KWELI Samia Suluhu Hassan: Rais Magufuli anawasalimia, anasema tuchape kazi tulete tija kwa Taifa letu

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Leo, Machi 15, 2021 Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Tanzania ameanza ziara mkoani Tanga na akiwa kwenye kiwanda kimojawapo alichozindua kinachoshughulika na matunda wilayani Korogwe, alipata nafasi ya kusalimu wananchi baada ya kuombwa na mkuu wa mkoa wa Tanga ambapo alianza na salamu kutoka kwa Rais Magufuli

"Kabla ya kuwapongeza niwasalimie salam za Rais anawasalimia, anasema tuendelee tuchape kazi, kipindi hiki tushikane tujenge mshikamano, tujenge upendo, tuchape kazi tulete tija kwa Taifa letu"

Baada ya salam hizo Mama Samia amewapongeza kwa kuwa na kiwanda kwani ni mkombozi.

1658211004066.png
 
Tunachokijua
Rais John Magufuli hakuweza kuonekana kwenye hadhara tangu Februari 27, 2021 ambapo hali ya sintofahamu ilivuma kwa wananchi na watu kuanza kuhoji sehemu ambayo Rais Magufuli alikuwepo.

Kutokuonekana kwake mbele ya umma kuliibua maswali mengi, huku baadhi ya watu wakidai kuwa ni mgonjwa na hali yake ya kiafya siyo nzuri.

Kauli ya Makamu wake Samia inaweza kuchukuliwa kama jibu kwa watu wote wanaodhani kuwa hali ya kiafya ya Rais Magufuli sio nzuri.

Wakati huo Samia Suluhu Hassan alikuwa ni Makamu wa Rais (Kwa sasa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania). Samia Suluhu alipokuwa katia ziara ya kikazi Mkoani Tanga, Machi 15, 2021 aliwaambia wakazi wa Tanga na Tanzania kuwa Rais Magufuli yuko salama na anawasalimia. Alisema

"Mheshimiwa Rais anawasalimia na anawashukuru sana sana, kwa kazi nzuri mlioifanya mwaka jana mwezi wa kumi ya kurudisha serikali ya chama cha mapinduzi madarakani, anasema tuko salama, tuchape kazi, tujenge upendo na mshikamano"

Hata hivyo siku ambayo Samia alitangaza kifo cha Rais Magufuli, Machi 17, 2021 alisema Rais Magufuli alianza kuugua Mach 6, 2021 na alilazwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

Machi 14 hali yake ilikuwa mbaya na alipelekwa Hospitali ya Mzena aliendelea na matibabu chini ya uangalizi wa madaktari na wauguzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete hadi umauti ulipomkuta.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom