Yaliyojiri kesi inayomkabili Mbowe na wenzake leo Februari 4, 2022. Kesi imeahirishwa. Shahidi wa 13 kuendelea kutoa ushahidi Februari 7, 2022

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,800
Habari Wakuu,

Leo 04/ 02/ 2022 shahidi wa 13 anatarajiwa kuanza kutoa ushahidi wake kwenye kesi inayomkabili Mbowe na wenzake 3.

Kujua Kesi ilipoishia fungua kiungo hiki: Yaliyojiri kesi ya Mbowe 01/02/2022. Luteni Denis Urio amaliza kutoa ushahidi wake. Shahidi wa 13 kuanza 04/02/2022

Updates:


Jaji ameingia Mahakamani

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani

Wakili wa Serikali Robert Kidando Ikupendeze Mheshimiwa Jaji naitwa Robert Kidando nipo pamoja na wakili:
  • Abdallah Chavula
  • Jenitreza Kitali
  • Nassoro Katuga
  • Esther Martin
  • Ignasi Mwinuka
  • Mawakili Wa Serikali Waandamizi na,
  • Tulimanywa Majige, Wakili wa Serikali
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na wakili:
  • Michael Mwangasa
  • Gaston Garubindi
  • Michael Lugina
  • Sisty Aloyce
  • Iddi Msawanga
  • Maria Mushi
  • Evaresta Kisanga
  • Khadija Aaron
  • Dickson Matata
  • John Mallya
  • Nashon Nkungu
Kibatala: Kwa nafasi ya pekee naomba kumtambulisha Wakili Alute Mughwai Lissu, Pamoja Kwamba hayupo katika Quorum yetu, lakini ni mgeni wetu wa pekee leo.

Wakili Alute Mughwai Lissu: Mheshimiwa Jaji Kwa nafasi ya pekee nashukuru kuwepo mahala hapa na kusikiliza shauri hili

Jaji: karibu sana

Jaji anaita Washitakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na Leo tuna shahidi Mmoja, Tupo tayari Kuendelea

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Nasisi pia tupo tayari Kuendelea

Jaji: shahidi wa ngapi

Wakili wa Serikali: Mh Jaji Shahidi Wa 13

Shahidi: NAITWA Tumaini Sostenes Swila, miaka 46, Kabila mndali, dini mkiristo, kazi ni Askari Polisi

Shahidi: Naapa Mbele ya Mahakama hii Kuwa Ushahidi nitakao toa utakuwa wa kweli, kweli tupu Eehee Mwenyezi Mungu Nisaidie

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Shahidi Unasema Unaitwa nani

Shahidi: Tumaini Sostenes Swila

Wakili wa Serikali: Robert Kidando Unafanya kazi gani

Shahidi: Ni Askari Polisi

Wakili wa Serikali: Una Cheo gani

Shahidi: Ni Mkaguzi wa Polisi

Wakili wa Serikali: Kituo Chako Cha Kazi?

Shahidi: Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi, Mkoa wa Kipolisi Temeke

Wakili wa Serikali: Majukumu yako ni yapi

Shahidi: Ni Kuzuia, Kukamata, na Kupeleleza Makosa ya Jinai

Wakili wa Serikali: Kazi hiyo sasa umefanya Kwa Muda gani

Shahidi: Miaka 24

Wakili wa Serikali: Katika Shughuli hiyo ya Upelelezi, Kitu gani hasa unafanya

Shahidi: Shughuli Mbalimbali Katika Upelelezi, ikiwemo Kukagua Eneo la Tukio, Kuchora eneo la Tukio, Kuku Sanya Vielelezo, Kuhoji Mashahidi, Kukamata Watuhumiwa, kuwahoji Watuhumiwa, Kuandaa Barua Mbalimbali za Kuomba Uchunguzi wa Vielelezo, Kupeleka Vielelezo Maabara, Kuchukua Maandishi ya Sampuli za Watuhumiwa, Kuandaa Taarifa za Wapelelezi, Kusimamia Gwaride la Utambuzi wa Watuhumiwa, Kuwafikisha Watuhumiwa Mahakamani ikiwa ni pamoja na Kutoa Ushahidi Mahakamani

Wakili wa Serikali: Umesema Umekuwa Katika Upelelezi Kwa Miaka Mingapi

Shahidi: 24

Wakili wa Serikali: Taaluma ya Upelelezi Umepataje

Shahidi: Kwa kuhudhuria Kozi Mbalimbali pamoja na uzoefu Kazini

Wakili wa Serikali: Unasema huko Mkoa Wa Kipolisi Temeke, Ofisi ya RCO, Elezea upo Kwa Muda gani Katika Kituo hicho cha kazi

Shahidi: Nipo tangu OCTOBER 2015, Lakini Ulipofika Mwezi January Mwaka 2020 nilipata Uhamishoni wa Muda Kwenda Makao Makuu Ndogo ya Upelelezi, Jijini Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Baada ya Kupata uhamishoni huo wa Muda, Ieleze Mahakama Ulikaa Kwa Muda gani

Shahidi: Nilianza Kufanya Kazi Ofisi ya Makao Mkuu ya Upelelezi toka January 2020 Mpaka August 2021 nikarudi Kituo Changu Cha kazi

Wakili wa Serikali: Na wakati Unapata uhamishoni Wa Muda, kwenda Ofisi Ndogo ya Upelelezi, Ni Shughuli gani ulikuwa unafanya

Shahidi: Nilikuwa Nafanya kazi Katika Kitengo X

Jaji: Rudia Kitengo gani

Shahidi: Kitengo X

Jaji: Unaweza Ku-spell

Shahidi: X ya herufi Wakili wa Serikali: Kitengo X kinajishughulisha na nini

Shahidi: Makosa yanayotishia Usalama wa nchi pamoja na Ustawi wa Taifa

Wakili wa Serikali: Katika Makosa yanayotishia Usalama na Ustawi wa Nchi, Kitu gani Kina fanyika haswa

Shahidi: Kina husika na Makosa yanayotishia Usalama Wa Nchi, Nchi Nzima

Wakili wa Serikali: Sasa Ukiwa hapo ulikuwa na nafasi gani?

Shahidi: Nilikuwa naendelea na Upelelezi pamoja na Makosa Mengine

Wakili wa Serikali: Hebu Elezea Mnamo Tarehe 14 July 2020 ulikuwa wapi na unafanya nini

Shahidi: Nilikuwa Katika ofisi Za Mkurugenzi Wa Makosa ya Jinai Nchini, Ofisi Ndogo za Dar es Salaam, Nikiendelea na Majukumu yangu Ndipo nilipopokea Simu Kutoka Kwa Katibu muhtasi Kutoka Kwa Mkurugenzi Wa Makosa Ya Jinai Nchini, akitaka ni file katika Ofisi Ya Mkurugenzi wa Makosa Ya Jinai Nchini Wakati huo alikuwa Afande Robert Boaz

Wakili wa Serikali: Baada ya Kupokea Wito huo Ulifanya nini

Shahidi: Nilienda Moja kwa Moja Mpaka Ofisi ya Mkurugenzi Wa Makosa ya Jinai Nchini, Nikawakuta Afande Robert Boaz na Ramadhan Kingai

Wakili wa Serikali: Ilikuwa Muda gani

Shahidi: Majira ya Saa 4 Asubuhi

Wakili wa Serikali: Ulichukua Muda gani Kufika

Shahidi: Ilikuwa kama Dakika 15 Kufika Ofisi Ya Mkurugenzi wa Makosa Ya Jinai

Wakili wa Serikali: Baada ya Kukuta DCI pamoja na Kingai nini kiliendelea

Shahidi: Baada ya Kuwakuta Pamoja Kamishina ROBERT BOAZ wakati huo akiwa DCI alinitaka Kupokea Maelekezo Kutoka Kwa Afande Ramadhan Kingai ambaye ni Kamishina Msaidizi wa Polisi

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuwa DCI Kukwambia Upokee Maelekezo hayo nini kiliendelea

Shahidi: Baada ya Kupokea Maelekezo hayo tukitoka Pamoja na Afande Ramadhan Kingai Kamishina wa Polisi, Ofisini Kwangu, Akanipa Maelekezo Ya Kufungua Jalada la Uchunguzi Maelekezo hayo alinipa takiwa tayari yameandikwa katika Karatasi

Yalikuwa yanaeleza kuwa Mnamo tarehe 14 July 2020 Majira ya Saa 2 na Nusu Asubuhi, Mkurugenzi Wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai ROBERT BOAZ Kamishina Msaidizi Wa Polisi alipokea Taarifa Kutoka Kwa Luten Denis Urio, Juu ya Uwepo wa Kundi linaloratibiwa na Freeman Aikael Mbowe la Kutaka Kufanya Vitendo Vya Uhalifu.. Ambavyo ni Kulipua Vituo Vya Kuuzia Mafuta, Kuchoma Masoko Moto pamoja na Maeneo yanye Mikusanyiko wa Watu wengi, Kukata Miti Mikubwa katika Barabara Kuu kwa Lengo la Kuzuia Magari yasipite, Kufanya Maandamano Nchi Nzima yasiyokuwa na Ukomo, Na Kuwadhuru Viongozi Mbalimbali Wa Serikali.. Kwa Lengo la Kuleta Taharuki Nchini kufanya Nchi isitawalike..

