RUSHWA: Kijana aliyekuwa akiwalaghai na kuwatapeli Maofisa wa Jeshi la Polisi kwa ahadi za ajira akamatwa

bloggerboy

JF-Expert Member
Nov 13, 2017
568
1,211
Afande pokea taarifa kuhusiana na mahojiano yaliyofanyika leo Tarehe 04/04/2022 baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa wa makosa ya utapeli David Damas Otieno @ MAJOR GENERAL MRAI miaka 39, kabila mjaruo, kazi mkulima, dini mkristo mkazi wa Dar es salaamu ambaye amekamatwa leo Tarehe 04/04/ 2022 katika eneo la Msamvu wilaya ya Morogoro mjini mkoa wa Morogoro. Ametaja jumla ya matukio 21 aliyowahi kutapeli akapata pesa na mengine aliahidiwa lakini hakupata pesa Kama ifuatavyo:

1. RPC IRINGA _ JUMA BWILE
Aliwasiliana naye Nov. 2021 ili mtoto wake atafutiwe ajira ktk idara ya usalama wa Taifa akamtumia 150,00/= kwa awamu mbli ya Kwanza 100000/= ya pili 50,000/=

2.OCD MUSOMA
Alitaka ahamishiwe Kahama, alituma 250,000/=

3.RPC KAGERA _ REVOCATUS MALIMI
Alitaka nafasi ya ajira ya TAKUKURU kwa kijana wake, alituma 400,000/=.

4. OCD KAHAMA
Alitaka apandishwe cheo, alituma pesa 270,000/= awamu ya kwanza, na awamu ya pili alituma samaki wakubwa Aina ya Sato waliokaangwa kwenye gari la HAPPY NATION la Mwanza Dar es salaamu ambao aliwauza kwa 65,000//=

5. STAFF OFFICER MOROGORO _ KUNGURA. Baada ya kupandishwa cheo kuwa ACP akitokea OCD Mvomero
alitaka kuwa RPC mkoa wa GEITA Ili awe karibu na nyumbani kwao sababu anakaribia kustaafu, hakutuma pesa alishtuka.

6 DEBORA DAUDI MAGRIGIMBA
Alitaka arudishiwe nafasi ya RPC baada ya kuhamishwa KUTOKA RPC SINGIDA KUWA STAFF OFFICER CENTRAL POLICE DAR ES SALAAMU.
Hakutuma pesa waliwasiliana Kama ndugu wakabila moja la wasukuma ingawa mtuhumiwa siyo msukuma.

7. OCD KISHAPU SHINYANGA
Alitaka kupandishwa cheo na ahamishiwe SHINYANGA Mjini kwani KISHAPU ni kijijini Sana
aliahidi kutuma million mbili lakini kabla hajatuma alipata msiba.

8. MICHAEL DELELI _ Aliyekuwa RTO KILIMANJARO
Alitaka arudishiwe kuwa RTO MOROGORO baada ya kuhamishwa kuwa RTO KILIMANJARO, aliahidi kutoa million moja Ila mtuhumiwa alizima simu yake kwa kuwa anajua kuwa anatafutwa na polisi kwa vitendo vyake hivyo vya kutapeli.

9. MZIRAI _ OCS MEATU
Alitaka apandishwe cheo TOKA ASP kuwa SP na ahamishiwe SHINYANGA Mjini au Kahama sababu alikaa na cheo hicho zaidi ya miaka 08. Alituma 60,000/= za voucher.

10. OCD LUANGWA
Alitaka mtoto wake apate ajira ktk idara ya usalama wa Taifa, aliahidi million moja lakini hakutuma.

11. RTO KAGERA
ALitaka awe RTO MWANZA, aliahidi kutoa million moja baada ya siku tatu lakini hakutuma.

12. OCD TARIME
Alitaka kuwa OCD ILEMELA MWANZA
alituma 200,000/=

13 OCD RUVUMA
Alitaka ahamishiwe Bagamoyo karibu na familia yake, aliahidi million moja lakini hakutoa.

14 RCIO IRINGA CHARLES BUKOMBE
Alitaka arudishiwe nafasi ya RTO na apangiwe MOROGORO, aliahidi kutoa zawadi suala lake likifanikiwa.

