leverage ni kama burn notice kama uliangalia,kwanza mtindo wao si mwendelezo wa story,kila episode inakuja na tukio na inaisha hapo hapo,kwahiyo episode lingine inakuja na jipya.
Leverage ni kama kundi la watu binafsi ( wapo kama 5) ambalo halijulikani kwa serikali,inafanya mambo yake kivyake kuwasaidia watu ambao wamedhulumiwa,mtu akidhulumiwa hata awe mjanja wao wanakuja kumtapeli halafu mhanga anarudishiwa mali zake na faida juu,maana wao wanatapeli matapeli na wakitapeli lazima tapeli akimbie nchi ili serikali isimkamate,na tapeli wakimfilisi wanamfilisi kweli,kiujumla wanacheza na watu wa kila aina iwe institutions za serikali au binafsi ila mwishoni wakimtapeli tapeli hamna ushahidi unaowafunga,kiujumla wanasaidia wahanga