Heparin
Senior Member
- Sep 24, 2021
- 127
- 420
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Arusha Thomas Ole Sabaya amewaonya wakazi wa Longido kutokuchagua wapinzani kwenye uchaguzi ujao wa serikali za mitaa, kwani serikali haitopeleka huduma muhimu kwenye maeneo yatakayokaliwa na viongozi wasiotokana na CCM.
Sabaya aliyekuwa akizungumza kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Longido ametoa kauli hiyo muda mfupi, baada ya kufanyika kwa maandamano ya CHADEMA mkoani Arusha.
Amesema yeyote atakayechaguliwa nje ya CCM atawajibika yeye na wananchi wake kujitafutia huduma muhimu na Mkuu wa mkoa hatokanyaga katika maeneo yenye kuongozwa na wapinzani.
Kauli ya Ole Sabaya imekuwa na hisia mseto mitandaoni,watumiaji wengi wa mtandao wa X (zamani twitter), wakisema kuwa rais Samia Suluhu Hassan hajaeleweka vyema na wasaidizi wake serikalini na ndani ya chama chake kutokana na kutoishi kwenye falsafa yake ya maridhiano.
Wengine pia akiwemo mwanasiasa John Heche anasema kauli kama hizo zinasababisha chuki zisizo na msingi kwenye jamii kwa kuaminisha watu kuwa watanzania walio nje ya CCM hawana haki kama walizonazo wanachama wa chama hicho tawala.
Rais Samia alitambulisha falsafa yake ya Maridhiano na upatanishi katika kujenga upya Tanzania tuitakayo, suala ambalo ndani yake linahimiza ushirikiano,ustahimilivu na kufanya kazi kwa pamoja na vyama pinzani katika kujitafutia maendeleo.