15.OCD MAGU
Alitaka ahamishiwe kuja Morogoro au Chalinze ili awe karibu na familia yake, aliahidi million moja lakini hajatuma.

16.RTO TARIME LORYA
Alitaka arudishwe Mwanza, alituma 150,000/=

17. OCD MAKETE
Alitaka ahamishiwe Bagamoyo aliahidi zawadi likifanikiwa.

18. OCD ILAMBA _ SINGIDA
Alitaka ahamishiwe wilaya ya Manyoni, aliahidi million moja lakini hakutuma.

19. OCD BIHARAMULO
Alitaka ahamishiwe GEITA
Aliahidi million moja lakini hakutuma.

20. RTO LINDI
Alitaka ahamishiwe Morogoro, aliahidi zawadi akifanikiwa.

21. OCD TANDAHIMBA
Alitaka ahamishiwe Chalinze, aliahidi 500,000/= lakini hakutoa.

Mtuhumiwa baada ya kukamatwa alipekuliwa maungoni ambamo alikutwa na simu tatu:
ITEL MBILI, TECNO MOJA, RADIO CALL MOJA Aina ya BAOFENG NA CHARGER YAKE MOJA, PESA TASLIMU 55,600/= NA CHARGER YA SIMU MOJA. Pia alipekuliwa katika chumba Namba 05 Cha Guest iitwayo THREE ROOF iliyopo maeneo ya Msamvu ambako alikutwa amefikia na vitu vifuatavyo vilichukuliwa:
Bag moja dogo la mgongoni rangi ya ugoro likiwa na nguo mbalimbali, N_ CARD_ 1000, 0000,0058, 9675, na charger ya simu.
Kesi ya KUJIFANYA AFISA WA SERIKALI IMEFUNGULIWA
Naomba kuwasilisha.

====

Dar es Salaam. Maofisa wa Jeshi la Polisi zaidi ya 20 wanadaiwa kutapeliwa fedha kwa njia ya mtandao na mtu aliyejitambulisha kuwa na cheo cha Meja Jenerali wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), kutoka kitengo nyeti serikalini.

Tukio hilo linadaiwa kuwa la kwanza kutokea nchini na ukizingatia Jeshi la Polisi ndilo lenye dhamana ya kushughulika na uhalifu wa kimtandao, lakini inadaiwa mtuhumiwa huyo aliweza kujipenyeza kwa maofisa hao bila kugundulika na kufanikiwa kuwatapeli.

Vyanzo vyetu vimedokeza miongoni mwa wanaodaiwa kutapeliwa ni maofisa waliotaka kupewa wadhifa wa ukamanda wa polisi wa mikoa (RPC), waliotaka kupandishwa vyeo na waliotaka kuwa wakuu wa polisi wa wilaya (OCD) au kuhamishwa kituo kimoja kwenda kingine.

Mbali na kundi hilo, lipo kundi la maofisa waandamizi wa Polisi ambao waliingia kwenye mtego na kutuma fedha, ili watoto wao watafutiwe kazi kwenye idara nyeti za Serikali.

Vyanzo vya kuaminika vililiambia Mwananchi kuwa mtuhumiwa huyo anayejulikana kwa jina la David Otieno aliyekuwa akijitambulisha kama Meja Jenerali Mrai, alikamatwa Aprili 4, 2022 eneo la Msamvu mkoani Morogoro.

“Sielewi alikuwa anatumia nini kuwafanya hawa maofisa watume fedha kwa mtu ambaye hawajakutana naye, hawamfahamu kwa sura, wanaongea tu kwa simu na wanajua kuna utapeli mwingi kwa njia ya mtandao,” kilidokeza chanzo kimoja.

