye chumba chake, mama akanishika mkono akanipeleka hadi kwenye chumba nacholala.

Tukafika tunakaa kwenye masofa ya pale chumbani.
"Kwahyo mama leo hatuli?.."
"Kwani we unanjaa?.."
"Hapana sina njaa ila naona hapakuwa na pirika pirika zozote za kula."
"Basi kama hauna njaa achana na maswali hayo, nataka nikwambie kitu nisikilize kwa makini." hiyo siku mama alinielezea mambo yote yaliyo watokea mwanzo mwisho ndio nikajielewa sasa mi ni nani.

Siku zikaenda hatimae wiki mbili zikakatika, siku yakurudi shule ikafika, baba alinipeleka na gari lake hadi shuleni akanishusha yeye akaenda kazini. Siku hiyo nilikuwa nawaona watu baadhi, tofauti kabisa na siku zote kuna wanafunzi wenzangu nilikuwa nawaona wanatembea na vitu vyakutisha mwilini mwao. Tuliingia darasani tukakaa kwenye madawati, punde si punde mwalim wetu akaingia, Nilishtuka kidogo baada yakumtazama usoni alikuwa na macho yanayo waka kama tochi yalitisha sana.

Nikamshtua mtu ambae nakaa nae dawati moja nikamwambia.
"Angalia kwenye macho ya mwalim unaona Nini?.." akanijibu.
"Mi naona yuko sawa tu kama siku zote." nikajua kabisa yale macho sio ya kawaida nayaona mimi peke yangu kwakuwa ndio mwenye uwezo wakuona vitu ambavyo mtu wakawaida hawezi kuona, mwalim akaanza kuita majina aliita wote akamaliza Kisha akasimama akasema.

"Hivi Lucy msuya, Jackline Gerald, Juma issa, maulid hamza, helen pamoja na roda wako wapi mbona Leo hawajaja shule?.. anayejua taarifa zao ainuke atuambie?.." mwanafunzi mmoja akanyosha mkono, akaruhusiwa na mwalim akainuka akasema.
"Mwalim lucy msuya nasikia et amepotea wazazi wake wanamtafuta siku ya tatu sasa haonekani nyumbani, kuhusu Helen alifariki wiki iliyopita kwenye mazingira ya kutatanisha watu wanasema et ameuwawa na wachawi.." alisema yule mwanafunzi...

"Wewee!!.. Hilo neno la wachawi toa, serikali yetu haiamini uchawi kabisa, huyo atakuwa amekufa kwa siku zake tu, msije mkaamini uchawi hata siku moja tumeelewana?..."
"Ndio mwalimu" waliitikia wanafunzi ila mimi sikuitikia nilikuwa nawasikiliza tu.
"Haya ambae anataarifa za wengine atuambie, haya zakhia hapo sema." akainuka zakhia akaanza kuongea.
"Mwalim, jackline na roda ni marafiki zangu, nakumbuka siku nne zilizopita walinipitia nyumbani wakasema tuje twisheni halafu tupite kwako et unashida na sisi, mi nikakataa maana nilikuwa najihisi vibaya nikashindwa kuja, ndio wakaniaga wanakuja twesheni watapita na kwako, sijui sasa ilikuwaje ila kesho yake Sasa asubuhi nikasikia et roda amekutwa amekufa wakati akiwa amelala kwenye chumba chake, na kwa jackline pia nikasikia story kama hiyo hiyo. Kwahyo roda na Jackline hawapo tena wamesharifiki."

"Wazazi wao siwana namba zetu mbona hawajatutarifu walimu?.."
"Mwalimu mi sijui sasa labda wamejisahau"
"Halafu swala la mimi kuwaita ni uongo mimi sikuwaita labda waliamua kukudanganya tu." alisema mwalimu...ITAENDELEA...

Usikose sehemu ya 28

RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu Ya 28

TULIPOISHIA...
"Wazazi wao siwana namba zetu mbona hawajatutarifu walimu?.."
"Mwalimu mi sijui sasa labda wamejisahau"
"Halafu swala la mimi kuwaita ni uongo mimi sikuwaita labda waliamua kukudanganya tu." alisema mwalimu...

SONGA NAYO...
Mara nikasikia mwalim akiongea kimoyo moyo.
"Mbona naumbuka mimi, sijui kwanini nimewaulizia ningeachana nao tu"
Niliyasikia maneno Yale, nikapata picha kidogo. Mwalim akainuka akaanza kufundisha, nilikuwa na muona tofauti na siku zote nilihisi jambo ila sikuwa na papara nilitulia huku nikizidi kumsoma, Baada yakumaliza kutufundisha aliondoka. Masaa yakazidi kusogea hatimae mda wakutoka shule ukafika tukaruhusiwa kurudi nyumbani mi nikamfata yule mwalim akiwa amesimama nje ya darasa kisha nikamuuliza.

"Kitu gani ambacho unakificha?.."
"We mtoto naficha kitu Gani Kiaje?.. Hebu nenda nyumbani."
"Mwalim mi siondoki hadi uniambie kwanini unaficha ukweli wakati unajua kabisa sababu ya watoto wenzetu kupotea??.."
"Heeeeh!!!..." Niliona mshangao mkubwa kutoka kwa mwalim alishtuka!!.. hakutegemea kama tamuuliza swali kama lile.
"Hebu nenda nyumbani we mtoto wenzako wote wameshaenda we bado uko hapa tu takutandika fimbo ondoka haraka nikifumbua mambo nisikuone"
"Haya fumbua macho hutoniona kama ulivyosema" nilisema huku nikipotea kimiujiza, mwalim alipofumbua macho alishtuka!!!!... Baada yakutoniona ila sauti anaisikia, aliogopa akaanza kukimbilia ofisini, Mi nikamwambia.
"Tutazungumza vizuri usku, takuja kwako" nilisema huku nikiwa sionekani mwalim alikuwa anageuka nyuma kutazama sauti yangu inatokea wapi ila hakuona mtu, akafika ofisini anafungua mlango kwa pupa akazama ndani huku akisema.

"Jini!!!.. Jamani jiniii!!.." Walim wenzake pale ofisini walishtuka wakafungua mlango wamtazame huyo jini ila hawakuona chochote wakaurudishia mlango Kisha wakamfata yule mwalim aliyekuwa anajulikana kwa jina la madam tinna.
"Wewe umekuaje mbona unaingia ofisini unapiga makelele umechanganikiwa au?.."
"Hapana sijachanganyikiwa ila nikweli nimeona jini, sogeeni hapa dirishani niwaoneshe" alisema madam tinna huku akisogea hadi dirishani, na walim wenzake wakamfata kwa nyuma hadi dirishani.

"Haya angalieni yule pale mtoto jini" alisema madam tinna akiwaonesha walim wenzake, mi nilimpungia mkono nikimuaga huku nikibadilisha macho yangu yakawa yanawaka moto machoni, ndo alizidi kubaha huku akitapa tapa mule ofisini, akawa anawaonesha walim wenzake niliposimama walim wakasogea kuangalia, ila hawakuniona wala hawakuona chochote.
"Wewe utakuwa umechanyikiwa wewe, unatuonesha jini wakati sisi hatuoni chochote, huyu tumpeleke hospital atakuwa hayuko sawa." Walim wenzake wakamtoa ofisini wakiwa wamemshikilia hadi kwenye maegesho ya magari.
"Jaman mi sijachanganyikiwa jini yule pale kabisa hamumuoni??.." alisema huku akitazama niliposimama akielekeza kwa mkono, walim na wenyewe wakaangalia ila hawakuona chochote.
"Mi nimewaambia huyu amechanganyikiwa tumuwahishe hospital" alisema mwalim huku wakimuingiza ndani ya gari, madam alikuwa mbishi hakutaka kuingia ndani alikuwa analalamika yeye hajachanganyikiwa.

Punde si punde gari la baba likafika pale shuleni, nikalisogelea nikafungua mlango nikapanda ndani ya gari.
"Yusrat pale kuna nini mbona kama kuna vurugu" aliniuliza baba, sikutaka kumficha nilimuelezea yote mwanzo mwisho.
"Duuh!!.. Basi huyo mwalim wenu atakuwa anahusika kwa asilimia kubwa anatakiwa aeleze vizuri amewapeleka wapi, Anza majukumu ndo kazi Yako hiyo ya kwanza tetea watu." alisema baba huku akiwasha gari, tukaondoka maeneo ya pale shule.

Wale walim walifanikiwa kumuingiza ndani ya gari madam tinna, baadhi wakaingia kumshikilia maana alikuwa hataki kabisa kupelekwa hospital akidai yeye ni mzima. Gari ikawashwa wakampeleka hospital ya karibu na shule ile hapakuwa mbali Sana dakika kadhaa tu walifika wakampeleka hadi kwenye kitanda wakamfunga na kamba ili asilete vurugu daktari akamchoma sindano yakumlaza kwanza maana alikuwa amepandisha mori hakutaka kabisa kuwekwa pale, jinsi alivyokuwa anakataa nakuleta vurugu ndivyo walim wenzake walikuwa wanaamini kweli amekuwa chizi. Baada ya mda alitulia akalala.

Mimi baada yakufika nyumbani na baba tulishuka ndani ya gari tukaingia ndani, nilibadilisha nguo za shule Kisha nikamfata mama, chumbani kwake nikaanza kumuelezea yaliyotokea shuleni, mama alisaport kile ambacho nilichokuwa nataka kufanya. Mda ukaenda hatimae usku ukaingia baada yakumaliza kula niliingia chumbani kwangu nikapanda juu ya kitanda nikakaa Kisha nikakunja miguu, nikatoweka ndani ya chumba kile nikatokezea hospitalini. Madam Tinna alishtuka!!.. Baada yakuniona pale alikuwa tayari ameshazinduka, akapiga kelele.
"Jiniiiii!!!... Huyooo!! Muoneni jiniiiii!!!..." mule kwenye kile chumba walikuwepo daktari na walim wenzake wawili. Walishtuka na wenyewe baada ya zile kelele za madam tina wakajua ukichaa umepanda tena wakaangaza angaza ndani ya kile chumba kama kuna kitu ila hawakuona.

"Jamani kama nilivyo waambie tumempima anaonekana hana tatzo lolote akili zake ziko sawa wala hana shida yoyote, ndomana nimewaita usku huu ili niwaambie na ingewezekana mngemchukua maana alikuwa ametulia kabisa ila nashangaa anapiga kelele hivi sijui shida Nini Sasa." alisema daktari.

Mi nikamsogelea madam tinna nikiwa na sura yakutishaa makucha yangu yalikuwa yamechongoka na meno pia yalitokeza nilitisha sana, nikamshika mguu kisha nikaanza kumkwaluza kwakutumia makucha yangu. Kwakuwa alikuwa amefungwa kamba akashindwa kuamisha mguu ila alikuwa anatapa tapa sana. Nilimkwangua kisawa sawa nikamwambia
"Sema ukweli wako ulio ufanya kwa wale watoto wanafunzi wenzangu bila hivyo nakuuwa kwa mateso makubwa mnoo." nilisema huku nikizidi kumkwaluza hadi kwenye mapaja dam zilimtoka kweli kweli.

Daktari na wale walim walishtuka sana baada yakuona vidonda vyakutisha kwenye miguu ya madam tina huku dam zikimtiririka.
"Jamani maajabu hiki Nini?... Mbona sijawahi kuona kitu kama hichi?.. Yani mtu anatokwa na vidonda ghafla tu?.." alisema daktari hata wale walim walishangaa wakabaki wameduwaa, mi nakazidi kumuazibu hadi akasema.
"Jamani nasemaaa, usiniuweee!!.. usiniuweee!!.." alisema madam tinna huku akipiga kelele.
"Haya sema haraka kabla sijakukata shingo" nilisema huku nikiwa nimemkazia sura ya kutisha alikuwa analia kama mtoto.
"Jamani Nasema mimiii!!... Nasemaaaa!!!... Mwalim wenzangu mi ndio nimemuuwa, Lucy msuya, Helen, roda, juma issa, maulid hamza, jackline Gerald, Wanafunzi wangu wa darasa la pili."
"Heeeh!!.. Kiaje mbona hatukuelewi?.."
Madam tinna akanitazama huku akisita kuongea nikazidi kumchoma choma na makucha yangu akapiga kelelee.
"Unaniumizaaa!!.. Nasemaaa!!.. Niache nasemaaa!!.."
"Haya sema haraka." nilimjibu, akaanza kuongea, huku walim na daktari wakisikiliza kwa makini.
"Miezi sita iliyopita nilijiunga na freemason ili niwe tajiri, nilichoka maisha yakimaskini niliyokuwa naishi kamshahara nilikokuwa napewa shuleni kalikuwa kadogo sana kasingetosha mahitaji yangu. Nilijikuta nakopa mwezi mzima mshahara ukija unakuta na madeni kibao nalipa na bado nabaki nadaiwa madeni mengine, Nikamfata rafiki yangu mmoja nikamuelezea matatzo niliyonayo, akaniambia.

"Hiyo sio kazi yakutegemea hiyo niyakujishikiza tu, leo usku twende nikupeleke sehemu ukawe tajiri, uko tayari rakini sio tunaenda kule unaanza kukataa au unasema hauwezi?.. Hapana ukifika kule unatakiwa ukubali kila utacho ambiwa na ukifata masharti utayopewa utakuwa tajiri mkubwa sana." alisema yule rafiki yangu na kwakuwa nilikuwa na uchu sana na hela nilikubali akanipeleka kwenye chama chao cha kishetani nikaungwa na mimi nikawa mwanachama wao ila wakanipa sharti nimtoe mama yangu, nilikataa ila badae nikakubali maana walisema nisipo mtoa wataniua mimi na mimi sikuwa tayari kufa kwa wakati huo, nikamtoa mama angu, iliniuma sana ila nilijikaza.

Baada ya siku kadhaa nilikuwa na mabadiliko makubwa sana, kwenye kabati yangu kila siku nikiamka nakuta begi la pesa limejaa maburungutu ya misimbazi, Sasa niliona raha ya maisha. Nilikula bata sana hadi nikafikiria kuacha ualimu ila rafiki yangu akanikataza akaniambia "hutakiwi kukaa bila kazi watakushtukia bora ujishikize kwenye hiyo hiyo kazi ili maswali yasiwe mengi."......ITAENDELEA...

RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu Ya 29

TULIPOISHIA..
Nilikula bata sana hadi nikafikiria kuacha ualimu ila rafiki yangu akanikataza akaniambia "hutakiwi kukaa bila kazi watakushtukia bora ujishikize kwenye hiyo hiyo kazi ili maswali yasiwe mengi."......

SONGA NAYO...
nilimuelewa rafiki yangu nikanunua gari, najua iliwashangaza sana walim wenzangu maana mkifikiria mshahara tunaopewa harafu nanunua gari iliwachanganya kidogo ila niliwajibu mi naishigi kwa marengo na nina miladi mingine inayoniingizia pesa ndomana nimepata pesa zakununua gari, mlinielewa ila haikuwa hivyo ile gari ilitokana na pesa za kishetani.

Siku zilizidi kwenda siku Moja wakaniambia nimtoe mtoto wangu wakiume nilikataa katu katu, ila rafiki yangu akanishawishi akijitolea mfano yeye hana familia kabisa wote amewatoa kafara sikukubaliana nae nilikataa ila niliporudi nyumbani nikakuta mtoto wangu ameshakufa iliniuma sana nikamwambia yule rafiki yangu mi najitoa kwenye chama chao akaniambia haiwezekani kutoka na pia ule ndo ulikuwa mda wakupata matunda sasa wakile nilichokifanya, nikamuelewa kishingo upande, siku zikazidi kusogea maisha yangu yakabadilika kabisa nikawa naishi kwenye mjengo mkubwa wenye gorofa na magari kama yote watu walishangaa sana mafanikio yangu ya ghafla wakasema nimeitoa kafara familia yangu lakini mi sikuwajali nilijali maisha yangu.

Siku moja wale viongozi wakifreemason walinitokezea nyumbani kwangu wakaniambia siku zijazo kutakuwa na kikao cha wanachama wa freemasons kwahyo wanahitaji dam na nyama za watoto wenye umri kati ya nane hadi kumi, wawe ishirini. Na walinichagua mimi nifanikishe jambo lile, niliogopa sana huku nikiwa sijui taanzia wapi na tawatolea wapi ila kwa badae nilikuja kupata jibu nilipokumbuka kuwa wanafunzi ninao wafundisha shuleni wanaumri huo, nikawauwa wanafunzi sita wa kwenye darasa langu kisha nikaenda ile shule ya jirani nikachukua na wengine sita nikatafuta tafuta na wengine nikakamilisha idadi ya watoto ishirini ambao niliambiwa na wale viongozi, kisha nikawapeleka sehemu husika na kikao chenyewe kilifanyika juzi tu.
Na nahisi sina mda mrefu wakuishi duniani maana wamesikia nimetoa siri zao hawatoniacha salama kabisa, naomba mnisamee sana familia za watoto hao kule walipo wanisamee sana ni shetani tu alinipitia na tamaa za mali tu." Alisema madam tinna huku akiwa analia, mi nikatoweka mahala pale nikarudi nyumbani kwenye chumba changu.

Madam tinna baada yakutoa story ile iliwahuzunisha sana walim pamoja na daktari hawakuwa nalakumfanya walimuonea huruma tu wakamuuliza.
"Sasa mbona ulikuwa unalia halafu kuna kitu kama unaonesha ilikuwa ni nini?.."
Aliuliza mwalim mmoja.
"Alikuwa ni mwanafunzi wangu wa darasa la pili na yeye ndio aliyenifanya niongee story hii maana amenitesa akisema niseme ukweli kwa niliyoyafanya nahisi ananguvu kubwa sana sjui nizakichawi au zaaje ila ameniumiza sana na hapa alikuwepo ila nyie hamkuweza kumuona maana mrengwa alikuwa ni Mimi na haya majeraha yeye ndio amesababii..." alisita kuendelea na neno lile baada yakuona vile vidonda vyote vimepotea na miguu yake imerudi kama kawaida alishangaa sana, hata walim na daktari walistaajabu maana yale majeraha yalifutika ghafla sana. Punde si punde wakatokezea viongozi wawili wa chama cha kifreemason, Madam tinna alishtuka sana hadi walim na daktari wakahisi kuna kitu yeye anakiona ila wao hawakioni.

Wale viongozi wa chama cha freemasons wakasema.
"Unajua kabisa adhabu utayoipata halafu unatoa siri zetu kwa makusudi sindio?.."
"Jamani mi mbona sijasema siri yoyote.."
"Hahaha!!!... Hujasema siri yoyote?.. Hujui kama kila siku tunadanganya watu kwamba hatutoi kafara halafu wewe unatoboa siri kwamba uliuwa mama ako, mtoto wako pamoja na watoto ishirini.."
"Kwani uongo si nyie ndio mlinituma?.."
"Hata kama ni kweli hutakiwi kusema maana mtaani chama chenu kinajengewa sifa mbaya hadi watu wanaogopa kujiunga na chama chetu kila siku tunapambana kuweka mabango mtaani kuwa hatutoi kafara ili watu waje kwa wingi halafu wewe unatoa siri kwa hawa watu na wenyewe wakitoka hapa waende kuwaambia wengine tuzidi kuwa na sifa mbaya sindio?.. Ngoja nikuoneshe"

alisema yule kiongozi kisha akawanyoshea kidole walim pamoja na daktari akawatoa kumbukumbu zote za ile story aliyowahadithia madam tinna, yakuhusu kuuwa watoto ishirini na kutoa kafara familia yake yote, wakazitoa zile kumbukumbu. Kisha wakamgeukia madam tinna sasa wakaanza kumnyonga akawa anatapa tapa, walim na daktari walishangaa kuona madam anatapa tapa huku akiwa anatoa povu wakamfungua zile kamba haraka haraka ila walikuwa wamechelewa madam tinna alifariki. Wale viongozi wa chama cha kifreemason wakaondoka baada yakumaliza kazi yao iliyowaleta.

Daktari akamsogelea akasikiliza mapigo ya moyo wake, alikuwa ameshafariki hawakuwa na lingine zaidi yakumfunika na kumpeleka mochwari ndo ukawa mwisho wa madam tinna.
Mi nikiwa nyumbani kitandani nilikuwa nashuhudia kila kitu kilichokuwa kinatokea. Baada yakuona mwisho ulivyokuwa nikalala, alfajiri niliamshwa na mama akiniuliza kazi ile iliendaje, nikamuelezea kila kitu ilivyokuwa akanipa pongezi sana huku akisema.
"Mtoto mdogo lakini unaakili zakikubwa hongera sana mwanangu"
"Asante mama" nilijibu, ilipofika asubuh nilijiandaa baba akanichukua kama kawaida akanipeleka shule tukiwa njiani na baba akaniuliza ilivyokuwa nikamuelezea na yeye akanipongeza. Ile siku alitaka kuona hadi navyoingia darasani kwahiyo nilishuka kwenye gari na yeye akashuka Kisha tukaingia shuleni, tukakutana na mwalim mmoja akasalimiana na baba na mimi nikamsalimia kisha akasema.
"Leo tunamsiba wa mwalim nwenzetu madam tinna kwahyo hakutokuwa na masomo Leo ni vyema huyu mtoto ungerudi nae nyumbani" alisema mwalim na baba akamuelewa huku akimpa pole kwa niaba ya mwalim wenzake, baba alikuwa anaelewa kila kitu maana nilimuelezea mwanzo mwisho ndomana aliingia nami shuleni akiwa anahisi huenda kusiwe na masomo maana aliyefariki ndio mwalim wetu wa darasa na kweli ikawa hivyo, akanirudisha nyumbani yeye akaenda kazini.

Siku zikazidi kwenda miezi, Miaka ikakatika, hatimae nikatimiza miaka kumi na tano nikiwa nimeshakumbana na majanga ya kila aina, nilikuwa nishasaidia watu wengi sana wanao pitia matatizo ya nguvu za Giza.

Nikiwa form two, Siku moja tulipokea ugeni wa wanafunzi wa shule ya jirani kidato cha pili pia, tukafanya nao mtihani wa ujirani mwema, nikiwa nimekaa kwenye bustani nilishuhudia wanafunzi wawili wa shule ya jirani waliokuwa wamekaa karibu yangu jinsia ya kike wakiinuka na kugombana Sikujua wanagombania nini maana hata maongezi yao sikuyatilia maanani, nikainuka nikasikia wanagombana huku wakisema.

"Mshenzi mkubwa wewe kumbe snichi eeeh!!!... Ile siku namtambulisha kwako kumbe ulimtamani eeeh??.. Nasema leo utanikoma"
"Hapana merry yeye ndio ananitaka ndomana nimekuletea hizi karatasi anazonitumiaga uzione, ningekuwa namtaka nisingekwambia naomba uniachie basi ujue watu wanaanza kusogea unamfaidisha nani Sasa?.." Alisema yule mdada mwingine, ndo nikajua wanagombania mwanaume.

"Mmmh!!.. Watu wamekuja shule kusoma au wamekuja kutafuta wanaume?.. Mmmh!!.. Watoto wadogo wanawaza mapenzi?.. Kazi ipo.." nilistaajabu maana sehemu ile walim wakiwaona ni hatari kwao kugombania mambo hayo, nikataka kuzipiga hatua kuondoka zangu mara nikasita nikasimama baada ya kusikia yule merry akisema.
"Unajitetea eeeh??.. Hivi unanichukuliaje unazani Jana sikuwaona kule shuleni mkiwa kule nyuma ya choo mmekumbatiana?.."
"Aaah!!.. Merry mimi kabisa??.. Labda ulinifananisha."

"Kwani mi sikujui hadi useme nimekufananisha?.. Nasema leo ndio mwisho wako wakuishi hapa duniani kesho huioni umenikwaza sana rafiki mnafki wewee!!.." Watu wengi walikuwa wamesogea pale kushuhudia ule ugomvi ila hawakusikia yale maongezi maana merry na yule mwenzake walikuwa wanazungumza taratibu mnoo.
Yule binti alipiga magoti chini kumuomba msamaa merry, nahisi alikuwa anamjua vizuri ila merry alimsukuma chini yule rafiki yake kisha akaondoka zake, mara ikasikika sauti ikisema...ITAENDELEA..

Usikose sehemu ya 30

RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu Ya 30

TULIPOISHIA..
Yule binti alipiga magoti chini kumuomba msamaa merry, nahisi alikuwa anamjua vizuri ila merry alimsukuma chini yule rafiki yake kisha akaondoka zake, mara ikasikika sauti ikisema...

SONGA NAYO...
"Anna Leo utakoma yani umemchokoza mchawi wa shule mbona utaipata pata" alikuwa ni mwanafunzi mwenzao wa kule kwenye ile shule wanayo somea.
"Nenda basi ukaniombee msamaha, mi hata sikufanya kwa makusudi July mwenyewe ndo alinilazimisha." alisema yule anna, akiwa anamwambilia kwenye sikio lake kama anamnong'oneza.
"Weeeeeh!!!.. niende kukuombea msamaha halafu anigeuzie kibao Mimi, weeee!!.. Naijua hiyo nenda mwenyewe!!.." alisema yule mvulana. Anna akazipiga hatua za kuondoka mahala pale, akiacha minong'ono kwa wanafunzi wenzangu ambao nilikuwa nasoma nao.
"Yani huyu mdada ni zaifu kweli kweli yani anampigia magoti kabisa?.. Yani ingekuwa ni mimi kingeeleweka nisingekubali kushindwa kirahisi tungedundana." Mara mwingine akadakia.
"Kwanza pale alivyomsukuma chini, nilishikwa na hasira nikatamani angekuwa amenisukuma mimi nikamuonesha kazi, ningemfumua hadi akaenda kusimulia kwao."
Nilitabasam baada yakusikia maneno ya wale wanafunzi wenzangu kisha nikazipiga hatua za kuondoka, mara nikasikia sauti nyuma ikiita.

"We dada!!.. We dada!!.. Samahani simama kidogo." Nikageuka nyuma nikagundua anayeitwa ni Mimi, nikasimama.
"Samahani dada mi mi mwanafunzi mwenzako ila natokea ile shule ya jirani yenu, naomba tufahamiane kama hautojali mi naitwa samir sijui wewe unaitwa nani?.."
"Mi naitwa yusrat."
"Ooh! unajina zuri"
"Hata lako pia ni zuri."
"Kipindi tunafanya mitihani nilikuona nikatamani uwe rafiki yangu"
"Ooh!! Hilo tu wala hata usijali"
"Ikiwezekana uwe hata zaidi ya rafiki"
"Kiaje mbona sijakuelewa?.."
"Yani ni hivi mi nimetokea kuvutiwa na wewe yani nimekupenda hata mitihani sijafanya vizuri nilikuwa nakutazama na kukufikiria wewe tu naomba uwe mpenzi wangu." alisema yule mvulana anayeitwa samir mi nikamjibu.

"Naomba nikuulize swali kwanza"
"Uliza tu hata usijali"
"Hivi shule yenu inamatatizo Gani?.."
"Kiaje nifafanulie kidogo nikuelewe matatizo kiaje?.."
"Inaonekana wanafunzi wa shule yenu wanawaza mapenzi tu, wale wasichana wa shule yenu walikuwa wanagombania wanaume na wewe ndo wale wale hivi mnamapepo gani?.. Hamuwahurumii wazazi wenu wanao hangaika kuwatolea ada?.. ili msomo halafu nyie mnakuja kufanya upumbafu yani unashindwa kufanya mtihani ambao ndio maisha yako ya kesho unaniwaza Mimi?.. Kwanza kijana mdogo sana hata miaka kumi na tano sizani kama umeshafikisha. Kwanini lakini mnawaza ujinga??.."
"Samahani dada naomba usiende kunisema kwa mwalimu"
"Siwezi kufanya kitu kama hicho ila nakupa darasa tu badilika we bado mtoto mdogo waza masomo hayo mambo utayakuta tu, unajua mi nawahurumia wazazi wenu wanajua watoto wao wako shule wanasoma elimu ya maisha yao ya mbeleni, kumbe wanasoma elimu mapenzi hivi kizazi hiki kimekuwaje? Mbona kimeharibika sana, nakuomba tu ubadilike uwaze masomo tu usiwaze habari za mapenzi naomba nikwambie tu ukweli mi si binadam ni jini takufatilia kila unachofanya kama hutobadilika kila siku takuwa nakuadhibu." Alionekana kama hajakubaliana na nililo mwambia ya kwamba mi ni jini, akajua nasema vile kwaajili ya kumtisha tu akapuzia ila akanionesha kama vile ameelewa.
"Sawa dada naomba niende ila tafadhali naomba tena usije kumwambia mwalim yoyote yule"
"Usijali" akaondoka nikamtazama nikatikisa kichwa, et hata mtihani hakufanya vizuri kwaajili yangu kijana mdogo kama yule?.. Daaah!!. Nikaondoka maeneo Yale.

Mida ya usiku wa siku ile sikulala kabisa usingizi hakuja niliwaza lile neno alilosema merry akimwambia mwanafunzi mwenzake "Leo ndio siku yako ya mwisho kuishi duniani, mmh!!.."
Lile neno lilijirudia mara mbili mbili kichwani mwangu, nikajifunua shuka nikaliweka pembeni Kisha nikakaa pale pale kwenye kitanda nikiwa na gauni langu la kulalia, Nikatoweka ndani ya chumba kile nikatokezea kwenye nyumba Yakina merry yule aliye mwambia mwenzake kwamba hatoiyona siku ya kesho yake.

Nikamkuta akiwa chumbani na bibi yake wakiwa wanavaa kaniki za kichawi wakifanya maandalizi ya kwenda kuwanga.
"Bibi Naenda mwenyewe au tunaenda wote?" aliuliza merry akimuuliza bibi yake, mi nikiwa nimesimama pembeni nikiwatazama hawakuwa na uwezo wakuniona uwezo wao ulikuwa mdogo sana.
"Tunaenda wote maana ile nyumba inaonekana inaimani ya mungu japo imani yao sio kubwa kivile ila twende wote utapokwama takusaidia" bibi yake alimjibu.
"Sawa bibi" alijibu merry halafu wakakaa kwenye ungo zao kisha wakatoweka, nikawafata nyuma nyuma nione wanaenda wapi na wanaenda kufanya Nini.

Wakafika hadi kwenye nyumba moja kubwa kiasi, wakashuka wakaingia hadi kwenye chumba kimoja cha ile nyumba kwakupitia kwenye ukuta, Iliwatetelesha kidogo ila yule bibi alikuwa ananguvu za ziada wakatua salama ndani ya kile chumba wakiwa na ungo zao, Kitandani alikuwa amelala anna yule rafiki na huyo merry. mi nilifika nikasimama karibu na kitandani alichokuwa amelalia Anna.
"Mmalize sasa haraka tuondoke zetu tukauwe na wengine siunajua leo tunakazi yakuuwa watu watatu."
"Sawa bibi" alisema merry kisha akanyosha mkono ukatoka mwanga kama radi hivi ukawa unaenda kwenye shingo ya Anna, nikauzuwia nikaushika bila kuonekana wao wakaone uko kwenye shingo ya Anna, merry akaanza kunyonga kwa nguvu.
"Bi...bi m...mbona najinyonga wenyewe"
"Kiaje we nyonga kwa nguvu muuwe kabisa leta nikusaidie" bibi akashika yeye akaanza nyonga.
"Bi...bi.. Unani..uaaaa.." alikuwa anamnyonga mjukuu wake bila kujua, mara merry akadondoka chini habari yake ikaishia pale akafariki. Bibi yake alishangaa inakuaje anayenyongwa ni mwingine na anayeanguka ni mwingine, akamuamsha mjukuu wake kwakumtikisa na kumuita kwa sauti rakini hakuamka akashika mapigo ya moyo wake ndo akajua ameshakufa, alistaajabu inakuaje anakufa yeye. Wakati akiwa anashangaa shangaa, nikaunyosha mkono wangu kumuelekezea yeye kisha nikavikunja vidole, Akaanza kujinyonga mwenyewe kwakutumia mikono yake, alijitahidi kuishusha mikono yake ili itoke shingoni lakini hakuweza alijinyonga mwenyewe hadi akadondoka chini akafariki. Nikaitowa ile miili ndani ya kile chumba nikaipeleka hadi kule kwenye nyumba yao ndani ya chumba cha merry nikaiweka kwenye kitanda kisha nikatoweka nikarudi nyumbani nikafika nalala, sasa usingizi uliweza kuja nilala usingizi mnonoo.

Siku zilizidi kwenda na Miaka ikakatika huku nikizidi kukutana na matukio makubwa makubwa, nikiwa na miaka 20.
Nikiwa chuo mwaka wa kwanza, kwenye chuo cha mkoa wa dar es salaam, nakumbuka ilikuwa ni siku ambayo tulipewa chuo mapumziko ya wiki Moja mi na rafiki zangu tukapanga twende morogoro kutembea tembea, tukiwa ndani ya gari yangu ambayo nilinunuliwa na baba pia nikapewa na dereva wakuniendesha, tukiwa njiani Tulishuhudia kwa mbele bonge la ajali halafu ilikuwa ajali ya ajabu sana Basi la abiria lilipinduka mara mbili na sababu ya kupinduka et ilikuwa imegonga mbuzi.
"Mmmh!!.." niliguna maana ilikuwa ni kitu ambacho akiingii akilini, tulisimama kwa nyuma tukilitazama lile gari lilivyokuwa linabiringita marafiki zangu walikuwa wameshika vichwa vyao huku kila mmoja akilalamika kivyake.
"Mungu wanguu!!!.. Jamaniiii!!.. ona inavyobiringita kuna mtu wakupona kwelii!!!.."
"Tulia kwa uwezo wa mungu watapona hata msijali" nilimjibu rafiki yangu.

Haikuwa ajari ya kawaida punde si punde Wakatokezea watu watano wakiwa wamevalia nguo nyeusi huku ikiwa inamichirizi myekundu, walisogea hadi pale lilipodondokea lile gari Kisha wakaingia ndani ya gari lilokuwa limeharibika vibaya sana.
Nikamshtua rafiki yangu mmoja aliyekuwa amekaa karibu yangu nikamwambia aangalie mbele pale kwenye ajali kama ataona chochote. Akaangalia ila akasema haoni chochote, ndo nikajua wale ndio waliosababisha ile ajali hawaonekani kwa macho ya kawaida.

Mara nikaona wanaitoa miili ya wale watu waliopata ajali halafu wakawa wanaipanga pale barabarani, hili nikahisi labda na wenzangu wanaona nikawauliza wakasema hawaoni chochote, nikafungua mlango wa gari kisha nikaanza kuelekea kule kwa wale watu wenye maumbile yakutisha.
"We yusrat unaenda wapi huko?.."
"Nyie tulieni humo humo ndani ya gari msitoke ngoja nishugurike na hili kwanza." nilisema huku nikizidi kuzipiga hatua nikawakaribia wale viumbe, walipo niona wakasitisha lile zoezi walilokuwa wanafanya wakasimama wote wakanitazama.....ITAENDELEA...

Usikose sehemu ya 31
 
Agizo la majini 31-35RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu ya 31

TULIPOISHIA..
"Nyie tulieni humo humo ndani ya gari msitoke ngoja nishugurike na hili kwanza." nilisema huku nikizidi kuzipiga hatua nikawakaribia wale viumbe, walipo niona wakasitisha lile zoezi walilokuwa wanafanya wakasimama wote wakanitazama....

SONGA NAYO..
"Atakuwa hatuoni tuendelee" alisema mmoja wao kisha wakainama wakaanza kuwatoa dam wale abilia halafu zile dam wakawa wanaziweka kwenye dumu kubwa walilokuja nalo. Kwenye ile barabara, hiyo siku palikuwa kimya sana hapakuonesha hata dalili za watu kupita pita wala ata gari tofauti na hiyo basi iliyopata ajali.

Nikiwa nimesimama pale pale nikanyosha mkono Kisha nikasonta kidole nikionesha ishara nikalidondosha lile dumu la dam likamwagika chini zile damu zote zikamwagika.
"Wewe mbona umemwaga tena tutatimiza saa ngapi Sasa?.."
"Sijamwaga Mimi, naliinua dumu hata haliinuki"
Nilipo hakikisha damu zote zimemwagika nikaruhusu dumu linyanyuke.
"Mbona sielewi nini hiki??.."
"Au yule mdada anatuona??.."
"Mi sijui mjaribu tuone kama anatuona" alisema yule mwingine Kisha akatuma kombora la kimiujiza kunifata nilipo nikalikwepa.
"Oya anatuona bhana, na inaonekana sio mtu wa kawaida" Wote wakaacha kufanya walichokuwa wanafanya wakasimama Kisha wakasogea sehemu nilipo, nami nikasogea tukakaribiana kabisa.

"We ni nani unayeharibu mambo ya watu?.."
"Na Nyie ni wakina nani mnayeuwa watu wasio na hatia?.."
"Sisi ni wafu tulio hai na hii ndio kazi yetu tumepewa agizo na majini wakishetani tuje kutoa watu damu nakupeleka kuzimu na hii ndio juisi yetu na hawa watu ndio nyama zetu, nawe ni nani?.." aliongea yote hata ambayo hakuulizwa
"Mi ni binadam nayetetea watu wanaonewa na nguvu za giza."
"Hahaha!!.. Et unatetea watu!!.. Hahaha!!..mbona hujatetea hawa hadi wamekufa."
"Hao hawajafa nikitaka kuwarudisha tawarudisha."
"Unajiamini nini wewe na unawezo Gani wakuona kama hawajafa??.."
"Mnataka kujua uwezo wangu njoeni mnijaribu." nilisema kisha mmoja akasogea ili anitext, Akarusha ngumi yenye moto mkononi nikaikwepa akarusha na teke, zote zikawa chafu nikazikataa.

"Mmeona uwezo wangu au Bado??.."
"We ni mchumba tu na utabaki kuwa hivyo, unakula kipondo kisha nakupeleka kuzimu unakuwa mwali wangu."
"Haya sawa mi ni mchumba na kama ukiweza kunipiga niko tayari unipeleke huko kuzimu kwenu ukanioe."
"Unazarau eeeh!!.."
"Zarau gani sasa wakati nimekujibu vizuri tu tena kimahaba et baby mzim!!!.. acha basi maneno fanya vitendo" alishikwa na hasira akanirukia, upesi nikamkwepa akapitiliza akadondoka chini.

"Hahaha!!.. Baby mwenyewe ndo uko hivyo??.. Hata nguvu huna utaweza kunilidhisha kweli?.." aliinuka akiwa na hasira akachomoa tusindano twingi kwenye mfuko wa ile nguo yake nyeusi, kisha akanirushia, nikatuona nikatugandisha juu juu hewani kwakutumia macho yangu Kisha nikatugeuza nikatuagiza turudi tulipotokea, akatuona akajaribu kutukwepa, twingine tukamchoma twingine akatukwepa. Kumbe tule tusindano tulikuwa na sumu, akayeyuka akawa moshi kisha ukaishilia hewani.
"Baby mzimu byee tutaonana kuzimu"
"Utakufa tu we binti na lazima talipa kisasi changu." ulisema ule moshi huku ukiishilia, nilijua kabisa ule mzimu umekufa duniani ila kule kuzimu bado utaendelea kuishi shida ni kuwa duniani hatoweza kuja tena.

"Sasa nyie kama kiongozi wenu ndo amekufa kizarau hivi nyie ndio mtafanya nini?.." niliwaambia wale wanne waliobakia, ila hawakutaka kunisikiliza wakanivamia kwa pamoja wakiwa wameshika nyavu ya kimiujiza ili wanivilingishieno, sikuondoka nilisimama pale pale wakaifikisha ile nyavu yao wakaanza kunivilingishia, wakataka kuninyanyua ili waondoke nami mara wakashangaa wameniacha chini, wakarudi Tena chini wakashikana mikono Kisha wakainyosha mikono yao juu kikatokea kiumbe cha ajabu juu kikiwa na mabawa kikashuka hadi nilipokuwa nimesimama sikushtuka wala kusogea nilisimama pale pale, kikaasama mdomo wake mkubwa kikasogea hadi karibu na kichwa changu kikanimeza mzima mzima wakaona nimeingia kwenye kinywa cha kiumbe kile, kumbe nilikuwa nimesimama pale pale na sikuwa nimeondoka. Alipoasama nilimtupia mdomoni kitu akakimeza akijua ni Mimi, mara kile kiumbe kikaanza kuhangaika kilitapa tapa mwisho kikapasuka vipande vipande kama kipulizo.

Hawakukata tamaa wakawamsha wale abilia waliokuwa wamewalaza pale chini, wakainuka wakiwa kama mazombie wenye sura za kutisha wakaanza kusimama kwakuyumba yumba, kisha wakatoweka mahala pale wakatokezea kwenye lile gari langu walimo rafiki zangu pamoja na dereva wangu, Nikapaza sauti.
"Jay funga vioo vya gariiii!!!..." alishangaa huku naye akiuliza.
"Nifunge kwanini?.."
"Acha maswali nimekwambia fungaa!!.." safari hii alinielewa akafunga vioo, wale abilia waliogeuzwa mazombie hawakuwa wanaonekana kwa marafiki zangu wala kwa dereva wangu jay, Wakalishika gari wakaanza kulinyanyua wakalipindua kabisa taili zikawa juu, nilisikia kelele za marafiki wakilalamika.
"Yusrat njoo utusaidie tunakufaaaa!!!.." Sikutaka kuwazuru wale abilia waliogeuzwa mazombie maana nilijua ni wazima Nikiwaumiza watakufa kweli kweli. Wale zombies wakalibinua tena gari likasimama kama mwanzo kisha wakalibinua Tena taili zikawa juu Tena.

Nikaona wale mazombies wanaongozwa na wale wafu walio hai, nikawageukia wale mizimu, wakashtuka wakaanza kurudi nyuma baada yakuyaona macho yangu yaliyokuwa ya blue yakitoa mwanga kama radi, Huku yakizidi kuwaunguza. Sikupenda zarau hata kidogo kwakuwa wao walinionesha zarau yakuwatengeneza wale abilia wawe zombie kisha wakawahangaishe rafiki zangu badala ya kupambana na mimi muhusika, ikabidi na mimi niwaoneshe zarau zangu zilivyo. Nikatoa kisu cha kimiujiza nikakituma kilikuwa kikali kikawa kinawafata huku kikizunguka kama feni, kilikuwa kinawakata kata kwaanzia miguuni hadi kwenye vichwa vyao sekunde kadhaa wote kikawafyeka, vipande vya nyama vilikuwa vinaruka tu, mwisho vikajikusanya vyote Kwa pamoja vikamungunyika vikawa Moshi ukaishiria hewani, ikawa ndo mwisho wao wakuikanyaka tena dunia.

Wale abilia walio badilishwa kuwa mazombie baada ya wale wanao waongoza kuyeyuka wakadondoka chini, wakiiacha gari yangu ikiwa mataili juu. Nikasogea kwenye ile basi iliyopata ajali, nikachungulia ndani ya ile basi kulikuwa na abilia wakiwa wazima kabisa ila hawakuwa na uwezo hata wakujitingisha kwa macho yakawaida wangekuja watu wangewaona wamekufa na wangeona dam nyingi zikiwa zinawavuja ila mimi kwakuwa nilikuwa nauwezo wakuona yasiyo onekana sikuziona dam niliwaona wakiwa kawaida tu, tena wakiwa wanahema.

Nikalinyoshea mkono lile gari nikaonesha ishara kama nalinyanyua, likaanza kujinyanyua mwisho likasimama sawa sawa, nikainua mkono tena nikakunjua viganja vyangu nilivyokuwa nimevikunja ukatokea moshi wa blue ukaenda hadi kwenye lile basi ukaingia hadi ndani ya gari lile, zile alama za kupondeka pondeka zikaanza kutoka kabisa gari likajikunjuruwa sehemu zote zilizokuwa zimeharibika zikakaa sawa ikarudi kama zamani, Wale watu walikuwa ndani ya gari wakaanza kuinuka kila mtu akajikuta yuko kwenye siti yake aliyokuwa amekaa, na dereva akajiona kama alikuwa usingizini pamoja na konda. Dereva akasikika akisema.

"Walioenda kujimba dawa wawahi wamekaa mda mrefu hadi napitiwa na usingizi." Na konda akadakia.
"Kama ulikuwepo sjui wanajisaidia mawe mi mwenyewe nilikuwa nimepitiwa na usingizi nimesimama hapa.."
Nilitoweka maeneo yale nikatokezea sehemu ilipo pinduliwa gari langu kisha nikaliinua kwa ishara likakaa sawa, nikawainua na wale abilia waliogeuzwa zombie. Walijishangaa kujikuta wamelala pale chini wakainuka.
"Nyie mnajisaidia mawe wahini gari linaondoka" alisema konda, wakatoka mbio kulifata gari wakafika wanapanda likawashwa safari ikaanza.

Nikafungua mlango wa gari langu nikazama ndani, Marafiki zangu pamoja na dereva walishangaa kuona lile basi lilopata ajali likiondoka walihisi wanaota wakafikicha macho Yao.
"We yusrat kimetokea nini mbona tunaona maajabu ya Karne??.."
"Hakuna maajabu kila kitu kiko vile vile unavyokiona"
"Inawezekana vipi lile gari likaweza kwenda wakati lilikuwa limepata ajali mbaya sana, imekuaje??..."
"Mnakumbuka niliwaambia ile sio ajali ya kawaida?.."
"Ndio ulituambia rakini inawezekana vipi? Mbona tunaona mazinga umbwe.." aliuliza mwingine.
"Halafu mbona tulikuwa tunakuona unaruka ruka mwenyewe mara uonekane kama unaongea mara uiname mara uinuke ulikuwa unafanya nini kule??.." aliuliza dereva jay.

"Jamani twendeni tawaambieni tukifika tunapoenda." nilisema nikiwa nafikiria cha kufanya nikawaza haraka haraka nikapata wazo.
"Eheeeh!!.. Halafu mbona hili gari lilikuwa linapinduka pinduka kama kuna watu walikuwa wanatusukuma?.. Huku kuna majini au?.." aliuliza rafiki yangu angel....ITAENDELEA...

Usikose Sehemu ya 32RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu Ya 32

TULIPOISHIA..
"Eheeeh!!.. Halafu mbona hili gari lilikuwa linapinduka pinduka kama kuna watu walikuwa wanatusukuma?.. Huku kuna majini au?.." aliuliza rafiki yangu angel....

SONGA NAYO...
Sikutaka kulijibu lile swali alilouliza, nilichofanya nikuwapulizia Moshi wakauvuta wote ukawatoa kumbukumbu zote za eneo lile.
Tukawa tunaendelea na safari huku tukipiga story tu za kawaida wote wakasahau kama waliona ajali na vile vitu vilivyotokea kule njiani gari kupinduka pinduka.

Hiyo siku tulitembea sehemu mbali mbali, mwisho tukapanga twende hifadhi ya taifa mikumi, kweli tukaenda hela nilikuwa nazo za kutosha niligharamikia kila kitu, Tukaicha gari yangu pale packing kisha Tunakapanda kwenye gari ya kubebea watalii aina ya 'LAND CRUISER WAR BUS 4×4!' Likawashwa Kisha tukaanza kuingia ndani ya mbuga za mikumi, Tulisimama juu tukawaona wanyama wengi huku tukipiga na picha, tulikuwa watu Saba, Marafiki zangu watatu na dereva wangu, Pamoja na mwenyeji wetu na dereva wa lile gari jumla tulikuwa saba.

Tulizidi kuingia ndani kabisa ya mbuga tukafika sehem rafiki yangu mmoja akataka kujisaidia haja ndogo, akamuambukiza na mwingine wote wakasema wanataka kujisaidia gari ikasimamishwa wakashuka ikabidi yule mwenyeji wetu awaelekeza kwenye kichaka kidogo wakaenda wakajisaidia, ila kipindi wanajisaidia nilihisi kuna kitu cha hatari kipo kule walipoenda Naam!!. Mashaka yangu yalikuwa sahihi kuna kiumbe wa ajabu aliwatokezea uso wake ulikuwa umetapakaa dam na alama za kupasuka pasuka nguo yake ilikuwa imechanika chanika halafu makucha yake yalikuwa marefu mnoo na alikuwa na rasi nyingi kichwani, mwili wake wote pamoja na ile nguo aliyokuwa amevaa vilijaa damu.

Marafiki zangu walishtuka baada ya kumuona yule kiumbe wakapiga kelele moja tu kisha wakanyamaza kimya mi na wale wengine tuliobaki kwenye gari tukakimbilia kule zilipotokea zile sauti ila hatukuwakuta.
"Mi nimewaelekeza waje hapa, wameenda wapi Tena?.." alisema mwenyeji wetu, Nikajaribu kuwatafuta kihisia walipo elekea ila sikuhisi chochote wala kuwaona.
Nilishindwa kuelewa kwanini siwaoni wakati nauwezo wakumuona mtu ata akiwa mbali, Tukaanza kuwatafuta pale kwenye lile poli na sehemu zingine zingine ila hatukuwaona.
"Watakuwa wameenda wapi Hawa?.." alionekana kubaha yule mwenyeji wetu huku akifikiria sehemu wanayoweza kuwa wameenda.

Tuliwatafuta hata tukajisahau gari tukaicha mbali, mara mbele yetu wakatokezea Simba watatu wakawa wanatusogelea, mwenyeji wetu akasema.
"Msikimbie turudini nyuma pole pole." Ila rafiki yangu mmoja aliyebaki na dereva wangu hawakuweza kuvumilia kabisa wakaanza kutetemeka huku yule rafiki yangu angel akanikimbilia akanishika kwa nyuma.
"Sasa wewe badala uende kwa wanaume unakuja kwangu" nilimuuliza angel ila sikuwa nafocus na swali langu focus yangu ilikuwa ilikuwa ni wale simba walionekana wananjaa hawakuonesha hata dalili yakutupotezea walionesha wanatutamani sana, Walizidi kutusogelea rafiki yangu angel na dereva wangu uvumilivu ukawashinda wakakimbia na yule dereva wa lile gari iliyotuleta na yeye akakimbia tukabaki wawili TU, na mwenyeji wangu alipoona wametufikia kabisa na yeye akachanja mbuga akatoka nduki, mi ndio nilikuwa karbu na wale simba kwahyo walikuwa wananifata Mimi, wale simba wakaachana na mimi wakawakimbiza wale waliokimbia, niliwaza nikitumia nguvu zangu naweza kuwauwa wale Simba ikawa tatizo jingine ila nikasema potelea pote nikaagiza upepo mkalii ukawafata wale Simba waliokuwa ndo wamemkamata mwenyeji wetu ili waanze kumtafuna sasa, mara upepo nilio watumia ukawakumba ukawapeleka mbali kabisa wale simba.

Mwenyeji wetu akabaki pale chini anahema kwa nguvu huku akishukuru mungu kwakuponea chupu chupu, walimjeruhi kidogo na makucha yao kipindi wamemshika.
Mi nilikuwa nawaza marafiki zangu walipo Nikajaribu kuwaangalia tena kwakutumia nguvu zangu ila sikuwaona niliona giza tu, nilizidi kushangaa kuwa kwenye hali ile nikampitia yule mwenyeji wetu nikamuinua nikamshikilia Kisha nikaenda nae hadi kule gari lilipo, tulikuta wamejificha ndani ya gari angel, dereva wangu, na dereva wa lile gari walionekana kuogopa sana.

Mwenyeji wetu akasema.
"Jamani turudini tulipotoka tukaombe msaada zaidi wakuja kuwatafuta hawa walipotea kimaajabu, inawezekana walikamatwa na wanyama wakawapeleka mbali wakawafanya msosi huko huko, dereva washa gari ugeuze turudi." dereva akamjibu.
"Gari haiwaki yani ingekuwa inawaka hata hapa msingetukuta tungekuwa tushaondoka."
"Kwahyo mngetuacha??.."
"We unacheza na kufa? Ndio tungewaacha."
Kipindi wanaongea vile mi mawazo hayakuwa pale kabisa nilikuwa nawasikia ila nilikuwa nawaza rafiki zangu walipo pelekwa.

Mara ghafla!!.. tukasikia kishindo kikubwa juu ya gari, walishtuka waliokuwa wanabishana wakainama chini, angel na dereva wangu wao walikuwa wamejificha chini kabisa huku wakiwa wanatetemeka angel alionekana amejikojolea kwa uoga tu.
"Huyo atakuwa ni simba au chui." alisema mwenyeji wetu akiwa ameinama chini, niliyebaki nimekaa kwenye siti ni mimi peke yangu.
"wewe dada nawe siulale chini unataka waondoke na kichwa chako?.." alisema mwenyeji wetu, mi nikamjibu.
"Sasa kila kitu mmefunga milango na vioo mmepandisha mpaka juu mnaogopa nini Sasa?.."
"Dadaa!!.. Hao viumbe ni hatari hata vioo wanaweza kuvunja we lala chini"
"Hata kama nikilala bado niyale yale wakivunja wakaingia ndani si bado tu taonekana." nilisema, huku mtikisiko wa gari ukizidi kuongezeka.

Nikaangalia juu ya gari lile kwa jicho langu la tatu, hakuwa Simba alikuwa ni yule kiumbe niliyemuona kwenye maono akiwachukua rafiki zangu wawili nikajisemea kimoyo moyo.
"Eheeeh!!!.. Huyu ndio nilikuwa namtaka sasa ngoja nimfate aniambie marafiki zangu wako wapi." nilisema huku nikijitoa mara mbili, mwili wangu ukabaki ndani ya gari, nafsi yangu ikatoweka nikatokezea juu ya lile gari.

Yule kiumbe Alishtuka! kidogo baada yakuniona nikiwa kwenye umbo lile.
"Niambie marafiki zangu umewapeleka wapi?.." nilimuuliza yule kiumbe.
"Hahahaha!!.. Huwezi kuwapata marafiki zako nimekuja kukushikisha adabu ili jue kuwa sisi hatuchezewi hata kidogo." alisema yule kiumbe, tulikuwa tunaongea sauti ambayo hawakuweza kuisikia waliomo ndani ya gari.

Sikutaka kusubiri alinipandisha hasira nikamrushia kombora takatifu akalikwepa likapita na mkono wake wa kushoto, ukadondoka chini ulitoa sauti kubwa hadi waliokuwa ndani ya gari walishtuka, mwenyeji wetu akaniangalia pale kwenye kitu nilichokuwa nimekaa akaniona nimelala akaniamsha.
"Wewe dada unapataje usingizi wakati tuko kwenye matatizo." alisema huku akinitikisa, nafsi yangu kule juu ya gari ikaanza kuishiwa nguvu maana alikuwa anautikisa mwili wangu. kule juu Nafsi yangu iliyeyuka ikatokezea kwenye mwili wangu.

"Wewe unaniamshia nini siuniache nilale??.." nilisema nikiwa na hasira ila sikutaka kuzionesha.
"Wewe unalalaje wakati tuko kwenye matatizo najaribu kupiga sim hapa zinaruka mtandao unakataa, wote humu wanaogopa ndomana nimekuamsha wewe ambae sio muoga unipe ushauri tunafanyaje??.."
"Tafadhali naomba uniache nilale kwanza kidogo nausingizi mkubwa mnoo kidogo tu tamka kisha takwambia chakufanya." nilisema akaonesha kushangaa kauli yangu akakubali kishingo upande akarudi chini alipokuwa.

Kule juu nikasikia sauti ya kile kiumbe ikisema.
"Hahahah!!.. Umeniogopa eeeh!!!.. Mbona umekimbia sasa??.." Mtikisiko ndani ya gari ulizidi kuwa mkubwa na niliona watu walivyozidi kutetemeka. Nikatoka kwenye mwili wangu nafsi yangu ikarudi juu ya lile gari.
"Nimerudi Sasa!!!.." nilisema..
"umeona nguvu zako ndogo ukaenda kuongeza sindio??.."
"Achana na hayo maswali niambie marafiki zangu wako wapi?.."
"Hebu angalia kwenye huu mkono wangu ulio ukata" niliangaliaa nikashangaa ule mkono ulikuwa umejiunganisha ukarudi kama mwanzo.

Nilishikwa na hasira nikamtupia kombora lililojaa moto akaruka sarakasi akarikwepa, na yeye akarusha kombora lake nikarikwepa pia kwakuruka tikitaka.
Hasira zikazidi kunipanda nikamrushia kile kisu changu kinachozunguka kama feni, kamwe kile kisu hakiwezi kukwepwa kilimkata kata mwili wote kuanzia vidole vya miguu mpaka juu kichwani kwenye nywele vipande vya nyama vidogo vidogo kama vile vyakupika vikadondoka kwa wingi chini, nikiwa najiandaa kurudi ndani ya mwili wangu mara nikaona vile vipande vya nyama vikipanda juu ya gari vikijikusanya taratibu taratibu ukajitengeneza mguu mara mguu mwingine ukajitengeneza tena mara kiuno kikajiunganisha na tumbo, kifua, mikono mwisho kikajiunganisha kichwa, kikarudi kama mwanzo, kikaanza kucheka.....ITAENDELEA..

Usikose sehemu ya 33

RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu Ya 33

TULIPOISHIA...
Mara nikaona vile vipande vya nyama vikipanda juu ya gari vikijikusanya taratibu taratibu ukajitengeneza mguu mara mguu mwingine ukajitengeneza tena mara kiuno kikajiunganisha na tumbo, kifua, mikono mwisho kikajiunganisha kichwa, kikarudi kama mwanzo, kikaanza kucheka...

SONGA NAYO...
Nilishangaa!!.. nikarudi nyuma kidogo, kilizidi kucheka huku kikijitingisha kichwa chake chenye manywele mengi.
"Huwezi kuniua kirahisi hivyo, Nimetumwa nije nikushikishe adabu nimeambiwa umewaziwia watu wetu wasifanye kazi Yao, Tena ukawauwa kabisa sasa lazima ulipe kwa ulichofanya, na marafiki zako nishawapeleka kuzimu wako wanaliwa nyama huko!!!.. Hahahaha!!.." kilizidi kucheka kwa zarau.

Kikajinyosha shingo vizuri mishipa ikasikika inalia kikakunja sura kikaanza kurusha makombora mfurulizo, nikaruka nikayakwepa kwa kasi ya hali ya juu kipindi natua juu ya lile gari nikakutana na kombora moja likanipata kisawa sawa likanirusha nikaenda kujibamiza kwenye mti mkubwa uliokuwa karibu na pale tulipo paki ile gari. Baada ya kujibamiza kwenye ule mti nikadondoka chini, Nilihisi kama kiuno kimevunjika, Wakati niko pale chini naugulia maumivu mara kile kiumbe kikatua karibu yangu kikawa kinanitazama huku kikicheka.

