Duru: ' Utata wa Utatu', Katiba, Muungano na Kura ya Maoni

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
15,410
31,397
Sehemu ya I

Bandiko Duru: Hatima ya Muungano na dalili za kuvunjika mapema tulisema bila kura ya maoni na Katiba ,tuna ahirisha tatizo la Muungano kwa muda.

Kuna 'utatu' wa ''Katiba, Muungano na Kura ya maoni'' . Madai ya katiba ni katika eneo la madaraka ya Rais, kuimarisha taasisi na kuzifanya huru, utaguzi wa madaraka na suala la Muungano.

Ukweli, Muungano ni sehemu muhimu ya uandikaji wa katiba, suala lilodumu takribani miaka 60.
Muundo wa Muungano unaacha maswali yasiyo na majibu '' Loose ends'', kuanzia kwa Karume, Aboud Jumbe, G55, Jaji Nyalali, Jaji Kisanga, na kamati zingine ikiwemo maarufu ya Jaji Warioba.

Zaidi ya 75% ya Watanzania walizaliwa baada ya Muungano. Ni kizazi kinachohoji na kina weledi kuliko cha wakati wa Muungano ambacho kilikubali Muungano bila kuhoji ''conventional'

Usahidi wa hoja hii unatolewa na maneno ya Mzee WArioba akisema '' kulikuwa na makundi yaliyotaka muundo wa Muungano wa Serikali 1, Serikali 2, Serikali 3 na Hata kuvunja Muungano'.

Katika makundi aliyotaja Mzee Warioba, ni kundi moja tu lina msimamo wa uhakika, lile la Kuvunja Muungano.
Makundi ya Serikali (S1,S2,S3) yanaonyesha kutaka Muungano yakiwa na misimamo tofauti na hati hati.

Makundi tajwa hapo juu yanatupa swali muhimu lisilotakiwa kuulizwa.
Kizazi cha Muungano Wazee '' conventional'' hakitaki kueleza , kudadisiwa au kuhojiwa.
Ni kizazi kilichokubali Muungano kwa majibu rahisi ' Ni tunu, tuliachiwa na Wazeu, ni Muungano wa kipekee etc''

Linapoulizwa swali la maudhi kilakaulizwa '' Kwanini kusiwepo kura ya Maoni'' kwa Zanzibar kuamua iwapo inataka Muungano au la, kizazi cha Wazee kinaliona swali hilo ni la kihuni, kihaini na kihalifu.

Kizazi cha Wazee kinaamini Muungano usihojiwe na utakuwepo tu ukubalike ''conventinally'.
Ni kizazi kisichoangaalia mabadiliko ya nyakati , watu na mazingira. Hakitaki kusikia kura ya maoni! hivyo tu!!

Kura ya Maoni ni suala linalokamilisha 'utatu' wa Katiba na Muungano.
Mambo hayo 3 huwezi kuyatenga ikiwa nchi inataka suluhu ya kudumu ya aina yoyote ile itakayokubaliwa.

Kuandika katiba inakubaliwa na kila mmoja wetu wakiwemo wahafidhina wa CCM.
Kwa pamoja, watu wanakubaliana katiba iandikwe upya, iwe shirikishi kulingana na matakwa ya nyakati

Kura ya maoni inaepukwa tu kwa hofu ingawa linajulikana ni suala muhimu sana kabla ya kuandika katiba kwani italeta muafaka kwamba nchi mbili zinakubaliana au hazikubaliani.

Katika kukwepa kura ya maoni kuna maswali yanaulizwa, na hakika yanafikirisha.
1. Kwanini iwe Zanzibar?
Ni muda mrefu Zanzibar ikiwa nchi ndogo inalalamika kuonewa na Tanganyika.
Kanuni za asili zinaipa Zanzibar haki ya kura ya maoni ili kutendewa haki.

Ikiwa Tanganyika itashiriki na kuamua uwepo wa Muungano, itathibitisha madai ya Zanzibar kwamba inafanywa koloni kwa ubabe tu.

Si mara ya kwanza kutokea duniani, kanuni zinapipa Zanzibar haki ya kura ya maoni kama ilivyokuwa kule East Timor mwaka 1999 ilipoamua kujitoa Indonesia, au Eritrea 1993 kujitoa Ethiopia, au Quebec Canada 1980 na 1995 kutoka Shirikisho la Canada, na pia Scotland kutoka UK. kwa uchache wa kutaja.

2. Je katiba yetu inaruhusu Kura ya maoni?
Jibu lni rahisi, je mchakato wa kuandika katiba kuanzia Mzee Warioba na kamati ya Mkandala ulifuata sheria au katiba ya sasa? Ni mambo mangapi yanakiukwa katika katiba hii inayolindwa dhidi ya kura ya maoni?
Katiba JMT inapokiukwa na Katiba ya Zanzibar ni sheria gani inafuatwa ?

Je, mgogoro wa Jaji Mkuu kuteuliwa au kuondolewa CAG vilifuata sheria za nchi?
Hoja hii haina maana ya kuhalalisha haramu, ina maana moja kwamba nafasi ya kuanzisha mchakato wa kura ya maoni ipo tena kwa kufuata sheria kama utashi wa kisiasa upo, utashi ule ule unakiuka katiba ya leo

Hoja ya Mwisho ni ya Muungano , suala linalochelewesha katiba, ni mwiba kwasababu watawala hawataki kusikia tofauti na wanavyotaka.

Ni suala lililoua Bunge la Katiba na historia yake si nzuri. Kila jitihada zinafanywa kuliepuka kwa udi na uvumba.

Je, suala la Muungano liangaliwe kwa kutumia darubini gani? Mchakato wa Rasimu ya Warioba?
Rasimu ya CCM ya katiba pendekezwa? au Kamati ya Prof Mkandala?

Waziri husika anasema mchakato wa kuandika katiba utaanza mwezi wa Septemba.

Hakuna anayejua mchato utaanza alipoishia Mzee Warioba au kuna namna tofauti.
Maoni ya Mzee Warioba ndiyo maoni ya Wananchi.
Hakuna chombo au tume nyingine yoyote iliyokuja na maoni shirikishi zaidi ya Tume ya Mzee Warioba.

Kuna hoja potofu eti maoni ya Tume ya Mzee Warioba yamepitwa na wakati.
Ni hoja za kipuuzi sana kwasababu endapo tungekuwa na katiba baada ya Bunge la Katiba, leo tusingeifuta kwa hoja kwamba maudhui yake yamepitwa na wakati.

Jitihada za kuua maoni ya Tume ya Mzee Warioba zinafanywa kwa kutumia chombo mbdala '' Kamati ya Prof Mkandala' iliyoundwa kumshauri Mh Rais lakini si shirikishi wala si ya kikatiba.

Kamati ya Prof Mkandala na uwepo wa Tume ya Haki jinai chini ya Jaji Chande na kutangazwa na Msajili wa vyama mchakato wa Tume huru ya uchaguzi kunaeleza kitu komoja, suala la kuandika katiba halipo.

Kilichopo ni kuweka viraka katiba ya 1977 kwa kisingizio kwamba mambo muhimu yameshughulikiwa na Tume husika hakuna haja ya kufumua katiba iliyopo. Yote yanAtokea kwasababu tu ya kukwepa suala la Muungano.

Itaendelea
 
Sehemu ya II
Ikifanyika mizengwe ya kuweka Viraka Katiba ya 1977 kwa kutumia kamati ya Prof Mkandala, Tume ya Haki jinai na Tume huru ya uchaguzi kupitia msajili, hilo halitatua tatizo la Muungano.
Licha ya muundo wake kuwa na matatizo, nyakati na kizazi havitoi nafasi ya kuisimamia tena.

Kuna maswali yanayohitaji majibu. Mfano, je Wananchi wanataka Muungano au la!
Ikiwa la! nini kifanyike. Ikiwa wanataka ni muundo gani wanaoutaka. Hayo yanatanguliwa na jibu la kura ya maoni.

Scotland, moja ya nchi za Falme za Uingereza (United Kingdom) imetaka kujitenga iwe na mamlaka kamili 'sovereignty' kwa muda mrefu, ikiwa ni agenda ya Chama cha Scottish Natioanl Party (SNP).

Muungano kati ya Scotland na England ulichagizwa na sababu za kiusalama wakati huo kwa England.
Hoja ya Scotland inasimama katika Utamaduni na uchumi wakiamini nje ya UK watakuwa bora.

Ili kuimarisha Muungano mwaka 1979 walifanya kura ya maoni ya kupata Utaguzi 'devolution' iliyoshinda lakini ikashindwa kwa sababu za kiufundi (siyo kuiba kura). Idadi ya wapiga kura ilikuwa chini ya kiwango kilichojiandikisha.

Mwaka 1998 ikaitishwa kura nyingine ya utaguzi 'devolution' ya kuwa na Bunge, ikapita, wakawa na Bunge kama ilivyo kwa Zanzibar. Mwaka 2014 kukawa na kura ya maoni Scotland ya kujitoa kutoka UK. Kura ikashindwa kwa 55%.

Canada: Mwaka 1980 chama kilichoongoza jimbo la Quebec, Parti Quebecois (PQ) kilishinikiza serikali ya shirikisho kwa kura ya maoni kuamua endapo jimbo lipewe 'mamlaka kamili' yaani sovereignty.Kura ilishindwa kwa 59%.

Mwaka 1995 Parti Quebecois kilishinikiza kura nyingine ya maoni baada ya kampeni kali. Matokeo yalikuwa kushindwa kwa 50.1% . Tangu wakati huo hali imeimarika kwasababu kura mara 2 ni uthibitisho wa kauli ya Umma.

East Timor: Tofauti na wengine walioungana ilinyakuliwa na Indonesia. Baada ya vurugu Indonesia ikawapa chaguo la kuwa na autonomy kwa maana mamlaka yake chini yake. Vurugu ziliendelea na UN kuingilia kati.
Kura ya maoni wa Timor wakashinda na wakajitoa.

Eritrea: Historia inafafana kidogo na East Timor. Waitaliano walipoondoka Ethiopia ikanyakua Eritrea.
Upinzania ukaendelea hadi kura ya Maoni chini ya UN mwaka 1993 . Kwa 99% Wa Eritrea wakajitoa Ethiopia.

Kwa mifano hiyo michache, kura ya maoni ni muhimu ingawa kwa siasa za Tanzania haipewi kipaumbele.
Kama ilivyokuwa Scotland, Quebec , Timor na Eritrea, ni wakati Zanzibar ipewe haki ya kura ya Maoni
Kura ya Maoni kwa Zanzibar ihusu uwepo au kutukuwepo Muungano si kuamua aina ya Muungano

Haiwezekani upande wowote kudai Muungano uendelee au hapana kwasababu hakuna ushahidi wa takwimu.

Kwa karibu sana Tume ya Warioba iliyokusanya maoni inaweza kutumika kama kipimo ''Yardstick' ingawa haikuwa kura ya maoni. Wananchi walitoa maoni kwa kuzingatia mwongozo wa uwepo wa Muungano kwa mujibu wa Tume Swali lingekuwa YES or NO matokeo yangekuwa ns sura tofauti.

Kwa Tanzania Chama cha ACT kina 'agenda' sawa na SNP ya Scotland au PQ ya Quebec. Chama cha ACT hakiamini katika upekee wa kujitawala ''semi autonomy' kama SNP au PQ kwa sasa na wala hakiamini katika kurekebisha muundo wa Muungano.ACT kinaamini katika mamlaka kamili ambayo ni ' sovereignty'

Tofauti na SNP au PQ, ACT hawataki kudai hivyo au kusema wanataka kujitoa katika Muungano.
ACT wakiwa washirika wa CCM katika serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU) wana uwezo wa kuwashawishi CCM Zanzibar wadai kura ya maoni kwanza kama walivyofanya SNP au PQ. Chama cha ACT kimejielekeza katika kuwasumanga na kuwatusi Watanganyika wa kawaida kana kwamba tatizo limesababisha nao.

Kutafuta majibu ya tatizo la Muungano si ''uchuro'' wala azma ya kuvunja, ni kutafuta ukweli utakaokuwa dira.
Kuwa aminishwa Wananchi kwa nguvu tu Muungano ni tunu ya Taifa ni dhanapotofu inayochangia kuudhofisha.

Mjadala wa Katiba iwe kuweka viraka ile ya 1977 au kuandika Mpya hautawezekana kwa njia yoyote ile bila kugusa Muungano. Mjadala wa aina hiyo huitwa mfu kabla ya kuanza '' Dead on arrival'.

Jamii inakubaliana kwamba katiba ya 1977 ina matatizo mengi ikiwemo muundo wa Muungano.
Hata wanaotetea uwepo wa serikali katika mfumo wowote wanaamini Katiba ya 1977 ina matatizo.

Tatizo linakolezwa baada ya Zanzibar kudurusu Katiba ya 1984 kwa toleo la 2010.

Katiba ya Zanzibar 1984 toleo 2010 limetoa utaguzi 'devolution' kwa Zanzibar yenyewe bila kushirikisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) tofauti na kilichotokea 1979 na 1998 kule Scotland.

Wataalam wanasema Katiba ya 1984 toleo la 2010 iliandikwa 'unilaterally'' .
Katiba ya Zanzibar kujiamulia ' semi autonomy' imeleta mkanganyiko mkubwa wa kikatiba.

Katiba ya JMT na ile ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) vinakinzana, wala hakuna ukuu wa moja dhidi ya nyingine. Hoja kwamba ni katiba za nchi mbili hivyo zina usawa inatumiwa na wapuuzi tu wasioshughulisha akili.

Katiba ya JMT si ya nchi mshirika. Hata kwa ''mtaani'' tu huwezi kuweka mizani kati ya Mama na Mwanae.
Ulinganifu unaweza kuwekwa kwa katiba ya Tanganyika na Zanzibar na si vinginevyo.

Haitoshi kusema tu kuna mkanganyika, bandiko linalofuata tutaanisha baadhi ya maeneo yanayoonyesha tatizo la Muundo wa Muungano, udhaifu wa katiba ya JMT 1977, ukuu wa Katiba ya Zanzibar ya 1984 toleo 2010.

Inaendelea.....
 
Sehemu III
(Katiba ya JMT 1977 na Muundo wa Bunge la JMT)

(1) Sehemu ya Katiba ya JMT (1977) Sehemu ya Kwanza (1) inasema Tanzania ni NCHI moja na ni Jamhuri ya Muungano, Sura ya Kumi na moja ibara 152 (3) Ikieleza Katiba ya 1977 kutumika Tanzania Bara vile vile Tanzania Visiwani.

(2)Sehemu ya Kwanza Ibara ya (3) inaeleza Mambo ya Muungano kama ilivyoelezwa katika nyongeza ya Kwanza, na Mambo yasiyo ya Muungano nyongeza ya Pili orodha ya Kwanza. Orodha ya Pili ina mambo yanayohitaji 2/3 ya kura za Wabunge wa Tanzania Bara na 2/3 ya Wabunge wa Tanzania Visiwani.

Kabla ya kupitia mkanyiko wa katiba ni vema tuapte picha ya Bunge la JMT ili kuweza kuoanisha hoja

(3)
Kwa mujibu wa tovuti ya Bunge ya JMT idadi na mgawanyo wa Wabunge ni kama ifuatavyo
1. Wabunge wa kuchaguliwa kutoka majimboni - Tanzania bara 264 , Zanzibar 50
2. Viti Maalumu Wanawake 113
3. Wabunge wa kuchaguliwa kutoka Baraza la Wawakilishi (BLW) Zanzibar - 5
4. Mwanasheria Mkuu wa Serikali- 5
5. Wabunge wa kuteuliwa na Rais wa JMT- 10

Jumla =393 (Kwa mujibu wa tovuti ya Bunge).

(4) Wabunge wa kuchaguliwa na kuteuliwa na viti Maalum kutoka Zanzibar idadi yao takribani 80.
(hii ni kwa kadirio kwamba wa viti maalumu ni 1/3). Takwimu mpya zikipatikana tutadurusu upya.
Wabunge 5 kutoka Baraza la Wawakilishi ni kiungo cha mijadala ya Bunge na ile ya BLW Zanzibar(BLW).

(5) Katiba ya JMT 1977 Sehemu ya Tatu (84) na (85) vinaeleza utaratibu wa kumpata Spika na Naibu Spika wa Bunge.
Taratibu hizo pia zimeanishwa katika kanuni za kudumu za Bunge.
Ibara ya 93 inasema kikao cha Bunge kitaongozwa na Spika au Naibu Spika au Mbunge aliyechaguliwa na Bunge kwa ajili hiyo. Ibara ya 94(1) inaeleza kiwango cha kikao cha Bunge ni nusu na kura itaamuliwa kwa kufuata wingi wa kura ispokuwa kama imeelezwa vingine (mfano mambo yanayohitaji 2/3)

(6) Katiba (1977) (89) inatamka uwezo wa Bunge kuunda kamati kupitia kanuni za Kudumu.
Kanuni za Bunge kwa mujibu wa tovuti imeanisha aina za kamati za Bunge

(7) Muundo wa Kamati za Bunge (Kwa hisani ya tovuti ya Bunge) unadwa na kamati 19: Uongozi ,Kanuni za Bunge
Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Maji na Mazingira Elimu, Utamaduni na Michezo ,Miundombinu ,Nishati na Madini, Afya na Masuala ya Ukimwi,Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo ,Utawala, Katiba na Sheria,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Ustawi na Maendeleo ya Jamii , Ardhi, Maliasili na Utalii ,Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Uwekezaji wa Mitaji ya Umma, Bajeti ,Sheria Ndogo ,Hesabu za Serikali ,Hesabu za Serikali za Mita

Mkazo (bolded) ni kamati zinazohusu mambo ya Tanganyika au Tanzania Bara tu.

Tumeweka maelezo hayo juu makusudi kabisa. Baadhi ya Wasomaji wanaweza kutoona umuhimu wake, mbele ya safari itatusaidia kuonyesha matundu na ubovu wa katiba na vyombo vingine kama Bunge.
Mfano, mtu anaposema jambo fulani haliwahusu Wazanzibar imekuwa ni kawaida kupata 'reactions' kwamba mtu huyo analeta siasa za Ubaguzi. Kusema jambo haliwahusu Wazanzibar si maneno ya watu, Katiba ya JMT(1977) Sehemu ya Kumi na Moja Ibara ya 152 Nyongeza ya Kwanza , orodha ya kwanza na ya Pili. Mambo yasiyo ya Muungano ina maana ima hayahusu Tanganyika au hayahusu Zanzibar na huo si UBAGUZI kwa mujibu wa Katiba.

Tutaangazi Muundo wa Katiba katika vyombo vya Umma kama serikali na Bunge

Inaendelea sehemu ya IV
 
Sehemu ya IV

Mambo ya Muungano kama yalivyo katika Nyongeza ya katiba ya JMT 1977
1. Katiba ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Muungano
.2. Mambo ya Nchi za Nje.
3. Ulinzi na Usalama.
4. Polisi.
5. Mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari.
6. Uraia.
7. Uhamiaji.
8. Mikopo na baiashara ya Nchi za Nje
.9. Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
10.Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika,ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwanchini Tanzania unaosimamiwa na Idara ya Forodha.
11.Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta nasimu
.12.Mambo yote yanayohusika na sarafu na fedha kwa ajili yamalipo yote halali (pamoja na noti); mabenki (pamojamabenki ya kuweka akiba) na shughuli zote za mabenki;fedha za kigeni na usimamizi juu ya mambo yanayohusikana fedha za kigeni.
13.Leseni ya viwanda na takwimu.
14.Elimu ya juu.
15.Maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa yamotokaa na mafuata ya aina ya petroli na aina nyinginezo zamafuta au bidhaa, na gesi asilia.
16.Baraza la Taifa la Mitihani la Tanzania na mambo yoteyanayohusika na kazi za Baraza hilo
.17.Usafiri na usafirishaji wa anga.
18.Utafiti.
19.Utafiti wa hali ya hewa.
20.Takwimu.
21.Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano.
22.Uandikishaji wa Vyama vya siasa na Mambo mengineyanayohusiana navyo.

Mambo yanayohitaji 2/3 ya pande zote, yaani Tanganyika na Zanzibar
1. Kuwapo kwa Jamhuri ya Muungano.
2. Kuwapo kwa Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano.
3. Madaraka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
4. Kuwapo kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano.
5. Madaraka ya Serikali ya Zanzibar.
6. Mahakama Kuu ya Zanzibar.
7. Orodha ya Mambo ya Muungano
 
Sehemu V

Katiba ya JMT 1977 imeanza kutumika mwaka huo. Kwa maana kwamba mpangilio wa Wabunge (rejea bandiko 3 (3)) upo tangu siku ya kwanza ya katiba ikutumika na ilisema 'Bungeni la Jamhuri ya Tanzania' na Kwamba Tanzania ni nchi Moja.

Katiba ya JMT 1977 inatambua uwepo na mamlaka ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na vyombo vyake.

Katiba imetamka katika sura 3 (64)(1) '' Mamlaka ya Kutunga sheria ya Mambo ya Tanzania Bara (Tanganyika) yatakuwa mikononi mwa BUNGE la Jamhuri ya Muungano.

Katiba na Kanuni za Bunge hakuna mahali Bunge limeelekezwa kukaa kama mamlaka ya kutunga sheria ya mambo ya Tanganyika likiwa na Wabunge wa Tanganyika tu kama ilivyo Baraza la Wawakilishi.

Kwa mantiki Bungel lenye Wabunge kutoka Zanzibar linatunga sheria za Tanganyika kinyume na katiba ilivyoagiza.

Huu ndio mwanzo wa hoja kwamba Tanganyika imevaa koti la Muungano.
Hoja hiyo ina tatizo kwasababu Watanganyika hawana uwezo wa kutunga sheria za nchi y (Tanganyika) kwa uwepo wa Wazanzibar ndani ya Bunge.

Bunge linaweza kuwa na Spika Mzanzibar, Naibu Spika Mzanzibar au Mwenyekiti aliyechaguliwa na Wabunge ikiwa Spika na Naibu hawapo kama ilivyoelezwa na Katiba (rejea bandiko la 3).

Katiba inasema, akidi ya Bunge ni nusu yao na ikiwa kura zitafungana kura ya Spika au Naibu itakuwa na uamuzi.

Kwa minajili ya mjadala, fikiria kwamba Bunge lenye Wabunge 393 ukiondoa wabunge takribani 80 wa Zanzibar, wanaobaki 213 ni Tanganyika. Ukiondoa kura ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wanabaki Wabunge 212

Wabunge 212 wa Tanganyika wanapofungana( 106 wakisema Yes na 106 wakisema NO) kwa kura wakijadili jambo lisilo la Muungano kama Afya, Elimu ., Utalii, Mandini na Nishati watakaoamua amua jambo hilo ni Wabunge 80 wa Zanzibar kwa maana kuwa majority ya 80 ndiyo itaamua Yes or No.

Hili si sahihi kwa Watanganyika ambao kwa namna yoyote hawawezi kuamua jambo katika Baraza la Wawakilishi.

Katiba inatamka tu mambo ya Tanganyika lakini hakuna utaratibu wa kitaasisi kuanzia Bungeni wa namna ya kutenga mambo ya Tanganyika kutoka yale ya Muungano.
Matokeo ni ya watu wasio na masilahi na Tanganyika wanaamua mustakabali wa masilahi ya Tanganyika.

Tunaposema Wazanzibar hawana masilahi ni kwasababu uwepo wao Dodoma ni kwa ajili ya Zanzibar kama katiba inavyosema, na kwamba katiba inasema yapo ya Muungano( rejea bandiko IV).
Hili si jambo la Ubaguzi, ni ukweli uliopo ndani ya Katiba.

wanaodhani Tanganyika imevaa koti la Muungano wapo sahihi kabisa, lakini koti lina gharama kubwa na ni zito kulibeba tofauti na inavyodhaniwa ikiwa ni pamoja na kupoteza uhuru wa kuamua mambo yanayoihusu.

Utata wa kutokuwa na mipaka ya jambo gani ni la Tanganyika Bungeni limesababisha kamati za Bunge zilizoundwa kwa kanuni za Bunge (rejea bandiko 3) kuwa na Wazanzibar wakisimamia mambp ya Tanganyika.

Hoja yao ni kwamba hili ni Bunge la Muungano , ukweli unabaki kwamba hawapaswi kuwemo katika kamati za Bunge zinazosimamia mambo ya Tanganyika wasiyo na masilahi nayo. Katiba imeeleza wazi kuhusu hili

Mbunge wa Chadema Kenan amekaririwa akisema '' Waliporudi kutoka Dubai kwenye ziara ya DP World' Wabunge wa Zanzibar katika kamati walisema ' Bandari si suala la Muungano halihusu Zanzibar''.

Bandari licha ya kuwa jambo la Muungano (rejea IV) wao Wamelisimamia kwamba si la Muungano wakiwa ndani ya Bunge lililoundwa na katiba ya JMT 1977 waliyo apa kuitetea.

Wazanzibar walikwenda Dubai kwa masilahi binafsi. Kitendo cha kuwemo Bungeni wakati suala la bandari linajadili hakikuwa sahihi, hawana masilahi na suala la Bandari wala si watiifu kwa JMT, vipi washirikishwe!

Tayari walisema bandari ni jambo lisilowahusu hivyo basi kura zao ambazo zingeweza kubadili msimamo wa kura za Watanganyika hazikupaswa 'kuhesabiwa''. Hata sauti za Ndioo kwa watu 80 zinanguvu. Kwanini wawemo Bungeni kujadili mambo wanayosema hayawahusu na kwa hakika si ya Muungano?

Wabunge Wazanzibar walisafiri kwa gharama za kodi za Watanganyika bila kuwa na masilahi na Tanganyika.

Uwepo wa Wazanzibar katika Kamati za Bunge za mambo ya Tanganyika si sahihi hawana masilahi na Tanganyika kwa mujibu wao, na katiba ya JMT 1977 imewapa nafasi ya kutohudhuria mambp yasiyo ya Muungano.

Hakuna njia ya mkato katika suluhu ya utata kama huu isipokuwa tu kupitia Katiba mpya kama alivyoshauri Mzee Warioba

Kuna suala la mambo ya Muungano kuongezwa kutoka 11 hadi 22 (rejea bandiko IV)
Je, hoja hiyo ina mantiki? Ina ukweli!