Wakili wa Serikali: Elezea Kuilezea hiyo Taarifa

Shahidi: Na Matendo hayo yalipamgwa Kufanyika Katika Mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Arusha na Kilimanjaro

Wakili wa Serikali: Endelea Kueleza Kilichotokea Baina yako na Kingai

Shahidi: Baada ya Kupokea Maelekezo hayo alinitaka nifungie Jalada Kisha nipeleke Ofisi Ya DCI, Nilienda Moja kwa Moja katika Ofisi Inayohusika na Kitabu cha Kufungua Majalada, Ofisi Ya Mnadhimu, Ambapo Nilienda na Kuchukua Kitabu hicho na Kufungua Jalada la Uchunguzi lenye Kumbukumbu namba CD HQ/PE/60/2020

Wakili wa Serikali: Elezea hizo Taratibu za Kufungua hilo Jalada baada ya Kuchukua hichi Kitabu

Shahidi: Kitabu Kile Kina onyesha Tarehe ya Kifungua, Muda, Jina la Mlalamikaji na Taarifa Yenyewe

Wakili wa Serikali: Wakati unafungua Jalada hilo, Mlalamikaji alikuwa nani

Shahidi: Mlalamikaji alikuwa Afande Robert Boaz Kamishina Wa Polisi na Mkurugenzi wa Makosa Ya Jinai Nchini

Wakili wa Serikali: Nani alikuwa analalamikiwa

Shahidi: Mlalamikiwa katika Jalada hilo alikuwa ni Freeman Aikael Mbowe

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuwa Umefungua Jalada hilo, Ulifanya nini?

Shahidi: Baada ya Kufungua Jalada hilo, niliweza Kuandika Minutes Kwenda Kwa Mkurugenzi Wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, nikimkulisha Kuwa nimefungua Jalada la Uchunguzi dhidi ya Freeman Mbowe, Kwa Kutaka Kufanya Vitendo Vya Uhalifu, Kama ambavyo nimevitaja hapo Juu, nikaandika, Naleta Jalada Kwako Kwa Maelekezo zaidi

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuwa Umeandika hiyo Minute's Ulifanya nini sasa na hilo Jalada

Shahidi: Nilienda Moja kwa Moja Mpaka Ofisini Kwa Mkurugenzi wa Makosa Ya Jinai

Wakili wa Serikali: Baada ya Kupeleka Jalada hilo nini Kilifuata

Shahidi: Siku ya Tarehe 15 July 2020 Saa 5 Asubuhi nikiwa Katika Ofisi Ya Mkurugenzi wa Makosa Ya Jinai, Nilikabidhiwa Jalada hilo la Uchunguzi ambalo Kumbukumbu namba zake nilizitaja ambalo lilikuwa limetolewa Maelekezo na Robert Boaz Kamishina Wa Polisi na DCI Akinitaka nimsaidie Kamishina Msaidizi Wa Polisi Ramadhan Kingai Kufanya Upelelezi, ambaye wakati huo alikuwa ni RCO wa Arusha

Wakili wa Serikali: Maelekezo yaliyolewa kwenda kwa nani

Shahidi: Maelekezo Yakitolewa Kwemda Kwa Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi Wa Polisi Pamoja na Mimi Kumsaidia Upelelezi

Wakili wa Serikali: Hayo Maelekezo ya Kumsaidia ACP Kingai Yalikuwa ni Maelekezo gani

Shahidi: Yalikuwa ni Maelekezo Ya Kutaka ACP kingai Kuendelea Kuwasiliana na Mtoa Taarifa ili aweze Kumtafutia Watu ambao Walikuwa Wanahitajika na Freeman Mbowe Katika Kutenda Vitendo hivyo Maelekezo Yalikuwa pia Kuwa Alikutana nao Watu hao, awape tahadhari ya Vitendo ambavyo wataenda Kukutana navyo huko

Wakili wa Serikali: Dhumuni hasa la Maelekezo hayo yalikuwa ni nini

Shahidi: kupata Taarifa na Kuwajua Watu Wanaoshirikiana na Freeman Mbowe, Na Pia Watu ambao Watakuwa wamepatikana Kutoka kwa Luten Denis Urio afikishwe kwa ACP Ramadhan Kingai Kisha na Yeye afikishe kwa DCI

Wakili wa Serikali: Sasa Baada ya Kuwa Umepewa Jalada na Maelekezo hayo Ulifanya nini

Shahidi: Miliwasiliana kwa al Simu na ACP Ramadhan Kingai ambaye kwa wakati huo alikuwa Arusha, Baada ya Kumjulisha alisema lihifadhi Jalada hilo nitakupa Maelekezo

Wakili wa Serikali: Baada ya Sasa Kuwa Umemjulisha ACP Kingai, Nini Kiliendelea Katika Ushauri huo Shahidi Baada ya Kuwasiliana na ACP kingai na Kumjulisha Maelekezo ambayo yapo Katika Jalada na Yeye Kuniambia Kuwa ni hifadhi, Niliweza Kuandika Taarifa ya Kukiri Kupokea, KishaNika hifadhi Jalada hilo katika kabati langu la Chuma ambapo natumia Kuhifadhi Vifaa Vyangu Vya kazi..

Wakili wa Serikali: Baada ya Mawasiliano hayo na Kingai nini Kiliendelea

Shahidi: Mnamo Tarehe 18 July 2020 nikiwa naendelea na Majukumu Yangu katika Ofisi Ndogo ya DCI Nilipokea Simu Kutoka Kwa Afande Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi Wa Polisi, akinijulisha kuwa Luteni Denis Urio tayari amepata Vijana Wa Kuwapeleka Kwa Freeman Aikael Mbowe Na akanitaka niende Kufungua Jalada la Kesi katika Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Unamaanisha Nini Ukisema Kufungua Jalada la kesi

Shahidi: Ni Jalada ambalo linafunguliwa katika Report Book tofauti na lile Jalada la Upelelezi na Linafunguliwa katika Vituo Vya Polisi Pia alini elekeza baada ya Kufungua Jalada hilo niongee na Mkuu Upelelezi Mkoa wa Polisi Wa Ilala aweze Kuhamisha Jalada hilo Ofisi Ya Mkurugenzi wa Makosa Ya Jinai Nchini

Wakili wa Serikali: Wewe Ukafanya nini

Shahidi: Niliweza kwenda Kufungua Jalada hilo Kama nilivyo elekezwa na ACP kingai, Nika Fungua Jalada la Kutaka Kula Njama Kutenda Vitendo Vya Kigaidi

Wakili wa Serikali: Baada ya Kupokea Maelekezo hayo Shughuli hiyo Uliweza Kutekelezaje

Shahidi: Niliweza Kufika Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam, Nika Fungua Jalada hilo, Mlalamikaji Robert Boaz Kamishina Wa Polisi, Jalada hilo alinielekeza Kufungua Kuwa Mnamo Mwezi kati ya May na July 2020 Kuna Kundi la Watu Wamepanga Kufanya Vitendo Vya Kigaidi Katika Mikoa Mbalimbali Nchini, Kwa Lengo la Kuleta Taharuki, Na Nchi isitawalike Aidha nilifungua Taarifa hiyo Kufuatia Maelezo Ya ACP kingai ambaye alitaka nisiandike Jina la Mtuhumiwa Freeman Aikael Mbowe Katika Taarifa hiyo, Ili kuepusha uvujaji wa Taarifa Kwani kama Jina lake lingekwepo katika Taarifa hiyo angeweza Kujua na Kusitisha Utekelezaji wa alilokuwa amepanga pamoja na Wenzake..

Wakili wa Serikali: Kitu gani Kingine kiliendelea Shahidi: Baada ya Jalada Kufunguliwa ambapo lilikuwa na Kumbukumbu namba CD/IR /2097 /2020 Nilimjulisha ambaye alikuwa kaimu Mkuu Wa Upelelezi Mkoa wa Ilala ambapo wakati huo alikuwa FADHIL BAKARI

Wakili wa Serikali: Sasa Baada ya Kumjulisha ACP FADHIL BAKARI nini kiliendelea

Shahidi: Niliondoka na Kuendelea na Kazi Zingine

Wakili wa Serikali: Sasa Elezea baada ya Siku ya Tarehe 18 July 2020, Nini Kiliendelea

Shahidi: Mnamo Tarehe 27 July 2020 nikiwa Ofisi Ndogo ya Upelelezi Dar es Salaam Nilipokea Jalada lenye Kumbukumbu namba CD /IR/2097 /2020 Kosa Kula Njama za Kutaka Kufanya Vitendo Vya Kigaidi

Jalada hilo lilikuwa limetolewa Maelekezo na Afande Robert Boaz Kamishina Wa Polisi na Mkurugenzi wa Upelelezi Makosa Ya Jinai Nchini akitoa Maelekezo Kwa Afande Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi Wa Polisi Pamoja na Mimi akitutaka tuendelee na Upelelezi Wa Kosa hilo

Wakili wa Serikali: Sasa Kitu gani Kingine kiliendelea Shahidi: Niliweza Kumjulisha Afande Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi Wa Polisi, kuwa nimepokea kwa niaba yako Jalada Na mimi ni Msaidizi Wako katika Upelelezi Wa Jalada hilo

Wakili wa Serikali: Baada ya Kumjulisha Kingai nini hasa kiliendelea

Shahidi: aliniambia Kuwa yeye anaendelea na Ufutailiaji na Mtoa Taarifa, atanipa Maelekezo ya Nini cha Kufanya

Wakili wa Serikali: Baada ya hapo sasa, Kitu gani hasa kiliendelea katika Jalada hili

Shahidi: Nilikiri Kupokea Jalada hilo Kisha nikalitumza katika Kabati langu la Chuma, Ilipo fika Tarehe 06 August 2020 Mimi nikiwa hapa Dar Es Salaam Majira ya Saa 2 Usiku, Nilipokea Simu Kutoka Kwa Afande Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi Wa Polisi akinijulisha Kwamba Tayari Wamekamatwa Watuhumiwa Wawili na Wapo Njiani Kuja nao Dar es Salaam kwa ajili ya Kuendelea na Upelelezi zaidi Akaniambia akifika atanijulisha..

