Serikali yatolea ufafanuzi taarifa ya nafasi ya masomo ya kidato cha 5 ya mwanafunzi Sifika Ruben kupewa mtu mwingine

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Serikali kupitia Ofisi ya Rais -TAMISEMI jana tar 25/9/2023 imetoa ufafanuzi wa taarifa zilizokuwa zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuhusisha mwanafunzi Sifika Daniel Ruben aliyesoma Shule ya Sekondari ya Mkombozi Wilayani Same, Kilimanjaro kupangwa Shule ya Sekondary Namwai kwa masomo ya kidato cha tano na nafasi hiyo kupewa mtu mwingine na hivyo kumukosesha Sifika haki ya kuendelea na masomo.

Ambapo imebainika kuwa binti aliyekuwa analalamika (Sifaeli Tawel Elirehema) alidanganya taarifa zake na kuchukua jina la mwanafunzi halisi Sifika anaendelea na masomo yake hivi sasa katika Shule ya Sekondari Namwai.

Pia soma
- Shule ya Sekondari Mkombozi: Sifika Danieli Rubeni alidanganya taarifa ya kuuzwa kwa nafasi yake ya kidato cha tano

Tamisemi.jpg
 
Ni mjinga tu ndo angekubalina na upuuzi huu, eti wameuza jina,kwa dunia hii kweli,huyo mnunuzi anakuwa amelipa shilingi ngapi kwa mamlaka!?
 
Dogo Sifael ni muongo pro max...

Ana kipaji, apewe nafasi pale eagle wing
Wewe ndiye umewaza kisawasawa, huyu anahitajika kufanyiwa uchambuzi wa kina...pale eagle pangeweza kumfaa zaidi, make ni zaidi ya Kibwetere na pasta Michael wa kule Kenya.
 
Wewe ndiye umewaza kisawasawa, huyu anahitajika kufanyiwa uchambuzi wa kina...pale eagle pangeweza kumfaa zaidi, make ni zaidi ya Kibwetere na pasta Michael wa kule Kenya.
Ana kipaji kikubwa sana

Maana kuwadanganya watu wazima, mpaka wakamnunulia vifaa vya kwenda shule, kufika kule akawapa jambajamba walimu mpaka wakachanganyikiwa sio mchezo..

Hajaishia hapo tuu, amehakikisha mpaka imeenda viral nchi nzima, mpaka wizara husika zimetoa matamko
 
Nimekumbuka chanzo cha wanafunzi kuweka picha kwenye fomu ya kumaliza darasa la saba nafikiri kwenye miaka ya 90s...Aliepewa Jina la kufanyia mtihani darasa la saba akafauli kwenda kidato cha kwanza ila mwenye Jina aliama shule na hakufaulu mtihani wa darasa la saba kwenda kidato cha kwanza.
Wazazi wa mwenye Jina kusikia hivyo, then wakamwambia kijana wao aende akaripoti shule...ngoma ilikuwa ngumu sana.
 
Back
Top Bottom