RPC Arusha na ulinganishi wa vyeo JWTZ na PT

RPC Arusha na ulinganishi wa vyeo JWTZ na PT

unazidi kudhihirisha ujinga wako maana katiba katiba ndio imeainisha kisheria na ndio imefafanua
sasa hiyo maana yako ya endelea kuiokoteza huko wikipedia
Ujinga uko wapi? Kwa hiyo ukii challenge katiba ni ujinga? Unafikiri kwa nini huwa mabadiliko ya katiba hutokea?
 
Ebu nichangie kidogo.
JWTZ na PT kuna commisioned officer na non commssioned officer.

Kwanza tuelewe commissioned officer ni yupi na non commissioned officer ni yupi?

Commissioned officer ni yule anayevikwa vyeo na Amiri mkuu wa jeshi yaani Rais wa nchi kwa wakati huo mfano sasa ni Dr. John pombe Magufuli. Hawa commissioned officer ufanya kaz kwa niaba Rais popote walipo wanamuwakilisha Rais maana haendi vitani.

Non commissioned officer ni yule asiyevikwa na Amiri jeshi au Rais.

Sasa tuje kwenye vyeo;

Nitachambua haraka haraka kidogo

Ila nitachambua vyeo vya kuanzia kamisha. Kwa maelezo zaidi nmefungua kurasa kuhusu mambo ya vyeo.

JWTZ kamisheni uanzia luteni usu(nyota moja) cadet officer au afisa mwanafunzi. Hapa ndipo Rais utunuku vyeo kwa JWTZ.

Polisi tofauti kidogo uanzia Assistant commissioner of Pilice (ACP) yaan kamishna msaidizi wa polisi. Hapa ndo Rais uanzia kutunuku vyeo kwa polisi.

Hapo inamaanisha ACP wa polisi ni sawa na Luteni Usu nyote moja wa JWTZ. Kwahiyo hapo inamaana ACP wa polisi kicheo ni Mdogo kwa Captain wa JWTZ

Pia Tuelewe vyeo vya JWTZ ni vikubwa zaidi ya Polisi maana km ACP ndo utunukiwa vyeo au ndo uanza kuwa kamisha wakt JWTZ huyu ni sawa na Luteni usu ina maana gm 1000 za polisi ni sawa na Kg 1 Za jwtz it means kg 1000 za JWTZ ni sawa na GM mil moja za polisi. Lugha nyepesi twasema Hatua moja za JWTZ ni sawa na hatua 1000 za polisi.

NOTE: ni mdogo kicheo lakini kiutawala ni mkubwa, ACP kapewa mamlaka makubwa kushinda captain mf kamanda wa mkoa au wilaya..

Mkuu umejitahidi kudadavua lakini naona unarudia makosa yaleyale.
hizi ni kada mbili zenye majukumu tofauti.Makamishna wengi huteuliwa na Rais mfano TRA,Bandari,Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nk.Huwezi kulinganisha Kamishna kwa vigezo vya JWTZ.Kila kitengo kina majukumu yake na ambaye hajateuliwa na Rais katika fani fulani haina maana ni mdogo kuliko aliyeteuliwa na Rais katika fani nyingine.
 
Yuko sahihi Assistant Commissioner ni sawa na Canal kwa TPDF rank ya juu yake kwa TPDF ni Brigadea General na Senior Assistant Commissioner kwa wizara ya mambo ya ndani, sijui kuhusu salary scale over.
Labda tuongelee neno Commisioner. Je police ni wakati gani anakuwa commissioned na mwanajeshi anakuwa commisioned wakati gani. Hii inajulikana. Luteni usu anakuwa commisioned so he is a commisioner from nyota moja
 
Kiitifaki ya kupigiwa saluti,Commisioned officer (CP) wa polisi ni sawa na commisioned officer (2lt wa nyota moja) wa Jwtz.

Chini ya Commisioned rank, vyeo hivyo huitwa other ranks.

Kwa hiyo kwa cheo chake cha ACP ukilinganisha na Jwtz ni cheo cha pili kurudi chini ya commisioned officer ambacho ni Warrant officer class2 na hata mishahara ukiichunguza inalingana.

Asijikweze, sababu hata vita vikizuka, akishikizwa jeshini, lazima atapewa mafunzo (refresher) wakufunzi wakiwa ni hao other ranks na atakasimiwa na kuvishwa vyeo vya other ranks na hilo halina ubishi ni kanuni.

Halafu tukija kwenye sheria za kijeshi (military defence act) hao civilian police ni idara za kiraia zinazofanya kazi zinazofanana na za kijeshi, wakiwemo magereza na zimamoto.
Hivyo Jwtz hawaruhusiwi kumkamata raia na kumuweka rumande za jeshi akiwemo yeye, kwa sababu anahesabika kuwa ni raia kwenye vitabu vya sheria za majeshi.
Juu ya hapo vita vikizuka polisi anakuwa ni mpiganaji na mpiganishaji atakuwa 2LT mpaka Captain
 
Juu ya hapo vita vikizuka polisi anakuwa ni mpiganaji na mpiganishaji atakuwa 2LT mpaka Captain

Hatuongelei Vita.Hapa tunaongelea muktadha alioongea RPC wa Arusha kwamba ana uwezo wa kumchukulia hatua mwanajeshi yoyote isipokuwa Brig.General na kwenda Juu.
Vita kati ya Nchi na Nchi ni Majukumu waliyopewa kuyafanya JWTZ na sio Polisi.Sio busara kutaka Polisi wafanye majukumu yasiyo yao.Ni sawa na kumwambia Kamishna wa TRA aende vitani kwa sababu nae ni Commissioned Officer au Officer wa JWTZ aende kukusanya Kodi kwa sababu ni Commissioned Officer.Kila Kada ina majukumu yake.
 
Labda tuongelee neno Commisioner. Je police ni wakati gani anakuwa commissioned na mwanajeshi anakuwa commisioned wakati gani. Hii inajulikana. Luteni usu anakuwa commisioned so he is a commisioner from nyota moja

Hapa ndipo sielewi kabisa maana naona tunaenda nje ya mada.
Sasa tukishajua nani ni Commissioned ndio tutajua nani ana mamlaka kati ya Luteni Usu na Mkuu wa Polisi wa Mkoa(RPC)?.
 
kwahiyo ishu ni siraha sio!!

unawajua alshabaab,unajua kuna vyuma wanavyo havijawahi kushikwa na askari yeyote yule chini ya ardhi ya tz[emoji16][emoji16].

je kwa kigezo hicho wanapaswa kuitwa jeshi zaidi ya jwtz?
Hawapaswi kuitwa jeshi kwasababu halikuundwa na serikali ya tanzania, halina mashiko kwenye NDA
 
Mr Pianoman huelewi ulichoandika.
Commisioned officer anapewa na Rais wa nchi si vinginevyo.
JWTZ kuanzia 2Lt ni commisionend officer.
Wengine ni other ranks.
Vyeo vya Police ni non commisioned offrs labda makamishena waliopewa na Rais kiutaratibu kiutawala.
Jibu liko wazi, mmeelewa??
 
Wewe jamaa hapa umeongea pumba tupu.
Kama polisi hawana silaha zenye nguvu wanapambana vipi na majambazi au majangiri?
Wanapambana nao kwa silaha za kawaida, sio silaha kubwa, smg ni silaha ya askari mmoja mmoja, ninapoongelea silaha kubwa naongelea mizinga, mabomu, othwr weapon beyond smg buddy!
 
Kuwa usalama wa raia sio kigezo Cha kutokuwa jeshi bali huo ni mgawanyo tu wa majukumu.
Au wewe ulitaka majeshi yote yakalinde mipakani halafu huku mitaani Nani angetoa huduma?
Umechanganyikiwa wewe sio bure, jeshi huwaga halijihusishi na majukumu ya kushughulika na raia, labda inapotokea mamlaka za kirai zinaposhindwa ndipo jeshi hufanya kazi kwa kusaidia mamlaka za kiraia.
 
