Sijakamatwa wala kushikiliwa na mtu yeyote!

Status
Not open for further replies.
Mkuu Kitila,

Pole na uzushi huu ambao Brazamen anajua dhamira (motive) yake ilikuwa ni nini.

Mimi nilijiunga na JF kwa nia njema kabisa ya kushiriki na watanzania wenzangu popote pale walipo iwe ughaibuni au mahali pengine kubadilishana mawazo na kupeana taarifa mbalimbali na mambo mengine.

Pia wanachama wenzangu mkifuatilia sbabu za mimi kujiunga na mtandao huu niliwahi kuziweka huko nyuma katika posting zangu.

Siku hizi ukipita na kukutana na watu utakumbana na maneno eti ukifanya mambo ya kijinga au upuuzi basi utaanikwa JF, hii naona ni moja ya sifa ya uimara wa JF ambao ni- "we dare to talk openly".

Pia sasa kuna baadhi ya wanachama ambao wametumwa kuja hapa JF kuleta zogo mimi nawaambaia sasa muache na muwe makini.

Kwa mtazamo wangu ni kwamba JF imeanza kuwa sumu kwa baadhi ya watu ambao ni MAFISADI na sasa wanaogopa namna ambavyo wataanikwa hapa JF.

Cha msingi ni wale wana JF wote kuhakikisha kwamba tunasimama imara kwa hoja zenye nguvu na zenye vigezo na mantiki zisizo tetereka na kuwa tayari kuwaanika wale wote iwe MAFISADI AU WATOTO WAO na washirika wao kama ambavyo CCM na matawi yake London imejaa watu ambao viza zao zimeisha muda na wengine wamejilipua.

Mkuu Kitila endelea kushiriki JF bila woga na usibabaishwe na makelele ya walio na sera za kifisadi.

Idumu JF!
 
Hivi wanausalama wa Tanzania wana jurisdiction ya kumkamata mtu nje ya nchi? Nadhani tungeishuku hii stori toka mwanzoni.

Mimi niliuliza "Ya kweli haya?" kwa sababu kuna kitu kilionekana kuto add up.

Sikufikiri kwamba wanausalama wa Uingereza wangeweza kujishusha hivi, ajua wanausalama wa Tanzania hawana jurisdiction.

Fungia member aliyeleta uzushi huu.
 
Loh! angalau sasa ninaweza kupata kifungua kinywa changu. Ingawa stori yenyewe ilionekana kuwa odd lakini sikutaka kuipuuzia. Pole Kitila kwa usumbufu ulioletwa na Brazameni.
 
Wakuu,

Imebidi nitafute internet kukanusha taarifa ya kukamatwa kwangu. Bahati mbaya nimekuta ile thread husika imeshafungwa na imebidi nianzishe mpya.

Ni hivi, sijahojiwa, sijakamatwa wala kushikiliwa na mtu yeyote. Pamoja na matatizo mengi ya kiuongozi ya serikali yetu, siamini kwamba kuna mtu kule serikalini anaweza kuthubutu hata kufikiri kumkamata mtu kwa sababu ya kuuliza swali ambalo halipendi.

Sielewi nia hasa ya taarifa hii. Ama ni mwendelezo wa vitendo vya kujaribu kuichafua JF ili tuonekane sisi ni wazushi ili watu waache kuamini taarifa zetu za hapa hasa kuhusu ufisadi, au ni mwendelezo wa woga ambao umejikita miongoni mwa baadhi ya watanzania katika kuogopa vivuli vyetu (fear of unknown).

Kama ni kwa ajili ya woga, napenda kuwatia moyo watanzania popote walipo kuwa viongozi wetu wakiwatembelea popote mlipo msisite kuwauliza maswali magumu au yanayowakera kwa kuhofia kukamatwa. Kama unaogopa sana kukamatwa, hakikisha huvunji sheria za nchi yetu na nchi nyingine uliopo au utakayotembelea.

Poleni sana kwa wale waliopata usumbufu kwa taarifa hii.

Once again, I assure you that I am safe and well, and I am on my way home in Southampton.

Ni mimi mwanachama mwenzenu,

Kitila.

