Series (Special thread)

Series (Special thread)


Daaah mdauuuu.... Bonge la series la kihunihuni madawa ya kulevya , magang na wanasiasa na vatican wanavyopambana kuicontrol pwani . Nimependa ushirikianao wa wale machalii wa tatu, mtoto wa mpelelezi na watoto wawili wa makundi hasimu lakini wao wakaja kuwa marafiki wakafanya kakundi chao cha mtu tatu mmoja akili nyingi (mtoto wa polisi ) , mmoja mtata kuua nje nje (familia ya Gippsy) na kajamaa kapole (familia ya Aureliano) na jangili baba kubwa Samurai.... dadadeki ni siku nyingi tangu 2016... ila imepata order ya Season two mwaka huu...
 
Hivi mkuu hii BB ina uzuri gani hasa? Story yake ikoje yani? Naomba kujua. Kozi nilikua nayo kompliti sizon one - five lakini nilifuta. Em nambie nifanye namna niisake tena.

Story inahusu mwalimu wa somo la kemia aliyekuja kugundulika na kansa ambayo siku zake za kuishi zilikuwa zinahesabika,akajiingiza kwenye utengenezaji wa madawa ya kulevya (kwa kutumia taaluma yake) kwa kushirikiana na mwanafunzi wake ili kuwaachia familia yake (yenye mtoto mkubwa mlemavu) pesa ya kujikimu na kusoma hadi atakapofikisha miaka 18 wakati huo shemeji yake alikuwa mtu wa kitengo.
Mwanzoni inaonekana kama inaboa lakini ukimaliza episode 1,hutataka kuiacha kabisa mkuu Ollachuga Oc.
 
Mkuu hii movie money heist, nifanye vipi ili niweze kuidownload torrent
Umo Umo kwenye hiyo link inakuja Kama na kavideo flan kana alama ya kuplay.. kaclick kataonyesha chini previous, next na mengine mengine scroll chini Kuna options mbili za kuvuta kupitia magnetic au torrent... Click unayopenda mzigo huo
 
Luke cage vipi inatazamika?
Daah.. Kaka mkubwa series za Marvel bwana zinanichoshaga wanawapa characters wao nguvu kubwa sana kiasi kwamba unajua tu Hakuna atakacho feli niliangalia mbili tatu kwa kweli ni nzuri zina action Kama hii Lakini hazinivutii kivile.. Napenda zile hata star wa series anakula kichapo anajipanga Kama ilivyokuwa kwa Daredevil na Agent Carter lakini hizi zilizofuata ni Kama superpower flani ambazo sio genre nayoifurahia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom