ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,053
49,737
Usiyempenda kaja.
---
1701714360915.png
Mkutano Mkuu maalum wa kumchagua Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Arusha, umemchagua Loy Thomas Sabaya, kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoani humo.

Sabaya ambaye ni Baba mzazi wa aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya ameshinda nafasi hiyo baada ya kupata kura 473, akifuatiwa na Ndg Daniel Mrisho Pallangyo aliyepata kura 374, Solomon Ole Sendeka Kivuyo kura 59 na Edna Israel Kivuyo aliyepata kura 10.

Sabaya anachukua nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Zelothe Stephen aliyefariki hivi karibuni.

My Take
Kama wewe ni mtoto wa mkulima shika jembe ukalime maana siasa ni connection ya wenye majina.

Pia soma; CCM yateua Wagombea katika ngazi ya Mkoa na Wilaya. Baba wa Sabaya (aliyekuwa DC Hai), ateuliwa kugombea Arusha
 
1701705297897.png

Mkuu wa Mkoa wa Njombe na Msimamizi wa Uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Antony Mtaka amemtangaza Loy Thomas Sabaya kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha kwa kupata kura 463 kati ya kura 907 huku kura moja ikiharibika.

Loy Sabaya ni Baba Mzazi wa aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya.

Wagombea wengine ni pamoja na Dkt. Daniel Pallangyo 374, Solomon Kivuyo kura 59 pamoja na Edna Israel Kivuyo kwa kupata kura kumi.

Uchaguzi wa nafasi ya CCM Mkoa wa Arusha unafanyika baada ya kufariki kwa Zelothe Steven aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha.
 
Huyo atakuwa ni baba wa Lengai Ole Sabaya, sasa sijui atalipiza vipi kisasi kwa kosa gani alilowahi kufanyiwa wakati mahakama ilimkuta na hatia mpaka kumfunga gerezani mwanae.

Hapo kama ni kisasi basi atalipiza kwa adhabu aliyopewa na mahakama, kwasababu ile adhabu hakupewa na wale waliomfanyia ubaya mwanae.

Ila CCM mna ushirika usio na mashaka na shetani, siku zote mpo nae bega kwa bega kwenye shughuli zenu, na wala hamuoni aibu yoyote.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Ongeraa,tuna imani ni jembe kama mwanae.
Il

like father like a son..mambo yatakuwa mazuri

Mafisadi na wakwepa kodi ..na wanaomkwamisha mama chali
 
Back
Top Bottom