“Kuna RPC mmoja alituma fedha kwa awamu mbili za Sh100,000 na Sh50,000 ili mtoto wake atafutiwe kazi katika moja ya idara za Serikali na mwingine akatuma Sh400,000. Yaani ni simulizi ambazo zinachekesha kidogo,” ilielezwa.

Chanzo kingine kilidai “Kuna ofisa mmoja alitaka apandishwe cheo na akatuma Sh270,000 na baadaye akamtumia jamaa zawadi na jamaa akapokea mzigo huo jijini Dar es Salaam.

Huyo jamaa amekiri kufanya matukio zaidi ya 25 na hayo ni kwa maofisa wa Jeshi la Polisi, haieleweki kama kuna makundi ya maofisa kutoka idara zingine,” alidokeza ofisa mmoja wa Polisi wa Morogoro aliyekataa kutajwa jina gazetini.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Musilimu alipotafutwa na Mwananchi juzi na jana kuzungumzia suala hilo, alisema hawezi kuzungumzia kwa sababu si la kipolisi na hata kama lingekuwa la kipolisi, lingeweza kuzungumziwa na Msemaji wa Jeshi la Polisi au Mkuu wa jeshi hilo (IGP), Simon Sirro.

Lakini vyanzo vya uhakika vya Mwananchi kutoka mkoani Morogoro na maeneo mengine vilisisitiza mtuhumiwa huyo alikamatwa Aprili 4 na mpaka jana mchana alikuwa bado anashikiliwa na polisi mkoani humo kwa hatua zaidi.

Mwananchi liliendelea kudokezwa na vyanzo vingine kuwa wapo maofisa walijikuta wakiingia kwenye mtego wa mtuhumiwa huyo na kufanikiwa kuwashawishi kutuma viwango tofauti vya fedha, lakini hawakutuma baada ya kumtilia shaka.

“Maofisa wengine ni kama walikuwa tomaso, wakakubaliana kwamba akifanikisha ama kumhamisha kwenda anakotaka au kuwasaidia ndugu na jamaa zao ndio wangetuma zawadi kama asante. Hiyo ndio pona yao,” kilidokeza chanzo chetu.

Wengine waliahidi kutoa fedha taslimu kati ya Sh500,000 na Sh1,000,000, lakini hawakutuma na baadhi yao ni wale waliotaka kupata wadhifa katika vituo vya kazi ambayo walikuwa wameichagua.

Mwananchi lilipoendelea kuitafiti habari hiyo, lilifanikiwa kupata taarifa kutoka Morogoro zikidai baada ya mtuhumiwa kukamatwa katika nyumba moja ya wageni iliyopo eneo la Msamvu na kupekuliwa, alikutwa na vitu mbalimbali, ikiwamo simu ya upepo (radio call) aina ya Baofeng.

Katika siku za karibuni, kumeibuka makundi ya watu wanaojihusisha na utapeli wakitumia majina ya viongozi na watendaji wenye uamuzi serikalini na kwa sehemu kubwa ya wanaotapeliwa ni wanaotaka vyeo au ajira serikalini.

Kauli ya Polisi
Akizungumzia suala hilo kwa mara nyingine jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Musilimu alisema hawezi kulizungumzia kwa kuwa si la polisi.

“Mimi siwezi kuongea kwa sababu sielewi chochote kuhusu suala hilo, hiyo taarifa hata mimi nimeiona kwenye mitandao tu,” alisema Kamanda Musilimu.

Aliongeza kuwa kama suala hilo lingekuwa la kipolisi, lingeweza kuzungumzwa na Msemaji wa Jeshi la Polisi au Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro.

Jitihada za kumtafuta Sirro zinaendelea kwa kuwa jana hazikuweza kuzaa matunda hata alipopigiwa kwa simu yake ya kiganjani.

Hata hivyo, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, David Misime alipoulizwa kuhusu taarifa za kutapeliwa kwa maofisa hao, alijibu kwa njia ya WhatsApp kwa kutuma ujumbe ulioandikwa kwenye ukurasa wa Twitter wa Jeshi la Polisi ukionyesha kwamba taarifa hiyo ni feki, ipuuzwe.

Alipoulizwa kuwa Mwananchi lina taarifa za kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo, ambaye bado anashikiliwa kwenye kituo kikuu cha polisi mkoani Morogoro, Misime hakujibu tena swali hilo.

Mtuhumiwa akamatwa

Vyanzo mbalimbali vya habari mkoani Morogoro vinaeleza kuwa ni kweli mtuhumiwa huyo anashikiliwa na polisi mkoani humo.

Chanzo kingine kilisema mtuhumiwa huyo aliwatapeli kwa kuwaambia watu, wakiwemo maofisa wa polisi kuwa anaweza kuwahamisha, kuwapandisha vyeo na wengine kuwatafutia ndugu zao nafasi za kazi kwenye majeshi.

“Ni kweli huyo mtu amekamatwa na hili suala lipo kwa mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Morogoro (RCO), yeye anaweza kulielezea vizuri zaidi kwa kuwa suala hili lipo mezani kwake,” kilisisitiza chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa jina.

Chanzo: Mwnaanchi
 
Hahaaa ndiomaana waliambiwa wawape hizo kazi watu wenye elimu hawataki ,oogh tunataka la saba ndio matokeo yake haya jitu limebeba manyooota mabegani lakini kichwani hewa, kama lile liliostaafu dodoma sijui wanaliita mbwa koko sijui nani, hovyoooo sasaahivi linahenyea mafao wanalipita kwenye korido kama hawalijui
 
Duuuh

Yaan ni sawa na wale vijana wanaopita mitaani kuiba Mbwa ambao weww ndio unaamini watadhibiti Mwizi…

Tapeli anatapeli wanaopaswa kudhibiti utapeli

Ila atakuwa kama si Askari basi ana connection na wahusika…haiwezekan apate ujasiri hivyo

Pia inathibitisha madai ya kuwa Jeshi la Polisi ni shamba darasa la mambo ya Rushwa
 
Afande pokea taarifa kuhusiana na mahojiano yaliyofanyika leo Tarehe 04/04/2022 baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa wa makosa ya utapeli David Damas Otieno @ MAJOR GENERAL MRAI miaka 39, kabila mjaruo, kazi mkulima, dini mkristo mkazi wa Dar es salaamu ambaye amekamatwa leo Tarehe 04/04/ 2022 katika eneo la Msamvu wilaya ya Morogoro mjini mkoa wa Morogoro. Ametaja jumla ya matukio 21 aliyowahi kutapeli akapata pesa na mengine aliahidiwa lakini hakupata pesa Kama ifuatavyo:

1. RPC IRINGA _ JUMA BWILE
Aliwasiliana naye Nov. 2021 ili mtoto wake atafutiwe ajira ktk idara ya usalama wa Taifa akamtumia 150,00/= kwa awamu mbli ya Kwanza 100000/= ya pili 50,000/=

2.OCD MUSOMA
Alitaka ahamishiwe Kahama, alituma 250,000/=

3.RPC KAGERA _ REVOCATUS MALIMI
Alitaka nafasi ya ajira ya TAKUKURU kwa kijana wake, alituma 400,000/=.

4. OCD KAHAMA
Alitaka apandishwe cheo, alituma pesa 270,000/= awamu ya kwanza, na awamu ya pili alituma samaki wakubwa Aina ya Sato waliokaangwa kwenye gari la HAPPY NATION la Mwanza Dar es salaamu ambao aliwauza kwa 65,000//=

5. STAFF OFFICER MOROGORO _ KUNGURA. Baada ya kupandishwa cheo kuwa ACP akitokea OCD Mvomero
alitaka kuwa RPC mkoa wa GEITA Ili awe karibu na nyumbani kwao sababu anakaribia kustaafu, hakutuma pesa alishtuka.

