Bianca tunampenda ila ndiyo hivyo tena mkuu.
Episode ya kwanza itaanza na shot ya juu ikiangalia miamvuli meusi ikinyeeshewa mvua nyepesi. Camera itapan huku na kule kuonyesha magari meusi yakilindwa na majamaa yenye suti nyeusi, miwani meusi na vi earpice vyeupe vyenye coils masikioni. Tutagungundua kuwa watu hao wapo makaburini na litaonyeshwa jeneza lililofunikwa na bendera ya UK likishushwa kaburini mdogo mdogo. Picha ya Bianca kwenye frame itaonekana kwa pembeni, halafu watatupa shots za Isabel akiwa na sura ya ukauzu, huku Paul, mume wa Bianca, na mtoto wake wakiwa wanalia....
Baada ya hiyo scene ya mazishi itakayokkuondolea kila doubt kwamba demu hayupo tena duniani, ndiyo utaanza kuona makeke ya Jackal sasa.