Shaka : Baada ya kifo cha Hayati Dkt Magufuli,wale wote Waliombeza Rais Samia Ujenzi wa miradi ya kimkakati leo wanaumbuka, Wami ilikuwa 47% leo 89.2%

CM 1774858

JF-Expert Member
May 29, 2021
4,986
4,084
SHAKA ;RAIS SAMIA AMEWAUMBUA WALIOBEZA MIRADI YA KIMKAKATI.

Ataja kukamilika kabla ya wakati ujenzi wa daraja la Wami ni kielelezo cha uwezo wa serikali ya awamu ya sita

Na Mwandishi Wetu,Pwani

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka amesema Chama hicho kinaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati inavyoendelea kutekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.
IMG-20220918-WA0218.jpg

Amesema hata baadhi ya watu waliokuwa wakibeza na kutoa kauli za kejeli kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo sasa wameumbuka.
IMG-20220918-WA0233.jpg

Shaka ameyasema hayo leo Septemba 18, 2022 baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja jipya la Wami ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 89.02 na zaidi ya Sh. bilioni 75 zimepangwa kutumika.
IMG-20220918-WA0222.jpg

Aidha amesema jambo la kufurahisha ni kwamba ujenzi wa daraja hilo unakwenda kuandika historia ya kuwa miongoni mwa miradi michache nchini iliyokamilika kabla ya muda uliopangwa.
IMG-20220918-WA0195.jpg

"Wakati Rais Samia Suluhu Hassan anaingia madarakani kulikuwa na maneno mengi sana kuhusu daraja hili la Wami na si hili tu bali maneno yalikuwa mengi Rais Samia hataendeleza mirad hii ya kimkakati,
IMG-20220918-WA0238.jpg

Wiki mbili zilizopita tulikuwa Mwanza, tumeona ujenzi wa daraja la Kigongo - Busisi unavyokwenda kwa kasi kuliko tunavyofikiria. Tumeona ujenzi wa meli MV. Mwanza unavyokwenda kwa kasi kuliko tunavyofikiria na leo niko hapa daraja la Wami nashuhudia kwa macho yangu, mikono yangu lakini ukisimama hapa ukiangalia kule mbele unaona namna gani ambavyo Pwani na Tanga inavyong'ara kupitia daraja hili,” amesema.
IMG-20220918-WA0240.jpg

Aliongeza kuwa, fedha zote zimetoka kwa wakati na hivyo ukichukua asilimia 47 na asilimia 42.2 unapata asilimia 89.2 kati ya hizo kazi kubwa imefanyika katika kipindi cha mwaka mmoja na miezi kadhaa ya Rais Samia Suluhu Hassan huku akieleza kwamba hapo ndipo unaona namna gani ambavyo Watanzania wananufaika na kodi zao kwa sababu fedha iliyotoka kwenye daraja hilo ni ya ndani.
IMG-20220918-WA0216.jpg

"Hakuna fedha ya mjomba hakuna fedha ya msaada ni fedha ya watoka jasho wa Tanzania ndio imefanya kazi hii na mtaalamu alikuwa ananiambia katika historia ya nchi yetu na mimi nimefuatilia iko hivyo, hili litakuwa daraja la kwanza kukamilika kabla ya wakati uliokadiriwa, daraja hili lilikadiriwa litumie miaka minne lakini tutalifungua kabla ya Novemba ambao tungetegemea kwamba ndio mwezi wa mwisho,” amesema.

=== ===
 
Binti Suluhu anastahili pongezi,Mataga walishasema kuwa Demu hawezi,lakini hata sisi CHADEMA tungejenga zaidi ya hapo kama Magufuli asingetupora Uchaguzi wetu.
 
Ataja kukamilika kabla ya wakati ujenzi wa daraja la Wami ni kielelezo cha uwezo wa serikali ya awamu ya sita

Na Mwandishi Wetu,Pwani

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka amesema Chama hicho kinaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati inavyoendelea kutekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema hata baadhi ya watu waliokuwa wakibeza na kutoa kauli za kejeli kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo sasa wameumbuka.