Inaendelea.....
 
VI

MAMBO YA MUUNGANO KUONGEZWA KINYEMELA

Tafsiri ya neno 'nyemela' ni kuvizia au kutenda jambo kwa usiri. Yapo madai ya Wazanzibar kwamba mambo 22 yaliyotajwa katika bandiko IV yameongezwa kinyemela.

Hoja ni kwamba mkataba wa Muungano ulikuwa na mambo 11, na sasa ni 22 na kuna wapuuzi wanasema yamefikia 36. Ni kweli kwamba mkataba ulikuwa na mambo 11. Ni upuuzi kusema ni 36 bila kuainishwa katika katiba ya JMT 1977.

Kumbukumbu zinatueleza, katiba ya 1977 iliandikwa Dar es Salaam na Kamati Maalum.
Miongoni mwa wajumbe ni Marhum Mzee Thabiti Kombo Jecha kutoka Zanzibar, mmoja wa Wanamapinduzi na Mzee aliyeheshimika Unguja, ndani ya ASP, TANU na CCM. Mzee Kombo ndiye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati

Wengine ni Mzee P. Msekwa na Mzee Nicodemus Banduka kwa kutaja wachache
.
Inatosha kusema Wajumbe kutoka Zanzibar na Tanganyika walikuwepo chini ya Mzee Kombo pale Motel Agip

Katiba ya 1977 imeanza kutumika April 26, 1977 kwa mujibu wa Katiba 152(2). Hii ina maana kwamba mambo 11 yaliyoongezwa kufikia 22 yalikuwa na ridhaa ya watu kutoka pande zote ndani ya kamati, ndani ya Bunge Maalumu

Katiba imeanisha Wabunge wa Zanzibar wa kuchaguliwa, kuteuliwa , Viti maalumu na Wabunge wanaotoka Baraza la Wawakilishi (rejea bandiko IV) . Wabunge hao wanajua uwepo wa ongezeko la mambo 11 kufikia 22.

Baraza la Wawakilishi kupitia Wabunge 5 linajua uwepo wa ongezeko la mambo 11 katika katiba.

Tangu 1977 hatujasikia hoja binafsi kutoka kwa Wabunge wa Zanzibar wakilalamika kuongezwa mambo ya muungano na kufikia 22. Sheria inaruhusu kupeleka mswada binafsi.

Chama cha CUF kiliwakuwa Chama kikuu cha upinzani Bungeni. Ni chama hicho ndicho kimegawanyika na kuundwa ACT Wazalendo. Wabunge wa CUF na sasa ACT hawajawahi kuleta hoja ya kupinga ongezeko la mambo ya Muungano.

Katiba inatambua uwepo wa muungano unahitaji 2/3 (rejea bandiko IV(3). Wazanzibar kupitia 2/3 yao wangeweza kuhoji ongezeko la Mambo ya muungano ikiwa ilifanyika kinyume. Haijawahi kuhojiwa

Ni kwa mantiki nzima ya uandikaji wa Katiba na ushiriki wa Wazanzibar ndani ya Bunge Maalumu la Katiba na Bunge la JMT , kinachosemwa kimeongezwa kwa siri 'kinyemela' si kweli.

Ni hoja inayojengwa kuwapumbaza watu kwa malengo binafsi. Ni hoja inayosemwa na Chama cha ACT Wazalendo bila msingi wowote. Inasikitisha upotoshaji huo unafanywa na Viongozi ima kwa kukusudia au kutojua , lengo likiwa kuwatwika lawama Watanganyika. Ni hoja ya Kipuuzi sana isiyozingatia ukweli ikibebwa na Chama cha Siasa.

Pamoja na upuuzi wa hoja hiyo, hatuwezi kuipuuza kwasababu imeingia akilini mwa Watu hasa Wazanzibar wakiamini Tanganyika imebadili Katiba kwa siri ikiwa yenyewe na kuongeza mambo ili kuionyonya Zanzibar.

Hebu tuangalie baadhi ya mambo yaliyoongezwa ili tupate ukweli Tanganyika inafaidika na nini
1. Hali ya Hewa.
Hoja hapa ni kwamba Tanganyika inaidhulumu vipi Zanzibar kwa kuwa na Hali ya hewa kama jambo la Muungano.

2. Utafiti:
Tanganyika inanufaika na nini kupitia utafiti kama jambo la Muungano. Majuzi Zanzibar wamesaini 'MoU' na Tanzania (kituko) kuhusu madini na moja ya mambo ndani ya MoU ni utafiti. Je, Tanganyika inafaidika na nini.

3. Takwimu:
Tanganyika inafaidika vipi na Takwimu kuwa jambo la Muungano

4. Elimu ya Juu:
Zanzibar imepata chuo kikuu miaka 10 iliyopita. Wazanzibar wengi walioko madarakani sasa hivi wamesoma elimu ya Juu Tanganyika. Elimu ya Juu kuwa jambo la Muungano linainufaisha vipi Tanganyika yenye vyuo vikuu zaidi ya 10.

Hiyo ni mifano michache ya kuonyesha kwamba hoja ya kuongeza mambo ya Muungano kinyemela ili kuidhulumu Zanzibar na kuifaidisha Tanganyika kama inavyoenezwa na baadhi ya Viongozi ni ya kipuuzi sana ikilenga kuituhumu Tanganyika tu ili kujenga chuki. Chuki inayoenezwa na ACT Wazalendo ni 'exploitations' ya ignorance ya watu.

HITIMISHO
Katiba ya JMT ya Mwaka 1977 iliandikwa na Kamati iliyowashirikisha Wajumbe kutoka Zanzibar, ilisimamiwa na Mwenyekiti kutoka Zanzibar, iliandika orodha ya mambo ya Muungano na mambo hayo yaliafikiwa na Bunge Maalumu la Katiba lililokuwa na Wazanzibar.

Uwakilishi wa Zanzibar upo na haujawahi kuhoji kwa taratibu za kisheria isipokuwa kuongelea vichochoroni.
Na kwamba hakuna unyemela wowote uliofanyika.

Kwamba, mambo yaliyoongezwa yanaifaidisha Zanzibar na hayana manufaa yoyote kwa Tanganyika.
Kwamba, Wazanzibar wanaweza kutumia Baraza la Wawakilishi kuyaondoa mambo hayo kama walivyofanya suala la Bandari, mafuta na gesi.

Na kwamba, Wazanzibar wadai kura ya Maoni (rejea bandiko la II) waamue hatma yao.
Kwamba, ni wakati wote kwa pamoja kudai Katiba mpya itakayo tofautisha kwa uwazi ya Tanganyika na ya Zanzibar

Sehemu inayofuata tutajadili 'Kamati ya pamoja ya Fedha' ya JMT

Inaendelea...
 
VI

AKAUNTI YA PAMOJA NA TUME YA PAMOJA YA FEDHA

Moja ya malalamiko ya 'uonevu' wa Muungano yanayotolewa na Wazanzibar kupitia chama cha ACT Wazalendo ni kutofanya kazi kwa Akaunti ya Pamoja ya Fedha kati ya Serikali Mbili yaani JMT na SMZ

Tume ya pamoja na akaunti vimetajwa Katika Katiba ya JMT 1977 Sura ya Saba na vifungu vinavyofuata

Akaunti ni sehemu ya Mfuko mkuu wa Hazina ya JMT inayochangwa na Serikali Mbili kwa shughuli za Mambo yanayohusu Muungano. Katiba inaeleza uwepo wa Tume ya Fedha itakayokuwa na Wajumbe wasiozidi Saba watakaochaguliwa na Rais wa JMT.

Katiba ya SMZ 1984 Toleo 2010 Sura ya Kumi na Moja (124)(1)(b) inatambua uwepo wa Akaunti na Tume ya Pamoja.

Madai ya Wazanzibar kuhusu uwepo wa Tume ya pamoja ya Fedha na Akaunti ya pamoja ni ya kweli.

Maudhui ya madai ya Wazanzibar kuhusu Tume ya pamoja ya Fedha na akaunti ni ya Kipuuzi.
Neno Upuuzi si tusi kwa maana ya kwamba ni '' nonsense' yaani kisicho na sense au kisicholeta maana.

Kwanza, Katiba inasema akaunti itakuwa ya Serikali MBILI, ya JMT na SMZ. Hii serikali ya JMT, Zanzibar imo.

Katiba ya JMT Sura ya Tatu (64)(1) inasema mamlaka ya kutunga sheria ya mambo ya TANZANIA BARA (Tanganyika) yatakuwa chini ya BUNGE. Kwa msingi huo Katiba inatambua uwepo wa Tanganyika.

Kinachotakiwa ni Tume au akaunti kati ya Tanganyika na Zanzibar , siyo Jamhuri ya Muungano vs Zanzibar

Katiba ya JMT 1977 (34)(1) inaleta uchechefu kwa kusema '' Kutakuwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano itakayosimamia mambo ya Muungano ya Jamhuri ya Muungano na mambo mengine yahusuyo Tanzania Bara (Tanganyika). Kwa maneno mengine serikali ya JMT inasimamia Fedha za Tanganyika katika akaunti ya Pamoja.

Kujichanganya kwa Katiba na Muundo wa Muungano ni tatizo.

Kisichitambulika ni kwamba Watanganyika wangependa sana kuwa na akaunti ya Pamoja lakini hawana chombo cha kusimamia akaunti . Rais akiteua Wajumbe wasiozidi 7 anaweza kuwatea wa upande mmoja kama ambavyo Wizara ya Mawasiliano ya Tanganyika inaongozwa na Wazanzibar. Hivyo Tume inaweza kuwa na Wazanzibar 4, 5 au wote kwa kutumia madaraka ya Rais. Hata kama watateuliwa Watanganyika bado wanawajibika kwa Rais wa JMT siyo Tanganyika kwasababu Tanganyika au Tanzania Bara inayotajwa haina uongozi.

Kwa mantiki hiyo Fedha yote ya Tanganyika inakuwa ya JMT halafu ile ya Zanzibar inakuwa ya Zanzibar.
Huu ndio msingi wa hoja kwamba Zanzibar hawachangii Muungano kwasababu wao tayari ni JMT.

Kwa muda mrefu akaunti ya pamoja ni kama Tanganyika haitaki kwa maelezo ya Viongozi wa Chama cha ACT.

Hakuna aliyewahi kusema kwa uwazi kwanini akaunti ya pamoja haifanyi kazi.

Ukimya huo ukatumiwa kuwapumbuza watu hadi Tarehe 11 December 2021 ambapo Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hussein A .Mwinyi alikaririwa na gazeti la Mwananchi alipoulizwa kwanini akaunti haifanyi kazi akajibu hivi:

'' Suala la akaunti lina ugumu kulitekeleza, akaendelea kusema ' Kodi za TRA zinazokusanywa Zanzibar zinabaki Zanzibar. Kukiwa na akaunti ya pamoja itabaidi Zanzibar na Tanganyika zichangie kama sheria inavyosema kisha Fedha zigawanywe baada ya kuondoa matumizi kama ya Jeshi. Rais Mwinyi akasema hilo litakuwa gumu kwa Zanzibar''

Rais Mwinyi amemaliza utata wa kipuuzi wa siku nyingi kwamba Zanzibar inachangia Muungano kupitia TRA .

Mwinyi kasema pesa za TRA zinabaki Zanzibar akithibitisha kauli ya Gavana wa Bank Kuu ya Tanzania wakati huo Marhumu Beno Ndulu aliyesema ni takribani miaka 30 Zanzibar haichangii Muungano.

Tanzama link ya gazeti la Mwananchi hapa chini

Kwa kauli ya Rais Mwinyi, Tanganyika inatamani sana akaunti ya pamoja kwasababu hadi sasa Taasisi za Muungano ikiwemo mishahara ya Wabunge wa Zanzibar wanaokaa Dodoma kujadili yasiyowahusu inatoka Hazina Dar es Salaam kama kodi za Watanganyika.

Tunahitimisha hoja hii kwa kusema , matatizo ya Katiba kutoitambua Tanganyika kwa muundo rasmi yanaleta tatizo kubwa sana na kutishia Muungano. Uwepo wa Serikali ya Tanganyika utawaleta Wabia mezani kila mmoja akiwa na kitu na si kama ilivyo sasa ambapo kodi za Tanganyika zipo mezani Zanzibar wakililia kugawana tu.

Akaunti ya pamoja itasaidia sana kumaliza utata wa namna gani Muungano uhudumiwe.
Zanzibar watachangia kwa ukubwa wao, Tanganyika watachangia kwa ukubwa wao na mgawanyo utafanywa kuzingatia hayo kama kipo cha kugawana kwa maana kwamba gharama za Muungano zitaondolewa kwanza.

Ni kwa msingi huo hoja ya ACT Wazalendo ya akaunti ya pamoja ni nzuri, malalamiko kwamba Tanganyika inanufaika ni ya kipuuzi. ACT wanapaswa kueleza akaunti ya pamoja inachangiwajwe na inagawanywa vipi na gharama za Muungano zinabebwa vipi. Siyo suala la kugawana tu kuna kuwajibika pia

Bandiko lijalo tutaangalia Katiba na Taasisi za Muungano kama kuna umuhimu wa kuwepo

Inaendelea...
 
VII
TAASISI ZA MUUNGANO

Turejee bandiko VI juu, Rais H.A ametoa ushahidi kwamba kodi zinazokusanywa na TRA Zanzibar zinabaki huKo na hivyo hakuna Mchango wa Zanzibar Hazina Kuu Dar es Salaam.
Hazina kuu ndiyo itoayo pesa za kuendesha Taasisi za Muungano kama Wizara ya Ulinzi, Mambo ya ndani, nje n.K

Moja ya kero za Wazanzibar ni kile wanachodai kutoruhusiwa kuingiza bidhaa kutoka Zanzibar bila kulipia kodi za TRA.
Wazanzibar wanasema '' ikiwa sisi ni nchi moja' kwanini bidhaa za Zanzibar zinatozwa tena kodi.

Katika Mafao Wazanzibar huukubali Utanzania, kinyume chake ni Wazanzibar na Tanganyika ni nchi jirani.
Ikiwa 'sisi ni nchi moja' iweje Leseni ya udereva tu ya Tanganyika haitambuliki Zanzibar?

Kuingiza bidhaa Tanganyika bila kulipia kodi ni kero iliyotatuliwa na VP Philipo Mpango.

Kuingiza bidhaa kutokea Zanzibar ni hasara, kodi inayokusanywa Zanzibar haifiki Hazina Dar es Salaam.

Kwa mantiki Zanzibar inatumia muungano kama uchochoro wa kuingiza bidhaa hafifu au kodi ndogo kwa kujua zitaingia Tanganyika bila kodi. Gharama zitalipwa na Mtanganyika pale TRA inapokosa vyanzo .

Bidhaa hafifu zinaweza kupenya kwasababu Tanzania Bureau of Standard haina mamlaka Zanzibar. Huko kuna Zanzibar Bureau of standards (ZBS). Ikiwa ni nchi moja tofauti hizi zinatoka wapi? Lakini ZBS wanataka bidhaa zikikaguliwa Zanzibar ziingie Tanganyika bila ukaguzi wa TBS. Hii si kwamba ni hasara bali ni hatari

Kero nyingine ya kitaasisi ni kugawana misaada ya nje. Kwamba Zanzibar ipewe sehemu yake , kinachobaki ni cha Tanganyika na kitatumika kuhudumia Tanganyika na Taasisi za Muungano kama Wabunge kutoka Zanzibar, Wizara za Muungano na mamlaka au mashirika ya Muungano.

Kwa vile ZRA haileti mapato Hazina, kwanini Watanganyika waendelelee kuwalipa Wabunge wa nchi ya Zbar?

Mfano, kila sh 100 , Zanzibar ina 1/3 ni sawa na sh 33.3 . Shilingi 66.7 ni za Tanganyika na Taasisi za Muungano.

Kero nyingine ni ajira za Taasisi za Muungano. Imeamuliwa Zanzibar ipewe 21% ya ajira za Muungano kwa maana mambo ya Muungano yakiwemo yale yanayolalamikiwa na Wazanzibar yasiyo ya Muungano.
Mfano mzuri ni wa hivi karibuni ambapo Mzanzibar aliajiriwa kama Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika.

Mawasiliano na uchukuzi si jambo la muungano kwa mujibu wa katiba lakini inaongozwa na ina ajiri Wazanzibar kama ilivyo kwa wizara za kilimo, mifugo, utalii , Afya, Tamisemi, madini n.k.

Wakati Wazanzibar wakipewa 21% hakuna mahali SMZ inawajibika kulipa mishahara , marupu rupu na mafao ya Wafanyakazi hao (21%)wa Muungano. Kwa maneno mengine Zanzibar wanapewa haki Tanganyika inabeba Wajibu.
1. Kunyima fursa kwa vijana wa Tanganyika ambao hawana fursa hiyo Zanzibar
2. Kulipia ajira zinazotolewa mahususi kwa Wazanzibar na si Utanzania kama kijana wa Kigoma au Mtwara.
3. Kupata Watumishi 'incompetent' kwasababu hawana interview isipokuwa Uzanzibar kama kigezo

Katika Taasisi zinazoshangaza ni Bunge. Kwamba Katiba imeanisha wazi uwepo wa mambo ya Tanganyika.

Ilitegemewa Bunge kujadili mambo ya Muungano kisha Wabunge wa Zanzibar waondoke ili lijadili mambo ya Tanganyika. Hii ni kwa mujibu wa Katiba . Kuwaondoa Wabunge wa Zanzibar kutasaidia mambo mawili

1. Idadi ya takribani 80 ni kubwa kwa kulipiwa gharama kama Wabunge. Kukaa Dodoma kwa mambo yasiyohusu Muungano au kushiriki Kamati za mambo ya Tanganyika ni kumuongezea gharama mlipa kodi wa Tanganyika. Hakuna sababu za Wabunge hao kukaa mathalani miezi 2 katika Bunge la Bajeti bila kazi yoyte.

Taasisi nyingine ni ya elimu ya juu ambayo hutoa Mikopo kwa Wanafunzi.
Kuna HESLB ya Tanzania kwa Vijana wote halafu ZHESL ya Zanzibar kwa ajili ya Vijana wa Zanzibar tu.
Uwepo wa vijana wa Zanzibar katika HESLB unaongeza 'strain of resources'.

Kuna Vijana wa Tanganyika watakosa mikopo ili fungu maalumu lielekezwa kwa Vijana wa Zanzibar wenye fursa mara mbili HESLB na ZHSELB kwa 'special treatment'

Pesa za HESLB zinatoka mfuko wa Hazina Dar na ushahidi wa Rais Mwinyi ni kwamba Zanzibar haichangii.
HESLB ni zao la kodi za Watanganyika kwa Vijana wao kama ilivyo ZRA na Vijana wa Zanzibar

Taasisi nyingine ni Wizara ya Mambo ya nje. Kero za Wazanzibar ni teuzi za Mabalozi zizingatie uwiano kwamba iwepo idadi maalumu ya Mabalozi kutoka Zanzibar. Gharama za Balozi zinatoka Hazina Dar es Salaam.

Kwamba Zanzibar inataka nafasi lakini mchango wa kuendesha Balozi unabaki mzigo wa Tanganyika.

Tutaendelea kufanya tathmini ya Taasisi ,

HITIMISHO
Kwa vile mambo ya Tanzania Bara (Tanganyika) hayapo wazi, kila cha Tanganyika ni mali ya Muungano.

Kuna ushahidi wa Rais wa Zanzibar kwamba haichangii kuendesha Muungano.
Hii ina maana kwamba mzigo wa kuendesha Muungano umebebwa na Mlipa kodi wa Mtanganyika.

Wakati hilo likitokea Zanzibar imechukua fursa ya kutumia jina la Muungano kutafuta fursa. Mfano, kuna Wabunge, HESLB, Balozi, 21% ya ajira za muungano ni maeneo yanaytoa ajira kwa Wazanzibar bila kuwa na mchango wowote Hazina, kwa mujibu wa Rais Mwinyi.

Hii ina maana Tanganyika inatoa soko la bidhaa na ajira kwa Wazanzibar lakini hawawajibiki kuendesha shughuli za Taasisi husika au Muungano. Kuna umuhimu wa kuwa na Akaunti ya pamoja ya Fedha Zanzibar ionekane inachangia nini kwa uwazi na si inataka nini.

Ni muhimu kutenga yasiyo ya Muungano ili Watanganyika wawe na serikali itakayosimamia mambo yao

Yote hayo yanawezekana pale tu Kura ya maoni kwa Zanzibar ili kuamua ikiwa Muungano unahitajika
Ikitokea kukubali kura ya maoni ita 'define' aina ya Muungano utakaokuwa na Washirika wakiwajbika, wakiwa na haki sawa na wakiwa na fursa sawa bila utegemezi.

Inaendelea .....


Allen Kilewella
 
VIII

KATIBA ' MBILI ' KATIKA NCHI MOJA

Ipo hoja kwamba Tanzania mbele ya uso wa Dunia ni nchi moja , Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Katiba ya 1977 sehemu ya kwanza (1) inasema '' Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano'
Katiba ya Zanzibar 1984 toleo 2010 inasema '' Zanzibar ni miongoni mwa nchi Mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwanza, Zanzibar imeshajitanabahisha kuwa ni Nchi. Pili, Katiba inasema 'ni miongoni mwa nchi mbili''
Haijulikani nchi hizo ni Zanzibar na Tanganyika au Zanzibar na Tanzania.

Kwa utata huo pengine ndiyo sababu iliyopelekea Rais SSH kuagiza Wizara ya madini ya Tanzania kuingia makubaliano (MoU) na Wizara ya madini ya Zanzibar, tukio la Kwanza tangu kuundwa Muungano 1964

Kuna sababu ya kuamini nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano ni '' Tanzania na Zanzibar''.
Ingalikuwa sivyo, vipi chi mbili ndani ya nchi moja zinaingia MoU?

Kuna utata ulioifanya Tanganyika iwe Tanzania na ni Jamhuri ya Muungano ikiwa haina uwezo wa kuamua mambo yake, ikiwa inatumia rasilimali zake katika muungano, ikitumiwa na nchi ya Zanzibar kinyume na malengo ya Muungano ''abuse'

Kugawa Mikoa na Wilaya:
Katiba ya JMT 1977 sehemu ya Kwanza (2) inampa madaraka Rais wa Jamhuri ya Muungano kugawa Jamhuri ya Muungano katika Mikoa, Wilaya na maeneo mengine, na kwa upande wa Zanzibar atashauriana kwanza na Rais wa Zanzibar

Katiba ya Zanzibar inasema ' Rais aweza kuigawa Zanzibar katika Mikoa, Wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.

Katiba ya JMT inatofautiana na ile ya Zanzibar . Kwamba kwa kuzingatia katiba ya Zanzibar, ni nchi na anayeweza kugawa maeneo ni Rais wa Zanzibar bila kushauriana na Rais wa JMT kama katiba ya JMT inavyosema. Hii inaonyesha ''UKUU' wa katiba ya Zanzibar dhidi ya ile ya JMT.

Dharau za Zanzibar dhidi ya Katiba ya JMT zinachangia haya ya Uzanzibar na Utanganyika

MAJESHI
Katiba ya JMT 1977 Sura ya Tisa (146) inasema ''Marufuku kuunda Majeshi ya ulinzi yasiyo Majeshi ya Ulinzi ya Umma'' Katiba ya Zanzibar 1984 (2010) inasema '' Baraza la Wawakilishi laweza kutunga sheria zinazofaa kwa ajili ya kuwawezesha Wananchi kutumikia katika Majeshi katika ulinzi wa Taifa'

Baraza la Wawakilishi lina uwezo upi wa kuunda Majeshi kwasababu Ulinzi ni suala la Muungano na Amir Jeshi ni mmoja tu, Rais wa JMT.


SHERIA NA MAMLAKA
Katiba ya JMT 1977 Sehemu ya Kwanza (3) inatoa mamlaka ya Rais kwa mambo yote ya Muungano ndani ya Jamhuri ya Muungano. Bunge limepewa uwezo wa kutunga sheria kwa mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano. Rejea bandiko II kuhusu uwakilishi wa Zanzibar ndani ya Bunge la Tanzania.

Kuna Wabunge wa kuchaguliwa, wa Viti Maalum, kutoka Baraza la Wawakilishi na wa kuteuliwa na Rais.
Wote wapo Bungeni Dodoma kwa ajili ya masilahi ya Zanzibar .

Katiba ya Zanzibar 1984 toleo 2010 Sura ya Kumi na Tatu (132) inasema hakuna sheria yoyote itakayopitishwa na Bunge la Muungano itakayotumika Zanzibar mpaka sheria hiyo iwe ya mambo ya Muungano iliyopitishwa kwa kufuata vifungu vya Katiba ya Muungano.

Ibara ya (2) inasema sheria hiyo haitatumika hadi kwanza ipelekwe Baraza la Wawakilishi na Waziri husika

Hoja: Kuna dharau Katiba ya Muungano na Bunge na kuipa Katiba ya Zanzibar ukuu kuliko katiba ya JMT.
Bunge la Tanzania lina wawakilishi (Wabunge) kutoka Zanzibar tena likiwa na Wabunge mahususi 5 wanaotoka Baraza la Wawakilishi.

Sheria zinazotungwa na Bunge la Muungano zinapitishwa kwanza na Wabunge wa Zanzibar , halafu zina baraka kutoka Baraza la Wawakilishi kupitia Wabunge 5. Sheria hizo hupitia Kamati za Bunge zenye Wazanzibar.

Kitendo cha Katiba ya Zanzibar kutaka sheria iliyotungwa na Bunge isitumike kwanza Zanzibar ni kudhalilisha Katiba ya Muungano inayotoa mamlaka kwa Bunge na Rais kutekeleza majukumu ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano.

Pili, kutaka sheria ipelekwe Baraza la Wawakilishi kinatueleza jambo moja, kwamba Wabunge wa Zanzibar katika Bunge la Tanzania hawana kazi au hawana uwezo au hawafikri vizuri kiasi kwamba hawaaminiwi kwa maamuzi hadi sheria ipitie Baraza la Wawakilishi. Ikiwa ni hivyo ipi ni sababu ya Zanzibar kuwa na Wabunge 80 kwa gharama za Hazina Tanganyika tukielewa Wabunge hao ima hawaaminiwi na Wazanzibar au ni Wabunge dhalili kuliko wale wa Baraza la Wawakilishi.

Kama Wazanzibar imani na Wabunge kutoka Zanzibar kwanini liwe tatizo la kuidharau katiba ya JMT iliyotungwa na Wazanzibar wakishiriki? Kuleta Wabunge wasio aminiwa na Wazanzibar wenyewe halipaswi tatizo ya Muungano la kudhalilisha Katiba ya JMT.

Inaendelea
 
IX

WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO
'WAZIRI KIONGOZI WA SMZ'

Katiba ya Jamhuri ya Mungano 1977 k'Katiba ya JMT' Sura ya Tatu (51) (1) na kuendelea inamtambua Waziri Mkuu (PM) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, uteuzi, kuthibitishwa na majukumu yake.

Majukumu ya PM ni kusimamia shughuli za kila siku za Serikali, na ni kiongozi wa Serikali Bungeni.
Pia atatekeleza majukumu mengine kama atakavyoagizwa na Rais katika kuamua sera kwa ujumla

PM atawajibika kwa Rais katika kufanya maamuzi ya sera kwa ujumla na Mawaziri watawajibika chini ya PM wawapo Bungeni. Mawaziri wote watateuliwa na Rais kwa kushauriana na PM. Rais kwa kushauriana na PM atateua Naibu Mawaziri.

Baraza la Mawaziri litaongozwa na Rais na kama hayupo VP na kama hayupo ni Waziri Mkuu (PM)
Rais wa SMZ ni Mjumbe wa Baraza la Mawaziri.

Katiba ya SMZ Zanzibar ya 1984 toleo 2010 haitaji wala kumtambua Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.

Hoja:
Kwa mtazamo, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano hatambuliki Zanzibar hata kwa shughuli zilizo chini ya mamlaka ya Jamhuri ya Muungano. Zaidi, kiitifaki Waziri Mkuu hana nafasi isipokuwa tu kwa heshima lakini si kiitifaki

Kwa upande wa Tanganyika, PM ana madaraka ya kusimamia mambo ya Muungano na mambo ya Tanganyika.

Swali la kujiuliza, je ni kweli hana mamlaka Zanzibar? Je upatikanaje wake unatumia taratibu gani!

PM anateuliwa na Rais kwa vile yeye ndiye atakayeongoza na kusimamia shughuli za serikali zikiwemo sera.

Jina la PM linapelekwa Bungeni kwa ajili ya kupigiwa kura na kuidhinishwa au kukataliwa.
Kuna kura ya kutokuwa na imani naye ikitokea Bunge linaamua hivyo

Bungeni, PM atapigiwa kura na Wabunge wote wakiwemo wa Zanzibar (wa kuchaguliwa, kuteuliwa , Viti maalumu na kutoka Baraza la Wawakilishi). Hawa jumla yao ni takribani 80.

Bunge lenye Wabunge 393 ukiondoa AG wanabaki 39 na ukitoa 80 wa Zanzibar wanabaki 312 wa Tanganyika

Wabunge 312 wa Tanganyika wanaomtegemea PM kama kiongozi wa serikali kwa mambo ya Muungano lakini pia mambo ya Tanganyika. PM ana nafasi kubwa sana katika kusimamia na kutekeleza sera za Tanganyika.

Uchaguzi wa PM Bungeni unahusu Tanganyika kwasababu Katiba ya Zanzibar haimtambui PM wala majukumu yake ndani ya Muungano kule Zanzibar.

Ikitokea Wabunge 312 wa Tanganyika wakafungana kwa kura (156 vs 156) kwa wanaaotaka kumthibitisha au kumkataa PM, Wabunge watakaoamua amua nani awe PM wa Jamhuri ya Muungano ni wale 80 kutoka Zanzibar

Inaweza kutokea Wabunge wa Tanganyika wakamkataa Waziri mkuu aliyepenekezwa lakini kura za Wazanzibar takribani 80 zikamthibitisha na kinyume chake pia ni ukweli.

Kwamba, anayefanya kazi za Tanganyika hatakubaliki lakini Wazanzibar wanamthibitisha Bungeni

Kwa manenio mengine, Wabunge wa Zanzibar wana kura ya turufu ya kumthibitisha au kumkataa Waziri Mkuu asiyehusika wala kutambuliwa na katiba ya Zanzibar.

Wabunge wa Zanzibar wa kuchaguliwa kwa idadi jumla ya 50 wanachaguliwa na Wananchi wachache kuliko Wabunge 3 wa majimbo ya Dar es Salaam.

Wabunge 50 wa Zanzibar anaoweza kuamua nani awe au asiwe Waziri Mkuu wa Tanzania mwenye mamlaka Tanganyika na si Zanzibar wanachaguliwa na idadi ya Wananchi sawa na Wananchi wa majimbo 3 ya uchaguzi Dar es slaam.

Lakini pia si kweli kwamba PM hana mamlaka Zanzibar. Ikiwa Rais na Makamo wake hawapo , kikao cha Baraza la Mawaziri ambacho Rais wa Zanzibar ni mjumbe kitaendeshwa na Waziri Mkuu asiyetambulika Zanzibar lakini mwenye kauli juu ya mambo ya Muungano kwasababu Mawaziri wote wapo chini yake.

Katiba ya 1977 haiweki wazi Waziri Mkuu anayetajwa ni wa Tanganyika au ni wa Jamhuri ya Muungano.

Ikiwa ni wa Jamhuri ya Muungano mbona Katiba ya Zanzibar haimtambui na anawezaje kutekeleza majukumu hayo akiwa Zanzibar?.

Ingawa katiba inasema majukumu ya Muungano yatatekelezwa kwa sheria za mambo ya Muungano, Waziri mkuu hana nafasi ya kumsimamia mtu au sera yoyote Zanzibar.

PM anabaki kuwa na kauli ndani ya Baraza la Mawaziri tena akiwa na mamlaka makubwa kuliko Rais wa Zanzibar.

KiUtendaji ni Waziri Mkuu wa Tanganyika anayesimamia mambo ya Muungano kwa 'remote' kule Visiwani lakini anachaguliwa na Wazanzibar Bungeni ambao kura yao inaweza kumthibitisha au kumkataa tena wakiwa na Wapiga kura wachache.

Je, bado tunaamini hatuhitaji katiba ili ku 'streamline' haya mambo?

Itaendelea
 
X

HAZINA YA FEDHA- DAR RES SALAAM

Zanzibar kupitia Baraza la Wawakilishi waliondoa mafuta na gesi wakidai hayakuwa mambo ya Muungano na yaliongezwa kinyemela ( Upotoshaji, Wazanzibar wana uwakilishi na walishiriki kuandika katikba 1977)

Waliondoa pia Bandari katika mazingira hayo hayo licha ya kwamba yalikuwa mambo ya Muungano

Kuondoa mambo yasiyo ya Muungano si tatizo, lengo la Zanzibar ni kutaka rasilimali zake zitumike kwa ajili ya Wazanzibar. Mapato ya gesi na Mafuta kama yatakuwepo pamoja na Bandari za Zanzibar yataingia mfuko wa Hazina Zanzibar ambao hauna uhusiano wowote na suala la Muungano.

Katika mambo yenye gharama kama Ulinzi na usalama, Mambo ya ndani na nje na taasisi za Muungano kama Elimu ya juu hutawasikia Wazanzibar wakidai kuyaondoa katika Muungano. Elimu ya Juu si suala la Muungano , ingalitarajiwa waliondoe, hawawezi kuondoa Elimu ya Juu kwasababu kwao ina manufaa mengi.

Suala la Bandari limeibua hisia kwa Watanganyika si kwasababu wanahitaji bandari za Zanzibar.

Hisi ni namna Zanzibar imekuwa na dharau katiba ya Muungano.

Watanganyika wanajiuliza, je, kama DP World wangetoa Dollar milioni 40 kwa ajili ya kuimarisha Bandari za Tanzania, Wazanzibar wangekaa kimya?

Jibu ni hapana wangedai wapewe kwasababu ni msaada wa Jamhuri ya Muungano.
Mkataba wa Bandari unahusu bandari za Tanzania katika hilo Wazanzibar wanasema Bandari haiwahusu

Swali ni je, bandari , madini , mafuta na gesi za Tanganyika haziwahusu Wazanzibar?

Wakati Zanzibar ina Hazina yake ya fedha, Hazina ya fedha za Tanganyika inaitwa Hazina ya Tanzania.

Kwamba Tanganyika haina Hazina isipokuwa Hazina iliyopo inachanganya fedha za Muungano (ambazo Zanzibar haichangii kwa mujibu wa Rais Mwinyi, H) na Fedha za Tanganyika.

Mauzo ya madini, mazao ya Kilimo na mifgo, Utalii , Bandari yanaingia Hazina kuu Dar es Salaam.

Wiki hii bandari ya Dar es Salaam imepewa hati kwa mchango wake HAZINA YA DAR ES SALAAM

Hazina ya Dar es Salaam ndiyo inayotoa fedha zote za kuhudumia Muungano pamoja na ruzuku ya bajeti ya SMZ, na Gawiwo la 4.5% kupitia BoT bila kusahahu gharama kubwa ya Wabunge kutoka Zanzibar.

Hizi ni fedha na kodi za Tanganyika zinazotumika katika kuendesha shughuli za Muungano ikiwemo mambo yasiyo ya Muungano kama Afya na Elimu ambayo Mzanzibar anayeishi Tanganyika anapata kama Mtanganyika.

Ni kupitia HAZINA ya Dar es Salaam kila rasilimali ya Tanganyika inageuka kuwa rasilimali ya Muungano ambayo Wazanzibar wana haki . Rasilimali za Zanzibar zinabaki kuwa za kwao na Mtanganyika hana haki

Ni Upumbavu na ni wale wasio na elimu wanaosema 'KOTI' la Muungano linainufaisha Tanganyika.

Kinyume chake koti la Muungano linaidhoifisha Tanganyika kwasababu inatumia rasilimali zake kuendeleza maeneo yasiyochangia ukuaji wa pato la Tanganyika.

Mfano, Mkoa wa Mwanza ni wa Pili kwa kuchangia GDP lakini unapata rasilimali kidogo ukilinganisha na Zanzibar.

Katika hali hii hakuna njia ya mbadala ya kurekebisha hali isipokuwa kuwa na Katiba, na Wazanzibar waulizwe kwanza ikiwa wanautaka Muungano kama tulivyoonyesha Scotland, Timor, Eritrea na Quebec

Itaendelea
 
XI

'COUNTRY CODE NUMBER'' NA TUME YA MAWASILIANO

Posta na Simu ni jambo la muungano tangua ulipoasisiwa kwa kuzingatia usalama.
Mawasiliano ni sehemu za ulinzi na usalama wa nchi hasa zama za ujamaa na mawasiliano hafifu za 60S, 70s, 80s.

Umuhimu wa shirika la Posta si kwa Tanzania tu, katika nchi ya Marekani Posta ni shirika lililotajwa katika katiba kwa uanzishwaji na uendeshwaji wake. Uteuzi wa Viongozi na Wajumbe wa Bodi ni wa kipekee.

Kwa Tanzania, kama nchi moja namba ya mwasiliano ya simu (country code ni 255) ikiwa ni pamoja na Zanzibar.

Hata hivyo inadaiwa kwamba Zanzibar ilikuwa na country code ambayo haijatumika kwasababu ya ''Muungano''

Soko huria zimelamzimisha kuanzishwa kwa mamlaka ya mawasiliano( TCRA) ili kuratibu taratibu za mawasiliano

Katika siku za karibuni Wazanzibar wamedai country code yao kama sehemu ya kuifanya Nchi na mamlaka yake.

Hoja kubwa ni kwamba TCRA inakusanya pesa lakini Zanzibar haifaidiki hata kama kuna simu za Wazanzibar kutoka nje ya nchi. Wazanzibar wakadai wapewe mgao wa pesa kutoka TCRA. Kero hiyo ikakubaliwa

Ipo kampuni iliyokuja Zanzibar kuboresha mawasiliano ya simu na kuacha utegemezi wa makampuni ya Tanganyika. Kutokana na idadi ya wateja na ukubwa wa soko la Tanganyika kampuni ikalazimika kuhamia Tanganyika.

Mtandao wa TCRA unaonyesha uwepo wa makampuni ya simu 6 makuba yenye watumiaji Takribani Milioni 64.

Mkoa uliosajili Wananchi wachache kwa Tanganyika ni Katavi ambao ni 662, 521.
Idadi ya Usajili wa watumiaji kwa Unguja na Pemba ni takribani 750,000

Hii ina maana moja, kwamba, idadi ya waliosajiliwa Katavi ni takribani sawa na ile ya Zanzibar

Katika hali ya kawaida , Wazanzibar wamgeshaondoa suala la mawasiliano katika mambo ya muungano
Kinyume chake TCRA ina ofisi Zanzibar kama zilivo za kanda zingine na hakuna malalamiko ya Wazanzibar

TCRA inakusanya pesa Trilioni zaidi ya 7 kwa mwaka. Katika kiwango hicho kuna sehemu Zanzibar inapewa kwasababu ni sehemu ya Muungano na kwamba Wananchi wake wanatumia mawasiliano.