6 DEBORA DAUDI MAGRIGIMBA
Alitaka arudishiwe nafasi ya RPC baada ya kuhamishwa KUTOKA RPC SINGIDA KUWA STAFF OFFICER CENTRAL POLICE DAR ES SALAAMU.
Hakutuma pesa waliwasiliana Kama ndugu wakabila moja la wasukuma ingawa mtuhumiwa siyo msukuma.

7. OCD KISHAPU SHINYANGA
Alitaka kupandishwa cheo na ahamishiwe SHINYANGA Mjini kwani KISHAPU ni kijijini Sana
aliahidi kutuma million mbili lakini kabla hajatuma alipata msiba.

8. MICHAEL DELELI _ Aliyekuwa RTO KILIMANJARO
Alitaka arudishiwe kuwa RTO MOROGORO baada ya kuhamishwa kuwa RTO KILIMANJARO, aliahidi kutoa million moja Ila mtuhumiwa alizima simu yake kwa kuwa anajua kuwa anatafutwa na polisi kwa vitendo vyake hivyo vya kutapeli.

9. MZIRAI _ OCS MEATU
Alitaka apandishwe cheo TOKA ASP kuwa SP na ahamishiwe SHINYANGA Mjini au Kahama sababu alikaa na cheo hicho zaidi ya miaka 08. Alituma 60,000/= za voucher.

10. OCD LUANGWA
Alitaka mtoto wake apate ajira ktk idara ya usalama wa Taifa, aliahidi million moja lakini hakutuma.

11. RTO KAGERA
ALitaka awe RTO MWANZA, aliahidi kutoa million moja baada ya siku tatu lakini hakutuma.

12. OCD TARIME
Alitaka kuwa OCD ILEMELA MWANZA
alituma 200,000/=

13 OCD RUVUMA
Alitaka ahamishiwe Bagamoyo karibu na familia yake, aliahidi million moja lakini hakutoa.

14 RCIO IRINGA CHARLES BUKOMBE
Alitaka arudishiwe nafasi ya RTO na apangiwe MOROGORO, aliahidi kutoa zawadi suala lake likifanikiwa.

15.OCD MAGU
Alitaka ahamishiwe kuja Morogoro au Chalinze ili awe karibu na familia yake, aliahidi million moja lakini hajatuma.

16.RTO TARIME LORYA
Alitaka arudishwe Mwanza, alituma 150,000/=

17. OCD MAKETE
Alitaka ahamishiwe Bagamoyo aliahidi zawadi likifanikiwa.

18. OCD ILAMBA _ SINGIDA
Alitaka ahamishiwe wilaya ya Manyoni, aliahidi million moja lakini hakutuma.

19. OCD BIHARAMULO
Alitaka ahamishiwe GEITA
Aliahidi million moja lakini hakutuma.

20. RTO LINDI
Alitaka ahamishiwe Morogoro, aliahidi zawadi akifanikiwa.

21. OCD TANDAHIMBA
Alitaka ahamishiwe Chalinze, aliahidi 500,000/= lakini hakutoa.

Mtuhumiwa baada ya kukamatwa alipekuliwa maungoni ambamo alikutwa na simu tatu:
ITEL MBILI, TECNO MOJA, RADIO CALL MOJA Aina ya BAOFENG NA CHARGER YAKE MOJA, PESA TASLIMU 55,600/= NA CHARGER YA SIMU MOJA. Pia alipekuliwa katika chumba Namba 05 Cha Guest iitwayo THREE ROOF iliyopo maeneo ya Msamvu ambako alikutwa amefikia na vitu vifuatavyo vilichukuliwa:
Bag moja dogo la mgongoni rangi ya ugoro likiwa na nguo mbalimbali, N_ CARD_ 1000, 0000,0058, 9675, na charger ya simu.
Kesi ya KUJIFANYA AFISA WA SERIKALI IMEFUNGULIWA
Naomba kuwasilisha.
Nauona huu uzi ukipotelea kusiko julikana very soon
 
