Serikali iitishe kura ya maoni Wazanzibari waamue upya kama wanautaka muungano ili isionekane tunawalazimisha

Zanzibar ingekuwa huru, ingepinga hatua kubwa kimaendeleo na ingepata fursa nyingi kuliko kuendelea kukaliwa na mkoloni Tanganyika
Comoro na Madagascar ni visiwa huru, kuna maendeleo yoyote ya maana?
 
Ukanda wa pwani hawawezi kuupata.

Haijawahi kutokea mahali popote Duniani, kisiwa kumiliki inland, ila kuna inland countries nyingi zinazomiliki visiwa.
Kasema kimhemko tu na udini, toka lini kisiwa kikawa na inland 🤣
 
Wazibar walioko Tanganyika,wote wahame,warudi Zanzibar,hiyo ni kura ya maoni tosha,kama hawataki muungano.
Mkuu kwani wale wasomali pale Ilala au Wahindi kule Posta tumeungana nao?

Kuishi somewhere hakuhusiani na muungano.
 
Na sisi Watanganyika tuulizwe kama tunautaka muungano.Huyo kupe katuchosha maana ni jeuri.
 
Kauli zozote za kishujaa kuhusu muungano ni nakili kutoka kwa waasisi wa mataifa haya mawaili. Huenda labda kwa wakati huo muungano ulikuwa na manufaa lakini sio sasa. Kama nyumba ya zamani inaweza kuvunjwa na kujengwa mpya inayoendana na wakati, basi hata muungano kwa sasa ni jumba la kale linalotakiwa kuvunjwa na kujengwa upya kwa mahitaji ya sasa.

Kama wazanzibar walio wengi wanaunung'unikia muungano basi kuna hatari kubwa kizazi kijacho kikaja kuingia vitani kudai uhuru wao. Yapo mengi ambayo wazanzibar wanaamini muungano unawakosesha.

Kwa mfano Zanzibar wanabendera lakini bendera yao haitambuliki popote zaidi ya wao wenyewe. Zanzibar ilikuwa nchi na sio Kijiji kwa hiyo Zanzibar ilipaswa kuwa na kiti kwenye mabaraza yote ya umoja wa Afrika! Kwa sasa hawana.

Zanzibar hawana muwakilishi hata katika mashindano ya kimataifa, Zanzibar kama wanaona muungano hauna manufaa tena kwao tusiwalazimishe. Ndoa yoyote huwa inavunjwa kwa hiyari serikali ione umuhimu wa kuruhusu kura ya maoni, ili wazanzibar waamue kwa sababu kizazi kilichopo sasa sio kile Cha mwanzo mwa 1965.
Nyerere alikosea sana hicho kisiwa kinatakiwa kuchukuliwa jumla kama India alivyofanya pale Kashmir.
 
Halafu tukutane nao EAC.

Kitakachotokea:

1. Kama Samia atakuwa bado madarakani, italazimu Tanganyika kuongozwa na Rais wa mpito kwa mara ya pili.

2. DPW itabidi iende kue desha bandari za Zanzibar, maana imekuja Tanzania kama deal la wazanzibari.

3. Zanzibar litakuwa taifa la kwanza la kigeni kuuziwa umeme na TANESCO.

4. Mchele na ndizi toka Tanganyika zitaanza kuuzwa Zanzibar kwa kutumia sarafu ya Marekani.

5. Itakuwa patashika Tanganyika itakapotangaza wahamiaji toka Zanzibar kutakiwa kukamilisha taratibu za uhamiaji, huku wengi wakiamua kuukana uraia wa Zanzibar ili kukidhi sheria ya uhamiaji ya Tanganyika!!

Katika porojo ni rahisi sana kusema Muungano uvunjike, lakini kiuhalisia, hilo likitokea, inaweza kuchukua hata miaka 50 mpaka Zanzibar kutengamaa kama Taifa.
Kwa Leo ni kama gumu ipo siku litawezekana kwa mtutu wa bunduki
 
Wanalia lia sana hawa watu ifike wakati maamuzi magumu yachukuliwe wenyewe wamejaa kuuza samaki hadi vichochoroni huko bara lakini hawataki wabara wakafanye kazi,na kazi zenyewe wawe wanaweza sasa kufanya,huku wanapewa URC,DC na nyadhifa mnalimbali kwao ni wao kwa wao bado hawaoni hayo yote
Ni sawa
 
Kauli zozote za kishujaa kuhusu muungano ni nakili kutoka kwa waasisi wa mataifa haya mawaili. Huenda labda kwa wakati huo muungano ulikuwa na manufaa lakini sio sasa. Kama nyumba ya zamani inaweza kuvunjwa na kujengwa mpya inayoendana na wakati, basi hata muungano kwa sasa ni jumba la kale linalotakiwa kuvunjwa na kujengwa upya kwa mahitaji ya sasa.

Kama wazanzibar walio wengi wanaunung'unikia muungano basi kuna hatari kubwa kizazi kijacho kikaja kuingia vitani kudai uhuru wao. Yapo mengi ambayo wazanzibar wanaamini muungano unawakosesha.

Kwa mfano Zanzibar wanabendera lakini bendera yao haitambuliki popote zaidi ya wao wenyewe. Zanzibar ilikuwa nchi na sio Kijiji kwa hiyo Zanzibar ilipaswa kuwa na kiti kwenye mabaraza yote ya umoja wa Afrika! Kwa sasa hawana.

Zanzibar hawana muwakilishi hata katika mashindano ya kimataifa, Zanzibar kama wanaona muungano hauna manufaa tena kwao tusiwalazimishe. Ndoa yoyote huwa inavunjwa kwa hiyari serikali ione umuhimu wa kuruhusu kura ya maoni, ili wazanzibar waamue kwa sababu kizazi kilichopo sasa sio kile Cha mwanzo mwa 1965.
Hakuna Uhuru wa kugawa nchi! Wwchaga hawawezi kuamka kesho asubuh na kutaka kujitenga, kwa sababu yoyote ile! Hilo ni kosa la uhaini! Muungsno sio tatizo hata kidogo, tatizo ni siasa mbovu za ccm!
 
Mimi sio mzanzibar ila ukanda wa pwani wote ni sehemu ya zanzibar .Pia usiwe na wasiwasi kwa sababu hata muungano unapovunjika yoyote anaweza kuishi popote kwa kufuata sheria.

Mzanzibar anaweza kuomba uraia wa huku na huku akapta kule ,juzi tu hapa wapemba wamepewa uraia huko kenya.
Wakitaka tuwaongezee na mafia
 
Mkishaungana. Kuulinda sio lelemama. Mfano wa Kosovo ilikuwa nguvu kutoka nje kama hao wanaolialia Zanzibar dhidi ya muungano. India ina majimbo 3 yanatawaliwa kutoka serikali kuu kwa sababu ya vuguvugu ya kujitenga. Qubec, Canada ukiwaachia kidogo tu wanameguka. California, USA inatamani mpaka kesho imeguke kutoka ilipo. Catalunya, Hispania vuguvugu ni hizo hizo lakini dola ipo lazima ilinde eneo lake. Hakuna dola inapenda ardhi yake imeguke.
muungano udumu tu na matatizo yaliyopo.
 
Kura ya maoni ya nini wakati wa muungano watu hawakuulizwa. Kwanza muungano uvunjwe alafu anayetaka muungano aseme kama hawa Comoro
 
Back
Top Bottom