Serikali kutodhibiti idadi ya wageni wanaoingia nchini kwa kisingizio cha Utalii, inahatarisha Usalama wa Taifa dhidi ya virusi vya Corona

Acha uongo wewe...Port Health kila Siku pale KIA kwenye arrival side sana scan watu wanaoingia kuhusu Afya...

Same to JNIA .

Sent using Jamii Forums mobile app
ninajaribu kubahatisha tu kwa ulichomaanisha maana duuh hiyo lugha uliyotumia hapo ni chiboko yake . nahisi ulitaka kumaanisha KIA wako vizuri kupima afya za wageni. ndg yangu,corona mpk ulaya imefika na ninaamini imepitia airport. siamini kwamba sisi ni hodari kupima afyya za watu kushinda uswis
 
mmteule,
Mkuu mbona unapayuka kama upo klabuni. Ummy mwalimu waziri wa afya amesema watalii kutoka china wameongezeka kuingia hapa nchini kipindi hichi ambacho wamekumbwa na janga hili la corona
 
Acha uongo wewe...Port Health kila Siku pale KIA kwenye arrival side sana scan watu wanaoingia kuhusu Afya...

Same to JNIA .

Sent using Jamii Forums mobile app
Ina maana Hizo nchi za ulaya zilizopiga marufuku, wachina hawana vifaa hivyo?!! USA mwenyewe, (baba lao) anaogopa sembufe nyie WANA TUKUNYEMA!! SHAME ON U!! Kipindu pindu tu huwa kikianza ni tabu sembuse huo??
 
mmteule, Mkuu kama uyasemayo ni Kweli,kwanini Wahusika hawatoi Tangazo la Kuzuia Watu kutoka Nchi zilizoathiriwa haswa China,Korea! IPO Kimya,huoni ukimya Pia una Madhara yake hata Kwa Watalii wa Kizungu pia,na Afya Zetu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa sasa kila kitu kiko wazi, tishio la kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Corona lipo kwa kila nchi, na Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi zilizotajwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kuwa na hatari kubwa zaidi za kukumbwa na janga hilo wakati wowote ule kuanzia sasa.

Mpaka sasa safari za ndege kutokea China zinaendelea huku idadi ya wasafiri kutokea China kuingia Tanzania ikielezwa kuongezeka karibu mara tatu zaidi (mojawapo ya sababu zinazotajwa ni kuwa Wachina wanakimbia maambukizi ya Corona huko kwao).

Ni wakati muafaka sasa kwa serikali ya Tanzania kuchukua hatua ngumu na haraka ya kusitisha safari hizo.

Asiyesikia la mkuu...
Asiyeziba ufa...
Mkataa pema...
Samaki mkunje...
Heri nusu shari...
 
Mungu baba atuepushe na kikombe hiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mungu ameshatupa akili, maarifa na maamuzi ya kufanya ili kupambana na virusi vya Corona, tatizo letu ni shingo ngumu, hatutaki kuchukua hatua madhubuti, tunajifariji kwa woga, ujinga na uvuvi tuliouficha katika kichaka cha dua na maombi huku tukidhani Mungu hajui. Sasa ngoja kiwake ili akili itukae kisawa sawa.
 
Wanasubiri waje watuambie "Serikali haijaleta Corona" Nakwambia this time watakipata kile walichokitafuta kwa muda mrefu.
 
Serikali yetu ina watu wa ajabu. Watu waliobahatisha uongozi bila ya kuwa na sifa za uongozi. Hata kama hatuna akili, tunashindwa hata kuiga mataifa mengine walivyofanya?

Tamaa ya pesa ndogo kutoka kwa watalii wa China isitufanye kuwa punguani.
 
ninajaribu kubahatisha tu kwa ulichomaanisha maana duuh hiyo lugha uliyotumia hapo ni chiboko yake . nahisi ulitaka kumaanisha KIA wako vizuri kupima afya za wageni. ndg yangu,corona mpk ulaya imefika na ninaamini imepitia airport. siamini kwamba sisi ni hodari kupima afyya za watu kushinda uswis
Pole ndugu..

Port health -taasisi ya serikali pale airport inahusika na kufanya checking za afya

KIA-Kilimanjaro International Airport

JNIA-Julius Nyerere International Airport


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kipindi ninatetea wale wanafunzi wa Kitanzania warudishwe nyumbani nilipokea matusi na kejeli!! Sasa ndo mpembue mliokuwa mnapinga. Wachina wanapata usafiri wa kuja huku ikiwa wao ndio wahanga wakubwa wa COVID-19 na mnawakataa watanzania wenzenu!

Ilipaswa uwekwe utaratibu wa kuwapokea hao wanafunzi lkn badala yake wanaingia wachina kwa wingi!! Huku ndo kuruka majivu na kukanyaga moto.. time will tell
Inasikitisha sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani wanazuia sisi tusiende lakini wanawaruhusu wachina kuingia, Tena Sasa maambukizi nje ya China Ni makubwa zaidi
 
Back
Top Bottom