Wakili wa Serikali: Baada sasa ya Kukupa Taarifa hiyo, Elezea Kama alilufamisha Kuhusu Watuhumiwa hao Wamekamatwa wapi na wakina nani

Shahidi: Alichokisema ni kwamba amekamata Watuhumiwa Wawili Katika Mji wa Moshi hakuniambia Majina

Wakili wa Serikali: Sasa Baada ya ACP Kingai Kukupa Taarifa hiyo Shahidi: Ilipo fika Tarehe 07 August 2020 Majira kati ya Saa 11 na Saa 12 Alfajiri nilipigiwa Simu na Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi Wa Polisi akinitaka nikutane naye Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam Mapema Saa 1 Asubuhi

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji samahani kabla ya kuendelea Kuna jambo moja naomba tukutane faragha na wenzetu kuhusu mwenendo wa kesi hii..

Wakili Peter Kibatala: Sawa mheshimiwa Jaji

Jaji: Kwa muda gani

Wakili wa Serikali: Kwa dakika 10 mpaka 15

Jaji anatoka Mahakamani (11:27 AM)

Jaji amerejea Mahakamani (11:37 AM)

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Kwa Upande wa Jamhuri tupo tayari Kuendelea

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Nasisi tupo tayari Kuendelea

Jaji: sehemu ya Mwishoni alisema alieleza Kufika Kituo cha kati Kati ya Saa 11 na 12 Asubuhi

Wakili wa Serikali: Baada ya Kupokea Maelekezo Hayo wewe Ulifanya nini

Shahidi: Nilijiandaa Kwenda Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam ambapo Nilifika kabla ya Saa 1 Asubuhi

Wakili wa Serikali: Ulipofika hapo Ulifanya nini

Shahidi: Niliweza Kumkuta Afande Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi Wa Polisi akiwa pamoja na Askari Wawili ambao siwafahamu na Mmoja nilikuwa Namfahamu ambaye ni ASP Jumanne Malangahe, Wale wawili Nilikuja kuwafahamu baadae ambao ni Inspector Mahita na Constable Goodluck

Wakili wa Serikali: Na unasema Ulimkuta ACP kingai na ASP Jumanne, hivi ASP Jumanne yeye Ulimfahamu vipi

Shahidi: ASP Jumanne nilimfahamu zaidi Ya Miaka 10 Wakati akiwa anafanya Kazi Mkoa wa Pwani

Wakili wa Serikali: Sasa hawa wakina ACP Kingai na ASP Jumanne uliwakuta Sehemu gani pale Kituo cha Polisi

Shahidi: Niliwakuta Nje ya Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam, Ambapo Afande Kingai alinitaka nipokee Simu Mbili Kutoka Kwa Goodluck ambapo zilikatwa Kutoka Moshi Kwa Watuhumiwa. Nilipokea Simu Mbili, Moja aina ya Itel Nyeusi na Nyingine ni Tecno Nyeusi pia

Wakili wa Serikali: Baada ya akuzipokea ikafuata nini baada ya Kukabidhiwa

Shahidi: Afande Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi Wa Polisi alinitaka pia Nikabidhiwe Maelezo Ya Mashahidi yaliyo andikwa huko Moshi pamoja na Hati za Kuchukulia Mali

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuwa Umemkabidhiwa Vitu hivyo Ulifanya nini

Shahidi: Nilichukua na Kwenda kuvihifadhi katika Kabati langu la Chuma lilipo katika Ofisi ambayo nilikuwa natumia katika Makao Makuu Madogo Ya Upelelezi Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Kwa Siku hiyo Kitu gani kiliendelea

Shahidi: Afande Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi Wa Polisi alinitaka nishirikiane na Inspector Mahita na DC Goodluck Kuhusu Watuhumiwa Wengine Kwa Lengo La kuwakamata

Wakili wa Serikali: Hebu fafanua katika Eneo la Ufutailiaji

Shahidi: Siku hiyo alituelekeza tumfuatilie Mtuhumiwa Khalfani Bwire Katika Maeneo ambayo Taarifa Zimeelekeza

Wakili wa Serikali: Maelekezo hayo walikuwa Wamepewa akina nani

Shahidi: Inspector Mahita, na Mimi Mwenyewe

Wakili wa Serikali: Sasa Baada ya Kukwambia Kuwa kuna Watuhumiwa ambao walikuwa wamekamatwa, Hebu elezea ni Watuhumiwa gani walikuwa Wamekamatwa

Shahidi: Ni Adam Hassan Kasekwa na Mohamed Abdilah Ling'wenya ambapo Watuhumiwa hao nilikuwa nimekabidhiwa simu zao

Wakili wa Serikali: Ni wakati gani Ulifahamu Kuwa Watuhumiwa hawa walikamatwa

Shahidi: Ni baada ya Kukabidhiwa Simu. Adam Mbali na Kuwa na Simu aina ya Itel, Kwenye hati ya Kukamatia Mali pia ilionyesha amekamatwa na Bastola aina ya Luger yenye namba 5340

Wakili wa Serikali: Rudia tena namba

Shahidi: 5340

Wakili wa Serikali: Kwa Ling'wenya Alikamatwa na nini

Shahidi: Simu aina ya Tecno ambayo ilikuwa na Rangi Nyeusi

Wakili wa Serikali: Umezungumzia Kuhusu Kuchukua Simu Mbili na Hati za Kukamatia Mali, Elezea Watuhumiwa hao wakati Unamkabidhi wa Walikuwa Wapi

Shahidi: Wakati huo Asubuhi Sikuweza Kuwaona, ila walikuwa Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Hebu Elezea sasa Maelekezo ya Kufuatilia Taarifa za Khalfani Bwire mliyatekelezaje

Shahidi: Tulifutilia Maeneo Mbalimbali Kulingana na Taarifa zilizokwepo, Ilipo +fika Majira ya Saa 5 Asubuhi, nilipigiwa Simu na Afande Jumanne Malangahe wakati huo akiwa Mrakibu wa Polisi walitaka nirudi iliniweze Kukabidhiwa Maelezo Ya Watuhumiwa ambao Walikuwa wamemaliza Kuwahoji yeye na Afande Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi Wa Polisi

Wakili wa Serikali: Elezea Sasa Mkiwa Na Mahita na Goodluck ni Maeneo gani Mlifuatilia hizo Taarifa

Shahidi: Tulifutilia Maeneo ya Sinza, Oysterbay na Coco beach na Baadae Temeke

Wakili wa Serikali: Wakati Unapigiwa Simu na ASP Jumanne ulikuwa wapi

Shahidi: Wakati huo nilikuwa Maeneo ya Sinza

Wakili wa Serikali: Baada ya Kupokea Simu Ulifanya nini

Shahidi: Mimi na Wenzangu Tulirudi Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam ambapo ASP Jumanne aliweza Kunikabidhi Maelezo ya Mohammed Ling'wenya wakati huo ACP kingai aliweza Kunikabidhi Maelezo Ya Adam Kasekwa

Wakili wa Serikali: Sasa Maelezo haya Ulikabidhiwa Ukiwa wapi

Shahidi: Nilikabidhiwa Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuwa umepokea Maelezo hayo ya Watuhumiwa Wawili Wewe Ulifanya nini

Shahidi: Niliyachukua na Kuyapeleka katika Ofisi niliyokuwa natumia katika Makao Makuu Ndogo ya Upelelezi Dar es Salaam na Kuhifadhi katika Jalada Kisha katika Kabati la chuma

Wakili wa Serikali: Ulisema Wakati huo ulikuwa Ofisi ya DCI Makao Makuu Ndogo Dar es Salaam, na Umekuwa Ulielezea hapa Kufuata Maelezo Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam na Vielelezo Vingine, Kwanini ilikuwa hivyo

Shahidi: Kwa sababu pale Ndipo Jalada lilipo kuwa limefumguliwa na Watuhumiwa walipokuwa wamefilishwa kwahiyo Shughuli Nyingi zilikuwa zinafanyikia pale

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuwa umechukua Maelezo ya ASP Jumanne na ACP kingai nini Kiliendelea

Shahidi: Mimi na Wenzangu Inspector Mahita, DC Goodluck Tuliendelea na Zoezi la Kumtafuta Khalfani Bwire Kwa Kurudi Eneo la Sinza

Wakili wa Serikali: Maeneo gani ambayo Mlienda.

Shahidi: Temeke tulifika Saa 12 Jioni

Wakili wa Serikali: Baada ya hapo Nini sasa kiliendelea

Shahidi: Tulihairisha Kuendelea na Zoezi hilo mpaka Siku inayofuatia

Wakili wa Serikali: Siku inayofuatia ni Siku gani

Shahidi: Ni Siku ya Tarehe 08 August 2020 Majira ya Saa nne Asubuhi, Nikiwa Katika Ofisi Ya Mkurugenzi wa Makosa Ya Jinai, nilipigiwa Su na Afande Jumanne Malangahe Mrakibu Msaidizi Wa Polisi, Alinitaka nifike Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam kwa ajili ya kazi

Wakili wa Serikali: Elezea Kama Ulifanya Maelekezo aliyokupa

Shahidi: Nilifika Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam Muda Mfupi Nikakuta yupo a Inspector Mahita na DC Goodluck akanijuliisha kuwa amepewa Maelekezo na Afande Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi Wa Polisi ya kuhamisha Watuhumiwa Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya Kutoka Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam na kuwapeleka Kituo cha Polisi Mbweni

Wakili wa Serikali: Baada sasa ya hapo Nini sasa kiliendelea

Shahidi: Tukiwa chukua Watuhumiwa hao kutoka Mahabusu ya Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam na Kuwasafirisha kwa kutumia Gari na Kwenda nao Kituo cha Polisi Mbwe

Wakili wa Serikali: Na Ulisema Maelezo hayo ya kuhamisha Watuhumiwa yalikuwa yanahusu Watuhumiwa gani

Shahidi: Ni Adam Hassan Kasekwa na Mohamed Ling'wenya

Wakili wa Serikali: Mlitumia Gari gani

Shahidi: Gari ya Polisi ambayo alikuja nayo Ramadhan Kingai Kutoka Mkoa wa Arusha, Gari aina ya Fortuner

Wakili wa Serikali: Kituo cha Polisi Mbweni Kipo wapi

Shahidi: Kanda Maalum Ya Dar es Salaam, Mkoa wa Kipolisi Kinondoni na Wilaya ya Kipolisi Kawe

Wakili wa Serikali: Akina nani wengine Walishiriki zoezi hilo

Shahidi: zoezi liliongozwa na ASP Jumanne Malangahe, Inspector Mahita na Constable Goodluck

Wakili wa Serikali: Na wewe Ulishiriki Vipi

Shahidi: Na Mimi pia nilishiriki

Wakili wa Serikali: Iliwachukia Muda gani Kufika Kituo cha Polisi Mbweni

Shahidi: ilichukua Muda Usiozidi Saa 1

Shahidi: Leo anaongea taratibu Kuliko Mashahidi wote ambao waliwahi Kufika Katika kesi hii, Kila Muda Jaji na Mawakili wa Serikali Wanamkemea na Kuomba aongeze Sauti

Wakili wa Serikali: Kitu gani Kingine kiliendelea Kule Kituo cha Polisi Mbweni

Shahidi: ASP Jumanne alimuagiza Inspector Mahita Kuwakabidhi Watuhumiwa katika Chumba Cha Mashtaka

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuwakabidhi Watuhumiwa katika Chumba Cha Mashitaka nini kiliendelea

Shahidi: Baada ya Kuwakabidhi Watuhumiwa hao Tuliendeleana zoezi la Kutafuta Watuhumiwa Wengine, liliongozwa na ASP Jumanne ambapo alikuwa anaendelea Kupokea Taarifa, akiwepo Mtuhumiwa Khalfani Bwire

Wakili wa Serikali: zoezi kiliendelea kwa namna gani

Shahidi: Tuliendelea Kuwatafuta Watuhumiwa hao Mpaka Saa 1 Usiku

Wakili wa Serikali: Saa 1 Usiku nini Kilitokea

Shahidi: Samahani Mheshimiwa Jaji nilikuwa naomba Kwenda Short call Kuna Dawa nazo tumia Kwahiyo naomba Mahakama inivumilie nitakuwa naenda Mara kwa Mara

Shahidi anatoka kwa kusindikizwa na Askari Magereza Mmoja

Shahidi amerejea

Wakili wa Serikali: Shahidi Ulisema Kwamba Zoezi la Kufuatilia Taarifa liliendelea Mpaka Saa 1 Jioni, Nini kiliendelea

Shahidi: Ilipofika Jioni Saa 1, ASP Jumanne alituambia tusitishe zoezi Mpaka Siku inayofuatia

Wakili wa Serikali: Ili inayofuata ni Siku gani

Shahidi: Tarehe 09 August 2020

Wakili wa Serikali: Tarehe 09 August 2020 Nini kiliendelea

Shahidi: Ilipofika Tarehe 09 August 2020 Jioni nikiwa Katika Majukumu Mengine, nilipigiwa Simu na Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi Wa Polisi akinijulisha Kuwa amefanikiwa Kumkamata Khalfani Bwire akiwa na Simu Mbili na aKanitaka nisiondoke katika

Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam ili anikabidhi Simu za Khalfani Bwire..

Wakili wa Serikali: Nini kiliendelea

Shahidi: Majira ya Saa 3 na Nusu Nikiwa kwenye Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam Afande Ramadhan Kingai alifika akiwa pamoja na Afande ASP Jumanne Malangahe, Inspector Mahita na Constable Goodluck Baada ya Kufika alimuagiza Constable Goodluck anikabidhi simu Mbili zilizo kamatwa Kwa Khalfani Bwire. Simu hizo nilizo kabidhiwa Simu Moja aina ya Bundy yenye Rangi Nyeusi, Simu Nyingine aina ya Techno ambayo ni Smart phone yenye Rangi ya blue, Na ilikuwa na Cover Jeusi

Wakili wa Serikali: Baada ya Kukabidhiwa Simu hizo Ulifanya nini

Shahidi: Nilienda Kuhifadhi Simu hizo Ofisini Kwangu Ndani ya Kabati

Wakili wa Serikali: Sasa ni Shughuli gani Nyingine ili endelea

Shahidi: Wakati na kabidhiwa Simu hizo, Afande Kingai alinitaka pia niziandikie Barua Kwenda Ofisi Ya Uchunguzi ya Makosa ya Mtandao

Wakili wa Serikali: Baada ya Maelekezo hayo sasa nini hasa Kiliendelea

Shahidi: Siku inayofuatia Tarehe 10 August 2020, Afande Ramadhan Kingai alinijulisha kuwa tayari amewasiliana na Shahidi Luten Denis Urio, Wa JWTZ ili afike Siku inayofuatia kwa ajili ya Kuandika Maelezo Yake

Wakili wa Serikali: Baada ya ACP Kingai Kukupa Taarifa hiyo Kuhusu Tarehe 10 August 2020, Nini Kiliendelea

Shahidi: Niliweza Kuwasiliana na Luten Denis Urio Kwa Njia ya Simu, ili aweze Kufika Kwa ajili ya kuandika Maelezo yake

Wakili wa Serikali: alifika Muda gani Katika hiyo Tarehe 11 August 2020

Shahidi: Alifika Majira ya Asubuhi

Wakili wa Serikali: Baada ya Luteni Denis Urio nini Kiliendelea

Shahidi: Niliweza Kuandika Maelezo Yake na Aliweza Kueleza Jinsi alivyo Pata Taarifa

Wakili wa Serikali: Ongeza sauti

Shahidi: Niliweza Kushuka naye na Kwenda Katika Ofisi ni iliyokuwa natumia, na Niliweza Kuchukua Maelezo yake

Wakili wa Serikali: Ulichukua Muda gani Kuandika Maelezo yake

Shahidi: Ilikuwa Asubuhi, Ulichukua Saa Nzima

Wakili wa Serikali: Kitu gani Kingine kiliendelea

Shahidi: Wakati naandika Maelezo Yake alieleza Kuwa alikuwa akifanya Mawasiliano na Freeman Mbowe kwa kutumia Mtandao Wa Telegram, na alisema Kwamba Alikuwa ana wasiliana na Freeman a Mbowe Kwa namba yake ya 0719 933386

Namba ya Freeman Mbowe, pia alinitajia namba zake aliyokuwa anatumia 0787555200 Ya Mtoa Taarifa Denis Urio, na pia 0754612518 namba ya Denis Leo Urio, Pia alinitajia namba Nyingine Ya Mtuhumiwa Freeman Mbowe 0784779944

Wakili wa Serikali: Wewe Ulichukua Hatua gani sasa

Shahidi: nilimtaka anikabidhi Simu ambazo amekuwa alifanya naye Mawasiliano, Ambapo aliridhia Kunipa Simu aina Ya Techno

Wakili wa Serikali: Kwanini Wewe Uliaka akukabidhi Simu

Shahidi: Ilikuwa ni Kwa ajili ya kwenda Kufanya Uchunguzi Wa Kisayansi, ambapo Urio alisema ni Kwa Telegram

Wakili wa Serikali: Wewe ulipo taka yeye akukabidhi Simu hiyo, alikwambia nini

Shahidi: aliridhia lakini akaomba atoe line ambayo alikuwa alifanyia Mawasiliano na Freeman Mbowe ambapo angeiwasilisha Siku inayofuatia

Wakili wa Serikali: Baada ya yeye Kusema ameridhia na akaomba atoe Card ya Vodacom, wewe Ulijibu nini

Shahidi: Milimkubalia, Huku nikijua Mawasiliano ambayo yanafanyika Kwenye Telegram Yanabakia Kwenye Kifaa na siyo Sim Card

Wakili wa Serikali: Nini kiliendelea baada ya Kumkubalia Kutoa ile su Card

Shahidi: Niliandika Hati ya Makabidhiano, Huku nikiandika IMEI namba, Kwa ajili ya Kupokea hiyo Simu

Wakili wa Serikali: Hati hiyo ya Makabidhiano Ilikuwa na nini

Shahidi: Hati ilikuwa inaonyesha Simu nimepokea kwa nani, Jina. Lake, Mtu anaye Mkabidhi Pamoja na Kuandika IMEI namba zake kwa kuanzia namba 35 na Kuishia 040 na IMEI Nyingine inaanza namba 35 na Kuishia namba 057

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuwa Umerekodi Vitu hivyo, gani Kitu gani Kingine Ulifanya katika hiyo Hati

Shahidi: Hiyo Hati Nilisaini na Niliye Mkabidhi naye alisaini Wakili wa Serikali: Baada ya Kusema alikukabidhi Simu aina Techno, Je zile simu Nyingine alikwambia zipo wapi

Shahidi: alisema zipo Nyumbani Morogoro na. Akahaidi kuleta Siku inayo fuatia

Wakili wa Serikali: Siku inayofuatia ilikuwa lini Shahidi: Ilikuwa Tarehe 12 August 2020 katika Ofisi Ndogo ya Upelelezi Dar es Salaam, allifika Majira ya Asubuhi

Wakili wa Serikali: Nini kiliendelea

Shahidi: aliweza Kunikabidhi Simu Tatu Samsung Duos yenye Rangi Nyeupe, simu Nyingine ni simu aina ya Techno C9 yenye Rangi Nyeusi, Simu Nyingine aina ya Itel yenye Rangi Nyekundu

