Ebe
JF-Expert Member
- Apr 18, 2013
- 914
- 1,133
Kasome katiba ibara ya 147 ndo utajijua kuwa hujui unachokisema, unaongea maneno ya vijiweni.Tafsiri ya Jeshi na majukumu yake Dunia nzima havitofautiani. Na neno linalotumika kuwatambua ni moja tu! Nalo ni Jeshi.
Kwa Tanzania Polisi kuitwa Jeshi ni neno lililozoeleka na linalotumika mara kwa mara kwenye mazungumzo na kusikika masikioni mwa watu kwa njia ambayo linaonekana limetumika pahala sahihi lakini maana yake ni tofauti kabisa na lilivyozoeleka kutumika.
Wanaolinda mipaka au ardhi ya nchi/Dola kwa kutumia nguvu ya silaha dhidi ya wavamizi wa nje hiki kikundi cha jumla ya watu kinaitwa Jeshi. Dunia nzima ndivyo kinatambulika hivyo.
Kikundi cha jumla ya watu waliyopewa mamlaka ya ndani ya Dola/nchi kulinda usalama wa raia na mali zake hiki kikundi kinajulikana ni Polisi.
Polisi ni Polisi na Jeshi ni Jeshi.