Kitila.
Nadhani ungeanza kwa kumshukuru Brazameni kuliko kukosa busara na kumshambulia na hasa Lunyungu anaejifanya kuwa kipenzi wako.

humu JF huwa kuna habari zinaletwa haraka haraka kulikuwa na habari ya Gavana Balali kuwa deported lakini baadae hazikuwa na ukweli,

magazeti yanaandika habari kutokana na uvumi, Brzazameni labda alisikia uvumi na ukapigiwa simu na Invisible haukupatikana,

alichokifanya ni mapenzi makubwa juu yako na kuwa concerned na wewe.kuliko kuanza kumtukana na kumuona ni CCM. kama mimi ni CCM ningemlaumu Brazameni kwa kukuza au kukupa umaarufu kwa habari hii.
naamini nia ya brazameni kuandika hapa ilijikita kwenye UJF zaidi kuliko chochote.

ningekuwa wewe ningemshukuru Brazameni kwa kuonesha moyo wa upendo wa kukufuatilia baada ya mkutano.

Lunyungu.

Hapa umekosea sana hakukuwa na suala la UCCM bali UJF, mtu kuwa concern na mwana JF mwenzake kuna ubaya gani?

na habari hii imezidisha kumpamba Kitila inaonesha jinsi gani wanaJF wenzake walivyo na mapenzi nae.

tuchukulie kuwa Brazameni ni Chadema kwangu mimi habari hii ni kuipakazia serikali ya CCM kuliko unavyodai wewe.

ANYWAY Chadema ina wenyewe na wenyewe ni nyinyi ila kwa hili la kumpazia Brazameni umechemsha ndugu yetu.
 
Duh.. kumbe nimemiss kitu hapa... pole mzee Kitila kwa usumbufu. Yote ni sehemu ya mapambano ya kifikra..
 
Kitila JF 2, Mama Balozi 0!

Sielewi nia hasa ya taarifa hii. Ama ni mwendelezo wa vitendo vya kujaribu kuichafua JF ili tuonekane sisi ni wazushi ili watu waache kuamini taarifa zetu za hapa hasa kuhusu ufisadi, au ni mwendelezo wa woga ambao umejikita miongoni mwa baadhi ya watanzania katika kuogopa vivuli vyetu (fear of unknown).

Mkuu Kitila Bravo & Salute,

1. Kwa kusimama kidete na kuhesabiwa, kwa kuwauliza the right questions viongozi wetu magoi goi ambao wangependa na sii wananchi wote tuwe magoi goi wa kufikiri kama wao, kwa hilo ninakupoa Salute!

2. Now this guy aliyeleta hizo habari, ninafahamu as a fact kuwa ana jina lingine maarufu sana hapa JF, alipopata hizo habari kama anavyotetewa na mkuu wangu Kifimbo, basi angejaribu kuwa-pm watu hapa ili kuzihakiki,

Kina Invisible, walipokamatwa that is exactly how it was done, kulikuwa na mawasiliano mazito behind the scene kati ya wanachama hapa, by the time Mkulu MMJ anaposti wazi hapa, ilikuwa ni hours later baada ya mikakati mingi ambayo tayari ilikuwa imeshapangwa, kwa sababu ni lazima wakuu muelewe kuwa huwa walikukamata hawana uhakika kama ni wewe kweli, kwa hiyo filimbi za mapema hapa zinaweza kuwaamsha kuwa kweli ni wewe hasa, kwa sababu kwenye ishu ya kina Invisible, kuna chumba cha pili ambako kulikuwa na wanaoifuatilia JF kwenye internent,

Sasa my point ni kwamba next time lazima tuwe waangalifu sana na haya mambo, maana kama kweli Kitila angekuwa ameshikwa, na waliomshika hawana uhakika basi kukimbilia hapa na kuweka tu kungeweza kuwapa ukweli kuwa ni yeye Kitila waliyenaye,

Anyways nafikiri huyu mkuu Brazameni, huwa simuelewi vizuri, lakini ninaamini ni a good man na sometimes anapitiwa tu na mambo, kwa sababu nilipoleta ujumeb mzito wa serikali, alitoa majibu ya kejeli sana, lakini baadaye akaanza kunitafuta kwa pembeni kuomba msamaha, ndio maana ninasema kuwa sometimes anapitiwa na wa kumsamehe.