Wakili wa Serikali: Haya Makabidhiano wewe Ulifanya nini

Shahidi: Niliandaa Hati ya Makabidhiano Ya kila Simu, nikamsainisha na Mimi nikasaini

Wakili wa Serikali: Hebu Elezea Mahakama ni simu ngapi ulipokea Kutoka Kwa Luten Denis Urio

Shahidi: Simu ambazo Nilipokea zilikuwa ni Jumla ya Simu Nne

Wakili wa Serikali: Mara baada ya kuzipokea Ulifanyia nini

Shahidi: Niliweka Exhibit Label PF 143 Kwenye kila Simu

Wakili wa Serikali: Kwanini uliziwekea Exhibit Label Kwa Kila simu

Shahidi: Kwa Lengo la Kuzitofautisha, Ili zisiweze Kuchanganyika

Wakili wa Serikali: Na Hiyo PF 143 ilikuwa na nini

Shahidi: Kituo cha Kesi ilipofunguliwa, Namba ya Jalada, Tarehe ya Kuweka hiyo Lebel, Jina la Mmiliki (Kielelezo) kosa, aina ya Kielelezo na Utambulisho Wake

Wakili wa Serikali: Baada ya KuViwekwa Exhibit Lebel PF 145 Ulifanya nini

Shahidi: Nilichukua na Kwenda Kuvihifadhi katika Ofisi ninayo tumia na Kuhifadhi ndani ya Kabati la Chuma, ambalo Mimi nalitumia

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Bado tunaendelea na Cross Examination, Kwa Ruhusa Yako tunaomba Break fupi ili tukirejea tuweze Kuendelea

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Hatuna Pingamizi

Jaji: Basi tuta break Mpaka Saa 7 na Dakika 45, tutarudi kuja Kuendelea

Jaji anatoka (1:10 PM)

Jaji ameingia (2:19 PM)


Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa tena

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Quorum ya Upande wa Jamhuri ipo Vile Vile na tupo tayari Kuendelea Wakili

Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji na sisi pia Quorum yetu ipo Vilevile na tupo tayari Kuendelea

Jaji: Shahidi nakukumbusha Ulikuwa chini ya Kiapo na Utaendelea Kuwa Chini ya kiapo

Shahidi: Sawa Mheshimiwa Jaji

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Ulikuwa Ukieleza Mahakama Jinsi gani Ulivyo kabidhiwa Simu Kati ya Tarehe 12 August 2020. Je, ulikuwa na Idadi ya Simu Ngapi Mpaka Siku hiyo

Shahidi: Mpaka Tarehe hiyo ya 12 August 2020 nilikuwa nimesha pokea Jumla ya Simu 8

Wakili wa Serikali: Natukianza na Simu hizo, Je ukiziona Utaizitambuaje

Shahidi: Nita iona kwa Kutambua Jina, Rangi pamoja na PF 145 ambayo itaonyesha Jina la Mmiliki, Kosa, Namba ya Jalada Wakili wa

Serikali: Unamaanisha Nini unaposa Kwamba Kwenye PF 145 itaonyesha Jina la Mwenye Mali

Shahidi: Katika Vielelezo Nilivyo pokea, Simu Nne zilitoka kwa Shahidi Luten Denis Urio na Simu Nne zilitoka Mbili kwa Khalfani Bwire na Simu Moja Moja zilitoka kwa Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya

Wakili wa Serikali: Na Unaposema Kwamba Kwenye PF 145 inamajina, Je Majina gani hayo

Shahidi: Majina ya Watuhumiwa ambayo ni Adam Kasekwa, Khalfani Bwire na Mohamed Ling'wenya

Wakili wa Serikali: Na Vielelezo Vingine Vina Majina ya nani

Shahidi: Vina Majina ya Luten Denis Urio

Wakili wa Serikali: ambae ni nani

Shahidi: Ni Shahidi Katika Shauri hilo

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shahidi ameonyesha Uwezo wa Kuitambua, Naomba Kwa ajili ya Kumbukumbu nipatiwe Kielelezo namba P28 Mpaka Kielelezo namba 35

Wakili wa Serikali: anafungua Mfuko wa Vielelezo (Transparent plastic Bag)

Wakili wa Serikali: Shahidi Angalia Vielelezo hivyo Ka Unavitambua Ieleze Mahakama

Shahidi Afande Swila anapekua na kukagua kimoja kimoja

Wakili wa Serikali: Elezea Sasa Kama umevitbua kwa kuanza na Tarehe 07 August 2020

Shahidi: Tarehe 07 August 2020 Nilipokea simu aina ya Itel ambayo Inaonyesha kwenye PF 145 Jina la Adam Kasekwa Namba ya Jalada ni CD /IR 2097 /2020

Wakili wa Serikali: Simu aina gani

Shahidi: Simu aina ya Itel

Wakili wa Serikali: Ulizungumzia Kuhusu IMEI

Shahidi: IMEI kwenye simu hii ni 353736820265

Wakili wa Serikali: Unasema kenda, kenda ni Namba gani

Shahidi: Namba 9

Wakili wa Serikali: Simu Nyingine

Shahidi: Ni Simu aina ya Techno Yenye Rangi Nyeusi, ambayo Nimeitambua Kupitia Exhibit Lebel Ambayo Inaonyesha Namba ya Jalada la CD/IR /2097 /2020 Pia imeandikwa aina ya simu, Na inaonyesha Simu hiyo imepatikana kwa Mtuhumiwa ambaye ni Mohammed Abdilah Ling'wenya

Wakili wa Serikali: VIpi Kuhusu IMEI namba Shahidi: IMEI namba imeandikwa IMEFUTIKA

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Naona ametambua P 35

Wakili wa Serikali: Twende Kwenye Simu za Tarehe 09 August 2020

Shahidi: Simu nilizo pokea Tarehe 09 August 2020 ni Mbili ambazo ni Za Khalfani Bwire Simu aina ya Bundy, Nimeitambua Kupitia Lebel namba ambayo Inaonyesha Namba ya Jalada ambayo ni CD/IR /2097 /2020

Na Simu hii inaonyesha ni aina ya Bundy IMEI namba 359440075933775 Na Simu hii ilipatikama Maungoni Mwa Khalfani Bwire

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji ametambua Exhibit P 30

Wakili wa Serikali: Simu Nyingine kwa hiyo Tarehe 09

Shahidi: Simu Nyingine ni simu aina ya Tecno Yenye IMEI namba 355019115930845 Simu hii nayo ilipatikana Maungoni Mwa Khalfani Bwire Inaonyesha Namba ya Kesi ambayo ni CD/IR /2097 /2020

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji ametambua Exhibit P 32

Wakili wa Serikali: Twende Simu uliyokabidhiwa Tarehe 11 August 2020

Shahidi: Naitambua Simu aina ya Techno Yenye IMEI namba 358721101132040

Wakili wa Serikali: Imetoka Kwa nani

Shahidi: Imetoka Kwa Denis Leo Urio ambaye ni Mmiliki ambayo Inaonyesha Namba ya Kesi CD /IR /2097 /2020

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji ametambua Exhibit P 34

Wakili wa Serikali: Nani ambaye ameandaa PF 145 kwenye simu hii

Shahidi: Simu hii nimeandaa Mimi na Nimeandika kwa Mkono Wangu

Wakili wa Serikali: Twende simu za Tarehe 12 August 2020

Shahidi: Simu hiyo ni Techno Yenye IMEI Namba 358073079115221

Wakili wa Serikali: Ulipokea Simu hiyo Kutoka Kwa nani

Shahidi: Kutoka Kwa Luteni Deni Leo Urio, Inaonyesha Namba ya Jalada CD /IR/ 2097/2020

Wakili wa Serikali: Na Hiyo PF 145 Uliandaa lini

Shahidi: Ni Tarehe 13 August 2020

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji ametambua Exhibit P 28

Shahidi: Simu Nyingine ni Itel yenye IMEI namba 353487101333005

Wakili wa Serikali: Ulipokea Kutoka kwa nani

Shahidi: Kwa Luten Denis Leo Urio ambapo Inaonyesha Pia namba ya Jalada ambalo ni CD/IR/2097 /2020

Wakili wa Serikali: PF Uliandaa Lini

Shahidi: Tarehe 13 August 2020

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji ametambua Exhibit P 33

Shahidi: Simu Nyingine ni sumsumg yenye IMEI namba 354767086468291

Wakili wa Serikali: Ulipokea Kutoka kwa nani

Shahidi: Kwa Luteni Denis Urio yenye namba Ya Jalada namba CD/ IR/2097 /2020

Wakili wa Serikali: PF Uliandaa Lini

Shahidi: Tarehe 13 August 2020

Wakili wa Serikali: Ametambua Kielelezo namba 29

Wakili wa Serikali: Shahidi Umesema Kwenye hizi Simu za Tarehe 12 August 2020, Alafu PF 145 Uliandaa Tarehe 13 August 2020

Shahidi: Niliandika PF 145 Kutokana na Tarehe 12 August 2020 Kutokuwa na PF pale Ofisini

Wakili wa Serikali: Wakati Unatoa Ushahidi Wako Kuhusiana na Makabidhiano ya Simu Baina ya Wewe na Denis Leo Urio, Ulisema Kwamba Uliandaa Hati ya Makabidhiano Siku hiyo, Je Ukiona Utaitambuaje

Shahidi: Nitaitambua Kwa Jina langu Kwa sababu Wakati huo nilikuwa na Cheo Cha Assistant Inspector Swila, ambaye ndiyo Mimi, Niliandika Jina la Denis Urio ambaye ndiye amenikabidhi na Aina ya Simu na IMEI namba ambayo namba ya Kwanza inaanza na 35 na namba tatu za Mwisho ni 040 Na IMEI namba ya Pili ni 35 na Mwisho ni 057

Wakili wa Serikali: Hii Hati ya Makabidhiano ambayo Uliandaa wakati anakabidhi Simu, Yenyewe ina matumizi gani

Shahidi: Tunatumia Kukabidhiwa Vitu ambavyo Vimekamatwa kutoka kwa Mtuhumiwa, Kukabidhiana Kutoka Kwa Askari Kwenda Kwa Askari

Wakili wa Serikali: Mwanzoni Ulisema Kwamba Hati hiyo ni ya Watuhumiwa, Kwanini Ulitumia Hati hiyo kwa Denis Urio ambaye unasema ni Shahidi

Shahidi: Nimeitumia kwa sababu yeye ni Shahidi, la ambavyo tunakabidhiana kutoka kwa Askari Kwenda Kwa Askari

Wakili wa Serikali: Kwenye fomu hiyo tutatambuaje Kama yeye ni Shahidi

Shahidi: Kwa sababu yeye Haionyeshi Tarehe Ya Kukamatwa Kielelezo hicho

Wakili wa Serikali: Utaitambuaje

Shahidi: Niliandika Jina. Langu Assistant Inspector Swila na Niliandika Jina la Luten Denis Urio.. Sehemu za Kujaza Tarehe ya Kukamatwa na Muda Niliweka Alama ya Deshi

Wakili wa Serikali: Na Luteni Urio alifanya nini Kwenye Hati hiyo

Shahidi: Aliweza Kusaini na Mimi nikasaini Kisha nikaandika Tarehe ya Siku anayonikabidhi

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Kumuoyesha Shahidi Kielelezo

Wakili wa Serikali: Umetambua ni Kielelezo gani

Shahidi: Kielelezo hichi nimekitambua Ka Hati ya Makabidhiano Baina yangu na Luteni Denis Urio, Jina. Langu, Tarehe, Namba ya Kesi ya Jalada na Sehemu ambazo nimejaza Deshi

Wakili wa Serikali: Unaomba Mahakama ifanye nini

Shahidi: Naomba Mahakama Ipokee Kielelezo hiki Kama Kielelezo Hati ya Makabidhiano inaenda Kwenye Benchi la Jopo la Mawakili Wa Utetezi na Wanaikagua kwa Pamoja

Wakili Nashon Nkungu: Mheshimiwa Jaji Kwa niaba ya Mshtakiwa wa kwanza sina Pingamizi

Wakili John Mallya: Mheshimiwa Jaji Kwa niaba ya Mshtakiwa wa Pili Sina Pingamizi

Wakili Dickson Matata: Mheshimiwa Jaji Kwa niaba ya Mshtakiwa wa tatu Sina Pingamizi

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kwa niaba ya Mshtakiwa wa Nne hatuna Pingamizi Hati ya Makabidhiano inaenda Mezani Kwa Jaji sasa

Jaji: Kutakuwa ni Kielelezo namba Ngapi WS: Robert Kidando Tulikomea Kielelezo namba 38 kwa hiyo hii itakuwa ni Kielelezo namba 39

Wakili wa Serikali: Sasa Inspector Swila Soma Kielelezo hiki Kuanzia Hapa Shahidi anasoma Kielelezo kwa mujibu wa Sheria ya Ushahidi...

Wakili wa Serikali: Jina la Anaye kabidhi ni la nani

Shahidi: Luten Denis Urio

Wakili wa Serikali: Jina la anayekabidhiwa

Shahidi: Ni Mimi ambaye kwa Kipindi hicho nilikuwa Assistant Inspector

Wakili wa Serikali: Kwanini Unasema hiyo sahihi ni ya Denis Urio

Shahidi: Kwa sababu Wakati anasaini nilikwepo

Wakili wa Serikali: Eneo ambalo ni Deshi, Deshi

Shahidi: Kuna Deshi Palipo Kamatwa, Tarehe pia Deshi, Saa Pia Deshi, Kutoka Kwa Mtuhumiwa ambaye ni Deshi ambaye anatuhumiwa Kwa Kosa la Deshi

Wakili wa Serikali: Kwanini

Shahidi: Kwa sababu yeye ni Shahidi

Wakili wa Serikali: Unasema zile simu Katika Siku Nne tofauti ulizo pokea ulikuwa unaenda Kutunza Katika Kabati lako, Hebu Ifahamishe Mahakama ni Eneo gani hilo

Shahidi: Nilikuwa natuma Kwenye Ofisi, Ndani ya Kabati ambapo natinza Vitu Vyangu na Kubakia na Funguo

Wakili wa Serikali: Kwanini Ulikuwa unavifungia Katika Kabati

Shahidi: Nilikuwa na Vifungia katika Kabati la Chuma kwa ajili ya Kulinda Usalama Wa Vielelezo

Wakili wa Serikali: Ni watu wangapi Mlikuwa Mnatumia hilo kabati

Shahidi: Kwa Kipindi hicho nilikuwa natumia Mimi Mwenyewe

Wakili wa Serikali: Baada ya hapo Nini kiliendelea

Shahidi: Niliweza Kumpigia Simu Afande Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi Wa Polisi Kumfahamisha kuwa nimeshapokea Simu Nne za Denis Urio Na akanielekeza Kuandaa Barua Kwenda Katika Ofisi Ya Uchunguzi Makosa ya Mtandao kwa ajili ya Uchunguzi

Wakili wa Serikali: Ilikuwa ni lini Wakati unampa Tarehe hiyo Shahidi: Ilikuwa ni Tarehe 12 August 2020

Wakili wa Serikali: Baada ya wewe Kumpa Taarifa hiyo nini Kiliendelea

Shahidi: Alinitaka Nikabidhi Simu hizo kwa DC Goodluck Siku ya Tarehe 13 August 2020

Niliweza Kuandaa Barua ambayo ilisainiwa na Afande Hamad Msangi Kamishina Msaidizi Wa Polisi aliyopo Makao Makuu ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Ofisi Ndogo za Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Ukisema Ilisainiwa na HAMAD MSANGI, Wakati Uliandaa Wewe, Ni Kwanini

Shahidi: Kwa sababu Barua yoyote inayo toka kwenda Maabara ya Uchunguzi au Taasisi Nyingine lazima Isainiwe natu wenye Cheo Cha Kamishina Msaidizi au zaidi ya Cheo hicho

Wakili wa Serikali: Barua hiyo ilikuwa inaenda wapi na Kwa ajili gani

Shahidi: Ilikuwa inaenda Maabara ya Uchunguzi Wa Kisayansi Kwa ajili ya Uchunguzi Wa simu Nane

Wakili wa Serikali: Hizo Simu Nane ni zipi

Shahidi: Moja ni Ile aliyokamatwa nayo Mtuhumiwa Adam Kasekwa aina ya Itel yenye Rangi Nyeusi Nyingine ni Techno aliyokamatwa nayo Mtuhumiwa Mohammed Ling'wenya, Yenye Rangi Nyeusi Simu zingine ninalizokatwa nazo Khalfani Bwire Moja aina ya Bundy Simu Ndogo Nyingine ni Smart Phone Techno Yenye Rangi ya Blue

Shahidi: Pamoja na Simu Nne ambazo Nilikabidhiwa na Shahidi Luten Denis Urio, Techno Nyeusi, Itel ya blue, Tecno Rangi tatu Mchanganyiko (blue, Nyeusi na Dhahabu)

Wakili wa Serikali: Katika ile Barua ambayo unasema ilisainiwa na HAMAD MSANGI, Simu hizo nane ulizitambulisha kwa namna gani

Shahidi: Kwa Majina na IMEI namba

Wakili wa Serikali: Wakati Unazichambua Simu hizi Mahakamani, Kuna simu Ulisema Kwamba IMEI namba ilifutika, Je IMEI namba yake kwenye Barua hiyo uliandikaje

Shahidi: Nili Washa Simu, Nikatumia formula ya *#06# baada ya hapo Ikawa imefuta IMEI namba

Wakili wa Serikali: Baada ya hapo unafanyeje

Shahidi: Unabonyeza Okey

Wakili wa Serikali: Baada ya Kumalizia Kupata Namba hiyo nilirudisha Simu katika hali yake ya Kawaida Kwa kuzima

Wakili wa Serikali: Katika Barua hii uliyoandika Kwemda Katika Kamisheni ya Makosa ya Mtandao, Kitu gani ulikuwa unahitaji

Shahidi: Tuliomba Kupata Mawasiliano yaliyo fanyika katika hizo Simu Kupitia Mitandao Ya Telegram, Facebook, Instagram na WhatsApp Pia tuliomba Kupatiwa Taarifa za Miamala ya Fedha pamoja na Usajili

Wakili wa Serikali: Ni namba zipo hizo ulizoomba Kupatiwa Taarifa za Usajili

Shahidi: Ni 0719933386 Namba Nyingine ni 0784779944, Nyingine ni 0782237913, Nyingine ni 0787555200 Pia Nyingine 0754612518, Pamoja na namba zingine ambazo siwezi Kuzikumbuka.

Wakili wa Serikali: Sasa Ulifanya Nini

Shahidi: Nilimuita DC Goodluck Akaja Ofisini Makao Makuu Madogo Ya Upelelezi, nilifunga Kwenye Bahasha na Yeye akiwepo, Kisha nikamkabidhi Pamoja na Barua

Wakili wa Serikali: Ulimkabidhi kwa ajili gani sasa

Shahidi: Ili apeleke kwenye Kitengo Cha Uchunguzi wa Makosa ya Mtandao

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuwa Umemkabidhi Vitu hivyo Kupeleka Maabara Kitu gani Ulifanya

Shahidi: Tarehe 14 August 2020 Afande Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi Wa Polisi alinitaka nifike Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam, katika Chumba Cha Kutunzia Vielelezo Ili niweze Kukagua na Kibadirisha, Kutoka Katika Kidaftari Kilicho katwa kutoka Nyumbani Kwa Mtuhumiwa Khalfani Bwire ili niweze Kubaini Maeneo yaliyopo Dar es Salaam na niweze Kuyatembelea kwa Lengo la Kubaini Kama Yapo au hayapo na Kubaini ya nafanya Shughuli gani

Shahidi: Mheshimiwa Jaji samahani naomba niende washroom Kabla shahidi hajaruhusiwa katoka Kizimbani kwa speed sana.. Tunaita 'mkukuu' Naona hapa Wakili Nashon Nkungu na yeye kaunganisha nyuma kufuata shahidi, akashuhudie, ni Washroom kweli au wash-something else..

Shahidi karejea sasa kutoka mjini Washroom..

Wakili wa Serikali: Sasa Hebu elezea Maelekezo hayo ambayo Umepewa na ACP kingai Uliyatekeleza kwa namma gani shahidi Tarehe 14 August 2020 Nilifika Chumba Cha Kutunzia Vielelezo Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam, na Kumkuta Mtunza Vielelezo Coplo Johnson ambaye aliweza Kinionyesha Vielelezo ambavyo Vilikamatwa kwa Khalfani Bwire Ingizo namba 211/2020 kutoka Katika Kitabu cha Kinacho hifadhi Vielelezo.. Tuliweza Kupata Ki Daftari hicho na Kukagua Eneo mbalo Kinaonyesha ni Daftari, Kilikuwa kina Michoro Ya Barabara..

Wakili John Mallya: Mhe Jaji naomba Shahidi azuiwe Kuhusu Kujadili Content ambayo Haipo Mahakamani, na Hawezi Ku tender

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kwa Kuongezea tu, Kidando alikuwa anasimama hapa kwa sababu ya Muda, Linalotendeka kwa Mwingine lifanyike Kote kote

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Naona Pingamizi halina Mashiko, Shahidi anasema Jambo ambalo ni Ushahidi Wa Moja kwa Moja

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji tukubaliame Rule of The game, asije Kusimama Mbele Mtu akasema suala la Muda

Wakili John Mallya: Mheshimiwa Jaji Nakubalina na Wakili Peter Kibatala, ila mimi na zungumzia Content ambayo bado haijaingia Mahakamani, pia anachokizungumzia kilikuja Mahakamani kikafukuzwa

Jaji: Bwana Robert Kidando Umeelewa

Jaji: Kwanza tukubaliane Kwamba Kilichokataliwa ni Kielelezo, Kuhusu Content mimi sijasoma Kama Nyie, Suala la kilikubaliwa au Kukataliwa ni Jukumu la Mahakama Kuja Kujadili Mbeleni.. Kwa sasa sioni Kama ni sahihi kumkataza Shahidi Kitu ambacho anaamini alikifanyia kazi..Kuhusu Muda tulikuwa tunazumgumzia Kuhusu Kurudia Maswali, na Mr Kidando aliposimama Alikuwa anasema usirudie Maswali Ndiyo Maana Juzi Ulizungumza Muda Mrefu niliona kwenye Vyombo Vya Habari.

Jaji: Wakili wa Serikali Tuendelee

Shahidi Niliweza Kuangalia Kwenye Kidaftari na Kujua ni Maeneo yapi

Wakili wa Serikali: Sasa Ulienda Eneo gani ambalo ulikuwa umeona kwenye Ali Daftari

Shahidi: Makutano ya Barabara ya Kilwa na Mandela, Nilibaini Kituo cha Mafuta cha GBP, pia Kituo cha Kuuzia Mafuta Cha Puma
Pia nilitembea Eneo la Kariakoo Jirani na Mwendokasi Kuna Kituo cha Bigbon, pia Nilienda Kituo cha Basi cha Morocco pia Nilikuta Kituo cha Kuuzia Mafuta cha Jina la Total Kituo hicho nacho Kilikuwa kina fanya Kazi ya Kuuza Mafuta

Wakili wa Serikali: Baada ya Kutembelea Maeneo hayo, Ulifanya nini

Shahidi: Baada ya Kufika na Maeneo hayo, niliweza Kumjulisha Afande Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi Wa Polisi, aKanitaka nichukue Sampuli za Maandishi ya Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Khalfani Bwire

Siku inayofuatia Tarehe 15 August 2020 kuanzia Majira kati ya Saa Nne na Saa Tano na Robo Niliweza Kumchukua Mahabusu Mtuhumiwa Khalfani Bwire nikampelela kwenye Jengo la Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa Wa Temeke ambapo tuliweza Kuchukua Sampuli ya Maandishi Kutoka Kwa Mtuhumiwa huyo

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuwa umemchukua Khalfani Bwire ni Utaratibu gani Ulitumia sasa

Shahidi: Niliweza Kumpa Karatasi Nane, na Kumpa aandike Maneno ambayo yalikuwa kwenye Kidaftari

Chini aliweza Kuandika Jina na Saini katika Kuthibitisha Kuwa Sampuli hiyo ya Maandishi ni ya kwake, kisha na Mimi nikathibitisha na Kumrudisha Kituo cha Polisi Chang'ombe

Chini aliweza Kuandika Jina na Saini katika Kuthibitisha Kuwa Sampuli hiyo ya Maandishi ni ya kwake, kisha na Mimi nikathibitisha na Kumrudisha Kituo cha Polisi Chang'ombe

Wakili wa Serikali: Je, Uliweza Kumfahamisha ni Kwanini Ulikuwa Unachukua Sampuli hizo. Je, Uliweza Kumfahamisha ni Kwanini Ulikuwa Unachukua Sampuli hizo

Shahidi: Niliweza Kumwambia kuwa Nachukua Sampuli katika Kuthibitisha Kuwa nataka Kuthibitisha uliyeandika ni wewe au Mtu Mwingine

Wakili wa Serikali: Ikawaje baada ya Kumwambia

Shahidi: Aliweza Kuthibitisha na Kusaini

Wakili wa Serikali: Baada ya Shughuli hiyo Hapo Chang'ombe, Kitu gani pia Ulifanya

Shahidi: Siku hiyo hiyo Tarehe 15 August 2020 Nilifika Kituo cha Polisi Mbweni ambapo palikuwa na watuhumiwa Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya Majira ya Saa Nane Mpaka Sa 9 na robo Niliweza Kuchukua Sampuli zao

Wakili wa Serikali: Ulitumia Utaratibu gani baada ya Kumtoa Mahabusu

Shahidi: Niliweza Kumfahamisha kuwa Kuna Daftari imekamatwa kutoka kwa Mtuhumiwa Khalfani Bwire, ambapo yeye amekataa Maandishi siyo ya kwake. Nikampa Karatasi Nane, aweze Kuandika Sampuli ya Mwandiko Wake

Shahidi: Aliweza Kuthibitisha kwa Kwa Mwandiko Wake

Wakili wa Serikali: Baada ya hapo Ulifanya nini kwa Mtuhumiwa Adam Kasekwa

Shahidi: Nilirudisha Adam Kasekwa Mahabusu ya Kituo cha Polisi Mbweni, nikamchukua Mohammed Ling'wenya ambaye milimfahamisha Kuhusu adhima yangu ya kuchukua Sampuli ya Maandishi zna yeye aliridhia, Kuanzia Saa 12 Mpaka Saa 1 Jioni

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuchukua Sampuli hizo ukawa Umechukua Sampuli ngapi

Shahidi: Na Yeye Mtuhumiwa Nilichukua Sampuli ya Karatasi zote Nane, na akaweza Kuthibitisha Kuwa Maandishi Yaliyopo katika Karatasi hizo ni ya kwake kisha akasaini

Wakili wa Serikali: Baada ya Kukamilisha Zoezi hilo Ulifanya nini

Shahidi: Baada ya Kukamilisha Zoezi hilo na Kumrudisha Mtuhumiwa Mahabusu Niliendelea na Majukumu Mengine.. Nikamjulisha Afande Ramadhan Kingai, Ambapo Siku inayofuata alinitaka niandae Jalada hilo

Wakili wa Serikali: Siku inayofuata ya Tarehe Ngapi

Shahidi: Tarehe 16 August 2020 alinitaka niandae Jalada hilo na Kupeleka kwa DPP kwa Mapendekezo ya Kuandaa Mashitaka

Wakili wa Serikali: Baada sasa ya Maelekezo Ya Kingai Ulifanya nini

Shahidi: Tarehe 17 August Niliweza Kuandaa Jalada hilo na Kuweza Kumpatia Afande Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi Wa Polisi ambapo alilisoma na Kisha kiliandalia Barua na Kulipeleka Ofisi ya DPP Zilizopo hapa Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama sasa Mnamo Tarehe 19 August 2020 ulikuwa wapi na Ulifanya Shughuli gani Kuhusiana na Shauri hili

Shahidi: Siku hiyo Tarehe 19 August 2020 nilikuwa hapa Dar es Salaam, niliweza Kushiriki katika Kuwapeleka Watuhumiwa Watatu Mahakama Ya Kisutu

Wakili wa Serikali: Watuhumiwa hao watatu ni akina nani

Shahidi: Ni Adam Hassan Kasekwa, Mohammed Abdilah Ling'wenya Ling'wenya na Khalfani Hassan Bwire

Wakili wa Serikali: Hatua ipi ya Kiupelelezi iliyokuwa Imefika Mpaka Mnawapeleka Washitakiwa Mahakamami Shahidi Baadhi ya Vielelezo Vilikuwa Vimeshapelekwa Maabara ya Uchunguzi, Watuhumiwa Walikuwa wameshaandikwa Maelezo Yao, pamoja na Hati za Kukamatia Vielelezo hivyo vilikwepo Jaladani

