Kitila Mkumbo
JF-Expert Member
- Feb 25, 2006
- 3,352
- 1,935
Wakuu,
Imebidi nitafute internet kukanusha taarifa ya kukamatwa kwangu. Bahati mbaya nimekuta ile thread husika imeshafungwa na imebidi nianzishe mpya.
Ni hivi, sijahojiwa, sijakamatwa wala kushikiliwa na mtu yeyote. Pamoja na matatizo mengi ya kiuongozi ya serikali yetu, siamini kwamba kuna mtu kule serikalini anaweza kuthubutu hata kufikiri kumkamata mtu kwa sababu ya kuuliza swali ambalo halipendi.
Sielewi nia hasa ya taarifa hii. Ama ni mwendelezo wa vitendo vya kujaribu kuichafua JF ili tuonekane sisi ni wazushi ili watu waache kuamini taarifa zetu za hapa hasa kuhusu ufisadi, au ni mwendelezo wa woga ambao umejikita miongoni mwa baadhi ya watanzania katika kuogopa vivuli vyetu (fear of unknown).
Kama ni kwa ajili ya woga, napenda kuwatia moyo watanzania popote walipo kuwa viongozi wetu wakiwatembelea popote mlipo msisite kuwauliza maswali magumu au yanayowakera kwa kuhofia kukamatwa. Kama unaogopa sana kukamatwa, hakikisha huvunji sheria za nchi yetu na nchi nyingine uliopo au utakayotembelea.
Poleni sana kwa wale waliopata usumbufu kwa taarifa hii.
Once again, I assure you that I am safe and well, and I am on my way home in Southampton.
Ni mimi mwanachama mwenzenu,
Kitila.