Kwa hesabu za kawaida tu, mapato yanayotokana na mawasiliano kwa Tanganyika 62 Milioni haiwezi kulinganishwa na Zanzibar hata kidogo. Mawasiliano ndani ya mkoa wa Katavi yanaweza kuwianishwa na ya Zanzibar.

Ni jambo la kushangaza kwamba TCRA inatoa huduma Tanganyika lakini kila huduma inayotolewa kuna 'pesa' zinakwenda Zanzibar. Kwamba, mwamala wa fedha kutoka Kigoma kwenda Mpanda una 'senti' zinazokwenda Zanzibar. Simu , txt n.k. zote zinazofanyika katika soko la Watu milioni 62 kuna sehemu inagaiwa Zanzibar.

Mambo kama haya yanaleta sintofahamu na hayawezi kueleweka kwa urahisi hasa kwa Watanganyika.

Tutengeneze mfumo ambao Zanzibar watakuwa na mamlaka zao na country code yao, halafu tuwasiliane kama tunavyofanya na nchi nyingine. Kukusanya pesa kwa mawasiliano ndani ya Tanganyika si kuwatendea haki Watanganyika. Haya hayasemwi kwasababu ya Tanganyika ni kawaida, ikitokea Zanzibar ni kero

Tunahitaji mfumo mpya, wa sasa una matundu mengin yasiyo shoneka

Inaendelea
 
XII

MFUKO MKUU WA HAZINA , WAZANZIBAR KUKOPA

Katiba ya JMT 1977 Sehemu ya kwanza (133) inasema serikali ya JMT itatunza akaunti ya pamoja itakayoitwa '' akauti ya fedha ya pamoja'' ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na itakuwa SEHEMU ya Mfuko Mkuu wa Hazina ya JMT.
kaunti ya pamoja itaweka fedha zitakazochangwa na SERIKALI MBILI.

HOJA
Akaunti ya Pamoja ya fedha itakayoendeshwa na Tume ya pamoja ya watu wasiozidi 7 ni pi?

Rais wa Zanzibar Mh Hussein Mwinyi kasema fedha zinazokusanywa na TRA zinabaki Zanzibar kwa matumizi ya huko.

Gavana wa BoT Marhumu Beno Ndullu alisema '' Hakuna rekodi ya Zanzibar kuchangia Muungano kwa miongo zaidi ya miwili' yaani miaka zaidi ya 30.

Bajeti ya SMZ haina sehemu ya fungu linaloonyesha kutoa fedha kwa ajili ya akaunti ya pamoja ya Fedha.

Kwa maneno mengine hii akaunti ya pamoja ya fedha ya Jamhuri ya Muungano ni ya fedha za Tanganyika na itakuwa sehemu ya Mfuko wa Hazina Kuu ya Tanganyika. Yote yanafanyika kwa jina la JMT.

Hakuna mfuko wa JMT wala Hazina ya JMT bali Mfuko wa Tanganyika na Hazina ya Tanganyika.

Jambo la pili linaloshangaza ni katiba inaposema ''fedha zitakazochangwa na serikali mbili''
Yaani Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Kama kuna mambo ya kupumbaza ni kudhani kuwa Tanzania ni nchi tofauti iliyoungana na nchi ya Zanzibar na sasa wana mfuko wa Pamoja. Mtu aliyeandika hili, na wale walikubali ni watu wa ajabu sana.

Tanzania ina Zanzibar na ndiyo JMT na haiwezi kuungana na Zanzibar.

Ibara ya (141)(1) inasema Deni la Taifa litadhaminiwa na mfuko wa mkuu wa Hazina wa Serikali ya JMT.
Fedha za Tanganyika katika mfuko Mkuu wa Hazina kwa jina ya fedha za JMT ndizo zinalipa Deni la Taifa.

Madeni ni ya ndani na nje , pia mishahara na maTumizi ya Wizara na Taasisi za Muungano.

Deni la Mishahara ya 21% ya Wafanyakazi kutoka Zanzibar yanalipwa na Mfuko Mkuu wa Hazina uliobatizwa jina la Mfuko Mkuu wa JMT. Lengo la Kuwa na akaunti ya Pamoja ni kugawana mapato na matumizi ya JMT.

Upo ushahidi usio na shaka wa Zanzibar kutochangia Muungano, Mfuko Mkuu wa Hazina wa JMT unabaki kuchangiwa na Tanganyika lakini kuna Wajumbe Wasiozidi Saba wakiwemo Wazanzibar wanaogawa pesa hizo kwa JMT na Zanzibar halafu madeni yanalipwa na JMT.

Kama hili halitoshi kumtia mtu wazimu, sijui kipi kilchobaki

Kwa Muda mrefu Makamo wa Rais wa Zanzibar Bw Othman Masoud Othman (OMO) na Viongozi wa ACT Wazalendo walio hai na waliotangulia mbele ya haki wanadai Zanzibar ikope bila idhini ya Jamhuri ya Muungano.

Madai haya yana ukweli kwasababu ikiwa wanakopa na Kulipa wao kwanini wazuiliwe?

Kinyume na madai ya ACT Wazalendo, wanachokitaka akina OMO ni Zanzibar kwenda kukopa yenyewe lakini ipewe udhamini na JMT kwa maana kwamba Mfuko mkuu wa Hazina wa Tanganyika kwa jina la Tanzania uchukue dhamana hiyo.

Kwamba, Zanzibar wakikataa kulipa, ni fedha za Tanganyika kutoka Hazina zitakazohudumia deni lao

Ndicho kilichotokea miaka michache iliyopita ambapo SMZ ilikataa kulipa Deni la Umeme la Tanesco.

Suala limekuwepo wakati wa JK hadi Magufuli, lakini limememalizwa Haraka sana na SSH kwa kuamuru deni la Zanzibar lisamehewe kwa maaana kwamba JMT kupitia mfuko wa Mkuu wa Hazina wa Tanganyika ulipe Bilioni 60 kwa matumizi ya umeme Zanzibar.

Hakuna sababu za kuzuia Wazanzibar kukopa na kulipa wenyewe bila udhamini wa Tanzania.
Kuna sababu za kuhoji kwanini Zanzibar inahitaji udhamini wa mfuko wa Hazina Tanganyika kwa jina la Tanzania

Mvurugano uliousoma hapo juu ni kwasababu Katiba iliandikwa katika nyakati tofauti, tunaposoma sasa hivi na kama yupo anayeamini bado katiba hiyo ni nzuri, anahitaji msaada wa haraka wa afya.

Bila uwepo wa Serikali ya Tanganyika hakuna namna Watanaganyika wataendelea kubeba mzigo wa Muungano.

Ni ujinga kuita mfuko Mkuu wa Hazina wa Tanganyika kwa jina la Tanzania. Ni kejeli kuteua Wajumbe kutoka Zanzibar kuwa katika Tume ya pamoja ya Fedha ili kugawa na kulipa matumizi ya Serikali ya JMT kutoka mfuko Mkuu wa Hazina Tanganyika.

Ni udanganyifu wa hali ya juu kuita madeni ya Muungano wakati mlipaji ni Tanganyika.

Ni udhalilishaji kumpa Mtanganyika gharama za madeni ya mishahara ya 21% ya Wazanzibar walioajiriwa kwa Uzanzibar tu na si sifa huku SMZ ikichangia Sifuri ( ZERO) katika Muungano .

Itaendelea
 
XIII

MUUNGANO 'FAIR AND EQUITABLE ' YAANI HAKI NA SAWA

'Fair ' ni neno la Kiingereza likieleza 'haki' na 'Equitable' ni Usawa katika haki kwa kuzingatia mantiki.
Haya ni maneno yanayosomeka kana kwamba yana maana sawa, ni kweli lakini kimantiki si kweli.

Tutafafanua maneno hayo kwa kutumia mifano ya Muungano.
Wazanzibar wanalalmika kwamba katika Muungano, Zanzibar iliingia kama nchi huru na inapaswa kuwa sawa na mshirika mwenzake Tanganyika.Ni 'Fair' au haki wanachokisema Wazanzibar kwasababu ni kweli ilikuwa nchi huru iliyoungana na nchi huru nyingine. Lakini hiyo 'Fair' haitoshi bila kuwa na neno 'equitable'

Ikiwa tutasema ni Fair kwa Zanzibar kama mshirika ina maana kwamba Tanganyika na Zanzibar zitakuwa sawa katika kuchangia muungano , kugawana mapato, mikopo na Misaada. Lakini je, hiyo itakuwa ' equitable' ?

Uchumi wa Zanzibar ni mdogo ziaidi ya mara 20 ya Uchumi wa Tanganyika. Kama tulivyoeleza awali, mfano wa Bajeti ya Zanzibar kulingana na Bajeti ya Wizara ya ulinzi inaeleza jambo.

Ikiwa kutakuwa na fairness basi nusu ya Bajeti ya Zanzibar sawa na 1.4Trilioni itakwenda Wizara ya Ulinzi peke yake.

Zanzibar ina eneo dogo na watu wachache kiasi kwamba huenda kwa upande wa Ulinzi wanahitaji Brigade moja tu.

Kusema Zanzibar ilipe nusu ni 'Fair ' haki lakini hakuna usawa kwa kuzingatia mantiki ' Equitable'

SMZ Zanzibar inaajjiri watumishi takribani 12,000 wakitoka katika idadi ya watu 1.5Milioni.

Wazanzibar ndani ya Muungano wanataka 21% ya ajira za Muungano. Ikiwa , kwa mfano tu, ajira za Muungano ni 100,000 Zanzibar wanapata 21,000 ya Watumishi. Kwamba Wazanzibar wanapata ajira nyingi kuliko kule Zanzibar wakati huo huo wakidai usawa na Haki. Lakini je, hao 21,000 wanalipwa mishahara na SMZ? Jibu ni Hapana

Hakuna ' fair and equitable' kwa Zanzibar kuleta watumishi halafu mzigo wa kuwalipa ubebewa na Tanganyika

Kupata ajira za Muungano ni 'Fair', kupewa 21% ya ajira siyo 'equitable' na kwa Tanganyika siyo Fair wala Equitable.

Tanganyika kubeba gharama za Muungano peke yake na Zanzibar kutochangia siyo fair wala Equitable

Kufanya Fedha za Tanganyika ni za Tanzania na kuzipeleka katika shughuli Zanzibar siyo Fair wala Equitable

Kutafuta kero za Wazanzibar bila kuwasikiliza Watanganyika siyo fair au equitable

Kutowapa Watanganyika Serikali inayosimamia rasilimali zake ni kutokuwa 'Fair and Equitable''
kwamba hakuna haki wala usawa wa mantiki.

Kuchukua rasilimali za Tanganyika na kuzifanya za Muungano halafu kuziundia kamati wakiwemo Wazanzibar kugawana mapato yake siyo 'fair au equitable'

Hoja hapa ni kwamba hii dhana ya Chama cha ACT na baadhi ya Wazanzibar wakitaka ' Haki na Usawa' katika mUungano ina maana , kwa bahati mbaya haizingatii mantiki.

Haiwezekani upande mmoja ukadai kutotendewa 'fairness and equitable' lakini upande huo huo uki practice the same.

Tanganyika ipewe serikali yake kama Zanzibar halafu kuwe na 'fair and equitable' kwa maana haki na usawa uangaliwe kwa mantiki. Huwezi kufanya upande mmoja ubebe mwingine halafu ukabaki na 'fairness and equitable'

Hivyo, Wazanzibar wanaohubiri 'fair and equitable' wajielimishe kwanza kuhusu mantiki za hayo, kwasababu haki si kutendewa abali kutenda kwa mwingine. Tanganyika inahitaji sana 'fair and equitable' lakini kwanza iwepo

Inaendelea ....
 
XIV
'' HE WHO PAYS THE PIPER CALLS THE TUNE''
ANAYEMLIA MPIGA ZUMARI NDIYE ACHAGUAYE NYIMBO

Bandiko XIII lina dhana ya 'Fair and Equitable' inayotumiwa na Wazanzibar kwa maana ya 'Haki na Usawa'

Haki na Usawa haviji bali kwa vitendo na kuwajibika. Haki haisimami kwa mtendewa bali pia kwa Mtenda.

Ili kuwe na haki na usawa ni lazima Wazanzibar waishi kauli zao ' Walk the talk' wakimaanisha wanachokisema na kukisimamia kwa vitendo.

Ukimya wa Watanganyika haina maana wameridhika, bali 'hawana pa kusemea'
Wao ni Tanzania kila kilicho chao ni cha Tanzania. Wamevaa 'kot izito la Muungano, lenye makorokoro wakiwemo chawa, kupe n.k '' Ni wapumbavu na wajinga peke yao wanaodhani koti la Muungano ni jema!

Katika kujenga usawa wanaousema Wazanzibar na katika kusimama na dhana ya 'walk the talk' ni wakati sasa ;

1. Wachukue dhamana ya kuchangia muungano kwa vitendo na rasilimali si kwa maneno matupu kwa dhana ya 'fair and equitable', lakini pia Zanzibar isiwe inferior katika muungano. who pays the piper calls the tune.