Sasa makamanda wanakuwaje na tamaa za vyeo ? Ina maana hawajui utaratibu. Wanamuamini vipi mtu ambaye hawajamuona/ kumjua na unashawishika unamtumia hela zote hizo ? Au bwana Otieno alikuwa anatumia mbinu ipi mpaka wanajaa ?
Halafu sisi tukitapeliwa tunategemea tukapeleke mashtaka kwao ambapo nao wana stress za kutapeliwa 😅😅😅😅hapo lazima utapeliwe tena mdi9 maana maafande wakorofi sana
 
Kwangu mimi habari sio huyo jamaa alieyewatapeli, habari ni jinsi jeshi la polisi linavyonuka rushwa...kumbe hata huko Usalama watu wananunua nafasi sio.

Hiyo ni kashfa kubwa sana ndani ya jeshi la polisi, kwa wenzetu walioendelea hao maafisa wote ilibidi waunganishwe na huyo tapeli.
 
Sasa makamanda wanakuwaje na tamaa za vyeo ? Ina maana hawajui utaratibu. Wanamuamini vipi mtu ambaye hawajamuona/ kumjua na unashawishika unamtumia hela zote hizo ? Au bwana Otieno alikuwa anatumia mbinu ipi mpaka wanajaa ?
Huyo inaonyesha wanamjua alikuwa connected mahali na alishawahi fanikisha mambo hadi wakamwamini ila ndio hivyo tena labda connection ilipotea akaendelea tu kupiga pesa kitapeli a maintain life style yake
 
Kwangu mimi habari sio huyo jamaa alieyewatapeli, habari ni jinsi jeshi la polisi linavyonuka rushwa...kumbe hata huko Usalama watu wananunua nafasi sio.

Hiyo ni kashfa kubwa sana ndani ya jeshi la polisi, kwa wenzetu walioendelea hao maafisa wote ilibidi waunganishwe na huyo tapeli.
You have a bright mind
 
Hahaaa ndiomaana waliambiwa wawape hizo kazi watu wenye elimu hawataki ,oogh tunataka la saba ndio matokeo yake haya jitu limebeba manyooota mabegani lakini kichwani hewa, kama lile liliostaafu dodoma sijui wanaliita mbwa koko sijui nani, hovyoooo sasaahivi linahenyea mafao wanalipita kwenye korido kama hawalijui
Ndugu hao maaskari wenye vyeo Hivyo wengi wao ni wasomi wakubwa sana. Huwez kuwa RPC eti una form four, sio jeshi la Sasa. Hata OCD tu huwapiti. Waliopo ni wale wanaoelelea kustaafu. Jeshi Sasa HIV Lina wasomi wengi piah
 
Hii habari sijaielewa Ina maana hao askari ndio wametoa rushwa ama wametoa report ya matukio ya huyo jamaa wanayemshikilia katk vituo vyao vya kazi.
 
Kuna watu wanazania kumbadilisha IGP ndo kutaboresha jesho la Police, kwa kifupi hakuna mwenye uafadhali ndani ya jeshi la police yaani hakuna mwenye uafadhali, Jeshi zima limeoza, Trafiki wanapiga wanagawa pesa hadi wizarani
 
Hao waliotoa rushwa je bado wapo kazini? Kama hawapo kazini kwanini wasiwe jela? Kumbe Rushwa ipo katika mfumo wa kipolisi!
Jeshi la Police hakun mwenye uafadhali, yaani Jeshi zima wanaishi kwa rushwa, unazani hao walio kuwa wanataka wahamishiww Kahama mara Morogoro si ili wapige sawa sawa? Mfano Kahama kuna pesa so kule wangepiga haswa, hili jeshi bila kuja kufumuliwa na kuundwa upya hakuna kitu
 
Back
Top Bottom