TAMISEMI imemwajiri Babu Lembrice Peter kwa kutumia namba ya kidato cha nne ya mtu mwingine

Alwatan kamba

Member
Nov 16, 2020
70
236
Ukistaajabu ya Abdallah Shonde utayaona ya "Babu Lembrice Peter" mwalimu mtarajiwa shule ya msingi Maliwa.

Tukiwa tunaendelea kubaini madudu na ukiritimba uliofanywa na TAMISEMI kwenye ajira mpya za walimu, nimebaini kuna mtu ameajiriwa kwa kutumia index namba ya kidato cha nne ya mtu mwingine.

Huyu mtu si mwingine bali ni BABU LEMBRICE PETER mwenye nambari ya kidato cha nne (S. 1802-0102/2010) ametumia namba ya kidato cha nne ya EMMANUEL MANEMBE MABHU( S. 1802-0102/2010).

Katika uchunguzi wangu nimebaini kuwa EMMANUEL MANEMBE MABHU aliyewahi kuwa mwanafunzi wa shule ya sekondari BWERI ndiye mmiliki halali mwenye index number ( S.1802-0102/2010). Hii ni kwa mujibu wa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne CSEE 2010. Pia unaweza kujiridhisha kwa kuangalia matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2010.

Katika matokeo yake EMMANUEL MANEMBE MABHU hakubahatika kuendelea na elimu ya kidato cha tano kutokana na matokeo yake kuwa hafifu kama ifuatavyo;

CIV-F, HIST-F, GEOG- F, KISW-F, ENG-F, BIO- F, MATH- F. Division: 0 point: 35

Katika hali ya kushangaza. Tamisemi imetumia namba hiyo hiyo ya kidato cha nne ya mtu aliyefeli kumwajiri BABU LEMBRICE PETER kama mwalimu wa History na Kiswahili kwenda kufundisha shule ya msingi Maliwa. Jina la BABU LEMBRICE PETER lipo ukurasa wa 21 kwenye ajira za walimu pia nimeweka kiambatanisho.

Maswali ya kujiuliza:

1. Imekuwaje namba ya kidato cha nne kuanzia center namba ya shule, namba ya mwanafunzi na mwaka wa kumaliza zifanane kwa kila kitu?

2. Watu watakuja na utetezi kwamba EMMANUEL MANEMBE alibadili majina na kutambulika kama BABU LEMBRICE. Kama ni hivo, imekuwaje Tamisemi ikaajiri mtu aliyefeli masomo ya kidato cha nne kwa kupata daraja sifuri?

3. Je, BABU LEMBRICE ana undugu au alicheza deal na moja ya mtumishi huko tamisemi akamfanyia mpango wa kupata ajira?

Kutokana na mapungufu yaliyo kwisha kubainiwa na mengine tutakayo endelea kuyabaini na kuyaibua hadharani. Tunaomba serikali isitishe kwa muda mchakato wa kuwaruhusu walimu wapya kuripoti vituoni badala yake mchakato wa kuwapangia walimu shule za kufanyia kazi urudiwe upya na uchunguzi kwa kupitia takukuru na TISS ufanyike ili watumishi wote waliohusika kufanya ubadhirifu kwenye hizi ajira wachukuliwe hatua kali za kinidhamu.

Kiambatanisho: majina na index namba ya BABU LEMBRICE PETER
IMG_20201129_0002.jpeg

Kiambatanisho: jina, matokeo(csee 2010) na index ya kidato cha nne ya EMMANUEL MANEMBE

IMG_20201129_0001.jpeg

Screenshot_20201129-135243~2.png
Screenshot_20201129-135243~2.png
 
Hii inaweza tokea kwani kipindi Cha kuregister ilihitajika namba ya form four kwenye mfumo watu wengine account zao zilifungwa eidha kwa kusahau password.

Wakawa wanafanya ujanja wa kufungua account nyingine kwa kutumia namba nyingine anajaza taarifa zake Kama kawaida na kutuma maombi.

Wahuni siyo watu wazuri ona sasa watu wanaitupia lawama TAMISEMI.
 
Hawa watu wanatuchezea akili,kuna watu wasomi wazuri wameaply lakini cha ajabu wameachwa anakuja kuchaguliwa ambaye hana sifa kabisa,hivi tamisemi wanasubiri hata hili aingilie mh.rais magufuli wakati udhaifu mmeuona,hawa jamaa bila michongo hupati ajira,watu wanawatu wao hata matangazo ya ajira ni geresha tu.Sisi tusio na michongo tumekata tamaa kuaply
 
Serikali hii usiiamini kwa asilimia nyingi kwa kila wanalolifanya au kulisema.
Kila jambo wewe shika 50% kisha 50% zinazobaki ndio uwaachie
 
Back
Top Bottom