Rostam Aziz: Historia ya Dkt. Slaa haimpi uhalali wa kujifanya anajali maslahi ya Mtanzania. Kampuni zangu hazihusiki na uwekezaji wa DP World

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,219
103,809

Mfanyabiashara mkubwa nchini Rostam Aziz amezungumza na waandishi wa habari Juni 26, 2023 ambapo ameeleza mambo mbalimbali ikiwemo sakata la bandari ya Dar na kuhusika kwake kwenye uwekezaji huo mkubwa.

---

Juzi katika mdahalo pale hoteli ya Serena nilisema kuwa sihusiki na hili jambo (mkataba wa bandari) kibiashara. Ningekuwa nahusika nisingekuwa jasiri wa kuyasema yale niliyoyasema katika mdahalo ule.

Unapohusika na jambo huwezi kulijadili, na pia huwezi kuwa na uwezo au neutrality (hali ya kutofungamana na upande wowote) ya kuzungumzia jambo lenyewe, hivyo ningekaa pembeni na kuacha wengine wajadili.

Mimi kama Rostam na kampuni zangu hatuhusiki na uwekezaji au utakaokuwa uwekezaji wa kampuni ya DP WORLD.

Mimi ni mfanyabiashara na nimewekeza ndani na nje ya nchi, na nimetangaza jina la Tanzania kote duniani kwa kuwavutia wawekezaji waje kuwekeza katika nchi yetu ili tuweze kupata ajira na tuimarisha uchumi wetu.

Watu wanapiga porojo na ninawapa changamoto waende mahakamani. Mimi ninaaminiwa na benki za ndani na za nje ndiyo maana wananikopesha,” amesema na kuongeza “Rais (John) Magufuli asigefungua viwanda vyangu kama mimi sio mfanyabiashara halali.

Mimi sifanyi kazi na serikali, huwezi kusikia Rostam anaomba tenda serikalini au anauza hata sindano serikalini. Mimi ni mfanyabiashara ninayefanya biashara na sekta binafsi ndio maana huwezi kunituhumu kuwa nimetoa rushwa au nimekula rushwa. Hayo maneno (ya Dkt. Slaa) ni ya uropokaji tu na yasiyifanyiwa utafiti.

Historia ya Dkt. Slaa haimpi heshima wala uhalali wa kujifanya eti yeye ni mtu wa kujali maslahi ya Watanzania. Siku zote amejijali yeye binafsi na maslahi yake binafsi.

Dkt. Slaa aliacha kazi ya utumishi wa Mungu kanisani baada ya utovu wa maadili kwa kuona maisha yake ni bora zaidi kuliko utumishi wa Mungu. Historia yake ni historia ya kukosa uaminifu an uadilifu.

Dkt. Slaa hakujiunga upinzani kutokana na imani yake kwa sababu jina lake lilikatwa alipogombea kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na sababu iliyotolewa wakati wa kukatwa jina lake ni sababu ya kukosa uadilifu alipokuwa mtumishi wa Mungu kanisani.

Huyu Bwana Dkt. Slaa anaangalia maslahi yake binafsi, hakuwa mwanachama wa CHADEMA bali alipoona jina lake limekatwa (alipogombea kupitia CCM) ndio akahamia CHADEMA

Watanzania wakumbuke kuwa, huyu mtu (Dkt. Slaa) alipokuwa CHADEMA mwaka 2015 alikisaliti chama chake wakati kukiwa kinaelekea kwenye uchaguzi, alikisaliti chama chake kwa kuhongwa, alihongwa ndipo akaasi na kukisaliti chama chake (CHADEMA). Alikaa zake pale Serena baada ya pale akapanda ndege kwenda Canada na kisha akapewa ubalozi

Kwa kifupi Dkt. Slaa hana uadilifu wala uaminifu wa kunisema, mtu ambaye hana msimamo, mbinafsi , anayeangalia maslahi yake na hajawahi kuchangia chochote katika uchumi wa nchi yetu kazi yake ni kupiga tu mdomo. Mtu wa namna hii kumjibu ni shida lakini ni lazima wakati mwingine umjibu

Historia ya Dkt . Slaa inatosha kabisa kueleza kuwa yuko tayari kupandikiza chuki na uhasama kwa ajili ya maslahi yake binafsi, kwa Kiswahili kifupi huyu jamaa (Dkt. Slaa) ni 'kizabizabina' ni fitina, mbinafsi. Na ni mtu wa kusema chochote na lolote na wakati wowote kwa maslahi yake binafsi"

Dkt. Slaa ananiita mimi fisadi, sasa mimi (Rostam) nafanya kazi na sekta binafsi wala sifanyi kazi na serikali nakuwaje fisadi, kwa hiyo nawafisadi sekta binafsi wenzangu, je watakubali nao? Sijawahi kupata skendo ya serikali na wala sijawahi kuomba ku-supply hata sindano serikalini

---

My Take

CCM na Team ya Magufuli mje na nyinyi mtujibu mlimnunua Dr. Slaa kwa bei gani
 
Mfanyabiashara mkubwa nchini Rostam Aziz amezungumza na waandishi wa habari Juni 26, 2023 ambapo ameeleza mambo mbalimbali ikiwemo sakata la bandari ya Dar na kuhusika kwake kwenye uwekezaji huo mkubwa.

Mimi sijui wamekosania nini. Rostam anasema Dr. Slaa historia yake haimpi heshima wala uhalali wa kujifanya mzalendo. Siku zote anajijali yeye na tumbo lake.

Anaendelea...anasema aliacha utumishi wa Mungu kwa kuona maisha yake ni bora zaidi ya kumtumikia Mungu. Alijiunga na Chadema baada ya kukatwa CCM. Akajitoa Chadema baada ya kununuliwa na kupewa ubalozi. Anasema hana msaada kazi yake ni kupiga domo tu. Aiseee anamuita Kizabizabina ni mtu wa kuogopwa kama ukoma.

@Dr.W.P.Slaa tunasubiri majibu

My Take
CCM na Team ya Magufuli mje na nyinyi mtujibu mlimnunua Dr. Slaa kwa bei gani

Duh sasa yeye Rostam anauzalendo gani?
 
Rostam Aziz Issue ya Bandari inakuuma nini?
Wewe ni msemaji wa Serikali?

Jaribu kutulia tumekuvumilia sana sana kwenye mambo ya Taifa gas, madini, umene ?
 
Back
Top Bottom