Mr Pianoman huelewi ulichoandika.
Commisioned officer anapewa na Rais wa nchi si vinginevyo.
JWTZ kuanzia 2Lt ni commisionend officer.
Wengine ni other ranks.
Vyeo vya Police ni non commisioned offrs labda makamishena waliopewa na Rais kiutaratibu kiutawala.
Jibu liko wazi, mmeelewa??
rais hatoki comm kwa wanajeshi au polisi pekee,mpaka tra anatoa comm.

swali ni je ni sawa kuwasaluti hao makamishna tra[emoji16][emoji16]
 
Ni kwel mkuu polisi kupande cheo ningumu sana kuliko ngamia kupenya kwe tundu lasindano tofauti na Jwtz vijana wadogo utawaona wana nyota au V ambapo ukienda polisi nivingumu kumkuta kijana ana miaka27 ana nyota au ata V3 , ninge mshauli Rais awapeleke viongoz wa jwtz wakaibadilishe polis kwenye utaratibu wakupanda vyeo.
Ilitokea kipindi cha nyuma, kuna mmoja alipelekwa huko na ndipo alikuwa na kauli ya kuiita polisi kuwa ni jeshi na ndio imepelekea hadi sasa wanajiita jeshi.
 
Wanapambana nao kwa silaha za kawaida, sio silaha kubwa, smg ni silaha ya askari mmoja mmoja, ninapoongelea silaha kubwa naongelea mizinga, mabomu, othwr weapon beyond smg buddy!
smg haijawahi kuwa silaha ya kawaida.ndio maana ni marufuku kampuni ya ulinzi kuwa nayo.

hata hizo kubwa inategemea unaziangaliaje,captain wa urusi anaongoza combania yenye silaha kubwa kuliko combania ya kibongo,je captain wa kibongo ni mdogo kwa captain wa kirusi??
 
Ilitokea kipindi cha nyuma, kuna mmoja alipelekwa huko na ndipo alikuwa na kauli ya kuiita polisi kuwa ni jeshi na ndio imepelekea hadi sasa wanajiita jeshi.
unataka kusema alienda kuandika katiba pia?
 
kwa mujibu wako wewe au?

Kwa mujibu wa katiba hayo ni Majeshi

ova
Mzee baba usijilishe Upepo na kujitoa ufahamu... Lugha ya kiswahili inaupungufu mkubwa wa Misamiati... Hivyo neo JESHI kwa Convinience likabidi litumike pia kwa hivyo vyombo vingine vya Kiraia...

Nyie ni POLICE FORCE and NOT ARMY/ MILITARY.....
 
A wishful thinking!! Polisi ni idara ya kiraia. Kijeshi kuna commissioned na non commissioned. Sasa huwezi kumlinganisha gazetted officer wa polisi na commissioned officer a jeshi. Vyeo vya makamishina hutolewa na rais, ambapo kuanzia luteni usu jwtz. Mwenye nyota moja jw ni kamishna, hiyo ni fact, huwezi kumlinganisha na gazetted officer.
Huu Ukweli sijui kwanini hawataki kuusikia.. Ila wanafahamu na pia nasikia wanafundishwa....

hizi ni siasa wanataka kuleta
 
smg haijawahi kuwa silaha ya kawaida.ndio maana ni marufuku kampuni ya ulinzi kuwa nayo.

hata hizo kubwa inategemea unaziangaliaje,captain wa urusi anaongoza combania yenye silaha kubwa kuliko combania ya kibongo,je captain wa kibongo ni mdogo kwa captain wa kirusi??
Hapo ni kutokana na jeshi lao na uwezo walionao zaidi kwenye vifaa. Pia kumbuka hata hao Russian Police wana uwezo wa vifaa lakini bado wanaitwa Polisi na sio jeshi la polisi

 
Back
Top Bottom