Shahidi: Katika Hatua Nyingine Upelelezi Ulikuwa unaendelea ili Kupata Taarifa za Simu Nane zilizo kuwa zime pelekwa katika Ofisi Ya Uchunguzi Wa Makosa ya Mtandao

Wakili wa Serikali: Sasa Baada ya Siku hiyo ni Shughuli gani zingine Ulizo fanya katika Shauri hilo

Shahidi: Watuhumiwa Wengine Waliendelea Kukamatwa na kufikishwa Mahakamani Mwezi September, Ambapo Watuhumiwa hao ni Justin Elia Kaaya, Khalid Athuman na Gabriel Muhina

Wakili wa Serikali: Watuhumiwa Walikamatwa Kipindi gani

Shahidi: Walikamatwa kwa Tarehe tofauti kuanzia Mwezi August Mpaka September na Mahakamani Walifikishwa kwa Tarehe Tofauti

Wakili wa Serikali: Zaidi ya Ukamataji wa Watuhumiwa hao watatu Shughuli gani Nyingine Ulifanya

Shahidi: Tarehe 16 September 2020 Niliweza Kuandika Barua ya Kupeleka Sampuli za Maandishi ya Watuhumiwa watatu Khalfani Bwire, Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya katika Kitengo Cha Uchunguzi kwa ajili ya Uchunguzi Wa Miandiko yao na Kufanya Ulinganifu wa Daftari lililokamatwa Kwa Mtuhumiwa Khalfani Bwire Siku hiyo hiyo kabla ya Kuandaa Barua Niliweza Kufika Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam kwa ajili ya Kuchukua Daftari na Notebook kutoka katika Ingizo namba 211/2020

Wakili wa Serikali: Ulichukua kutoka kwa nani

Shahidi: koplo Johnson wa Chumba Cha Kutunzia Vielelezo Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuchukua Ukafanya nini

Shahidi: Nilienda navyo Ofisi ya Mkurugenzi Wa Makosa Ya Jinai, Dar es Salaam Kuandaa hiyo Barua,nikaambatanisha na Sampuli za Maandishi, Kidaftari na Barua ambayo ilisainiwa na Afande Hamad Msangi Kamishina Msaidizi Wa Polisi anayefanya Kazi Katika Ofisi Ya Mkurugenzi wa Upelelezi Makosa Ya Jinai, Ofisi Ndogo za Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Kidaftari na Note book Vilienda wapi

Shahidi: niliweza Kuambatanisha na Barua, na Vielelezo nikavipa namba Kuanzia B1 Mpaka B9 Kielelezo ambacho kinabishaniwa Niliandika A1 Ambacho ni Kidaftari Chenye Michoro Halafu B1 Mpaka B9 ni Sampuli ya Maandishi ya Khalfani Bwire pamoja na Notebook pamoja na Maandishi akiwa katika Shughuli zake za kawaida

Wakili wa Serikali: Za Watuhumiwa Wengine Ilikuwaje

Shahidi: C1 Mpaka C10 zilikuwa za Sampuli za Maandishi ya Mohammed Ling'wenya Pia D1 Mpaka D9 zilikuwa Sampuli za Adam Kasekwa

Wakili wa Serikali: hizi Sampuli ambazo umeambatanisha Kupeleka Katika Maabara ya Uchunguzi, Je Tarehe ulikitoa wapi hicho Kidaftari

Shahidi: Nilikuwa nimekifungia Mimi Katika Kabati la Chuma ambalo Mimi nilikuwa nalitumia, Nilienda Kukabidhi Katika Maabara Ya Uchunguzi Kwa koplo Khamis

Wakili wa Serikali: Shughuli gani sasa Nyingine Ulifanya

Shahidi: Niliendelea na Majukumu Mengine, Mpaka Tarehe 25 November 2020 Nilipokea Maelekezo Kutoka Kwa Afande Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi Wa Polisi akinitaka niandae Barua Mbili, Moja Barua ya kwenda Kwa Mrajisi Wa Silaha ili Kupata Taarifa Za Mmiliki Wa Silaha iliyokamatwa Kutoka Kwa Mmiliki Adam Kasekwa ambayo ni Bastola aina ya Luger yenye namba A5340. Pili alinitaka niandae Barua ya Kumkabidhi Detective Constable Goodluck kwa ajili ya Kupeleka Silaha Bastola aina ya Luger yenye namba A5340 katika Maabara ya Uchunguzi Wa Kisayansi, Kitengo Cha Uchunguzi Wa silaha Pia Barua hiyo ilikuwa inahusisha Kukabidhi Risasi Tatu ambazo zilikatwa Kutoka Kwenye Magazine kutoka kwa Mtuhumiwa Adam Kasekwa

Wakili wa Serikali: Ni Kwanini sasa Silaha hizo Mlikuwa Mna aandikia Barua, Ili nini sasa?

Shahidi: Kwa ajili ya Uchunguzi, ila pia ili Kujua Ka Silaha hizo Zina fanya kazi

Wakili wa Serikali: Kazi ya Kuandaa Barua hizi Ulifanyia Wapi

Shahidi: Nilifanya Ofisi Ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa Ya Jinai, Ofisi Ndogo za Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuandika Barua hizo Elelezea Upelekaji Wa Bastola na Risasi

Shahidi: Kabla yaKuandika Barua hizo Niliweza Kumuita Detective Constable Goodluck aweze Kuja na Kuchukua Bastola na Risasi na baada ya Kuja nazo Niliweza Kuhakikinsilaha hiyo aina ya Luger A5340 yenye Risasi Tatu Ndipo Niliandaa Barua hiyo ambayo ilisainiwa na HAMAD MSANGI Kamishina Msaidizi Wa Polisi ambaye anafanya Kazi Katika Ofisi Ya Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa Ya Jinai, Ofisi Ndogo za Dar es Salaam, Na Barua ya Pili pia ilisainiwa na huyo huyo ACP Hamad Msangi

Wakili wa Serikali: Unasema ulikuwa unahakiki, wewe Ulikuwa unahakiki nini

Shahidi: Nilikuwa nahakiki Serial number ya silaha na kuiangalia hiyo Silaha Kama Yenyewe

Wakili wa Serikali: Kipi ulikiona

Shahidi: Niliona Kweli hiyo ni Silaha aina ya Luger yenye namba A5340

Shahidi: Yapo Nje ya Silaha, Upande wa Kulia Ukishika silaha

Wakili wa Serikali: Sasa hii Bastola amekuja nayo Goodluck, Je Upande Wa Risasi ulihakiki nini

Shahidi: Nilihakiki Kama Risasi ni tatu, Nikakuta kweli ni Risasi tatu

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuthibitisha Ka Risasi ni tatu Ulifanya nini

Shahidi: Niliweza Kufunga Silaha hiyo Katika Bahasha, akaweza Kuondoka nayo Kwenda Kukabidhi Katika Kitengo Cha Uchunguzi Wa Kisayansi wa Silaha na Milipuko

Shahidi: Mheshimiwa Jaji samahani naomba niende chooni

Wakili wa Serikali: Shahidi nasema Ulifanya nini sasa Kuhusu ile Barua ya kwenda Kwa Mrajisi Wa silaha

Shahidi: Nilifunga na Kupeleka Katika Masijara ya Siri, Kwa ajili ya kwenda Ofisi Ya Mrajisi Dodoma Na Barua iliondoka Siku ileile

Wakili wa Serikali: Hebu ieleze Mahakama Silaha hiyo Ukiona Leo unaweza Kutambuaje

Shahidi: Naweza Kuitambua Kwa aina yake Ya Luger Serial Namba yake A5340 na Kama nilivyosema Mwanzo serial Namba hiyo ipo
Upande wa Kulia

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Kupatiwa Kielelezo namba P3

Wakili wa Serikali: Shahidi Kwa Kuchukua Tahadhari zote, Hebu Tizama Silaha hiyo na useme Kama unaweza Kuitambua

Shahidi: Kama Nilivyosema awali, Silaha hii ina Jina Upande Wa Kushoto Luger na Upande Wa Kulia ina Serial number ya A5340, Hii ni Silaha ambayo Niliandikia Barua Kwenda Kitengo Cha Uchunguzi

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Bado tunamaswali katika Examination inchief, na Sasa ni saa 11 Kasoro Dakika 5, Hivyo tunaomba Hairisho Mpaka Jumatatu Tarehe 07 February 2022

Mahakama ipo Kimya, Jaji anaandika Kidogo

Kibatala: Mheshimiwa Jaji hatuna Pingamizi

Jaji: Kufuatia Ombi lililoletwa na Upande wa Mashitaka, Mahakama Inakubali Kuhairisha Kesi Mpaka Jumatatu Tarehe 07 February 2022, Shahidi Utaendelea Kuwa Kizimbani Kutoa Ushahidi Wako, Washtakiwa wataendelea Kuwa Rumande chini ya Magereza

Jaji anatoka
 
Hizi siku mbili zilikuwa ngumu sana kwangu. Mawakili wa serikali walitukatili sana kutoleta mashahidi. Kufuatilia hii kesi inanikumbusha uhondo niliokuwa naupata enzi nikisoma novel za Willy Gamba.

Naweka kambi hapa kufuatilia michongo.

Mungu ibariki JF na mleta mchongo kwa updates zako zilizotukuka
 
Mkuu The Sheriff ahsante sana kutuunganisha na yanayojiri Mahakamani.

Mungu mkuu atatushindia na hii kesi ya Michongo
 
Ikupendeze mheshimiwa@sheriff
Upande wa jamhuri JF quorum iko kama awali na tuko tayari
 
Back
Top Bottom