2. Haakuna sababu ya kuwa na akaunti ya pamoja ya fedha au Tume ya pamoja ya fedha kugawana fedha za Tanganyika. Uwepo wa akaunti ni pamoja na kuchangia na kugawana kilichopo. Tume na akaunti ya nini ikiwa mchangiaji ni Tanganyika peke yake. Si 'fair and equitable ' kwa Rais kuteua watu 7 wakiwemo Wazanzibar kugawana kilichochangwa na Tanganyika kwa mlango wa akauti ya pamoja.

Tanganyika kubeba mzigo wa Muungano siyo 'fair and equitable' , Zanzibar ionekane katika kuwajibika si ionekane katika fursa na faida za Muungano pekee. Gharama za Muungano zigawanywe ili Zanzibar iwe mshiriki wa maana.

3. Wazanzibar wawajibike kwa mambo yanayowahusu. Wabunge wa Zanzibar wanakuja Dodoma na wana haki ya kura za mambo ya muungano na yasiyo ya Muungano. Wana haki ya kura 2/3 kuzuia jambo hata lenye manufaa kwa Tanganyika. Wanaamua mambo ya Tanganyika yasiyowahusu wakisema hivyo kama hili la Bandari.

Ni kwa muktadha huo, Wabunge wa Zanzibar walipwe mishahara na mafao yao na SMZ kutoka kodi za Wazanzibar
Siyo fair and equitable , Wabunge wanaokuja kwa ajili ya Zanzibar kulipwa gharama kwa kodi za Tanganyika.

SMZ ilipe Wabunge wa Zanzibar kutimiza dhana ya 'walk the talk' ya 'fair and equitable'
Bila hivyo Wabunge hao wasilalamike kwa lolote kwasababu 'who pays the piper calls the tune'.

Tanganyika

4. Wazanzibar wasiishi kuomba fursa tu lazima pia wawajibike katika fursa hizo.
Asilimia 21 ya ajira wanazopewa za Tanzania zikiwemo zile zisizo za Muungano ni ' fair but not equitable'

Watu milioni 1.5 kupewa asilimia 21 na watu milioni 60 kupewa asilimia 79 hakuna 'fair and equitable'.

Kiuhalisia Wazanzibar wanaopewa 21% pia wana fursa ya 79% za Watanganyika kwa jina la Tanzania.

Huku si kuwatendea haki Watanganyika. Wazanzibar wajiulize 'fair and equitable wanayoihubiri' ni ipi hiyo?

21% ya ajira wanazodai 'fair' zinalipwa na kodi za Tanganyika 'unfair'. Hkuna 'fair and equitable' kwa kigezo chochote.

Muungano uwepo au la, 21% ya ajira zinazokwenda Zanzibar zitabaki Tanganyika. Taasisi zinazoitwa za Muungano ni Taasisi za Tanganyika. 21% inayotolewa inawanyima fursa zinazotpatikana nchi ni mwao Tanganyika.
Zanzibar wana upendeleo maalumu wa nafasi kwa vijana wao katika ubaguzi wa ajira.

Wazanzibar waishi wanayoyasema 'walk the talk',wawajibike kwa kulipa hiyo 21% mishahara na mafao

Hai ishii hapo, Wabunge wa Zanzibar wamelalamika kuhusu nafasi za Ubalozi. Kwamba, Uteuzi wa Balozi uzingatie pia Muungano. Hii ni hoja nyingine ya kupuuzi kwasababu Balozi za Tanzania linahudumiwa na kodi za Tanganyika.

Ingalikuwa na mantiki ikiwa Wabunge wangeomba nafasi za Balozi kuhudumia na Mabalozi wake.
Hapo ndipo 'fair and equitable ' inapokuwa na maana.

' Fair and equitable' ni dhana isiyo maananisha haina Zanzibar iwe tegemezi, kinyume chake iwe Mshiriki

Inaendelea....
 
XV

UKO WAPI MCHANGO WA ZANZIBAR KATIKA MUUNGANO?

Kauli ya Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Rais wa Zanzibar aliyoitoa kupitia gazeti la Mwananchi la December 11 ,2022 imemaliza sintofahamu iliyozushwa na viongozi wa ACT Wazalendo kuhusu akaunti ya Pamoja ya Fedha ya Muungano na Tume ya Fedha ya Pamoja.

Mara nyingi aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Bw Othman Masoud Othman (OMO) ameishtum Tanganyika kunufaika na Muungano hivyo haitaki kuunda akaunti ya pamoja ya Fedha wala Tume ya pamoja ya Fedha itakayosimamia mapato na matumizi.

Kwa kauli za Rais Mwinyi,tatizo lipo kwa Zanzibar kwasababu uwepo wa akaunti ya pamoja unazitaka pande mbili zichangie mfuko, zigawane gharama zitokanazo na kinachobaki kinaenda Zanzibar.

Yes, kinaenda Zanzibar kwasababu kile cha Tanganyika kinabatizwa jina la Tanzania na kuwa cha pamoja.

Makamu wa Rais OMO kwa makusudi na kwa kudhamiria alizusha tuhuma dhidi ya Tanganyika bila sababu.

Chama cha ACT Wazalendo kijitokeze kuomba radhi kuhusu uongo na uzushi wa kipuuzi uliousambaza kwa kuilaani Tanganyika bila sababu. Hili tu linaonyesha dhamira ovu ya ACT Wazalendo kwa Watanganyika

Ubishi wa kwamba kuna akaunti ya pamoja umefika mwisho na OMO aombe radhi katika kulinda heshima ya ACT

Kauli ya Rais Mwinyi pia ilimaliza ubishi wa Zanzibar kufanyiwa 'double taxation' kwamba TRA inachukua kodi na ZRA inachukua kodi. Hoja ya Wazanzibar ni kwamba kwanini kama nchi moja bidhaa kutoka Zanzibar zitozwe kodi na TRA zikiingia Tanganyika ili hali TRA imechukua kodi zikiwa Zanzibar

Kauli hii kama ile ya akaunti ya pamoja zilizungumzwa na kuwaaminisha Wazanzibar wanatendewa uovu.

Rais Mwinyi kathibitisha hakuna kodi ya TRA inayokuja bara, zote zinabaki Zanzibar.

Hii ina maanakuwa akaunti ya pamoja wanayotaka Wazanzibar ni ya kugawana fedha za Tanganyika.

Ina maana kwamba Zanzibar haina mchango wowote katika shughuli za Muungano.
Inathibitisha kauli ya Gavana marehemu Ndullu kwamba Zanzibar haijachangia Muungano kwa zaidi ya miaka 40

Taarifa za 'quarter' za BoT zinathibitisha kwa kuonyesha jinsi mikoa ikiwemo michanga kama Geita na Simiyu inavyochangia pato la Taifa. Taarifa hiyo haionyeshi Zanzibar kwasababu kodi na mapato yake yanabaki huko.

Hayo yote yakitokea, Zanzibar wanalalamika na kusikilizwa kwa kile kinachoitwa Kero za Muungano.
Kila wanachotaka wanapewa na sasa tunaambiwa imebaki kero moja ya akaunti ambayo hawataki kuimaliza

Ikiwa Zanzibar inasikilizwa kwa kero ni wakati sasa wa Zanzibar kuonekana inachangia katika muungano.
Muungano unaipa Zanzibar fursa nyingi sana lakini haina mchango wa aina yoyote

VIongozi wa ACT walikaririwa akisema 'Muungano unatakiwa ' kwasababu za kijiografia ambazo Zanzibar inazipata kama vile kufikia masoko ya EAC, SADC n.k.

Kwahiyo Zanzibar inahitaji Muungano kwasababu za kiuchumi , jambo jema kabias.

Swali, Tanganyika inahitaji Muungano kwa jambo gani ikiwa ndani ya Muungano imetumia rasilimali zake peke yake

Ikiwa muungano unalengo la kiuchumi na inatakiwa hivyo, ni wakati Tanganyika ipunguziwe mzigo wa kuuendesha kwa kuona mchango wa Zanzibar.

Vinginevyo kutoa fursa kwa Zanzibar kwa mtindo wa nataka, nipe, namimi hauwatendei haki Watanganyika

Inaendelea
 
XVI

ZANZIBAR IWAJIBIKE ISISUBIRI FURSA ZA MUUNGANO

Ni dhahiri Zanzibar haina mchango wa kodi za TRA kuingia mfuko Mkuu wa Hazina Dar es Salaam.
Mfuko Mkuu wa Hazina Dar es Salaam ni fedha za Watanganyika zinazotokana na kodi rasilimali zao
Rais wa Zanzibar na Gavana wa BoT walmethinitisha katika nyakati tofauti

Madai ya kamati ya pamoja ya fedha ni njama za kugawana fedha na rasilimali za Tanganyika
Uongo unaosambazwa na Chama cha ACT kupitia viongozi wake ni chuki tu dhidi ya Watanganyika

Kuna hoja kwamba Tanganyika kama Zanzibar inalalamika kuonewa katika Muungano.
Hoja inajengwa na viongozi wa ACT Wazalendo ili kuonyesha usawa kati ya Tanganyika na Zanzibar

Ni hoja ya kipuuzi kama zingine Tanganyika haiwezi kuonewa na Zanzibar na wala haina malalamiko

Watanganyika wanasema hakuna eneo Zanzibar inaibiwa au kudhulumiwa kwa kuzingatia ka uchumi

Hoja kwamba Tanganyika inanufaika na Muungano imekosa elimu ya aina yoyote ile katika uso wa dunia

Wanachosema Watanganyika ni Zanzibar katika udogo wake iwajibike na si kudai fursa peke yake.

Kuwajibika kwa Zanzibar hakuwezi kuwa sawa na Tanganyika. Ingawa Wazanzibar wanautaka usawa, kwa kutumia elimu na mantiki kama tulivyoeleza hakuna usawa.
Tanganyika ni kubwa na shea yake katika muungano iwe gharama au mapato itazingatia ukweli huo.

Kuwajibika kwa Zanzibar ni kuchangia Muungano kwa kiasi kile kinacholingana na uchumi wake ili kupunguza mzigo kwa Tanganyika. Mfano, Zanzibar iwajibike kulipa gharama za Wabunge wake. Zanzibar iwajibike kulipia Wanafunzi wake mikopo ya Elimu ya juu na si kupewa kama 'scholarship'

Zanzibar iwajibike katika Wizara nyeti kama Ulinzi , Mambo ya ndani, Mambo ya nje, Muungano na zile zinazohusiana na Muungano. Wizara hizo ni chanzo cha ajira ambazo Zanzibar hupewa 21%

21% ya ajira zinazotokana na Muungano ilipwe na Zanzibar. Ni utegemezi wa hali ya juu kudai fursa isizoweza kuzilipia. Tatizo hilo limefikia mahali Wazanzibar wanatumia umeme kisha kuleta bili kwa Watanganyika.

Hatudhani kuna Mtanganyika anayelipiwa umeme na Serikali, iweje wao wabebe hata mzigo wa Zanzibar

Zanzibar wajihudumie wanapokuja katika shughuli zinazohusu Muungano na si kutegemea mafungu ya Muungano, na watambue mafungu ya Muungano ni fedha za Tanganyika.

Watanganyika wana hoja kwamba ili kuondoa malalamiko na tuhuma ziszizo na ukweli, Wazanzibar kupitia Baraza la Wawakilishi waondoe yafuatayo kama walivyoondoa GESI, MAFUTA NA BANDARI

1. Waondoe Elimu ya Juu, kama hawaondoi wawajibike kulipa mikopo ya Wanafunzi kutoka Zanzibar si kutegemea fedha za Tanganyika kwani kufanya hivyo ni kuwanyima Wanafunzi wa Tanganyika fursa ya kodi kutoka rasilimali na kodi za nchi yao.

2. Waondoe Tafiti, Hali ya Hewa na mengine wanayodhani si ya Muungano wakidai yameongezwa kinyemela.

Ushiriki wa Zanzibar katika Muungano uwe wa kuwajibika kwa kuhudumia Muungano ni si kukaa pembeni wakisubiri fursa, wakidai fursa kama haki yao ingawa hawana ushiriki wa kutengeneza fursa.
Zanzibar wawe washiriki wa Muungano si Tegemezi wa Muungano wakisubiri kupewa na kugaiwa!

Itaendelea
 
XVII

MUUNGANO KATIKA WAKATI MGUMU SANA

Ingawa viongozi na CCM wanadhani kuficha ukweli ni jawabu, Watanzania bila kujali upande wanakubaliana kwamba Muungano unapita katika wakati mgumu kuliko mwingine

Haina maana Muungano ulikuwa shwari, misuko suko ilikuwepo lakini Viongozi walizingatia malalamiko ya Wananchi

Kwa mfano, miaka ya nyuma Watanganyika waliingia Zanzibar kwa Passport.
Malalamiko yakamfikia Mwalim Nyerere ya kwamba ikiwa sisi ni nchi moja hali hiyo inawezakanaje?

Nyerere alitafakari na wenzake hasa hoja za Wabunge wa wakati huo na kuwashauri Wazanzibar hali ilivyo.
Mwl aliiona hoja na kisha kama kiongozi akashauri upande wa pili. Zanzibar wakaondoa sharti la Passport

Mwaka 1995 Zanzibar bila kujali Katiba ya Muungano waliamua kujiunga na OIC yaani umoka wa nchi za Kiislam

Wabunge wa Tanganyika wakaliona na wakadai uwepo wa serikali 3. Kundi la G55 likawasha moto mkali.
Mwl kwa kuiona hoja aliishauri Zanzibar kujiondoa, haiwezi kuvunja katiba. Mwalimu aliona na kuwa mshauri wa Tatizo

Huko nyuma Rais wa Zanzibar alikuwa makamo wa kwanza wa Rais na kulikuwa na makamu wa pili wa Tanganyika. Watanganyika wakauliza, Rais wa Zanzibar anachaguliwa na Wazanzibar ni vipi awe Makamo wa JMT?
Hilo likaonekana likatafutiwa ufumbuzi wa Busara.

Kwa bahati mbaya, tangu Mwl afariki kuna ombwe kubwa la Wazee wa Busara, Wabunge na Bunge kwa ujumla.

Hali ya kudharau Katiba ya JMT hasa kwa Zanzibar limekuwa jambo la kawaida tu.
Imefika mahali Tanganyika wanajiuliza , hii katiba inayodharauliwa ni ya JMT au ni ya Tanganyika

Kudharau Katiba kumewafanya Watanganyika watafute 'identity' ndani ya Muungano.
Hoja ni kwamba ikiwa Tanganyika itakuwa na muundo wake ni rahisi kusimamia Muungano kwa kuwa na washirika.

Kwasasa Tanganyika ndio Tanzania hivyo wapi inaweza kufikisha hoja zake hasa zinazohusu masilahi mapana

Tumeona Wazanzibar wakisikilizwa kwa kila wanachotaka kwa hoja za Kero za Muungano.

Hakuna mtu au kiongozi anayesimamia masilahi ya Tanganyika kwasababu viongozi waliopo ni Tanzania.

Mambo hayo yameongeza 'sensitivity' kwa Watanganyika na tofauti na zamani sasa wanahoji sana kila kinachotokea, iwe mambo ya Wizara, ajira, fursa, teuzi na kila kitu kwasababu wanahisi kubeba mzigo wa Muungano, washirika Zanzibar hawana mchango lakini wanapewa fursa kubwa kuliko Watanganyika.

Tatizo wasiloliona viongozi wetu ni moja, kama tulivyoeleza huko nyuma Tanganyika ndiyo imebeba Muungano kwa kila hali na rasilimali. Siku Watanganyika watakapo choka kwasababu hawasikilizwi au wanapuuzwa au wanatumiwa huo ndio utakuwa mwisho wa Muungano. Tanganyika ikiondoa rasilimali zake Muungano unakoma siku hiyo.

Inaendelea
 
XVIII

MADAI YA ACT WAZALENDO NA WAZIRI WA KATIBA ZANZIBAR

Taifa likiwa na vugu vugu la Katiba mpya, chama cha ACT Wazalendo kilna agenda ya Tume huru ya uchaguzi.

ACT yenye ushawishi wa siasa za Zanzibar ilishiriki vikao na Tume ya Mkandala kudai Tume huru ya uchaguzi

ACT wana kumbu kumbu ndogo au hawafahamu nini kinahitajika kwanza.

ACT imetokana na CUF ambayo kupitia maridhiano chini ya Maalim waliifanyia mabadiliko katika ya Zanzibar .

Marekebisho yaliunda serikali ya umoja wa kitaifa na kisha Tume huru ya uchaguzi yenye uwakilishi 50/50

Matokeo ya uchaguzi tunajua na historia isiyomwacha Marehemu Jecha inatueleza nini kilitokea

CUF wakielekea ushindi walipokonywa kwa kutumia mamlaka za kidola na vyombo vya kidola.
Uchaguiz ukaibiwa mchana kweupe na Tume Huru ya uchaguzi wakiwemo CUF wakiwa hawana la kufanya

Kwa muktadha huo, hoja ya Tume huru ya uchaguzi ni ya kipuuzi kwasababu kuu mbili

1. ACT wana ushahidi usio na shaka Tume huru pekee haitoshi bila udhidhibiti wa mamlaka za dola
2. Uundwaji wa Tume huru ni zao linalotokana na Katiba, hivyo, Katiba huanza ili kuzaa tume huru

Hoja ya ACT imewapa CCM nguvu sana kwasababu wana machaguo. Kwanza, Tume huru au Katiba mpya
CCM wanataka Tume huru kwasababu tayari wameshatengeneza mazingira ya kuihodhi Tume huru ya uchaguzi
Sheria ya usalama wa Taifa inaruhusu watumishi wake watende uovu bila kushtakiwa. Hili tu linatosha kabisa kuvuruga uchaguzi hata kama Tume yote itakuwa ya Wapinzani

Waziri wa sheria na Katiba wa JMT kasema kuna mchakato wa kutoa elimu ya Katiba kwa miaka 3.
Maana yake hakuna katiBa mpya kwa miaka 3 ijayo.
Waziri wa Sheria na Katiba wa JMT alisema inawezekana katiba mpya isihitajike bali marekebisho madogo.

Mkutano ulihudhuriwa na Makamo wa Rais na kiongozi wa ACT Wazalendo Bw Masoud Othman Masoud.
Waziri wa Sheria na Katiba Zanzibar Bw Harum A Suleiman alisema katiba ya sasa haina tattizo ikifanyiwa marekebisho machache.

Pengine ACT Wazalendo wanakubaliana na hoja za Mawaziri, lakini wajiulize historia inawafundisha kitui.

Muda mwingi wa kuitusi Tanganyika ungetumika kudai Katiba mpya.
Bw Othman alikuwepo wakati Waziri wa sheria na Katiba wa Zanzibar anatamka kauli za kuendelea na Katiba ya sasa. Bw Othman hakutoa maoni baada ya mkutano kana kwamba hakuisikia kauli ya Waziri wa SMZ yeye akiwa Makamo.

Ni wazi kauli ya Waziri Suleiman haikuwa yake bali pia ya Makamo wake wa Rais aliyetulia wakati ikitolewa.

Katiba mpya si takwa la kisiasa ni takwa la kijamii na kizazi cha sasa.

Washiriki wa Mkuatano ni viongozi wastaafu, Katiba haiwagusi katika maisha yao yaliyobaki.
Madai kwamba yanahitajika marekebisho katika Katiba ya sasa yanaweza kuleta matatizo nchini,

viongozi wasome alama za nyakati na nyuso za Watanzania na waiangalie Dunia na matukio kabla ya maamuzi

Miaka 10 iliyopita kulikuwa na ' Arab spring' mageuzi yaliyozikumba nchi za Kiarabu hata kutetemesha Falme kubwa kama Saudi Arabia. Ni mageuzi yaliyoongozwa na Kizazi cha sasa kwa hoja ya kutosikilizwa na Wazee waliodumu madarakani. Ni mageuzi yaliyotokana na Vijana kuamua hatma ya mataifa yao.

Mwaka huu umekuwa wa matukio Africa Magharibi hadi kuichanganya ECOWAS na Dunia. Serikali za Kiimla zinaondolewa kwa nguvu. Hoja ni kama ile ya Arab Spring kwamba Kizazi hakisikilizwi na kimetekelekezwa

Tanzania ingetaka kubaki kama nchi ya ''Amani' lakini pia Tanzania ni sehemu ya system ya Dunia.

Jambo la kusikitisha chama kilichobeba agenda ya Katiba kwa muda mrefu (Chadema) kulegeza uzi wa kudai Katiba hasa baada ya Kuachiwa kwa Mhe Mbowe.

Kwasasa kauli mbiu ya Chadema ni Tume Huru ya uchaguzi n Uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu.

Ni kama agenda ya katiba imekufa. Swali kulikoni huko Chadema?


Itaendelea
 
XIX

CHADEMA NA MKENGE WA KATIBA

ACT Wazalendo walivyotawanyika katika hoja kwamba, hawataki Muungano lakini hawataki taratibu za kufikia malengo ikiwa ni pamoja na kutumia Baraza la Wawakilishi, Bunge au Mikutano kushinikiza hoja yao.

Tumeona walivyochezewa 'shere' kwa kuingia SUK.Hoja kubwa ya ACT ni ni Tume Huru ya uchaguzi
Wameshahu historia ya Tume huru ya CUF iliyofuta matokeo mwaka 2020

Hoja kwamba Watanganyika ni Wakoloni na wanaidhulumu Zanzibar haina mantiki wala mashiko na ni ya kipuuzi. Ni Hoja inayokidhoofisha ACT upande wa Tanganyika.

Kwa kauli za matusi na kashfa dhidi ya Watanganyika ni aghalabu chama kinaweza kukua.
ACT Wazalendo inachofanya ni 'Autolysis'

Chadema ilibeba agenda ya Katiba. Kilichompleka Mwenyekiti wa CDM Magereza ni kudai katiba.

Hilo lilifanyika makusudi ili kuzima moto wa madai ya Katiba.
Kinyume na matarajio, vijana wa CDM waliendeleza agenda licha ya kutokuwepo Mwenyekiti.

CDM ilisusia vikao vyote vya Msajili na hilo likatengeneza Ombwe kubwa kiasi cha kulazimisha Mwenyekiti aachie.

Mh Mbowe akiwa magereza na Makamo wake Tundu Lissu akiwa nje ya nchi, Vijana wa CDM walichukua agenda mbili, kwanza kushinikiza Mwenyekiti aachiwe na kutumia kifungo chake kuendeleza agenda ya Katiba Mpya.

Serikali iligundua kumshikilia Mbowe kuna '' madhara'' kuliko kumwacha huru.

Njia iliyotumika ni kumleta karibu '' Keep your friends close, but your enemies closer'.
Hicho kilimlazimu Rais amwite Mbowe Ikulu mara moja kabla hata ya kukutana na wenzake ndani ya Chama.

Tangu wakati huo Mh Mbowe alipoteza uwezo wa kuzungumzia jambo la Katiba kwa kisingizio yupo katika mazungumzo na CCM na Serikali.

Katika hotuba zake Mh Mbowe alisema wazi hatoki katika mazungumzo.Kwamba anaamini Rais SSH ana ni njema.

Mbowe amepoteza vitu viwili. Kwanza, uwezo wa kujadiliana 'bargaining chip' . Pili, akawachanganya Chadema.

Mh Mbowe alipoteza bargaining chip ya COVID19 Bungeni. Mbowe alikwenda katika majadiliano bila kitu kama kishikizo cha mazungumzo.

Mh. Mbowe asingeanza mazungumzo hadi Maamuzi ya Chadena juu ya kuwafukuza COVID19 yaheshimiwe.

Mbowe hakufanya hivyo COVID19, Bunge na Mahakama wanapitisha Muda. CDM na Mbowe ni wapottezaji 'losers'

Kuwachanganya Wanachama agenda ya Katiba ikapoteza nguvu, CDM wakiyasubiri mazungumzo kati Marafiki Mh Mbowe, Mh Kinana na Mh Rais.. Mh Mbowe akageuza mambo ya Kichama kuwa ya uswahiba

Mbowe alidai mazungumzo yanaendelea licha ya kuonywa na kutahadharishwa kwamba hamkani si shwari.

Wakati 'mazungumzo' yasiyo na ratiba yakiendelea, CCMna Serikali yake ilitumia muda huo kupitisha sheria kama ile ya usalama ili kujihakikisha inatenda mambo yake kwa mkono wa dola.

CCM na Serikali yake waliendelea na mchakato wakimshirikisha Prof MkandaLA na Msajili wa vyama.
Mbowe anajua Msajili amefanya nini CUF na NCCR ! lakini akaamua kuendelea kushiriki nao vikao vya TCD.

Majuzi, aliyekuwa Waziri M h Ndumbaro akasema Katiba mpya inasubiri elimu ya miaka 3.
Kwamba Wananchi hawana ufahamu pengine akidharau Tume ya Jaji Warioba iliyokuwa imesheheni nguli

Kauli ya Ndumbaro ni ya Serikali. Ni kauli iliyowagusa akina Mbowe kwa taharuki kwamba wanajitoa katika mazungumzo. Ni jambo la kushangaza kwasababu alama zote za nyakati na historia inaonyesha wazi CCM hawawezi kukubali mabadiliko ya Katiba inayowasaidia kufaidi hatamu na Ulaji walio nao.

Swali linalogonga vichwa vya Wachambuzi na wenye fikra tunduizi ni hili '' Hivi Mh Mbowe hakujua , hakusoma historia au alijua vyote lakini kwa kuongozwa na utashi binafsi alikubali kuingia MKenge wa Katiba''

Si sahihi kumtuhumu Waziri Ndumbaro, alichosema ndicho CCM na Serikali yake vilikusudia.

Na wala Mh Mbowe asilaumiwe kwasababu naye huenda alikuwa na utashi wake.

Kundi la kuulizwa ni Viongozi wa CDM wa Kamati na Halmshauri kuu, haya mauza uza yalitokeaje wakiwa ni viongozi? Walimwachaje Mh Mbowe afikishe Chama kupoteza agenda ya Katiba?

Itaendelea
 
Back
Top Bottom