Shaka ameyasema hayo leo Septemba 18, 2022 baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja jipya la Wami ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 89.02 na zaidi ya Sh. bilioni 75 zimepangwa kutumika.

Aidha amesema jambo la kufurahisha ni kwamba ujenzi wa daraja hilo unakwenda kuandika historia ya kuwa miongoni mwa miradi michache nchini iliyokamilika kabla ya muda uliopangwa.

"Wakati Rais Samia Suluhu Hassan anaingia madarakani kulikuwa na maneno mengi sana kuhusu daraja hili la Wami na si hili tu bali maneno yalikuwa mengi Rais Samia hataendeleza mirad hii ya kimkakati, wiki mbili zilizopita tulikuwa Mwanza, tumeona ujenzi wa daraja la Kigongo - Busisi unavyokwenda kwa kasi kuliko tunavyofikiria. Tumeona ujenzi wa meli MV. Mwanza unavyokwenda kwa kasi kuliko tunavyofikiria na leo niko hapa daraja la Wami nashuhudia kwa macho yangu, mikono yangu lakini ukisimama hapa ukiangalia kule mbele unaona namna gani ambavyo Pwani na Tanga inavyong'ara kupitia daraja hili,” amesema.

Aliongeza kuwa, fedha zote zimetoka kwa wakati na hivyo ukichukua asilimia 47 na asilimia 42.2 unapata asilimia 89.2 kati ya hizo kazi kubwa imefanyika katika kipindi cha mwaka mmoja na miezi kadhaa ya Rais Samia Suluhu Hassan huku akieleza kwamba hapo ndipo unaona namna gani ambavyo Watanzania wananufaika na kodi zao kwa sababu fedha iliyotoka kwenye daraja hilo ni ya ndani.

"Hakuna fedha ya mjomba hakuna fedha ya msaada ni fedha ya watoka jasho wa Tanzania ndio imefanya kazi hii na mtaalamu alikuwa ananiambia katika historia ya nchi yetu na mimi nimefuatilia iko hivyo, hili litakuwa daraja la kwanza kukamilika kabla ya wakati uliokadiriwa, daraja hili lilikadiriwa litumie miaka minne lakini tutalifungua kabla ya Novemba ambao tungetegemea kwamba ndio mwezi wa mwisho,” amesema.
IMG-20220918-WA0005.jpg
IMG-20220918-WA0013.jpg
IMG-20220918-WA0009.jpg
IMG-20220918-WA0010.jpg
IMG-20220918-WA0011.jpg
IMG-20220918-WA0007.jpg
IMG-20220918-WA0017.jpg
IMG-20220918-WA0027.jpg
IMG-20220918-WA0018.jpg
IMG-20220918-WA0026.jpg
IMG-20220918-WA0029.jpg
IMG-20220918-WA0016.jpg
IMG-20220918-WA0006.jpg
IMG-20220918-WA0022.jpg
IMG-20220918-WA0014.jpg
IMG-20220918-WA0012.jpg
 
Kweli kuna hela za mchezo!
Magari yote hayo kumsindikiza Shaka!!
Tutatoana macho kwenye tozo.
 
Maendeleo yanapaswa kuwa "attributed" na serikali na wala siyo mtu fulani. Hizo fedha za miradi zinatokana na kodi za Watanzania, ama mikopo ambayo watawajibika kuilipia madeni yake. Kwa hiyo inatosha tu kusema serikali inakaribia kumaliza ujenzi wa daraja hili.

Hiyo minguo ya rangi za kijani na njano sijui hata zinatafuta nini hapo, na huyo mwenezi pia sijui anajipekeka hapo na sifa zake kufanya nini?

Kenge mjusi
 
Back
Top Bottom