Natamani kusema 'nakuhakikishia hata kuwepo' ila haya mambo huwezi jua.
Hakuna mantiki ya kumfufua na hakuna namna ya kutuaminisha alipona kule Spain. Ukimuangalia huyu demu kwa jicho lingine, unaweza kusema yeye ndiye alikuwa adui na Jackal ndiyo steringi eti... Na Season 2 itamfanya Jackal awe main protagonist huku akina Isabel, Mzee Winthorp na Whitelock wakiwa main antagonists.
Jackal ataendelea kutembeza adhabu kwa wahuni kwenye system, huku akifukuziwa na akina Osita (na Osita atakuwa anamsaidia kisiri siri ili amshughulikie kwa ndani Isabel), huku pia akijitahidi kunusuru ndoa yake na kuwalinda awapendao. Itakuwa rahisi zaidi ya audiences kuconnect na Jackal na kumpa support.