Otherwise, Mkuu Kitila, ngoja nitafute mwananchi yoyote aliyekaribu na huko ulipo, ili angalau akupatie ki-pack cha beer kwa gharama yangu mkuu, maana uliyoyafanya jana nimeyasikia kutoka kwenye "the Horse's Mouth" Duh yaaani ni long live JF!
 
Kitila.
Nadhani ungeanza kwa kumshukuru Brazameni kuliko kukosa busara na kumshambulia na hasa Lunyungu anaejifanya kuwa kipenzi wako.

humu JF huwa kuna habari zinaletwa haraka haraka kulikuwa na habari ya Gavana Balali kuwa deported lakini baadae hazikuwa na ukweli,

magazeti yanaandika habari kutokana na uvumi, Brzazameni labda alisikia uvumi na ukapigiwa simu na Invisible haukupatikana,

alichokifanya ni mapenzi makubwa juu yako na kuwa concerned na wewe.kuliko kuanza kumtukana na kumuona ni CCM. kama mimi ni CCM ningemlaumu Brazameni kwa kukuza au kukupa umaarufu kwa habari hii.
naamini nia ya brazameni kuandika hapa ilijikita kwenye UJF zaidi kuliko chochote.

ningekuwa wewe ningemshukuru Brazameni kwa kuonesha moyo wa upendo wa kukufuatilia baada ya mkutano.

Lunyungu.

Hapa umekosea sana hakukuwa na suala la UCCM bali UJF, mtu kuwa concern na mwana JF mwenzake kuna ubaya gani?

na habari hii imezidisha kumpamba Kitila inaonesha jinsi gani wanaJF wenzake walivyo na mapenzi nae.

tuchukulie kuwa Brazameni ni Chadema kwangu mimi habari hii ni kuipakazia serikali ya CCM kuliko unavyodai wewe.

ANYWAY Chadema ina wenyewe na wenyewe ni nyinyi ila kwa hili la kumpazia Brazameni umechemsha ndugu yetu.

Kifimbo futa usemi wako juu ya mimi kujifanya kipenzi .Siwezi kujifanya kama najuana na mtu ama nina access naye .Soma maelezo ya Mzee atakueleza namna ya kupeleka habari tata bna nzito kama hizi.Ok now where is he kusema lolote hadi sasa ?JF haiwezi kutumika kama Chaka ili ishuke credibility kama Makamba no .Hapa ni mahapa pasafi na uvumi unakuwepo lakini mleta uvumi anaweka sawa uvumi.Mara ngapi nimeleta hapa uvumi na kuuweka wazi ? OK sasa Kitila is here huyu Brazamen yuko wapi kusema lolote .CCM inawatuma watu hapa lakini inawatuma wasio wajanja na ndiyo wanazidi kuichafua .Wanakuja na hoja tupu a vibweka leo unasema Lunyungu nini ? Weeeeeeeeeeeeeee koma kabisa bwana mdogo .Mimi sibahatishi news nikisema huwa nina info za ndani na kama huna basi uliza kama alivyo shauri ES.Hakuna kuangaliana usoni na ku concern za kipumbavu namna hii nadiriki kusema ni ujinga mkubwa bora uache .Hili ni dua la kuku na some sort a scare kwa mtu mzima .Nakula nawe sasa kwa busara na uhuni .Nimefungua ukurasa njoo jibu nije tena .
 
Kitila tuko pamoja ndugu yetu, hatupendi mabaya yatufike, ni kweli tulikwishaanza kuamini hiyo thread ya brazamen. tunashukuru hata kwa kukanusha kwako, bigup
 
Kifimbo futa usemi wako juu ya mimi kujifanya kipenzi .Siwezi kujifanya kama najuana na mtu ama nina access naye .Soma maelezo ya Mzee atakueleza namna ya kupeleka habari tata bna nzito kama hizi.Ok now where is he kusema lolote hadi sasa ?JF haiwezi kutumika kama Chaka ili ishuke credibility kama Makamba no .Hapa ni mahapa pasafi na uvumi unakuwepo lakini mleta uvumi anaweka sawa uvumi.Mara ngapi nimeleta hapa uvumi na kuuweka wazi ? OK sasa Kitila is here huyu Brazamen yuko wapi kusema lolote .CCM inawatuma watu hapa lakini inawatuma wasio wajanja na ndiyo wanazidi kuichafua .Wanakuja na hoja tupu a vibweka leo unasema Lunyungu nini ? Weeeeeeeeeeeeeee koma kabisa bwana mdogo .Mimi sibahatishi news nikisema huwa nina info za ndani na kama huna basi uliza kama alivyo shauri ES.Hakuna kuangaliana usoni na ku concern za kipumbavu namna hii nadiriki kusema ni ujinga mkubwa bora uache .Hili ni dua la kuku na some sort a scare kwa mtu mzima .Nakula nawe sasa kwa busara na uhuni .Nimefungua ukurasa njoo jibu nije tena .

Kwani wewe ni nani hadi nifute usemi? kwangu mimi Kitila na Brazameni nawapa uzito mmoja ni wachangiaji wazuri JF siwezi kuwagombanisha wala kuwabagua.

Lunyungu kama una information za ndani mbona hukutupa habari za Chenge hadi the Guardian (UK)likatuletea?
Mie nakuona **** tu.
 
Kitila JF 2, Mama Balozi 0!

Mkuu Kitila Bravo & Salute,

1. Kwa kusimama kidete na kuhesabiwa, kwa kuwauliza the right questions viongozi wetu magoi goi ambao wangependa na sii wananchi wote tuwe magoi goi wa kufikiri kama wao, kwa hilo ninakupoa Salute!

2. Now this guy aliyeleta hizo habari, ninafahamu as a fact kuwa ana jina lingine maarufu sana hapa JF, alipopata hizo habari kama anavyotetewa na mkuu wangu Kifimbo, basi angejaribu kuwa-pm watu hapa ili kuzihakiki,

Kina Invisible, walipokamatwa that is exactly how it was done, kulikuwa na mawasiliano mazito behind the scene kati ya wanachama hapa, by the time Mkulu MMJ anaposti wazi hapa, ilikuwa ni hours later baada ya mikakati mingi ambayo tayari ilikuwa imeshapangwa, kwa sababu ni lazima wakuu muelewe kuwa huwa walikukamata hawana uhakika kama ni wewe kweli, kwa hiyo filimbi za mapema hapa zinaweza kuwaamsha kuwa kweli ni wewe hasa, kwa sababu kwenye ishu ya kina Invisible, kuna chumba cha pili ambako kulikuwa na wanaoifuatilia JF kwenye internent,

Sasa my point ni kwamba next time lazima tuwe waangalifu sana na haya mambo, maana kama kweli Kitila angekuwa ameshikwa, na waliomshika hawana uhakika basi kukimbilia hapa na kuweka tu kungeweza kuwapa ukweli kuwa ni yeye Kitila waliyenaye,

Anyways nafikiri huyu mkuu Brazameni, huwa simuelewi vizuri, lakini ninaamini ni a good man na sometimes anapitiwa tu na mambo, kwa sababu nilipoleta ujumeb mzito wa serikali, alitoa majibu ya kejeli sana, lakini baadaye akaanza kunitafuta kwa pembeni kuomba msamaha, ndio maana ninasema kuwa sometimes anapitiwa na wa kumsamehe.

Otherwise, Mkuu Kitila, ngoja nitafute mwananchi yoyote aliyekaribu na huko ulipo, ili angalau akupatie ki-pack cha beer kwa gharama yangu mkuu, maana uliyoyafanya jana nimeyasikia kutoka kwenye "the Horse's Mouth" Duh yaaani ni long live JF!

Mkuu ES.

Kitila ni mtu maarufu sana anajulikana sana,sababu hatumii pen name na alikuwa rais wa Daruso hivyo hakuna haja ya kuhakikisha kama ni yeye. naona Brazamen anaonewa bure na Lunyungu na kulikuza jambo lisilo na msingi.
 
Kifimbo udaku hauna nafasi na uetetezi wa kijinga .Unataka habari nyeti ziwe ni za chenge tu ? Wewe naona una matongo tongo bado katika hii forum.Acheni uhuni hapa forum na tukate issue uzushi na spinning huko huko si hapa .Msome vyema ES narudia msome vyema ES na taratibu za kuleta habari ambazo hazina uhakika .
 
Mkuu Kitila pole sana, sikupata nafasi ya kuusoma huo uvumi. Na Brazameni aliyeuanzisha ajitokeze kueleza alikoipata ili tuweze kutoa hukumu ya haki. Sidhani kama mtu mwenye akili timamu anaweza tu kuzua jambo ambalo anajua punde tu ukweli utadhihirika na kumuumbua, inawezekana hata yeye labda aliamini ni ya kweli. Atueleze ilikuwaje, itatusaidia feedback kwa siku na matukio yajayo.
 
Kifimbo udaku hauna nafasi na uetetezi wa kijinga .Unataka habari nyeti ziwe ni za chenge tu ? Wewe naona una matongo tongo bado katika hii forum.Acheni uhuni hapa forum na tukate issue uzushi na spinning huko huko si hapa .Msome vyema ES narudia msome vyema ES na taratibu za kuleta habari ambazo hazina uhakika .

Matongo tongo unayo wewe ambaye hujui kuwa wabunge wa kuteuliwa wa Chadema wote wana toka Kilimanjaro. kamjibu Kubwajinga kule kwenye udikteta Chadema.
 
Kifimbo na Lunyungu acheni basi hizo. Turudi kwenye hoja tuache kushambulia personalities. OK?
 
Glad to know that you're okay and thanks for raising EPA issue during that meeting.
 
Mzee kifimbo

Acha matusi, jibu hoja kwa hoja bila matusi.
 
maelezo ya wengi nimeyasoma na mzee ES kamaliza kila kitu.

tusubiri Brotherman aje hapa atueleze kilichomsibu hadi akatuletea kanya boya au kama aliamua kutuchezea akili au kama alivyoainisha mtu mzima mwenzangu aje aombe radhi jamvi na mkuu kitila kwa usumbufu aliosababisha

mzee ole heshima mbele jitahidi kuwa mlezi wa jamvi letu kwa uadilifu, hivi kumwambia mtu matongo tongo si lugha ya matusi? mbona hujazungumzia hili na kumkamata mmoja tu?
 
Umeshamfungia huna haja ya kuandika hili tena kwani hawezi kujitetea,lakini bi senti 50 kasema mambo ya ngono umemuacha huo ndio uonezi wa JF?

kifimbo umemfungia miezi mingapi? kwa kosa lipi?
 
Glad to know that you're okay and thanks for raising EPA issue during that meeting.

Haikuwa mahala pake tena nasikia alifanya hivyo baada ya gavana na viongozi wote kuondoka. Michuzi blog kasema wakati dr.Shein anaongea Wazimbabwe wakapandisha sauti zao.nae angefikisha ujumbe wakati huo.

kwangu mimi Kitila Mkumbo (Asha Abdala) ni mnafiki tu.
 
maelezo ya wengi nimeyasoma na mzee ES kamaliza kila kitu.

tusubiri Brotherman aje hapa atueleze kilichomsibu hadi akatuletea kanya boya au kama aliamua kutuchezea akili au kama alivyoainisha mtu mzima mwenzangu aje aombe radhi jamvi na mkuu kitila kwa usumbufu aliosababisha

mzee ole heshima mbele jitahidi kuwa mlezi wa jamvi letu kwa uadilifu, hivi kumwambia mtu matongo tongo si lugha ya matusi? mbona hujazungumzia hili na kumkamata mmoja tu?

Umeshamfungia huna haja ya kuandika hili tena kwani hawezi kujitetea,lakini bi senti 50 kasema mambo ya ngono umemuacha huo ndio uonezi wa JF?

kifimbo umemfungia miezi mingapi? kwa kosa lipi?

Uamuzi huo ulifuatia aliyoandika hapa (pamoja na posts nyingine zilizofutwa) utaona kuna stars kwenye maandishi yake: http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=12264&page=16
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom