Jasusi anayejinasibu kuwa shushushu mbobebezi, alishindwaje kujua ukweli wa Sifika Daniely

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
1,126
4,169
Yericko Nyerere, aliandika huko Facebook

Mh Waziri wa Elimu Prof Adolf Mkenda okoa mstakabali wa maisha ya binti huyu.

"Kaka Yericko pole na Majukumu, Naomba kaka nisaidie, mtoto huyu kwenye picha anaitwa SIFIKA DANIELY RUBEN, naomba apate Haki zake, Ipo hivi kaka, Nilikuwa natafuta binti wa kazi za ndani, Nikapata binti kutoka Hedaru, alipofika nikamuhoji ili kujua ametoka wapi hasa, na familia yake ipoje.

Akaniambia amemaliza Form Four, Ana Division One ya 10, Nikamuuliza Kwanini hujaenda shule, Akasema shule aliyopangiwa wameuza jina lake, Alipoenda kuripoti aliambiwa nafasi yake haipo. Nimeumia Kiukweli naomba nisaidie kwa wahusika binti apate haki yake, Mimi sina kipato kikubwa lakini kwa shule ya serikali nitamsomesha, lakini anapataje haki yake maana mimi kumpeleka shule binafsi uwezo sina.

Shule aliyomalizia Form Four ni MKOMBOZI SECONDARY SCHOOL ipo Hedaru Wilaya Ya Same. Shule aliyopangiwa aripoti Form Five Inaitwa NAMWAI HIGH SCHOOL Ipo Mkoa wa Kilimanjaro Sanya Juu,
Na Mchepuo aliopangiwa ni PCM

Namba yake ya Mtihani ni S.P. 0708/0136

Naomba Nisaidie Huyu Mtoto apate haki Yake Arudi shule Mimi nilitaka mfanyakazi ndo nimeletewa Huyo na Moyo wangu Umekosa Amani Nafasi yake Imeuzwa Kisa Alichelewa Kurepoti shule Wazazi wake Hawana Msaada Tena Maana Baba yake ni masini kabisa, na Mama Yake mzazi kwa sasa ni Mgojwa. Naomba Nisaidie apate hake yake Mimi Nitamsomesha Kwa hikihili kipato changu kidogo Nilichojaliwa".

===
Pia Soma Shule ya Sekondari Mkombozi: Sifika Danieli Rubeni alidanganya taarifa ya kuuzwa kwa nafasi yake ya kidato cha tano
 
Jina amepewa m5oto wa kigogo wa CCM na historia inaonyesha CCM wanasoma kijanjajanja hasa kwa kutumia majina na vyeti vya watu wengine.
 
Back
Top Bottom