Dini zinamtenganisha mtu na utambulisho wake wa uungu matokeo yake ni nusu mtu

Lord genesis

Member
Jan 3, 2024
25
47
According to sauti ninayopigaga nayo story kichwani, Mtu yani mimi na wewe tunakamilishwa na sehemu kuu mbili sehemu, sehemu ya kwanza ni UZIMA (UMUNGU/KUSUDI) na sehemu ya pili ni UHAI (BINADAMU).

Yaani ili kupata mtu kamili inatakiwa uhai wa mtu upokee uzima wa mtu kwa asilimia mia moja. kifupi uzima hauna haja ya kupokea uhai kwasababu uzima ni ukamilifu wa mtu hata bila uhai, ila uhai wa mtu si kamili bila uzima ambao ndio unabeba kusudi, utambulisho vipawa na vipaji .

Nitaanza na uzima kisha nitaendelea na uhai kisha nitafundisha jinsi ya kutengeneza daraja la kuuvusha uzima kuja kwenye uhai ili tupate mtu mkamilifu.

UZIMA/ UMUNGU ni msingi wa uwepo wa mtu ama kitu chochote unachokiona katika physical realm na yale tusiyoyaona. Uzima umegawanyika katika sehemu kuu mbili. Sehemu ya kwanza ambayo ndio chanzo cha uwepo wa mtu na vyote vilivyopo nitaita sehemu hii ROHO.

ROHO ni NGUVU ya kwanza ambayo uwepo wake unatambua kikamilifu kuhusu uwepo wake.. (inatambua kwanini iko na yenyewe ni nini katika nini) na hubaki katika utambuzi wa uwepo wake kikamilifu toka milele iliyopita na milele ijayo (NOW)

Uwezo wa kutambua yakuwa iko huipa sifa nguvu hii nakuifanya kuwa nguvu pekee yenye wazo thabiti... wazo la nguvu hii ni thabiti kwasababu wazo lake linafit kusudi la uwepo wake kikamilifu nguvu hii ndiyo ile inayojitambulisha kama NIKO AMBAE NIKO kwenye bible.

Hiki ni kiwango ambacho kimebeba nguvu ya uwepo wa kila kitu pamoja na mtu. kuwepo kokote kule kumetokea hapa kwenye nguvu inayojua ya kuwa ipo. kwahiyo kama tunaelezea historia ya mtu basi hapa ndipo uwepo wake ulipoanzia kwenye utambuzi wa kwanza wa uwepo. I AM THAT I AM.

na kiwango cha pili ni NENO. sehemu hii inazaliwa ndani ya wazo thabiti. wazo ambalo linalotambua kikamilifu uwepo wa uwepo wake, kwa jinsi wazo ama nguvu inapojaa kikamilifu katika kuutambulisha uwepo wake ndipo kiwango hiki huzaliwa kama wazo la uumbaji(NENO).

sehemu hii ni NENO(UTU/KRISTO). ni neno kwa sababu kwa jinsi ROHO(BABA, UUNGU) ilivyo ji-identify kikamilifu ama kujiita sawasawa na inavyojitambua(neno) ndipo mimi na wewe tulipotokea na ndipo simba alipotokea ndipo milima na miti ilipotokea.

Wazo lililojispecialized kuwa wewe kuwa wewe lilitokea hapa kwenye kiwango cha NENO(UTU) ila uwepo wako ulitokea kwenye kiwango cha kwanza ROHO(UUNGU) . Hapa ndipo kusudi la kila mmoja lilitokea kama shauku ya nguvu ya kwanza ya uwepo ROHO kujitambulisha ama kujiita katika vipawa, vipaji, ubunifu na yote yanayotofautisha mtu na mtu.

I AM SINGER. I AM WHAT WHAT WHAT

kwa ufupi sana huo ndio UZIMA itaendelea sehemu ya pili ambapo nitaelezea UHAI. NA TUTAONA JINSI MTU ANAVYOTEKWA NA KUJITAMBULISHA SAWASAWA NA UHAI/MAPITO YAKE na kusahau kuwa uhai wetu umeitwa ili kuuthibutisha uzima wetu katika ulimwengu wa kuonekana.

GONGA LIKE ILI NIJUE WATU AMBAO WAKO INTERESTED.
 
Wewe ni mswahili, hakuna kitu hapo umeandika, sema mawazo yako sio sheria so tunahitaji kujifunza zaidi,

Kwa faida yako na wengine watakaosoma hii , nikwamba roho ni maana ya kitu, yaani kila kitu ukionapo kina roho, ndio maana hata meza kabla yakuwa meza ilikuwa mbao, na mtu kabla ya kuwa marehemu alikuwa mwanadamu, kila kitu kina roho.
 
Maneno si maana na maana si neno waweza kulitumia vyovyote kwa maana iliyomo kichwani mwako. Mfano. "Moyo wangu umefurahi" kwa maana ya moja kwa moja moyo ni kiungo tu kilichopo mwilini hakina hisia yoyote ya kufurahi.

Umeelewa nadhani
 
Ni sawa tu, lakini huu mkanganyiko ndo ulisababisha ule msemo wa ukweli unauma/ukweli mchungu, na hata kama unayo maana ya neno flani na unaona kabisa unajilazimisha kukubali na huo ukweli amba wewe unaona ni ukweli ikiwa ukweli mwingine hauutaki zaidi ya huo basi wewe haijalishi unajisikia furaha kiasi gani kama sio sahihi sio sahihi tu hili halipingwi
 
Napenda sana kujifunza hii sio vita napenda kuelekezwa sana tu ila saaa maana na neno ni vitu tofauti kabisa mm kuna maana nailenga kwa kutumia neno ROHO.
 
Ni sawa tu, lakini huu mkanganyiko ndo ulisababisha ule msemo wa ukweli unauma/ukweli mchungu, na hata kama unayo maana ya neno flani na unaona kabisa unajilazimisha kukubali na huo ukweli amba wewe unaona ni ukweli ikiwa ukweli mwingine hauutaki zaidi ya huo basi wewe haijalishi unajisikia furaha kiasi gani kama sio sahihi sio sahihi tu hili halipingwi
Usahihi ni mtazamo wa mtu waweza kuona si sahihi kwengine likawa sahihi. Usahihi is not universal perceived
 
Wewe ni mswahili, hakuna kitu hapo umeandika, sema mawazo yako sio sheria so tunahitaji kujifunza zaidi,

Kwa faida yako na wengine watakaosoma hii , nikwamba roho ni maana ya kitu, yaani kila kitu ukionapo kina roho, ndio maana hata meza kabla yakuwa meza ilikuwa mbao, na mtu kabla ya kuwa marehemu alikuwa mwanadamu, kila kitu kina roho.
Na hata mbao ilikuwa mti
 
Back
Top Bottom