Kikainama chini kikanishika t-shirt yangu niliyokuwa nimevaa kikaniinua juu kwa mkono mmoja kisha kikanibamiza tena kwenye ule mti, nilihisi kila kiungo cha mwili wangu kimevunjika maana nilihisi maumivu makubwa sana nikadondoka chini kama limzigo, sikujua kilicho endelea nilikuja kushtuka kwa badae kidogo, Nikajigeuza pale kiuchovu nikatazama kule gari lilipokuwa limepaki nikaona moshi unatoka kwenye gari kama vile linataka kulipuka, Kwa kasi ya ajabu nikajiinua nikasimama Kisha nikapiga hatua za haraka kuelekea kule gari lilipo mara nikapigwa teke la kichwa nikadondoka chini, nikainuka haraka haraka ili nimuone aliyenipiga, Ni yule kiumbe ndio alikuwa amenipiga hakuwa ameondoka kama nilivyozani mwanzo.

"Hahahaha!!.. Unabahati umekuja kupambana kinafsi ungekuja na mwili wako ungekuwa umeshakufa." kilisema kile kiumbe huku kikizidi kucheka, ndio nikakumbuka kweli mwili wangu niliuacha kwenye gari ndomana hata sikuweza kufa maana nafsi haifi. Nikiwa nawaza vile mara nikasikia kikisema Tena.
"Pambana uokoe mwili wako pamoja na rafiki zako maana gari inaripuka mda si mrefu na huo ndio utakuwa mwisho wako utakufa mazima!!.. Hahahaha!!.." kilisema huku kikicheka.

Niliposikia maneno yale hasira zikanipanda nikafumba macho nikaikutanisha mikono kama vile nashukuru kisha nikaomba kwa hisia, baada ya sekunde kadhaa nikaona wingu jeusi kabisa likiwa karibu na macho yangu zilikuwa ni nguvu za aina ya wingu, nikaifunia mikono yangu lile wingu likaingia kwenye mikono, nikaacha yale maombi nikakitazama kile kiumbe kilichokuwa bado kinacheka kwa zarau, nikainua mkono mmoja juu nikamrushia lile wingu nikiwa nimelibadilisha nakuwa wingu sumu!!, likamvaa kama nguo alikuja kushtuka limeshamzingira na kumuingia kwenye mwili wake alijaribu kujisaidia rakini tayari alikuwa ameshachelewa lile wingu lilikuwa limeshamuingia mwilini, taratibu kila kiungo kikaanza kubadilika nakuwa kama lile wingu mwisho mwili wote ukawa wingu ukapotelea juu habari yake ikawa imeishia pale, Maana nisingetumia mbinu ile nisingeweza kumteketeza maana alikuwa ananguvu kubwa sana ndomana aliaminiwa na wale waliomtuma wakahisi hata yeye mwenyewe mmoja anaweza kuifanya ile kazi.

Nikanyosha mkono juu kuelekeza lilipoelekea lile wingu kisha nikatazama juu ya wingu ikaja kama picha nikawaona marafiki zangu wakiwa wamefungwa kwenye mti ambao hakuwa mbali na pale nilipokuwa nimesimama. Baada yakuona walipo nikaifunga ile picha kwa ishara ya mkono, nikazipiga hatua sasa ili niwafate kule, mara nikaona lile gari likizidi kutokwa na moshi mwingi, nikasogea hadi pale kwa lile gari nikawaona waliomo ndani ya gari wakihangaika maana walikuwa wamefunga hadi vioo na walishindwa kuvifungua rafiki yangu angel alikuwa ameshazimia dereva wangu alikuwa na hali mbaya ila alikuwa bado ananguvu kidogo na wale wenyeji wetu pia walikuwa wanaelekea kuishiwa nguvu, hawakuwa na uwezo wakuniona pale nilipo nimesimama, nikanyosha mkono wa kulia nikaukatisha ule moshi wote usiendelee kutoka kisha nikazipiga hatua kuelekea kule walipofungiwa marafiki zangu.

Baada yakupiga hatua kadhaa nikauona ule mti haukuwa mbali sana ila marafiki zangu sikuweza kuwaona maana walikuwa wamewekwa kimiujiza na ndomana nilikuwa nimeshindwa kujua walipo, Nikanyosha mkono kueleza kwenye ule mti nikanuia maneno kadhaa kisha nikakunja mikono, nikaangalia tena pale kwenye ule mti nikawaona wakiwa wamefungua mikono kwa nyuma ila kamba walizofungiwa hazikuwa zinaonekana kwa macho ya kawaida unaweza hisi walikuwa wanaigiza ila walikuwa wamefungwa kweli kweli, nikasogea hadi pale karibu yao kisha nikayatoa macho yangu kuyaelekeza kwenye ile mikono yao ukatokea mwanga kwenye macho yangu ukaenda hadi kwenye ile mikono yao zile kamba zikaonekana nikazikata kwakutumia ule ule mwanga. Wakashangaa!!..

"Heeeh!!.. Fetty!! mikono yangu imejiachia imefunguka!!" alisema rafiki yangu happy.
"Hata na mimi sielewi imekuaje, labda yule kiumbe amesikia kilio chetu akaona atuachie tu."
"Wewee!!.. fetty ona chui zile kule zinakuja huku tulipo, tuinuke haraka tuondoke."
"We usiogope wale chui hawatotuona siunakumbuka simba walipita hapa hapa na hawakutuona"
"Acha kujidanganya wale walikuwa wanatuona sana tu sema walikuwa wameshiba tu, Tuondoke haraka kabla hawajatuona. wakatugeuka msosi" alisema happy kisha wakainuka wakaanza kuondoka eneo lile, nilikuwa nawatazama tu maana nilijua hata ningesema kitu wasingeweza kunisikia, nikatoweka mahala pale nikatokezea kwenye gari nikaingia ndani ya mwili wangu.

Nikainuka sasa kama vile nimetoka usingizini.
"Heeeh!!.. We binti ndio unaamka saizi wenzako tunahangaika wewe umelala tu, nakuamsha hata uamki usingizi gani huo!! wewe unaweza kuuzwa ukiwa umelala." alisema yule mwenyeji wetu.
"Sasa kama usingizi ulikuwa umenizidia ningefanyaje?.." nilimjibu kisha nikatazama kwenye siti ya nyuma, nikaona dereva wangu akimpepea angel nikajifanya kama vile sijui nikamuuliza.
"Amefanyaje huyo?.." dereva wangu akanijibu
"Amezimia" Nikaunyosha mkono kumuelekezea angel kisha nikaurudisha. Baada ya dereva kumpepea kwa sekunde kadhaa akazinduka. angel baada ya kuzinduka akajiweka nguo yake vizuri iliyokuwa imepanda juu nakusababisha mapaja yake kuonekana, alikuwa anaona aibu maana alikuwa ananuka mikojo na harufu yake ilikuwa imetanda kwenye lile gari ila hakuna aliyemlaumu wala kumtenga maana wanajua waliyo yapitia kwa binti kama yeye mbichi mbichi ilikuwa ni ngumu kuvumilia kama wanaume tu ndo walikuwa na hali mbaya vile sembuse binti mlaini kama yeye, nikaipoteza ile harufu kwakutumia nguvu zangu..

Baada ya mda kidogo fetty na happy wakafika wakaanza kugonga gonga kwenye kioo, nikamwambia yule dereva.
"Fungua vioo na milango wenzetu wamekuja."
"Nishawaambia vioo havifunguki wala milango hamuelewi?.."
"We nisikilize mimi fungua" yule dereva alikuwa bado mbishi hakutaka kunielewa, nikainuka nikasogea hadi kwenye ule upande wake kisha nikavishusha vioo nikafungua na milango, alishangaa!! huku akiniangalia mara mbili mbili mi sikumjali, Marafiki zangu wakaingia ndani ya gari wakakaa kwenye siti.
"Nyie mlikuwa wapi??.. Tumewatafuta mpaka tumechoka."
"Hata tukiwaambia hamuwezi kutuamini mtahisi tunawadanganya kwahyo bora tusiwaambie tu imlad tumerudi salama tunashukuru mungu." alisema happy na fetty akasema.
"Dereva washa gari tuondoke turudi tulipokuwa huku hapafai."
"Gari haiwaki imegoma labda msubiri tushuke kwanza tukaangalie tatizo ni nini" alisema dereva nami nikamwambia.
"Nyie msishuke, washa gari tuondoke" dereva alinipiga jicho akaingiwa na kaimani kidogo kutokana na nilicho kifanya mwanzo.

Akawasha gari na ikawaka.
"Woyooooooo!!!.." mi na marafiki zangu tulipiga kelele za furaha, Yule mwenyeji wetu wakutuonesha wanyama aliduwaa maana alifikiria ilivyo wahangaisha kuwaka halafu niliposema mimi washeni na ikawaka alistaajabu akiwa anahisi mi sio mtu wa kawaida aliyatoa macho yake akiniangalia, na yule dereva alinipiga jicho kali akiwa ananishangaa pia!!. nami nilijua wanachowaza, sikutaka kusema chochote nilijifanya kama vile siwaoni......ITAENDELEA..

RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu Ya 34

TULIPOISHIA...
Yule dereva alinipiga jicho kali akiwa ananishangaa pia!!. nami nilijua wanachowaza, sikutaka kusema chochote nilijifanya kama vile siwaoni......

SONGA NAYO...
Dereva akaligeuza gari tukarudi, tukiwa kwenye gari tunarudi tunakawa tunapiga story mbili tatu huku kwakina happy wakisema kule kuna mashetani sio pazuri, wakaomba turudi tu dar. Baada yakufika tukashuka kwenye ile gari tukaenda kupanda kwenye gari yangu tukaondoka safari ilikuwa ni kuelekea dar, Baada ya mwendo mrefu kidogo tukiwa kwenye barabara traffic akatuambia tuweke gari pembeni kuna msafara wa muheshimiwa unapita, tukatii agizo tukaweka gari pembeni tukatulia pale kusubiria ule msafara upite kwanza, haikuchukua mda mrefu ule msafara ulipita alikuwa ni raisi wa awamu ile ndio alikuwa anapita, Watu walijaa pembeni ya barabara wakimshangilia na yeye alikuwa amesimama juu ya gari anawapungia mkono, wananchi wakawa wanamfata nyuma nyuma.

"Nasikia raisi atasimama kwenye ule uwanja wa pale mbele aongee na wananchi"
"Unauhakika?"
"Ndio nauhakika kwani hujafika kule kwenye uwanja?. Mi Nilienda na watu wamejaa wanamsubiria afike, Nasikia atahutubia halafu asikilize kero za wananchi."
"Kumbe!!. Twende Sasa."
"Mi naenda nyumbani kwanza kuna kitu nafata tangulia takukuta." Yalikuwa ni mazungumzo ya watu waliokuwa wamesimama karibu na gari langu wakitazama ule msafara unavyoishilia.

"Mmesikia hao watu wanavyoongea? Raisi atasimama hapo mbele." nilisema.
"Twendeni tukamsikilize maana namkubali hatari halafu nasiku sijamuona live nataka nimuone tena." alisema fetty
"Hakuna ambae hampendi huyu raisi labda mafisadi na wenye majipu yaliyoiva." alisema dereva wangu. Baada ya mda matraffic waliruhusu gari ziendeshwe, dereva wangu akawasha gari kisha tukafata msafara ulipoelekea baada ya dakika kadhaa tulifika kwenye ule uwanja, watu walikuwa wamefurika hakukuwa hata na nafasi kubwa watu walijazana kama utitiri, dereva akalipeleka gari pembeni kwenye magari mengine yalipowekwa kisha tukashuka tukasogea sogea kwakujibana bana ili tumuone vizuri raisi akiongea.

Alianza kuongea huku tukiwa makini kumsikiliza, akiwa anaendelea kuongea nilishangaa kuona watu wa ajabu, nikamshtua happy aliyekuwa amesimama karibu yangu nikamuonesha wale watu ila yeye alisema anaona watu tu wakawaida wakimtazama raisi, nikajua kabisa wale nawaona mi mwenyewe au labda watu wenye jicho la ziada ndo wanawaona.

Walikuwa wamejifunika kwaanzia kwenye kichwa mpaka kwenye miguu, walikuwa na manguo mekundu yenye mchanganyo na weusi, mmoja tu ndio alikuwa amevaa nguo nyeupe ila walikuwa wameficha sura zao zilikuwa hazionekani na walikuwa wanapita kwa watu waliosimama Kisha wanawashika pua wanawabinya halafu wanatega kakikopo frani hivi damu zinamiminika kutoka kwenye pua na kuingia kwenye kile kikopo, ajabu watu walikuwa hawashtuki wala kupatwa na tatizo lolote, Yule aliyekuwa amevaa nguo nyeupe ndio alikuwa ameshika chombo kikubwa ilikuwa kama ndoo hivi ila ilikuwa inaizidi ndoo kwa ukubwa ilikuwa kama diaba, Wale wenye manguo mekundu na meusi walikuwa wanatoa damu kwa watu na zile kopo zikijaa wanakuja kumimina kwenye ile diaba aliyokuwa ameishika yule mdada mwenye manguo meupe.

Nikasikia kwa mbali kidogo yule mdada mwenye manguo meupe akiulizwa swali na mmoja kati ya wale waliovaa nguo nyekundu.
"Vipi malkia Hulya hawa watu tulio wachukua na hizi damu vinatosha?.." yule mdada akamjibu.
"Vingekuwa vinatosha siningekwambia, unasemaje Vinatosha wakati hiki chombo hakijajaa dam?.."
"Malkia hadi tujaze?.."
"Unashangaa Nini?.. Eeeh!!.. Hadi mjaze hamjui kama kesho kutwa tunasherehe inatakiwa majini wa kishetani wanywe dam yakutosha, na nyama ziwe nyingi."
"Mi nahisi kama watu tulio wachukua ni wengi sana kwa nyama zenyewe zinatosha."
"Sawa nakuhusu dam je?.. Wale wote itawatosha?.. Halafu nishakwambia fata amri yangu mbona unakiburi sana unatoa wapi jeuri yakuhojiana na Mimi?.."
"Samahani malkia wangu." alisema yule mtu mwenye manguo mekundu huku akiinama kidogo nakukunja mikono. Alipo maliza kufanya hivyo alizipiga hatua akaondoka na kopo lake.

Nikamwambia happy.
"Happy simameni hapa hapa narudi mda si mrefu"
"Kwani we unaenda wapi?." aliuliza.
"Nakuja sasa hivi tu nyie simameni hapo hapo msitoke" nikazipiga hatua za haraka haraka kwajibana bana Kwa watu nikajiweka kwenye maumbile yakutokuonekana na watu waliokuwa wamesimama pale kisha nikasogea hadi alipokuwa amesimama yule mdada mwenye manguo meupe, pembeni kidogo kwenye uwazi.

"Mambo dada" nilimsalimia huku nikisimama mbele yake.
"Weeweeh!!.. Unaniona Mimi??.."
"Ndio nakuona kwani we ni nani hadi nisikuone."
"Mi sio binadam mi ni jini nashangaa unionaje?.."
"Mbona binadam wote waliosimama hapa wanakuona vizuri sema kila mtu yuko bize kusikiliza maneno ya raisi." niliamua kumshtua kidogo.
"Wananionaje?.."
"Mi ndio nimewafanya wakuone, na wanakuona vizuri tu unavyo wafanyia kuchukua dam zao halafu unawaacha wawe hai kwa mda ili wakifika makwao wafariki sindio?.. Ila nashukuru kwakulinda heshima ya raisi maana wakifia hapa atanyoshewa vidole yeye nakusemwa vibaya, kwa hilo nawashukuru ila nataka nikwambie, Mipango yenu imefeli." nilisema kumtisha tu na kweli mbinu ile ilizaa matunda na wakati anataka kujibu kitu nikaipoteza ile dam kimiujiza kikabakia chombo chake tu.

Alishtuka!!.. Baada yakuona hamna dam kwenye kile chombo alichokuwa amekiweka pale chini, alishikwa na hasira akajua mi ndio nimefanya vile, Ghafla!!. Akabadilika akawa nyoka mkubwaa akashusha kichwa chake ili animeze nami nikabadilika nikawa Tai mkubwa mwenye miguu mifupi, tukaanza kupambana sasa nikawa namdonoa kwenye kichwa namkwarua na makucha kila alipojaribu kunikamata alishindwa nikapatia nafasi pale pale nikaanza kumdonoa mwili wote nikamdonoa mpaka kwenye macho nikiwa juu juu kila alipoenda nilimfata mpaka nikamtoboa macho nikatoka nayo yote nikayatupa pembeni kabisa, Wale wenye manguo mekundu walikuwa wameshatuona wakaja baadhi fasta, malkia wao akadondoka chini akabadilika akarudi kwenye umbile la kibinadam, akawa anaugulia maumivu huku akishika sehemu yanapokaa macho.

Wale wenye manguo mekundu wakamtoa mikono wakagundua hana macho, wakakasirika Wakabadilika na wenyewe wakawa tai wakanifata kule kule juu hewani nilipokuwa, ila wenyewe walikuwa tai wadogo wadogo sio kama nilivyokuwa mimi wakanivaa wote kwa pamoja, wakanishika mabawa kila nilipojaribu kuyavuta nilishindwa wakayavuta kwa nguvu ili wanitoe kabisa nisiwe na mikono kama malkia wao alivyopoteza kiungo cha muhimu kwenye mwili wake.

Nikiwa kwenye umbile lile Nililivimbisha tumbo kisha nikajamba msuzi mtakatifu ukatoka na upepo mkaliii ukazipitia zile tai zote zilizokuwa zimenishika zikaenda kudondokea kwenye lile jukwaa alilokuwa amesimama raisi, ila hakuna aliyeshtuka wala kuwaona wale tai ila walianguka vibaya baadhi walifariki pale pale wengine wakabadilika na kuwa na umbo la kibinadam, wakawa wanaugulia maumivu.

Nikiwa kule kule hewani nikabadilika nikawa binadam mwenye mabawa, nikahisi kama kuna kitu kibaya kinaenda kutokea nikageuza shingo kuelekea kule walipokuwa wamesimama marafiki zangu nikawaona wale viumbe waliobakia kule chini mwenye manguo mekundu wakisogea hadi walipo marafiki zangu nakutaka kuwatoa dam.

Kwa kasi ya ajabu nikapiga mbawa nikatoka spidi hadi nikawafikia nikawatandika mateke ya mwana ukome wakadondokea mbali kabisa kama vifurushi vya mihogo habari yao ikashia pale, Nikatafuta baadhi walio salia salia nikawateketeza wote hadi wale waliokuwa wamedondokea kwenye jukwaa nikawaangamiza kisha nikamfata malkia wao akiwa anatapa tapa pale chini maana nilikuwa nimemjeruhi vibaya mnoo nikamuongezea na upofu kabisa.

Nikainama pale chini nikamshika vizuri kisha nikamwambia.
"Zilirudishe nafsi za watu wote ulio wachukua, najua unazo wewe."

"Hahaha!!... Nafsi nishazituma kwetu halafu Nakusikitikia sana umeingia kwenye vita ambayo hauiwezi hata kidogo, Mi ni mke wa mfalme wa majini na umenifanya hivi mke wake unategemea mme wangu atakaa kimya?.. Umeingia kwenye anga mbaya Sana!!.. Hahahaaaa!!...." alisema huku akicheka nikampiga kibao cha nguvu kisha nikasema....ITAENDELEA...

Usikose sehemu ya 35

RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu Ya 35

TULIPOISHIA..
"Hahaha!!... Nafsi nishazituma kwetu halafu Nakusikitikia sana umeingia kwenye vita ambayo hauiwezi hata kidogo, Mi ni mtoto wa mfalme wa majini na umenifanya hivi mtoto wake unategemea baba angu atakaa kimya?.. Umeingia kwenye anga mbaya Sana!!.. Hahahaaaa!!...." alisema huku akicheka nikampiga kibao cha nguvu kisha nikasema....

SONGA NAYO...
"Nachotaka ni nafsi za hawa watu zirudi sio maneno maneno yasio na kichwa wala miguu"
"Kwanza wewe ni nani unayetaka nafsi zao nakuharibu mipango yetu."
"Mi ni mtetezi wa watu, na staki mchezo kwenye hili."
"Hahahaha!!... Et mtetezi!!.. hahaaaa!!.. Hakuna unayeweza kumuokoa karibia nusu ya hawa watu tushawauwa." Alisema huku akicheka, Nikainua mkono kikatokea kisu kikiwa kinawaka moto, kisha nikamchoma nacho kwenye paja akaanza kupika kelele.
"Naongea unanichekea?.. Unanijua vizuri?.." Nikakichomoa kile kisu nikamdunga tena kwenye mguu mwingine, sikutaka kupoteza mda nikawa namdunga kote kote miguuni nikafata kwenye kiuno, alikuwa anapiga kelele sio za nchi hii, hadi ndege kwenye matawi zilikuwa zinakimbia ila Watu hawakuwa wanasikia chochote.

"Kama unataka uwe salama zirudishe nafsi za hawa watu" nilisema huku nikizidi kumdunga kwenye kiuno chote hadi sehem ya Siri, nilimdunga tena nikakikandamiza kabisa kile kisu nikaichana chana sehemu yake ya siri.
"Nazirudishaaaa!!!.. Nazirudishaa!!.. Niacheeeee!!..." alisema huku akilia.
"Usinipotezee mda haraka, zirudishe maana raisi anataka kuondoka na watu wataondoka." Akanyosha mikono yake miwili juu ikatokea kama chumvi nyeupee kwenye ile mikono yake kisha akairusha kuelekea kwa wale watu wote, nafsi zikarudi kwenye miili yao.

"Sisi sio chakula chenu, tafuteni chakula kingine sio sisi, mungu ametuumba na kutuleta duniani tuishi na siku akitaka kuturudisha alipotutoa ni yeye mwenyewe, nyie mnatufanya msosi kwa mamlaka ya nani?.. Mnasema et dam yetu ni tam zaidi ya juisi kwani nyie hamna dam msijitoe mwenyewe? Kama hamna basi ndo mpambane na hali zenu, Nakuacha hai nenda kampe taarifa mme wako na umwambie hichi nilichokwambia ole wako usimwambie takufata huko huko nikuangamize." Baada yakumaliza kuongea maneno yale ya vitisho yule malkia hulya alitoweka mahala pale baada ya Mimi kumruhusu, niliinuka kisha nikazipiga hatua za kuelekea walipo rafiki zangu.

Nikawashtua tukaelekea kwenye gari maana raisi ndo alikuwa amemaliza kuhutubia ndo alikuwa anaondoka.
"Yusrat hivi huhisi njaa?.."
"Mmh!!.. Mi mbona najihisi kawaida tu."
"Saa kumi hii inaenda saa kumi na moja, bado hatujaweka chochote tumboni, tutafute sehemu ilipo hoteli tukale maana nahisi utumbo unatetemeka." alisema angel, hoja iliyoungwa na wengine, Tukamsimamisha mtu mmoja tukamuuliza hoteli ilipo maeneo ya pale akatuelekeza. Tukapanda kwenye gari yangu tukaelekea kule alipotoambia, kwakuwa msafara ulikuwa umeshapita hakukuwa na jam njiani tukaingia kwenye lami kisha mataili ya gari yakaanza kuikanyaka ile lami kwa mwendo wa wastani baada ya dakika kadhaa tulifika lile eneo ilipo hoteli ilikuwa karibu na barabarani tukakata kona tukapaki gari tukashuka tukaingia ndani ya hotel, Baada yakufika kila mtu aliagiza msosi wake tukaanza kula, ila wakati tunakula nikashtuka kitu baada yakuona wahudumu pale wawili wakiwa wanatuangalia Sana, nilishtuka zaidi baada yakuwaangalia kwa jicho la tatu nikagundua sio watu wa kawaida walikuwa wanamaumbile ya nyoka na wale ndio walio tuletea chakula kile tulichokuwa tunakula.

"Jamani simshamaliza kula?.. Tuondoke hii sehem sio salama kabisa" niliwaambia marafiki zangu, mara mmoja wa wale wahudumu akaja hadi pale tulipokuwa tumekaa akachukua vyombo kisha akatuletea na bili tunayodaiwa nikamlipa ila wakati nampa Hela mkononi mwili wangu ulipigwa na shock, nikaganda kwa mda badae nikarudi kuwa sawa ila nilipowaangaza angaza wale wahudumu sikuwaona tena niliwaona wengine wengine tu, Mara muhudumu mwingine kabisa akaja.
"Karibuni sana menu hii yapa chagueni mnakula chakula kipi?.."
"Heeeh!!.." wote tulishangaa tukamuuliza.
"Dada nyie simmetuhudumia hapa na tumemaliza kula mda si mrefu na tukalipia?.."
"Hapana sisi hatuja wahudumia kwanza ndio mmefika sasa hivi nilikuwa nimekaa paleee ndo nawaona mnaingia mda huu nakukaa hapa."

"Heeeeeh!!!.." Marafiki zangu pamoja na dereva wangu walishangaa nami pia nilistaajabu.
"Jamani huyu dada atakuwa kachanganyikiwa tuondoke zetu." baada ya happy kusema hivyo tukainuka tukaondoka zetu yule muhudumu akabaki amesimama ameduwa ila mi nilihisi kitu sio hali ya kawaida ile, moja kwa moja tukapanda kwenye gari dereva akaliwasha tukaanza safari yakurudi dar.
"Jamani kuna watu wanaweza kuwa sehemu kimwili tu ila kiakili hawapo kabisa, Sasa kama yule mdada anasema kabisa 'Et nyie ndio mmeingia sasa hivi' Bosi wake angemsikia siangemfukuza kazi kabisa, inaonesha hayuko makini na kazi yake." alisema fetty hoja iliyoungwa na wenzake, mi sikusema chochote nilikuwa nawaza tu wale wahudumu waliotoweka pale ghafla halafu na yale maumbile Yao nikajua kabisa ile ni hatari.

Safari ilizidi kushika hatam baada ya mwendo kama wa saa moja tukiwa kwenye poli poli, nikasikia kelele zikitoka kwenye gari nikahisi labda nasikia mwenyewe.
"Jamani mnaisikia hii sauti inacheka?.." happy aliuliza ndo nikajua hadi wengine wanaisikia. Ilikuwa inaongezeka kadri ya sekunde zilivyokuwa zinazidi kusogea, Ikawa kero sasa.
"Jamani nini hiki au ndio lile shetani la kule polini limetufata hadi huku" alisema fetty akiwa ameziba masikio.
"Hapana sio lile hii ni sauti ya kike" alisema happy, sauti ilikuwa inazidi kuwa kali mpaka dereva akapaki gari pembeni na yeye akaanza kuziba masikio. Mi nilikuwa nauwezo wakuzimudu zile sauti ila nilikuwa nashindwa kuelewa zile sauti zilikuwa zinatokea wapi maana kila nilivyojaribu kuangalia kama kuna kiumbe chochote sikuona kitu.

Mara Angel akiwa amejificha chini kabisa kwa uoga akiwa ameshika na masikio yake kwa namna yakuyaziba akasema.
"jamani nahisi haja kubwa naombeni tutoke mnishindikize nikajisaidie." mara fetty akadakia.
"Jamani na mimi nahisi haja kubwa." happy na yeye akasema.
"Twendeni tu wote tukajisaidie maana nami najihisi hivyo hivyo pia" Nikiwa kwenye mshangao mara na dereva akasema.
"Jamani kile chakula tulichokula sio cha kawaida kuna vitu itakuwa wametuwekea, maana na mimi najihisi hivyo hivyo kama nyie."
"Sasa watuwekee vitu kwani wanatujua au wanaugomvi na sisi?.. Au kuna mmoja wetu anajuana nao na wanabifu?.." alisema happy.
"Jamani tusijadiri sana tutajinyea ujue!!! Tushukeni tuingie kwenye vichaka tukajisaidie" wakaanza kushuka mmoja mmoja wakatoka wote nikabakia mimi kwenye gari.

"Yusrat mbona we hushuki au we hujihisi kama sisi?.." aliuliza happy.
"Nyie nendeni mtanikuta hapa hapa kwenye gari tunaweza kutoka wote wakaiba gari" nilisema wakaelewa wenyewe wakaingia kwenye vichaka kwaajili ya kujisaidia, ila na mimi nilikuwa nahisi tumbo linasokota sokota ila nilijikaza tu, ile hali ya mtu kusikika anacheka ilikuwa imetulia sasa.

Baada ya dakika kama mbili nikiwa nimetulia kwenye gari nikashtuka baada yakusikia kelele moja tu ikiishia hewani nilikuwa naifahamu ile sauti ilikuwa niya angel, nikailock gari kila kitu kisha nikatoweka nikatokezea polini ile sehemu aliyoingia angel kujisaidia, nikaona kinyesi chake tu yeye hakuwepo pale, mara na wakina happy na fetty pamoja na dereva wakaja lile eneo wakiwa wanakimbia.
"Vipi imekuaje mbona tumesikia sauti ya angel halafu tunakuja hatumuoni, Ameenda wapi?.." aliuliza fetty.
"Mi mwenyewe sielewi alipoenda nimesikia kelele nikakimbia nikaja kuangalia kuna nini nashangaa simuoni."
"Hapana yusrat we utakuwa unajua alipo maana sisi tumekuacha kwenye gari inakuaje tunakuja tunakukuta hapa wakati kule ni mbali na sisi ndio tulikuwa karibu karibu ila tumekukuta wewe." alisema happy.

"Happy sikubaki kule kwenye gari nami nilizidiwa nikaja kujisaidia sikuwa mbali na hapa ndomana nimewahi kufika."
"Sawa tunafanyaje sasa kumpata maana isijekuwa yamemkuta kama yaliyotukuta sisi kule kwenye mbuga za mikumi?..." alisema happy ile nataka kujibu mara tukasikia sauti ya angel ikilia upande wa pili, nikatamani kutoweka ila nikashindwa kwa sababu nilikuwa na marafiki wangeniogopa wangeona nimetoweka ghafla vile na ni kitu ambacho hawajawahi kuniona nafanya vile.

Basi Baada yakusikia sauti ya angel tukakimbia wote kufata sauti inapolilia kadri tulivyokuwa tunazidi kukimbia ndivyo sauti ilivyokuwa inazidi kusogea, Ghafla wakati tukiwa tunakimbia kwa kasi!!! fetty akakanyaga sehemu akadumbukia kwenye shimo refu....ITAENDELEA...

Usikose sehemu ya 36
 
Agizo la majini 36-40RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu Ya 36

TULIPOISHIA..
Ghafla wakati tukiwa tunakimbia kwa kasi!!! fetty akakanyaga sehemu akadumbukia kwenye shimo refu....

SONGA NAYO...
Wote tukasimama, tukasogea hadi sehemu lilipokuwa lile shimo maana tulikuwa tunakimbia kwa kuachiana nafasi kwahyo ile sehemu aliyodumbukia ndio njia aliyokuwa anapita yeye, sehem ilivyokuwa inaonekana hapakuwa na dalili yakuonesha kama kuna shimo majani yalikuwa yamejaa eneo lile ndomana fetty hakuliona, tukachungulia ndani ya shimo.

Lilikuwa shimo refu mnoo hatukumuona fetty tuliona giza tu.
"Jamani ndo nini hiki tunafanyaje Sasa?.. Yusrat inamaana ndo tumempoteza Fetty?.. Staki kuamini mbona sielewi haya mambo yanavyoenda?.." alisema happy akiwa analia
"Tulia happy hatujawapoteza watarudi tu."
"Watarudi kiaje yusra? Ona fetty amedumbukia kwenye hili shimo refu hivi hata kama yuko mzima atatokaje Sasa?.." alisema happy akiwa analia, mara tukasikia sauti ya angel ikiongeza kulia safari hii ilikuwa inalia kwa nguvu kuliko mwanzo, Wote tukageuza shingo zetu kuelekeza inapotokea tukakimbia kuifata tukazidi kuongeza mwendo, Tukasimama ghafla!!.. Baada yakuona michirizi ya damu ikiwa imedondokea kwenye majani tukafatilia taratibu ilipoelekea tukaona imeingia kwenye kichaka kidogo, tukaingia ndani ya kile kichaka.

"Heeeh!!.. Yusra hii si nguo ya angel aliyokuwa amevaa juu??.." alisema happy kwa mshangao tukaiangalia vizuri kweli ilikuwa yenyewe sema ilikuwa imejaa dam.
"Jamani!!!.. Kimemsibu nini angel?. Au ndio ameuwawa" alisema happy.
"Njoeni kwa huku muone kitu" alisema dereva wangu tukasogea kuelekea kule alipo yeye ili tuone alichokiona yeye.
"Nini hiki?.." aliuliza happy.
"Sijui ni maini sijui ni dam iliyoganda hata sielewi" alisema dereva wangu.
"Jamani angel amekufa?.." alisema happy akiwa amejishika kichwa chake kwa mikono miwili.
"Hapana hajafa bhan we kuona dam tu ndo unahisi amekufa bado yuko hai." nilisema nikiwa nampa matumaini japo nilihisi inaweza ikawa ni kweli amefariki maana zile dam sio ishara nzuri.

Tukakivuka kile kichaka tukaendelea kuzifatilia zile dam upande wa pili zilikuwa zinazidi kwenda mbele ila ule upande yalionekana majani yamelala kama vile kuna kitu kilikuwa kinapita au kama sivyo basi angel ndiye alikuwa anapelekwa kwakuburuzwa, mara tukaona meno mawili yako chini kwenye dam zilizokuwa zinaendelea kwenda mbele.
"Heeeh!!.. Inamaana angel ametolewa hadi na meno?.."
"Acha na hayo meno njoeni muangalie hapa mbele" alisema dereva wangu tukasogea hadi pale.

"Heee!! Hee! Heeeh!!!. Jamani Si moyo huu?.. Au ni Nini?.."
"Ndio ni moyo tena unaonekana sasa hivi ndo umetolewa siunaona ulivyo bado unadunda dunda." alisema dereva wangu.
"Aaaaah!!!... Jamaniii!!.. Angel wangu amekufaaaaa!!!.. Aaaaahaaa!!!.. rafiki zangu jamani nyote mnaniachaa!!.." alisema happy akikaa chini na kuunguruma wakulia Lia, hata mimi machozi yalinitoka nikachutama chini niliamini kweli itakuwa angel amekufa. Hata ham yakusonga mbele tena ilikata kabisa maana zile sauti za angel kulia zilikuwa zimeshakata mda mrefu sasa.

Dereva wangu yeye hakukata tamaa alituacha pale kwenye ule moyo akasogea kwa mbele zaidi.
"Njoeni haraka muone hukuuu!!.."
"Heeeeh!!!." niliinuka haraka na happy akaacha kulia akainuka tukakimbilia kule alipo dereva wangu, tukamkuta angel amelala chini ametapakaa dam mwili mzima halafu juu alikuwa amevaa sindiria na sketi tu, nikakumbuka shati yake tuliiyona kule kwenye kile kichaka.
"Sasa hizi dam zote zimetokea wapi?.. Mbona haonekani kama ameumia sehem?.." aliuliza happy akiwa anamkagua kama kuna sehem ameumia.
Nikainama nami, alikuwa amelala kifudi fudi nikamgeuza nikishirikiana na dereva wangu, ndo tukaona majeraha sasa alivyoumia baada ya kumgeuza na kuwa Chali, nikamshika upande wa moyo, mapigo yake yalikuwa yanadunda kwa mbaali. Ndo nikajua ule moyo tuliyo uona kule sio wa kwake pengeni yule kiumbe aliyemchukua alituwekea njiani ili tuogope tukate tamaa yakusonga mbele, niliwaza hivyo.

nikamfunua mdomo nikamuangalia hakuwa na meno mawili ya mbele, na dam zilikuwa zimemjaa mdomoni, nikahisi alivyokuwa anaburuzwa alijigonga sehem ndo meno yake ya mbele yakatoka, alionekana amezimia.
"Mshikeni huko miguuni mi nimshike kichwa tumpeleke kwenye gari." alisema dereva wangu jay, mi na happy tukainama ili tumshike miguu, Ghaflaa!!!... kikatokea kiumbe cha ajabu kilikaa kama sokwe rakini kilikuwa na mapembe halafu kilitapakaa dam mwilini kilitisha sana.

Happy na dereva wangu jay baada yakugeuza shingo na kukiona kile kiumbe walishtuka!!.. wakamuachia angel wakakimbia mbio za sitorudi tena, hawakujua hata wanaenda wapi kila mtu alikimbilia njia yake. Mi nilibaki nimesimama nikimwaangalia yule kiumbe aliyekuwa anacheka kwa zarau.
"Kwahyo wewe ndio umemfanya hivi rafiki yangu sindio?.."
"Sio huyo tu hata yule aliyedumbukia kwenye shimo mi ndio nimemdumbikiza, lile ni shimo lakutengeneza tu nenda sasa hivi kama utalikuta!!!.. Hahahaaaa!!!.. haahaaaaa!!.." mwanzo kilianza kuongea vizuri mwisho kikaanza kucheka kwa zarau, ndo makosa kiliyo yafanya.

Nilirusha kisu changu kinachozunguka kama feni kikamfyeka shingo, kichwa chake kikadondoka chini kikiwa kimegandia kwenye cheko, Na mwili wake wote ukafyekwa vipande vipande habari yake ikaishia pale.
Nilifurahi kupata ile nafasi yakuwa mwenyewe, Nikanyosha mkono kuelekeza kwenye madonda ya angel nikayatoa yote akawa kama mwanzo, akaanza kukohoa ili amke. Ghafla!!.. wakatokea mabinti wanne walio valia nguo nyeupee, Nikamzimisha kwanza angel ili asiinuke nishughurike na wale kwanza.

"Hakuna adhabu inayo kustahiri zaidi ya kifo yani umempa upofu malkia wetu, na umemuumiza vile!!.. Tena hutakiwi kufa kifo cha kawaida inatakiwa kufa kifo cha mateso makali."
"Hiyo jeuri yakuniua hicho kifo mnaitolea wapi?.. Kama mnaweza njoeni mniue tukione hicho kifo." nilisema huku nikiwatazama.
"Hahahaaaaa!!!.. Hujijui kama hapo ulipo we ni mfu uliye hai, umekula chakula chetu na nyote bado kidogo tu habari yenu iishe, au umenisahau mimi muhudumu niliyewaletea chakula, hahahaha!!!.. Hahaaaaa!!.." alisema kwa sauti na wenzake wakaungana nae wakaanza kucheka wote, Nilishtuka!!.. Baada yakusikia maneno yale.

"Na mimi ndio nilikuwa nacheka kule kwenye gari na sababu ya nyie tumbo kusokota nikile chakula tulichowapa, na hiyo ni awamu ya kwanza bado awamu nyingine ya kuvuruga tumbo safari inayofata mnakufa mazima, Hahahaaaa!!.. Acha nikujuze tu sisi ndio tumewaleta kwenye hili poli ili tuwaangamize vizuri, hivi unajua wenzako wako wapi sasa hivi?.. Wako mikononi mwetu, hahahaha!!!.." Nilibaha baada yakusikia maneno yale ila sikutaka kuonesha kama nimeshtuka.

Wakati najiuliza maswali niliona vitu kama bini ndogo ndogo zikija kwenye macho yangu, kwa kasi ya ajabu nikainama chini tule tupini tukapita, tulikuwa tudogo sana kwa macho ya kawaida ilikuwa ni ngum kutuona.
"Hahahaha!!.. Mnataka mnitie ukipofu kama malkia wenu?.. Hili mmefeli mi sio mtu wa mchezo mchezo hii ngoma sio ya levo zenu." naona labda hawakuelewa nilivyosema mimi sio levo yao, wakarusha makombora yao mfurulizo nikapotea kimiujiza yakapita kama hamna kitu, Nikarudi nikiwa nacheka.

Wakajigeuza kuwa nyoka wakubwa kiasi chake nikawaambia.
"Jamani mbona mnarudia makosa, hivi malkia wenu hakuwaambia kilicho mfanya vile ni nini?.. Mi nawaomba tu bora mbadilike muwe hata viumbe vingine sio nyoka, mkiwa hivyo mnanirahisishia kazi" hawakutaka kusikia wakasogea ili wanigonge wote kwa pamoja nikatoweka wakagonga hewa.

Nikatokezea juu yao nikiwa Tai mkubwa nikaanza kuwadonoa kwenye vichwa vyao mmoja nikamtoa macho kabisa kama malkia wake, Wakavimbisha midomo yao wakanitemea mate nikayakwepa, Wakazidi kunipandishia hasira nikazidi kuwadonoa huku nikiwakwaruwa na makucha kabisa ili kuwashikisha adabu vizuri nyoka moja nikaimeza, zikabakia tatu walipoona hali inazidi kuwa mbaya wakabadilika wakarudi kwenye umbile la kibinadam wakiwa wanaugulia maumivu.

Nami nikarudi kwenye umbile la kibinadam nikaimana pale walipodondokea, kila mmoja akiwa anashika kiungo chake, wakataka kutoweka kimiujiza nikawatuliza chini, nikazivunja nguvu zao wote kisha sehemu walipodondokea nikaitengeza ikawa inawaka moto mkaliiiii.....ITAENDELEA...

Usikose sehemu ya 37..RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu Ya 37

TULIPOISHIA..
Wakataka kutoweka kimiujiza nikawatuliza chini, nikazivunja nguvu zao wote kisha sehemu walipodondokea nikaitengeneza ikawa inawaka moto mkaliiiii.....

SONGA NAYO..
Ule moto uliwateketeza taratibu, kila walivyotaka kutoweka walishindwa hadi wote wakateketea wakageuka kuwa majivu.

Baada ya kumaliza ile kazi nikamuamsha angel, akaamka akiwa anajishangaa mara akainuka haraka haraka akasimama akanikumbatia huku akionekana kuwa na uoga mwingi.
"Anataka kuniua!!!... anataka kuniuaaaaa!!..." alisema angel akiwa amenidandia kwa uoga.
"Nani huyo anataka kukuuwa?"
"Sijui ni linani ila linatisha Sana!!.."
"Usijali haliwezi kukuuwa mi nipo Kwaajili yakukusaidia." nilisema halafu nikatoweka nae kimiujiza tukatokezea ndani ya gari, Alishtuka!! Huku akishangaa kujikuta ndani ya gari wakati tulikuwa polini, aliniogopa! akaanza kusogea mwisho kabisa wa siti, nilihisi kama yale matukio yakumuona yule kiumbe na jinsi alivyotokezea ndani ya gari yanaweza kumtesa sana angel, nikamshika kichwa nikazifuta kumbukumbu zote za yale matukio asiyakumbuke kabisa baada yakumaliza kufanya hivyo nikautoa mkono. akashtuka!!.. Baada yakujikuta yuko pale na Mimi akasema.

"We yusra wengine wako wapi mbona siwaoni?."
"Mi sijui naona umerudi wewe peke yako wengine hujaja nao labda nishuke nikawaite." nilisema nikitumia mbinu ile yakumtoka.
"Usitoke ndani ya gari kaa humo humo naenda kuwaita tu harafu narudi nao."
"Haya sawa." aliitikia angel nikaingia ndani ya poli, moja kwa moja nikaenda hadi kwenye lile shimo alilodumbukia fetty, Ila sikuliona lile shimo ndo nikakumbuka maneno ya yule kiumbe lile shimo halikuwa la kawaida lilikuwa la kutengenezwa.

Nikanyoosha mkono kuelekezea pale chini lilipotokeaga shimo, mwanga nilio utoa kwenye mkono ukaenda kukugusa pale chini, shimo likatokea kisha nikazama ndani ya shimo.
Baada ya dakika moja nikarudi juu nikiwa nimemshikilia Fetty na mikono, alikuwa amezimia nikamlaza chini. Kisha nikausogeza mkono wangu karibu na uso wangu nikatazama video iliyojitokeza kwenye mkono wangu.

Nikamuona dereva wangu akiwa na happy wamewekwa mtu kati na nyoka nne hazikuwa zinawang'ata zilikuwa zinawatisha tu, zilitengeneza kama duara halafu zikawa zimesimama vichwa zimewaelekezea wao. Jay na happy walikuwa wamesimama katikati wakionesha kuogopa Sana, Nilipo angalia vizuri nikagundua wale sio nyoka bali ni sanamu tu walizoziacha wale wadada nilio wateketeza na moto na mmoja nikammeza, walifanya hivyo ili kuwatisha tu wasitoke.

Nikatoweka mahala pale nilipokuwa nikatokezea kule walipo jay na happy, Nilijiweka umbile la kutokuonekana nikawapoteza wale nyoka wote, happy na jay wakashtuka baada yakuona zile nyoka hazipo wakaanza kukimbia kuelekea kule tulipo paki gari. Nami nikatoweka nikatokezea pale nilipo mlaza fetty nikamnyanyua kisha nikatoweka nae nikatokezea nyuma ya gari langu, nikamuamsha fetty akazinduka akasimama akiwa na maruwe ruwe nikamshika kichwa nikamtoa kumbukumbu zote mbaya alizopitia, tukiwa tumesimama pale mara tukawaona happy na jay wakija kwa mwendo wa Kasi, nikawakimbilia ili niwawahi kabla hawajafika pale kweli nilifanikiwa nikawasimamisha.

"Yusra tuache twende kwanza tukiwa ndani ya gari tutakwambia yaliyotukuta huku sio pazuri kabisaa!! twende!.." alisema happy akiwa anapumua kwa Kasi, Nikawashika vichwa vyao nikawatoa kumbukumbu zote mbaya kisha nikawaachia.
"Yusra vipi wakina angel wameshatoka kujisaidia?.." aliuliza happy.
"Ndio wamesharudi fetty yule pale nyuma ya gari amesimama na angel yuko ndani gari ni nyie tu ndio tulikuwa tunawasubiri." nilimjibu kisha tukasogea hadi ilipo gari tukapanda wote pamoja na Fetty niliyekuwa nimuacha nyuma ya gari amesimama.

"Jamani wote simmemaliza kujisaidia twendeni Sasa." nilisema tukiwa ndani ya gari wote wakaitikia dereva akawasha gari tukaondoka hakuna hata mmoja aliyekuwa anakumbuka yote yaliyotokea kule polini, tulipiga story na kufurahi huku safari ikiwa inaendelea.

Baada ya mwendo wa hatua ndefu kidogo, dereva akaitoa gari barabarani akaiweka pembeni kando ya Barabara.
"We jay mbona unatoa gari kwenye Barabara??.." nilimuuliza.
"Tumbo linaniuma sana siwezi kuendesha kama kuna mtu anaweza aje aendeshe tuendelee na safari." alisema akiwa amelishika tumbo lake.
"Jamani mi najua kuendesha ila nahisi na mimi tumbo linaniuma." alisema happy.
"Heeeh!!.." wote wakaanza kulalamika tumbo huku wakiwa wameyashika matumbo Yao, nilishangaa mara na mimi nikahisi linaanza kunisokota, nikakumbuka maneno ya yule mdada jini aliyejigeuza muhudumu kule hotelini. Nikaona lile jambo alilosema linaweza kwenda kutimia, Nikachukua mkoba wangu nikajifanya natoa kitu.

"Jamani kile chakula tulichokula kule nahisi sio kizuri ndo kinatuletea haya matatizo ya tumbo chukueni hii dawa mnywe hii dawa inatoa uchafu wote mwiliini nilitembea nayo kama bahati tu nilipewaga na bibi..." kabla sijamaliza kuongea tayari walikuwa walishaninyankuwa wakaanza kunywa kwakupokezana mi sikuwa na shida sana maana ile sumu nilikuwa nauwezo kuitoa kwa njia yoyote Ile na ile dawa niliitengeneza kimiujiza pale pale halafu nikadanganya kuwa nilipewaga na bibi.

Baada ya kunywa ile dawa wakaanza kuhisi kama kichefu chefu, mmoja mmoja akawa anatoka kwenye gari anaanza kutapika Hadi wote wakaenda nje kutapika. Tulikuwa tumetembea na maji wakajisafisha kisha wakapanda kwenye gari tukaendelea na safari, ile sumu iliyoingia mwilini wangu kwa njia ya chakula nilichokula kule hotelini, baada yakuhangaika sana mwilini wangu iliteketea yenyewe maana ilikuwa haina nguvu kwenye mwili wangu.

Tulifika dar usiku kabisa marafiki zangu waliifurahia sana ile safari wakaomba kesho yake twende sehemu nyingine, nikajisemea kimoyo moyo.
"Mngekuwa mnakumbuka yaliyo watokea msingekuwa hata mnafurahi hivyo wala ham yakusafiri tena msingekuwa nayo."

Siku hiyo ikapita ikaingia siku nyingine wakina happy wakaniomba twende sehemu nyingine nikakataa nilichokuwa naogopa ni kuwasababishia matatizo mengine maana walipata mateso kwaajili yangu sema hawakuwa wanakumbuka chochote niliwaza kama mmoja angepoteza maisha ingekuwa mi ndio nimesababisha, kila walipo omba watoke na mimi nilikataa kwakuwa mi kila sehemu napoenda mara nyingi matukio ya ajabu yanatokeaga na wale watu ninao pambana nao wakionaga wamenishindwa mimi wanawazuru watu wangu wakaribu ili wanipate kiurahisi ndo nilichokuwa naogopa hicho.

Siku zilizidi kwenda huku yale majini niliyo yaulia malkia wao yakizidi kunifata, siku moja nikiwa nimelala walinitokezea majini sita wakiwa wanasura za kutisha wote walikuwa ni wanaume, nilijaribu kupambana nao lakini hiyo siku walinizidia nguvu maana walikuwa wananguvu nyingi sana tena walikuwa wameziunganisha nguvu zao ndomana ilikuwa ngum kupambana nao, baada yakunizibiti walinichukua wakanipeleka moja kwa moja kwenye mji wao wa majini unaoitwa trofi ule mji ambao baba na mama waliagizwa wakaichukue remote kwa mfalme wa kipindi kile halafu waizime!!, ndo nilipelekwa kwenye huo mji, na nachuoni ilikuwa inatakiwa kesho yake niingie darasani.

Nilipelekwa nimezimia kutokana na kipigo kikubwa walichonipa, nilikuja kushtuliwa na dam niliyomwagiwa kichwani nikafumbua macho nikaona lipande la mtu lililo jazia likiwa mbele yangu, nikaangaza angaza kuangalia nilipo, nikaona niko kwenye chumba kilicho tapakaa dam kila pembe ya chumba kile halafu nilikuwa nimefungwa minyororo mikononi pamoja na miguuni, nilikuwa na bembea juu juu.

Wakati nashangaa shangaa nikapokea ngumi ya shavuni nikadondosha dam ile sijakaa sawa nikapigwa nyingine kwenye shavu la pili nilitembezewa kichapo kikali hakujali anapiga wapi alinipiga mwili wote hadi nikahisi matiti yangu yanataka kuchomoka aliyabonda bonda kisawa sawa.

Alisitishwa kunipa kichapo kile na sauti yakiume iliyokuwa inaingia kwenye chumba kile.
"Umeshamtepetesha kisawa sawa?.."
"Ndio mtukufu wangu mfalme damor nimeshafanya hivyo." alisema yule kiumbe aliyejazia akiwa anainamisha kichwa chini ishara yakumpa Salam, nilishtuka kidogo baada yakusikia jina lile likitajwa maana mama alishawahi kunitajia hilo jina kwahyo nililikumbuka vizuri.

"Wewe ndio umemtia upofu mke wangu halafu ukaharibu sehemu zake za siri ili asinizalie mtoto sindio?.." alisema yule mfalme damor akiwa na sura ya hasira, sikujibu kitu nilishtukia kitu kinapenya katikati ya tumbo langu nikashusha kichwa chini kuangalia kilichonichoma tumboni ni nini.
Nikaona ni chuma chenye tumisumari tulio chongoka, mfalme akazidi kukizamisha ndani kwa nguvu akiwa amekunja sura, nilihisi maumivu makali sana ila nikajikaza, maumivu yalizidi zaidi pale alipokizungusha kile chuma...ITAENDELEA...

Usikose sehemu ya 38RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu Ya 38

TULIPOISHIA..
Nikaona ni chuma chenye tumisumari tulio chongoka, mfalme akazidi kukizamisha ndani kwa nguvu akiwa amekunja sura, nilihisi maumivu makali sana ila nikajikaza, maumivu yalizidi zaidi pale alipokizungusha kile chuma...

SONGA NAYO..
Nilihisi utumbo unakatika nililia kichini chini huku nikikunja sura yakuugulia maumivu, mfalme damor akiwa anaendelea kunizungushia lile lichuma mara akaingia mdada akiwa ameshikiliwa mkono na mtu, baada yakumtazama vizuri ndio nikamkumbuka ni yule mdada niliyemtoa macho yote mawili.

"Mme wangu naomba nimuadhibu mwenyewe ili nipoze machungu yangu." alisema yule mdada akiwa haoni, yule mtu aliyemleta akamsogeza hadi nilipo mimi, damor akasogea pembeni ili kumpa nafasi mke wake na yeye anitese. Yule mdada ambae ndo malkia wa mji ule wa trofi akanishika maeneo ya uso kwa style ya kunipapasa kisha akasema.
"We unamacho mi sina macho unaonaje hayo macho yako ukanipa Mimi?.." alisema yule malkia, sikumjibu kitu nilikaa kimya akaendelea kuongea.
"Uwezo wakupata macho mengine nilikuwa nao ila niliyakataa macho yote kwasababu nilikuwa nayasubiri macho yako wewe uliyenitoa ndo unipe." Alisema huku akinipapasa papasa akaishusha mikono yake hadi chini akazishika sehemu zangu za Siri kwakuziminya minya huku akisema.

"Za kwako ni nzima ila za kwangu zimeharibika, unaonaje tukiwa sare sare yani na za kwako tukaziharibu mmmh!! Etii!!.." alisema yule malkia huku akikenua kenua meno kama vile anaongea kimasihara masihara.
"Bogi naomba uniangalizie hapo siraha nzuuri yakumtolea macho huyu mrembo na nyingine yakumfanya awe kama mimi huku chini kwake." alisema malkia yule, yeye mfalme damor alikuwa amesimama pembeni anashuhudia tu mke wake anachotaka kufanya hakusema chochote alikuwa kimya.

Yule bogi akasogea sehemu zilipo siraha akachagua anayoona itamfaa malkia wake baada yakuipata nzuri akasogea hadi pale akiwa ameishikilia ile siraha akafika anampa malkia kwakumshikisha kwenye mkono. Kilikuwa ni chuma kilicho chongoka kama sindano.
Malkia akanigusa sehemu zangu za siri kisha akasema
"Tunaanza na huku kwanza ili uwe unajiona kipindi dam zinakutiririka." alisema huku akikichomeka kile chuma kwenye uke wangu, alifanya kama anachoma choma kwa nguvu akachomoa akachoma kwa juu kidogo ya uke na niya yake alikuwa anataka kuitoa nyama yote kabisa.

Ila kila alivyochoma ile chuma haikuweza kupenya kwenye ngozi yangu ilikuwa inadunda tu kila alivyojaribu tena na tena alishindwa sehemu zangu za siri nilizibadilisha zikawa ngum zaidi ya jiwe kwahyo kila alipojaribu kunichoma kile chuma kilishindwa kuzama kabisa.
"Mke wangu leta hiyo siraha nikusaidie we sogea pembeni kidogo" alisema mfalme damor akapewa ile siraha na yeye akawa anajaribu kunichoma ila alishindwa wote waliokuwemo mule ndani ya kile chumba walijaribu jaribu ila hawakuweza ikaletwa siraha nyingine tena kali zaidi ya Ile lakini bado ilishindwa.

"Mke wangu tuachane na hilo swala lakumfanya awe kama wewe maana limeshindikana, we tumtoa tu macho halafu tumuuwe habari yake itakuwa imeishia hapo, we hilo tatizo ulilopata hata lisikupe shida utatibiwa utapona tu." alisema mfalme akiwa anambembeleza mke wake, malkia akamuelewa akatikisa kichwa kuashiria amekubaliana na wazo la mme wake.

Mfalme akasogea hadi karibu yangu akiwa ameshikiria chuma mkononi, akakichomeka kwenye jicho langu moja kwa nia yakulitoa, akagusa kila engo anazojua yeye lakini jicho halikutoka akajaribu tena na tena lakini alishindwa, akaachana na lile jicho la kulia akaja kwenye jicho la kushoto lakini bado mambo yalikuwa yale yale wote ndani ya kile chumba wakajaribu lakini hawakuweza.

"Mke wangu utayapata macho mengine achana haya, maana huyu mtu sio wakawaida haiwezekani kila tunachofanya tunashindwa wakati tumemfunga minyororo ili nguvu zake zisifanye kazi lakini bado tu hatuwezi kumzuru, chakufanya hapa anyongwe tu" alisema mfalme damor na mke wake akakubaliana na wazo lake maana alikuwa anasikia walivyokuwa wanahangaika kunitoa macho ila wakashindwa. Nikakumbuka sababu iliyofanya mwili wangu uwe vile, ilikuwa hivi baada ya mfalme kuchomoa lile lichuma alilokuwa amenichoma nalo tumboni, Kutokana na nguvu iliyomo mwilini mwangu utumbo wangu ukajiunga maana ulikuwa unaelekea kukatika kutokana na lile lichuma kuukata, kisha mwili ukajirefresh maumivu yote niliyokuwa nimeyapata yakaisha ngozi ya mwili wangu ikajiwekea protector ndomana walishindwa kupitisha tena chuma chochote ndani ya mwili wangu.

"Bogi nenda kapige kengere ya dharula majini wote waje wamshuhudie mtu aliyemtoa macho malkia akinyongwa hadharani." alisema mfalme damor, bogi bila ajizi akafata amri ya mfalme wake akaenda, baada ya dakika kadhaa akarudi.
"Mtukufu mfalme nimeshapiga kengere majini wameshaanza kuja kwenye uwanja wakunyongea." alisema bogi.
"Haya mfungue huyo twende tukamnyonge mbele ya majini wa trofi." bogi akanifungua kisha akanipeleka hadi kwenye ule uwanja wakunyongea majini wenye makosa makubwa.

Majini walikuwa wamekuja kwa wingi kunishuhudia, nikasogezwa hadi karibu na kitanzi.
"Huyu binadam ndiye aliyeharibu mpango wa mke wangu wakupata dam ya sherehe yetu na amesababisha hadi sherehe yetu imehairishwa maana hatuna chakula chakutosha wala hatuna damu yakutosha na kingine huyu ndiye aliyemtoa macho mke wangu kipenzi, Sasa namrisha awekewe kitanzi anyongwee" alisema mfalme damor Majini wakaripuka kwa furaha wakifurahia mi kunyongwa.

