Mbunge Cherehani: Tumuombee Rais Samia akamilishe Miradi ya Maendeleo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
942
GDUOOVMXcAAoSfG.jpg

Watanzania wamehamasishwa kuendelea kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan ili aweze kutekeleza na kukamilisha miradi ya maendeleo anayotekeleza.

Rai hiyo imetolewa leo Januari 7 na Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Dk. Emmanuel Cherehani alipoongoza harambee kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa Kanisa la Mtakatifu Theresia, Parokia ya Chona Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga.

GDUOOZSWwAAHvy_.jpg

Mhe. Cherehani amesema kuwa Mhe. Rais Dk. Samia amekuwa akitekeleza miradi mingi ya maendeleo nchini na katika Jimbo la Ushetu pia, huku akibainisha baadhi ya miradi hiyo ni kama ujenzi wa barabara, vituo vya afya, shule na madaraja ambapo miradi hiyo imelenga kuboresha maisha ya wananchi.

"Mhe. Rais Dk. Samia anafanya kazi kubwa sana usiku na mchana kuhakikisha tunapata maendeleo. Sisi kama wananchi jukumu letu ni kumuunga mkono pamoja na kumuombea miradi hiyo ikamilike kwa ajili ya maendeleo yetu," amekaririwa Mhe. Cherehani.

Amesema kuwa Rais Samia ametoa kiasi cha Shilingi Bilioni 4 kwa ajili ya ukarabati wa barabara na ujenzi wa madaraja katika Wilaya ya Ushetu.

Kadhalika, Dk. Cherehani amesema kuwa Rais Samia ametoa Bilioni 1.8 kwa ajili ya vifaa vya kisasa katika Zahanati na Hospitali ya Wilaya kwa ajili ya kuwahudumia wananchi bila kuwabagua.

Pia Dk. Cherehani amesisitiza umuhimu wa wazazi na walezi kuhakikisha kuwa wanatenga muda wa kuzungumza na watoto wao ili kuimarisha malezi bora kwao na kulelewa katika maadili mema yanayompendeza Mungu.

GDUONFvXMAAX18n.jpg

Kwa upande wake Mkurugenzi wa WAZOHURU MEDIA GROUP LIMITED ya Jijini Dodoma Ndg. Mathias Canal amesihi wananchi wa Jimbo hilo kuendelea kumuombea na kumuunga mkono Mbunge wao kwani wana kiongozi mwenye ari ya maendeleo, Mpenda watu na mchapakazi.

Naye Bi Neema Mgheni ambaye ni Mkurugenzi wa Gold Fm mjini Kahama amewasihi wananchi kuendelea kuunga mkono juhudu za serikali katika kuwaletea maendeleo huku akisisitiza umuhimu wa waumini kusikiliza na kufanyia kazi maelekezo ya viongozi wa dini katika kukmarisha maadili ya jamii.
 
Attachments

  • GDUONFtWQAAwZTJ.jpg
    GDUONFtWQAAwZTJ.jpg
    277 KB · Views: 2
  • GDUONFvXoAA7ojl.jpg
    GDUONFvXoAA7ojl.jpg
    183.6 KB · Views: 2

Hatujali ni mapadiri/masheikh au wachungaji. Huyu Samia ni Rais asiyefaa kwa lolote. Ni mchumaji kwa ajili ya ndugu zake na wajomba zake tu!
Nilikasirika sana nilipoona eti amenunua milima ili ya uluguru ambayo wachimbaji wadogo walikuwa wanafaidi muda mrefu. Nilikasirika zaidi kujua kuwa anashirikiana na wale wajomba aliowamilikisha bandari zetu zote na sasa yuko mbioni kuwamilikisha mbuga zetu zote.
Anashirikiana na maharamia wa ghuba na sasa anataka madini ya mbugani yachimbwe!!
Huyu Huyu Huyu!!!!?? Hana nia njema na taifa wala wananchi wa nchi hii!!

Kuweni macho hata kiini macho cha R4 alichokopi kwa Raila hatatekeleza na nia yake ni kuhadaa Ulimwengu na wafadhili.
Amini usiamini uchaguzi ujao utaporwa kwa kushirikiana na wajomba ya ghuba!
Povu kwa wale watumwa wa milele yanaruhusiwa!
 
Sio kila anayeombewa anampango wa kuombewa.
Wengine hawataki.
Je, yeye ameridhia kuombewa?
Na akiombewa atakamilisha? Usicheze na maombi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom