Nimekuunga mkono Mkuu....Watu wanafikiri Brigdea Jeneral ni cheo kikubwa sana jeshini kumbe cha kawaida tu ..
Nani kakuambia ni cheo cha kawaida.Umeshawahi pitia angalau JKT.
Ukijua tu maana ya neno brigade utajua sio cheo cha ki sport.
Ngoja nikupe flow chart ya mchoro
Askari mmoja-Section-Platoon-kombania-Kikosi-Battalion-Brigade
askari wakiwa labda tisa inakuwa ni section
section zikiwa angalau 9 zinakuwa platoon
platoon zikiwa mbili au tatu inakuwa ni kombania
Kombania zikiwa sita hadi kumi inakuwa ni kikosi
vikosi vikiwa vingi inakuwa na battalioni
Battalion juu yake ni brigade
Unaposikia ni mkuu wa brigade ya mfano mashariki unaweza kuta anaongoza Dar,Tanga hadi Mtwara
Ukisikia brigade ya kati unaweza kuta ni Tabora,dodoma,
Brigadier ni mtu mkubwa sio wa ki sport hata wakati wa vita vya Kagera kina Musuguri,Mayunga,Marwa,Kombe,Kiwelu,Kimario,Mwita Ernest Kiaro.John Butler Walden walikuwa ni ma brigadier.
Sasa katika medani za kivita ni hivyo ila Jeshini kuna taaluma zingine.
Ukiwa daktari wa jeshi lakini brigadier maana yake kwa taaluma yako hiyo unakuwa unaongoza brigade kwa huo udaktari wako