Nikapandishwa juu nikasimamishwa juu ya kiti, kitanzi kikawekwa kwenye shingo yangu kisha kiti kikatolewa, kile kitanzi kikaanza kunikaba, wale majini walizidi kupiga kelele ya furaha huku wakishangilia kabisa.
Ila mi sikuwa nahisi chochote yani kama vile tu shingo yangu haikuwa imeguswa na kitu chochote nilikuwa najiona kama nabembea tu, sekunde na dakika zikazidi kusogea, watu walishangaa!!!.. kuona hata sifi, nikacheka kwa zarau
"Hahahaaa!!!... Hahahahahaha!!.."
Mfalme alishtuka! baada yakusikia cheko langu maana waliokuwa wananiona vizuri ni majini waliokuwa kwa mbele yangu, yeye hakuwa ananiona usoni maana walikuwa wamekaa kwa nyuma, akainuka pale alipokuwa amekaa akastaajabu akasogea hadi kwenye kitanzi akashuhudia nikikenua meno nikicheka, tena nilivyo na zarau nikamtembea mate usoni, majini wakashika vichwa kushangaa lile tukio la kuwa hai kwenye kile kitanzi ambacho kiliuwa Kila ambae kilimgusa shingo yake, wakazidi kushangaa tena baada ya mimi kumtemea mate mfalme wao katiriiii.

Mfalme damor alishikwa na hasira, akamuita bogi.
"Bogii njoo mshushe hapa nimkate kichwa chake mi mwenyewe niletee na panga." bogi akaenda hadi kwenye kile chumba nilichokuwa nimefungiwa mbio mbio akarudi akiwa na panga mkononi maana kile chumba kilikuwa na kila aina ya siraha.
Nikatolewa kile kitanzi nikashushwa chini, nikiwa nimesimama kichwa changu kikainamishwa chini. Mfalme akaushika upanga vizuri akaupandisha juu kisha akaushusha kwa nguvu kwenye shingo yangu, upanga ukadunda kama mpira ukamponyoka mfalme ukaenda kudondokea mbali kabisa, majini waliokuwepo pale walishtuka!!.. Huku kila mmoja akibaki mdomo wazi wengine wakashika vichwa vyao kwa mishangao tu.

"We bogi unanileteaje panga butuuu?.. Kalete panga kaliii halafu upite na magereza uje na mfungwa mmoja"
"Sawa mtukufu mfalme" aliitikia bogi kisha akaondoka, mfalme alikuwa na walinzi wengi ila alimpenda sana bogi ndomana mda mwingi alikuwa nae na alikuwa anamtuma yeye maana alikuwa anamuamini sana.

Baada ya dakika kadhaa bogi akarudi akiwa na panga mkononi pamoja na mfungwa mmoja akafika anampa banga mfalme kisha akamsogeza na yule mfungwa.
"Muinamishe chini huyo mfungwa" alisema mfalme damor na bogi akatii akamuinamisha, mfalme ili kujaribisha kama lile panga ni kali akamkata kwanza yule mfungwa shingo, panga likapita kama halijagusa kitu, kichwa cha yule mfungwa kikadondoka chini huku dam zikiruka, panga lilikuwa kali sana.

Mfalme damor alipojirisha kuwa lile panga nikali akamrisha na mimi nisogezwe nikainamishwa tena, safari hii alijikakamua kwa nguvu zake zote akaushusha ule upanga kwenye kichwa changu ukadunda tena ukamponyoka ukaenda hadi kwenye ule umati wa majini ya trofi ukamchoma mmoja wao, akakatika katikati....ITAENDELEA....

Usikose sehemu ya 39

RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu Ya 39

TULIPOISHIA...
Safari hii alijikakamua kwa nguvu zake zote akaushusha ule upanga kwenye kichwa changu ukadunda tena ukamponyoka ukaenda hadi kwenye ule umati wa majini ya trofi ukamchoma mmoja wao, akakatika katikati....

SONGA NAYO...
Mfalme alishangaa ile hali yakushindwa
kunichinja shingo yangu, hata majini wote waliokuwepo pale walistaajabu sana. Mara ghafla!!.. Nikaona majini wote wameganda kama sanam nikageuza shingo kuwaangalia na wengine kama wako vile, wote hakuna ambae alikuwa anaweza hata kujitikisa.

Ghafla!!.. Wakatokea baba na mama nikiwa na shangaa shangaa wakasogea hadi karibu yangu wakanishika mikono Yao kisha tukatoweka eneo lile. Tukatokezea dar nilipokuwa naishi karibu na chuo nilichokuwa nasomea, baada yakufika baba na mama wakanikarisha chini wakaanza kuniambia.
"Sisi tulijua uko unaendelea na masomo, kumbe ulikuwa umetekwa na majini?.."
"Ndio, walifanya hivyo baada yakumzuru malkia wao aliyekuwa anaua na kutoa dam za watu hapa duniani."
"Sawa, sisi tumekuja kujua baada yakupigiwa sim na mwalim akisema imepita wiki sasa haujaingia darasani ndomana akatupigia kutupa taarifa, baada yakupata ile taarifa ndo tukaanza kukutafuta sasa kwenye sim ila ukawa hupatikani ndo tukakutafuta kwakutumia nguvu zetu, ndo tukakuona umetekwa kwenye mji wa trofi."
"Shukrani sana wazazi wangu"
"Usijali yusra tuko pamoja na wewe bega kwa bega, endelea kusaidia watu ukizidiwa sehem uwe unatuita tunakuja kukusaidia." alisema baba.
"Sawa nimewaelewa" niliwajibu, baada ya kupiga story kadhaa wa kadhaa waliondoka kwakutoweka nikabaki mwenyewe.

Siku zilizidi kwenda miaka ikakatika hadi nikamaliza chuo, baada yakumaliza chuo nikaona sasa nitembee mikoa tofauti tofauti ili nisaidie watu wanaoteswa na wachawi, majini mashetani na kadharika, nimetembea mikoa tofauti tofauti hadi nimefika kwenye mkoa huu wa tanga eneo hili la bombo ndo nikakutana na wewe roy kiukweli nimetokea kukupenda sana sijawahi kupenda kabla ndo mara ya kwanza napenda...." alimaliza kuelezea yusrat story ya maisha yake pamoja na wazazi wake.

******************
Ilinisisimua sana ile story ilikuwa ni siku ya pili sasa toka aanze kunisimulia, kwakuwa hakiba ya pesa nilikuwa nayo yakutosha haikuwa tatizo kabisa tulikuwa tunapika tunakula huku anaendelea kusimulia hadi Ile story ikaisha.

"Duuuh!!.. Yusrat kipenz changu, uliyopitia ni mengi mnoo hongera kwa ujasiri ulio nao."
"Kawaida tu hii ndio kazi yangu, kwahyo nishaizoea"
"Sasa mi nataka nikuulize kitu, hiyo kazi unayofanya anakulipa nani sasa?.."
"Sikia roy hii kazi siifanyi kwaajili yakulipwa nafanya kwa mapenzi yangu tu na kuhusu maswala ya pesa wale majini wa mji wa jozi huwaga wananileteaga hela za kutosha pamoja na dhahabu nyingi tu navikutaga ndani ili nizidi kutekeleza agizo la wale majini wazuri na wenye roho ya utu, naona zile Hela nazokutaga ndo wanazifanya kama malipo yangu ila mi hata wasingekuwa wananiletea ningeendelea kufanya tu maana napenda kusaidia watu."
"Ooh!! Sawa hongera"
"Asante roy Wangu" alijibu yusrat.

**********
Kule Kwenye familia yakina juma, baada ya tangazo ile siku kutolewa kuwa yoyote anayejua ndugu wa marehemu baba juma au mke wake aende kutoa taarifa kwa mwenyekiti. Hakuna ambae aliyejitokeza hadi ikaamuliwa miili ile izikwe kiserikali, na kweli mazishi yalifanyika kiserikali. Na haya yote mi nilikuwa nayoona baada ya yusrat kunionesha mwanzo mwisho ilivyokuwa.

"Yusrat hivi kwanini unionesha matukio ya hii familia wakati hata sina undugu nayo?.."
"Ndio wale walio fariki huna ukoo nao ila dam ipo..."
"Dam ipo kiaje mbona sikuelewi."
"Yani yule mtoto wakiume waliyemuacha, anayeitwa juma kila nikitazama naona dam uliyonayo wewe na yeye anayo hiyo hiyo."
"Niweke wazi sasa mbona unazidi kunichanganya, ndio najua kila mtu anadam hata wewe pia unadam maana nusu ni jini na nusu ni mtu sasa unataka kumaanisha Nini?.."
"Namaanisha hivi, yule juma anaweza kuwa ni mdogo wako" alisema yusrat.
"Mmmh!!.. hapana sio mdogo wangu maana mama ake kipindi ameachika kwa baba hakuwa na mtoto wala mimba, Halafu we unakisia tu unasema inawezekana yani inamaanisha huna uhakika na hilo jambo unalo sema." nilisema nikiwa siamini kile nachoambiwa.

"Uhakika ninao ila nimekwambia inawezekana kwa sababu sijaangalia vizuri, ila asilimia kubwa naona ni mdogo wako maana dam yenu naona ni moja, halafu maswala yakutoka na mimba ni siri ya mama, kama alitoka na mimba yenye mwezi mmoja au miwili?.. We ungejuaje au ungeonaje?.." yusrat alisema neno ambalo lilinigusa.

"Ila kweli inawekazana mi nilikuwa nabisha kwasababu sikufikiria hivyo, kama kweli umeona dam zetu ni sawa basi kweli atakuwa ni mdogo wangu." nilisema na yusrat akaongea.
"Chakufanya hapa inabidi tumlete juma karibu halafu tujihakikishie asilimia mia kama kweli ni ndugu Yako na njia ya kumtoa pale kwa mama Lucy, nakuwekea sura nyingne ya bandia ili wasije kimbia wakizania we ni mzim, tukishamaliza sasa tunaenda kwa mama lucy kumuelezea ila unatakiwa utumie uongo kidogo kwamba mama juma aliachika kwa baba ako akiwa na mimba ya juma na mimba ilikuwa ishaanza kuonekana, kwahyo utasema juma ni mdogo wako umekuja kumchukua."

Niliielewa mbinu aliyetumia yusrat, baada yakuniwekea sura bandia tukaondoka tukaenda hadi kwa mama lucy.
"Karibuni ndani kaeni hapo" alisema mama lucy akitukaribisha baada yakufika ndani kwake, tukakaa.
"Asante sana dada, najua hutufaham ila mimi ni kaka ake na juma naitwa mau na huyu dada anaitwa yusra ni mke wangu." nilijitambulisha
"Mmmh!!.. Kaka ake na juma?.. Ngoja nimuite, Jumaaaa!!.. Jumaaa!!.."
"Naaam!!!.." aliitikia juma huku akitoka chumbani nakuja hadi sebureni tulipokuwepo.
"Naam!! Mama."
"Et juma huyu mkaka unajua?.."
"Hapana simfaham" alijibu juma.

Mi nikaongea.
"Juma hebu kaa hapo tuwaelezee vizuri, Dada kabla ya mama ake na juma kuolewa hapo kwenye hiyo nyumba alikuwa ameolewa na baba angu kama mke mdogo ila bahati mbaya waliachana na baba na kipindi mamdogo anaondoka alikuwa na mimba ndogo hata mzee mwenyewe aliniambiaga Mimi, na chanzo cha baba kumuacha mama juma nikwakuwa alikuwa anachepuka na mwanaume mwingine ambae ndo huyo amekufa nae, kwahyo mama juma aliolewa tena akiwa na mimba ya baba huku akimdanganya huyo mwanaume wake kuwa mimba niyake wakati sio yake." nilimaliza kuelezea.

"Sasa kwanini hukuja kipindi wako hai unakuja wakati huu ambao wameshafariki mi takuamini vipi?.." alisema mama lucy
"Kwanza mzee wangu ameshariki na yeye ndio aliniambia haya maneno na sikutaka kuja kusema hivi kipindi wako hai kwasababu ningewaharibia ndoa yao maana mme wake angeona alidanganywa kuambiwa mtoto ni wake wakati sio wake kwahyo lazima angemuacha, ndomana nikawaacha sikutaka kuwaharibia ila nimeona juma amebaki peke yake na amebaki mpweke akijua hana ndugu tena wakati tupo, ndomana nimekuja kumchukua nikaishi na mdogo wangu."

"Sawa nimekuelewa, juma kajiandae uende na kaka ako." alisema mama lucy juma akaenda ndani akabadlisha nguo akatoka na begi la nguo.
"Hapana juma liache hilo begi we toka na hizo hizo nguo ulizovaa tutaenda kukuchukulia nguo zingine" nilisema tukamuaga mama lucy kisha tukaondoka.
"Roy tusiende kule kwenye kile chumba ni kidogo twende kwangu ni nyumba kubwa na inavyumba vingi." alisema yusrat, sikutaka kumbishia kwakuwa tushakuwa kitu kimoja kwhyo sikuona shida, tukaenda hadi kwake. Baada yakufika yusrat alituangalia vizuri nakukuta kweli mi na juma ni ndugu wa dam, ilikuwa ni usku sasa tukalala.

Asubuh nikiwa nimerudi kwenye sura yangu na wala juma hakuona utofauti wowote kwenye sura niliyo amka nayo, tukaenda wote kutembea tembea tukiwa na juma, mwisho tukaenda Raskazone beach kuogelea tuliinjoi sana ile siku, juma alikuwa anajua kuogelea alikuwa anatuzidi wote. Aliogelea akasogea mbali kidogo mara tukaona amezama tukapuzia tukajua anacheza ule mchezo wakuzama ili kubana pumzi, dakika zikazidi kwenda hakuibuka ikabidi mi na yusrat tusogee hadi pale alipozamia tukazama ndani ya maji tukaanza kumtafuta ila pote hatukumuona mara na sisi tukatoweka bila kujijua...ITAENDELEA...

Usikose sehemu ya 40

RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu Ya 40

TULIPOISHIA..
Dakika zikazidi kwenda hakuibuka ikabidi mi na yusrat tusogee hadi pale alipozamia tukazama ndani ya maji tukaanza kumtafuta ila pote hatukumuona mara na sisi tukatoweka bila kujijua...

SONGA NAYO..
Tukajikuta Tumedondokea mapangoni sehem yakutisha tukajiinua pale chini mi na yusrat tukaanza kuangaza angaza mazingira ya pale, tulikuwa ndani ya pango kubwa sana, palikuwa kimya mnoo ila palionekana kuna watu maana kuna miti ilikuwa imechomekwa kwenye kuta zile huku ikitoa moto ulio leta mwanga kwenye mapango Yale. Yusrat akanishika mkono kisha akaanza kuniongoza tukaelekea kwenye ile njia ilikuwa mbele yetu tukazidi kusonga mbele, mara yusrat akaanza kumuita juma.

"Jumaaaaa!!.. Jumaaa!!.." sauti yake ilisikika inajirudia rudia ndani ya pango lile huku ikitoa mwangwi, kimya kikatawala. Mara tukasikia sauti inajibu "Naaam!!!.. Nipo hukuuu!!.." tulisikia sauti ya juma ikijibu huku ikijirudia rudia.
Tukakimbilia kule sauti ilipotokea, tulizidi kusonga mbele kwa kasi mara tukatokezea sehemu yenye uwazi mkubwa tukasimama tukaanza kuita tena.
"Jumaaa!!.. We jumaa uko wapii!!.." niliita mara ikasikika sauti ikijibu.
"Nipo hapaa!!.." ile sauti ilijibu huku akionekana mtu anatokezea hakuwa juma ila sauti yake ilikuwa inatoka kama ya juma..

Yule mtu usoni alikuwa na manyoya kama ya sokwe na mikononi pamoja na miguuni ila alionekana anaumbo la kibinadam tofauti yake ilikuwa ni yale manyoya na makucha marefu aliyokuwa nayo kwenye viganja vya mikono pamoja na miguuni, alikuwa ni jinsia ya kiumbe na hakuwa amevaa nguo bali alikuwa amejiziba sehemu ya mbele na ngozi ya chui.

Tukaona anazidi kutusogelea huku akicheka.
"Hahahaha!!.. Nyie ndo mmetumwa et eeh?.." kabla hatujajibu swali lake alianza kututembezea mkono alipiga ngumi moja yusrat akainama chini ikapita ikanipata mimi kwenye uso maana mi nilikuwa nyuma ya yusrat, nikaona mawenge mawenge nikadondoka chini kama limzigo nilikuwa naona kwa mbali sana kutokana kizungu zungu nilichokipata, yusrat akaanza kupigana na yule mtu sokwe. Yusrat alionekana mwepesi sana alikuwa anayakwepa tu mapigo ya yule kiumbe akaanza kumpa na yeye yule mtu sokwe alichezea kipigo kila alivyojaribu kukwepa alikutana nayo yusrat alikuwa anapiga mateke makali, Mimi kile kizungu zungu kilikuwa kimeshaondoka nikainuka nikasimama pembeni kidogo nishuhudie ule mpambano, yule mtu sokwe alikula ngumi za usoni mfurulizo hadi akatokwa na dam mdomoni ila dam yake ilikuwa ya blue nilishangaa dam ile, uso wake ulikuwa umetepeta akayumba yumba akadondoka chini, nikamsogelea yusrat nikamuuliza.
"huyu ni kiumbe gani? Mbona anatoa dam ya blue?.."
"Huyu ni jini na inaonekana hapa hatuko duniani!!.." alisema yusrat mi nilishangaa kusikia maneno Yale, mara tukaona yule mtu sokwe akijiinua kwa kitete, akasimama kimawenge mawenge huku dam ya blue ikimtoka, yusrat akanisogeza pembeni akakunja ngumi akajiandaa kupigana nae, mara yule mtu sokwe akasema.

"Nyie ni wakina nani na mmetokea wapi?.."
"Kwani hapa tuko wapi?.." yusrat akauliza na yeye.
Yule kiumbe akamjibu.
"Badala mnijibu swali langu mnaniuliza tena nyie mtukuja sehemu ambayo hamuijui?.." alisema yule mtu sokwe huku akionesha sura ya hasira baada ya kuulizwa vile, yusrat akasema kistaarabu.
"Sisi tulikuwa tunaogelea tu kwenye maji ghafla tukazama ndo tukajikuta tuko huku hata hatujui tumefikaje fikaje.." ikasikika sauti ya yule kiumbe ikisema.
"Na yule kijana mliyekuwa mnamuita ni nani yenu?.."
"Ni mdogo wangu wa dam kabisa" nilijibu huku nikiwa nashauku yakumuona alipo.

"Twendeni huku mnifate" alisema yule sokwe mtu, akiongoza njia huku akitembea kwakuchechemea kutokana na kile kipigo alichokipata kwa yusrat, alizidi kutuingiza ndani kabisa ya pango mara kwa mbele tukamuona juma amefungwa kamba mikononi, miguuni akiwa amezibwa pia na mdomo. Yule kiumbe baada yakufika akamfungulia juma zile kamba, Juma baada yakufunguliwa akatukimbilia kuja kutukumbatia alionekana ni mtu aliyejawa na uoga Sana.

Nikamuuliza
"Imekuaje?.." akasema.
"Mi nilikuwa naogelea tu mara ghafla nikajikuta nimedondokea huku sijui hata nimefikaje fikaje, ile najiinua ili niangalie niko wapi ndo nikamuona huyo kiumbe akinisogelea nikapiga kelele ila hakujali akanikamata na kunifunga kamba.." alisema juma.

Yusrat akamgeukia yule sokwe mtu akamuuliza.
"We ni nani na kwanini uko hapa peke Yako?.." yule kiumbe akajibu.
"Mi ni mlinzi wa hapa na sio kwamba niko peke yangu kwenye hili pango, tuko majini wengi Sana, kila sehemu kuna ulinzi mimi ndio nimewekwa hapa mbele kuna walinzi wengine wako huko nyuma."
"Kwani hapa tuko wapi?.." aliuliza tena yusrat.
"Hapa mko kwenye mji wa majini."
"Mji wa majini?... Mji gani huo?.." aliuliza yusrat, akajibiwa na yule mtu sokwe alionekana amekuwa mpole tofauti na pale mwanzo.
"Mko pembeni kabisa ya mji wa jozi" Yusrat alishtuka kusikia vile akauliza Tena.
"Heeeh!!.. sasa kwanini mko kwenye hili pango linanini?.."
"Hapa tumekuja kujificha, kutokana na vita kubwa iliyotokea, mfalme wetu wa mji wetu wa jozi aliuwawa na aliye muuwa ni mwanae, na mashetani wa trofi na mji wote umetekwa na mfalme damor ameingiza majeshi yake ameupindua ufalme, na sisi tukapata bahati ya kutoroka na mke wa mfalme na mtoto wake Sarha pamoja na majini baadhi ndo tumekuja kujificha huku, Mwanzo nilipo waona nikazani ni maadui ndomana nikawashambulia" alimaliza kutoa maelezo mafupi yule kiumbe, Yusrat alionesha kushtuka nami pia nilishtuka maana alikuwa ameshanipa story ya mji huo kwahyo nilikuwa nayajua baadhi ya mambo..

Alionesha sura ya huzuni sana yusrat, nikamsogelea nikamkumbatia kumtuliza maana machozi yalikuwa yameshaanza kumrenga renga, Mara ikasikika sauti ya yule sokwe mtu ikiuliza.
"Nimesikia mnasema mmetokea duniani, bila shaka nyie ndio mtakuwa mmechagulia na miungu wa mji huu mje muukombea mji huu kutoka kwenye miliki ya mashetani wabaya.." yusrat akamjibu.
"Sina hakika ila inaweza ikawa hivyo, maana huku mtu haji bahati mbaya kama hana agizo lolote la kupewa."
"Ooh kumbe unaelewa sana mambo ya huku?.."
"Sio yote naelewa baadhi tu maana nishawahi kufika huku nikiwa mdogo na wazazi wangu ndio wale binadam walio kuja huku na kupewa agizo la kwenda kuizimisha bom lililo letwa na mashetani wa trofi na kweli wakafanikiwa"

"Oooh!!.. Kumbe wale ni wazazi wako? Mtoto wa mashujaa!!! Twendeni kabisa huku malkia na watoto wake wakuone.." alisema yule sokwe jini huku akionesha uso mwenye furaha, akatuongoza tukaanza kumfata alipokuwa anaelekea njiani tukakutana na walinzi wengi akawa anaongea nao rugha ambayo hatukuielewa basi wakatufungilia mlango wakaturuhusu tukapita, tukakutana pia na wengine mbele nao pia akaongea nao tukazidi kusonga mbele pango lile lilikuwa lefu kweli kweli baada ya mwendo mrefu hatimae tukafika kwenye mlango husika pale pia kulikuwa na walinzi.

Akaongea nao pia wakaelewa mlango ukafungiliwa, tukaingia ndani kulikuwa ni ndani ya pango lakini mule ndani palikuwa pametengenezwa vizuri sana palivutia juma na mimi tulishangaa uzuri wa mule ndani, hatukuwa tumefika mwisho yule jini sokwe akatupeleka sehemu nyingine Tena vyumba vilikuwa vingi, Tukafika kwenye mlango hivi ulio tengenezwa kwa dhahabu ulikuwa unang'aa sana jini sokwe akagonga mlango ukafunguliwa na binti mzuri sana mwilini alivaa nguo zilizo ng'aa na alijaa vito vya thamani akatukaribisha ndani kisha akatuonesha sehem ya kukaa tukakaa kwenye makochi yaliyokuwepo pale yalikuwa mazuri sana yalimeremeta, yule mdada baada yakutuelekeza sehem yakukaa aliondoka, yule jini sokwe yeye hakukaa alisimama tu nyuma ya sisi.

Wakati tukiwa tumekaa pale tunashangaa shangaa mara tukamuona yule binti aliyetukaribisha ndani mule akija na watu nyuma wakimfata, yusrat alionesha kushtuka baada yakuwaona wale watu walio kuja na yule mdada akasimama..ITAENDELEA....

Usikose sehemu ya 41
 
[4/2, 14:24] AzEr: Agizo la majini 41-45

RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu Ya 41

TULIPOISHIA..
Wakati tukiwa tumekaa pale tunashangaa shangaa mara tukamuona yule binti aliyetukaribisha ndani mule akija na watu nyuma wakimfata, yusrat alionesha kushtuka baada yakuwaona wale watu walio kuja na yule mdada, akasimama..

SONGA NAYO..
Wale watu walio kuja walionesha na wenyewe kushangaa, sarha akawahi akamkumbatia yusrat huku machozi yakimtoka.
"Bibi yangu habari za siku nyingi?.." alisema Sarha, na yusrat akajibu.
"Nzuri tu sijui nyie"
"Huku sio kwema kabisa ndomana tumekuja kujificha huku"
"Daah poleni sana huyo mlinzi wenu ameniambia baadhi ya mambo, yamenihuzunisha sana.."
"Daah ndo hivyo mzee wetu ameshafariki tuko huku tu tunasubiria msaada, ndo wewe umekuja Kwaajili ya hilo swala nadhani?.."
"Sina hakika ila nahisi hivyo."
"Na hao uliokuja nao ni wakina nani?.."
"Huyo kijana ni mpenzi wangu anaitwa roy na huyo ni mdogo wake anaitwa juma, tulikuwa duniani tunaogelea tu beach ghafla ndo tukajikuta tuko huku kwenye hili pango"
"Ooh sawa asilimia mia nyie ndio wahusika" alisema sarha kisha akamuachia mikono yusrat na mama yake malkia yurha na yeye akasogea kumkumbatia yusrat.

"Umekuwa sasa mara ya mwisho kuja ulikuwa kadogo, umetutenga sana wazazi wako wenyewe wanakujaga siku moja moja kutuona ila wewe ndo haujagi kabisa" alisema malkia yurha.
"Hapana kinacho nikwamisha ni majukumu mliyonipa nakuwa bize sana kusaidia watu nashindwa hata kuja huku maana nikikaa siku moja tu huku ni kama nimekaa wiki duniani, ndomana nashindwa kuja huku, hata hivyo nashangaa kwanini bado nawakumbuka wakati nilikuwa kadogo kabisa.."
"Hahahaha, nguvu uliyo nayo ndo inasababisha kumbukumbu zako za miaka yote zibaki vile vile ingekuwa uko kwenye hali ya ubinadam wa kawaida ungeshatusahau mda mrefu na usingetukumbuka hata kidogo.." alijibu malkia yurha.
"Ooh sawa nimekuelewa." alisema yusrat.

Baada ya mazungumzo yale walikaa wote kwenye yale masofa wakaanza kupiga story za hapa na pale, juma alikuwa anashangaa tu maana alikuwa haelewi chochote, Mara nikasikia yusrat akimuuliza sarha.
"Vipi niambie ilikuaje mpaka baba yako mfalme akapinduliwa na nyie mlitokaje Kule kwenye kasri yenu ya kifalme?.."

Sarha akaanza kuelezea.
"mfalme wa mji wa trofi damor, baada yakuona ameshindwa kupitisha nguvu zozote za kishetani mpakani kwetu alitumia mbinu nyingine, alijitoa nguvu zote mwilini za kishetani akawa jini wa kawaida tu kisha akavuka kwenye mpaka wetu akaingia ndani ya mji huu, na hiyo siku ndo mdogo wangu surha alikuwa matembezi matembezi tu akiwa na walinzi baadhi mdogo wangu kuna wakati anakuwa na roho ya huruma na Kuna wakati anakuwa mkorofi sana, sasa ile kutembea tembea akamuona kijana mmoja handsome akiwa amekaa chini katikati ya njia alionekana amechomwa na mwiba mguuni maana dam za kijini zilikuwa zinamtoka Sana, mdogo wangu baada ya kufika pale nakumuona yule kijana anahali ile, roho ya huruma ilimuingia akashuka kutoka kwenye usafiri aliokuwa ameupanda akasogea mpaka alipokaa yule kijana akiugulia maumivu ya kuchomwa na mwiba.

Akamshika mguu Kisha akamsaidia kuuchomoa ule mwiba, kisha akaagiza walinzi wake watafute kitu cha kumfunga pale alipo chomoa ule mwiba, walinzi wakatafuta wakakileta mdogo wangu surha akamfunga vizuri kisha akaanza kuongea nae.
"Pole sana utapona tu, vipi we unaitwa nani na kwanini unatembea peku kwani hauwezi kupaa?.."
"Hapana naweza kupaa ila nilipenda tu kutembea tembea kwa miguu ndo bahati mbaya mwiba ukanichoma, Mi naitwa hoju sijui wewe?.."
"Mi naitwa surha, kwani we unaishi wapi?.."
"Mi naishi hapo mbele tu sio mbali na hapa."
"Sawa inuka nikupeleke ukapumzike."
"Hapana usijali ni hapo tu tapaa nafika hata usijali"
"Sawa siumesema ni maeneo ya hapa hapa basi baadae takuja kukuona nione hali yako inaendeleaje"
"Sawa hakuna shida." alijibu yule kijana kisha surha akapanda kwenye usafiri wake na walinzi wake pia wakapanda wakarudi kwenye kasri yetu ya kifalme, mdogo wangu baada ya kufika nyumbani hiyo siku hakuwa na raha kabisa hakutaka kuongea na mtu yoyote, alikuwa anamuwaza sana yule kijana alitokea kumpenda ghafla, hata kabla ya hiyo baadae kufika aliondoka tena hakwenda na mlinzi hata mmoja alienda yeye kama yeye alitoa mabawa kisha akapaa, alifika yale maeneo aliyo elekezwa akamuangaza angaza kwenye nyumba za pale, mwisho akamuona anatoka nje akamfata kisha akamuuliza.

"Vipi hali Yako unaendeleaje?"
"Naendelea vizuri tiba yako ya kwanza imenibonya"
"Mmh!!.. Kweli?.."
"Ndio nahisi maumivu yamekata kufikia kesho nahisi takuwa nishapona"
"Sawa mi nilikuwa nimekuja kukujulia Hali tu"
"Sawa karibu ndani Sasa"
"asante imlad nimepaona unapoishi takuja kesho"
"Sawa nashukuru kwakunijali"
"Kawaida tu hata usijali" alisema surha kisha akarudi nyumbani akiwa na furaha tofauti na pale mwanzo, alikuwa mchangamfu sana na alipofika tulipiga nae story mbali mbali alionekana kama amechanganyiwa ndim alikuwa mapepe sana, kesho yake ikafika akaenda tena kwa yule kijana safari hii alimkuta amepona kabisa hadi alibaki anashangaa, mdogo wangu alikalibishwa mpaka ndani hiyo siku ndo ilikuwa mwanzo wa mapenzi yao, alikuwa ametokea kumpenda sana kwahyo hakukataa alipo ombwa alale na yeye, sarha akatolewa usichana wake na yule kijana.

Mapenzi yao yakazidi kupamba moto na siku nazo zikataradadi, surha alikuwa aelewi wala hasikii kwa yule mwanaume alimpenda kupitiliza, tulijua mahusiano yake kwakuwa alishakuwa mkubwa hakuna ambae alimbuguzi ila huyo mwanaume aliyekuwa anamsemea hatukuwahi kumuona. Siku moja yule mwanaume akamwambia sasa yeye asili yake akajitambulisha kwake kwamba yeye ndio mfalme damor wa mji wa trofi, Surha alishtuka kidogo ila hakujali sana maana alikuwa ameshampenda, kila alicho ambiwa na damor alitekeleza, alikuwa tayari hata kuiangamiza familia yake yote lakini sio kumpoteza mwanaume yule, alimwambia wakitimiza mipango yote atamuoa na yeye ndiye atakuwa malkia wa miji yote yani mji wa trofi na mji wa jozi, mdogo wangu alifurahi sana kusikia vile.

Siku moja damor alimpa sumu mdogo wangu, aiweke kwenye kinywaji atachokunywa baba, Surha hakujifikiria mara mbili mbili alikubali agizo lile na kweli akaenda kumuwekea baba sumu kwenye kinywaji, baba alipokunywa alifariki pale pale na surha akakimbilia kwa damor, walinzi wa baba ndo walikuja kutuambia kwamba aliyeuwa ni surha kwasababu yeye ndio alimletea kinywaji baba yake na baada ya mda povu likaanza kumtoka mdomoni, kwahyo moja kwa moja muhusika ni surha, ilikuwa ngum kuamini ila ilitubidi tu tuamini maana ule ndio ulikuwa ukweli wenyewe.

Baada ya kifo cha baba ulinzi ukateteleka, mfalme damor akaenda kumleta mganga wake hodari, yule mganga akamkata mdogo wangu mkononi kidogo akachukua dam yake kisha akachanganya na dawa zake kisha akavunja nguvu zote zilizokuwa mpakani, sasa pakawa wazi kiumbe yoyote mwenye nguvu za kishetani akawa anauwezo wakuingia kwenye huu mji wetu.

Mfalme damor kwakuwa na yeye alitokea kumpenda sana mdogo wangu surha akaamuwa kumuoa, akambadilisha na jina akawa anaitwa Yurhi akaishi nae kwenye mji wa trofi kwa mda mrefu kidogo baada yakuinjoi na mke wake kwa miezi kadhaa akaingiza Sasa majeshi yake ya kijini naya kishetani kwenye mji wetu wa jozi akawa anauwa kila aliye leta ubishi walinzi wetu wote wa mpakani wakauwawa kisha wakawa wanapita mtaani kisha wanafyeka maaskari wote na wote wanao wapinga, majini wengine walikuwa wanakimbilia ndani kujificha maana mji ulichafuka sana, majini wetu waliuwawa wengi ukipita mtaani wamepangana kama sisimizi, miezi sasa ilikuwa imepita baada ya kifo cha baba, taarifa zile za majeshi wa trofi kuvamia kwenye mji wetu tukazipata.

Tukajipanga kutoroka ila tungetorokea wapi wakati mji wote umechafuka?.. Tukiwa ndani tukasikia kelele za majeshi wa kishetani wakija kwenye ile kasri yetu ya kifalme, tukachungulia dirishani tukaona walinzi walio kuwepo kule nje getini wakijitahidi kupambana nao ila wote waliuwawa, Yale majeshi ya kishetani yakiongozwa na damor yalifungua geti kisha yakazama ndani.....ITAENDELEA...

Usikose Sehemu ya 42..

RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu Ya 42

TULIPOISHIA..
Tukachungulia dirishani tukaona walinzi walio kuwepo kule nje getini wakajitahidi kupambana nao ila wote waliuwawa, Yale majeshi ya kishetani yakiongozwa na damor yalifungua geti kisha yakazama ndani.......

SONGA NAYO..
Mama akasema "Nifateni huku napoenda."
Majini wote tulio kuwemo mule ndani na wale majini wengine walio kimbilia kwenye lile jumba letu kujilinda pamoja na wafanyakazi na walinzi wote tukamfata mama. Alitupeleka kwenye gorofa ya chini kisha akaingia kwenye chumba kimoja hivi ambacho hakikuwa kinafunguliwa mara kwa mara, wote tukamfata mama, ajabu mama akashika pale chini huku mdomo akiuchezesha akiashilia anaomba kitu baada ya mda ukaonekana mlango wakushuka chini kabisa. Tukiwa tunashangaa shangaa mara tukasikia vishindo vya yale majeshi yakishetani yakizama ndani..

Mama akaufungua haraka haraka ule mfuniko wa lile shimo kisha majini wote tukaanza kushuka chini kwenye ile njia ya siri ambayo hata mimi nilikuwa siijui, Baada ya mda wote tukawa tumefanikiwa kushuka chini, mama akaufunika ule mfuniko kisha akanuia tena maneno yake pale, tukaanza kutembea kwenye ile njia ya chini chini iliyokuwa na giza kubwa tukawasha moto kwenye miti iliyokuwa pale pembeni ya Kuta kisha walinzi wakaishika ile miti ikawa kama tochi yetu wakaongoza njia wakawa wanatumulikia.

Ile njia ya siri ilikuwa ndefu sana tulitembea mpaka wote tukachoka tukaamua kupumzika kwanza maana sisi hatukuzoea kutembea vile tulizoea kupaa au kupanda usafiri.

Upande wa kule kwenye kasri yetu ya kifalme, yale majeshi yakishetani yalitutafuta sana ila hayakufanikiwa kujua tulipo, kila chumba waliingia ila hayakuona chochote wala dalili yoyote yakuonesha kama kuna majini ndani mule, walitafuta mpaka wakachoka ikabidi wakamjuze mfalme wao damor.
"Mtukufu mfalme tumewatafuta kote hatujawaona"
"Unataka kuniambia walitoroka kabla ya sisi kufika hapa?.."
"Sijui mkuu ila nahisi itakuwa hivyo."
"Kwaanzia sasa hivi hii falme Iko chini yangu, panga vikosi vyako vizuri dumisha ulinzi wa hapa kisha chukuwa majeshi baadhi uingie nayo mtaani, pora kila kitu cha thamani. Yoyote akileta ubishi mmalizeni uwa wote kabisa tubakie na wanao tutii tu na kufata sheria zangu." alisema mfalme damor.
"Sawa mtukufu mfalme" alijibu kiongozi wa majeshi yale aliyejulikana kwa jina la bogi.

Tulipokuwa sisi, baada ya kumpumzika kwa mda kidogo tuliinuka kisha tukaendelea na safari ile, tulitembea sana uzuri njia ilikuwa pana ndomana tulitembea kwakujiachia baada ya mwendo mrefu mnoo ndo tukafika kule mlipo tokezea nyie, baada ya kusogea kidogo mama akasema pale abakie mlinzi mmoja wakutoa taarifa kama kuna hatari yoyote inayokuja, maana sisi tunamilio yetu yakujuzana kama kuna hatari inakuja, hata wewe huwezi kusikia inasemwa kimoyo moyo ndani kwa ndani, ila huku sisi tunasikia. Hata kipindi nyie mnafika tuliusikia huo mlio wa hatari, tukawa tunajiandaa kuondoka kwakupita njia nyingine ya juu ila tukiwa tunataka kuondoka tulisikia mlio wa amani, ndo tukajua waliokuja sio watu wabaya..

Basi bhan tuliacha walinzi njiani wakupambana na hatari kama ikija, mama akatuleta hadi hapa tulishangaa palivyo pazuri inaonesha baba na mama walikuwa wanapatunza kisiri siri bila sisi kujua, na sababu ya wao kufanya hivyo ni kusudi hatari yoyote ikitokea tukimbilie huku kujificha.

Baada ya mfalme damor kuamuru majeshi yote yaingie mtaani, agizo lile lilitekelezwa bogi akachukuwa majeshi baadhi akaingia nayo mtaani Sasa, waliuwa sana majini wetu walikuwa wanaingia kila nyumba kisha wanapora kila kitu cha thamani, wamama, watoto, wababa walilia sana nakusaga meno lakini waliambulia kipigo, wanaume wote wenye nguvu walikamatwa na kupelekwa kwa kiongozi wao kusudi yao ilikuwa nikuongeza vikosi ndomana waliwakamata wanaume, waliwapeleka kwenye jeshi lao yule ambae hakuwa tayari alikatwa kichwa.

Uchumi wa mji wetu ukazorota hali ikawa mbaya maendeleo yaliokuwa yanakuwa kwa kasi Yakashuka kwa siku mbili tu majini wetu wakawa wanapigika kisawa sawa. Kinacho wasaidie ni ile hali ya kutokusikia njaa wanaweza kuishi bila kula kwa mda mrefu kidogo na wasizulike, kinacho watesa ni kipigo wanacho kipata kila siku, hawaishi kwa raha majumba yote mazuri mazuri yametekwa na mashetani mji umechafuka majini wetu wanatumikishwa kama punda wanapigwa mijeredi wakiregea regea, hali imekuwa mbaya sana.

Uhalisia ndo uko hivyo, mdogo wangu surha yeye yuko kwenye mji wa trofi ndo anaongoza watu wa huko, mme wake mfalme damor ndo yuko huku kwenye mji wetu anatesa wananchi wetu.

Yusrat baada yakuelezewa ile story na sarha alionekana kama anatafakari kitu Kisha akasema.
"Kama mdogo wako ndo malkia wa mji wa trofi basi namkumbuka mi ndio nilimtoaga macho kipindi kile ameenda duniani kuchukua dam za watu, ila!!.. kwanini sikumkumbuka kama ndo surha kipindi kile?.."
"Yule hana Tena asili ya kwetu, ameshapandikizwa mashetani mwilini mwake hata ukimuona huwezi kujua kama ndo yule mdogo wangu, ndomana hukuweza kumfaham, na kipindi kile ameenda duniani nahisi alikuwa ameenda kuchukua dam ya sherehe yao ya yeye na mme wake maana utaratibu wa mji wao ndo uko hivyo binti ukiolewa na mfalme wewe ndio unatakiwa kwenda kutafuta dam ya sherehe yenu."
"Ooh sawa hapo nimekuelewa." alisema yusrat.

Mi na juma tulipata kujua baadhi ya mambo, tukaelewa kilicho tuleta pale ni nini. Tukasikia sarha akisema "hamna mda wakupoteza, nishawaelezea mshaelewa mtaanzia wapi kutekeleza kilicho waleta, twendeni kwenye maabara, tukawape nguvu na nyie muwe kama yusrat kisha mkaifanye hiyo kazi Sasa." alisema kisha akainuka na sisi tukainuka tukamfata alipokuwa anaelekea. Yusrat yeye alibaki tulienda mi na mdogo wangu juma, alikuwa na umri mdogo ila alikuwa na mwili mkubwa tulilingana mwili na urefu pamoja nakuwa nilikuwa nimemzidi miaka mingi, ila alikuwa amepanda hewani alikuwa anakuwa kwa haraka sana.

Basi tukazidi kuzipiga hatua kuelekea kule kwenye maabara, baada ya hatua kadhaa tukafika kwenye mlango wa maabara ile ya siri iliyotengenezwa na wazazi wao, Sarha akakishika kitasa cha mlango kisha akafungua tukazama ndani, mule kulikuwa kumejaa vioo tu na chini kulikuwa na marumaru iliyong'aa sana ukitazama chini unajiona. tukiwa tunashangaa shangaa maadhari ya mule ndani tukapigwa na kitu kichwani tukadondoka chini tukazimia..

Tulipo zinduka tulijikuta tumelazwa kwenye vitanda vilivyokuwa kwenye maabara ile, juma alikuwa amelazwa kwenye kitanda kingine na mimi nilikuwa kwenye kitanda kingine, nahisi tuliamka kwa pamoja maana nilipogeuka alipolazwa juma alikuwa anashangaa shangaa tu kama mimi, ndani ya maabara Ile hapakuwa na watu wengine tofauti na sisi.

Nikajiinua nikakaa kisha nikashuka chini ya kitanda kile, nilijihisi mwili umekuwa mwepesi mnoo nikajinyosha nyosha viungo wakati nanyosha mkono mara nikaona vitu vinatoka kwenye vidole vyangu viwili vikaenda kuchoma kwenye vioo vilivyokuwa kama ukuta, vioo vile vikatobolewa na vile vitu vilivyotoka kwenye vidole vyangu, nilishangaa hali ile hata juma alishangaa akaniuliza.

"Kaka nini hicho umetoa mbona sijaelewa?.."
"Mi Mwenyewe sielewi nahisi tumetoka kama tuchuma tudogoo tulio chongoka kama tuvisu."
"Eeeh!!.. hebu jaribu tena tuone" alisema juma huku akiinuka kutoka kitandani na kusimama pale pembeni ya kitanda, nikajaribu kufanya kama mwanzo ila hatukutoka.
"Sasa mbona tumegoma kutoka??.." wakati nikijiuliza vile mara nikasikia sauti ya kike ikitokea kwenye mlango wa kioo ulio kuwepo pale.
"Ujafanya inavyotakiwa ndomana hatujatoka." alikuwa ni sarha...
"Mbona nimefanya vile vile nilivyo fanya mwanzo?.."
"Hapana ulikosea rudia Tena"
"Nikarudia tena safari hii nikaunyosha mkono wa kulia vizuri nikavikunja vidole kama spiderman, mkono ukawa kama unatetemeka ukaelekea uelekeo tofauti na nilipoelekeza, tukatoka tuvisu tuwili kwa kasi ya ajabu tukampita juma kwenye sikio kidogo tumpitie tukaenda kuchoma kwenye vioo...."ITAENDELEA..

Usikose sehemu ya 43...

RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu Ya 43

TULIPOISHIA..
Nikavikunja vidole kama spiderman, mkono ukawa kama unatetemeka ukaelekea uelekeo tofauti na nilipoelekeza, tukatoka tuvisu tuwili kwa kasi ya ajabu tukampita juma kwenye sikio kidogo tumpitie tukaenda kuchoma kwenye vioo...."

SONGA NAYO...
"Hivyo Sasa!!.. Ila unatakiwa kukaza mkono sio kuuweka kilele mama" alisema Sarha, nikarudia tena kufanya safari hii nilizidi kuwa bora nilifanya kwa usahihi.
"Haya nifateni nikawaelekeze jinsi yakuzitumia hizo nguvu" alisema sarha kisha akaelekea kule kwenye mlango wa kioo akaufungua kisha tukatokezea sehemu hivi yenye upana mkubwa palikaa kama uwanja wa mpira ila ulikuwa wasaizi tu sio mkubwa kivile.

Baada yakufika pale nikaona kitu kama jiwe kikija kwenye uso wangu kwa kasi ya ajabu nikaruka sarakasi halafu nikalidaka lile jiwe.
"Good!!.. Vizuri sana" alisema sarha huku akipiga makofi, mi nilijihisi mwepesi mnoo nilizidi kushangaa hali Ile nikamuuliza sarha.
"Naomba nikuulize kitu!. Hivi mbona najihisi mwepesi mnoo au ndio umetuwekea zile nguvu ulizokuwa unasema?.."
"Ndio mnanguvu kubwa sana milini mwenu, na ndomana mnajihisi wepesi hata kupaa mnaweza hata kupiga makombora ya kila aina, hata kitu cha hatari kikija kuwazuru kwa kasi ya namna Gani mtakiona tu, pokea hiyo" alisema sarha akirusha tuvitu kama tumisumari kuelekeza kwa juma, tulikuwa twingi juma akajivingirisha kama feni akatukwepa kwa kasi mnoo, ye mwenyewe baada ya kutua alijishangaa sana kama vile kuna kitu kilikuwa kinatuongoza maana unajikuta mwili unatenda tu hata kabla hujajiandaa.

"Nyie ni wepesi kuelewa sitofanya kazi kubwa, naomba juma utoweke maeneo haya yani upotee" alisema sarha kisha akajaribu kutoweka akawa anaruka ruka ila hakufanikiwa kupotea.
"Sio unaruka ruka, yani unatulia halafu unavuta hisia kisha unafikiria kuondoka eneo hili au unafikiria kutoonekana, hebu roy fanya wewe tuone" Nami nikajaribu kufanya nikasimama wima nikatulia kisha nikafumba macho nikaongea kinafsi "nataka nisionekane"

"Waooo!!.. vizuri sana" alisema sarha, mi nilishangaa maana nilikuwa nawaona kama kawaida tu ila kumbe wao wakitazama kwa macho ya kawaida hawanioni.
Nikamuuliza juma
"Vipi juma hunioni hapa nilipo?.."
"Ndio sikuoni ila nasikia sauti Yako"
alisema juma, ndo nikaamini kweli sionekani nikajirudisha kwenye hali yakuonekana.

"Haya juma na wewe fanya hivyo kama kaka yako" Juma na yeye akajaribu kufanya vile kweli akaweza hatukuwa tunamuona ila sauti yake tulikuwa tunaisikia na alikuwa amesimama pale pale alipokuwa, hakuwa ameondoka.
"Pia mnaweza kufanya sauti zisisikike nikunuia tu unachotaka." alisema Sarha akaongeza neno lingine.
"Pia kuna ile unafika sehemu mwili unasisimka unahisi kuna kitu ila hukuioni, unavuta tu hisia unafumba macho halafu unafumbua unakiona hicho kitu, hiyo nayo waambia niyakujifundishia tu ila kwa nguvu zilizopo mwilini mwenu mnauwezo wakuona kitu kisicho onekana hata bila kufanya hivyo ila nimewaambia hivyo kama tahadhari tu maana kuna sehemu unaenda unakuta yule mtu ananguvu kubwa sana mwili wako unakwambia kuna kitu ila hicho kitu hukioni, basi mnafanya hivyo nilivyo waambia." alisema Sarha.

"Sawa tumekuelewa" tulijibu mi na juma.
"Kingine ukitaka kufanya chochote yani mfano unataka kumtumia mtu kombora la aina yoyote, unajiamini kwanza yani unaweka imani na nguvu zako halafu unafikiria kile kitu unachotaka kufanya kitatokea tu. Mfano roy jaribu kunipiga na kitu chochote ukiwa umesimama hapo hapo utacho fikiria kitatokea hicho hicho." alisema sarha nami nikafikiria haraka haraka chakufanya nikawaza niurefushe mkono uwe mrefu umfikie pale sarha alipokuwa amesimama, nikaunyoosha mkono nikawaza vile na kweli mkono ukarefuka ukafika hadi kwenye shingo ya sarha nikafikiria kumniga mkono ukamniga kweli, nikafikiria kuurudisha mkono urudi kawaida na kweli ukarudi" nilishangaa ule uwezo nilio kuwa nao.

"Mmenielewa sasa?.. Yani mnacho fikiria kufanya basi kitatokea, kama unafikiria kupaa basi utapaa kama unafikiria kukwepa kitu basi utakikwepa ukifikiria kumpiga mtu wa mbali basi utampiga ukitaka kumtazama mtu aliyeko mbali unawaza tu hivyo nataka kumuona frani na kweli utamuona sehemu alipo, tumeelewana?.."
"ndio tumekuelewa" tulijibu, maelekezo yale yalikuwa mepesi mnoo kama kunywa maji tu, Basi akatuelekeza na mengine mengine akajazia jazia tukaiva kwa siku moja tu tukamuelewa yote.

Basi baada ya maelekezo yale akaturudisha hadi pale sebureni tulipokuwa tumekaa mwanzo, tukamkuta yusrat akipiga story na malkia yurha mama ake na sarha.
"Sasa hawa tayari wameshaiva nilikuwa nawaelekeza elekeza baadhi ya mambo maana nguvu nimewawekea ila jinsi yakuzitumia ndo ilikuwa mtihani, sasa mnaweza kwenda kuianza kazi yenu."

"Mmh sasa tunaenda wenyewe bila hata maaskari wakati ulisema majeshi yakishetani ni mengi mnoo" alisema juma kiuoga.
"Hapana mkienda na maaskari mtaharibu kila kitu maana mtauwawa chakufanya hapa mtumie akili tu kila kitu mnachokifanya mfikirie kwanza kabla ya kutenda, kwa nyie mlio chaguliwa kazi ni nyepesi nikutumia tu akili maana bahati pia inawabeba, kingine huku pia tunamajeshi yakijini kwahyo mkiwa mnaelekea mwisho kukamilisha mtatuita tuje kusaidia palipo baki kwakutumia ule muito tulio waelekeza."
"Ooh!!.. sawa hapo tumekuelewa, kwahyo tunapita ile Ile njia mlio pitia nyie kipindi mnakuja huku sindio?" niliuliza, mara malkia yurha akasema.
"Ndio mnapitia hiyo hiyo njia mnanyoosha moja kwa moja mkifika mwisho mtanuia maneno mtasema 'funguka njia ya siri ya jumba la kifalme' na ule mfuniko utajifungua mtatokezea sasa ndani ya kile chumba" alisema malkia yurha tukamuelewa tukaagana pale halafu tukaanza kuondoka sasa.

Tulitembea sana, baada ya umbali mrefu tulifika mwisho, tukaona tungazi twakupanda juu kidogo tukapanda tukaona mfuniko ambapo ndo njia yakupita, tukasogea hadi pale mi nikaushika ule mfuniko kisha nikanuia maneno tuliyo ambiwa na malkia yurha na kweli mfuniko ulijifunua wote tukapanda juu kisha tukaufunika tena ule mfuniko, nikanuia maneno pale ule mfuniko ukajifunika. tulishangaa kidogo maana ule mfuniko ulibadilika rangi ukawa unafanana na maru maru iliyokuwepo pale chini ya sakafu hapakuonesha hata dalili ya njia kwa jinsi palivyokuwa.

Tukiwa ndani ya kile chumba Mara ghafla wakatokezea viumbe wa Tano Wakutisha, tulishtuka maana ilikuwa ghafla sana halafu walikuwa wametuzunguka wametuweka mtu kati.
"Hahahaha!!.. Tulijua tu kama hapa kuna njia ndomana tumekaa kulinda hapa, sema tulishindwa kujua kodi zakuufunua huo mfuniko, sasa kwa usalama wenu ufungueni huo mfuniko haraka tuwaachie huru, si tunamtaka mtabiri, mama sarha pamoja na huyo mwanae, fungueni twende tukawachukua tunao wahitaji basi nyie tuwaache muende." alisema mmoja kati ya wale viumbe wakishetani.

"Hahahahaaaa!!.. kwa hilo msahau hatuwezi kuufungua, na hao majini mnao wataka hamuwezi kuwapata." nilisema kwa ujasiri.
"Mnaleta kiburi eeh!!. ngoja tuwaoneshe" alisema yule kiumbe aliyeongea mwanzo, Akarusha kitu kama nyavu zenye tumisumari, zikatufunika wote tukiwa tumesimama pale katikati ile nyavu ilitufunika na kutubana kisawa sawa tule tumisumar tukawa tunachoma kwenye miili yetu, kweli tulikuwa tunahisi maumivu yasio ya kawaida.
"Nyie simnaleta jeuri, haya kuleni chuma hicho, kwa usalama wenu tupeni kodi za kufunua huo mfuniko."
Sisi mda huo tulikuwa vibaya, tule tumisumari tulio chongoka tulizamana ndani ya mili yetu kwaanzia miguuni hadi kichwani, usoni kote macho tuliyafumba, mara nikasikia yusrat anaongea kwa taabu.

"Hatu..wezi kuwa..wapa hizo Kodi." baada yakusema hayo mi nilihisi kama kuna kitu kimeongezeka mwilini mwangu nguvu zikaongezeka nikaishika ile nyavu na misumar yake nikaivuta nikaichana chana vipande vipande tukachomoka ndani ya ile nyavu, wale mashetani walishangaa sisi kutoka kirahisi vile nahisi walikuwa wanauamini sana ule mtego wao.

"Mnashtuka nini, nyie ni watoto tu kwetu kama mnataka kuzipata hizo paswed, tuthibitini kwanza mkiweza tutawaambia." mi nilisema huku wote tukiwasogelea, wakabadilika wote wakatoka kwenye umbo la kibinadam wakawa na umbo la kizombi nyama ya miili yao ikawa inapukutika, zilikuwa zinajimega mega wakawa wana miili yenye madonda mwili mzima, juma akamrushia kombora mmoja wao ila kama tu alimpapasa hakuhisi chochote kilicheka sana kile kiumbe, ilionesha wakiwa kwenye hali ile ni ngum sana kupigika...ITAENDELEA..

Usikose Sehemu Ya 44.RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu Ya 44

TULIPOISHIA..
Juma akamrushia kombora mmoja wao ila kama tu alimpapasa hakuhisi chochote kilicheka sana kile kiumbe, ilionesha wakiwa kwenye hali ile ni ngum sana kupigika..

SONGA NAYO..
Wakazidi kutusogelea huku wakitembea kiupande upande kama mazombie, yule kiumbe aliyerushishwa na juma hakukubali kamlareko na yeye akamrushia juma kombora lililokuja na cheche za moto, juma hakuwa mzembe alikuwa mwepesi vibaya mnoo akaruka kiupande lile kombora likapita likaenda kugonga kwenye ukuta, ukuta ukatoboka hadi chumba cha pili kikaonekana.
Tukashikana mikono mimi, yusrat pamoja na juma tukaunganisha nguvu kwa pamoja ukajichora mduara wa moto ukiwa hewani saizi yakiuno, sisi tukiwa tumesimama katikati ya ule mduara, tukaupanua ule mduara ukazidi kuongezeka kwakusogea mbele zaidi, wale viumbe wakishetani wakaanza kurudi nyuma, mwisho wakafika ukomo wa kile chumba kwenye ukuta.

Hawakuwa na chakujitetea ule moto ulikuwa unapita kama panga ulikuwa unawakata kata viunoo, viwili wili vya juu kwaanzia tumboni vikadondoka chini, na viwili wili vya chini navyo vikafatia. Baada ya lile tukio tukajua tushawamaliza tukazipiga hatua za kuondoka kwenye chumba kile mara ghafla!!. Tukaona vile viwili wili vikisogeleana kwaajili yakujiunga. Tukasimama kwa mshangao mimi kwa kasi ya ajabu nikanyoosha mikono yangu miwili kisha nikatoa acid kwenye mikono yangu ilitoka kama maji ikaenda kwenye vile viwili wili vyote vikateketea vikayeyuka.

Baada yakuhakikisha vile viumbe vimeyeyuka vyote, tukafungua mlango tukatoka sasa ndani ya chumba kile tukazipiga hatua za tahadhali tukiangalia huku na kule kama kuna ulinzi wowote baada yakuangaza angaza kwa mda kidogo tukagundua jumba lile la kifalme lilikuwa na ulinzi wakutosha, walinzi walikuwa wanapita pita kila mda wakati tumejibanza sehem tunachungulia kwenye kibalaza kilichokuwa pale mbele huku tukijadiliana jinsi yakupita pale, mara tukasikia sauti ikitokea nyuma yetu.

"Nyie ni wakina nani na mnafanya nini hapo?.."
Tulishtuka baada yakusikia vile wote tukageuka kwa pamoja, macho yetu yakakutana na walinzi wanne wamesimama mbele yetu huku wakiwa na sura za userious, Tuligeuka mabubu ghafla, mara tukasikia yule yule aliyeongea mwanzo akiongea Tena.
"Au nyie ndio wale tunao watafuta?.. Washikeni hao kisha tuwapeleka kwa mfalme akawaone kama ndo wenyewe." alisema yule mlinzi aliyeonekana kama kiongozi wawale wenzake.

Wakasogea kwaajili yakutukamata, waliyatimba kweli kweli walichezea moto ambao hauguswi, ile wanatugusa tu wakapigwa na kitu kama short ya umeme wakadondoka chini nakukata moto, Akabakia amesimama yule kiongozi wao akiwa ameasama mdomo kwa mshangao akataka kukimbia ili akampe taarifa mfalme, nikarusha kitu kwa mbele yake ukatokea kama ukuta akajigonga akadondoka chini naye akakata moto.

Tukawashika miguu kisha tukaanza kuwaburuza mpaka kwenye kile chumba tulichotoka chenye njia ya Siri, baada yakuwafikisha ndani ya chumba kile tukawauwa kabisa kisha tukawatoa nguo zao ile miili tukaipoteza kimiujiza, tahadhali ikiwa ni kwamba hata walinzi wengine wakija ndani yakile chumba wasiweze kuona chochote au kujua lolote. Baada yakufanya vile tukajibadilisha muonekano tukachukua sura za wale walinzi pamoja na mavazi Yao waliyokuwa wamevaa tukayavaa sisi na yusrat akabadilika akachukua maumbile ya mlinzi mmoja kati ya wale walinzi sasa akawa na maumbile ya kiume.

Baada yakumaliza lile zoezi tukatoka ndani ya chumba kile tukaanza kuzipiga hatua za kidoria, tukiwa kama walinzi wa jumba lile la kifalme, tulizidi kusonga mbele zaidi tukakutana na walinzi wengine wengine na maaskari pia na majeshi yakishetani ila walitupita tu hawakuweza kutushtukia maana tulikuwa na sura za wale walinzi wa kweli, tukafika sehemu tukaona ngazi zakupanda kwenye gorofa inayofatia, bila kupoteza mda miguu yetu ikakanyaga gia tukapanda juu, baada yakufika juu tukaona walinzi wengi tu wanatembea tembea, ulinzi ulikuwa ni mkubwa kwa sababu mji ulikuwa bado hujatulia vizuri mfalme alikuwa anaamini wale majini walio kimbia kujificha ipo siku watarudi kulipiza kisasi ndomana alikuwa ameweka walinzi wengi ili hata kama wakija wakamatwe mapema.

wakati tukiwa tunasogea kwenye ngazi ili tupande juu tena kwenye gorofa ya mwisho aliyopo mfalme damor, mara walinzi waliokuwa wamesimama pale kwenye zile ngazi wakatuzuia.
"Nyie huku mnakuja kufanya Nini?.. Wakati mnatakiwa kulinda kule chini tu?.. Kwanza mnamakosa mnajua kabisa hamna kigezo chakufika hata hapa mlipo, ila nyie mlivyo na kiburi mnakuja tu hata bila wasi wasi hivi hamjioni hapo begani kama levo yenu niya chini? Na kingine mnatembea watatu wakati kila sehemu tumewagawa watembee wanne wanne mwingine yuko wapi?..." aliuliza mlinzi mmoja kati ya wale waliokuwa wamesimama pale mwanzo wa zile ngazi zakupanda juu.

Tulishtuka kidogo maana ule utaratibu tulikuwa hatuujui na kweli wale watu tulio wauwa walikuwa wanne halafu sisi tulikuwa watatu, tulishikwa pabaya nikajitutumua nikasema.
"Aaah! mwenzetu!!. amebaki chini sisi tumepanda huku juu kwa dharula tu kuna tatizo kule chini kuna siri kubwa ipo kule na inatakiwa tumwambie mfalme tu sio mtu mwingine yoyote."
"Hata kama iwe vipi hamruhusiwa kupanda huko juu kama ni siri kubwa niambie mimi nikamwambie mwenyewe maana ndo naruhusiwa kwenda kuonana na mfalme pamoja na hawa wenzangu nyie hamruhusiwi kabisa.

"Basi takwambia ila hatutakiwi kuongelea hapa twende na wenzako sehem tukawaambie huko maana hapa majini wengine wakitusikia ni hatari kubwa Sana." nilisema, yule mlinzi akasema.
"Sawa twende kulee kwenye kile chumba tukaongelee mule" alisema huku akiwaambia na wenzake wote tukazipiga hatua hadi tukafika kwenye kile chumba kisha yule mlinzi akaufungua mlango tukazama ndani wote kisha akaufunga mlango kwa ndani.

"Haya sasa humo hakuna anayeweza kusikia tuambieni sasa hiyo siri halafu na sisi tukamfikishie mfalme." alisema yule mlinzi akiwa na shauku yakujua hiyo siri, mimi nikamsogelea huku nikiwakonyeza yusrat pamoja na juma, nikamwambia yule mlinzi.
"Iko hivi nyie wote mnakufa!!.." bila kupoteza mda tukaanza kuwashughurikia wale walinzi tukawafyeka shingo zako kwakutumia mikono yetu iliyotoa makucha marefu naya kuchongoka kama nyembe. Baada yakumaliza lile zoezi tukawatoa nguo zao tukazivaa sisi halafu tukachukua na sura zao kisha ile miili tukaipoteza, kile chumba kikabakia safi.

Tukatoka ndani yakile chumba tukazipiga hatua mpaka pale kwenye zile ngazi tukapanda juu, moja kwa moja tukaelekea kwenye mlango uliokuwa unaonekana kwa mbele tukakutana na walinzi ila hawakusema chochote tukafungua mlango tukaingia ndani ya kile chumba, kilikuwa nikibalaza anachokaaga mfalme pale mbele kulikuwa na kiti cha mfalme ila kilikuwa wazi hakuwepo mfalme nyuma ya kile kiti walikuwepo walinzi watatu wamesimama.

"Samahani mfalme yuko wapi tunashida nae ya muhimu sana." alisema yusrat akiwa kwenye umbile la kiume, wale walinzi wakuu wamfalme wakajibu.
"Ametoka kidogo ameenda kwenye chumba chake kaeni hapo kwenye sofa mumsubiri anakuja mda si mrefu." alisema mmoja kati ya wale walinzi, nasi tukaitikia.
"Sawa!" kisha tukakaa mara yusrat akanisogelea akaninong'oneza kitu, nikatingisha kichwa kuashiria nimemuelewa, Bila kuchelewa yusrat akanyoosha mkono kuwaelekezea wale walinzi, walishtuka!!. baada ya kuona wanasotwa wakataka kupaniki yusrat akawagandisha, waliganda wakiwa wamekunja sura zao mwingine aliganda akiwa anapiga hatua zakutufata.

Wakabadilika wakawa masanam punde si punde wakabadilika tena wakawa udongo wakamong'onyoka wakateketea wote, pale chini ukasambaa mchanga. Yusrat akanyosha mkono tena ule udongo ukapotea pakawa safi, nasi bila kupoteza mda tukajibadilisha tukachukua sura na miili ya wale walinzi kisha tukasogea tukasimama nyuma ya kiti cha mfalme, tukiwa tumesimama pale mara tukaona mlango unafunguliwa aliyekuwa ameingia si mwingine ni mfalme damor......ITAENDELEA...

Usikose sehemu ya 45..RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu Ya 45

TULIPOISHIA..
Nasi bila kupoteza mda tukajibadilisha tukachukua sura na miili ya wale walinzi kisha tukasogea tukasimama nyuma ya kiti cha mfalme, tukiwa tumesimama pale mara tukaona mlango unafungiliwa aliyekuwa ameingia si mwingine ni mfalme damor......

SONGA NAYO...
Alisimama mlangoni kisha akawa anatutazama mara akaonesha sura ya walakini kama vile kuna kitu anafikiria mara akarudi alipotokea mlango ukafungwa.

Tuliangaliana kwa mshangao tukahisi labda tutakuwa tumeshtukiwa, wakati tukiwa kwenye Hali ile ya mshangao mara akaingia kijakazi mmoja wa kike akiwa ameshika sahani iliyo kaliwa na kikombe kwa juu, alifika anaviweka pale kwenye meza ya mfalme kisha akaugeuza mwili wake akazipiga hatua za kurudi alipotoka.

Tulipo inua vichwa vyetu kuangalia ndani ya kile kikombe kuna Nini!!., tuliona kimejaa dam.
Yusrat akamwambia juma.
"Juma kalete kile kikombe chenye dam niwaoneshe kitu" juma bila ajizi akazipiga hatua chache hadi pale kwenye ile meza akachukua kikombe tu akaacha sahani akamletea yusrat, yusrat akakipokea kwa mikono miwili akakishikilia vizuri kisha akawa anaitazama ile dam iliyokuwa kwenye kikombe, mara akaasama mdomo wake akatoa hewa iliyo fanana na moshi, ule moshi ukaingia kwenye kile kikombe baada yakumaliza zoezi lile akampa juma ili akirudishe kile kikombe pale mezani, juma akiwa ananyanyua mguu ili apige hatua ya kwenda pale mezani mara ghafla!!.. Mlango ukafunguliwa akaingia mfalme damor, juma akabaki amedema huku akiwa amekishikilia kile kikombe chenye dam.

Mfalme damor hakusema chochote, alizipiga hatua hadi kwenye kiti chake akakaa, juma akasogea hadi pale mezani akakiweka kile kikombe pale mezani.
Mfalme damor akageuza shingo akamtazama kisha akamuuliza.
"Mbna sielewi hichi kinywaji ulikuwa nacho wewe halafu hii sahani ilikuwa hapa hapa mezani imekuaje kuaje au ulikuwa unaiba kinywaji changu ili unywe?."
"mtukufu mfalme hapana kijakazi ameileta hapa mda si mrefu sasa nilikuwa naingalia kama ni salama."
"Kwani hiyo ni kazi Yako?. We kazi yako hauijui?.."
"Mtukufu mfalme kwa Hilo naomba unisamehe nilitaka mfalme wangu unywe kitu salama"

"Hebu nenda kamuite mganga wangu kule kwenye chumba chake, fanya haraka sana." alisema mfalme damor akionesha sura ya hasira.. Juma akashtuka akashangaa, kwanza kilicho mfanya ashangae nikusikia aende akamuite mganga wakati hajui hata chumba chake kiko wapi!!. Pili alijua kwenye kile kinywaji kulikuwa na sumu aliyo iweke yusrat kwahyo ilimshtua kusikia vile, hata sisi pia maneno yale yalitushtua.

"Unashangaa nini yani nakuagiza unaanza kunitumbulia mimacho, we Saru umeshaanza kuwa na kiburi et eeh?.."
"Hapana mtukufu mfalme naenda! naenda!!.." alisema juma huku akizipiga hatua za haraka haraka akaondoka mahala pale, Baada ya juma kuondoka mfalme akatugeukia sisi kwa nyuma akaanza kutuuliza.
"Rajo na bofiz naomba mnijibu saru alikuwa anakifanya nini kinywaji changu?.."
"Mtukufu mfalme sisi tuliona alikuwa anakiangalia tu kama kiko salama ndo kipindi anataka kukirudisha wewe ukatokea hakuwa anafanya chochote kibaya." nilisema Mimi, mfalme akaonesha sura ya upole akajibu.
"Ooh!!. Sawa" akageukia mbele.

Upande wa kule alipokuwa juma, alikuwa anatanga tanga tu asijue pakuelekea. Mara akaona walinzi wanne wakipita maeneo yale akawasimamisha akawauliza.
"jaman samahanini hivi chumba cha mganga wa mfalme kiko wapi?.." mmoja akanijibu.
"Heeeh!!. Unatuuliza tena sisi wakati wewe na wenzako ndo mnaendaga na mfalme kila siku kwenye chumba cha mtabiri?.." juma akajibu
"Kwanza umechanganya mi namuulizia mganga sio mtabiri unaye msemea wewe."
"Heeeh!!!.. Makubwa mtabiri sindio huyo huyo mganga au imekaaje hiyo?.."
"Huyu atakuwa amechanganyikiwa sio akili zake hizo yani mtu mmoja anawagawa wanakuwa wawili wakati anajua kabisa?.., tumuelekezeni TU atakuwa leo hayuko sawa." alidakia mwingine.
"Sasa sikia nenda moja kwa moja mpaka kule mwisho utaona kona inakata kulia nenda nayo hiyo utaona vyumba viwili upande huo ila we gonga chumba cha kwanza kabisa ndo chumba cha mtabiri." wale walinzi walimaliza kutoa maelekezo kisha wakaondoka zao, juma akazipiga hatua kuelekea alipo elekezwa na kweli akafika akagonga mlango ukafunguliwa na mzee wa makamo, akamuelezea kama anaitwa na mfalme kisha akaja nae moja kwa moja hadi ndani ya sebure Ile.

"Mtabiri wangu, mganga wangu wa ukweli ninae kukubaliiii!!, karibu sana kaa hapo." alisema mfalme damor akiwa anatabasam
"Asante mfalme wangu nimeitikia wito wako" alisema mtabiri yule akiwa anaangaza angaza kila sehem ya sebure ile iliyokaa kama kibalaza, mtabiri alionesha kuingiwa mashaka na kitu ndomana macho yalikuwa hayatulii sehem moja pia alikuwa anatuangalia sana sisi.

"Sasa nilicho kuitia ni hichi hapa, angalia hicho kinywaji kama kiko salama maana nimeingiwa na mashaka ghafla!!." alisema mfalme huku akikisukuma kile kinywaji hadi karibu na mtabiri, mtabiri akakichukua kisha akakishika akaanza kukiangalia kwa umakini,
"Mmmh!!.." aliguna mtabiri kisha akakiweka chini kile kinywaji.
"Kuna nini mbona umeguna? Au kina sumu?."
"Bila shaka mfalme hichi kinywaji kina sumu na hii sumu ni kali sana, kwanza nani aliyekileta hichi kinywaji?." nikataka kujibu mimi juma akawahi akajibu yeye.
"Ni kijakazi wa humo" alisema juma.
"Haya naomba uende ukamuite aje haraka sana" alisema mfalme, juma akaenda hadi kwenye chumba chao akagonga mlango mdada mmoja akafungua.

"Naomba uniitie yule dada aliyempelekea kinywaji mfalme" yule dada hakujibu kitu akafunga mlango baada ya mda kidogo ukafunguliwa tena sasa aliyetoka safari hii ndo alikuwa muhusika mwenyewe akamwambia.
"Twende unaitwa na mfalme"
"Naitwa?.. Kwani nimefanya Nini?.." alisema huku akiwa anaufunga mlango nakunifata nyuma, alionesha sura ya kiulizo.
"We twende utajua huko huko" juma alimjibu, ila akasimama akamgeukia yule Binti.

"Sikia nikupange kitu, ukiulizwa kile kinywaji ulikimimina wewe ukatae useme ulikikuta tu jikoni kimeshamiminwa we ukakichukua tu, sawa!!. tumeelewana?.."
"Hayo yote yanatokea wapi?. kwani kuna Nini? Mbona sikuelewi?."
"We useme nilivyo kwambia ukijichanganya utajua mwenyewe." alisema juma huku akizipiga hatua za kwenda mbele na yule kijakazi akiwa nyuma ake anamfata, wakafika hadi sehemu husika.

"Mtukufu mfalme yule binti aliye leta hicho kinywaji ndo huyu hapa." alisema juma kisha akaja kujiunga nasi sehemu tulipokuwa tumesimama.
"Wewe binti hichi kinywaji ulikitolea wapi?.." aliuliza mtabiri.
"Nilikitolea jikoni kwani kina Nini?.." aliuliza yule kijakazi akiwa amepiga magoti.
"Hichi kinywaji kina sumu, hebu tuambie kwanini umeweka sumu kwenye kinywaji cha mfalme ulitaka umuuwe?.."
"Hapana!!!.. hapana!!.. Siwezi kufanya hivyo siwezi kabisa!!.., mi nilikuta hicho kinywaji kimeshamiminwa kwenye hicho kikombe mi nikakichukua hivyo hvyo nikaja nacho, labda kosa langu ni Hilo." alisema yule kijakazi akiwa ameinua mikono ishara yakuomba msamaha, hadi tulikuwa tunamuonea huruma.

"Nikikuangalia nakuona kabisa unasema uongo, naomba useme ukweli kabla hujapewa adhabu ya kunyongwa" alisema mtabiri.
"Basi nasema ukweli kabisa!!!. Hicho kinywaji sikukuta kimemiminwa kama nilivyo sema mwanzo bali nilikimimina mwenyewe kisha nikakileta sikuweka chochote kibaya."
"Hapo sawa naona kabisa umesema ukweli, haya unaweza ukaenda." alisema mtabiri yule kijakazi akainuka haraka haraka huku akisema asante nyingi nyingi, akaondoka pale kwa kasi akafungua mlango akatokomea.

"Sasa mbona umemuambia aende!! wakati bado hatujamalizana nae?.." alisema mfalme akiwa anashangaa maamuzi ya mtabiri.
"Tushamalizana nae amesema ukweli wake nami nimeona kweli alikuwa anasema ukweli, ulitaka umuulize nini tena kingine?.." aliuliza mtabiri.
"Sawa!!. kwahyo tunafanyaje hebu jaribu jaribu kuangalia kwenye maono Yako uone aliyeweka hiyo sumu ni nani.." alisema mfalme, mtabiri akajibu.
"Sawa ngoja niangalie"
"Ila subiri usiangalie kwanza kuna kitu nimekumbuka wakati naingia hapa nilimuona huyu mlinzi wangu saru akiwa amekishika hichi kinywaji nilipo muuliza akasema et alikuwa anakiangalia kama kiko salama wakati uwezo huo hana na anajua kabisa sio kazi yake, hebu naomba naye muulize aseme kama alivyo niambia tuone kama na yeye anasema ukweli." alisema mfalme damor, Mtabiri akamtazama juma kisha akasema.

"Hebu sema ulivyo muambia mfalme?.." juma akiwa na kitetee akasema.
"Hicho kinywaji mi nilikuwa nakiangalia tu kama kiko salama"
"Hapana mfalme huyu anasema uongo itakuwa yeye ndio muhusika" alisema mtabiri........ITAENDELEA..

Usikose Sehemu ya 46.
[4/2, 14:24] AzEr: Agizo la majini 46-49RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu Ya 46

TULIPOISHIA..
"Hebu sema ulivyo muambia mfalme?.." juma akiwa na kitetee akasema.
"Hicho kinywaji mi nilikuwa nakiangalia tu kama kiko salama"
"Hapana mfalme huyu anasema uongo itakuwa yeye ndio muhusika" alisema mtabiri........

SONGA NAYO...
"Au kama sio muhusika basi aliyeiweka hiyo sumu atakuwa anamfahamu, naomba utuambie ukweli" alisema mtabiri huku akiwa anamtazama juma.
Juma akasema
"Ukweli ndio huo mi sijui chochote nilikishika tu hicho kikombe kwaajili yakuangalia kama kina usalama kisha nikataka kukirudisha ndo mfalme akatokezea."
"Sawa! inaonesha we sio muhusika ila kuna kitu unakijua, hebu wewe rajo tuambie ukweli maana nyote mnaonekana kuna kitu mnakijua" alisema mtabiri akininyoshea kidole Mimi, nilishtuka kidogo ila nikawa sawa.

"Aaah!! mtabiri kama alivyosema saru ndo hvyo hvyo nasi tulimuona anakiangalia tu kama kiko salama."
"Hapana!!.. Inaonesha kuna kitu mnajua mnakificha hebu bofiz tuambie na wewe ukweli wako?.." alisema mtabiri mkono akimnyoshea yusrat aliyekuwa kwenye umbo la bofiz.
"Aaah!!. Kama alivyoona rajo basi na mimi niliona hvyo hvyo hakuna kibaya alicho kifanya." alisema yusrat, mtabiri akamkazia macho kisha akasema.
"Inaonesha unasema uongo, mashaka yangu kwako yamekuwa makubwa kuliko kwa wenzako inaonesha wewe ndio uko karibu na ukweli, naomba uniambie hii sumu iliyoko kwenye hiki kinywaji hujaiweka wewe?.."
"Ndio sijaiweka mimi na sijui aliyeiweka." alisema yusrat akiwa hana hata wasi wasi.

Mtabiri alikunja sura akaanza kujipiga piga kichwani ilionesha kichwa kinamuuma.
"Mtabiri wangu nini kimekusibu?.. Mbona unajipiga piga hivyo?.." mfalme alimuuliza.
"Sielewi mfalme wangu nahisi kuna kitu kinanichanganya, ghafla naona ukweli uko mbali na hawa inaonesha hawa walinzi wako hawajui chochote, kila nikijaribu kumtafuta muhusika kichwa kinagonga haji kabisa kwenye ufaham wangu, tuachane na hili litanipasua kichwa changu hiyo sumu ikamwagwe, tuendelee na mambo mengine." alisema mtabiri.

"Sasa mbona sikuelewi!!. Hivi huoni kama hili jambo ambalo limetokea ni hatari kwangu, kama mbaya wangu yuko karibu sitauwawa Mimi?.." alisema mfalme damor akiwa anajiinua kutoka kwenye kiti chake na kusimama.
"Nisikilize, we usile wala kunywa chochote mpaka uniite mimi kwanza niangalie kama kitakuwa salama, tumeelewana?.."
"Ndio nimekuelewa" alijibu mfalme huku akiwa anaushusha mwili wake kwenye kiti cha kifalme. Mtabiri baada yakumaliza kuongea vile alizipiga hatua za kuondoka mahala pale mwisho akatokomea.

Mfalme damor akiwa amekaa kwenye kiti chake, mara mlango ukafunguliwa kwa Kasi akaingia ndani mlinzi mmoja akiwa anahema kwa kiasi chake, akasogea hadi karibu na mfalme kisha akasema.
"Mtukufu mfalme, kuna taarifa tumeletewa kuwa mke wako malkia yurhi yuko njiani anakuja."
"Ooooh! Waooo!!.. Hizo habari ni nzuri kwangu, nahisi alikuwa anataka kunifanyia surprise sasa nimewahi kuzipata taarifa acha na mimi nimfanyie surprise, hivi anatumia usafiri gani kuja huku?.."
"Wako kwenye usafiri wa farasi pamoja na majeshi kadhaa"
"Oooh!! sawa rajo twendeni tukampokee." alisema mfalme akituambia sisi walinzi wake tumfate bila ubishi tukamfata nyuma, tukaenda mpaka chini tukapanda usafiri wa farasi kisha tukaanza kuondoka tukiwa na walinzi wengine baadhi.

Sisi tukiwa mstari wa nyuma ya mfalme, Nikapata wazo nikawasogelea zaidi yusrat na juma kisha nikawaambia.
"Malkia yurhi akifika huku na Yale majeshi aliyokuja nayo itakuwa kazi ngum kwetu kukamilisha mpango wetu maana watakuwa na nguvu kubwa zaidi cha kufanya hapa mi nawafata huko huko kabla hatujakutana nao niwe nishafanya kitu."
Walitikisa kichwa kuashilia wamekubaliana na Mimi.

Nikatoweka mahala pale na farasi wangu nikatokezea kwenye msafara wa malkia yurhi nikajichanganya nyuma ya majeshi Yake, hawakuweza kunitambua kwakuwa walikuwa wengi sana na pia ilikuwa ni ngum wote kukalilika.
Nikiwa nyuma ya msafara ule nikaanza kuwafyeka wale wa nyuma wote, nilikuwa na kisu kama kile cha yusrat kinacho zunguka kama feni na pia kile kisu hakikuwa kinaonekana kwa macho ya kawaida kilikuwa kinatoa vichwa vya mashetani wale kimya kimya, wale mashetani walikuwa wanadondoka chini farasi zinaendelea na msafara hakuna ambae alishtuka kama wengine wanapungua nyuma kwakuwa hawakuwa wanageuka nyuma, nyuso zao wote zilikuwa zinaelekea mbele hakuna kugeuka nyuma na kingine kilichokuwa kinawadanganya ni miguu ya farasi zilizokuwa hazijabeba chochote, basi walivyokuwa wanasikia zile hatua walijua wako kamili kama angetokea hata mmoja wakugeuka nyuma angeshtuka sana jinsi farasi zilivyokuwa tupu.

Kisu cha changu nilikuwa nakirusha tu kinaenda kufyeka vichwa kama ishirini kisha kinarudi nakishika tena nakirusha kinaenda tena kinafyeka vichwa ishirini kinarudi hivyo hivyo hadi wakabakia wachache hakuna ambae alishtukia hata mmoja, nikarusha tena kikafyeka haraka haraka vichwa na miili vikadondoka chini wakabakia kumi tu hawakuwa wanasikia vishindo vya wenzao kudondoka kwa sababu niliwatoa uzito walikuwa wanadondoka kama makaratasi tu nikarusha tena kile kisu kikadondosha vichwa vya wale kumi akabakia malkia yurhi peke yake.

Nikamwita "malkia yurhiiiiiii!!!.." Akasimamisha farasi tu bila kugeuka nyuma na zile farasi zingine zilizokuwa tupu zikasimama pia, nikasema.
"Sasa malkia gani unaenda tu hata huangalii nyuma kama majeshi yako yapo salama?.. Mmmh!!. Et nakuuliza malkia mrembo" nilisema kwa nyodo, malkia yurhi alionesha kushtuka akageuka nyuma upesi.
"Heeeeeh!!!.." alishtuka Akaasama mdomo akiwa haamini anachokiona farasi zilikuwa zimepangana msururu mrefu kweli kweli zikiwa hazina mwanajeshi wake hata mmoja tofauti na Mimi, alihisi kupagawa akaona maruwe ruwe akailalia ile farasi akazimia pale pale juu akiwa anataka kudondoka nikaruka kutoka kwenye farasi nikamuwahi nikamdaka kisha nikatoweka nae mahala pale farasi zote zikabaki zimesimama tu vile vile.

Ule msafara wa mfalme damor wa kwenda kumpokea malkia yurhi, ulizidi kuchanja mbuga baada ya mwendo mrefu kidogo waliona msururu wa farasi kwa mbali zikiwa zimesimama mfalme akageuka nyuma akamuuliza yusrat ambae alikuwa kwenye muonekano wa bofiz.
"Zile si farasi zile?.."
"Ndio ni zenyewe mfalme wangu" alisema yusrat sauti ya base
"Halafu mbona simuoni rajo yuko wapi?.." aliuliza mfalme baada yakugeuka nyuma nakuona walinzi wake wa karibu wakiwa wawili tu.
"Mtukufu mfalme humuoni si huyu hapa?.." alisema yusrat, mfalme akageuka nyuma tena akaniona.
"Ooh!! sawa maana nilikuwa simuoni."
"Alikuwa amesogea kwa pale pembeni ndomana hukumuona" alisema yusrat kisha akanisogelea akaniambia.
"Unabahati wewe umekuja mda muafaka vipi kazi umeimaliza?.."
"Ndio nimefyeka wote kasoro malkia yurhi tu"
"Ooh vizuri zile farasi zilizo simama kule mbele ndo zilikuwa zimebeba yale majeshi?.."
"Ndio zenyewe."
"Hongera kazi nzuri."
"Asante" nilijibu.

Safari ikazidi kushika hatam baada ya mwendo kidogo tukafika karibu na zile farasi, mfalme akaamrisha baadhi ya maaskari waliokuwa mbele wanaongoza msafara washuke wakaangalie kwanini zile farasi zimesimama na zimetokea wapi.
Wakashuka kama kumi wakasogea hadi kwenye zile farasi wakaanza kuziangalia juu mpaka chini ila hawakufanikiwa kuzijua wakazidi kusonga mbele zaidi, ghafla!!.. Wakaona wanajeshi kumi wakishetani wakiwa chini ya farasi wamekatwa vichwa, askari mmoja akapaza sauti.
"Mtukufu mfalme ndo huu msafara tuliokuja kuupokea maana hawa wanajeshi walio fariki hapa wanatoka kwenye mji wa trofi."
"Heeeeh!!!.. Unasemaje wewe?.." alishtuka mfalme akauliza kwa mshangao akatoka kwenye farasi akaruka chini kisha akakimbilia
kule walipo wale askari, na sisi walinzi wake wa karibu tukaruka tukamfata nyuma.

"Heeeeh!!!.. Nani amewauwa kikatiri namna hii??? Na mke wangu yuko wapi mtafuteni haraka nendeni Hadi kule muone kama mtamuona..." Mfalme alisema kwa machungu huku machozi yakiwa yanamtiririka mashavuni alikuwa na hasira pia za watu waliofanya ukatiri ule, wale maaskari wakazidi kusonga mbele zaidi mara wakaona wanajeshi ishirini wakiwa wameuwawa kama wale wa mwanzo vile vile.

Wakamuita Tena mfalme, mfalme akatoka mbio akakimbilia kule alipoitwa nasi tukamfata, alipofika akaona jinsi wanajeshi wake walivyouwawa kama wale wa mwanzo akashikwa na hasira akachomoa upanga kwenye kiuno cha askari mmoja akamfyeka kichwa huyo huyo askari kichwa chake kikadondoka chini, akanigeukia mimi akaniwekea panga shingoni, nilishtuka nikaanza kurudi nyuma akawa ananifata.....ITAENDELEA...

Usikose Sehemu ya 47.RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu Ya 47

TULIPOISHIA..
Kichwa chake kikadondoka chini, akanigeukia mimi akaniwekea panga shingoni, nilishtuka nikaanza kurudi nyuma akawa ananifata......

SONGA NAYO...
"Yani mnanishangaa shangaa badala mumtafute mke wangu fanyeni hivyo haraka Sana" alisema mfalme kwa hasira akiwa anautoa upanga kwenye shingo yangu, bila kuchelewa tukaingia katikati ya zile farasi tukaanza kumtafuta mke wake.

Nilijifanya kujitafutisha, tukatoka kwenye ule msururu wa farasi tukawa tunamtafuta kwenye ile njia waliyo pitia, tukaenda mbele kabisa lakini mwili wa mkewe haukupatikana tukageuza tukarudi kumpa taarifa.
"Mtukufu mfalme tumetafuta kote hatujamuona, tunaona tu maiti za majeshi walio uwawa.

"Unasema nini wewe?.. Au mke wangu hakuja na huu msafara?.." aliuliza mfalme kwa jaziba.
"Mtukufu mfalme ndo huu huu msafara na malkia yurhi alikuwa mbele ya huu msafara siunaona farasi yake ile palee" alisema askari mmoja, mfalme akageuza shingo kuangalia kule mbele alipo elekezwa na yule askari kwa kidole, bila kupoteza mda akazipiga hatua za haraka haraka kwenda kwenye ile farasi, akafika anaingalia vizuri nakuona kweli ni yenyewe.

"Endeleani kumtafuta, kama ndo hii farasi aliyokuwa amepanda basi atakuwa hayuko mbali, rajo turudini." alisema mfalme akituambia sisi walinzi wake na baadhi ya maaskari turudi nae kwenye kasri ya kifalme, wengine wakabaki wanamtafuta. Tulipanda juu ya farasi tukaondoka mahala pale, Mfalme alionekana kuwa na hasira Sana pia na mawazo mengi, kilikuwa kinatembea kiwili wili tu ila nafsi ilibaki kule tulipo Toka.

Baada ya mwendo mrefu kidogo tulifika kwenye kasri ya kifalme tukashuka chini moja kwa Moja tukaingia ndani, mfalme akaelekea kwenye chumba cha mtabiri na sisi walinzi wake watatu tukamfata nyuma hadi ndani ya chumba kile cha mtabiri.

"Naomba uniangalizie hali ya mke wangu kama ni mzima au amekufa na atakuwa yuko wapi saivi?.." alisema mfalme maneno ya haraka haraka akiwa anamwambia mtabiri
"Sawa ngoja niangalie" mtabiri alifumba macho kisha akawa ananuia maneno anayo yajua yeye, alipomaliza akasema.
"Inaonesha malkia yurhi bado ni mzima na kuhusu sehem alipo, inaonesha ametekwa japo sijajua ni wapi."
"Hebu angalia ujue ni wapi twende tukamkomboe kabla hajauwawa." alisema mfalme, mtabiri akamjibu.
"Kiukweli sioni amewekwa sehem gani ila naona tu ametekwa."
"Yani umeona ametekwa halafu unashindwa kuona alipo?.. Ndo nini Sasa unataka kuniambia nguvu zako ni ndogo huwezi kuona alipo?.."
"Nahisi hivyo maana hapa kila nikijaribu kuangalia sioni alipo"
"Haya naomba uangalie walio mteka ni wakina nani?.." alisema mfalme na mtabiri akawa anaangalia.

"Mmmmh!!.." aliguna mtabiri baada yakuona kitu akasema.
"Naomba uwaambie walinzi wako wote watoke nje" alisema mtabiri na mfalme akatekeleza akatuambia twende nje na sisi tukatoka tukafunga mlango kwa nje, tukaweka maskio kwenye ule mlango ili tusikie walichokuwa wanazungumza, tulisikia kwa mbali mtabiri akiongea.
"Kati ya hao walinzi wako kuna mmoja ndo amemteka, sijajua sasa kama ni kwa nia nzuri ama mbaya ila usioneshe dalili yoyote kama umejua we vunga ili tumtegee mtego tumnase kiulaini."
"Haya sawa niambie sasa ni nani kati ya hao walinzi wangu?.."
"Kiukweli Sijajua ni yupi ila kati ya hao watatu."
"Halafu unajua naanza kuwa na mashaka na huo uwezo wako, yani wewe ukiona kimoja kingine hukioni ndo nini sasa unatakiwa uone vyote."
"Kweli mfalme wangu nahisi uwezo wangu umepungua sio kama ule wa mwanzo" alikili mtabiri, mfalme akasema.
"halafu kingine umesema mmoja kati ya walinzi wangu ndo amefanya hivyo mbona sasa nilikuwa nao wote kwenye ule msafara, huyo mmoja alimteka saa ngap?.."

"Mfalme wangu hivi kipindi mnaenda kumpokea malkia yurhi, unauhakika hao walinzi wako wa karibu walikuwepo wote?.." mfalme alionekana kutafakari kitu kisha akasema.
"Mmh!.. Kweli hawakuwepo wote kuna mmoja sikumuona tena nilimuangaza angaza kwa yale majeshi mengine sikumuona, ila baada ya sekunde kadhaa tu et nikamuona."
"Basi huyo ndo atakuwa muhusika" aligongelea nyundo mtabiri, sisi tukiwa mlangoni tuliyasikia kwa mbali yale maongezi.

Mfalme akasema
"Ooooh!!.. Kumbee!!.. Nishamjua aliyemteka mke wangu ni rajo sindio?.."
"kama huyo ndo hukumuona basi ndo huyo huyo."
"Ngoja nimfate aniambie kwanini amemteka mke wangu na asipo nipa jibu la kueleweka namchinja kichwa chake."
"Hapana mfalme wangu usifanye hivyo, we tulia jikaze jifanye kama haujui chochote usimuoneshee dalili zozote maana ukifanya mambo kwa pupa unaweza kumkosa hata mke wako, mi takuita nikuelekeze cha kufanya sasa hivi kapumzike kwanza."
"Yani nikapumzike mke wangu ametekwa?.. Huo usingizi nautolea wapi?.."
"Mfalme wangu naomba unisikilize Mimi, sawa ametekwa ila kuwa na amani hawezi kufanywa chochote kibaya inaonekana yuko sehem salama kabisa."
"Wapi sasa hiyo sehem salama?.."
"Kwa kweli sijajua ni wapi ila inaonesha ni sehemu salama." mfalme hakuongeza neno lingine alijiinua pale alipokuwa amekaa akasogea hadi mlangoni akataka kufungua mlango ukagoma kwakuwa tulikuwa tumeufunga kwa nje. Tukaufungua kwa nje mfalme akatoka amefura kwa hasira hakusema chochote akatupita akazipiga hatua za haraka haraka na sisi tukamfata tukaenda mpaka kwenye chumba chake akafika anaufungua mlango akazama ndani kisha akajifungia.

Sisi tukabaki pale sebureni
"Kwhyo tunafanyaje sasa, bro umeshajulikana kama wewe ndio muhusika" alisema juma.
"Mi nachoona hapa ni kudili na yule kwanza maana atatuharibia mipango yetu" nilisema, wakina yusrat wakaniuliza.
"Yule nani wakudili nae?.." nikawajibu
"Njoeni nifateni" bila ubishi wakanifata moja kwa moja tukarudi tulipotoka, tukaenda mpaka kwa mtabiri tukafika tunagonga mlango baada ya sekunde kadhaa mtabiri akaufungua ile anasogeza shingo kuona anayegonga nikamkwida shingoni nikaanza kumnyonga kwa kutumia mikono yangu mara akapotea kimiujiza nikabaki naniga hewa, tukazama ndani.

"Hayupo mbali yuko hapa hapa, yule pale juu" alisema yusrat nami ndio nikakumbuka mbinu niliyo elekezwa na sarha jinsi ya kumuona mtu aliyejificha kwa nguvu za Giza, nikafumba macho nikafanya kama nilivyoelekezwa nikafumbua nikamuona amenasia juu ya Dali nikamshusha chini kwa kumnyoshea kidole akadondokea kwenye kitanda chake, akajiandaa ili apotee tena nikamuwahi nikautoa uwezo wake wa kupotea kwakukunja viganja vya mkono wangu na kunuia nachotaka na kweli nikafanikiwa nikamsogelea sasa nikamkwida shingoni tena, nikayatoa makucha yangu nikawa nayachomeka kwenye shingo yake yakazama kabisa ndani dam zikawa zinachuruzika nakunilowanisha mwilini na usoni nikakikata kichwa chake kabisa dam zikaruka juu nikabaki nimeshikilia kichwa tu kiwili wili kikadondoka chini, dam zikatapakaa ndani ya chumba kile, nikakitupa kile kichwa chini kisha nikaunyosha mkono wangu nikaupoteza ule mwili ukatoweka kisha nikakausha dam zote hali ikawa shwari hata zile dam zilizo nirukia na zingine kuwarukia wakina yusrat zikapotea tukawa kama tulivyo ingia.

Tukazipiga hatua za kusogea mlangoni mara tukasikia mlango unagongwa bila wasi wasi wowote nikasogea nikaufungua mlango nikamuona mlinzi mmoja akiwa amesimama akasema.
"Niitie mtabiri nimeagizwa kwake" nikamuuliza
"Aliyekuagiza nani?.."
"Ameniagiza mfalme"
"Haya niambie nimfikishie taarifa"
"Hapana amesema ni mwambie mwenyewe." nikaona kama analeta ubishi nikamkaba roba
"Haya sema kabla sijainyofoa roho Yako" akaanza kusema kwa tabu nikamregezea kidogo
"Ameniagiza nije nimuite aende kuna kitu cha muhimu anataka amuoneshe" alisema yule mlinzi wa kasri ile, sikutaka kumuachia aende Kwa kuwa amejua asili yangu nikamnyonga kabisa akafariki, nikaupoteza ule mwili.

Yusrat na juma wakatoka nje tukaondoka maeneo Yale.
"Sasa kazi imeanza kila tutae kutana nae tunaisafirisha roho yake." alisema yusrat nasi tukamuunga mkono, tukazidi kuzipiga hatua, mbele tukakutana na walinzi wanne wakiwa wanafanya doria, hatukutaka kujichosha sana tulirusha visu vikaenda kuwafyeka vichwa kisha vile visu vikarudi mikononi mwetu, kama kawaida tukaipoteza ile miili tukasonga mbele, mpango wetu ilikuwa ni kwenda kumuangamiza mfalme damor moja kwa moja tukaenda hadi chumbani kwake tukagonga mlango, mara akatokezea mlinzi mmoja ndani ya chumba kile alionekana kuwa na wasi wasi hatukutaka kumruhusu apite tuliitoa roho yake, kisha tukaufungua mlango tukazama ndani ya chumba cha mfalme.

Hatukumuona mfalme tukawa tunamtafuta kila sehem ila bado tuligonga mwamba hakuonekana, yusrat akaonekana anafikiria kitu kisha akasema.
"Picha kama inanijia hivi!!!.. itakuwa yule mlinzi tuliye muuwa hapo mlangoni alituona kipindi tunawauwa wale walinzi wanne kule, ndo akaja kumpa taarifa mfalme na inaonekana mfalme ametoroka itakuwa humu Kuna njia ya siri." alisema yusrat nasi picha ikaanza kutujia maana yule mlinzi alitoka ndani ya chumba kile akiwa na wasi wasi kweli kweli.....ITAENDELEA..

Usikose Sehemu ya 48.
RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu Ya 48

TULIPOISHIA..
Alisema yusrat nasi picha ikaanza kutujia maana yule mlinzi alitoka ndani ya chumba kile akiwa na wasi wasi kweli kweli.....

SONGA NAYO..
"Sasa tunafanyaje?.." aliuliza juma.
"Itajulikana mbele kwa mbele tupige mruzi wa ishara majini yaliyopo kule mapangoni yaje tuanze mapambano Sasa"
"Mmmh!!.. Tutaweza kweli majeshi mengi hivi?..." Aliuliza juma.
"Acha uoga tunaweza kikubwa kujiamini halafu sisi tunanguvu za kutusaidia hatuwezi kushindwa." alisema yusrat tukamuunga mkono akapiga mruzi wa kimoyo moyo huku sauti ikiwa haitoki ila kule mapangoni sauti ilisikika vizuri sana vikosi vikajipanga kisawa sawa vikaanza safari sasa yakuja kwenye kasri ya kifalme vikiongozwa na sarha.

Huku sisi tulikuwa tushatoka chumbani kule, sasa tulikuwa tunazunguka ndani ya jengo lile kila tuliye kutana nae tulimuangamiza, nje kulikuwa na majeshi mengi sana hatukutaka kutumia nguvu kwa wale wa ndani tulikuwa tunarusha visu tu vinafanya kazi yake kisha vinarudi. Yale majeshi ya kijini yaliyotoka kule mapangoni na sarha, yalipita kwenye ile njia ya siri kisha yakaingia ndani ya jengo lile la kifalme, wote walitoa mapanga kila waliyekutana nae walimfyeka, sisi upande wa Kule juu tuliwamaliza wote tukashuka chini tukakuta na wenyewe ndo wanawamalizia wa chini, wote kwa pamoja tukatoka nje sasa tukasimama kwenye ngazi za jengo lile.

"Duuuuuh!!..." Niliduwaaa maana ilikuwa Utitili sio utitili majeshi yalikuwa mengi yasio na mfano, nilihisi haja ndogo na kubwa vikitaka kutoka kwa pamoja, juma yeye ndio alikuwa anatetemeka balaa alitamani kukimbia, yusrat pamoja na sarha hawakuwa na wasi wasi wowote maana walizoea mambo yale, sisi ndio tulikuwa na wasi wasi maana tukiangalia nyuma kikosi chetu hata watu mia tano hawakufika ila wenyewe ilikuwa ni maelf na maelf na wote walikuwa wameshika panga, ndani ya geti yalikuwa yamejaa majeshi na nje ya geti pia yalijaa, tuliyaona vizuri kwakuwa tulikuwa tumesimama juu kwenye ngazi ya kwanza kabisa kwa hiyo hadi nje ya geti tuliweza kuona, haukuonekana hata mwisho wa yale majeshi ilikuwa ni nyomi kweli kweli.
"Hakuna kurudi nyuma nikupambana nao" alisema yusrat.
"Duuuh!!. Hapana jaman hata kama tumechaguliwa na tuna bahati ila sio kwa hili nyomi hapa tumeyatimba hata dakika mbili hatuchukui tunafyekwa." alisema juma akionesha uoga wa wazi wazi.

"Hebu jiamini bhan acha uoga uoga" nilimwambia juma lakini mi mwenyewe nilikuwa na hali mbaya nilijikaza tu. Sasa hivi tulirudi kwenye maumbo yetu asilia, tulikuwa tushatoka kwenye maumbo ya wale walinzi wa mfalme.

"Hahahaaa!!.. Nyie jisalimisheni tu hivi mnajiamini nini?. Hamuoni hata wingi wetu hamuogopi?.. Hahahahahaa!!.." alisema mfalme damor kwa zarau huku akicheka, tulisikia sauti tu ila hatukumuona baada yakuangaza angaza macho tulimuona anatokezea mbele ya majeshi yale, akaanza kutembea kwa madoido kuja sehemu tulipo, nikamrushia kisu kikamfata kwa kasi ya ajabu akakikwepa kikazunguka kikarudi mikononi mwangu.

"Hahahaha!.. Hivi mnafikiri mnaweza kuniangamiza kwa huto tuvisu twenu twakukatia nyanya?.. Hahahahaha!!.." alikauka kwa kicheko kisha akatulia akasema.
"Haya sasa simnataka vita haya ngoja niwaachie uwanja bye bye" alisema mfalme damor kisha akapotea mahala pale. Yale majeshi yake yakaja mkuku mkukuu kutushambulia nasi tukachomoa panga kimiujiza tukaanza kuwafyeka kila aliyesogea alipata ukilema na kufariki, upande wa juma ujasiri ulimvaa akaanza kuwakata kata kama yuko buchani, nami upande wangu nilikuwa nawafyeka kama nafyeka majani ilikuwa ni vita kali kweli kweli, yusrat na sarha walikuwa moto wakuotea mbali maana walikuwa wazoefu wa mambo Yale.

Majeshi yetu pia yalikuwa yako vizuri maana kipindi wako kule mapangoni walikuwa wanajifua kisawa sawa wakijiandaa kwaajili ya vita, walikuwa wameiva kisawa sawa kikosi chetu kilijaa watu wenye uwezo mkubwa, uwezo wa jini wetu mmoja ni sawa na majini wao ishirini, tuliwazidi mbali uwezo tulikuwa wachache lakini tulikuwa zaidi ya hatari yenyewe.

Dakika kadhaa tu tukafyeka majeshi yote aliyokuwa ndani ya geti, tukatoka nje sasa tukawaanza na wale waliokuwa nje tuliwachinja vichwa, mikono, miguu, viuno yani tuliwachinja bila huruma, lakini Bado majeshi yalikuwa bado mengi mnoo, tukachomoa tuvisu twetu tukawa tunavirusha tunaenda kufyeka watu ishirini kisha tunarudi, tunavishika tena tunavirusha huku tukiwa na panga tunachinja chinja visu vikirudi tunarusha tena huku tukiendelea kupambana, tulikuwa na speed ya hali ya juu.

Tulipambana kweli kweli hadi tukaanza kuhisi miili yetu inaanza kuchoka sasa maana tulipambana mda mrefu halafu majeshi hata hayapungui kama vile ndo yanaongeza, Tulichofanya tulirusha visu na mapanga vikawa vinapambana vyenyewe na yale majeshi sisi tukawa kwenye hali yakutokuona tukapumzika sehemu kuvuta nguvu mpya. Yale majeshi yakawa yanapambana na visu pamoja na mapanga vilikuwa vinawafyeka kama vile vimeshikwa, bora kupambana na mtu unayemuona maana utajua anataka kunipiga wapi ila ilikuwa ni ngum kupambana navyo walichalangwa chalangwa dam za rangi ya blue zilikuwa zimetapakaa kila sehemu ya maeneo yale, tulitulia zetu sehemu mapanga na visu vyetu vikizidi kuwateketeza ila walikuwa bado wengi mnoo, maana yale majeshi yote yaliyokuwa yameingia mtaani kunyanyasa raia yalipata taarifa yakaja kupambana na sisi kwahyo walikuwa wanaongeza badala yakupungua.

Mda ulizidi kuyoyoma visu vyetu na mapanga vikizidi kuwafyeka tu, sisi tukiwa tumepiga nne tu, sasa wote tukainuka tukaingia ulingoni tukiwa na nguvu mpya tuliwacharanga mpaka wakajuta kuzaliwa tulikuwa na kasi isio ya kawaida tulikata kata viungo vyao, upande wangu, upande wa juma nawa yusrat pamoja na sarha na wale majini wengine tulikuwa hatushikiki waswahili wanasema 'usinichafue men' Hakuna aliyekuwa anaweza kupenyeza panga lake kwetu, sasa kwenye mbavu zetu tuliyatoa mabawa tukawa tunapaa juu juu tulikuwa kama upepo na wenyewe et wakawa wanatufata huko huko juu ili wapambana na sisi waliula wa chuya tuliwafyeka fyeka miili yao ikawa inadondoka chini kama mizigo ya mihogo.

Sasa walikuwa wamepungua tulijawa na matumaini, tukaongeza kasi huku tukirusha vile visu kwa kasi ya ajabu vilitusaidia sana baada yakupambana kwa mda mrefu sasa walibakia wachache Sana, wakataka kukimbia kwakupotea tukawawahi tukawatuliza chini kwakuondoa nguvu zao, mimi, yusrat, juma pamoja na sarha, tukarusha visu vikaenda kuwafyeka wale themanini waliokuwa wamebakia majeshi yote tukawa tumeyafyeka, miili ilikuwa imetapakaa kila sehemu hakukuwa na sehemu hata yakukanyaga, tukaipoteza miili yote kisha tukaenda hadi getini tukafungua geti tukazama ndani, napo miili pamoja dam vilitapakaa tukavipoteza vyote.

"Aliyebakia hapa ni damor" alisema Sarha.
"Hata hayuko mbali yuko hapa hapa yule pale nishamtuliza" alisema yusrat, sarha akamuuliza.
"Mmh!!.. we ulimgandisha saa ngapi?.."
"Kipindi tunapambana nilimuona akiwa anapaa juu akitaka kukimbia nami nikamgandisha huko huko juu." alisema yusrat, bila kuchelewa yusrat akambadilisha kuwa udongo akiwa kule kule juu kisha akamganduruwa ule udongo ukadondoka chini ukajigawa vipande vipande kisha ukatoweka wote, habari yake ikawa imeishia pale pale.

Baada yakumaliza ile kazi tukajiangalia sasa kama tuko salama, mimi yusrat pamoja na juma tulikuwa salama kabisa hatukuwa tumezurika sehemu yoyote ila sarha alikuwa amejeruhiwa kwenye mbavu alichanwa na upanga, na wale maaskari wakijini waliobakia walikuwa wameumia sehemu mbali mbali za mwilini.

Tukaingia ndani ya jumba lile la kifalme kulikuwa kumetapakaa dam pamoja na miili, kama kawaida yetu hatutaki uchafu wala kujisumbua kusafisha tukaipoteza ile miili pamoja na zile dam zote, tukapanda juu kote tukafanya hivyo kisha tukashuka chini, moja kwa moja mpaka kwenye kile chumba chenye njia ya Siri, Tulishtuka baada yakukuta ile njia haipo yani imepotea na kule chini kwenye mapango walikuwa wamebakia majini wengine malkia yurhi niliyemteka na kumpeleka kule pamoja na mama sarha, Tulishtuka....ITAENDELEA...

Usikose sehemu ya mwisho ya kigongo hikiii...RIWAYA: AGIZO LA MAJINI
MTUNZI: MR ROYNOO
WHATSP NO: 0786978618

Sehemu Ya 49 (Mwisho)

TULIPOISHIA..
Tulishtuka baada yakukuta ile njia haipo yani imepotea na kule chini kwenye mapango walikuwa wamebakia majini wengine malkia yurhi niliyemteka na kumpeleka kule pamoja na mama sarha, Tulishtuka....

SONGA NAYO...
Sarha akasogea kisha akasema.
"Mi ndio niliipoteza hii njia ili isionekana kiurahisi, maana kule mapangoni wamebakia wachache wangevamiwa wasingekuwa na uwezo wakujitetea ndomana nilifanya hivyo."
"Ooh!!. Sawa" Sarha alisogea hadi pale ilipokuwa njia akanyoosha mkono wake akanena maneno kadhaa, njia ikaonekana tena mfuniko ukiwa umejifunua.

Wakashuka majini baadhi wakaenda kuwaita wale walio bakia kule mapangoni, sisi tukabaki tumesimama kwenye kile chumba tuki wasubiri. Baada ya mda kupita walirudi wakiwa na surha aliyebadilishwa jina na mfalme damor nakuitwa yurhi, Walikuja na mama sarha pamoja majini wengine wengine chumba kilikuwa hakitoshi ilibidi wengine tupungue tutoke nje ya chumba kile, baada ya wote kuisha ile njia ya siri ilifungwa na sarha kisha wote tukaondoka mahala pale tukaenda moja kwa moja mpaka kule juu kwenye kiti cha kifalme, Surha alitolewa sumu ya kishetani aliyowekea na damor, iliyofanya asiwe anajielewa hadi kudiriki kumuuwa baba ake baada ya kutolewa alirudi kwenye hali yake ya kawaida akawa kama mwanzo alikuwa analia sana nakujutia aliyoyafanya, wote walimsamee.

Ilikuwa ni furaha kubwa sana, ilibidi iandaliwe sherehe yakutupongeza kwa kazi nzuri tuliyo ifanya. Wananchi sasa walikuwa huru na amani ilirejea mtaani furaha maishani mwao ikawa kama zamani, Wananchi na sisi wote tulijumuika pamoja nakusheherekea kupata uhuru, vifijo na nderemo vilitamaraki kila mtaa kwenye wale majini walio toka kule mapangoni, alikuwepo mtabiri mmoja aliyekuwa anatafutwa sana na mfalme damor ili amuangamize maana alikuwa anauwezo mkubwa sana, Ukimuona huwezi kujua kama ni mtabiri kwa jinsi alivyojiweka ili asijulikane.

Mtabiri yule aliifunga mipaka yote ya mji wa jozi hakuna yoyote mbaya angeweza kupita pale mpakani, majeshi yalikuwa machache ila yalikuwa na nguvu sana na wali ongezewa na nguvu za giza milini mwao, wakawa na nguvu maradufu. Mtabiri alipewa jukumu la kumchagua kiongozi mpya wa mji ule, baada yakuangalia kwenye mitambo yake na kuona anayefaa alimchagua sarha kuwa malkia wa mji ule wa jozi na sarha alitakiwa achague mwanaume wakumuoa ili awe mfalme.

Sarha alimchagua juma kwakuwa alitokea kumpenda sana japo alikuwa kijana mdogo ila mimi na yusrat tulipinga lile jambo.
"Hapana juma bado mdogo usikudanganye huo mwili wake anatakiwa kurudi duniani akasome, sasa akiwa huku mipango ya maisha yake ya mbeleni siitavurugika?."
"Maisha gani hayo ya mbele mnayosemea?. Kila kitu sisi tunacho hata akienda kusoma ataenda kutafuta vitu ambavyo sisi tunavyo, na hata asome vipi au awe tajiri wa namna gani hawezi kufikia hata robo ya utajiri wetu, sasa anaenda kusoma Nini??.." Alisema sarha na mtabiri akaongezea.

"Aliyoyasema malkia ni sahihi na naona nyota zao zinaendana kabisa waacheni waongoze mji wetu wa jozi maana ndo utakuwa uongozi salama zaidi."
"Mmmh!!.." ilibidi tukubali tu sisi tulichokuwa tunafikiri juma bado ni mdogo kumuoa sarha mwenye miaka mia nne huko ilikuwa kama sio sawa ila hatukuwa na jinsi maana muhusika mwenyewe ambae ni juma alikubali sasa sisi ni nani tupinge tuliruhusu ndoa ifungwe. Ndoa ikafungwa ikapigwa sherehe ya nguvu ilikuwa ni furaha sana, baada ya mambo yote kukaa sawa sasa tukawaaga Ili tuondoke.

Wakatupa dhahabu nyingi mnoo mabegi mawili yalijaa dhahabu pamoja na hela za kitanzania, majini wa jozi walikuwa wema sana na wao nyama ya binadam walikuwa hawalagi kabisa, sarha na mama ake walituomba sana tuendelee kusaidia wananchi wanao teseka duniani na wachawi majini wabaya, mashetani, vyote vinavyotumika kwa nguvu ya giza tupambane navyo visizuru watu wasio na hatia.

Baada ya kutupa maagizo hayo tulitoweka mahala pale tukatokezea duniani nyumbani kwa yusrat, jambo la kwanza lililo nijia kichwani ni kwenda kumteketeza mzee nyanda, Sikutaka kupoteza mda baada yakuweka yale mabegi chumbani nikamwambia yusrat akakubali tukaondoka wote moja kwa moja mpaka kwa mzee nyanda tukamkuta yuko dukani anahudumia, nilikuwa na hasira nae sana sikutaka kusubiri amalize niliingia mule mule dukani, akashtuka baada yakuniona akanishangaa akajisahau akaniuliza.
"Uwezo huo umeutolea wapi au amekupa nguvu yusrat?.." Wateja waliokuwa wamesimama pale dukani wakisubiri kuhudumiwa walimshangaa mzee nyanda anaongea peke yake maana Mimi hawakuwa na uwezo wakuniona.

Sikutaka kuremba muandiko nikamfyeka kichwa chake kwakutumia kisu, wateja walishtuka na kupiga kelele baada yakuona kichwa cha mzee nyanda kimedondoka chini huku dam zikiruka kwenye bidhaa zake kwao ilikuwa ni maajabu ya karne maana hawakuona kilicho mchinja shingo, mi nikatoweka zangu nikampitia na yusrat aliyekuwa ameganda juu tukaenda moja kwa moja mpaka kwenye vyumba vya misukule tukaifungulia yote tukairudisha kwenye hali ya ubinadam, shida ilikuwa ni kwenye ulimi hawakuwa na uwezo wakuongea tena maana wote walikatwa ulimi.

Hatukutaka kujua kama makwao watapokelewa au watakimbiwa sisi tulicho fanya nikuwasaidia waishi kama watu wengine, baada ya kuwatoa wote nakuwaachia waondoke tulipotea mahala pale tukawa tunaenda kila nyumba ya mchawi tunamfyeka, wachawi wote wa pale kijijini tuliwauwa kila kona ilikuwa ni msiba maana walikuwa wengi, baada yakumaliza lile zoezi tullirudi nyumbani kwa yusrat zoezi lililofata ni kwenda kutambulishana kwa wazazi wa pande zote mbili wakaridhia wote ndoa ikafungwa tanga, wazazi wa yusrat walikuja ikawa harusi ya kimya kimya bila watu kujua maana walifikiri mi ni mzimu, sasa tukawa mke na mme, tukawapa baadhi ya dhahabu wazazi wetu wa pande zote mbili tukawaelezea mwanzo mwisho tulivyo zipata wakaelewa.

Tukaondoka sasa tukaenda kuishi kigoma tukawapunguza wachawi wote waliokuwa wanaua wananchi wasio na hatia, tukatoka hapo tukaenda sumbawanga na penyewe tukafyeka wachawi na majini wabaya kila kinacho tumia nguvu za kiza tulikisambaratisha. Sasa ndo kazi yetu na ndo maisha yetu kusaidia watu kila mkoa tunazunguka tunaangamiza kila kibaya ni mr roynoo hapa niko na mke wangu mrembo yusrat, chaoooo......

MWISHO WA KIGONGO HIKI TUKUTANE KWENYE VIGONGO VINGINE..
 
Safi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom